Documentos de Académico
Documentos de Profesional
Documentos de Cultura
com
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1180 SHAABAN 1436, IJUMAA , JUNI 5-11, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=
Tuhuma za ugaidi:
JAJI Mstaafu Joseph Warioba (kushoto) akiwa na Waziri Mkuu mstaafu Dkt. Salim
Ahmed Salim.
Uk. 3
Tahariri/Habari
2
AN-NUUR
AN-NUUR
Na Mwandishi Wetu
mahakamani wimbo
wa DPP ni mmoja tu:
Mheshimiwa Hakimu, kesi
imeletwa hapa kutajwa
tu, mahakama yako haina
uwezo wa kusikiliza kesi
hii. Tunaomba kupangiwa
t a r e h e n ye n g i n e k wa
kutajwa tenani mwaka
nenda rudi gerezani
Segerea-Mahakama ya
Kisutu.
Imeongeza barua
h i y o n a k u d a i k u wa
wa m e b a m b i k i wa k e s i
ya ugaidi kutokana na
msimamo wao wa wazi
kudai mamlaka kamili ya
Zanzibar.
B a r u a i k a t a j a wa t u
wengine
ambao
yamewakuta kwa kuwa
na msimamo tofauti na
ule wa CCM wa mfumo
wa muungano wa serikali
mbili.
Katika kulifafanua hilo
b a r u a i m e s e m a k u wa
hata wazee na makada
wa chama kama Mzee
Hassan Nassor Moyo,
aliye Muasisi wa ASP na
muasisi wa CCM aliyebeba
kadi namba saba ya CCM,
amefukuzwa chama na
wajukuu wasioijua hata
hiyo historia ya CCM.
Pamoja na Mzee Moyo
wakasema kuwa ndiyo
sababu ya kufukuzwa
Waziri Mansour Yusuf
H i m i d n a a l i y e k u wa
Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar, Othman Masoud
kwa msimamo wao wa
kutetea Zanzibar ndani ya
muungano.
Tofauti iliyopo baina yao
Uamsho na waheshimiwa
h a o n i k u wa t u wa o
Masheikh wamepachikwa
tuhuma nzito za ugaidi.
Lakini wote yanawakuta
kwa kuweka wazi
msimamo wao juu ya
mfumo wa muungano
uliopo kuwa haufai.
Kwa upande mwingine
barua ikasema kuwa, hata
waheshimiwa sana huku
Bara walioweka msimamo
Habari
AN-NUUR
wafungwa na mahabusu
kuingia au kuingiza
madawa hayo, wamesema
hawajui kama ni utaratibu
au ni sheria kuwa kila
anayepelekwa gerezani, ni
lazima apekuliwe akiwa
amevuliwa nguo.
Wameeleza kuwa wakati
mwingine ukifikishwa
gerezani, katika ukaguzi
wao unalazimishwa
utoe haja kubwa lengo
ni kujirizisha kuwa
mtuhumiwa hana dawa
z a k u l e v ya , n a k a m a
huna utaletewa chakula
ule ili mradi utoe haja
wahakikishe huna kitu
ndipo uingie gerezani.
Aidha, wameeleza kuwa
kitendo cha kuvuliwa
nguo, kurushwa kichura
u c h i wa m n ya m a n a
kupekuliwa sehemu za haja
kubwa, ni suala la kawaida
unapopokelewa Segerea,
wakahoji katika hali kama
hiyo mtuhumiwa huyu
ataingizaje vilevi hivyo.
Kwa kweli ni
udhalilishaji mkubwa na
mateso makubwa, lakini
Makala
Na Mussa Ame
AN-NUUR
Inatoka Uk. 2
wa Mambo ya Ndani
Mheshimiwa Mat hias
Chikawe juu ya malalako
yao.
Wamesema kuwa kauli
ya Waziri Chikawe kuwa
mtuhumiwa aliyelalamika
k u d h a l i l i s h w a
achunguzwe isije ikawa
kafanyiwa mambo
ambayo ni mchezo
wake aliozoeya ni ya
kumdhalilisha mlalamikaji
na isiyotarajiwa kutoka
kwa kiongozi mstaarabu
wa serikali.
K wa l ug ha nye p e s i
tu, barua hiyo imemtaka
Mheshimiwa Chikawe
kupima kauli yake kwa
kujiuliza kama angeweza
kutoa kauli kama
hiyo iwapo ingekuwa
malalamikaji ni mtu
anayemuhusu.
Kwa kumalizia barua
hiyo imekariri madai ya
Makala
AN-NUUR
SIAD Barre
Somalia ya Kiingereza
Somalia ya Kiingereza au
British Somaliland lilikuwa
ni eneo linalokaliwa na
Uingereza katika Somalia ya
Kaskazini. Eneo hilo tangu
mwaka 1961 lilikuwa sehemu
ya Jamhuri ya Somalia na
mwaka 1991 likawa Jamhuri
ya Somaliland, yaani nchi
isiyotambuliwa na umma wa
kimataifa lakini yenye tabia
zote za nchi huru.
Uingereza iliingia katika
eneo hili baada ya Misri
kuondoka mwaka 1885,
baada ya kushindwa na
jeshi la Mahdi huko Sudan.
U i n g e r e z a i l i i n g i a k wa
sababu iliona umuhimu wa
kutawala pande zote mbili
za Bab el Mandeb, ikihofia
nchi nyingine za Ulaya hasa
Ufaransa iliyokuwa na koloni
lake la kwanza Ubuk (Obok)
katika nchi ya Djibouti ya
sasa tangu 1862. Somaliland
ilitawaliwa awali kama mkoa
wa Uhindi wa Kiingereza na
baadae ikawa chini ya Wizara
ya Makoloni huko London.
Hata hivyo Uingereza
ilikutana na upinzani mkali wa
wenyeji kuanzia mwaka 1899
wakiongozwa na kiongozi
wa k i d i n i , M o h a m m e d
Abdullah Hassan, aliyeitwa
na Waingereza Mullah
Majununi. Waingereza
walijibu vita iliyopiganwa
miaka 20 iliyoua takriban
theluthi moja ya wakazi wote
wa eneo.
Mwisho wake Uingereza
iliweza kumaliza upinzani
kwa teknolojia mpya ya
6
Na Mwandishi Wetu
KUNA usemi na usemi huu
ni wa Kichina ambao tafsiri
yake ni:
Nyayo iliyonyoka,
haikiogopi
kiatu
kilichopindika. Maana
ya usemi huu ni kwamba
mtu mwenye maadili
yaliyonyoka, haogopi
umbeya au udaku. Yaani,
huwa haogopi kusengenywa
au kutiwa hewani, kama
wasemavyo mitaani. Madhali
anachofanya au anachosema
mtu huyo ni cha haki na
cha kweli, kisicho ila wala
waa, madhali ameongoka na
amenyoka, hapaswi kuwa na
hofu ya kutiwa midomoni.
Kwa bahati mbaya,
baadhi yetu wenye uchu
ya kuwapiga darubini
wanasiasa, hususan wale
wenye madaraka, hatukosi wa
kuwatia hewani kila uchao.
Wanajitakia wenyewe. Hayo
husababishwa na hulka yao
kwani tabia moja waliyo nayo
wanasiasa, wa mirengo na
rangi mbalimbali za kisiasa,
ni ya kuupindapinda ukweli.
Hufanya hivyo wakijuwa
kwamba wanadanganya na
kwamba wanaowadanganya
wanajuwa kwamba
wanadanganywa. Lakini
hawawezi kujizuia
wasidanganye.
Inawezekana kwamba
wanapodanganya, nafsi
zao huisuta midomo yao.
Hatujui. Tujuacho ni kwamba
wa m e z o e a k u d a n g a n ya
na kwao kudanganya
kumekuwa kama mchezo.
Kama kucheza bao chini ya
mwembe.
Mtu huwa na mengi ya
kujiuliza anaposimama
Waziri Mkuu bungeni kama
alivyosimama Waziri Mkuu,
Mheshimiwa Mizengo Pinda
wiki iliyopita na kusema,
akiwa na macho makavu
na b ila ya k uyapepesa,
kwamba hayajui yaliyowafika
mashekhe 24 wa Jumuiya ya
Uamsho na Mihadhara ya
Kiislamu, kwa ufupi Uamsho,
waliokamatwa Zanzibar na
kupeleka kufungwa gerezani
Bara kwa tuhuma za ugaidi.
Mahabusu
hao
wanashitakiwa kwa makosa
manne ya ugaidi na kesi yao
iko katika Mahakama ya
Kisutu jijini Dar es Salaam.
Washitakiwa wamekuwa
wa k i l a l a m i k a n a k u d a i
kwamba mashitaka hayo
ni ya bandia na kwamba
kilichowachongea ni
msimamo wao wa kuupinga
mfumo wa Muungano uliopo,
halikadhalika kupigania
Zanzibar irejeshewe
mamlaka yake kamili.
Wamekuwa wakidai kwamba
huo msimamo wao ndio
ulioikera serikali na kuifanya
iwabambikie mashitaka ya
ugaidi.
Katika nyakati tofauti,
walipofikishwa mbele ya
Mahakama, mahabusu
h a o wa l i e l e z a , b i l a ya
kubania, unyama wanaodai
kwamba walifanyiwa
wakiwa gerezani. Shutuma
hizo zimeenea nchini,
zinazungumzwa mitaani,
b a r a z a n i n a z i m e t a j wa
kwenye vyombo vya habari.
Inawezekanaje kwamba
Waziri Mkuu awe peke yake
asiye na fununu yoyote ya
shutuma hizo? Itakuwaje
mtu mwenye wadhifa wa
kuongoza serikali, kama
Makala
AN-NUUR
Makala
AN-NUUR
kukhusu aliyoyatenda
Sayyid Said bin Sultan kwa
mfano hausomeshwi kabisa
katika shule za Tanzania.
Badala yake yanayooneshwa
vitabuni na kusomeshwa
ni maovu matupu kukhusu
Waislamu. Anayesifiwa ni
Mwingereza peke yake.
Tumeonesha waziwazi
kuwa usomeshaji wa historia
Tanzania umejaa propaganda
za udini dhidi ya Uislamu,
na Waswahili na Waarabu
wa n a t u m i wa t u k a t i k a
propaganda hizo. Hili liko
wazi kabisa kuwa miongoni
mwa wale waliopewa jukumu
la kuandika vitabu vya
historia vinavyofundishwa
m a s h u l e n i Ta n z a n i a
hawakuitendea haki ile
dhamana waliopewa na
wameonesha unafiki na
chuki zao za wazi kabisa
dhidi ya Uislamu, Waislamu,
Waarabu na Waswahili, na
wa m e o n e s h a wa z i wa z i
mapenzi yao juu ya siasa kali
za udini ambazo ukiziangalia
utaona hata hazilingani na
mafunzo ya Yesu.
Ili kuhakikisha uongo
huu na fitna hii inatapakaa
na kuganda katika bongo
za wanafunzi, basi kila
sehemu ilipotajwa utumwa
na kuoneshwa picha utaona
picha hiyo ni ya Mwarabu
au ya Mwafrika Mwislamu
ili kuonesha taswira ya kuwa
watendaji wa uovu huo si
wengine bali ni Waislamu.
Ingawa waandishi wa vitabu
kama hicho cha Historia cha
Form Two, Perazia Kaloly, na
Felix Kiruthu wamesisitiza
katika jalada la mwisho
la kitabu hicho umuhimu
wake wa kuweka michoro
ili kuonesha uhalisia thabiti
wa kitendo au tokeo lile,
wameandika yafuatayo:
Ilustrations and
photographs throughout
the book to depict authentic
situations.
Tafsiri: Michoro na picha
katika kitabu chote ni
kuonesha uhalisia thabiti wa
matokeo.
Inasikitisha kuona baadhi
ya picha zilizomo vitabuni
ama zimeghushiwa au zile
za matokeo yaliyobuniwa
ambayo kwa hakika
hayakutokea kabisa Afrika
Mashariki, na hata Afrika
kwingineko, bali zimeingizwa
kwa makusudi kwa lengo la
kupotosha ukweli na hapana
shaka zitakuja kuleta chuki
na mifarakano katika jamii,
kama si leo, basi karibuni.
Waandishi hao wa vitabu
hivyo vya shule vya historia
wamesahau kuwa tunaishi
katika ulimwengu ambao
umepevuka kimtandao
wa khabari, na ni rakhisi
mtu kugundua kila
lililoghushiwa. Nitanakili
picha nyingine ziliomo
vitabuni na mukhtasari wa
Makala
AN-NUUR
Makala
AN-NUUR
N AYATA FA K A R I m a j i b u y a
kiongozi mtendaji mkuu wa serikali
alipoulizwa swali bungeni akitakiwa
kutoa msimamo wa serikali kuhusu
kadhia ya masheikh na maulamaa wa
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya
Kiislamu (JUMIKI) wanaolalamika
kudhalilishwa ndani ya magereza
kiasi cha kutishia kuanzisha mgomo
wa kula.
Swali lililoulizwa kwa zaidi
ya sekunde 240, muulizaji akitoa
maelezo ya kina na kwa ufasaha,
linajibiwa kwa chini ya sekunde 150,
mjibuji akitoa kauli tata, zisizotoa
mwelekeo wa kutegemewa kuleta
utatuzi wa malalamiko.
Mara nyingi imetokea nikamsikia
kwa mashikio yangu Waziri Mkuu
Mizengo Kayanza Peter Pinda
akitoa maelezo yanayozua utata na
kusababisha mjadala mkali, lakini
sikufikiria kuwa kiongozi huyu
atafikia hatua ya kutoa matamshi
ya n a y o m v u a u a d i l i f u n a m n a
nilivyomshuhudia hivi karibuni. Na
kwa sababu nimekuwa nikimfuatilia
kauli zake na kuzipima, mantiki
ninayoipata binafsi na hapo hapo
nikitafakari kile alichokusudia
k u k i e l e we s h a a u k u d h a m i r i a ,
mantiki hiyo ndiyo anayotaka
igande sawasawa akilini mwa
wale wanaomsikiliza wakati huo
anapozungumza, na umma kwa
ujumla wake. Sasa nafika hatua
kujiuliza maswali ambayo sipati
majibu.
Waziri Mkuu Pinda, yule ambaye
alipoteuliwa tu kushika wadhifa huo
Februari 2008 aliliambia bunge kuwa
yu mtoto wa mkulima, akimaanisha
anatoka kwenye familia masikini,
naona amebadilika sana. Akiwa
aliyeanza vizuri na kwa umakini
utaratibu wa kuulizwa maswali
ya papo kwa papo bungeni na
kuyajibu kwa ufasaha, katika kipindi
cha karibuni, Waziri Mkuu Pinda
amekuwa kiongozi tofauti kabisa na
vile alivyojitokeza na kujionesha siku
hizo za mwanzo za uteuzi wake.
Waziri Mkuu Pinda amekuwa
mjanja badala ya Mtu makini. Mtata
badala ya kiongozi mnyoosha mambo
hasa anapoulizwa jambo lililojaa
utata, kila anapozungumza. Kiongozi
asiyetabirika hata pale unapotarajia
ajibu kwa ufasaha na umakini
akitumia maneno machache kuhusu
kile alichoulizwa.
Pengine Waziri Mkuu Pinda ni
kweli kama wasemavyo baadhi ya
ninaokutana nao tukamuongelea,
amekuwa ni muoga kiuongozi. Na
labda amekuwa hivyo kwa sababu
amejifunza katika miaka yake saba
ya wadhifa anaoshika, ukitaka
kuishi na mfumo wa uongozi wa
serikali inayoongozwa na Chama
Cha Mapinduzi (CCM), basi nawe
uwe muoga, usiyeaminika na mtu
dhaifu usiyetabirika. Hapo ndipo
Waziri Mkuu Pinda huyu tunayemjua
alipojifikisha. Nami namuona amefika
hapo hasa. Ndivyo watu hata wa
kawaida, achilia mbali wale wenye
weledi katika kuyatafakari mambo
yanavyokwenda ndani ya jamhuri
yao, wanavyomtathmini.
Watu hawa wa kawaida, ambao
RAIS Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto).
Katikati ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal.
mtu ungetarajia ndio mheshimiwa
angewashinda nyoyo zao katika
kumuamini na kumtetea anapojikwaa,
wanamuona Pinda amekengeuka
hata ile taswira ya kuwa ni mtu
makini, muadilifu na asiye na
makuu, aliyoijenga pale mwanzoni
alipoteuliwa. Siku wananchi hao hao
waliokuwa wamejenga imani naye,
wanamtizama kivingine kabisa.
Siku hizi tunazoenda na pengine
inachochewa na mwelekeo wa
uchaguzi mkuu wa Oktoba, Waziri
Mkuu Pinda amekuwa kiongozi
asiyeeleweka. Ni kama vile amesahau
jukumu la Uwaziri Mkuu. Wala
haoni vibaya tena kukwepa swali
la mbunge. Amekosa hata huruma,
kama vile alisahau alivolia bungeni
kuhusu mauaji ya watu wenye
ualbino.
Shida inakuja zaidi anapoulizwa
bungeni na mbunge wa kambi
rasmi ya upinzani, siku hizi ikiwa
imekolezwa mvuto na UKAWA
Umoja wa Katiba ya Wananchi usoni
anaonesha, siwezi kusema jeuri,
lakini labda kutokujali, na akianza
kujibu huanza kwa kejeli.
Ndivyo alivyosomeka alipoulizwa
na Mbunge wa Mji Mkongwe,
Muhammed Ibrahim Sanya wiki
iliyopita. Aliulizwa kama serikali
inaweza kuunda Tume ndogo
itakayoshirikisha pia wabunge
kutoka Zanzibar na Tanganyika,
kuchunguza malalamiko ya kuhusu
kinachoelezwa kama kesi ya tuhuma
za ugaidi inayowakabili viongozi
wa Uamsho, pamoja na vijana wao
wanaosaidia harakati za kuelimisha
Waislam juu ya haki zao zikiwemo za
kujihusisha na mambo yenye maslahi
na nchi yao.
Katika siku hii ya Alkhamis,
Mei 21, kama kawaida, ukumbi wa
bunge ulikuwa kimya wakati Mama
Spika Anne Makinda alipomuita
10
Makala
AN-NUUR
PICHA juu Msikiti wa Al Aqsa uliopo Jerusalem. Qubba (Dome of the Rock)
na Waislamu, na Msikiti
huo unaonekana
mnara wake wa rangi
ya dhahabu yenye
kupendeza kabisa. Sasa
Wayahudi mbinu zao
kubwa ni kuufanya
Msikiti huo uwe ndio
Msikiti wa Alaqsa na
ufahamike hivyo kwa
dunia nzima, ikiwa mie
na wewe vile vile tujuwe
hivyo.
M t e g o
h u o
umetuangukia na utaona
hata post card nyingi
zenye kutengenezwa na
Waislamu hutoa picha
ya msikiti wa Qubat
S a k h r a b a d a l a ya
Msikiti wa Al Aqsa.
Katika kipindi
ambacho Kiongozi wa
ki-Palestina Yasir Arafat
amezungukwa na kabla
ya kupewa uhuru wake
wakuondoka huko
Ramallah, television
nyingi duniani ikiwa
pamoja na za nchi za
Kiislamu zimekuwa
zikionyesha Msikiti
wa Qubat Sakhra
na kutoonyesha Qibla
cha mwanzo ambacho
Waislamu katika zama
za Mtume Muhammad
S . A . W wa l i p o k u wa
wakielekea nacho ni
Msikiti wa Al Aqsa. Huu
ni upotoshaji na kuna
haja kwa kila Muislamu
kuuelewa ukweli na
baada ya kuufahamu
ukweli akamfahamisha
mwenzake na kujuwa
hakika ni upi Msikiti wa
Al Aqsa na umuhimu
wake.
Wachache ndio wenye
kuelewa juu ya uhakika
wa Msikiti wa Al Aqsa na
ukweli ulivyo. Waislamu
wamepotezwa na
wamepotea na mara tu
M ayahudi watapotaka
kuitekeleza azma yao iliyo
ovu ya kuubomoa msikiti
wa Al Aqsa, Waislamu
wataona kuwa Msikiti wa
Al Aqsa upo na nini tena
cha kupiga kelele?
Hivi karibuni Wayahudi
wenye misimamo mikali
walikuwa na azma ya
kutaka kuuharibu na
kuubomoa Msikiti wa
Alaqsa lakini juhudi hizo
ziliweza kugundulikana
na mapema na vijana
shupavu wa Kiislamu
waliojitolea kupambana
na udhalimu na uharamia
wa Mayahudi wenye siasa
kali na kuweza kufanikiwa
kuizima dhana nzima ya
ufisadi huo.
Jambo
ambalo
lakusikitisha habari hii
ya k u t a k a k u v u n j wa
kwa msikiti wa Al Aqsa
haijaelezwa na vyombo
vya habari vya Magharibi
a m b a v y o n d i o wa t o a
habari wakuu na wenye
propaganda duniani kote.
La kushukuriwa ni kuwa
sio haba Waislamu nao
wameingia na kufanya
kazi katika Tekenolojia
ya habari Information
Technology na moja ya
mashirika ya Kiislamu
lilokuwa mstari wa
mbele kuzieleza habari
hizi ni International
Islamic News Agency.
Tutahitajika tufanye kazi
kubwa ya kuelimishana na
kuamshana juu ya khatari
iliyopo duniani kote katika
kuupiga vita vya dhahiri
na vya nadharia Uislamu
ili uwe dhaifu kama ulivyo
hivi sasa Ukoministi. La
kuwazindua maadui
hao ni kuwaambia kuwa
jitahada zao ni kubwa
lakini Allah ameahidi
kuwa ataulinda Uislamu na
ndio maana juhudi nyingi
zifanyazwo kuuangamiza
Uislamu unashindikana
n a h a u t a f a n i k i wa n a
matokeo yake kila kukicha
kunaonekana Uislamu
kuweza kupata nguvu.
Kutoka tokeo la
September 11 na
kuangushwa kwa serekali
ya Ta l i b a n ! t a k w i m u
zilizokuwa bado
hazijathibitishwa lakini ni
zenye kuaminika ni kuwa
zaidi ya watu nusu milioni
duniani kote wamesilimu
na hili ni tokeo kubwa kwa
watu wengi kuukubali
Uislamu kwa mara moja
tangu zama za Bwana
Mtume Muhammad
S.A.W.
Ewe Mola tufungulie
yalio ya haki na haki
tuijuwe na batil tuielewe
na tuiepuke AMIN
11
Makala
AN-NUUR
Mafundisho ya Quran
Fethullah-Gulen
WANAFIKI wametajwa
katika Quran kwamba
wa o : H a l i ya k u wa
wanayumba kati ya hilo
hawahusiki na hawa na
hawahusiki na hawa.
[A-Nisaa 143].
Maana wanayumba kati
ya waumini na kati ya
makafiri. Mara utawaona
huku na mara utawaona
huko wanasumbuwana na
WAARABU walitokana
na Nabii Ismail na
Wayahudi walitokana na
Nabii Is-haq. Kwa hiyo
Waarabu ni mabinamu
wa Wayahudi. Isikize
Biblia inavyotuambia juu
ya ndugu hawa-Waarabu
na Wayahudi:
Yale maji, ambayo
Ibrahimu alimuachia
Hajiri (Hagar) na mwana
wao Ishmaeli yakaisha
katika kiriba, akamlaza
kijana (Ishmaeli) chini
ya kijiti kimoja. (Hajiri)
Akaenda akakaa
akimkabili (Ishmael) mbali
naye kadiri ya mtupo wa
mshale, maana (Hajiri)
alisema, Nisimwone kijana
(lshmaeli) akifa (kwa kiu),
naye akakaa akimkabili,
akapaza sauti yake, akalia.
Mungu akasikia sauti ya
kijana (Ishmaeli). Malaika
wa Mungu akamwita
Hajiri kutoka mbinguni,
akamwambia una nini
Hajiri? Usiogope, maana
Mungu amesikia sauti ya
kijana (Ishmaeli) huko
aliko (Ewe Hajiri, hebu)
Ondoka ukamwinue kijana
(Ishmaeli), ukamshike
mikononi mwako, Kwa
kuwa nitamfanya kuwa
taifa kubwa (la Waarabu).
Mungu akamfumbua
m a c h o , n a ye a k a o n a
kisima cha maji (Zamzam)
akaenda akakijaza kiriba
maji, akamnywesha
kijana. Mungu akawa
pamoja na huyo kijana
kunyimwa mwangaza wa
macho yao na mwangaza
wa hisia zao na kuelewa
kwao. Kisha kwa hakika
wao kwa sababu ya kuwa
kwao wanadhani kwamba
maisha yamethibitika
katika maisha haya ya
dunia, tunawaona wamo
katika joto la kubobea juu
ya ladha za hii dunia.
Kwa hiyo, kuamini na
kukufuru kuko sawasawa
mbele zao. Mahali popote
ambapo starehe na
maisha laini yenye raha
yanapatikana, wanafiki
wa t a k we n d a k w e n y e
m a i s h a h a y o . Wa k a t i
wanapoona kwamba
maslaha yao yamo
katika kwenda Msikitini,
wanakwenda msikitini (Ila)
Na pindi wanaposimama
kwenda kwenye swala,
wanasimama hali ya kuwa
wavivu wanawaonyesha
watu. [A-Nisaa 143].
Aya ya Kumbukumbu
la Torati (Deuteronomy)isemayo:
Naye
(Musa)
alikuja kutoka Sinai.
Akawaondokea kutoka
Seiri kuja kwao; Aliangaza
kutoka kilima cha Parani,
na alikuja na watakatifu
elfu kumi. Kutoka
katika mkono wake wa
12
Tangazo/MASHAIRI
AN-NUUR
KHATMA YA MAFATANI
GHURURI YA 'VUNJAJUNGU'
TAMASHA LA KITAIFA
ILONGO MBEYA
05 12 JUNI , 2015
13
MAKALA
AN-NUUR
Inatoka Uk. 7
waliokuwa Bara wala
kuwasafirisha kutoka
Bara ndani mpaka pwani
wala kuwa madalali wa
biashara ya watumwa. Wao
walichokifanya ni kununua
watumwa walioletwa na
Waafrika kutoka Bara kwa
ajili ya kulima mashamba
ya mikarafuu, na kuelezea
ukweli ni Waarabu wachache
wa l i o m i l i k i m a s h a m b a
hayo. Wengi wao, kama
tulivyoonesha kabla,
walikuwa watu wa kawaida
waliokuwa wakipigana na
maisha na hadi kufanya kazi
ngumu pia.
Picha hii ya pili inaonesha
kuwa muuzaji, wamiliki na
wanunuzi wa watumwa ni
Waarabu Waislamu:
Tukiweka upande kuwa
hayo mavazi waliyovishwa
hao Waarabu pichani si ya
wale waliokuweko Afrika
M a s h a r i k i , ya a n i s i ya
Wayemen na Waomani.
Inasikitisha kuona jinsi
vile propaganda za udini
na chuki za waandishi na
mchoraji zilivyowapelekea
hata kuwafanya kuwa vipofu
wasione ukweli na haki. Soko
gani la utumwa katika Afrika
Mashariki lililokuwa lina
Waarabu peke yao ambao
ni wamiliki, madalali na
wanunuzi wa watumwa?
Wanataka kumdanganya
nani leo kuwa Waafrika na
wengineo hawakuwemo?
Wanataka kumdanganya
nani isipokuwa masikini
watoto wadogo wa shule,
kuwa wanunuzi wa
watumwa wakati ilipokuwa
ikifanywa biashara hiyo
walikuwa Waarabu peke
yao? Ukweli ni kuwa biashara
hiyo iliwagusa wachache
kutokana na makabila karibu
yote yaliyokuwa yakiishi
Z a n z i b a r n a P wa n i ya
Afrika Mashariki, wakati
ule wakiwemo Wazungu,
Wahindi, Waarabu, Waafrika,
Washirazi na kadhalika.
Jonathon Glassman ametuelezea:
Tafsiri: Zaidi ya hivyo,
v y o v y o t e v i l e u t u m wa
katika Zanzibar ulivyokuwa
ukionekana wakati wowote
ule, kulikuwa hakuna
chochote kile kinachoufanya
kuwa ni wa Kiarabu,
wamiliki wengi wa Watumwa
walikuwa Waafrika.
Akaongeza:
Ta f s i r i : K wa m a n e n o
mengine, kinyume na historia
za kigozi za Utumwa wa
Kiarabu ambao ulilenga
khasa kuondosha utumwa,
we n g i wa wa m i l i k i wa
watumwa walikuwa hawana
m u j i b u wa m a e l e z o ya
Stanley. Jiulize: Kwa nini
mchoraji hakuwaonesha
wauzaji na wanunuzi wa
Kiafrika na wanunuzi wa
makabila mengine? Kwanini
wakamataji/wamiliki,
madalali na wanunuzi wote
wawe ni Waarabu tu peke
yao?
Ni muhali katika
soko la nchi ambalo lina
mchanganyiko wa makabila
mbalimbali sokoni pale
upate watu wa aina moja tu,
hapo juu tunaona watumwa
ni Waafrika, muuzaji ni
Mwarabu, dalali ni Mwarabu,
na wanunuzi ni Waarabu
hii haiingi akilini. Lakini
kuchora yanayoingia akilini
si shabaha ya wenye lengo lao
lisilokhusiana na kuelezea ya
kweli, na hawa ni pamoja na
wafuasi wao ambao hurejelea
propaganda kikasuku bila
ya k u p i m a u k we l i u k o
wapi na bila ya kutumia
akili zao na bila ya kutumia
uadilifu. Madam hadafu yao
inawaelekeza kuwanyooshea
kidole cha lawama Waarabu
Wa i s l a m u p e k e ya o i l i
walifikie lengo lao, basi
hivyo ndivyo wafanyavyo,
na potelea mbali iwapo
wanaunyonga ukweli na
harufu ya mzoga wa uwongo
ikaenea ulimwenguni.
L e n g o l a o wa a n d i s h i
na wachoraji wameliweka
wazi wenyewe na lengo
hilo si kuelezea au kuchora
yaliyokuwa ya kweli, bali
kutapakaza propaganda
za chuki. Ukweli huingia
akilini katika bongo za wenye
kutumia akili zao. Utapakazaji
wa chuki hutokana na wale
wasioipendelea nchi yao
wema na salama kwani chuki
mwisho wake ni khasama na
uvurugaji wa nchi. Tanzania
leo ina matatizo mapevu na
mivutano ya siasa mbovu
za udini inayotokana na
propaganda chafu kama
hizo zenye kupalilia
mtafaruku. Sidhani kama
kuna Mwislamu yoyote leo
atakayekubali mwanawe
asomeshwe shuleni kuwa
ni wavyele wake tu ndio
waliofanya kila ovu kuanzia
ukamataji wa wanyonge
wa Kiafrika Bara, kuwauwa
idadi kubwa ya wanyonge
hao, kuwafunga minyonyoro,
kuwapakia pembe nzito za
ndovu, na wanapokhalifu
a m r i k u wa p i g a m b o k o ,
kuwaendesha kwa miguu
m p a k a p wa n i , k u wa t i a
mnadani, kuwauza
n a k u wa s a f i r i s h a n c h i
mbalimbali.
Inatoka Uk. 8
ulioshindwa kuwasaidia kwa
miaka mingi, basi wanatafuta
mbadala wake, lakini cha
ajabu baadhi ya Waislamu
wanaotumikia mfumo huo,
b a d o wa n a u r e m b a k wa
Waislamu mfumo ule ule
uliowaangusha! Mfumo
ambao wanajua unapiga vita
Uislamu!
Na nukta ya mwisho,
ningependa kuangazia
zaidi ushiriki wetu katika
siasa kama Waislamu na
maadili ya dini yetu. Baadhi
ya Waislamu wanaamini
k wa m b a u s h i r i k i we t u
kwenye mfumo wa siasa za
kisekula utatuletea manufaa,
ikiwa ni pamoja na kusaidia
kuondoa chuki iliyojengeka
dhidi ya Uislamu. Hawa
wako tayari hata kuvuka
mstari mwekundu na kuunga
mkono Ilani za vyama vya
kisekula kwa matumaini
hewa kwamba jamii ya
Waislamu inaweza kunufaika,
ingawa wanafahamu vizuri
kwamba vyama hivyo
vinapinga Uislamu kwa
asilimia mia moja. Ndugu
zangu katika Imani, si tu
kwamba jambo hilo siyo
14
Makala
Na Ben Rijal
Na Ben Rijal
ABU Nasr Muhammad
al- Farabi ni katika
vigogo wa Kiislamu
aliotopea katika
ilimu katika karne
ya tisa. Alikuwa
g w i j i wa k u e l e wa
lugha mbalimbali
na ndio aliosaidia
kueleweka nadharia
za Wanafalsafa wa
K i y u n a n i Pl a t o n a
Aristotle katika
ulimwengu wa
Kiislamu. Aidha ni
Al-Farabi aliompa
mvuto mkubwa
gwiji mwengine wa
Kiislamu kwa jina Ibn
Sina.
A l i ya f a n z i a k a z i
kubwa falsafa za
Plato na Aristotle na
k u we z a k u z i p a n u a
zaidi na kuweka fikra
zake. Kutokana na
umahiri wake wa ilimu
ya Falsafa, akaitwa
jina la utani Mallime-Sani ikimaanisha ni
anayofwatia bada ya
Plato na Aristotle.
Al-Farabi alizaliwa
mwaka wa 870 ikiwa ni
karne ya 8 na kufariki
mwaka wa 950 ikiwa ni
karne ya 10. Al-Farabi
alifanya kazi nzito
katika uga wa Falsafa,
lakini bahati mbaya jina
lake halikungaa kama
lilivyokuja kungaa
jina la Ibn Sina ambaye
gwiji huyu Ibn Sina
alimsoma vya kutosha
Al-Farabi na kujaribu
kuzifwata nyayo zake.
Al-Farabi katika ilimu
ambazo akizichezea
na kuzisarifu ilikuwa
falsafa, mantiki na
Fatilia
kuandama kwa Mwezi
Leo Ijumaa ni tarehe 17 Shaaban 1436
wawili wakiwa
Aristotel na Napoleon.
Kwa kuzichanganya
na kuingiza fikra zake,
ndipo waliokuja baada
yake kama Ibn Sina,
Yahya ibn 'Adi, alSijistani, al-'Amiri na alTawhidi kutekwa katika
falsafa ya Al-Farabi
mbali ya Wanafalsafa
wa Kiislamu hata gwiji
la Falsafa aliokuwa
Mkiristo wa huko Ulaya
Thomas Aquinas
Maisha yake
Jina lake khasa ni
Abu Nasr Muhammad
ibn Muhammad ibn
Tarkhan ibn Awzalagh
al-Farabi. Ingawa
baadaye Ibn Sina alikuja
kumfunika, lakini Ibn
Sina ujuzi wote kautoa
katika kumsoma AlFarabi. Ibn Sina alijaribu
kumsoma Aristotle
kuweza kufahamu juu
ya misingi ya kuhoji
na kuja na nadharia
ya falsafa ya Aristotle
ilimwia ugumu
kufahamu juu ya fani
hio (Metaphysic).
Lakini alivyosoma
maandiko ya Al-Farabi,
aliweza kuelewa kwa
urahisi kabisa. Ibn Sina
aliandika mwenyewe
juu ya maisha yake
na ndio ikapelekea
kufahamika zaidi na
maelezo juu ya maisha
ya k e k u t o k u wa n a
utata.
Al-Farabi ni kizazi
cha Mapersia. Alizaliwa
Turkestan na kuhamia
Baghdad kwenda
kujifunza lugha ya
Kiarabu na inafahamika
kuwa vitabu vyake
vyote aliviandika
akiwa yupo Baghdad.
Katika kupendelea
kujifunza na kufanya
tafiti, alisafiri na kuzuru
nchi nyingi na miji
ikiwemo Damascus,
Egypt, Harran and
Aleppo. Hapa Aleppo
kuna mengi ya kuacha
athari. Lakini Dola
Islamiyah (ISIS) kwa
sasa wanabomoa na
kuondosha alama
zote zenye athari za
Kiislamu.
A l i k u w a
akizungumza lugha
n y i n g i n a we n g i n e
wamefika kusema kuwa
zinafika hata zaidi ya 30
kitu ambacho kigumu
kuingia akilini. Juu ya
hayo katika miji yote
aliofika akakaa, basi
muda mfupi akiweza
kuzungumza lugha
ya mahala hapo.
Alipofika katika safari
zake katika mji wa
Hamdani mtawala wa
hapo baada ya kuelewa
uwezo wa kiakili na
ilimu wa Farabi, alikuja
kumfanya kuwa ndio
mtu wake wa karibu.
Maisha yake
yanaelezewa kinamna
yake, kwani hata
alivyomalizia uhai wake
wengine wanaelezea
kuwa alifariki kifo cha
kawaida na wengine
wanaelezea kuwa
alipokuwa katika safari
zake, alihujumiwa na
majambazi na kuuwawa
alipokuwa anatoka mji
wa Damascus kuelekea
Ascalon.
Baadhi ya kazi zake
ni kitabu cha muziki
cha Kitab al-musiqa
al-kabir, kitabu kizito
ambacho ndio AlFarabi ni al-Madina
al-fadila na al-Madina
al-fadila ndio yeye,
kwani bila ya kuandika
kitabu hiki, Al-Farabi
angekosa umaarufu
aliokuja kuupata na
kuzungumzwa. Kitabu
kimoja chenye vitabu
vingi ndani yake
ambacho alikiandika
ni Risala fi'l-'aql. Hiki
a l i k u wa a n a e l e z e a
juu ya ufahamu na
uhodari anaokuwa nao
mwanadamu. Kisha
akaandika kitabu juu
ya maandishi Kitab alhuruf na Kitab ihsa'
al-'ulum.
Falsafa ya siasa
Al-Farabi katika alMadina fadila hapa ndio
unamkuta anakwenda
sambamba na nadharia
za Plato. Unaposoma
Sura ya 1 hadi ya pili na
Sura ya 3 hapa unakuta
anapowachanganya
watu juu ya maelezo ya
maumbile na uongozi
uweje. Hapo anaielezea
roho inavyokuwa na
inavyomuelekeza
mtu, yeye mwenyewe.
I n a f a h a m i k a k u wa
alikuwa mtu wa
miraba minne mwenye
maguvu. Akipenda
kusoma na alikuwa na
kumbukumbu iso ya
kawaida. Akihangaika
katika Uungu na
AN-NUUR
kumpoteza katika
imani ya Kiislamu na
wengine, yeye na Ibn
Sina wamefika kusema
na kuwakufurisha kuwa
sio Waislamu kutokana
na maandishi yao khasa
katika Tawhid.
Katika hali ya kijamii,
Al-Farabi aliigawa jamii
katika mafungu 3, ikiwa
iliokamilika akiweka
kutokana na ukubwa
wa waliopo katika jamii
hio. Kisha akaelezea
j u u ya m i j i i l i o n a
utulivu na kupendeza.
Hapa kaandika kwa
upana juu ya miji hiyo
namna ilivyo na namna
inavyotakikana iwe.
Kisha akaandika juu
ya miji minne iliyo
ndani ya kukamatana
na rushwa. Akaielezea
miji ya wapumbavu almadina al-jahiliyya, miji
iliojaa ufuska -madina
al-fasiqa, miji iliyo na
mahaini, al-madina
al-mubaddala na miji
iliyoenda mrama almadina al-dalla.
Akafahamisha kuwa
wakaazi wa miji hio
mwishowe hupotea na
kutodhukuriwa tena.
Katika miji ya wala
rushwa, Al-Farabi
alielezea kutokana na
maandishi ya Plato na
kama utasoma nadharia
hizo, basi utaona AlFarabi maandishi yake
hayo kayaandika jana.
Al-Farabi alipendeza
sana katika ulimwengu
wa Ulaya na kupewa
mgongo na Waislamu.
M b a l i ya I b n S i n a ,
aliwaathiri nadhari zake
wasomi kama Yahya ibn
'Adi, Abu Sulayman alSijistani, Abu 'l-Hasan
Muhammad ibn Yusuf
al-'Amiri na Abu
Hayyan al-Tawhidi.
Na hao ndio waliokuja
kuita taaluma yake na
kuiweka katika Chuo
cha Al-Farabi.
Ya h y a i b n A d i
alikuwa Mkristo
anayeamini kuwa
Mungu ni mmoja.
Alikuwa kati ya
wanafunzi wa AlFarabi katika mji wa
Baghdad. Yahya alijikita
zaidi katika mantiki na
kuja kujikuta akipenda
kufahamu imani
ya kitu na siasa. AlSijistani huyu alijifunza
vya kutosha ilimu ya
mantiki kwa Al-Farabi
mpaka kushindwa
kuwatenganisha
m w a l i m u
n a
mwanafunzi.
Kwa wanafunzi
wa Falsafa, ni vyema
wakavipitia vitabu hivi
vya Al-Farabi navyo
ni: al-Madina al-fadila
(Juu ya miji na uzuri
wake) au Abu Nasr
al-Farabi's Mabadi'
Ara Ahl al-Madina alFadila. Kitabu chengine
ni Risala fi'l-'aql, Kitab
al-huruf, Kitab ihsa'
al-'ulum, Kitab almusiqa al-kabi. Vitabu
hivi vimefasiriwa kwa
Kiengereza na lugha
nyenginezo.
Waandishi wa kigeni
kama Alon, I. Black,
D, Galston, M, Netton,
I.R., wamemuandika
na kumnukuu kati
ya vitabu vyake na
kumweka juu baada ya
Plato na Aristotle.
Tafsri ya Kitab ihsa'
al-'ulum ilioandikwa
kwa lugha ya Kilatino
na Gerard wa Cremona.
15
Makala
AN-NUUR
Na Mwandishi Maalum
WA H E N G A w a
Waswahili walipata
kusema; Watende wao,
wakitenda wenzao,
huwa mwao!
Msemo huu utakuwa
kiini cha mjadala
wangu katika makala
hii inayonisukuma
kuandika mada yenye
k i c h wa c h a h a b a r i
kinachoonekana na
kusomeka hapo juu.
Kwa nini naandika
hivi? Wacha kwanza
niwarudishe kwenye
historia fupi.
Inafahamika
UWANJA WA VIJANA
JIONGEZEE MAARIFA
Jee unajua?
wa c h a m a t a wa l a ,
walijaribu kuiteremsha
bendera ya CUF
iliyokuwa imepachikwa
pale na mwanachama
mmoja wa chama hicho.
Hoja yao kuu ya kutaka
kuishusha bendera hii
walidai kuwa hawataki
CUF katika kijiji chao.
Hivi hii ni hoja sahihi
kisheria?
Nini basi kilitokea?
Mwenye bendera ya
CUF alipoona wanakijiji
wanataka kuishusha
bendera, alitoka na
panga akawaonya kuwa
atakayesogea kuishusha
bendera hiyo, atakiona
kilichomfanya punda
asiote nundu. Kifo
si swahiba mwema.
Wa k e r e k e t wa wa l e
walipoona hali
imekuwa ngumu,
waliita Polisi. Polisi
walipofika walipiga
risasi juu na kumtishia
mwenye kupachika
bendera. Akakimbia.
H a p o k wa m s a a d a
wa Dola, bendera ya
CUF ikashushwa juu
ya mlingoti na wana
CCM-DOLA wa Kwale.
H a b a r i
h i i
ilipowasilishwa
bungeni siku iliyofuata,
wahusika wote
wa k a c h u k u l i wa n a
Polisi na kuswekwa
rumande huko
We t e . K a t i ya h a o
waliokuwamo ni
Afisa Elimu Wilaya ya
Micheweni Mbwana
Shaame Hamad, Afisa
wa Tume ya Uchaguzi
Wilaya ya Micheweni
Bwana Khamis
Massoud na Mwalim
Mkuu skuli ya Shumba
mjini Mwalim Bakari.
Kuwekwa ndani kwa
wana dola hawa ambao
wanashika nyadhifa
nyeti za Serikali,
hakukudumu masaa.
Siku ya pili tu tangu
watiwe mbaroni, kauli
ilitumwa kwamba
watolewe mara moja.
Wa t u h u m i w a h a o ,
wakaachiwa huru
huku ikisemwa kesi
yao itasikilizwa wakiwa
nje kwa dhamana.
Wananchi wenzangu,
hebu tukae chini
tutafakari: ingekuwa
waliofanya jaribio hili
ni waumini wa chama
chengine au tuseme
wapinzani, ingekuwaje?
Jawabu utakalolipata,
malizia na ujumbe
wangu:
Wa t e n d e w a o ,
wa k i t e n d a we n z a o
huwa mwao! Na kwa
hali kama hii - Je,
tutafika?
16
SAUMU kilugha ni kujizuiya
na kitu, yaani kutofanya kitu
fulani; kama ilivyo kwenye
Qurni Tukufu:
"Hakika mimi nimeweka
n a d h i r i k wa M we n ye z i
Mungu ya kufunga; kwa
hivyo leo sitasema na mtu".
(Maryam : 26).
Kisharia Saumu ni kujizuia
kula, kunywa na matamanio
ya utupu; tangu alfajiri mpaka
kutua jua pamoja na kutia nia
ya hio saumu.
Hivi kutia nia ni kwa qauli
ya Mtume wetu Mpenzi
s.a.w. kwa kukhusu kila
ibada, yaani kutimia ibada
ni kuwepo na kutimia nia:
"Hakika ya kila kitendo ni
kwa nia yake".
Hukmu Yake: Saumu ni
nguzo ya nne kati ya nguzo
tano za Uislamu. Kulazimika
saumu kumekuja kwa
Qauli ya Mwenyezi Mungu
Mtukufu, na kufasiriwa
kwa qauli ya Mtume wetu
Mpenzi s.a.w. na wanazuoni
wakawafiqiana juu ya hili.
Amesema Mwenyezi Mungu
Mtukufu:
"Enyi mlio amini!
Mmeandikiwa Saumu,
kama waliyo andikiwa walio
kuwa kabla yenu ili mpate
kuchamngu. (Al Baqara :
183).
Na Mwenyezi Mungu
Mtukufu amesema:
"Basi ataye kuwa
mjini katika mwezi huu
naafunge.......".(Al Baqara :
185).
Na Hadithi ya Mtume
wetu Mpenzi s.a.w.:
"Umejengwa Uislam juu ya
(Nguzo) tano".
Katika nguzo tano hizo,
ikatajwa nguzo ya nne kuwa
ni Saumu ya mwezi wa
Ramadhani.
Mtu alimuomba Mtume
wetu Mpenzi s.a.w.
amfahamishe saumu
alioifaridhisha Mwenyezi
Mungu Mtukufu juu yake.
Akasema Mtume wetu
Mpenzi s.a.w.: Saumu ya
Mwezi wa Ramadhani".
Saumu imewajibikishwa
juu ya Muislamu, baalegh,
mwenye akili kaamili,
mwenye uwezo wa kufunga.
Saumu haimuwajibikii Kafiri
wa asili, wala haisihi juu
yake Saumu, kwa vile yeye
si mwenye kuhisabika kuwa
ni katika wenye kufanya
ibada. Vilevile Saumu
haimuwajibikii mtoto
mdogo. Saumu haimlazimikii
mtoto, lakini mtoto
huzoeleshwa kufunga tangu
udogoni. Vilevile Saumu
haimuwajibikii mgonjwa wa
akili. Hivi ni kwa qauli ya
Mtume wetu mpenzi s.a.w.:
"Imeondoshwa kalamu
(kulazimika na hukmu za
Sharia) kwa watu watatu:
mwenye kulala mpaka
aamke, mtoto mdogo mpaka
a b a l e g h e , n a m g o n j wa
wa akili mpaka apowe".
(Imehadithiwa na Abu Daud).
Ama yule asieweza
kufunga, au kama
atafunga atapata madhara
ambayo hayatarajiwi, hivi
MAKALA
AN-NUUR
17
MAKALA
AN-NUUR
SHUKURANI zote
anastahiki Mwenyezi
Mungu na rehema na
amani zimfikie Nabii
Muhammad ( S. A.W.)na
sahaba zake.
Ibada
ambazo
ametulazimisha Mola
wetu mlezi haikuwa ni
jambo lolote isipokuwa ni
mazoezi ya vitendo katika
kuendeleza kuitangaza
amani kati ya viumbe
(watu) kwa mfano Swala
tunagundua kuwa ndani
yake kuna ukumbusho wa
vyanzo wa salam (amani)
katika sehemu nyingi
kwanza pale unaposema
tashahudi (Tahiyatu) haifai
swala isipokuwa atoe
Muislamu salaam.
Ajitolee yeye mwenyewe
na awatolee waja wa
Mwenyezi Mungu walio
pembeni yake (amani
iwe juu yetu na waja wa
Mwenyezi Mungu walio
wema) na kutoka katika
nguzo hii inakuwa kwa
kutoa salam ambayo ni
moja ya nguzo za swala
basi muislamu huimaliza
swala yake kwa kusema
((amani iwe juu yenu na
rehema za Mwenyezi
Mungu na baraka zake))
kuliani kwake na kushotini
kwake.
Hata kama atakuwa
anaswali peke yake
hakuna hata mtu mmoja
pembezoni mwake hii ni
kuendeleza vyanzo vya
amani katika maisha ya
watu na baada ya hapo
atatoka katika swala na
haruhusiwi kusimama
hadi aombe dua hii:
Ewe Mwenyezi Mungu
wewe ni amani na kwako
ndiko kunakotoka
amani basi tupe uhai
wa amani umetakasika
ewe mwenye Utukufu
na Ukarimu)) haya yote
hupatikana katika swala
ama katika funga ndani
yake kuna mazoezi ya
kimatendo katika kueneza
amani (salam) imehimiza
18
Makala
AN-NUUR
KUMBUKUMBU
Na Alhaj Abdallah
Tambaza
MWEZI kama huu miaka
minne iliyopita, Rais Jakaya
Kikwete ilibidi akatishe
ziara nchini Botswana na
kurudi nyumbani kuongoza
maelfu ya waombolezaji
jijini Dar es Salaam katika
mazishi ya mmoja wa watu
mashuhuri kupata kutokea
katika ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati. Alikuwa
bingwa wa usomaji Quran;
bingwa wa unajimu; bingwa
wa tiba asilia; mtaalamu wa
nyota (horoscope) na pia
mwanasiasa nguli.
Safari ya Sheikh Yahya
kusaka elimu ilihamia
Zanzibar. Kule alikwenda
kujiunga na Zanzibar
Muslim Accademy
iliyokuwa ikiongozwa na
Mudir (principal) kutoka
chuo cha Al-azhar Sharif cha
Misri, Sheikh Mohammed
Addahani.
Yahya hakupata nafasi,
kwa sababu kwa mujibu wa
mudir wa chuo, hakufikia
vigezo vilivyohitajika
kujiunga chuoni pale.
Akisimulia kisa hicho,
Sheikh Ahmed Haidar
Mwinyimvua, Imam Mkuu
wa Masjid Mwinyikheri,
Kisutu Dar es Salaam,
aliyekuwa mwanafunzi
chuoni pale anasema:
Yahya aliondoka zake,
lakini siku chache baadaye
Mudir Addahani aliisikia
Quran Tukufu ikisomwa
katika Sauti ya Unguja na
mtu ambaye hakupatapo
kumsikia kabla; alitaka
kujua alikuwa nani yule
aliyesoma Qurani kwenye
Sauti ya Unguja.
Akajibiwa, Ah! ni
yule kijana Yahya ambaye
ulimkataa kujiunga na
Accademy yako.
Alijiuma vidole, akasema
yalikuwa ni makosa, atafutwe
haraka aje kujiunga na chuo
mara moja, anasema Sheikh
Haidar.
Pamoja na Sheikh Ahmed
Haidar, wanazuoni wengine
mashuhuri hapa nchini,
ambao alikutana nao pale
Muslim Accademy Zanzibar,
ni Sheikh Harith bin Khelef
(aliyekuja kuwa Mufti na
Kadhi Mkuu Zanzibar ),
Sheikh Mohammed Ali
Gongabure, aliyetoka
Mbwera, Kusini mwa
Tanzania na Khamis Said
Khalfan wa Madrassa ya
Mtoni jijini Dar es Salaam.
Hapa pia, mwanafunzi
Ya h y a a l i k u m b a n a n a
m s u k o s u k o m we n g i n e ;
maana alikuja kumkosoa
Mudir Addahani, kwamba
alikuwa akiwapendelea
wanafunzi fulani fulani
katika utoaji wake wa maksi.
Alifukuzwa chuo
kwa utovu wa nidhamu.
A l i o n d o k a n a k we n d a
alikaribishwa na Mfalme
Hassan, ambaye pia
alipumbazika na sauti
nyororo yenye mvuto na
kuliwaza aliyobarikiwa nayo
hayati Sheikh Yahya.
Msomaji zingatia kwamba
halikuwa jambo rahisi kwa
mtu Mweusi wa wakati huo,
kusoma kwa kiwango cha
Sheikh Yahya, tena elimu
yote hiyo akiwa ameipata
nchini mwake.
Katika fani ya tajwiid,
S h e i k h Ya h ya a l i b o b e a
zaidi katika ihkami, njia na
mahadhi; akiwa mzuri zaidi
katika mahadhi ya bayati,
sika na razdi (usomaji wa
Qurani una namna namna,
kama vile za waimbaji
zilivyo na base, tenor, tango,
rhumba na blues).
Kuna majina mengine
alikuwa ameyabuni
mwenyewe kama vile, sika
ya B a g a m o y o a m b a y o
imethibitika kwamba
inapatikana Tanzania tu:
Ah! hiyo razdi gogo
hiyo ni bayati mama ...ehe!
ehe! hapo hebu rudia
tena hapo kidooogo!
Kila mara alisikika Sheikh
Yahya akisema wakati mtu
mwengine akisoma Qurani
na yeye ni msikilizaji.
Katika safari yake ya
Uarabuni, Sheikh Yahya
aliweza kupata fedha nyingi
sana kwa maendeleo ya
dini ya Kiislamu pamoja na
scholarships zizisokuwa na
idadi alizowapatia vijana
wengine kwenda kusoma
huko.
Ukiacha umaarufu wake
katika kusoma Qurani,
19
AN-NUUR
Makala ya Mtangazaji
AN-NUUR
20
MAKALA
20
AN-NUUR
E-mail:info@hajjtrust.or.tz
WAKATI mashambulizi
makali yanayofanywa na
ndege za kivita za Saudi
Arabia dhidi ya Yemen
yakiwa yanaingia katika
m w e z i wa k e wa t a t u ,
maelfu ya raia wa nchi hiyo
wameendelea kuuliwa na
wengine wengi kujeruhiwa
huku miundombinu ya nchi
hiyo ikiharibiwa kabisa.
Hata hivyo pamoja na
kutokea madhara hayo
makubwa, kinachoshangaza
wengi ni kwamba bado
hakuna hatua za uhakika
za kupatikana misaada
ya dharura wala jitihada
madhubuti za kumaliza vita
hivyo zilizochukuliwa na
UN, ili kunusuru maisha ya
waathirika wa vita hivyo.
Ripoti za masharika ya
kutetea haki za binadamu
na ya utoaji misaada ya
kibinadamu zinasema kuwa
hadi sasa watu zaidi ya
4,000 wamepoteza maisha
katika mashambulio hayo
ya kinyama, 1000 kati yao
wakiwa ni wanawake na
watoto.
Wakati hali ikiwa hivyo,
zaidi ya Wayemen 7000
wamejeruhiwa katika
mashambulio hayo na
wengi wakiwa ni watoto,
wanawake na wazee.
Miundombinu na makazi
ya raia pia hayajasalimika
na mashambulio hayo ya
nchi kavu, bahari na anga,
ambapo zaidi ya nyumba
1000 zimeharibiwa. Vituo
vya afya vilivyoharibiwa
katika mashambulio hayo
wa Mataifa imepangiliwa
kwa mujibu wa sheria za
kimataifa, misingi ya haki
za binadamu na kulinda
m a t u k u f u ya k i u t u n a
kimaadili dhidi ya nchi
zinazokanyaga misingi hiyo.
Hatua ya mjumbe huyo
maalumu wa Katibu Mkuu
wa umoja wa Mataifa ya
kutaka jeshi la Israel
liingizwe kwenye orodha
hiyo nyeusi, imechukuliwa
kwa kutegemea uchunguzi
uliofanywa na umoja huo
kuhusu jinai zilizofanywa
na jeshi la Israel katika
m a s h a m b u l i z i ya k e ya
kikatili ya siku 50 huko Gaza.
Matokeo ya uchunguzi
huo yametangazwa mwezi
wa Aprili mwaka huu.
R i p o t i ya u c h u n g u z i
huo wa Umoja wa Mataifa
inaonesha kuwa, watoto 500
waliuawa huko Gaza wakati
wa mashambulizi hayo na
3,300 wengine walijeruhiwa
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.