Está en la página 1de 20

facebook: annuurpapers@yahoo.

com

Sauti ya Waislamu

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST


(7) HIJJA NI FURSA YA KIPEKEE!

ISSN 0856 - 3861 Na. 1173 JAMADIUL AKHER 1436, IJUMAA , APRILI 17-23, 2015

Mtume(saw) amesema, "Husamehewa


mwenye kuhiji na anaowaombea". Hakuna
katika ibada nyingine yoyote uhakika huu
wa Muislamu kukubaliwa maombi yake
na kupata fursa ya kuwaombea wengine,
kisha kukubaliwa, ila katika Hijja! Muda
unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni
Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola
2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa
huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana
nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480;
BEI TShs 800/=, Kshs 50/= 0717224437.

Silaha Msikitini Kidatu, Morogoro:

Balaa kubwa linakuja


Iwapo busara zaidi haitatumika, SIO ile
Mihemko ya Wabunge wetu Dodoma
Masheikh msanubiri, Anti Balaka, Seleka?

MUFTI wa BAKWATA Sheikh Shaaban Simba


(kulia) akiwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Sheikh Alhad Mussa. Picha chini, Sheikh
Mohamed Idd (kulia), kushoto Sheikh Mohamed
Issa.

MOJA ya picha zinazosambazwa mitandaoni zikionyesha wapiganaji


'Mujahidina' wakiwa na bendera ISIS.

Jihad kuangamiza Waislam


Somalia na siasa za Zanzibar
Soma Uk. 10

Tahariri

2
AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Balaa kubwa linakuja

TAARIFA za Kipolisi
zinadai kuwa kuna
silaha zimekamatwa
ndani ya Msikiti, juzi.
Kwa mujibu wa taarifa
ya Kamanda wa Polisi
Mkoani Morogoro,
L e o n a r d Pa u l , v i t u
vilivyokamatwa katika
Msikiti uliotajwa kuwa
ni wa Suni, Kidatu
wilayani Kilombero ni
pamoja na milipuko 30,
bisibisi, majambia?,
misumeno, nyaya za
umeme, bendera yenye
Kalima ya Shahada na
vitu vya kufunika nyuso
(mask).
Taarifa zaidi zinasema
kuwa mtu mmoja
aliyetajwa kwa jina la
Hamad Makwendo
ameuliwa na wananchi
wa kitongoji cha
N ya n d e o , b a a d a ya
kumjeruhi polisi kwa
jambia. Yote haya ni
kwa mujibu wa taarifa
za polisi.
Kingine kilichodaiwa
kukutwa katika
Msikiti huo au tuseme
walichokutwa nacho
watu hao ni bendera
nyeusi ikidaiwa kuwa
kama ya Al-Shabaab.
Ukichanganya
kuwa waliokamatwa
w o t e n i Wa i s l a m u ,
wa l i p o k a m a t i wa n i
Msikitini ikijumuishwa
na kukutwa na bendera
hiyo ya ki-Al-Shabaab/
IS, wala haitakuwa sahihi
kuvilaumu vyombo vya
habari vilivyosherehesha
zaidi na kusema moja
kwa moja kuwa magaidi
wakamatwa Msikitini.
Hiyo ndiyo biashara ya
sasa.
Jambo hili sisi
tutalitazama katika
sura mbili. Moja kama
Waislamu na pili kama
Wa t a n z a n i a . K i s h a
tutahitimisha kwa kutoa
ushauri wetu, nini cha
kufanya.
Hivi sasa Jihad Feki,
ikiwa kwa sura ya IS,
Al-Shabaab, na kwa jina
lolote utakaloita, iwe
kule Libya, Syria, Iraq,

Somalia, imekuwa ni
saratani yenye kutafuna
Uislamu na Waislamu.
Mzaha huo wa jihad
na batili (pseudo-jihad)
i n a u f a n ya U i s l a m u
uonekane kama alama
ya ukatili na kielelezo
cha itikadi ya kishenzi na
watu washenzi wasio na
ustaarabu hata chembe.
Matukio kama hili la
juzi Garissa, vyovyote
utakavyolitizama, iwe
la kweli au ni usanii
uliofanyika (staged/
false flag terror attack),
lakini athari iliyoachwa
katika vichwa vya watu
ni kuwa waliofanya
hivyo ni magaidi wa AlShabaab, ni Mujahidina,
ni Waislamu wa Somalia
wanaotaka kusimamisha
Dola ya Kiislamu. Sasa
yale madai kwamba
walifanya hivyo
k u l i p i z a k i s a s i k wa
Kenya kupeleka jeshi
Somalia, haifuti picha
hiyo inayojengwa.
Hali ni hiyo hiyo kwa
yanayodaiwa kufanywa
na IS, Boko Haram na
Al-Qaidah.
Saratani
hii
inatutafuna kutokana na
vita inayochukua ushuru
wa roho za Waislamu
kule Afghanistan, Libya,
S y r i a , I r a q , Ye m e n ,
Somalia n.k. Ushuru
huu na umwagaji damu
huu unatisha zaidi kwa
sababu ni Waislamu kwa
Waislamu wanashikiana
bunduki na kulipuana
huku kundi moja
likiamini kuwa lipo
katika Jihad. Lakini wote
hawa ama wanauziwa
au kupewa silaha na
kafiri/beberu. Hakuna
mmoja kati yao mwenye
kiwanda cha kumfanya
ajitegemee kwa silaha.
Kafiri anatajirika na
kukuza uchumi wake
kwa kumwaga damu
zenu wenyewe. Lakini
kwa namna hiyo,
mnasambaratika kama
nchi. Beberu na kafiri
a n a wa k a l i a k i r a h i s i
anakomba rasilimali

zenu.
Kwa
upande
mwingine, kafiri/
mabeberu wanatumia
Jihad hii feki, kusambaza
kitisho cha ugaidi
ili kupata sababu ya
kuwapiga Waislamu
na kuzivuruga nchi
nyingine wanazozilenga.
Uchochoro wa kupitia ni
kuwa na mawakala wa
kutangaza Jihad hii feki
iwe ya Syria, Libya, Iraq
au Somalia. Hili wimbi
tunaloshuhudia hivi sasa
asili yake ni mkakati
uleule uliotumika
kupata Mujahidina wa
kupigana kwa niaba ya
mabeberu Afghanistan.
Mawakala hawa
wamekuwa wakipita
kila mahali kuhimiza
Jihad Somalia na Syria.
Na kama Waislamu,
lazima tukubali kuwa
miongoni mwetu, wapo
mawakala wanaofanya
kazi hiyo ndio maana
wanapatikana vijana
wasio na hatia (innocent)
kama Mberesero
aliyekamatwa Kenya
au akina Ummul Khair,
wanajikuta katika
matatizo, kwa ujinga tu
na utoto wao.
Tu l i w a h i k u e l e z a
katika gazeti hili juu
ya Khatib mmoja
katika Msikiti mmoja
wa M i k o c h e n i , D a r
es Salaam, aliyetumia
Khutba ya Ijumaa
k u e l e z e a n a m n a ya
kuchinja makafiri.
Tuliwahi kueleza pia
juu hotuba zinazotolewa
katika baadhi ya Misikiti
jijini Mwanza zikihimza
Wa i s l a m u k u wa n a
silaha majumbani
mwao. Ukiwa na
mawakala kama hawa na
wakaachwa wakakoroga
bongo za Waislamu,
leo yanapotajwa haya
ya Kilombero, tayari
unakuta kuna msingi
wa kujenga hoja. Hata
kama itakuja kudaiwa
kuwa watu wale wa
Kidatu walibambikiziwa
silaha zile na bendera ile
nyeusi, lakini kwa kauli
hizi za mawakala wa
mabeberu zilizoachwa
zikaota mizizi katika
b a a d h i ya M i s i k i t i ,
utetezi unakuwa wenye
kupwaya.
Ambacho sisi
tulitarajia ni kuwa baada
ya kuibuka watu kama
hawa, basi Masheikh
wangechukua nafasi zao,

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

katika hafla za Maulid,


Khutba za Ijumaa na
Darsa za Misikitini,
hafla za ndoa na hata
katika maziko; jambo
hili lizungumzwe,
lifahamike. Lakini kwa
bahati mbaya Masheikh
wetu wamepiga kimyaa.
Mtu unajiuliza,
nini vipaumbele vya
Masheikh wetu kama
hili la kupotosha
Umma wa Waislamu na
lenye kuleta madhara
makubwa katika Dini
na jamii, hawalioni!
Ndio hapo tunauliza, je,
wanasubiri yaibuke yale
ya Anti-Balaka na Seleka
kule Afrika ya Kati ndio
waseme?
Tu n a u l i z a s w a l i
hili, kwa sababu
ukifuatilia yanayotokea
K e n ya , h u k o n d i k o
tunakosukumiziwa na
mabeberu. Kila likitokea
shambulio la kigaidi,
utasikia wakisema kuwa
Wakristo walitengwa
mbali na Waislamu, kisha
Waislamu wakaachiwa
Wakristo wakachinjwa
a u k u p i g wa r i s a s i .
Tunadhani nini sababu
ya propaganda hiyo?
Hebu turejee zile hasira
za Wabunge wetu katika
ile semina ya Suala la
Mahakama ya Kadhi kule
Dodoma, lakini turejee
tena ule upumbafu
uliokuwa ukiendelea
wa kupandikiza
chuki kuwa Waislamu
wanachoma makanisa
na kuuwa viongozi wa
Kikristo. Sasa chukua
upumbafu huo na chuki
hizi zilizosheheni katika
vifua vya miongoni
mwetu, halafu jaaliya
yaliyotokea Kenya
ingekuwa ni Tanzania
hali ingekuwaje!
Kwa hiyo, ukilitizama
Kiislamu au kama
Muislamu, utaona kuwa
balaa ambalo huenda
likatukumba, kwa kiasi
kikubwa litaharakishwa
na upumbafu unaotisha
tulio nao miongoni
mwetu. Leo pamoja na
yanayotajwa kufanywa
na Boko Haram,
likiwemo lile la hivi
karibuni la kuuwa zaidi
ya Waislamu 2000 na
kuchoma moto nyumba
zao kule Baga, bado
wapo miongoni mwetu
wanaodai kuwa Boko
Haram, ni mujahidina!
Hebu someni ujumbe
huu ukiwa miongoni wa

jumbe zinazomiminika
katika Chumba Chetu
cha Habari:
Ama kama nyinyi
An nuur ni wa kweli
na mko kwa ajili ya
Allah, hamko kwa
ajili ya twaghuti, wiki
hii wakufurusheni na
Masheikh waliokwenda
mahakama ya twaghuti
kuwashitaki murtadiina
Bakwata, siyo muishie
kuwakufurisha
mujahidina wa haki alshabaab, Boko Haram,
Al-Qaida, dawla islamiya
(IS)
Huyo ni msomaji wetu
0716 67 5313. Hillary
Clinton anasema wao
ndio walioanzisha AlQaidah ili wawatumie
kupigana na Mrusi,
msomaji huyu anasema
Al Qidah ni Mujahidina
wa Haki. Boko Haram
i n a u w a Wa i s l a m u
Nigeria ya Kaskazini,
msomaji huyu anasema
Boko Haram, ni
mujahidina wa Haki.
Unamsaidiaje mtu kama
huyu!
Msomaji huyu katika
ujumbe wake mwingine
anasema kuwa na Redio/
TV Imaan, gazeti Imaan,
Mizani, Kisiwa, An nuur,
ni ukafiri mtupu kwa
sababu yanasajiliwa na
twaghuti!
Kwa wiki hii, huyu
ndiye msomaji wetu
ambaye katuma ujumbe
wa maneno mara nyingi
kuliko msomaji yoyote
kupitia namba yake hii
ya Tigo. Kwa Sheria ya
Tume ya Mawasiliano,
huwezi kumiliki laini
ya simu na kuitumia
mpaka usajiliwe. Sasa
unashindwa kujua, nini
k i n a c h o wa f a n ya T V
Imaan wawe matwaghuti
kwa kusajiliwa na Tume
ya Mawasiliano lakini
isiwe utwaghuti kuwa na
laini ya Tigo iliyosajiliwa
na Tume hiyo hiyo ya
Mawasiliano au Idara
n y i n g i n e y o y o t e ya
serikali!
Sasa unatizama hali
kama hii inayodhihirisha
jinsi mtu alivyo mtupu
katika Uislamu (Quran
na Sunnah) na maarifa
ya ujumla ya kujitambua
anaishi wapi na aishi
vipi kwa mwongozo huo
huo wa Uislamu, lakini
ashajipa Ukamanda
wa Kuhimiza Jihad na
Inaendelea Uk.3

3
Na Bakari Mwakangwale
TAASISI za Kiislamu
nchini zimepinga Bakwata
k u wa m wa k i l i s h i wa
Shule zinazomilikiwa na
Taasisi za Kiislamu katika
mchakato wa uandaaji wa
muswada wa elimu wa
mwaka 2015.
Msimamo huo umekuja
kufuatia Shirikisho la
Wamiliki na Mameneja
wa Shule na Vyuo visivyo
vya Serikali Tanzania
(TAMONGSCO) kuitaka
Bakwata, kuwa mwakilishi
wa Shule za Kiislamu,
katika kuuendea mchakato
huo.
Wadau hao wa elimu
kutoka pande zote za dini
na Serikali, walikutana
mwishoni mwa wiki
iliyopita katika ukumbi
wa Shule ya Sekondari ya
Shaban Robart, Jijini Dar
es Salaam, kwa lengo la
kujadili sera mpya ya elimu
ya mwaka 2014 sambamba
na Muswada wa Sheria ya
Elimu ya mwaka 2015.
Akipinga pendekezo
l a TA M O N G S C O k wa
Serikali (Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi)
kuwa Bakwata ndiyo iwe
msemaji na mwakilishi
wa shule za Kiislamu,
Sheikh Mohammed
Issa, alisema Jumuiya za
Kiislamu hazikubaliani na
pendekezo hilo.
Shk. Issa, alisema zipo
sababu nyingi za kupinga
pendekezo hilo, moja wapo
ni kwamba katika sekta ya
elimu Bakwata, inamiliki
Shule chache nchini
ukilinganisha na Taasisi
nyingine za Kiislamu.
Hata hivyo, alisema
kumekuwa na kasumba
si kwa asasi zisizo za
Serikali tu bali hata kwa
Serikali yenyewe mara kwa
mara kuifanya Bakwata
kuwa ndio chombo cha
Waislamu kinachotakiwa
kuwawakilisha Waislamu
nchini, ilihali kuna Taasisi
za Kiislamu nyingi zenye
hadhi sawa na Bakwata.
Bakwata imesajiliwa
c h i n i ya R I TA , k a m a
ambavyo Taasisi nyingine
za Kiislamu zilivyosajiliwa
(RITA), kwa hiyo kisheria
Taasisi zote hizo zina
hadhi sawa. Na miongoni
mwa hizo Taasisi kuna
madhehebu tofauti tofauti
hivyo sio sahihi kuifanya
Taasisi hiyo pekee kuwa
ndiyo ya Waislamu wote
nchini. Alisema Shkh.
Issa.
Shkh. Issa alisema
wakati ikiwa hivyo kwa
Waislamu, kulazimishwa
Bakwata kuwa mwakilishi
na msemaji wa Waislamu
wote, hali ni tofauti kwa

Habari

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

BAKWATA yapingwa

SHEIKH Mohamed Issa (kulia), Sheikh Rajab Katimba (katikati) na Sheikh Ally
Bassaleh (kushoto).
Wakristo ambao Serikali kiongozi wa Taasisi ya madhehebu mbalimbali
h a i t a m b u i Ta a s i s i a u Answar Sunnah Tanzania kama vile Wakatoliki,
dhehebu moja la Kikristo. (BASUTA), alisema kwa Walutheri, Angalikana
Shkh. Issa ambaye ni Wakristo kuna Taasisi za n a m e n g i n e m e n g i ,

lakini Serikali haiegemei


katikaTaasisi ya dhehebu
moja.
Hata hivyo Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Sifuni Mchome,
alitoa muongozo juu ya
msimamo huo wa Taasisi
za Kiislamu kupinga
kuwakilishwa na Bakwata,
kwa kuwataka kulifikisha
suala hilo Wizarani kwa
maandishi.
Awali katika kikao hicho,
Taasisi za Kiislamu ziliitaka
Serikali kusimamia haki na
usawa katika suala zima
la usajili na ukaguzi wa
Shule za Serikali na Shule
binafsi, ili kuweka usawa
na kupunguza ugumu
katika uendeshaji wa shule
binafsi.
Mkutano
huo
ulishrikisha wadau
mbalimbali binafsi wa
elimu nchini na Serikali,
ambapo kwa upande wa
Serikali, miongoni mwa
waliohudhuria ni pamoja
na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Profesa Sifuni
Mchome na Kamishna wa
Elimu, Profesa Eustella
Bhalalusesa.

Inatoka Uk. 2

ukatili na mafundisho ya

kuwatia wengine katika


ukafiri!
Ukiacha hilo, kama
tulivyotangulia
kusema, tatizo jingine
ni la viongozi wetu wa
kidini wenye dhamana.
Wa m e k u wa k u we p o
kwao ni kama hawapo.
Pamoja na kazi
kubwa ya kudumu
wanayotaki wa kufanya
Masheikh wetu na wajuzi
wa Uislamu kuelimisha
jamii ya Kiislamu, lakini
kama dharura, kuna haja ya
jambo hili la Jihad bandia
kufafanuliwa vizuri na
jinsi linavyotumika
kuwavuruga Waislamu na
kuuchafua Uislamu.
Kwa upande mwingine,
kama nchi na kama
Watanzania, tutakuwa
tumefanya kosa kubwa

sana kama tutawatizama


vijana hawa wanaodaiwa
kukamatwa na silaha
kuwa ni magaidi kwa
sura inayotangazwa
ulimwenguni hivi sasa.
Tukiwatizama hivyo,
na tukijikubalisha
kuwa nchini tuna
watu wa namna hiyo,
tujue kinachofuatia
ni kuingizwa katika
Mchezo wa Kifimbo
Cheza unaoendelea
Kenya na Nigeria. Na
tumetangulia kusema,
tutizame zile chuki

Balaa kubwa linakuja

walizo nazo miongoni


mwetu linapokuja suala
la Uislamu na Ukristo
katika nchi hii, halafu
tujiulize, yakipangwa na
yakafanyika ya Garissa,
tutakuwa na kifua na
mioyo ya Wakristo wa
Kenya ambao kwa hakika
ndio wanaoifanya Kenya
mpaka sasa iwe salama
kwa kiasi kilichopo hivi
sasa?
T u w a t i z a m e
watuhumiwa hawa
huku tukirejea katika
ukweli usio na shaka
kuwa mitandao yote ya
mujahidina, kuanzia
Afghanistan, ilipewa
mafunzo na fedha na
mabeberu. Rejea kauli
ya H i l l a r y C l i n t o n :
We Created Al-Qaida.
Tutizame pia Operation
Cyclone. Lakini tudurusu
p i a ya l e a l i y o s e m a
mwanahistoria wa
Uingereza Mark
Curtis alivyoonyesha
k i n a g a u b a g a
katika kitabu chake
maridhawa, "Mambo
ya siri: Ushirikiano wa
Uingereza na Uislamuitikadi," kwamba serikali

makundi yenye uhusiano

na Al Qaeda kwa
sababu zile zile kama
mwanzo - kukabiliana
na ushawishi wa Russia,
na sasa ule wa China
ili kueneza nguvu za
Marekani juu ya uchumi
wa jumla wa kibepari
duniani.
Tusisahau pia kuwa
haya ya Waislamu kuwa
na hizi zinazodaiwa
k u wa s i a s a k a l i n a
mawazo haya ya kuwa
na silaha misikitini,
katika madrasa,
skuli na majumbani,
za kuwaangamiza
wanaodaiwa kuwa
makafiri, yanatokana na
hawa hawa wanaojifanya
viranja, wafadhili na
wataalamu wetu katika
kupambana na magaidi.
Kama alivyoandika
Dr. Nafeez Ahmed
(PhD) katika makala
na uchambuzi wake
Islamic State is the cancer
of modern capitalism:
Islamic State; US foreign
policy; funding, nchini
Afghanistan, USAID
iliwekeza mamilioni
ya dola kuwapatia
za kibeberu zinaendelea watoto wa shule "vitabu
kuunga mkono kwa siri v i l i v y o j a a p i c h a z a

kipiganaji ya Kiislamu".
Theolojia inayohalalisha
jihadi ya kuua ilisanifiwa
kwa michoro ya bunduki,
risasi, askari na mabomu
ya kutegwa. "Vitabu hivyo
vya kiada vilifikia hata
kusifu thawabu ambazo
wa t a p a t a " wa k i n g ' o a
macho ya adui Mrusi na
kukata miguu yake."
Kirusi hicho ndicho
kinatafuna vijana kama
hao wa Kidatu mpaka
leo. Ufumbuzi hapa sio
kuwaadhibu waathirika
wa kirusi hiki. Hawa ni
wagonjwa wanahitaji tiba.
Usalama wetu ni kutizama
kinakotokea kirusi hiki na
kukizuiya kuingia akilini
na mioyoni mwa vijana
wetu na watu wetu.
Tukizingatia ukweli huo,
tutatambua kwamba sisi na
vijana wetu hao, adui yetu
ni mmoja. Imekuwa bahati
mbaya tu wao wamekuwa
wapumbafu wanatumiwa
huku wakidhani
wanapigania Dini.
Lakini na sisi kama
tutawatizama kuwa
hawa ndio maadui
zetu. Ni Al-Qaidah, AlShabaab au IS wa kwetu,
tutakuwa wapumbafu
pia, kama walivyogeuzwa
kuwa wapumbafu

wanaopambana na
Boko Haram Nigeria na
wanaopambana na AlShabaab Somalia.

Makala

Sababu kubwa ya kufanya maasi

TUME (S.A.W.)
anasema kuwa
kila binaadamu ni
mwenye kukosea na bora ya
wanaokosea ni wale wenye
kutubia. Kwa kua kiongozi
wetu S.A.W. haongei kwa
mapenzi au uamuzi wake,
bali anachosema ni kwa
u o n g o z i wa k e A L L A H
SWT, basi ni wazi kwamba
kila binadamu kati yetu
atafanya kosa katika maisha
yake. Makosa kwa ufupi
yanakuja na kifurushi cha
kuwa binadamu.
Kinachomfanya Muislamu
asikate tamaa baada ya
kufanya makosa, ni ahadi
nyingi alizotoa Allah SWT
kuhusiana na huruma yake
kwetu sisi wakosaji. Anasema
Allah SWT kwenye Surat
al-Nisaa, Hakika Allah
hasamehe kushirikishwa
lakini anasemehe lolote
chini ya hapo kwa anaeamua
kumsamehe.
Pamoja na kuwa ahadi
za Allah SWT za malipo
mazito kwa wasiotubu zina
vitisho vikubwa vya adhabu
kali, lakini bado Waislamu
tunaenedelea kufanya maasi
na kuyarudiarudia kila mara
na wengi wetu hatimaye
tunaiacha dunia tukiwa
kwenye hali hiyo. Hasara
ilioje mwisho huo!!
Kweli kuna makosa
tunayofanya kwa bahati
mbaya na kuna mengine
tunafanya kwa kutokujua au
kwa kutokua na uelewa wa
amri za Allah SWT. Lakini
maasi ninayoongelea mimi ni
yale ambayo tunafanya hali
ya kuwa tunajua vizuri kuwa
tunavunja amri za ALLAH
SWT.
Katika kujiuliza sababu
za kumuasi Allah SWT
wakati tukijua, hivi karibuni
nimeona video moja kwenye
mtandao ikimuongelea
Muislamu mmoja ambaye
nadhani kwa mavazi aliokua
a me va a i ma n i mt u wa
India, Pakistan, Bangladesh
au Afghanistan. Ndugu
yetu huyu kapewa mtihani
mkubwa na Allah SWT. Ni
kilema ambaye hana mikono
kuanzia kwenye mabega.
Kila jambo analofanya la
kimaisha anatumia miguu
yake. Kupiga mswaki, kuoga,
kusaidia wanae home works,
kupika na mengine mengi.
Anatumia miguu yake na
jambo moja tu anaonekana
akifanya kwa kutotumia
miguu ni pindi anapotaka
kufungua Quraan kufanya
tilaawah ndio anaonekana
akitumia uso wake kufungua
kurasa za kitabu kitukufu.
La kusisimua mwili na
akili na hata moyo kama
bado una chembechembe za
imani, ni kwamba hamna
swala inayompita na ibada
zake nyingine anazingatia.
Anatawadhwa kwa kutumia
miguu na anarukuu na
kusujudu bila kua na mikono.
Naomba tuzingatie mtihani
wa huyu mtu vizuri kabla
hatujaendelea kusoma.
Kama kilema huyu
hapotezi ibada zake, kwa

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

WAPIGANAJI WA IS
nini sisi wazima tunadharau.
Huyu Muislamu ni dalili
tosha kuwa, ulemavu si
sababu ya kuvunja amri za
Allah SWT. Tunaweza kudai
kuwa maradhi kuna wakati
yanatuzuwia kuabudu, lakini
pia kuna wagonjwa wengi
wa maradhi tofauti ambao
wanatimiza amri za Allah
SWT. Kuna wagonja ambao
wamo jela ndani ya ngozi
zao; watu ambao miili yao
imepooza kuanzia shingoni
kwenda chini lakini bado
wanaabudu kadri ya uwezo
wao. Kwa hiyo maradhi, si
sababu ya kumuasi mmiliki
wa nguvu zote, Allah SWT.
Tunaweza kudai kuwa
hali ngumu ya kiuchumi
(umasikini), inaweza
kusabibisha mtu kuasi au
kutozingatia ibada zake.
Lakini wote tunajua
wa t u a m b a o u m a s i k i n i
hauwazuii kuabudu. Au
t u n a we z a k u s e m a , h a l i
nzuri ya kibiashara/uchumi
ndio sababu ya baadhi ya
Waislamu kutokuabudu
ipaswavyo. Lakini vilevile
wote tunajua kuwa kuna
Waislamu matajiri wakubwa
na ni watu wa mashughuli
m e n g i l a k i n i h a wa a c h i
ibada zao. Sasa kama
ulema, maradhi, umasikini
na hata utajiri si sababu ya
kukiuka amri za Allah SWT,
sisi tunaomuasi Mungu usiku
mchana, sababu inakuwa ni
nini hasa?
Allah SWT anaposema
hatujaumba majini na
binaadamu isipokua
waabudu, tujue kuwa Allah
SWT anayakusudia hayo.
Hamna mchezo na wala
hakutokuwa na mabadiliko
katika ahadi alizotoa Allah
SWT kwenye Kitabu chake
kitukufu.
Wakati Allah SWT anasema
kwamba hajaumba yote haya
akifanya mchezo, maana yake

ni kwamba sisi tunafanya


maasi mengi kwa upuuzi
na mchezo. Tunaabudu kwa
kusuasua na tunavunja sheria
zake kwa sababu hatuzipi
HARAM na HALAL uzito
wake. Tunafanya mambo
yaliyokatazwa kwa sababu
hatuzingatii vizuri balaa lake
na ghadhabu tunayomtia
Allah SWT.
Kwa ufupi sababu kubwa
ya Maasi ni kutokuzipa amri
za Allah uzito wake. Wengi
hatuko makini na Amri zake
Allah Subhanahu Wataala.
Lakini Allah kishatwambia
kuwa Yeye yuko makini na
kwamba Waman yaamal
mithqaal dharratin khairin
yarah waman yaamal
mithqaal dharratin sharran
yarah.
Imani ya Muislamu ni
kichwa cha Uislamu wake.
Muislamu bila Imani ni kama
mwili bila kichwa. S.A.W
anasema kuwa kwenye mwili
kuna nyama ambayo ikikaa
sawa basi mwili mzima
utakaa sawa na hio nyama
ni moyo. Imani ya Muislamu
inajaribiwa kwa njia tofauti
za kidini na za kidunia.
Muislamu anajaribiwa na
Ibada kama kusali kwa wakati
na kufunga Ramadhan na
ibada nyingine nyingi.
Lakini kwa kuwa Waislamu
wengi tumekua tunaacha
Ibada au hatuzifanyi kwa
wakati wake na hata bila
kujihisi kuwa tunakosea,
katika makala hii ntaongelea
vitu vya kidunia ambavyo
vinajaribu na kutingisha
Imani zetu kama Waislamu.
MuislamU, mbali na mambo
ya ibada, Imani yake inapata
majaribu kwa mambo
mawili makubwa: wakati wa
matatizo na wakati milango
ya neema imefunguliwa.
Sababu wengi wetu sisi
mtihani wetu ni ugumu wa
maisha, ntaliongelea jambo

la kubwana na vipi linatutia


kwenye mtihani.
Sio kitu cha kushangaza
kumkuta Muislamu kabanwa
kiasi kwamba anaongea
peke yake. Binadamu akiwa
kabanwa kiuchumi mawazo
yake yanafikiria nani wa
kumkopa au kumsaidia.
Mjomba, kaka, rafiki na mara
nyingi hata kufikiria vitu vya
haramu kama mikopo ya riba
au hata utapeli Allah apishe
mbali.
Ikiwa ni maradhi mtu
anawaza daktari mzuri wa
kumsaidia au kusaidia mtu
wake, au hospitali nzuri au
hata wapiga ramli au wenye
kudai kuweza kuwasiliana
na Mwenyezi Mungu wali ya a d h u b i l l a a h . H u y u
Muislamu kama anakumbuka
maneno machache tu ya Allah
na kwa kuyazingatia kwa
dhati kama vile Anaemcha
Allah atamjalia mlango wa
kutokea au inna maa alusr
yusran, basi ndani ya muda
mfupi anajikuta roho yake
imetulia hata kabla ya tatizo
kutatuka. Tatizo kubwa ni
kwamba Imani haziko thaabit
na tukikumbwa na majanga,
ALLAH SWT anakua wa
mwisho kabisa kumfikiria.
Muislamu wakati kabanwa
a n a t a k i wa k u k u m b u k a
k u wa k a t i k a n g u z o z a
Imani, ni kukumbuka na
kuzingatia kiundani kuwa
kuna nguzo inayoongelea
kuwa tunatakiwa kukubali
kuwa mazuri na mabaya
yote yonatoka kwa Allah au
kwa ruhusa yake. Ni kweli
tunatakiwa kutafuta kwa
bidii ufumbuzi wa matatizo
yanaotukabili, lakini
tunatakiwa kukumbuka
d a i m a k u wa b i n a d a m u
wanaotusaidia kiuchumi
kama ndugu na marafiki

au kimatibabu kama
madaktari, si wao ambao
ndio wanamaliza matatizo
yetu. Inabidi tukumbuke
kuwa hawa binadamu
wanaosimama na sisi wakati
wa shida, ni ZANA tu za
ALLAH anazotumia kututoa
kwenye matatizo yetu. Wao
wenyewe wanamtegemea
Allah kwa kila kitu kwani
mbinu za binadamu yoyote
zinategemea uamuzi wa Allah
SWT. Wama Tashaauun illa
an yashaa Allah Rabbu Alalameen.
Mfano wa kufuata
ni Nabi Ayyub ambae
alinyanganywa mali yake
yote na akapewa maradhi ya
ajabu lakini katu hakumpa
nafasi Iblis kumnyanganya.
Cha muhimu alichokua
kabaki nacho, IMANI yake
bi LLAAH. Hatuwezi kama
waislamu kuyumbishwa
na matatizo ya kidunia na
kuanza kutapatapa kama
myama aliekatwa kichwa
h a l a f u wa k a t i h u o h u o
tukadai kuwa tuna Imani na
uwezo wa Allah SWT.
Tu k i wa n a I m a n i
dhaifu na Qudra za Allah
tutakuwa kama wale
Q u r a a n i n a w a o n g e l e a
ndani ya ayah hii ya Surat alHujuraat ayah 14: Mabedui
wa m e s e m a t u m e a m i n i .
Sema: Hamjaamini, lakini
s e m e n i : Tu m e s i l i m u .
Kwani Imani haijaingia
katika nyoyo zenu. Imani
ilokamilika haitetereki kwa
lolote. Muislamu mwenye
Imani thabiti hamna janga
la kuitingisha Imani yake na
hofu yake mpaka anaingizwa
kaburini inakuwa ni ya
kumuogopa na kumcha Allah
na kuamini kikamilifu kuwa
hamna linaloweza kumtokea
zuri au baya bila Allah
kuliruhusu. Na Muislamu
likimtokea zuri anasema Alhamdulillah na likimtokea
baya anasema Inna Lillah
wa Inna Ilaihi rajioun.
Kuridhika ni katika
misingi ya Imani. Kuna ayah
ambayo inaonyesha kuwa
shukurani ya dhati ni nzito
kuliko aina nyingi za ibada.
Anasema Allah: Na mwenye
kutaka malipo ya duniani
tutampa; na mwenye kutaka
malipo ya Akhera tutampa.
Na tutawalipa wenye
kushukuru. Kana kwamba
wanaoshukuru kwa dhati
wana daraja tofauti kabisa na
wengine.
Uchumi mbaya, maradhi,
matatizo mengine, tafuta
sababu za kuyatoka, lakini
wakati huo wote unaosubiri
faraja na mfunguko, kuwa
na subira na uamini kuwa
hamna binadamu ambaye
Allah SWT hafatilii mambo
yake. Allah SWT anasema
na hizo siku tunazigawanya
baina ya watu. Kama leo sio
siku yako, kuwa na Imani ya
dhati kuwa yako inakuja.
(Makala na ZHK).

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Udhaifu UN, kiburi cha Israel


Askari wa kikwazo cha Palestina huru
Saudi Arabia
waonja
chungu

VITA YEMEN
NA SAUDIA:

U m o j a wa M a t a i f a ,
azimio ambalo
k i v i t e n d o l i l i i g a wa
Palestina katika sehemu
mbili za Wapalestina
na Wayahudi mwezi
Novemba 1947, ni
matukio mawili
muhimu katika historia

ASKARI wa Saudia
A r a b i a wa m e u a wa
na wengine kadhaa
kukamatwa mateka
katika shambulizi
la kulipiza kisasi
lililofanywa na
wapiganaji wa kabila la
Takhya nchini Yemen.
Ripoti zinasema kuwa
wanachama wa kabila
l a Ta k h ya J u m a p i l i
i l i y o p i t a wa l i f a n ya
shambulizi la kuvizia
dhidi ya kituo cha jeshi
la al Minare, karibu na
mpaka wa nchi hiyo na
Yemen.
Shambulizi hilo
limefanyika ikiwa ni
kulipiza kisasi cha
mauaji yanayoendelea
kufanywa na majeshi
ya Saudi Arabia dhidi
ya watu wa kabila hilo.
Ijumaa iliyopita
askari watatu wa Saudia
waliuawa na wengine
wawili kujeruhiwa na
roketi lililorushwa na
wapiganaji wa Huthi
huko Kusini mwa
mkoa wa Najran nchini
Saudia.

HUKU akisisitiza juu ya


kuendelea kuzingirwa
Ukanda wa Gaza huko
Palestina inayokaliwa
kwa mabavu na utawala
wa kizayuni wa Israel,
Ban Ki-moon, Katibu
Mkuu wa Umoja wa
Mataifa amesema kuwa
njia pekee ya kumaliza
mgogoro wa Waarabu
na Israel ni kubuniwa
k wa n c h i h u r u n a
ya kidemokrasia ya
Palestina.
Akizungumza hivi
karibuni na Sheikh
Abdallah bin Nassir
A a l T h a n i , Wa z i r i
Mkuu wa Qatar muda
mfupi kabla ya kikao
cha 13 cha Umoja wa
Mataifa cha kuzuia
uhalifu na kupatikana
uadilifu wa kisheria
huko mjini Doha, Ban
Ki-moon, alisema
kuwa ana wasiwasi
kutokana na kukwama
kwa mwenendo
wa mazungumzo
ya mapatano kati ya
Wapalestina na utawala
wa Israel.
Umoja wa Mataifa
umekuwa na nafasi
muhimu katika
kukaliwa kwa mabavu
ardhi za Wapalestina
na dhulma yote ambayo
imefanyiwa taifa
dhulumiwa la Palestina
tangu mwanzoni mwa
karne ya 20 hadi leo.
Kuwekwa Palestina
chini ya himaya ya
Uingereza kwa kipindi
cha miaka 30 katika
miongo ya mwanzoni
mwa karne ya 20 na
b a a d a e k u p i t i s h wa
azimio nambari 181
katika Baraza Kuu la

MUFTI Mkuu wa
Syria, Sheikh Ahmad
Badruddin Hassun,
amesema kuwa mji wa
Alepo ulioko Kaskazini
mwa nchi hiyo unalipa
gharama za kulinda
heshima na izza yake na
kwa sababu hiyo magaidi

wamekuwa wakiulenga
mji huo kwa makombora
yanayonunuliwa na nchi
za Saudi Arabia na Qatar
na kuingizwa nchini Syria
kupitia Uturuki.
Sheikh Hassun alisisitiza
kuwa ulimwengu
unapaswa kuelewa kuwa

d a m u i n a y o m wa g wa
katika mji wa Aleppo
gharama yake italipwa na
nchi za Saudi Arabia, Qatar
na Uturuki kwa sababu
Wasyria hawatasahau jinai
hizo.
Shambulizi lililofanywa
na makundi ya ISIS tarehe

ya Palestina ambayo umoja


huo ulikuwa na nafasi
muhimu katika kuyabuni
na kuyasimamia.
Hata hivyo inaelezwa
kuwa matukio hayo
yalichangia kwa kiasi
kikubwa kukaliwa
kwa mabavu ardhi za
Wapalestina na utawala
wa Kizayuni wa Israel
na kwa msingi huo, bila
shaka Umoja wa Mataifa
unabebeshwa lawama
kwa kuchangia sehemu
kubwa katika kuanza kwa
mzozo wa Wapalestina na
Wazayuni, mzozo ambao
bado unaendelea hadi
leo katika karne ya 21,
ambapo hivi sasa Katibu
M k u u wa k e a n a t a k a
uhitimishwe.
Kwamba baada ya
kupasishwa azimio hilo,
utawala haramu wa
Israel ulitangaza rasmi
kubuniwa kwake katika
ardhi za Wapalestina,
l a k i n i Wa p a l e s t i n a
wenyewe ambao ni
wamiliki halisi wa ardhi
h iz o h a wa ja ru h u s iwa
kubuni nchi huru hadi leo
ambapo ni karibu miongo
saba imepita tangu ardhi
hizo zikaliwe kwa mabavu
na Wazayuni.
Jambo la kushangaza
hapa ni kuwa mazungumzo
ya mapatano ya Waarabu
n a I s r a e l ya l i f a n y i k a
mwezi Oktoba 1991 kwa
usimamizi wa Umoja wa
Mataifa ambapo kwa
m s i n g i wa m a a z i m i o

nambari 242 na 338 ya


Baraza la Usalama la umoja
huo, jeshi la Israel lilitakiwa
kuondoka kwenye ardhi za
Wapalestina na kubuniwa
nchi ya Palestina.
Kwa mujibu wa
maazimio
hayo
yaliyopasishwa na Baraza
la Usalama katika miaka
ya 1967 na 1973 jeshi
hilo lilitakiwa kuondoka
katika ardhi za Palestina
zilizotekwa na kukaliwa
kwa mabavu na Israel
katika Vita vya Mwezi
Juni.
Lakini kwa masikitiko
makubwa maazimio hayo

kama yalivyo maazimio


mengine ya Umoja wa
Mataifa kuhusiana na
Palestina, yalitupwa
kwenye kapu la sahau na
hivyo kuwapa watawala
wa Israel uhuru kamili
wa kutekeleza mauaji
ya kutisha dhidi ya
Wapalestina wasio na
hatia pamoja na kupora
ardhi zao bila kujali.
Mauaji pamoja na
ujenzi wa vitongoji vya
walowezi wa Kizayunji
katika ardhi zilizoporwa
za Wapalestina umezuia
kikamilifu kubuniwa
kwa nchi huru ya
Wapalestina.
Inasikitisha kuona
kwamba upuuzwaji wa
maazimio ya Baraza la
Usalama na utawala
haramu wa Israel
unafanyika kutokana
na uzembe pamoja na
ushirikiano wa moja
kwa moja wa Umoja
wa M a t a i f a a m b a o
unadhibitiwa na nchi za
Magharibi zikiongozwa
na Marekani, nchi
ambazo ni waungaji
mkono wakubwa wa
utawala huo ghasibu.

Nitagombea
Urais -Clinton

Bi. Hillary Rodham Clinton


amejitosa tena katika siasa za
kusaka Urais wa Marekani
mwaka 2016, kwa ahadi
kuwa atakuwa kinara wa
Wamarekani wa kawaida
katika taifa ambalo ukosefu
wa usawa wa kipato unazidi
kutanuka.
Tofauti na miaka nane
iliyopita wakati alipogombea
na kushindwa na Barack
Obama, Clinton na historia
yake binafasi hawakuwa
fokasi ya ujumbe wake
wa kwanza wa kampeni.
Hakuzungumzia wakati
wake katika Baraza la Seneti
wala miaka yake minne
kama waziri wa mambo ya
kigeni, au uwezekano wake
wa kuandika historia kama
rais wa kwanza mwanamke
kuiongoza Marekani.
Badala yake, video yake ni
mkusanyiko wa wapigakura
wanaozungumzia maisha
yao, mipango yao na
matarajio yao ya baadae.
" W a m e r e k a n i
wamepambana kutoka
katika nyakati ngumu za
kiuchumi, lakini hali
iliyopo bado inaendelea
kuwanufaisha wale walioko
juu. Wamarekani wa kawaida
wanahitaji kinara, nami
nahitaji kuwa kinara huyo,"
alisema Clinton mwoshoni
mwa video ya tangazo lake.
Video hiyo ya Clinton
pamoja na mtandao wake
havikugusia masuala
ya kisera. Lakini ujumbe
huo ulinuiwa kuwavutia
Wa l i b e r a l i w a c h a m a
cha Democrats, ambao
wanachukulia usawa wa
kiuchumi kama suala la
kipaumbele.
Clinton sasa anapanga
kuelekea katika majimbo
yenye maamuzi ya Iowa na
New Hampshire, kuungana
na wapiga kura. Clinton
anatumai kuepusha makosa
ya mwaka 2008, alipoingia
katika kinyanganyiro hicho
kama mgombea anayepewa
n a f a s i k u b wa z a i d i ya
kushinda na kushangazwa na
Obama katika jimbo la Iowa.
Clinton mwenye umri
wa m i a k a 6 7 a n a i n g i a
katika kinyanganyiro hicho
akiwa na rekodi ndefu ya
utumishi wa umma, historia
itakayomsaidia lakini pia
kumuumiza.

Mufti asema Saudia, Qatar zinaua wananchi Wasyria


23 Machi dhidi ya mji huo
wa Aleppo lilisababisha
v i f o v ya wa t u 2 3 n a
kujeruhi wengine 30.
Wa t u wa S y r i a
wanaamini kwamba
wapiganaji wa ISIS
wanaofanya mauaji ya
kutisha kwa kutaka

v i c h wa v ya wa t u a u
kuwachoma moto wakiwa
hai, wanasaidiwa kifedha
na silaha na nchi za Saudi
Arabia, Qatar, Uturuki,
utawala wa Kizayuni wa
Israel na nchi za Magharibi
zikiongozwa na Marekani.

Makala

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Tujifunze kujadiliana kwa nguvu ya hoja


Na Abuu Nyamkomogi

WEZI Novemba
mwaka jana
n i k i wa k a t i k a
ziara ya kifamilia wilayani
Bukoba mkoani Kagera,
nilipata pia fursa ya
kumtembelea nyumbani
k wa k e r a f i k i ya n g u
wa karibu aliyekuwa
akifundisha katika shule
ya sekondari Nyanshenye
iliopo eneo la Nyamkazi
katika Manispaa ya mji
wa Bukoba.
Katika siku tatu
nilizokuwa na swahibu
wangu huyo, tulizungumza
na kujadiliana mintarafu
masuala mbalimbali
yakiwemo ya kisiasa,
ya kiuchumi pamoja na
ya kijamii yaliyokuwa
yakiendelea kujiri katika
ngazi ya kitaifa na ya
kimataifa kwa wakati huo.
Nakumbuka ilikuwa
ni siku ya pili baada ya
utekelezaji wa ibada ya
swala ya magharibi katika
msikiti mmoja uliopo eneo
la Kashai mjini humo
tukiwa mimi, swahibu
yangu huyo pamoja na
mwalimu mwingine
wa shule ya sekondari
Kahororo, ambaye kwa
bahati nzuri sote tulikuwa
tukifahamiana naye, mimi
binafsi nilifahamiana naye
tangu alipokuwa akiishi
jijini Mwanza kabla ya
kuhamia kwake mjini
Bukoba; na yule swahibu
wangu alipata kusoma
naye miaka michache
iliyopita katika Chuo
Kikuu kimojawapo
m i o n g o n i m wa V y u o
Vikuu vilivyopo mkoani
Morogoro. Kwa ufupi
wa maneno, sote watatu
tulikuwa tukifahamiana
vizuri.
Kufahamiana kwetu
huko kulitusukuma katika
mazungumzo ya hapa na
pale ya masuala kadha wa
kadha jioni ile yakiwemo
ya kitaifa na ya kimataifa.
Mojawapo ya suala la
kitaifa tuliloligusia katika
mazungumzo yetu hayo
ingawa kwa muhtasari
lilikuwa ni suala la kadhia
ya ufisadi wa akaunti ya
Tegeta ESCROW kwa
kuwa kipindi hicho
ndipo mjadala motomoto
kuhusu suala hilo ulikuwa
ukiendelea kushika kasi
kule bungeni Dodoma; na
kwa upande wa masuala
ya kimataifa tuliyaelekeza
mazungumzo yetu katika

MAAFA yanayosababishwa na mashambulizi ya Saudi Arabia nchini Yemen.


s u a l a l a u i b u k a j i wa
kundi linalojiita Dola la
Kiislaamu (IS) na athari
zake kwa Uislamu na
Wa i s l a m u p a m o j a n a
kutathmini mwenendo
wa harakati zake iwapo
zinaafikiana na Qur-an na
Sunnah au la.

kimafuhumu juu ya suala


la kundi la IS na uendeshaji
wa harakati zake. Mimi
pamoja na yule mwalimu
wa Kahororo tulivyokuwa
tukilitazama na kulielewa
au kulifahamu lile kundi
la Dola la Kiislaamu
sambamba na uendeshaji

makala au habari kuu


katika ukurasa wake wa
kwanza yenye anuwani
iliyosomeka 'Kwenda
Kupigana Somalia ni
Ukafiri' iliyoandikwa
na
mwandishi
aliyejitambulisha kwa jina
la Mussa Ame. Makala

MAAFA yanayosababishwa na mashambulizi ya Saudi Arabia nchini Yemen.


Suala hili la pili
lilituchukua muda
mrefu zaidi kulijadili
kuliko lile la awali
kiasi ambacho tulifikia
hatua ya kulihitimisha
kwa kukubaliana
kutokukubaliana kwa
salama na amani.
Hali hiyo ilitokana na
tofauti za kimtazamo na
za kiuelewa au /na za

wa harakati zake, ilikuwa


ni tofauti na mtazamo na
uelewa au/na mafuhumu
ya yule swahibu
wangu. Kwa hiyo ndio
tukaamua kukubaliana
kutokukubaliana pasi na
kukejeliana, kudhihakiana
na wala kukufurishana.
Naam, toleo la gazeti la
An nuur la juma lililopita
lilikuwa na habari-

hii iliibua sintafahamu


sambamba na mshangao
pamoja na maswali ya
kitaharuki, kwa baadhi
ya Waislamu niliopata
kufuatilia kwa karibu
mazungumzo yao katika
kundi moja la Watsap
ambalo nami ni miongoni
mwa wadau wake, dhidi
ya gazeti hili na mhariri
wake kwa upande mmoja;

na mwandishi wa makala
husika kwa upande wa
pili.
Nianze mjadala wa
suala hili kwa kunukuu
hapa
sehemu ya
mazungumzo ya baadhi
ya wanakundi kuhusiana
na makala husika kwa
ajili ya mjadala zaidi kama
yalivyowasilishwa kundini
na mwanakundi mmoja
sambamba na mrejesho
kutoka kwa baadhi ya
wanakundi.
Mwasilishaji taarifa:
Gazeti La Annur, Tanzania
lapoteza muelekeo.
Limetoa habari kuwa
kwenda kupigana Somalia
ni ukafiri. Kisha akatuma
kundini nakala ya ukurasa
wa kwanza wa gazeti la
Annuur lenye habarimakala husika kwa
ithibati zaidi halafu chini
yake akaandika hivi: Hii
ni nakala ya An-nuur
iliyotoka jana tarehe 10
April 2015
Mchangiaji wa kwanza:
Ninalo hapa yani hili
gazeti si la Kiislaamu.
Mwasilishaji taarifa:
Kinachoonekana zaidi
ni umamluki ulioingia
kwenye wanahabari
hawa dhidi ya Uislamu
na Waislamu. Mtume
(s.a.w) anasema "aljihadi
m a a d h w i i l a a ya w m i
l-qiyama" yaani jihadi
itaendelea hadi siku ya
qiyama.
Mchangiaji wa pili:
Kabisa yani sijuwi niliiteje
hili gazeti. Mwasilishaji
taarifa: Sasa wao kama
wanaona Somalia hakuna
jihad, wanaweza kutueleza
ni wapi jihadi IPO?
Mchangiaji wa tatu:
Wanapenda ubwabwa na
tende watu wa maulidi
mtihani sana.
Mwasilishaji taarifa:
Kinachosikitisha zaidi ni
ujinga wa mhariri wake,
anapoiweka habari hii
tena front page ikionesha
ni habari muhimu sana
kuliko zingine. Akiendelea
kulingania ujahili wake
anasema Somalia
wanaopigana ni Waislamu
wao kwa wao.
Mchangiaji wa nne: Wao
wanapenda kukuna nazi
hata kama ni wanaume
wamezoea kushika dufu
hawazi kubeba AK47.
Mchangiaji wa tano:
Kafiri wa kwanza yeye na
kwani yeye nani si nabii
wala si Mtume mdomo
Inaendelea Uk.8

Makala

7
Masoud Msellem

SHAMBULIZI la
karibuni la mauaji ya
wanafunzi 148 wasio
na hatia katika Chuo
Kikuu cha Garissa,
Kaskazini Mashariki
mwa Kenya ni tukio
ovu, la kutisha na
kumuhuzunisha kila
mtu. Kimsingi ni tukio
la kulaaniwa lisilokuwa
na uhalali kwa namna
yoyote.
Hata hivyo, baada ya
msiba wa tukio hilo,
umakini na uadilifu
unahitajika katika
matendo, kalamu,
matamshi na kauli zetu
hususan kwa vyombo
vya habari, wanafikra,
wasomi na
watu
jumla nk. Kukosekana
umakini na uadilifu huo
kutapelekea kuchochea
msiba mkubwa zaidi wa
kijamii na kisiasa kuliko
huu wa sasa.
Vyombo vya habari
hususan magazeti mbali
mbali vinaionesha
qadhia hii ya mauwaji ya
Garissa kana kwamba ni
vita baina ya Waislamu
na Wakiristo. Jambo
hilo sio sawa wala sio
uadilifu. Ajabu! vyombo
hivyo hivyo vya habari
vinaporipoti kuhusu
mauwaji ya Israel kwa
Waislamu wa Palestina
huwa havitamki kuwa ni
vita baina ya Waislamu
na Mayahudi.
Tu k u m b u s h e t u ,
mara nyingi kama
sio zote vyombo vya
habari vinaporipoti
matukio maovu
yanayonasibishwa
na Waislamu hukosa
uadilifu katika kuripoti
kwao. Kana kwamba
hadhira ya vyombo
hivyo ni wasiokuwa
Waislamu peke yao.
Wa k a t i m w i n g i
tunashuhudia vyombo
mbali mbali vya habari
kwa maksudi hupotosha
uhalisia wa matukio
hayo ili kuwatosa
z a i d i Wa i s l a m u .
Kwa upande wa pili,
ya n a p o j i r i m a t u k i o
a m b a y o Wa i s l a m u
ndio wahanga wakuu,
vyombo hivyo hivyo
huwa kama havipo au
huwa kimya cha mfu !
Kwa mfano, mauwaji
ya halaiki ya Waislamu
nchini Burma, mauwaji
ya halaiki ya Waislamu
nchini Jamhuri ya Afrika
ya Kati nk. Au walau
v y o m b o h i v y o v ya
habari kutaja kwamba
katika tukio la mauwaji
haya ya Garisa, mtu wa

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Umakini katika tukio la Garissa

Si Vita baina ya Waislamu, Wakristo

suala la kujikusanyia
maslahi na kuzowa
rasilimali hizo, madola
hayo huzozana wao kwa
wao kutokana na uroho
wao. Kila mmoja akitaka
ajipatie fungu nono.

BAADHI ya wanafunzi 148 wa Chuo Kikuu cha Garissa, Kaskazini Mashariki mwa Kenya wanaodaiwa kuuawa
hivi karibuni.

mwanzo kuuwawa ni
Muislamu aliyekuwa
mlinzi wa chuo hicho.
Aidha, wakati
m we n g i n e t u n a o n a
vyombo vya habari
namna
qadhia
zinazowahusu
Waislamu zinavyotiwa
chumvi na kulazimisha
kinyume na ukweli
ulivyo. Mfano mzuri
wa k a r i b u n i n i i l e
Operesheni ya Amboni
Tanga, licha ya Jeshi
la Polisi kukanusha
kwamba waliokabiliana
na polisi katika mapango
yale walikuwa wahalifu
na sio magaidi, bado
vyombo mbali mbali
vya habari vilionekana
kushabikia kwa nguvu
kubwa na kunadi
wimbo wa magaidi na
Al-Shabab.
Kwa
upande
mwengine, tukio au
m a t u k i o m a o v u ya
wasiokuwa Waislamu
ya n a p o r i p o t i wa n a
vyombo hivyo hivyo
huripotiwa kwa
heshima na uadilifu.
Lakini tukio hilo hilo

l a u l i n g e k u wa k wa
Muislamu, ingekuwa
balaa kubwa . Fikiria
suala la karibuni la
wafuasi wa Mchungaji
Josephat Gwajima na
jaribio lililoripotiwa
kuwa la kumtorosha
mchungaji huyo. Lau
ingelikuwa wafuasi
hao wa Gwajima ni
Waislamu, ingelikuwa
tarumbeta kubwa!
Ungeona vichwa
vya habari magaidi
wavamia hospitali na
bastola. nk. Au tukio
la siku chache zilizopita
l a P o l i s i w i l a ya ya
Kisarawe kumshikilia
Joseph Mumbi baada
ya kumkuta na bastola
na risasi 8 kwenye ibada
ya Ijumaa Kuu katika
Kanisa la Mt Stephano.
Angekuwa huyo sio
Joseph magazeti
yangesemaje?
Kimsingi mwenendo
huu wa vyombo vya
habari wakati mwengine
vikiwemo vya umma
kukosa uadilifu na
umakini ni jambo la
hatari sana ambalo

huchochea zaidi fikra


hatari ya ubaguzi na
udini ambayo itapelekea
m a h u s i a n o m a b a ya
zaidi ya kijamii.
Wa n a c h o p a s wa
kukijua na kutanabahi
vyombo vya habari,
mufakirina/wanafikra
na kila mmoja wetu ni
kuwa chanzo msingi
cha matukio kama haya
ya Garissa na mfano
wake ni mfumo batil
wa kibepari na madola
yake hususan Marekani
na Uingereza. Madola
hayo yana hali tatu:
Kwanza, yana ajenda
ya kutapatapa ya
kupambana na mfumo
ulioko dhidi yake ambao
bila ya shaka kwa sasa
ni Uislamu pekee.
Ndio maana wakabuni
kauli mbiu ya uongo
ya Vita vya Ugaidi.
Pili, madola hayo yana
shauku na ghera kubwa
ya kuzowa rasilimali za
nchi changa zikiwemo
nchi zetu kwa gharama
yoyote. Tatu, katika hili

Kila dola katika


madola haya mawili,
katika kufikia malengo
yao ya kujiimarisha na
kujihakikishia kupata
fungu kubwa na nono
zaidi, hutumia mbinu
mbalimbali hata chafu
na za kiharamia. Katika
hali hiyo ndio nchi zetu
hutoswa kuwa chambo
cha balaa na misukosuko
isiyokwisha. Kilichoko
sio mapambano baina
ya Uislamu na Ukiristo
wala kinyume chake.
Bali ni harakati za mfumo
wa kibepari na madola
yake kujimakinisha,
kujitanua na kujizolea
maslahi kwa namna na
mbinu yoyote hata kama
ni kuangamiza maisha
na kuzuwa migongano
ya kijamii.
K wa h a k i k a , n c h i
z e t u n a d u n i a k wa
ujumla inahitaji mfumo
mwengine mbadala ili
kuzitoa katika vurugu
na mabalaa kama haya.
(Kwa maoni:Mob:
0778 870609)

Makala

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Tujifunze kujadiliana kwa nguvu ya hoja


Inatoka Uk. 6
wake halipii kodi mwache
ajifurahishe.
Mwasilishaji taarifa:
Binafsi nilihudhuria
semina ya taasisi kongwe
ya IPC iliyofanyika
wilaya ya Same mkoani
K i l i m a n j a r o , i l i k u wa
mwaka juzi Desemba,
mhariri wa Annur
alianzisha mada kama hii
lakini vijana tulimpinga
sana hadi ikawa ni vurugu
kubwa.
Mchangiaji wa sita:
Kwanza mungemtia adabu
hata mdomo mngeupasua.
Mwasilishaji taarifa:
Mhariri huyu Siku zote
ameonekana kuwa ni
mpinzani mkubwa wa
jihadi kwa maslahi yake
binafsi.
Mchangiaji wa saba: Kwa
nini alitoka mrembo hata
kope zake hamkunyofoa
ilitakiwa kwa uchache hata
kofi angepigwa.
Mwasilishaji taarifa:
Ustaadhi Ilunga aliwapoza
vijana na kusema jihad IPO
na yeyote mwenye uwezo
ni rukhsa kwenda popote
penye jihadi kupigana.
Mwasilishaji taarifa:
Mhariri Aliwahi kusema
kwenye nakala zake
zilizopita kuwa kama
mujahidina wapo kweli,
basi waende Afrika ya
Kati, na hii ilikuwa ni
kejeli.
Mchangiaji wa tisa: Sana
sasa kama aliona kuna
umuhimu mbona yeye
hakuenda.
Ukiyadurusu kwa
makini mazungumzo
hayo hapo juu, utabaini
kuwa si mwasilisha
hoja wala wachangiaji
wa l i y o t h u b u t u s i t u
kukijadili, bali hata
kukidodosa kiini cha hoja
ya msingi iliyowasilishwa
na Bw. Mussa Ame katika
gazeti hili toleo la wiki
jana.
Naomba ieleweke
vyema na mapema
kwamba kusudio langu
hapa si kutaka kuunga
au kutounga mkono hoja
ya Bw. Mussa Ame bali
ni kutaka kuonesha jinsi
wengi wetu tusivyokuwa
na uwezo wa kukabiliana
na hoja kwa hoja na badala
yake kushughulika zaidi
na mtoa hoja badala ya
hoja na hata kwenda mbali
zaidi ya hapo.
Nitafafanua zaidi
kipengele hicho mara tu
baada ya kurejelea mfano

WAPIGANAJI wa ISIS
wa
tukio lililowahi
kutokea takriban miezi
sita iliyopita unaolandana
na mjadala wetu wa leo ili
kuonesha namna wengi
wetu tunavyokabiliwa
na tatizo la kutokuwa na
uwezo wa kukabiliana na
hoja kinzani.
Mfano wenyewe ni ule
uliowahi kubainishwa
huko nyuma na mwandishi
mkongwe na mwenye
tajiriba ya muda mrefu
katika tasnia ya uandishi
wa h a b a r i B w . O m a r
Msangi katika makala
yake ya mwezi Novemba
mwaka jana katika gazeti
hili iliyobeba anuwani
iliyosomeka : 'Volikano ya
Jihadi yaelekea Makkah'.
K wa m u k t a d h a wa
ninachokusudia kukieleza
na kwa faida ya wasomaji
ambao hawakupata bahati
au fursa ya kuusoma
mukadima wake katika
makala hiyo, nimwombe
Bw. Msangi aniruhusu
kunukuu kile alichoandika
katika utangulizi wake ule
kabla ya kuendelea na hoja

yangu katika makala yetu


ya leo.
''Kiasi cha wiki moja
iliyopita mtu mmoja
alinipigia simu akiniambia
kuwa alitaka kukutana
na mimi. Hata hivyo
akasema, kwa vile alikuwa
njiani akitokea Kampala,
atanipigia atakapofika
mwisho wa safari yake.
Hakuwahi kunipigia, ila
nikawa napokea ujumbe
wa maneno kupitia simu ya
mkononi. Zilikuwa meseji
nyingi kiasi zikifuatana
moja baada ya nyingine.
Kutokana na wingi wake,
sitaweza kuzinukuu zote,
ila ningependa kunukuu
mbili tu ambazo zilinifikia
siku ya Jumamosi
ilivyopita baina ya saa
moja na saa tatu asubuhi.
Ya kwanza inasema:
''Ewe jaahili murakkab!
Ewe khinziir wa Kishia!
Ewe mch umia tu mbo
unaejipendekeza kwa
serikali! Unasema IS
wanapewa msaada
na
USA-Israel.
Tumeshuhudia Mashia
na USA kuwapiga IS,

mbona umeufyata hujatoa


makala kuhusu hilo? Na
Alhamdulillah haukupita
m u d a h a t a wa m i e z i
miwili wakafarakana!
U n a f i k i we n u u k a wa
hadharani! Eti taifa la
Kiislaam mnaungana na
USA kuwapiga ndugu
I s l a m ? U n g e k u wa s i
khinziir ingetosha aibu
hiyo na usingerudia tena
kuwafanyia wajinga
''kadabra kaadabra''
kupinga Jihadi! Lakini
ndio hivyo, khinziir ni
khinziir tu. (0683-270987).
''Kabla sijamaliza
kusoma ujumbe huo, mara
ikaingia meseji nyingine.
Yenyewe inasema:
''Mlipoona (Mashia)
Jeshi la Allah sw linakaribia
k u o n d o a u t a wa l a wa
k i n a f i q ! U t a wa l a wa
watu wanaowakufurisha
Maswahaba kiraamin wa
Mtume s.a.w katika Iraq,
mkaona bora muungane
na USA kuwapondaponda
sasa nyie na USA mna
dini gani? Maana yake
inaonekana mnafanana
mpak a mk akub aliana

kumpiga adui yenu IS!


Allahu Akbar! Ungekuwa
si khinziir hili jambo
limekuvua nguo kabisa
lakini wapi bwana. Lini
khinziir atakuwa bora?
Dawa yako inaiva...subiri,
subiri, subir, subiri'' (0683270987).
Baada ya mfano huo
hapo juu, sasa nirejee
katika ufafanuzi wa kile
kipengele nilichoahidi
kwamba ningekitolea
ufafanuzi kutokana na
unyeti wake katika mjadala
wetu huu wa leo.
Awali ya yote,
mwasilishaji taarifa
alianza kutoa taarifa yake
kwa madai kwamba gazeti
hili limepoteza mwelekeo,
nukta ambayo nimeitumia
makusudi kama anuwani
kuu ya makala yangu ili
kuvuta hisia za wasomaji
na kuwajengea raghba
ya kusoma makala hii
na kuitafakari maudhui
yake kadri ya upeo wao
aliyowajaalia Allah (S.W.).
Ila nilichoongeza mimi
Inaendelea Uk. 12

AN-NUUR

Makala

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Saudia soko muhimu la silaha za Marekani


Na Shaban Rajab

NCHI ya Saudi Arabia


na baadhi ya Mataifa ya
Kiarabu Mashariki ya Kati
ni moja ya nchi ambazo
ni soko muhimu sana la
silaha za Marekani na
baadhi ya nchi za Ulaya.
Soko hili limekuwa
chanzo muhimu cha kukua
u c h u m i wa M a r e k a n i ,
kiasi kwamba Washington
imekuwa ikitumia kila
m b i n u i n a y o we z e k a n a
kuhakikisha kwamba
maslahi yake yanalindwa
katika ukanda huo.
Hata hivyo, pamoja na
kuwa soko muhimu la silaha
kwa Marekani, wachunguzi
wa mambo wanaona
kwamba kitendo chake cha
kuingia kijeshi kupambana
na vikundi vya wapiganaji
wanaopinga serikali ya
Yemen, kumefungua zaidi
milango ya soko hilo la
silaha kwa Marekani. Si
silaha tu, Saudia ambayo
inaonekana kuwa ni moja
ya nchi za Kiarabu ambayo
ni mshirika mkubwa wa
Marekani, imekuwa kama
kituo cha kusimamia maslahi
ya Marekani katika nchi
nyingine za ukanda huo na
pia na chanzo cha pato la
mafuta kwa Marekani.
Kwa mujibu wa
mtandao wa irib, mwaka
2013, Serikali za Marekani
na Saudi Arabia zilisaini
makubaliano ambapo
Washington iliuuzia utawala
wa k i f a l m e wa R i ya d h
silaha za kivita na zana za
kijeshi zenye thamani ya
dola bilioni 30. Makubaliano
hayo, yaliiruhusu Marekani
kuiuzia Saudi Arabia ndege
84 za kivita aina ya F15 kwa
thamani ya dola bilioni 30.
Andrew Shapiro, Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje
wa Marekani wa masuala
ya kisiasa na kijeshi alidai
kuwa Washington ilisaini
makubaliano hayo ya
kuiuzia Saudia silaha, ili
kuiimarisha kijeshi nchi hiyo
kwa ajili ya kukabiliana na
mashambulio yanayoweza
kuikabili. Takribani mwaka
mmoja nyuma, Congress ya
Marekani ilipitisha muswada
wa makubaliano ya kuiuzia
Saudi Arabia silaha zenye
thamani ya dola bilioni 60.
Mauzo hayo yalijumuisha
ndege za kivita aina ya
F15, helikopta za kijeshi,
makombora, mitambo ya
rada na darubini za kuona
kizani.
Hata hivyo, ili kupata
ridhaa ya Congress, serikali

Vita Yemen kuongeza soko

GARI la kurushia makombora la Jeshi la Saudi Arabia.


ya Washington ilihakikisha
k wan za k wamb a silah a
zitakazouziwa Saudia
h a z i t a k u wa t i s h i o k wa
utawala dhalimu wa Israel.
Pamoja na kwamba Saudia
inaonekana kama sahiba
mkubwa wa Marekani, lakini
Israel ndiye msimamizi
mkubwa wa kiusalama wa
maslahi ya Marekani ndani
ya Mashariki ya Kati na
wakati huo huo akiwa ndiye
adui mkubwa wa nchi za
Kiarabu katika ukanda huo.
Aidha gazeti la Financial
T i m e s l i n a l o c h a p i s h wa
nchini Uingereza lilibainisha
katika ripoti yake kwamba,
pamoja na faida za kifedha
za Marekani kuiuzia silaha
Saudia, lakini pia hofu juu
ya Iran imekuwa chachu kwa
Marekani kuziuzia silaha
zaidi nchi za Kiarabu za
Ghuba ya Uajemi, ambazo
nazo hazijiamini mbele
ya jirani yao Iran. Bila
shaka kukosekana imani
huko kumechochewa na
propaganda za kiuadui za
Marekani dhidi ya Taifa
hilo la Kiislamu tangu
mapinduzi ya Kiislamu
ya mwaka 1979. Ni ukweli
ulio dhahiri kwamba Iran
inachukuliwa kama mpingaji
namba moja wa utawala wa
kidhalimu wa Israel, ambayo
ni kipenzi muhimu kwa nchi
za Magharibi na Marekani.
Mara baada ya ushindi
wa Mapinduzi ya Kiislamu
ya Iran, nchi za Magharibi
na hasa Marekani zimekuwa
zikizishawishi nchi za
Kiarabu za eneo la Ghuba
ya Uajemi kununua silaha

kwa wingi kwa kisingizio


kwamba, zijiweke tayari
kukabiliana na uchokozi
wowote wa kijeshi unaoweza
kufanywa na Jamhuri ya
K i i s l a m u ya I r a n , h a s a
ikizingatiwa kwamba taifa
hilo limepiga hatua kubwa
kijeshi na kiteknolojia
katika ukanda huo. Zaidi ni
kwamba madai hayo ya nchi
za Magharibi yamekuwa
yakitumika kukuza farka kati
ya Mataifa ya Kiislamu katika
ukanda huo kupitia fitna
ya Ushia na Usunni. Kwa
mujibu wa gazeti hilo, katika
kipindi cha hiki nchi za Saudi
Arabia, Umoja wa Falme za
Kiarabu - Imarati, Kuwait na
Oman zimepanga kununua
silaha na zana za kijeshi za
Marekani zenye thamani ya
dola bilioni 123 ambao ni
uuzaji na ununuzi mkubwa
zaidi wa silaha kufanywa
katika mazingira ya amani.
Weledi wa mambo wanasema
hatua ya utawala wa kifalme
wa Saudia ya kununua
silaha za Marekani zenye
thamani ya dola bilioni 30,
ina umuhimu mkubwa mno
kwa uchumi ulioporomoka
w a Wa s h i n g t o n , k i a s i
kwamba wanayachukulia
makubaliano ya ununuzi wa
silaha hizo kama msamaria
mwema na muokozi wa
uchumi wa Marekani.
Kwa upande mwingine,
nchi za Kiarabu za Ghuba
ya Uajemi zinaona kuwa
kununua silaha za gharama
ya dola bilioni 123 kutoka
Marekani, kutazisaidia
pia nchi zao huko baadae
kuandaa maelfu ya nafasi za

kazi kwa raia zake.


Mbali na hayo, Washington
inaonekana kuwa na lengo
jingine katika makubaliano
ya kuuza silaha kwa nchi
hizo, ambalo ni kuanzisha
mfumo na muundo mpya wa
usalama katika Mashariki ya
Kati kwa ajili ya usafirishaji
nishati hasa mafuta
kuelekea Magharibi. Kama
inavyofahamika falsafa ya
mashirikiano ya Marekani
kwa nchi nyingine, haina
adui wa kudumu wala rafiki
wa kudumu. Vile vile ni
falsafa ya Marekani kwamba
inathamini yule ambaye
atainufaisha zaidi kuliko yule
anayeweza kuitia hasara.
We l e d i w a s i a s a z a
Magharibi wanaona kuwa
Marekani ina malengo
mengine nyuma pazia
inayoyafuatilia na pengine
muhimu zaidi katika uuzaji
na urundikaji wa silaha
katika eneo la Mashariki ya
Kati. Nayo ni wafarakanishe,
uwagawe na daima uendelee
kuwanyonya kirahisi.
Mwaka 2010 Taasisi ya
Utafiti wa Kimataifa wa
Amani ya Stockholm SIPRI
imetangaza kuwa, Marekani
ni mdhamini mkubwa wa
silaha kwa nchi za Kiarabu
zilizoko katika eneo la Ghuba
ya Uajemi kati ya mwaka 2005
hadi 2009. Taarifa iliyotolewa
na taasisi hiyo imeeleza kuwa,
Marekani ina mauzo ya silaha
ya asilimia 54 ya kwa nchi za
eneo hili, huku ikifuatiwa na
Ufaransa ambayo ina asilimia
21 katika eneo nyeti la Ghuba
ya Uajemi.
Ta a s i s i h i y o i l i e l e z a

kuwa, baada ya Marekani


na Ufaransa, nchi nyingine
zinazouza kiasi kikubwa
silaha kwa nchi za Kiarabu
za eneo la Ghuba ya Uajemi,
ni Urusi, Uingereza na
China. Hata hivyo inaelezwa
kuwa, Saudi Arabia ndiyo
inaongoza kwa kununua
silaha kwa wingi katika eneo
hilo kuanzia mwaka 1990
hadi 2009, ikifuatiwa na
Umoja wa Falme za Kiarabu.
Uk weli ni k uwa k at ik a
miaka ya hivi karibuni Saudi
Arabia imenunua silaha za
mabilioni ya dola bila hata ya
kukabiliwa na tishio lolote la
adui wa kigeni katika miongo
mitano iliyopita. Mbali ya
nchi hiyo, Qatar, UAE,
Kuwait na Bahrain pia miaka
mitatu iliyopita zilisaini
makubaliano ya kijeshi
na Marekani, Uingereza,
Ufaransa na Ujerumani
yenye thamani ya zaidi ya
dola bilioni thelathini. Kwa
kuzingatia hali hiyo tunaweza
kusema kuwa viongozi wa
nchi za Kiarabu kwa muda
mrefu wamezigeuza nchi
zao kuwa maghala ya silaha
zinazonunuliwa kutoka nchi
za Magharibi kwa kutegemea
pato la mafuta, bila hata ya
kuzitumia silaha hizo. Leo
silaha hizo zinawaangamiza
wao wenyewe.
Wa k a t i M a r e k a n i n a
wenzake wa Mag harib i
wakilenga soko la silaha na
kupata mabilioni ya dola,
wakati huo huo zimekuwa
zikifanya kila linalowezekana
kuzusha anga ya hofu na
ukosefu wa amani, kwa
kuituhumu Iran kuwa ni
tishio katika eneo la Ghuba
ya Uajemi, lengo kubwa zaidi
likiwa ni kuuza silaha kwa
nchi za Kiarabu.
Sasa silaha zilizokuwa
zikilundikwa ghalani
zimepata pa kuzitumia.
Wanaouliwa si wengine
bali ni jamii ya Waislamu
kwa madhehebu yao.
Waliozitengeneza
wanaendelea kutengeneza
fedha, wanaendelea kukoleza
f a r k a . Wa s i o n a h a t i a
wanapoteza maisha. Syria,
Iraq, Yemen, Libya, Misri ni
mfano mzuri. Kwa mfano
usiku wa kuamkia April 4,
yalifanyika mashambulizi
ya a n g a d h i d i ya k i j i j i
kimoja kilicho karibu na mji
mkuu wa Yemen, Sana'a, na
kuangamiza familia moja ya
watu tisa. Taarifa zinasema
kuwa watu wengine
watano walijeruhiwa
katika mashambulizi hayo
yaliyofanywa na muungano

Inaendelea Uk. 17

10

Makala

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Haki za Waislamu na mipaka ya Jihad


B

Na Mussa Ame

AADA ya kuandika
makala iliyopita juu
ya ukafiri wa kuuana
Waislamu kwa Waislamu,
nilipokea simu nyingi
sana zilogawika katika
makundi matatu. Kundi
moja walinilaumu sana na
kuona nimefanya dhambi
kubwa sana. Kundi la pili
walipongeza. akini Kundi la
tatu waliniomba nifafanue
mada zaidi kwa vile kuna
vipengele vingi nilivikiuka.
Mada hii itafafanua baadhi
tu ya vipengele na mada
itaendelea mpaka pale
wasomaji watakapoelewa
lengo la mada hizi.
Kuhusu vita vya Somalia
nakiri kwamba hapo
mwanzo wakati Wasomali
walipokuwa wakipambana
na Ethiopia walikuwa katika
jihadi, na pia walipokuwa
wakipambana na majeshi
ya M a r e k a n i wa l i k u wa
katika jihadi. Sasa baada ya
Mataifa hayo kuona kuwa
h a wa we z i k u wa sh i n d a ,
wakatumia mbinu ya
kuwagawa Wasomali katika
makundi yenye kupingana
na wameliweza hilo. Sasa
Wasomali wanapiganishwa

wenyewe kwa wenyewe. Ni


katika hali hii sasa, jukumu
la Waislamu waliobakia
n i k u wa s u l u h i s h a s i y o
kuchochea vita kwa kusaidia
Kundi lolote lile. Kwani
Waislamu kupigana wao kwa
wao ni kitendo cha kikafiri.

Vita vya Somalia


vinatumiwa sasa kama mradi
wa Mataifa kujipatia fedha
za kupigana na ugaidi. Kwa
hivyo kuendelea kwa mzozo
huo, ni faida ya makafiri si
Uislamu. Nchi zinazoshiriki
kulinda amani, hujivunia

mamilioni ya fedha ndiyo


maana wao hupendelea
mzozo usimalizike.
Ama kuhusu mapigano
yanayotokea huko Syria,
Yemen na Iraq pia ni vita
vya wenyewe kwa wenyewe.
Wanaouwa ni Waislamu na

wanaouliwa ni Waislamu na
damu ya Muislamu ni takatifu
sana ni haramu kuimwaga.
Na vita hivi vinapangwa na
makafiri kwa kuwashawishi
Waislamu kupigana kwa
visingizio mbali mbali, na
Wislamu hukumbwa na jazba
wakaingia vitani kumwaga
damu za wasio na hatia.
Leo nimeombwa nifafafue
haki za Muislamu, pia
wasomaji wengine wanataka
nielezee ni wakati gani huwa
halali kumuua Muislamu,
lakini naona mada hiyo
akipenda Allah (SW) nitaitoa
baadaye.
Allah (SW) anasema: Na
saidianeni katika wema na
uchaungu, wala msisaidiane
katika dhuma na uadui na
mcheni Allah (SW) hakika
Allah (SW) ni mkali wa
kuadhibu. (Maidah :2)
Katika kuifafanua aya
hiyo, amesema Imamu
Ta b a r a n y ( 1 / 2 2 7 ) k u wa
amesema Mtume (SAW)
Atakayekwenda kumsaidia
dhalimu na anajua kuwa
ni dhalimu ametoka katika
Uislamu.
Mtu huyu hawi kafiri wa
imani kwamba si Muislamu

Inaendelea Uk. 11

Jihad kuangamiza Waislam


Somalia na siasa za Zanzibar
Na Omar Msangi

MAALIM Seif Sharif Hamad

AKUMBUKA
n i l i w a h i
kuhudhuria
M k u t a n o m m o j a wa
REDET Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam. Ilikuwa
ni katika kile kipindi
cha Muwafaka wa Pili
wa Zanzibar baada ya
ule uliofuatia Uchaguzi
Mkuu wa 1995. Katika
Mkutano huo aliyekuwa
Waziri Kiongozi, Shamsi
Vuai Nahodha aliusifia
sana Muafaka huo
akisema kuwa ni wa
kupigiwa mfano kwa
sababu umetokana na
Watanzania wenyewe.
Kwamba haukuwa sawa na
ule wa awali uliovunjika
uliokuwa umesimamiwa
na akina Anyauko. Na
akahitimisha kwa kusema
kuwa huo ulikuwa ni
ushahidi kuwa Waafrika/
Watanzania, tunaweza

kutatua matatizo
yetu wenyewe bila
k u s i m a m i wa n a m t u
kutoka nje.
Kwa bahati mbaya hata
muafaka huo haukuzaa
m a t u n d a ya l i y o k u wa
yametarajiwa. Zanzibar
iliendelea kuonja tamu ya
siasa za chuki, uhasama,
visa vya Janjaweed
n a m e l o d y . Wa t u
wakaendelea kuuliwa,
kupigwa, yakawepo madai
ya kubakwa wanawake,
kuporwa mapambo yao
ya dhahabu na visa vya
kila aina.
Ukilitizama jambo
hili na yaliyokuja kujiri
baadae, unakuta kwamba
kumbe Zanzibar walikuwa
wamejidanganya kwa
kudhani kuwa wakikaa
kama CCM (Bara na
Visiwani), au kama
Watanzania, ni wamoja.
Rais Mstaafu Amani Abeid
Karume na Maalim Seif,

chini ya uongozi wa kamati


ya Wazee na Kamati ya
Maridhiano, walilitambua
hilo wakakaa kama
Wazanzibari. Wakafikia
Muafaka ulioleta amani
na utulivu. Muafaka
ulioleta Serikali ya Umoja
wa Kitaifa iliyofanya
Zanzibar ipumue.
Ukitizama yaliyojiri
katika Bunge Maalum la
Katiba lililopita Dodoma,
na kauli zinazoendelea
hivi sasa kwa upande
wa wa n a o i t wa C C M ,
Wahafidhina, Zanzibar
inaelekea kumeguka
warudi kule kule
walikokuwa. Hawa
Wazanzibari wahafidhina,
ni wazi kuwa nguvu yao
kubwa ni kwa CCM (Bara)
ambako ndio kwenye
serikali. Hali iliyojitokeza
Dodoma ikiendelea, ni
wazi hii hali ya muafaka
na maridhiano itakufa na
Inaendelea Uk. 11

Dkt. Ali Mohamed Shein

11

AN-NUUR

Makala

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Haki za Waislamu na mipaka ya Jihad

Inatoka Uk. 10

tena, ila ametenda vitendo


vibaya kinyume na desturi ya
Waislamu. Tuelewe utukufu
wa Muislamu na ubaya wa
kumuua Muislamu mmoja
tu aliyetoa shahada. Allah
(SW anasema: Kwa sababu
ya hayo tukawaandikia
wana wa Israili kwamba
atakayemwua mtu bila ya
yeye kuua mtu, au kufanya
fisadi katika nchi ni kama
amewaua watu wote, na
mwenye kumwacha mtu hai
(kumsaidia kuishi) ni kama
amewaacha hai watu wote.
Na bila shaka Mitume wetu
waliwafikia na hoja zilizo
wazi, kisha wengi katika
hao baada ya haya walikuwa
waharibifu sana katika nchi.
(Maida:32).
A ya h i y o a m e i t a f s i r i
I b n u A b b a s ( R A) k u wa
atakayezuia watu na kuua
watu wasio na hatia, huyu
ni kama amewahuisha wale
watu wote na atakayeua nafsi
moja, ni kama ameuwa watu
wote.
Said bn Jubayri (RA)
amesema, atakayehalalisha
damu ya Muislamu mmoja
asiye na hatia ni kama
amehalalisha damu ya

Inatoka Uk. 10
yaliyojiri hivi karibuni
katika msafara wa CUF
wa k i t o k a m k u t a n o n i ,
ni kwamba melody na
Janjweed yaweza kurejea
na Serikali ya Umoja wa
Kitaifa itaporomoka.
Ikifikia hapo, CCM
wahafidhina watapata
nguvu kubwa kutoka Bara
na pengine hata Jumuiya
ya Kimataifa na watakuwa
n d i o we n ye s e r i k a l i .
Waliosalia watakuwa Al
Shabaab. Wapizani wa
wahafidhina.
Ukisimama upande
wa hawa CCM na CUF
wanaotaka maridhiano
na serikali ya Umoja
wa Wazanzibari, hawa
wahafidhina nao
wanapewa nguvu kubwa
kutoka CCM, Bara na
Jumuiya ya Kimataifa.
N i Wa z a n z i b a r i
wa n a r a r u l i wa .
Wanararuana wenyewe
kwa wenyewe. Sera ya
wagawe uwatawale
inafanya kazi. Hakuna
kinachoendelea, si
katika elimu, uchumi
wala huduma za kijamii.
Zanzibar inabaki doro.
Kwa maana hii, CCM
Ba r a a u k u ndi l ol ot e
litakalodai kwamba
linaisaidia Zanzibar kwa
kuliunga mkono kundi

Waislmu wote duniani, na


atakayeharamisha damu ya
Muislamu mmoja ni kama
ameharamisha damu ya
watu wote. Na amesema
Mujahid (RA) atakayemuua
Mislamu mmoja tu
makusudi pasi na hatia
malipo yake ni moto. Allah
(SW) atamghadhibikia na
atamlaani na atamtayarishia
dhabu kali sana. Maneno
hayo ya Mujahid (RA ), ni
sawa na aya aya Suratulnisai
93 Na mwenye kumuua
Muislamu kwa kukusudia,
malipo yake ni jahannam,
humo atakaa milele, na
Allah(SW) amemghadhibikia
na amemlaani na
a m e m wa n d a l i a a d h a b u
kubwa.
Amesema Ibn Kathyr
katika aya hiyo kuna
makemeo makubwa sana
kwa anayeua kwa makusudi
kumuua Muislamu. Na
wameona Maulamaa wengine
kwamba atakayemuua
Muislamu kwa makusudi na
akafa hakutubia, basi ataingia
motoni milele, na kwa vile
atakuwa amelaaniwa. Ni
kutokana na uzito wa aya
hizo, ninahisi iko haja ya
kuzinduana kwa sababu kuna

MMOJA wa wananchi wa Yemen.


watu hufikiria kuwa kumuua
Muislamu ni jambo la mchezo.
Akishakuwa hakubaliani na
itikadi yako basi unaweza
kumchinja kama kuku.
Wako waliokuwa na fikra
ya kwamba kusimamisha
dola, kunahalalisha mauaji

ya Waislamu. Ni kutokana
na uzito wa aya hizo, ninahisi
iko haja ya kuzinduana kwa
sababu kuna watu hufikiria
kuwa kumuua Muislamu
ni jambo la mchezo
akishakuwa hakubaliani na
itikadi yako basi unaweza

Jihad kuangamiza Waislam


Somalia na siasa za Zanzibar

la Wahafidhina wasio
taka Serikali ya Umoja,
litakuwa linadanganya.
Haliwatakii mema
Zanzibar. Kwa upande
mwingine, mtu yeyote wa
nje, iwe ni CHADEMA,
NCCR au taasisi nyingine
yoyote, itakayosimama na
Wazanzibari kupambana
na CCM wahafidhina,
hataweza kuondoa tatizo
bali kutia petrol katika
moto. Itakuwa sasa
ushabiki wa kupingana
tu mradi kupingana
kama ilivyojitokeza pale
Dodoma. Namna pekee ya
kuwasaidia Wazanzibari,
ni kuwasaidia waweze
kukaa pamoja kama
Wazanzibari na kutambua
agenda zao ni zipi,
salama yao kama nchi
ipo wapi, fursa walizo
nazo, changamoto,
nguvu walio nayo,
madhaifu yao, maadui
na kila linalowahusu
kama Wazanzibari. Kama
hilo likishindikana, kwa
siasa hizi tulizoshuhudia

RAIS wa sasa wa somalia


Sheikh Mohamoud.
Dodoma, Mungu aepushie
mbali, laweza kuishia
katika kuraruana wenyewe
kwa wenyewe.
Sasa jaalia muafaka
huu wa kuwa na Serikali
ya Umoja wa Kitaifa,
uliwapeleka kuwa na
S e r i k a l i k a m a i l e ya
Umoja wa Mahakama za

Kiislamu Somalia. Baadae


wengine wakarudi katika
m e l o d y wa k i wa n a
CCM Bara na Jumuiya
ya Kimataifa nyuma yao.
Ikifikia mtafaruku wa
kuvunjika serikali hiyo,
mtu akitoka Bukoba,
Kigoma, Mwanza akidai
kuwa anakwenda Jihad
Zanzibar kwa kusimama
upande wa kundi moja
la Wazanzibar, hakuna
anachoweza kuwasaidia
z a i d i ya k u wa s a i d i a
kuuwana nwenyewe kwa
wenyewe.
Kisiasa
hapo
inawezekana kulikuwa na
matatizo ya namna mbili.
Moja ni kuwa inawezekana
hata katika kuweka
maafikiano yaliyozaa
Serikali ya Umoja wa
K i t a i f a , p a l i k u wa n a
ubinafsi. Watu walikuwa
wakitizama mbele maslahi
yao binafsi, sio nchi,
na wananchi. Kama si
hivyo, basi yalikuwa ni
maafikiano ya viongozi
wa juu tu, lakini makada

kumchinja kama kuku.


Wako waliokuwa na fikra
ya kwamba kusimamisha
dola a Kiislamu ni kwa
mapambano ya silaha, lakini
jee unapambana na nani na
Muislamu mwenzako?
Uislamu umekataza
kusimamisha jambo la
halali kwa kutumia njia za
haramu. Damu ya Waislamu
inayomwagwa Iraq, Syria,
Yemen na Somalia inafaa
tuiangalie kwa mtazamo
mpana zaidi. Jee, mizozo
hii ni lazima itatuliwe kwa
mtutu wa bunduki? Hakuna
suluhu katika mambo haya?
Kwa nini ni sisi Waislamu
tunaouwana sana kila
wakati. Iran ilipigana na
Iraq na waliokufa ni
m a e l f u y a Wa i s l a m u ,
baadaye tena, Waislamu
hao wakadanganywa kuwa
wakimuua Sadam Hussein
watakomboka, matokeo
yake ni vita isiyo na mwisho
mpaka leo. Waislamu wa
Libya wakatumiwa tena na
NATO wakihadaiwa kuwa
watasimamisha Uislamu
kwa kumuondoa Gaddafi,
maelfu wakauawa, majengo
yakabomolewa, mafuta yao

Inaendelea Uk. 13
waliowazunguka (CCM),
pengine na sehemu
ya wananchi (CCM)
hawakuwa tayari.
Sasa suala hapo haliwi
kushikiana mtutu, bali
Dawah/Elimu/Ufahamu.
Hawa makada wafikie
mahali waone kuwa
masilahi ya Zanzibar na
Wazanzibari, ni muhimu
zaidi kuliko masilahi yao
ndani ya CCM.
Toka imeporomoka
serikali ya Siad Barre,
Wasomali wamekuwa
katika machafuko. Juhudi
zote za kimataifa kuwaleta
pamoja zilifeli mpaka
i l i p o i b u k a U m o j a wa
Mahakama za Kiislamu.
Mara baada ya nchi kutulia,
m a b e b e r u wa l i o k uwa
wakichochea mgogoro
huo na ambao walikuwa
hawataki Somalia iwe na
amani, hilo likawa pigo
kubwa kwao. Kwanza
waliwachukua wale wale
wababe wa Kivita, wakawa
wanawasadia kupambana
na Serikali ya Umoja wa
Mahakama za Kiislamu.
Mabeberu wasivyokuwa
n a h a ya wa l a k u o n a
vibaya, eti hawa wababe
wa kivita ndio wakapaewa
hadhi na wadhifa kuwa
wanapambana na magaidi.
Magaidi wenyewe, eti
Inaendelea Uk. 13

12

MAKALA/MASHAIRI
SIASA NA DINI

1. Hebu niulize swali, mnipe jibu watunzi


Shida imenikabili , kwenu naomba ujuzi
Nielewe tafaswili , linitoke bumbuwazi
Hivi siasa na dini , zatofautishwa wapi
2. Siasa ni ya awali ,dunia imebarizi
Mitindo ya serikali , hasa zama zetu hizi
Viongozi mbalimbali, wanatupa shinikizi
Hivi siasa na dini, zatofautishwa wapi
3. Dini yaja namba mbili, nayo inatupa kazi
Tumekuwa madhalili, kwa nini hatujifunzi
Tumetupilia mbali, twafuata mageuzi
Hivi siasa na dini, zatofautishwa wapi
4. Siasa za viririrni, sasa zimeshika kazi
Ni mashuhuri nchini, kila kona ziko wazi
Zinatufundisha nini, na tufanye upembuzi
Hivi siasa na dini, zatofautishwa wapi
5. Maimamu membarini, hawajachoka kuazi
Mashekhe madarasani, watafuta wanafunzi
Mbona hatuonekani, kiwapi kipingamizi
Hivi siasa na dini, zatofautishwa wapi
6. Malenga wa redioni, naomba ufafanuzi
Nanyi wa magazetini, mlango wenu uwazi
Kwetu siasa na dini, uko wapi ubaguzi
Hivi siasa na dini, zatofautishwa wapi
7. Tamati natumaini, majibu kwenu wapenzi
Ifanyeni tathmini, msione upuuzi
La faida tubaini, litufae kwa Mwenyezi
Hivi siasa na dini, zatofautishwa wapi
Mtunzi ni:Zainab Mtima
Mbweni, Zanzibar
0717 165 602

NONGWA YA MAHKAMA YA KADHI


Adayo hupendeleya, wa dinenu wapinzani,
Mazuri kuyazuiya, yenu pasi hata soni,
Kukuswibuni mabaya, wao ndilo hutamani,
UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.
Daima huwatakiya, yale yanokudhuruni,
Ya shururi huridhiya, ninyi yanokufikeni,
Ya khairati udhiya, yenu kwao ng'amueni,
UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.
Gaidhi i dhahiriya, kutoka mwao vinywani,
Vyanda wanawaumiya, kwa indazo mitimani,
Waloficha batiniya, kungaye i kwa MANANI,
UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.
Si kwamba nawazuliya, ishanena QUR-ANI,
SURA ya TATU rejeya, si nyingine IMRANI,
AYA nawakashifiya, hayo zenye kubaini,
UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahahiriya.
MIATU wa THAMANIYA, ASHARA kwa tamakuni,
Soma thuma endeleya, hadi MIA ISHIRINI,
Humo utajioneya, yote kwa wake ndani,
UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.
ALLAH alotuambiya, si dhahania yakini,
Wenyewe mwashuhudiya, yawahusu wao nini!
MAHKAMA kugomeya, ya KADHI mahakamani?
UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.
Na hofu wamewatiya, viongozi wa nchini,
Si kwa hoja usuliya, kwa pogo yao mizani,
Lengo walokusudiya, lipate kuyumkini,
UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.
Nudhumu namaliziya, kwa nyote kukuombeni,
Kujifunza kuteteya, kwa pamoja yenu dini,
'Wenzenu' huwa pamoya, kwa yao hamuwaoni?
UKWELI wa QUR-ANI, si kombo u dhahiriya.
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Tujifunze kujadiliana kwa nguvu ya hoja


Inatoka Uk. 8

ni anuwani hii ndogo


'Tujifunze kujadiliana
k wa n g u v u ya h oja ' .
Kimsingi, hili ndilo suala
nililokusudia kulijadili
katika makala hii kupitia
mazungumzo yale ya
kundini na mfano ule wa

mashambulizi dhidi
ya Bw. Omar Msangi
nilioutoa hapo juu.
N i l i t a r a j i a
mwasilishaji taarifa
angejikita zaidi katika
maudhui ya mada ya
mjadala na kutupa hoja
mbadala kutoka katika
Qur-an na/au Sunnah
kwa kuonyesha kuwa
' K we n d a K u p i g a n a
Somalia si Ukafiri' kama
alivyofanya Bw. Mussa
Ame katika makala
yake yenye anuwani
' K we n d a K u p i g a n a
Somalia ni Ukafiri'.
Badala
yake
akakimbilia kulijadili
gazeti kwa kudai kuwa
limepoteza mwelekeo.
Bila kuathiri uhuru
wake wa kutoa maoni,
yumkini kwa maoni
yake hilo ni sahihi, nami
sina haja ya kuonesha
upinzani wowote juu ya
maoni yake kuhusu hilo,
ninachokishadidia hapa
ni kwamba mwasilishaji
taarifa ameshindwa
kukabiliana na maudhui
ya mada ya msingi kwa
nguvu ya hoja na badala
ya k e a n a l i s h u t u m u
gazeti lililotumika kama
nyenzo ya kuwasilisha
makala ile kwa
wasomaji; hali ni hiyo
hiyo kwa mchangiaji wa
kwanza na wa pili.
Hoja ya kujadiliwa
hapo haikupaswa
kuwa gazeti, kwani
lenyewe limetumika
kama nyenzo tu ya
kuwasilishia maudhui
kilichopaswa kujadiliwa
ni hoja ya Bw. Mussa
Ame.
Hilo linanikumbusha
ile kadhia ya
kushupaliwa na
hatimaye kufungiwa
kwa Redio Iman na
Mamlaka ya Udhibiti wa
Mawasiliano baada ya
kushindwa kuzikabili
hoja zilizokuwa
z i k i r u s h wa h e wa n i
kupitia chombo hicho
cha habari.

Katika sehemu ya
pili, mwasilisha hoja
ameshughulika na
wa n a h a b a r i b a d a l a
ya kushughulika na
habari iliyowasilishwa
n a m wa n d i s h i , h i i
ni sawa na kusema
ameshughulishwa
zaidi na mwandishi wa
habari-makala ile kuliko
maudhui ya makala
husika.
Vilevile, Kwa kuwa
mwandishi ameonesha
kwa mujibu wa Quran na Sunnah kuwa
kinachojiri Somalia
si jihadi, kwa hiyo
mwasilishaji wa taarifa
alipaswa kutoa dalili
mbadala kutoka katika
Qur-an na/au Sunnah
zenye kuonyesha
kwamba kinachojiri
Somalia ni jihadi badala
ya kutaka aonyeshwe
mahali jihadi ilipo,
kwani suala hilo si lenye
kuhusiana na maudhui
ya mada ya msingi ya
mwandishi.
Mchangiaji wa tatu na
wa nne, wao wameishia
kutoa kejeli kwa
mwandishi badala ya
kushughulika na hoja
yake.
Katika sehemu
ya tatu, mwasilishaji
taarifa anaonekana
kuvuka mpaka na
kumshambulia moja
kwa moja mhariri wa
gazeti hili badala ya
kushughulika na hoja ya
mwandishi wa makala
i l e k wa k u o n ye s h a
kuwa 'wanaopigana
Somalia si Waislamu
kwa Waislamu' kama
alivyobainisha yeye
katika makala yake
kuwa 'wanaopigana
Somalia ni Waislamu
kwa Waislamu'.
Mchangiaji wa tano
ameishia kumkufurisha
mwandishi wa makala
badala ya kujibu hoja
zake kwa nguvu ya hoja
mbadala.
Katika sehemu
ya nne, mwasilishaji
taarifa anadai kwamba
yeye na vijana wengine
walimpinga mhariri
alipoleta mada kama
hiyo katika semina kule
Kirinjiko Same. Japo
hakubainisha kama

walitumia nguvu ya
hoja au hoja ya nguvu,
yumkini walitumia hoja
ya nguvu ndio maana
pakatokea vurugu kama
anavyodai !
Yote kwa yote hata
kama walitumia nguvu
ya hoja kufanikisha
mapambano yao dhidi
ya mhariri mwenyewe

au hoja zake; kwanini


basi leo anashindwa
kukabiliana na hoja ya
mwandishi na badala
yake anaendelea na
mashambulizi yake
d h i d i ya m h a r i r i
ambaye kimsingi
hahusiki moja kwa
moja katika hoja
iliyotolewa na Bw.
Mussa Ame.
Mchangiaji wa
sita, wa saba na wa
nane, wao wameishia
kushadidia kutoa
kipigo dhidi ya mhariri
kule Kirinjiko huku
wakiiacha hoja ya
msingi ya mwandishi
ikielea hewani pasi na
kuikabili kwa nguvu
ya hoja mbadala.
Mwasilishaji taarifa
na mchangiaji wa
tisa wanaonekana
wakihitimisha
mazungumzo kwa
kuzidi kupambana
kwa hoja ya nguvu
na mhariri badala
ya kushughulika
na hoja ya msingi
ya mwandishi kwa
nguvu ya hoja.
Kwa muktadha
huu, ndio maana
naona kuna ulazima
na umuhimu wa
kujifunza kujadiliana
kwa nguvu ya hoja na
si hoja ya nguvu. Haya
shime ndugu zangu,
tuanze sasa kujifunza
hili kupitia kisa cha
Nabii Ibrahimu (a.s.)
na Mfalme Namrudha
(2:258).
(Mwandishi wa
makala hii ni msomaji
wa muda mrefu wa
gazeti la AN-NUUR
anayeishi jijini
Mwanza).

13

Makala

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Haki za Waislamu na mipaka ya Jihad


Inatoka Uk. 11

yakaibiwa na mpaka leo


hakuna Uislamu uliosimama
ila ni vita vinavyoendelea.
Mabeberu na NATO yao
wa n a v u n a n a k u k o m b a
mafuta bila ya udhibiti kutoka
serikalini kama ilivyokuwa
wakati wa Gaddafi. Hivi
hatuna akili sisi? Hatuyaoni
haya?
Syria kunatokea umwagaji
mkubwa wa damu, Somalia
miaka kadhaa ya vita
visivyokwisha, tumebakia
kumtaka Muhali Mungu
kwa kunyanyua mikono
kuomba Allahuma nsuru
Mujahidina fii Suria wa
Somalia, wa Iraq, wakati
tumekuwa kama vikaragosi
wa mabeberu tunaotumiwa
bila kutumia akili.
Afghanistan hatukujifunza,
Iraq hatukujifunza, Libya
hatukujifunza, sasa tupo
na IS, Al Shabaab, sisi watu
gani? Haya tumeanzishiwa
tena Yemen. Sasa kwa Yemen,
ni upande upi upo katika
Jihad? Saudi Arabia na
washirika wake au Wahoudh
na wananchi wa Yemen kwa
ujumla!
Waislamu walipouliwa
Jamhuri ya Afrika ya
Kati hakuna harakati
iliyohamasisha kupeleka

Inatoka Uk. 11
ni Serikali iliyotokana
na wananchi wenyewe
wa Somalia baada ya
Jumuiya ya Kimataifa
kushindwa kuleta amani
Somalia kama miafaka
iliyoshirikisha watu
kutoka nje ya Zanzibar
ilivyokwama.
Wa l i p o f e l i . N d i o
wakavamia kijeshi.
Wa k a i t u m i a E t h i o p i a
i k a va m i a i k a a n g u s h a
Serikali ya Umoja wa
Mahakama za Kiislamu.
Lilipotokea hilo,
Wasomali wakagawika
kama ambavyo hivi sasa
Wazanzibari wanataka
kugawika kuondoa Sera
ya Serikali ya Umoja wa
Kitaifa. Kundi likaenda
Nairobi kuunda Serikali
inayotakiwa na mabeberu
na kundi likabaki Somalia
na kuibuka Al-Shabaab.
Hawa waliounda Serikali
ya Mpito, walikuwa wale
wale waliokuwa viongozi
wa Serikali ya Umoja wa
Mahakama za Kiislamu.
Na hawa Al-Shabaab, vile
vile ni katika waliokuwa
katika Umoja wa
Mahakama za Kiislamu.
Ukichukulia mahesabu
mepesi kuwa hawa walio
serikalini wameritadi, ni

MOJA ya Ndege za kivita za Saudi Arabia zinazotumika kuishambulia Yemen.


wapiganaji kwa sababu
mabeberu walikuwa
hawakulitaka hilo kwa hiyo
hawakuleta mawakala wao
huku kuhamasisha Jihad. Au
wale waliokuwa wakiuliwa
Afrika ya Kati hawakuwa
Waislamu? Tena kama ni
Jihad ingekuwa ile maana
kule ilikuwa wazi-Wakristo
huku Waislamu kule. Mbona
hilo hatukuona likishabikiwa
kama hili la Somalia na Syria
inaloratibiwa na Wamarekani
na Mayahudi?
Wa k a t i Wa i s l a m u wa
B o s n i a wa l i p o u l i wa n a

kunajisiwa nchi za Kiislamu


zilinyamaza kimya,
hakuna nchi ya Kiislamu
iliyopeleka jeshi. Wapalestina
wanapouliwa na Waizraeli
hakuna umoja wa nchi za
Kiarabu wala harakati ya
ukombozi inayopeleka jeshi
na kuhimiza watu kwenda
huko kuwasaidia ndugu zetu
Wapalestina bali hufunga
mipaka yao mpaka misaada
wanayoletewa Wapalestina
na mashirika ya makafiri
isiwafike. Lakini leo Umoja
huo huo wa nchi za Kiarabu/
Kiislamu zipo na Marekani/

Israel kuipiga Syria, Iraq,


Yemen na Somalia! Hatuoni?
Hatujiulizi? Hatuna akili?
M t u m e ( S A W )
alitahadharisha sana
kuhusu haki za Waislamu.
Amesimulia Abuu Hurayra
(RA) amesema Mtume(SAW)
msihusudiane wala
msizidishianeni bei
minadani, msibughudhiane,
msihamane, wala asinunue
mtu juu ya bei ya mwenzake.
Kuweni waja wa Allah (SW)
mlio ndugu. Muislamu ni
ni ndugu wa Muislamu
mwenziwe, asimdhulumu

Jihad kuangamiza Waislam


Somalia na siasa za Zanzibar

wanafiki, ni makafiri, hapo


ndio tunapokosea. Wale
bado ni Wasomali, kama
ambavyo Al-Shabaab ni

Wasomali. Wakipigana
n i Wa s o m a l i k w a
Wasomali wanaopigana.
N i Wa z a n z i b a r i ,

wahafidhina wasiotaka
Serikali ya Umoja wa
Kitaifa, wanaopigana na
wanaotaka maridhiano.

BAADHI ya wananchi wa Somalia walioathiriwa na vita vinavyoendelea nchini humo.

azimdhalilishe wala
asimdogoshe. Uchamungu
upo hapa, akaashiria
moyoni mwake mara tatu,
Muislamu kwa Muislamu
mwenzake ni haramu damu
yake (asiimwage), mali yake
(asiichukue kwa dhulma) na
heshima yake (asiivunje).
(SM2564).
Usama bni Zayd (RA)
alipigana na kafiri katika
vita. Yule kafiri alipoona
anashindwa alitoa shahada,
lakini baadaye alipigana
tena upande uleule wa
makafiri. Usama bin Zayd
(RA) akakutana naye tena
wakapigana, na yule kafiri
akatoa shahada tena, na mara
ya tatu wakapambana mpaka
akampiga mkononi, mara ya
tatu wakapambana na akatoa
shahada tena mara ya tatu,
mara hii Usama bin Zayd
(RA), alimuua yule Muislamu
kwa sababu kwanza alikuwa
anafanya masihara ya
kusilimu. Alimpiga Usama
(RA) upanga. Habari hii
alipoisikia Mtume (SAW)
alikasirika na alimgomba
Usama (RA) na alimuuliza
jee ulimuua mtu baada ya
kutoa shahada na alimlipia
jizya, fidia. Katika riwaya
nyengine alimuuliza Usama,

Inaendelea Uk. 16

Mshindi katika vita


hiyo nani? Hakuna na
kutakuwa hakuna
wakiendelea hivyo. Kile
alichoeleza Mzee Nassoro
Moyo kilichofanyika kabla
na baada ya uchaguzi
mkuu Zanzibar, ndicho
pekee cha kuwapa
Wazanzibari ushindi na
ndicho pekee cha kuwapa
ushindi Wasomali, kama
utazungumza kwa
mtizamo wa kisiasa au
kidini. Na ndio Uislamu
na Quran inavyoagiza,
mnapogombana ndugu,
Wa z a n z i b a r i k wa
Wazanzibari, Wasomali
kwa Wasomali, Waislamu
kwa Waislamu, haijalishi
kama kundi moja litawaita
we n g i n e wa n a f i k i a u
makafiri, bado sumu ya
kutengana, kufarakana na
kugombana wenyewe kwa
wenyewe itawatafuna.
Na maadui wataingia
kusaidia pande zote mzidi
kutafunana. Al-Shabaab
h a wa n a k i wa n d a c h a
silaha. Kinachowafanya
wasipungukiwe na silaha
ni nini?
Wiki iliyopita niligusia
na kutoa ushahidi kuwa
silaha zinazotolewa na
Umoja wa Mataifa pamoja
na zile zinazotolewa na
Inaendelea Uk. 16

14

Makala

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Mchango wa Waislmau katika maendeleo ya Dunia


Abu Mussa Jabir bin Hayyan-(7)

Na Ben Rijal
Na Ben Rijal
ABUU Mussa Jabir Ibn
Hayyan ni katika ya
wasomi waliokuja kupata
msukusuko wa kufungwa
kifungo cha nyumbani
na babake naye kuuliwa
na watawala. Kati ya
wasomi wa siku hizo
waliokumbana na mateso
kutokana na viongozi
huwezi kusoma bila ya
kutajwa Jabir Ibn Hayyan.
Jabir Ibn Hayyan
katika midani za Ulaya
anajulikana kwa jina la
Geber, amezaliwa katika
mji wa Tus uliopo Iran
katika mwaka wa 721 na
wengine husema kuwa
amezaliwa mwaka wa 722.
Uasili wake haufahamiki
wengine wanafahamisha
kuwa ni Mfursi na wengine
wanatueleza kuwa ni
Mwarabu mwenye asili
ya Yemen.
Baba yake Hayyan al
Azdi alikuwa ni mfamasia
mjuzi wa uchanganyishaji
wa madawa na muungaji
mkono mkubwa wa
uongozi wa Banu Abass
d h i d i ya u o n g o z i wa
Banu Umayya wakati
akiishi katika mji wa Tus
nchini Iran. Kutokna
na misimamo yake hio,
alikamatwa na kuuliwa
t u k i o h i l o l i k a i f a n ya
familia yake kuhama Tus
na kuhamia Yemen na
hapa ndipo utatanishi
unapokuja juu ya asili ya
Jabir bin Hayyan wengine
husema ni Muarabu na
wengine husema kuwa ni
Mfursi.
Baada ya kukaa Yemen
na familia yake, msomi
huyu alirudi Kufa na
akasoma kwa Imam Jafer
al Sadiq na alipomaliza
m a s o m o ya k e a k a wa
anafanya kazi ya utabibu
wakati wa zama za Khalifa
Harun al Rashid. Katika
kuwa karibu na wakubwa
sio mara zote mtu hubakia
katika hali ya kukubalika

moja kwa moja kwani


alipofariki Khalifa Harun
al Rashid katika mwaka
wa 815, Jabir bin Hayyan
alikamatwa na kutumia
maisha yake yote yaliobaki
kuwa katika kifungo cha
nyumbani ikimaanisha
kuwa hakuwa na ruksa ya
kutoka nje ya nyumbani
kwake.
Somo la Kemia likiwa na
mchanganyiko wa mambo
ya kiroho (alchamey) ndio
alipozama sana na alikuwa
mcha Mungu na kila akikaa
alikuwa akifanya tafiti
alizokuwa anaziunganisha
na imani yake ya dini
kwani aliathirika sana na
mwalimu wake Imam Jafar
al-Sadiq.
Kila somo huwa na
m u a n z i l i s h i wa k e n a
kuelezewa kuwa fulani
ni baba wa somo hilo
(father of ) Jabir Ibn
Hayyan husemwa kuwa
yeye ndio baba wa somo
la Kemia kutokanana kazi
zake nyingi alizozifanza
na kugundua mambo
mbalimbali katika uga
wa kemia. Mbali na somo
la kemia Jabir Ibn Hayyan
alizama katika somo la
nyota, ufamasia, udaktari,
falsafa na uhandisi.
Inafahamika kuwa
utaalamu wake wa somo
la kemia ndio uliokuja
kuwapa mwongozo
Priestly na Lavoisier katika
karne ya 18 kwenye uwanja
wa kemia.
Jabir Ibn Hayyan
aliweza kugundua aina
ya vitu 19 katika uwanja
wa kemia na kwa kisasa
vitu hivyo vimepewa jina
la element.
Jabir Ibn Hayyan
a n a e l e z e wa k a m a n i
mtu mmoja wa mwanzo
alioanza kufanya
majaribio katika somo la
kemia, akifanya majaribio
ya kugeuza aina moja
ya kiungo cha maji maji
na kukileta katika aina
nyengine. Aidha alikuwa
akifanya majaribio ya
kuangalia aina ya vitu
vinavyokuwa vigumu
kisha vikawa kidogokidogo
vinabadilika na kuwa
na umaji maji. Katika
majaribio hayo aliweza
kugundua aina ya tindikali
ijulikanayo kwa jina la
acetic acid na kuweza
kufahamu kuwa siki nayo
ina maumbile ya tindikali,
akenda mbali zaidi pale
alipoweza kuitengeneza
tindikali ijulikanayo
kama hydrochloric acid,
akaja kugundua tindi kali

Abu Mussa Jabir bin


Hayyan

Mchoro unaomuonyesha
Jabir na vyombo
alivyokuwa akivitumia
ijulikanayo regia yenye
uwezo wa kuyayusha
dhahabu, akaipata
tindi kali ya citric acid
kutokana na ndimu na
jamii ya miti hiyo kama
machungwa na kugundua
aina ya tindikali ya tartaric
acid inayopatikana na
mabaki yaliotengenezewa
pombe ya wine. Kazi hizi
alizozifanya zilikubalika
na kuelezewa kuwa ni

mafanikio makubwa ya
somo la kemia zaidi ya
miaka alfu iliopita.
Jabir Ibn Hayyan
alivigawa vitu katika
makundi matatu
alipokuwa anafanya
majaribio. Kundi la
kwanza akaliita kundi la
spiriti ambalo vitu vyake
ukivipasha moto hupotea
kwa mvuke ikijumuisha
sulfur, ammonium
chloride na kundi la pili
akalita la metali ikiwemo
shaba, dhahabu, vyuma na
fedha na kundi la mwisho
ni vitu ambavyo havimo
katika kundi la vyuma na
dhahabu mfano wa jabali,
mkaa n.k. Mgao huu ndio
ukaja kutumiwa katika
mgao wa vitu vya metali
na visio vya metali.
Kuzama kwake katika
s a ya n s i n a u j u z i wa
kemia kulimsukuma
kuchanganya na masuala
ya kiroho. Alikuwa
akipenda kufanya
majaribio ya kila aina.
Aliweza kutengeneza
aina ya karatasi ambayo
ukiichoma kwa kibiriti
haiwaki. Na akatengeneza
a i n a ya w i n o a m b a o
unaweza kusoma ndani
ya giza. Katika vyombo
alivyokuwa akivitumia
katika majaribio ni aina
ya chombo kijulikancho
retort, pipette ya kuvutia
vitu vya maji kujuwa
kiwango ukitakacho
kuchanganya na kichupa
kidogo cha kuchanganyia
vitu (test tube) vitu
ambavyo vinatumika hadi
sasa katika maabara yote
duniani.
Jabir Ibn Hayyan
alimtangulia Muingereza
ambaye naye alikuwa
gwiji wa somo la kemia
na John Dalton ambaye
anazungumzwa kwa
mapana na marefu na Jabir

Fatilia kuandama kwa Mwezi

Leo Ijumaa Tarehe 27


Jumada-at-Thania 1436
AH yaani mfungo Tisa,
tarehe April 17, 2015.
Tutaangalia kuandama
kwa mwezi wa Rajabu
tarehe April 19, 2015.
Tutaangalia kuandama
kwa mwezi wa Shabana
tarehe May 18, 2015.
Tutaangalia kuandama
kwa mwezi wa
Ramadhani tarehe June
17, 2015.
Kutoka leo Ijumaa
tarehe 17 April hadi kufika
Ramadhani tumebakisha
siku 61.

Mwezi utazaliwa
tarehe 16 June 2015
saa 11:05 za jioni, Juni
16 hautoonekna mwezi
popote pale Duniani na
tarehe 17 utaonekana kwa
taklifu katika maeneo ya
Kusini-Mashariki ya Asia,
Kaskazini mwa Afrika,
Australia na Indonesia
lakini utaonekana kwa
urahisi katika maeneo
ya Afrika Mashariki na
sehemu mbalimbali za
Bara la Afrika. Ramadhani
Mosi itakuwa tarehe 18
Juni, 2015.

Ibn Hayyan kwa upande


wake anazungumzwa
kwenye historia tu.
Nyingi ya kazi kazi zake
takriban akiziandika kwa
njia ya alama na ilikuwa
sio rahisi kuzifahamu
nd i p o j i na l a k e J a b i r
likafananishwa na kazi
z a k e n a k u i t wa k wa
Kizungu gibberish
Alikwenda mbali katika
kuvijua vitu na uasili wake
na hapa akavigawa vitu
kutokana na ujoto wake,
ubaridi wake, ukavu wake
pamoja na hali ya unyevu.
Akaona moto kuwa una
sifa ya moto na ukavu,
dunia na udongo ukiwa
upo katika hali ya ubaridi
na joto wakati maji yakiwa
katika hali ya ubaridi na
unyevu na hewa kuwa ina
joto na unyevu.
Jabir Ibn Hayyan
inaelezewa kuwa
aliandika vitabu 112
kwa kumtunuku Khalifa
Harun al-Rashid pamoja
na kutengeneza Jadwedi
ya Emerald. Kati ya vitabu
hivyo, vitabu 70 ambavyo
vingi yake vilitafsiriwa
katika lugha ya Latino,
moja ya kitabu hicho ni
Kitan al-Zuhra mambo
ya kupiga bao na kuagua.
Kitab al-Ahjar hichi sio
kinazungumzia juu ya
mawe ila kilikwenda mbali
sana kuyasarfi mambo ya
kiroho.
Kazi za Jabir Ibn Hayyan
z i l i z o f a n y i wa t a f s i r i
katika karne ya 20 kwa
Kiiengereza ni pamoja na
The Arabic Works of Jabir
ibn Hayyan kimetafsiriwa
na Richard Russel in 1678.
New York, E. P. Dutton
(1928); vilevile na Paris, P.
Geuther. Tafsiri nyengine
ya kazi yake ni Syed
Nomanul Haq, Names,
Natures and Things:
The Alchemists Jabir ibn
Hayyan and his Kitab alAhjar (Book of Stones),
[Boston Studies in the
Philosophy of Science p.
158] (Dordrecht: Kluwer
Academic Publishers,
1994). Kuna na kazi
nyengine iliyotafsiriwa juu
ya alchemy ikiwa: * Donald
R. Hill, 'The Literature
of Arabic Alchemy' in
Religion: Learning and
Science in the Abbasid
Period, ed. by M.J.L.
Young, J.D. Latham and
R.B. Serjeant (Cambridge
University Press, 1990)
pp. 328-341, esp. pp 333-5.
Katika kazi ya karibuni
kabisa ni hii: * William
Newman, New Light on
the Identity of Geber,
Sudhoffs Archiv, 1985,
Vol.69, pp. 76-90.

15

Makala

Uislamu, maji na mazingira


Na Ben Rijal

K AT I K A m a k a l a m b i l i
nitayazungumzia aina ya
maji yaliotajwa katika Quran
na makala ya pili itakuwa ni
Maji na Mazingira.
Quran ni kitabu cha
uwongofu kwa Waislamu
na walimwengu kimeweka
wazi suala zima la maisha na
maumbile. Imefika wataalamu
wengine wamefika kuwa na
Maabara ya kufanya utafiti
juu ya aya zilizokuwemo
k a t i k a Q u r a n ( I s l a m i c
laboratory) na kuweza
kuzifanyia chambuzi za kila
aina pamoja na kuzifanyia

kazi.
A ya z i e l e z a o j u u ya
maji ni: 47:15, 56:31, 56:68,
77:27 na 88:17 aidha aya
25:53, 27:61, 35:12, 55:19
na 55:21 zina maelezo ya
bahari zinapoungana, aya
zinazoelezea juu ya mvua
2:163, 2:265, 6:99, 7:57, 8:11,
10:24, 13:17, 14:32, 15:22,
16:65, 18:45, 20:53, 22:5,
22:63, 23:18, 24:43, 25:48,
27:60, 29:63, 30:24, 30:48,
31:10, 31:34, 32:27, 35:27,
39:21, 40:13, 41:39, 42:28,
42:33, 43:11, 45:5, 46:24, 50:9,
56:69, 57:20, 78:14, 80:25
Aya zinazoelezea juu ya
Mito ni: Surah Al-Baqara

UWANJA WA VIJANA-JIONGEZEE MAARIFA

CHEMSHA BONGO

MAJIBU
CHEMSHA BONGO NO: 1
Weka duara kwenye jawabu ilio sawa, jawabu kamili
wiki ijayo.
1. Surah ilikyokuwa refu ina aya ngapi? Baqara Aya
286
2. Surah gani imeanza bila ya tamko Bismilahi
Rahman Rahim.
3. Surah za Makka ni ..85
4. Surah za Madinah .29
5. Wakusanyaji hadithi wawili mashhuri ni: Bukhari
na Muslim,
6. M t u m e S AW a l i k u w a n a u m r i g a n i
alipoteremshiwa Wahyi na Jibril? Miaka 40
7. Mke wa mwanzo wa Bwana Mtume SAW ni Bibi
Khadija
8. Hijra ya mwanzo Waislamu walikwenda wapi?
Ethopia
9. Safari ya Mtume SAW kutoka Duniani kwenda
Mbinguni inaitwa: Miraj
10. Mtume SAW alifwatana na nani alipohama
Makka kwenda Madinah? Syd Abubakar

:25, Surah Al-Baqara: 74,


Surah Al-Baqara: 249, Surah
Al-Baqara: 266, Surah AlImran: 15, Surah Al-Imran:
136, Surah Al-Imran: 195,
Surah Al-Imran: 198, Surah
An-Nisaa: 13, Surah AnNisaa: 57, Surah An-Nisaa:
122, Surah Al-Maaida: 12,
Surah Al-Maaida: 85, Surah
Al-Maaida: 119, Surah AlAnaam: 6, Surah Al-Aaraf:
43, Surah At-Tawba: 72,
Surah At-Tawba: 89, Surah
At-Tawba: 100, . Surah Yunus:
9, Surah Ar-Raad: 3, Surah
Ar-Raad: 17, Surah ArRaad: 35, Surah Ibrahim:
23, Surah Ibrahim: 32, Surah
An-Nahl: 15, Surah An-Nahl:
31, Surah Al-Israa: 90, Surah
Al-Israa: 91, Surah Al-Kahf:
31, Surah Al-Kahf: 33, Surah
Ta Ha: 76, Surah Al-Hajj: 14,
Surah Al-Hajj: 23, Surah AlFurqan: 10, Surah An-Naml:
61, Surah Al-AAnkabut:
58, Surah Az-Zumar: 20,
Surah Az-Zukhruf: 51, Surah
Muhammad: 12, Surah
Muhammad: 15, Surah AlFath: 4, Surah Al-Fath: 5, .
Surah Al-Fath: 17, Surah AlQamar: 54, Surah Al-Hadid:
12, Surah Al-Mujadala: 22,
Surah As-Saff : 12, Surah
At-Taghabun: 9, Surah AtTalaq: 11, Surah At-Tahrim:
8, Surah Al-Buruj: 11, Surah
Al-Bayyina: 8.
Tu k i a n g a l i a k u n a
aya nyingi katika Quran
zinazoelezea juu ya maji iwe
ya bahari, mito, mvua katika
Surah mbalimbali.
Sehemu ya kiwililiwili
chetu huchukua eneo
kubwa la maji iwe mate,
damu na sehemu ambazo
zinajiunga. Asilimia 75 ya
kiwiliwili cha mwanadamu
kimetengenezwa na maji na
maji husaidia kuratibu hali
ya joto kwenye kiwiliwili
kwa kutokwa na jasho. Maji
ni sehemu muhimu sana
kwa maisha ya mwanadamu,
atapokosa mtu maji kunywa
kwa siku chache mtu huyo
atapoteza maisha.
Kilimo chetu kinategemea
maji zaidi na bila ya maji
miti itatoweka na maisha
kumalizika. Sayari yetu
hii inakalika na kuendelea
kuwa na viumbe mbalimbali
kutokana na kuwepo kwa
maji. Uislamu umezungumzia
kwa mapana suala la maji
na namna ya kuyahifadhi.
Misikiti mingi duniani
imejengwa kwenye maeneo
ambayo hupatikana kwa
maji kirahisi. Quran inaeleza
katika Suratul Anbiyaa:
Je! Hao walio kufuru
hawakuona kwamba
mbingu na ardhi zilikuwa
zimeambatana, kisha
Sisi tukazibabandua?
Na tukajaalia kwa maji
kila kilicho hai? Basi je,
hawaamini? (21:30).
Quran inatueleza kuwa
maisha yanategemea maji
na viumbe vyote vilivyohai

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Maji kwenye maporomoko


vimeumbwa kutokana na
maji. Na tukajaalia kwa
maji kila kilicho hai? Basi je,
hawaamini? (21:30).
Unapata uzingatiifu
mkubwa unaposoma aya hizi
kuona kuwa Mtume SAW
katufahamisha zadi ya miaka
1400 kupitia Quran juu ya
somo la uhai (Biology) kuwa
viumbe vyote vimeumbwa
kutokana na maji na viumbe
hao hutegemea maji kwa
maisha yao.
Katika Suratul An Naml
tunaelezwa juu ya maji
yanavyopatikana.
AU NANI yule aliye
ziumba mbingu na ardhi,
na akakuteremshieni maji
kutoka mbinguni, na kwa
hayo tukaziotesha bustani
zenye kupendeza? Nyinyi
hamna uwezo wa kuiotesha
miti yake. Je! Yupo Mungu
pamoja na Mwenyezi
Mungu? Bali hao ni watu
walio potoka. (27:60)
Hakika maji ni tunzo kwa
mwanadamu kutoka kwa
Mola wetu na tunatakiwa
tusiyachafue. Maji siku zote
hutakiwa yawe hayana rangi,
harufu na ladha iliokuwa
mbaya na hayatakiwi kuwa
na nyongeza za kemikali
katika kuyatumia kufanyia
ibada iwe kutia udhu au
kukoga janaba na nifasi.
Bahati mbaya duniani
kote hivi sasa maji ambayo
ni tunzo tuliotunikiwa na
Mola wetu yanachafuliwa
p a k u b wa n a k u p e l e k e a
m a t u m i z i m a k u b wa ya
maji ya chupa yakiwa ndio
maji yalio safi na salama.
Huko nyuma hakukuwa
na mtindo wa kunywa maji
ya chupa na haya maji ya
chupa yanachangia kwa
upande mwengine matatizo
ya mazingira hasa kwa nchi
zinazoendelea kutokana
na kushindwa kuzirejeza
(recycling) na matokeo yake
kuzagaa kila mwahali.
Mito, maziwa na bahari
z o t e z i m e c h a f u l i wa n a
uchafu, maradhi kama
ya k i c h o c h o n a t a i f o d i

yanachangiwa kutokana
na maji machafu. Maji
yaliotuwama kuyachafua ni
hatari sana kwa afya zetu,
zaidi ya miaka 1,400 Mtume
SAW amekataza kunywa
au kukoga katika maji yalio
machafu na akakataza
k we n d a h a j a n d o g o n a
kubwa karibu na vianzo
vya maji. Aidha kakataza
kutupa uchafu katika maji
yaliotuwama.
Katika Suratul Al-Arraf,
Quran inasisitiza pakubwa
juu ya uhifadhi kwa kusema
wala msifanye uharibifu
katika nchi. Hii ni uhifadhi
wa mtizamo wa Mazingira.
Na kwa watu wa Madyana
tulimtuma ndugu yao
Shua'ib. Akasema:
Enyi watu wangu!
Muabuduni Mwenyezi
Mungu. Hamna mungu
mwengine isipo kuwa Yeye.
Imekwisha kufikieni hoja
wa z i k u t o k a k wa M o l a
Mlezi wenu. Basi timizeni
sawasawa vipimo na mizani,
wala msiwapunje watu vitu
vyao, wala msifanye uharibifu
katika nchi, baada ya kuwa
imekwisha tengenea. Hivi
ndivyo bora kwenu ikiwa
nyinyi ni Waumini. (7:85)
J u u ya u f i s a d i M o l a
anatufahamisha kuwa wale
wenye kufisidi basi yeye
Mola hapendi ufisadi uwe
kwa mimea au viumbe.
Hii ndio ile dhana nzima
ya uhifadhi na maendeleo
endelevu.
Na anapo tawala hufanya
juhudi katika nchi kwa
kufisidi humo na kuteketeza
mimea na viumbe. Na
Mwenyezi Mungu hapendi
ufisadi. (2:20)
Uislamu umejengeka zadi
katika uhifadhi na Waislamu
wanatakiwa kujifunza zaidi
kuelewa mchango wao katika
kuiweka dunia katika utulivu
wa kimaumbile na utulivu
wa imani.
Makala ijayo nitaangalia
j u u ya m a j i n a d u n i a
tulionayo.

16

Makala

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Haki za Waislamu na mipaka ya Jihad


Inatoka Uk. 13

utaifanyaje Laailaha illa


Llahu itakapokujia akhera.
(Nimefupisha maneno
ya kisa halisi). Muttafaq
.(Riyadh Salihyn mlango wa
49 hadithi ya 3-5)
Fikiria wewe mwenyewe
jinsi tunavyoyachukulia
mambo kirahisi, kwa kutaka
kuwahukumu watu, lakini
M t u m e ( S AW ) h a k u wa
hivi tulivyo sisi. Akikosea
Muislamu jambo dogo,
tayari kafiri auliwe, wakati
undani wake hatuujui wala
hatutakiwi kuwahukumu
watu ila tuwachukulie kwa
dhahiri tu.
Vita vina taratibu zake na
miiko yake. Jee vita hivi vya
sasa ambavyo vinapiganwa
kwa kisingizio cha kuleta
dola za Kiislamu kweli
vinafuata taratibu za Jihadi?
Amesimulia Abdillahi
bn Umar (RA) amesema
alikutwa mwanamke
ameuawa katika vita, Mtume
(SAW) akakataza kuuliwa
wanawake na watoto.
(SM1744 SB3014).
Amesema Imam Nawawy
katika sherhe ya hadithi hii
Wamekubaliana Maulamaa
wote kuifanyia kazi hadithi
hii kwa kuharamisha kuuliwa
wanawake na watoto (wa
makafiri) ikiwa hawapigani.
(Sherhe ya Imama Nawawy

Inatoka Uk. 13
Marekani, ndio hizo hizo
w anazotumia Al-Shabaab.

Kwa maana kuwa mchezo


unaofanyika hivi sasa ni
kuwapa silaha wote wawili
wamalizane wenyewe kwa
wenyewe.
Huko nyuma tuliwahi
pia kueleza kuwa wapo
makamanda wa AMISOM
na wa Jeshi la Uganda ambao
walikamatwa kwa kuwauzia
Al-Shabaab silaha. Japo
habari hiyo inapozwa na
kufanywa kuwa ni ufisadi tu
na njaa ya askari hao, lakini
ukweli ni kuwa X anayewapa
silaha Serikali ya Somalia,
ndiye huyo huyo anayewapa
Al-Shabaab.
Huko nyuma ilikuwa AlShabaab ikipata misaada
pengine kupitia nchi ya tatu
ya Kiislamu kama labda
Qatar/Saudi Arabia. Kwa
hiyo wenyewe wanadhani
wanapata msaada kutoka
kwa rafiki Muislamu.
Lakini kwa siasa za Qatar,
Saudia Arabia na jinsi
zinavyotumiwa na mabeberu
katika suala la Palestina,
Syria, zilivyotumika kuipiga
Afghanistan, Iraq na Libya,
ni mambo ambayo tulitakiwa
tutafakari kwa kina.
Tizama leo zinavyotumika
kuwasambaratisha

ya sahihi Muslim).
Sasa wewe unaambiwa
A l S h a b a a b wa m e i n g i a
Garissa wameuwa watoto
wa shule 150, unasema hiyo
ni Jihad! Wameingia Wetgate
Shopping Mall, Nairobi,
wameuwa wanawake na
watoto, unasema hiyo ni
Jihad. Unaweza kusema kuwa
wamesingiziwa. Ukisema
hivyo, lazima ukubali kuwa
jina hilo Al-Shabaab hivi sasa
linatumika kama jinamizi
la kuupiga vita Uislamu.
Kwa hiyo wewe kushabikia
Jihad ya Al Shabaab ni kutilia
nguvu propaganda hiyo.
H a wa wa l i o k a t a z wa
kuuliwa katika Hadithi
tuliyoinukuu, ni watoto
na wanawake wa makafiri.
Jee, vita hivi vya harakati
za ukombozi hawauawi
wanawake na watoto wa
Kiislamu? Linapopigwa
bomu Somalia kuwalenga
askari wa Somalia (Waislamu)
wakiwa mitaani, litachagua
wanawake wapita njia na
watoto? Kama wanauawa,
basi harakati hizi zina kasoro
katika aqida zake na pia
zinakosa fiqhi sahihi ya jihadi
badala yake zinatawaliwa
na hamasa na katika hali hii
inaupelekea kufikiri kwamba
huenda wasioutakia mema
Uislamu wameziteka harakati

WAPIGANAJI wa Al-Shabaab wa Somalia.


hizi kwa faida yao na kwa
hivyo tuzitizame harakati
hizi kwa macho ya tahadhari
badala ya kuzikumbatia na
kuzishabikia.
Hoja kubwa inayotolewa
kuhalalisha mapambano ya
kumwaga damu ni kwamba
wasiohukumu kwa kitabu cha

Allah (SW) ni makafiri. Kwa


hivyo ni halali kupambana
nao hata ukiwaua. Katika
hoja hii nasema hivi kila aya
imetafsiriwa na Masahaba
kwa hivyo si vizuri mtu
kutafsiri apendavyo.
Nitafafanua kwa kirefu
hoja hii Inshaallah toleo lijalo

kwa kuonesha tafsiri ya aya


hii sababu ya kuteremsha na
maoni ya Maulamaa katika
hukmu ya viongozi Wislamu
wasioongoza kwa Sheria za
Kiislamu.
Wabillahi tawfiiq.
(Itaendelea toleo lijalo
Inshaallah kwa yale masuala
ambayo bado sijayajibu.

sio Waislamu na kwamba


namna ya kuwaelimesha
wakubali Dola ya Kiislamu
ni kuwaletea Al-Shabaab
kutoka Zanzibar au Tanga.
Ukisema kuwa Somalia
kuna Civil War, maana yake
ni kuwa Wasomali waliopo
serikalini si watu kutoka
Kenya au Uganda na Burundi.
Ni Wasomali. Al-Shabaab, si
Mujahidina kutoka Arusha
wala Mwanza. Ni Wasomali.
Wanapigana na kuuwana
Wa s o m a l i . S a s a k a m a
wewe utamuita mwingine
Al-Shabaab mujahidina na
mwingine umkufurishe,
bado atabaki kuwa Msomali
na bado atakuwa Muislamu.
Ni Wasomali wanauwana
wenyewe kwa wenyewe.
Ni Waislamu wanauwana
wenyewe kwa wenyewe,
kama ambavyo wanaouwana
Syria, Iraq, Libya na Yemen,
ni Waislamu kwa Waislamu.
Ni Waarabu kwa Waarabu.
Katika suala la
Mahakama ya Kadhi juzi

Bungeni, wale CCM wote


Bara Wakristo waliokuwa
na CCM Zanzibar na CC
Waislamu Bara, katika suala
la Katiba Inayopendekezwa,
waliwatema CCM wenzao
Waislamu. Wakaungana na
Wakristo NCCR, Wakristo
CUF, Wakristo CHADEMA
na wengine kupinga. Katika
suala hili walisimama kama
Wabunge Wakristo, sio CCM
au Wapinzani. Wakafanikiwa
kuzuiya mpango wa serikali
kuleta Muswada wa Sheria ya
Mahakama ya Kadhi.
Kama lipo la kuwasaidia
Wazanzibari, ni kuwasaidia
wajitambue kuwa wao ni
Wazanzibari kabla ya kuwa
CCM na CUF. Kama lipo
la kuwasaidia Wasomali,
ni kuwafanya wajitambue
kuwa wao ni Waislamu
ni Wasomali. Wajue kuwa
Mabeberu wanaoisaidia
serikali kibaraka, sio kwamba
wanawapenda Wasomali hao
waliopo serikalini. Mabeberu
hao ni maadui wa Wasomali
wote, wanaotaka Dola ya
Kiislamu na wasiotaka.
Sasa wewe ukimuona
Msomali mwenzako,
Muislamu mwenzako kuwa
ni adui yako, ni ujinga tu
ambao utazidi kumpa nguvu
adui yenu awabamize kwa
kutumia mikono yenu
wenyewe.

Jihad kuangamiza Waislam


Somalia na siasa za Zanzibar

Wayemen! Utasema Saudia,


Qatar na Misri zinapigana
Jihad, Yemen?
Kuna mambo mawili ya
kutizama katika siasa za
Somalia. Wale walioungana
wakaunda Umoja wa
Mahakama za Kiislamu, awali
walikuwa katika makundi
mbalimbali yaliyokuwa
yakipingana. Inawezekana
katika kuungana kule, kuna
waliokuwa na nia thabiti
ya kutaka Uislamu na kuna
waliokuwa na nia ya kupata
maslahi binafsi. Na ndio
maana wakakimbilia Nairobi
kuunda serikali uhamishoni
baada ya kuona watapata
n g u v u ya M a r e k a n i n a
wababe wengine.
Ukiitizama Somalia ilivyo,
Al-Shabaab walioshika silaha
ni sehemu ndogo sana ya
wananchi. Wapo Waislamu
wengi ambao hawakubaliani
na sera za Al-Shabaab walio
katika makundi ya Twarika
mbalimbali. Na hawa
ndio wenye watu wengi

zaidi. Ni kama unavyoona


l e o h a p a k w e t u . Wa t u
wataona katika TV watu
sehemu mbalimbali duniani
wanaswali, lakini watasubiri
s wa l a wa l i y o t a n g a z i wa
na Sheikh Alhad au Mufti
wa Bakwata. Sasa ukisema
kuwa namna ya kuwafanya
hawa wafuate Kitabu na
Sunna, na waswali unayoita
wewe Idd ya Kimataifa, ni
kuwashikia AK-47, utauwa
Waislamu wangapi mpaka
hilo litimie? Lazima ukubali
kuwa hapo kuna tatizo la
ujinga wa muda mrefu na
ukosefu wa elimu. Na ujinga
hauondolewi kwa mtutu wa
bunduki, wala mabadiliko
ya kijamii na kiimani hayaji
kwa kufumba na kufumbua
kwamba unashika silaha
ghafla Jihad imewafanya
Waislamu safi wa kuhukumu
kwa Kitabu na Sunnah.
Huwezi kuwaita wale
wazee na vijana wa Kisomali
walio katika twarika za Ahlu
Sunna Wal Jamaa, kuwa

17

MAKALA

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Saudia soko muhimu la silaha za Marekani

Inatoka Uk. 9

wa m a j e s h i ya n c h i z a
Kiarabu, unaoongozwa na
Saudi Arabia.
Wakazi wa kijiji hicho cha
Okash, kilicho karibu na
kambi ya jeshi la anga ya
Jabal Shouaib, walinukuliwa
wakisema familia iliyouawa
ilikuwa na wanaume wawili,
m wa n a m k e m m o j a , n a
watoto sita. Shirika la habari
la Yemen la Sabaa, limetuma
picha za familia hiyo kwenye
mtandao wake. Bila shaka
hao wote na wengine
wa n a o e n d e l a k u p o t e z a
maisha ni Waislamu. Kisa ni
tofauti tu ya kimadhehebu,
tena inayochochewa na
makafir kwa maslahi yao.
Kwa ujumla tunachoweza
kusema ni kwamba
kinachodhidiri hivi sasa
katika mzozo wa Yemen
hata Syria na Iraq, ni
matumizi mazuri ya
mkakati wa kufarakanisha
ndugu na anayefarakanisha
akizidi kuweka mazingira
ya kuneemeka kiuchumi
huku waliofarakanishwa
wakijiangamiza wenyewe.
Faraka ya Ushia na
Usunni iliyopenyenyezwa
inawatafuna Waarabu na
Waislamu kwa ujumla. Saudi
Arabia inaongoza Kundi
la mataifa yenye Waislamu
Na Juma Kilaghai

HAINA mashaka
yoyote kuwa vyakula na
vinywaji vinavyotokana
na nafaka vinanoga!
Au unasemaje kuhusu
wali mweupe, pilau,
biriani? Na bado
hapo hujagusia chips,
chapati, kitumbua,
andazi, na bajia! Mhh
kule kuna soda, juisi,
ice cream, pipi n.k. We
wacha tu!
Mpaka siku mbili tatu
zilizopita sikuwa na
shaka yoyote ile kuhusu
ubaya wa kubugia kwa
w i n g i v ya k u l a v ya
nafaka. Tukumbuke
kwamba sukari, - yule
adui namba moja wa
afya, chimbuko lake
ni nafaka! Nilijua, na
naamini wengi wetu
tunajua, kuwa sukari ni
miongoni mwa vyakula
vikuu vinavyosababisha
mfuro (inflammation) na
kwamba mfuro ni moja
ya vyanzo vikuu vya
maradhi ya kimfumo
ndani ya mwili.
Nilijua kuwa
chimbuko la nafaka
kusababisha mfuro ni

Saudi Arabia, taifa hili


lina Waislamu wengi wa
dhehebu ya Shia, tofauti
na Saudi Arabia ambayo
i n a Wa i s l a m u w e n g i
wa dhehebu la Sunni.
Umekuwa ni msimamo
wa Saudi Arabia pale,
ilipoahidi kuwa itaendelea
kufanya mashambulizi
makali dhidi ya raia wa
Yemen mpaka wasalimu
amri na kumkubali
Rais Hadi, ambaye
raia hao hawamtaki na
ameshakimbia nchi.

L a k i n i k wa S a u d i a
kuendelea kuua Waislamu
wa Yemen kwa kutumia
hazina yake ya silaha
kutoka Marekani,
ni wazi kwamba ni
kicheko kwa Marekani
ambayo itajihakikishia
kuongezewa kandarasi
ya kuuza silaha zaidi kwa
Taifa hilo. Hii ni kutokana
na ukweli kwamba tayari
kuna mahali pa kuzitumia
silaha hizo hivyo
mahitaji yake yatazidi
kuongoezeka.
Katika mashambulizi
haya Saudi Arabia
inaungwa mkono na Israel
na Marekani. Bila shaka
ile falsafa ya Marekani
ya wagawe, watawale
ufaidikie kiuchukumi,
imechukua nafasi
yake. Kwa kuwa silaha
zilizokuwa zimerundikwa
kwa muda mrefu sasa
zimepata matumizi, bila
shaka watumiaji watumia
fursa iliyojitokeza kuagiza
zaidi ili hazina isipungue.
Na ni wakati huo ambapo
soko la silaha za Marekani
linapanuka zaidi.
Kwa mtindo huu kwanini
Waarabu, ambao ni ndugu
wa Kiislamu wasiendelee
kufarakanishwa hadi pale
watakapotahayari?

hupunguza kwa kiasi


k i k u b wa u we z o wa
mitochondria (viwanda
vya kuzalisha nishati
vilivyomo ndani ya
seli) kudhibiti chembe
chembe zilizobeba
umeme hasi (high
energy electrons)
zinazotumika wakati
wa uzalishaji wa nishati
inayotwa Adenosine
Tri-phosphate (ATP),
ambayo ni kwa ajili ya
matumizi ya baadaye
mwilini. Hizi high
energy electrons
husababisha kuzaliwa
kwa kiwango kikubwa
cha chembe zilizobeba
umeme chanya
zinazoitwa free radicals.
Chembe hizi zina uwezo
wa kubadilisha umbo
na utendaji kazi wa
vinasaba kwenye seli
(DNA mutations) na
kuharibu vimengenya
mbalimbali ndani ya
mwili!
Tafiti zimebaini kuwa

baadhi yetu miili yetu


huchakata wanga bila
madhara ukilinganisha
na wengine. Watu wa
aina hii husemekana
wana mifumo ya
ujenzi na uvunjifu
wa kemikali ambayo
inaendana na vyakula
vya wanga/nafaka au
C A R B O H Y D R AT E
TYPE kwa kitaalamu.
Njia pekee ya kujua
kama wewe ni miongoni
mwa waliomo katika
kundi hili au siyo ni
kwa njia ya kipimo cha
kutambua mfumo wako
wa ujenzi na uvunjifu
wa kemikali mwilini
(metabolic typing test).
Huko nyuma tuliwahi
kukiweka kipimo hiki
katika ukurasa wetu wa
FB na kuwakaribisha
wadau wajisaidie nacho.
Hivi sasa kipimo hiki
kiko katika mfumo wa
kijitabu na unaweza
kukipata katika ofisi
za Herbal Impact
zilizoko mtaa wa
Mosque, Kitumbini,
Dar es Salaam.
(Kwa maelezo zaidi
0754281131/0715281131)

MSURURU wa vifaru vya jeshi la Saudi Arabia.


wengi wa Sunni katika
eneo hilo la Mashariki ya
Kati katika mapambano
na makundi ya Waislamu
wa madhehebu ya Shia
yanayosaka mabadiliko ya
kiutawala katika nchi zao au
kupinga himaya ya Kisuni
katika nchi zao.
Hilo limesababisha kile
kinachoonekana kuwa ni
vita vya kimadhehebu. Hivi
sasa tunashuhudia raia wa
Yemen ambao wengi ni
Shia, wakiunda kikundi cha
wanamgambo wa Huthi,

ambao ni wapiganaji wa
Kiislamu wa dhehebu la
Shia, kuukabili utawala wa
Rais Hadi, ambaye wananchi
hao hawamtaki walkiamini
kuwa ni kibaraka wa Saudi
Arabia (Sunni) na mataifa
ya magharibi yanayounga
mkono Sunni. Hivi sasa Rais
Had, yupo mafichoni Saudia
akipata hifadhi ya nchi hiyo.
Nayo Saudia inapambana
kumrejesha swahiba wao,
ambaye anasimamia maslahi
ya o . Ye m e n n i t a i f a l a
Kiarabu lililopo jirani na

Tunajimaliza wenyewe kwa ulaji huu


sukari aina ya fructose
ambayo au tayari ipo,
au inakuwa ni moja ya
mazao wakati nafaka
inapochakatwa ndani
ya miili yetu. Watafiti
wanasema kuwa
Fructose huchochea seli
za mwili kuchoma nishati
(ATP) iliyohifadhiwa
h u m o k wa k a s i ya
kutisha na matokeo yake
seli husika hukumbwa
na 'shock'! Shock hii
hupelekea vinasaba
(DNA) katika hizi seli
kusambaratika! Watafiti
hawa wanaongeza kuwa
DNA iliyosambaratika
hujiunda katika kemikali
zinazojulikana kama
purines, ambazo nazo
huishia kujiunda kuwa
tindilkali ya urea, yaani
uric acid! Tindikali ya
urea husababisha seli
za mwili kukumbwa na
mfuro, huharibu mifupa
laini inayounganisha
v i u n g o v ya m w i l i ,
husababisha mishipa
ya damu kukumbwa

na mkakamo (haikubali
kupanuka wala
k u s i n ya a ) , k i t e n d o
ambacho huleta maradhi
ya mfumo wa mzunguko
wa damu, nakadhalika.
Kwa
upande
mwingine nilijua kuwa
glucose (sukari ingine
i n a y o p a t i k a n a k wa
wingi kwenye nafaka
na sukari ya mezani)
inaweza kuleta shida
kwenye ini, inaweza
ikasababisha unene
uliopea, inaweza
kuchochea kisukari cha
ukubwani, na pia kuwa
ni chakula kikuu cha
seli za saratani. Kitu
ambacho sikukijua ni
kwamba glucose pia ni
chanzo kikubwa sana
cha mfuro ndani ya
mwili!
Kwa mujibu wa tafiti,
Uchakataji wa glucose
huzalisha kemikali
i n a y o i t wa m a l o n yl coA. Malonyl-coA

18
Na Juma A. Simba

UNA
baadhi
ya
misemo
ya Kiswahili
unapoisikia ikisemwa
au unapoisoma, kuna
wakati unaweza maneno
yake ukayapita tu na
wala usiuone umuhimu
au tafsri ya msemo huo
mpaka likupatapo. Kwa
mfano kuna msemo
usemao Majuto ni
mjukuu, Msiba wa
kujitakia huambiwi pole.
Usipo sikiza la mkuu
huvunjika guu, na
kadhalika.
Katika misemo hii
ambayo nilo iaynisha
nataka niutumie huu
Msiba wa kujitakia
huambiwi
pole
kuhusiana na kadhia hii ya
kura ya maoni ya katiba,
ambapo Mheshimiwa
Spika Ameir Kificho
pale alipotumia mamlaka
yake ya kumkubali
M wa n a s h e r i a M k u u
mteule Said Hassan Said
alipowasilisha sheria ya
kura ya maoni barazani
kwa njia ya maandiko.
Mheshimiwa Spika
Kificho alitumia mamlaka
yake hayo kwa kukataa
upande wa upinzani
pale ulipowasilisha hoja
ya k wa m b a B a r a z a
la Wakilishi haliwezi
kutumika kuridhia sheria
ambayo jambo lenyewe
si la muungano kati ya
Zanzibar na Tanganyika,
kufanya hivyo ni kinyume
kabisa kwa mujibu wa
katiba ya Zanzibar na
hili Mheshimwa Kificho
alikuwa analijuwa fika.
Lakini afanyeje, na tayari
Mheshimiwa Kificho maji
alikuwa ameshayavuliya
nguo. Tayari alikuwa
a m e s h a ya v u l i a n g u o
tokea pale alipokuwa
Dodoma. Hivyo
asingeweza tena kuwa
kama ngombe kuutowa
ulimi wake kwenye
mdomo kuupeleka puani
na baadaye kuurejesha
mdomoni, kwa sababu hii
siyo tabia ya muungwana
na uungwana hasa wa
Kizanzibari. .
Kukubalika kupigiwa
kura ya maoni kwa katiba
hii kwa wajumbe wa
Baraza la Wakilishi
upande wa chama tawala
kulitarajiwa na wengi;
k u l i t a r a j i wa n a h a t a
wasio kuwa wanachama
wa chama tawala kwa
sababu ishara za matokeo

Makala

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Msiba wa kujitaki

SPIKA wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Pandu Kificho akiingia bungeni


mjini Dodoma kuliendesha bunge hilo.
haya yalianzia Dodoma
kibali kitoke Dodoma.
Tanganyika kupiga kura
ambako kwa wakati
Mfano isadifu kuwepo
kama Wanzibari mradi tu
huu maamuzi yote ya
hayo mafuta Zanzibar
katiba ipite. Utaratibu huu
au madini mengine ye
mpya wa kura ya maoni
Zanzibar kupitia chama
yote yale yenye thamani,
ni kuhakikisha tu katiba
tawala ndiko yanako
basi suala la uchimbaji
hii ima fa ima, vyo vyote
a m u l i wa wa k i b a k i a
wa madini hayo mpaka
viwavyo, lazima
viongozi wa chama tawala
ruhusa
itoke
Dodoma,.
Wazanzibari waikubali.
Zanzibar, kushangiria
ambapo masuala kama
L a k i n i m t u a n a we z a
kwa kupiga makofi,
haya na mengineo
kujiuliza, jee kura hizi
wingi wa vigelegele,
chama cha upinzani
za Wazanzibari walioko
shangwe na nderemo kwa
CUF katika kupigania
Tanganyika tunaweza
vibakwizo, Mapinduzi
kwake mamalaka kamili
kusadikishaje kwamba
Daima huku baadhi yao
ndio inayoyataka yasiwe
idadi ya kura zitazopigwa
ati wakiomba wapewe
Abadan kuamuliwa
ili kuchanganywa na za
kwake ni kwa kuomba
pole.Katika hili la kujitakia
hapa Zanzibar wapiga
ruhusa kutoka serikali
msiba wenyewe Chama
kura wake kweli ni
ya M u u n g a n o , b a l i
cha Mapinduzi hivi sasa,
Wazanzibar? Jee kuna
yaamuliwe Mbweni.
viongozi wake wanapita
takwimu yeyote ya
Kwa sababu Chama cha
kila pahala, mbali na
mwaka wo wote inyo
Mapinduzi kinajuwa fika
karibu Unguja na Pemba
onyesha Tanganyika kuna
kwamba juu kampeni
kuipigia debe katiba hii
Wazanzibari Wangapi?
zake zote kwa hapa
kupigiwa kura ya NDIO.
Wanzibari wengi hakika
Zanzibar hakikuweza
Katika kampeni yake
wamekuwa wakijiuliza
kufanikiwa kuwashawishi
inajaribu kuipamba
wenzetu ambao wana
Wa z a n z i b a r
walio
katiba hii iwezavyo na
lazimisha kwa nguvu zote
wengi juu ya kuikubalai
kuvifafanuwa baadhi ya
katiba hii lazima ipite
katiba ya serikali mbili,
vifungu kwa ukengeza wa
ni kwa uzuri gani hasa
pia kushindwa kupata
kuonesha uzuri wa katiba
uliomo ndani ya katiba
asilimia mbili ya tatu hata
hii ilivyo nzuri, lakini cha
hii? Jee wanachokiona
Dodoma kwenyewe, pia
kuvunda hakifukiliziki
kweli ni uzuri tu uliojaa
haijajipa matumaini
kwa udi wachilia mbali
katiba hii, hamna ubaya
kwamba hata kwenye
ubani. Miongoni mwa
na baadye kuupima
v i s a n d u k u v ya k u r a
sifa zipambazwo ambazo
uzuri na ubaya? Jee pale
itaweza kufanikiwa kwa
hazipambiki ni pamoja
mnapopaza sauti zenu
hapa Zanzibar.
na Rais wa Zanzibar
juu kusifu Mapinduzi
Hivyo kwa kutumia
kuwa Makamo wa Rais
Daima, mnakusudia
wa Muungano ambapo
sect: 34 sheria ya kura
mapinduzi gani hasa, ya
kiukweli atabakia kuwa
ya maoni Chama cha
kuomba ruhusa kutoka
tu na jina la Makamo
Tanganyika kutuchagulia
Mapinduzi kimeona ili
wa Rais lakini hata zidi.
hata rais wa Zanzibar
kiweze kushinda katika
Kwani hata itokeapo Rais
awe nani? Kwa sababu
hili la kupiga kura ya
wa Muungano atakapo
wanao ikataa katiba hii
maoni ni kuhalalisha
kuwa hayupo nchini
ni kwamba wanataka
kupiga kura kwa
hatokuwa na mamlaka ya
masuala ya Zanzibar
kutumiwa vitambulisho
kukaimu; hatokuwa na
wajiamulie wenyewena
vya Mtazania, kwa
mamlaka ya hata Zanzibar
yale
Muungano
kuwaorodhesha
anayoiongoza kuiamuilia
tuamuwe kwa pamoja
Wa t a n g a n y i k a w o t e
kujiunga na tasisi ya
ili kuondowa ule mfumo
waliopo Zanzibar kupiga
hapo Kenya wachilia
mithili y ukuloni mambo
kura kama ni Wazanzibari
mbali nchi za nje. Ruhusa
leo. Haya sio kabisa
na sio tena Watanganyika,
ya kufanya hivyo mpaka
yaliyo kuwa madhumuni
na Wazanzibari walioko

ya
Mapinduzi.
Hatukupinduwa kwa
sababu tu ya kutawaliwa
na watawala wa kigeni
au rangi, ili kukarabisha
utawala wa Waafrika
wenzetu ati tu kwa
sababu wao ni weusi.
Katiba hii ambayo hivi
sasa imeshikiwa bango
kupigiwa kura tarehe 30
Aprili, ilivyotengenezwa
ni kutunyanganya kabisa
umiliki wetu mamlaka
yetu, mwishowe Zanzibar
yetu. Hii ni katiba
ambayo lengo lake hasa
ni kututowa kikaangoni
kututumbukiza katika
moto.
Mwezi wa Aprili huu
tunao uanza umetengwa
kwa ajili ya kampeni rasmi
ingawa rasha rasha za
kampeni tayari tumesha
zishuhudia. Inawezekana
katika mwezi wa Aprili
katika kampeni wananchi
wakatiwa khofu na vitisho
ikiwa ni njia moja ya aina
ya kampeni, lakini aina
yeyote ya vitisho tusifike
pahala kujitafutiya msiba
w e n y e w e . Wa n a n c h i
wanapo piga kura
kuwachaguwa viongozi
wao, huwataka walio
wachaguwa wawe
ni wat u waaminifu,
waadilifu, wakweli, na
wawe wanayawakilisha
yale matakwa ya
wananchi wale walio
wengi, hasa inapo jitokeza
kuwa kinacho wakilishwa
kina faida na manufaa
kwa jamii yote. Uhuru
wa mwanadamu yeyote
yule una bora hata
ukaandamana na shida na
madhila. Hakuna utumwa
uungwanawala mzuri.
Wazanzibar ni watu
tulio zaliwa huru kama
wa l i v y o Ta n g a n y i k a ,
Muungano usiwe chanzo
cha kuujutia. Katiba hii
ambayo chama tawala
mnaipigia debe ya serikali
mbili haitotufaidisha,
tusiwasihi Wazanzibari
Wachilia mbali kutaka
kuwalazimisha kuipigia
kura. Muelewe fika wale
ambao maamuzi yenu
yatabakia kungangania
kuipigia kura katiba
hii ya serikalimbili, ipo
s i k u m a a m uz i ye nu
ya t a t u g h a r i m u s o t e ,
ikitokea sio sisi watoto
wetu au vijukuu vyetu,
hivyo tujiepusheni na
msiba huu wa kujitakia
kwa sababu hakutokuja
kuwepo wa kutupa pole.

19

Makala ya Mtangazaji

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Abbas: Israeli Prolonged Policy of Misleading, Deluding Fools Nobody


MOSCOW, (WAFA)
President Mahmoud
Abbas Tuesday slammed
Israels longstanding
policy of deception,
saying that it would no
longer fool anybody.
Speaking at the Peoples
Friendship University of
Russia, which conferred
upon him honorary
doctorate degree, Abbas
stated that the world is
still witnessing Israels
aggression and racism
against the Palestinian
people and that Israel
is still acting as a rogue;
placing itself above
international law and
continuing its occupation
of Palestinian territories.
He added that Israel

is still maintaining its


long-standing policy of
conducting a meaningless
vicious circle of
negotiations in an effort
to shirk the prerequisites
of just and comprehensive
peace, gain time and
impose a fait accompli
to make it impossible
to establish the future
Palestinian state.
We aspire to witness
peace reigning in the
region, so that all future
generations in our
homeland as well as
neighboring countries,
including Israel, enjoy its
fruits; a regional peace
under which all live in
security, safety, stability
and good-neighborliness,

NABLUS (Ma'an) -Israeli forces detained 31


Palestinians across Nablus
overnight including 20
Hamas affiliates and several
former prisoners.
Palestinian security sources
told Ma'an that more than
50 Israeli military vehicles
raided Nablus around 2:00
a.m. Wednesday without
informing the Palestinian
Authority until already
having entered the city.
Local sources added that
Israeli forces raided the
Balata refugee camp, alNamsawi area, the Asira
Street, the Old City and
other neighborhoods across
the city.
Witnesses also told Ma'an
that dozens of Israeli soldiers
raided the home of Abdullah
al-Aker, 32, searching the
house for three hours and
confiscating 40 thousand
shekels ($10,078), computers
and mobiles.
The following were
identified among those
d e t a i n e d We d n e s d a y :
Said Dweikat, Nidal Abu
Rmeileh, Wajih Abu Eida,
Abdullah al-Aker, Hussam
al-Bustami, journalist Amin
Abu Wardeh, Omar Abd alWahhab, Amjad Abu Ghosh,
Muhammad Sawalmeh,
Zahi Abu Eida, Samih
Eleiwi, Youssef Marshud,
Abu Hamzeh al-Jurf, Ziad
Mreish, Amjad Zamel, Sami
al-Assi, Anan Futouh, Saad
Khudrieh, Mona Abu Bakr
al-Sayeh, Ahmad Sawalha,
Omar Abd al-Wahhab,
Omar Issa Atallah, Abu
Hamzeh al-Jurf, Ghassan

Abu al-Baraa, Fares and


Ghanem Sawalmeh, Sheikh
Bassem Abu Juneid and
Jasser Abu Hamada.
Most of the detainees are
former prisoners.
The reported lack of
communication by Israeli
forces to Palestinian security
p r i o r t o We d n e s d a y ' s
raid marks a violation of
internationally recognized
policy regarding Palestinian
autonomy in the occupied
West Bank.
Israeli entrance into Area
A -- the approximately 20
percent of the West Bank
technically under full
Palestinian control as a result
of the Oslo Accords -- must
be taken in only coordination
with the PA.
Incidents of illegal Israeli
incursion occur on a routine
basis, with Israeli forces
carrying out an average of
75 raids a week on occupied
We s t B a n k Pa l e s t i n i a n
neighborhoods and villages
according to Hebrew and
English news site Haaretz.
Israeli security forces have
detained over 40 Palestinians
in the last week across the
occupied West Bank and
East Jerusalem for "illegal
activity."
The majority of Palestinian
political organizations are
considered illegal by Israel,
including those that make up
the PLO, and affiliation with
such parties is often used as
grounds for imprisonment,
according to Prisoner
Support and Human Rights
Association Addameer.

Israeli forces detain 31


across Nablus in mass raid

stated Abbas.
Abbas made these
remarks during his latest
official visit to Russia,
during which Russias
leader Vladimir Putin met
with him on Monday in his
Novo-Ogaryovo residence
outside Moscow.
The current state of
Israeli-Palestine relations
as well as armed conflicts
in the Middle East was at
the top of the talks agenda.
Now as the situation
grows more difficult in
the region, of course, it
is very important to hold
consultations on the full
range of issues. I mean
of course, primarily the
Israeli-Palestinian issue
but not only that, I would

like to discuss with you


the situation in Syria, Iraq
and now in Yemen, said
Putin addressing Abbas
at the start of the meeting.
Putin said, 'Its a
pleasure to note that
relations between
Palestine and Russia have
been growing steadily and
are constantly, step-bystep, becoming stronger.
He added, 'And now,
when the situation in the
region has become more
complicated, of course, it
is particularly important
to consult with you on all
the issues at hand.'
Abbas stated, 'I want
to note that we highly
appreciate the cooperation
with your country and the

efforts of Russia to solve


the Palestinian problem
with regaining of the
peace in our lands.'
He added, 'There
are many problems in
our region with which
Russia has to work
with and I must admit
that Russia's efforts are
successful.'
The two presidents
also held talks over
trade and the economic
situation between both
countries, with Putin
stating 'I am glad to
note that relations
between Palestine and
Russia were developing
and strengthening
constantly.'

Gaza Man Dies of Wounds Sustained


during Israeli Aggression
G A Z A , ( WA FA) A
Palestinian youth Tuesday
succumbed to wounds he
sustained during the 2014
Israeli summer aggression
on the Gaza Strip, whereas
another was slightly injured
in a building collapse,
according to medical
sources.
WAFA correspondent
reported that Eliwa Nidal
Eliwa, 22, was critically
injured during the summer
aggression on the strip,
yet his medical condition
did not improve. He was
pronounced dead Tuesday
after succumbing to his
wounds.
During the summer Israeli
aggression on Gaza last July
and August, more than 2,190
Palestinians were killed and
more than 10,000 others
injured by Israels deadly

airstrikes and artillery


attacks.
The Palestinian Authority
became a member at the
ICC on the 1st of April to
investigate crimes allegedly
committed during the Israeli
aggression on the Gaza
Strip during the summer
of 2014, a step pursued by
President Mahmoud Abbas
following the United Nations
failure to approve a draft
resolution calling for the
end of occupation and
establishment of a Palestinian
state within three years.
Meanwhile, a Palestinian
resident was walking past a
five-storey building, which
was severally damaged
during the summer
aggression, in Dir al-Balah
area in central Gaza, when
it collapsed to the ground,
leaving him with light
injuries.

During the Israeli summer


aggression on the Strip,
thousands of homes were
d e s t r o ye d a n d a r o u n d
170,000 Palestinians were
consequently left homeless.
Gaza still suffers from
the repercussions of the
Israeli aggression which
took place in the summer of
2014; the infrastructure along
with thousands of homes
were completely destroyed,
displacing thousands of
families who up until the
moment live in caravans on
the rubble of their homes.
Meanwhile, the UN
News Center stated that,
United Nations agencies
and offices were alarmed
over the limited progress in
rebuilding the lives of those
affected by last summer's
fighting between Israeli
forces and Palestinian armed
groups in the Gaza Strip.

AN-NUUR

20

MAKALA

20

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

AN-NUUR

JAMAADIUL AKHER 1436, IJUMAA APRILI 17-23, 2015

Safari ya Hijja Hijiria 1436

Tanzania Muslim Hajj Trust, uandikishaji unaendelea,


gharama za Hijja ni US Dollar 4400, tarehe za Safari ni:
11 na 13 Septemba, kurudi 7 Oktoba, 2015.
Wahi kujiandikisha sasa
Kwa mawasiliano: +255 222 182370
+255 222181577
0754 261910; 0717 000065
0786 383820
0784 272723
0713 764636
website-www.hajjtrust.or.tz

Akina mama wa Kiislamu wamtembelea Sheikh Ponda


Na Azza Ally Ahmed

Baadhi ya viongozi
wa Baraza la Wanawake
wa Kiislamu Tanzania
wamemtembelea Sheikh
Ponda Issa Ponda katika
gereza la Morogoro
m w i s h o n i m wa w i k i
iliyopita.
Viongozi hao
wamefanya ziara gerezani
hapo na kuonana na Sheikh
huyo anaeshikiliwa
gerezani hapo.
Viongozi
hao
waliowawakilisha
kinamama wenzao
wakiongozwa na Ukhti
Mayasa Sadallah ambaye
ni Naibu Katibu Mkuu wa
Baraza la wanawake wa
Kiislamu Tanzania akiwa
amefuatana na Amira
wa Baraza hilo Wilaya
ya Ilala, Ukht Hindu
Abdallah.
Akiongea na mwandishi
wa habari hizi Ukhti
Mayasa baada ya ziara
hiyo anasema anashukuru
sana kwa mapokezi na
ukarimu kutoka kwa

viongozi wa gereza hilo.


Tulipofika tulikuta
tayari kuna watu
wameshakuja kumuona
Sheikh hivyo zimebaki
nafasi za watu wawili
ambao ndio wanaoleta
chakula baada ya kujieleza
kuwa tumekuja kumuona
Sheikh PONDA na
tunatokea Dar es Salaam,
askari alituandika majina
na kusema nyie ingieni
na hao pia wanaotakiwa
kuleta chakula wataingia
hamna shida kwa kweli
tulisikia faraja sana.
Alisema Mayasa.
Alichousia na kusisitiza
Sheikh ni kuwa Waislamu
kudumisha mshikamano
pamoja na kuendeleza
Dini ya Allah bila kuchoka
kufanya daawa.
A l i o n g e z a M a ya s a
akisema huo ulikuwa
ndio ujumbe na nasaha
za Sheikh Ponda kwa
Waislamu.
Akielezea ukht Mayasa
kuhusu afya ya Sheikh
anasema anaonekana ni
mwenye afya njema hana
tatizo lolote.

MSAADA WA KULIPIWA ADA

Mimi ni Binti wa Kiislamu HAMIDA


RASHIDI. Pia ni yatima, ambaye ninasoma
Chuo cha Ualimu Ununio (Ununio Teachers
College) mwaka wa pili.
Nimesimamishwa masomo kwa kutolipa
ada na kushindwa kuendelea na masomo.
Mpaka sasa nipo nyumbani. Mlezi aliyekuwa
ananilipia ada ameshindwa kufanya hivyo
kutokana na hali yake kuwa mbaya kiuchumi.
Naomba kila atakae guswa na habari
hii anisaidie kwa kile atakacho jaaliwa na
Muumba wake kwani kutoa ni moyo. Toa
kile alicho kuruzuku Allah (S.w) hakika
hutopoteza utayakuta malipo yako mbele ya
muumba wako.
Kiasi cha ada ambayo nadaiwa ni Shilingi
laki Nane (800,000). Unaweza ukatuma kwa
namba ya mlezi wangu Yassin M. Mwagamile
0783 723312 au unaweza wasiliana na uongozi
wa chuo 0715 822332, 0687 505 292 au unaweza
lipia Benki ya KCB Account Namba 3300627761
kwa jina la Ununio Teachers' College kwa jina
la Mwanachuo HAMIDA RASHIDI. Ukituma
kwa akaunti ya chuo ni vyema ukatujulisha
kwa namba ya mlezi wangu.

CHEMSHA BONGO NO:2

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa, jawabu kamili wiki ijayo.



1. Sura za Makiya ni
2. Sura Madaniya ni ..
3. Anaitwa nani aliotafsiri Tafsiri ya Quran kwa jina la al-Tabari katika mwaka
wa 310 AH?
4. Mtume SAW alipewa Utume akiwa na umri wa miaka mingapi?
5. Ujumbe, Wahyi wa mwanzo aliteremshiwa Mtume SAW akiwa yupo wapi?
6. Vita vya pili Waislamu walivyopigana baada vya Badr vinaitwaje?
7. Mtume SAW alikufa akiwa na umri gani?
8. Taja jina la Mtume alioishi wakati mmoja na Mtume Mussa
9. Wataje watoto wawili wa Mtume Ibrahim na ..
10. Bibi Aisha alikufa akiwa na umri wa miaka mingapi?
Unajua

Kuwa Quran ndio kitabu kinachosomwa zaidi kila siku duniani?

Kuwa majina mengine ya Quran ni Al-Furqaan, Al-Kitaab, Al-Zikr, Al-Noor,
Al-Huda.

Mtume Mussa ametajwa katika Quran mara 136 katika Sura mbalimbali?

Quran ina Surah 114.

Suratul Naml ni Sura pekee Bismilalhi imetajwa mara 2.

Mtume amepokea wahyi kwa kipindi cha miaka 13 na kati ya hayo miaka
10 peke yake amepokea wahyi akiwa Madinah.

Kuwa jina la Bibi Maryam ni jina la mwanamke lilotajwa kwa jina.

Kuwa Quran ni kitabu pekee kilichohifadhiwa kwa ghibu na watu wengi
duniani hakuna kitabu chochote ambacho watu wamekihifadhi kwa ghibu zaidi ya
Quran.

Kuwa mwanadamu huvuta pumzi kwa kutumia gesi ya Oxygen na kutoa
Carbon dioxide wakati miti huvuta pumzi kwa kutumia gesi ya Carbon dioxide
na kutoa Oxygen.

Kuwa jangwa la Sahara ni kubwa kuliko yote duniani.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

También podría gustarte