Documentos de Académico
Documentos de Profesional
Documentos de Cultura
tz
Sauti ya Waislamu
SHURA YA MAIMAM (T) Inawatangazia Waumini wote kuwa kutakuwa na Ibada ya Itkaaf. Mahali: Masjid Mtambani, Kinondoni Siku: Jumamosi, Desemba 28, 2013 Muda: Saa tatu (3:00) usiku. Baada ya Sala ya Ishaai.
ISSN 0856 - 3861 Na. 1105 SAFAR 1435, IJUMAA , DESEMBA 27, , 2013 - JAN. 2, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Inshaa Allah, usikose Ibada hii adhwiim. Kny: Amir wa Shura ya Maimam.
MOJA ya nyumba iliyoteketezwa kwa moto kijiji cha Lwange, Kilindi Tanga.
2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
AN-NUUR
waliovamia nyumbani kwake. Bw. Musa Masanja wa Sakasaka Wilaya ya Meatu, alidai kuporwa shilingi 300,000 pamoja na simu mbili za mkononi na askari wa Operesheni. Katika Wilaya ya Itilima,Kijiji cha Mbogo Bw. Sita Rumala alidai kupigwa na kuvunjwa mkono. Alionesha wajumbe wa Kamatu mkono uliokuwa umefungwa bandeji ngumu (P.O.P). Bw. Munanka Machumbe (24) ambaye ni bubu alipigwa risasi tatu zilizomjeruhi mapajani na kuharibu sehemu za siri wakati akijaribu kuwahoji Askari wa Operesheni kwa ishara sababu za kumtesa baba yake. Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ali Mohamed (70) wa kijiji cha Iputi, alidai kurushwa kichura na kutandikwa bakora na Askari wa Operesheni Tokomeza. Hayo ni baadhi tu ya matendo maovu yaliyobainishwa na Kamati ya Bunge, yaliyofanywa na wale waliopewa dhamana ya kutekeleza operesheni hiyo. Bila shaka matendo mengi machafu ya namna hii yamefanywa katika maeneo mengine ya nchi, ambako Kamati ya Bunge haikuweza kufika na
AN-NUUR
JUMUIA ya Wanataaluma wa Kiislamu (TAMPRO) wametakiwa kujivunia Uislamu wao na kufanya kazi kwa bidii. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natti, katika mkutano wa mwaka wa jumuia hiyo uliofanyika juzi katika hoteli ya Lamada, Ilala Jijini Dar es Salaam. Mkurugunzi huyo amewataka Viongozi wa Jumuia kuwahamasisha zaidi Waislamu kujiunga kwa wingi na jumuiya hiyo, ili kujenga mshikamano na umoja wa wataalamu hao. Aidha Mkurugenzi huyo amewataka Waislamu kuacha kulalamika na kuwataka kuwa watendaji zaidi, ili kuweza kufikia malengo yao na kuikoa jamii na wimbi kubwa la umasikini. Aidha alisema kuwa matajiri wengi nchini ni Waislamu na iwapo wakitumia utajiri wao katika kuusaidia Uislamu, uislamu na jamii nzima kwa ujumla itafika mbali. Amewataka wasomi wa Kiislamu kujitambua na kujivunia kuwa Waislamu mahapa popote watakapokuwa na waitumie bahati hiyo kutenda yalio mema na kufuata maelekezo ya muumba wao. Aliwakumbusha wasomo hao kufanya kazi kwa bidii popote watakapokuwa kwani wapo kwenye Jihadi
Habari/Tangazo
AN-NUUR
Na Bakari Mwakangwale
CHAMA Cha Wananchi CUF, kimesema wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio watakaokuwa waamuzi wa mwisho katika kuipitisha au kuikataa Katiba mpya. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Msonge, Jimbo la Kawe, Jijini Dar es Salaam Ijumaa ya wiki iliyopita. Maalim Seif alisema hivi sasa mchakato wa Tanzania kupata Katiba mpya unaendelea na kwamba, kuna matumaini mwishoni mwa mwezi huu Tume ya Jaji Joseph Warioba, itatoa rasimu ya mwisho na kuikabidhi kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Mohammed Shein. Alisema viongozi hao wakishapokea rasimu hiyo, watashauriana ili waitishe Bunge la Katiba ambalo kazi yake kubwa itakuwa ni kuijadili rasimu hiyo, kisha kutoka na rasimu ya mwisho ambayo
Inawatangazia Waislamu wote kuwa kuimeandaa safari ya Hijja mwaka 2014 sawa na mwaka 1435 Hijria kwa USD 3,600. Kutakuwa na punguzo la asilimia 18 kuanzia muda huu mpaka Machi 22, 2014 Itakuwa dola 952 tu. Kuanzia 23 Machi 2014 kuna punguzo la asilimia 8 mpaka Juni 2014 itakuwa dola 3,312 tu. Mambo yatakayogharamiwa ni semina za Hijja, huduma za afya na kuchanja, airport charge na tiketi za ndege, nyumba Makka na Madina, Ihram na kuchinja kwa ajili ya Tama-Tuu, chakula wakati wote, usafiri na ziara Makka na Madina, Mahema Mina na Arafa. Umra mwezi wa Ramadhani itakuwa ni dola US 1975. Fomu zinapatikana Ofisi ya AHLUL DAAWA Dar es Salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini- nyumba namba 26 mkabala na Showroom ya magari Tel: 0713 730444 au 0773 804101 au 0785 930444 au 0773 930444. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982 au 0777 413 987. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es Salaam Tel: 0784453838. Abdalla Saleh Mazrui (Hoko) Dar es Salaam Tel: 0715 724 444. Dukani kwa Abdalla Hafidh Mazrui Wete Pemba Tel: 0777 482 665. Dukani kwa Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba Tel: 0777 456 911, Sheikh Daud Khamis Sheha Tel: 0777 679 692, Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel: 0777 417 736. Wahi kulipa ofisi ya Ahlul Daawa Dar es Salaam Tel: 0713 730 444 au 0773 804 101 au 0785 930 444. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982 au 0777 413 987. Maalim Seif Humoud Salim Tel: 0777 417 736. Sheikh Salim Mohamed Salim Tel: 0774 412 974 au Account No 048101000030 NBC Kariakoo. Atakayemaliza taratibu zote mwanzo ndiye atakayeshughulikiwa mwanzo. Ukilipa kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412 975. Kumbuka kikundi cha AhlulDaawa kwa bei nafuu kuliko wote na huduma bora kuliko wengi Wabillah Tawfiq
Inatoka Uk. 1 wa Mtuhumiwa. Alisema, ombi la pili la dhamana lifanyiwe kazi likizingatia mashariti yatakayowekwa na mahakama. Kufuatia hoja hizo za pande mbili za kesi, Mahakama Kuu ilitoa dhamana kwa mtuhumiwa wa Mauwaji ya Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Omar Musa Makame. Akitoa dhamana hiyo, Jaji Mkuu Omar Othman Makungu, amesema mtuhumiwa huyo amepewa mashariti mawili: Moja kuwa atalazimka kupata wadhamini wawili watakoweka dhamana ya laki tano kila mmoja wakiwa na vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi (ZAN ID).
Sharti la pili ni kuwa na barua ya sheha na kuripoti katika Mahakama mbele ya Mrajis Mkuu kila siku ya Jumatatu. Mapema mwendesha mashitaka wa serikali, Abdalla Issa Mgongo, alidai mahkamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo kesi hiyo ipangiwe siku nyengine kwa kutajwa. Mtuhumiwa Omar Musa Makame anadaiwa kumpiga risasi na kumuua Padre Mushi Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza Ibada ya Jumapili asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya Mji wa Zanzibar . Alitiwa mbaroni Machi 17, mwezi mzima baada ya tukio.
4
Na Omar Msangi Assalaam alaykum wtw. Kaka Msangi makala yako ya leo (Ijumaa iliyopita) ya: Waislamu TZ hatujachelewa Jihad imenichanganya. Ni vipi Waislamu wanaweza kupambana na serikali inayowapendelea Wakristo halafu Wakristo wasichukizwe?...Kaka Msangi, hii U-turn katika reporting kipindi hiki vipi? Huo ni ujumbe wa maneno ambao niliupokea kutoka mmoja wa wasomaji Ijumaa iliyopita mchana. Msomaji mwingine naye alikuwa na haya ya kuniambia, alisema: Muambieni Muhariri wenu Bwana Omar Msangi majibu aliyopewa ukurasa wa 8 An nuur ya jana anatakiwa abadilike na atafute habari katika vyombo vya habari kama Somalimemo.net Swahili. com atapata habari za Waislamu duniani sio kutoa habari katika vyanzo vya makafiri na akiendelea na kudhoofisha jihad, Allah atamuangamiza yeye. Kwa sasa hatujamtoa katika dini ila akiendelea tutamkufurisha na kumuona ni munafiki na kama anaogopa kuandika habari za jihad aache sio kurudisha nyuma Mujahidina. Bado kuna ujumbe mwingine ambao nao ningependa kuunukuu: AA ndugu Mhariri mfahamishe Omar Msangi kuwa Uislamu unatenguka kama udhu, yeye anaipinga Jihad kwa kuhofia kuviacha vitu vyake vizuri kama mke, watoto, nyumba, gari n.k akumbuke kuwa vyote hivyo ataviacha kwa lazima na akumbuke Qaarun katika suratu Qaswaswi aya ya 76, je, alienda na mali zake kaburini? Aache unafiki. Yupo wapi Rais wa wanafiki duniani Abdallah ibnu Ubaay ibnu Suluul? Hao wanaomtumia hawatomsaidia kitu siku ya kisimamo. Aaangalie suratu Abasa aya 34-37 Zimetajwa aya hapa labda na zenyewe niziweke ili ionekane maana mtuma ujumbe aliyoikusudia. Hakika Karuni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu (kuzichukua). Walimwambia watu wake: Usijione (usijigambe) hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojiona. (28:76) Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye. Na mamaye na babaye. Na mkewe na wanawe. Kila mtu miongoni mwao siku
Maoni yangu
AN-NUUR
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
hayo. Wakati huo huo mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa manne ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Mashariki na Pembe ya Afrika-IGAD, wameelekea Sudan Kusini kuanza juhudi za kumaliza mapigano hayo yanayozusha hofu ya kugeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mawaziri hao wanatokea Kenya, Djibouti, Ethiopia na Uganda. Kwa upande wake, Marekani imeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu mapigano ya Sudan Kusini, huku Waziri wake wa mambo ya nje, John Kerry akitoa wito wa kuwepo utulivu. Marekani na Uingereza zimeanza kuwaondoa wafanyakazi wake kutoka Juba. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon mapema wiki hii aliitisha mkutano wa Baraza la Uslama UN kujadili hali ya Sudan Kusini na imeazimiwa kupelekwa majeshi ya kusimamia usalama nchini humo. Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wameyakimbia makazi yao na kwenda kutafuta hifadhi kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa tangu yalipozuka mapigano siku ya Jumapili.
6
Na Omar Msangi BADO yanazidi kufichuka mambo ya kutisha katika kile walichofanyiwa Waislamu wa Kilindi kiasi miezi miwili iliyopita. Kwa hakika ni mambo ya kusikitisha na kuhuzunisha ambayo hayakutarajiwa kufanyiwa mwananchi katika nchi yake huru. Ni wazi kuwa kila mwenye chembe ya imani, utu na ubinadamu, atalaani vitendo kama hivyo vinavyodaiwa kufanywa na walinzi wa usalama wa raiya na mali zao. Inavyofahamika, hata kama ni jambazi, hukamatwa na kufikishwa mahakamani akashitakiwa huku haki zake zote za kibinadamu zikizingatiwa. Lakini yaliyojiri Kilindi, ni hadithi nyingine kabisa. Watu wamepigwa r i s a s i , m a l i zimeharibiwa, nyumba zimechomwa moto na mali kuporwa. Kwa sasa hakuna la ziada la kusema ila kuungana na watu wote wema kulani ukatili huo. Kwa tuhuma zozote zitakazo kuwa, hakuna namna ya kuhalalisha mambo waliyofanyiwa watu wa Madina na vijiji vingine vya Kilindi. Baada ya utangulizi huo, niseme kuwa inabidi kila wakati kuwa makini tusiunganishe mambo tukashindwa kuyaelewa kila moja kwa muktadha wake. Kwa mfano, mtu akipinga uingiliaji kati wa nchi za Marekani na NATO katika mgogoro wa Syria, haina maana kuwa anaunga mkono udikiteta na utawala mbaya anaodaiwa kuwa nao Bashar al Assad. Na ndio hivyo hivyo, kupinga baadhi ya Waislamu kujitenga na kuanzisha vijiji vya kwao pekee wakidai kusimamisha utawala wa Kiislamu ndani ya nchi, haina maana kuunga mkono ukatili, mauwaji na udhalimu unaodaiwa kufanywa na polisi walipovamia baadhi ya vijiji hivyo. Ni kweli Saddam Hussein alikuwa dikiteta kama ambavyo inaweza kudaiwa kuwa alikuwa Muammar Gadhafi na sasa Bashar al Assad. Swa l i ni j e, mtindo uliotumika kumngoa Saddam, umeleta nafuu yoyote kwa watu wa Iraq? Hilo ndio swali la kuhoji na kufanyia tathmini. W a p o w a t u katika Afghanistan
Makala
AN-NUUR
Ila Elimu kwanza sio kutoa vijana shule Tutaumwa mara ngapi ndio tujifunze?
wasiokuwa wakitaka nchi hiyo itawaliwe Kiislamu) wakipiga mateke maiti za askari wa Taliban waliouliwa na makombora ya Marekani.
Lakini hali ikoje leo? Wapo pia waliochekelea kupigwa Saddam na wengine wakashika silaha kushirikiana na NATO Kumngoa Gadhafi. Wenyewe
Kwa watu waliofika Hospitali ya Bombo kwa kweli waliwaona vijana waliokuwa wamefungwa pingu wakiwa katika vitanda vyao huku wakilindwa na askari. Taarifa zikafika vilevile kuwa kuna watoto wadogo wamefikishwa Tanga baada ya kukutwa porini. Watoto hawa walikuwa wamehifadhiwa katika moja ya shule za hapo mjini. Katika hali kama hiyo, vilevile zikafika taarifa tofauti kwa Waislamu wa Tanga kuwa hao walioletwa Hospitali ya Bombo na watoto waliookotwa porini, ni Waislam wa vijiji vya Madina, Dibungo na Lwande walioshambuliwa na askari pasi na sababu. Juhudi za Umoja wa Taasisi za Kiislamu Tanga (SHITA) chini ya Mayor Omari Guledi na Katibu wake Ahmed Mustafa kukutana na Mkuu wa Mkoa Chiku Galawa kupata ukweli zikagonga mwamba. Hali ikawa tete baada ya Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso mmoja katika masheikh vijana mjini Tanga kukamatwa na kuwekwa rumande kisha kuhamishwa Handeni ambako alifunguliwa kesi ya ''kushawishi mauaji.'' Ikavuma kuwa Inaendelea Uk. 7
7
Inatoka Uk. 6 Bashar. Hivi sasa mamilioni ya raia wasio na hatia wanataabika katika kambi za wakimbizi wakiwa hawana msaada wa kutosha katika majira haya ya baridi kali. Yamewafika masaibu haya kutokana na vita ya wapinzani wanaodai kupigana Jihad kumngoa Bashar al Assad. L a m u h i m u kufahamika hapa ni kuwa, hawa Al Nusra, hawakuanza katika mgogoro huu wa Syria. Na hawa al-Nusra Front, al Qaidah, Jeshi la Kiislamu (Iraq) na Lashkar-e-Taiba (LeT) katika Pakistan, ni makundi ya Kiislamu yanayofadhiliwa na baadhi ya nchi za Kiarabu na ndio yanayotumika kutafuta visingizio vya kupigwa Waislamu yakidaiwa kuwa ni ya kigaidi. Lakini inapokuja kusaidia kumpiga na kumtoa mtu asiyetakiwa na Marekani kama Bashar, hawa hugeuka kuwa maswahiba wakawa wanapewa silaha na mafunzo kutoka Marekani na NATO kupitia nchi za Kiarabu. Maji yamekuwa marefu kwa Free Syrian Army. Kama ilivyokuwa kwa Afghanistan, sasa inaonekana wanaoweza kupambana na jeshi la Bashar ni Waislamu walioaminishwa kuwa wanapigana Jihad. Hapa ndio wanaingia hawa Al-Nusra Front na wenzao. Kupitia kwa Saudi Arabia/Qatar, sasa hawa ndio watakuwa wakipata misaada ya silaha, fedha na kuungwa mkono kidiplomasia. Mapema mwaka 2010 mtandao wa WikiLeaks, ulifichua mawasiliano ya siri ya tarehe 30 Desemba 2009 ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton kwa mabalozi wake (US embassies) akisema kuwa Saudi Arabia imekuwa ndiye mfadhili mkubwa wa makundi ya Jihad ya Kisuni ambayo kwa msamiati wa Kimarekani, ni magaidi. Makundi hayo ni pamoja na Al-Nusra, na ndiyo yanayotumiwa kupigana Syria hivi leo. Wapo watu ndani ya AlNusra (hasa wale walio katika mawasiliano ya moja kwa moja na Prince Bandar Ben Sultan a.k.a. Bandar Bush) wanaweza wakajua
Makala
AN-NUUR
p a t a k u w a n a m a a n d a m a n o kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Chambuso. Askari wa FFU walizingira misikiti kadhaa Ijumaa hiyo, lakini hapakuwa na maadamano yoyote. Alipopata dhamana na kuachiwa Sheikh Chambuso alikuja
Tanga, aliwafahamisha Waislamu kuhusu misikiti iliyovujwa na kuchomwa moto, Qur'an zilizochomwa moto na nyumba za Waislamu z iliz o t e ke t e z wa kwa kisingizio cha ugaidi. Wananchi jioneeni wenyewe yote hayo katika hizi picha. (Maelezo ya msomaji An nuur)
wa Marekani na Jeshi la Kiislamu, haina maana kumuunga mkono Assad na ubaya wote anaodaiwa kuwa nao. Hoja ni kukataa k u t u m i w a . Kupumbazwa ukadhani unapigana Jihad, kumbe unatumiwa. Unapigana huku anayekupa msaada anapanga namna ya kukuangamiza baada ya kumaliza kazi aliyokutuma bila kutambua. Ujinga huu ndio inapasa Waislamu waepukane nao. Madina Madina ni kijiji kilichoanzishwa miaka ya 1990s, waanzilishi wakidai kuwa kwa kujitenga na kuishi hapo wataweza kusimamisha Shariah ndani ya nchi inayodaiwa haina dini! Walijenga na wakajishughulisha na kilimo na biashara mbalimbali. Pamoja na waanzilishi, baadae walipatikana pia watu wa kuhamia. Hata hivyo, baadae baadhi waliamua kuhama baada ya kuingia sera ya kutaka watu watoe watoto wao shule ikidaiwa kuwa kupeleka watoto shule ni ukafiri. Wapo waliohama baada ya kushindwa kukubaliana na sera hiyo na wapo waliobaki, lakini watoto wao wakaendelea kusoma. Lakini wapo pia ambao walitoa watoto wao shule. Hivi karibuni kuna vijana waliacha shule, wengine wakiwa kidato cha sita na baadhi wakiwa vyuo vikuu. Hawa inaaminika kuwa baada ya kuacha masomo, walikwenda Madina na kuanza maisha huko. Walitoweka katika mazingira ya kutatanisha, baadae ikafahamika kuwa wapo Madina. Baadhi ya vijana hawa walitoka katika shule za vipaji maalum kwa maana kuwa walikuwa vijana wenye akili nzuri na kwa hivyo tarajio la ummah wa Kiislamu na nchi kwa ujumla. Wapo pia baadhi ambao walikuwa wakimalizia masomo yao ya udakitari (medicine) katika moja ya vyuo vikuu nchini. Wanajulikana kwa majina na wala sio habari za amini ukipenda. Swali hapa ni je, ukirejea ile amri ya kwanza kwa Mtume (s.a.w) ya Iqra, inakubalika kuwazuiya Inaendelea Uk. 8
8
Inatoka Uk. 7 watoto kusoma? Inakubalika katika Uislamu kumtoa kijana aliye kidato cha sita au Chuo Kikuu ili aende Madina kwa kumlaghai kuwa hayo ni maandalizi ya kusimamisha Shariah? Katika jumla ya malalamiko ya Waislamu nchini ni kuwa wamebaguliwa katika elimu na ajira. Je, mtu ambaye leo katika karne hii ya 21 ya sayansi, tekinolijia, IT na utandawazi, anampumbaza kijana wa kidato cha sita/chuo kikuu na kumtoa katika masomo kwa madai kuwa huo ni ukafiri, ni kupoteza muda, bali akajitenge katika kijiji cha pekee kungoja Jihad, utasema huo ndio Uislamu? Au ndio namna ya kusimamisha Uislamu? Ieleweke vizuri hapa kuwa hoja sio kukubali au kupinga Jihad. Wala sio kuunga mkono au kupinga kusimamisha Khilafah. Hoja ya msingi hapa ni njia ya kupita. Kama ilivyokuwa Rwanda, kule Bangui, Afrika ya Kati, chuki imetumbukizwa baina ya Waislamu na Wakristo, sasa wanachinjana kijiji kwa kijiji. Seleka haijaanzishwa kama kikundi cha kupigania Uislamu, wala hawana mpango kabisa na kusimamisha Shariah! Mabeberu wamepata mwanya wa kuleta majeshi yao kwa kisingizio cha kulinda amani. Wakati wananchi wakiuwana, mabeberu wanavuna dhahabu, almasi na uranium. Imekuwa Congo (DCR) nyingine. Hebu natupate fundisho kama ni wenye akili. Katika nchi zote ambazo mabeberu wanatamani kuzikalia hivi sasa katika mtindo mpya wa ukoloni, uchochoro wao muhimu wa kupita, ni kupandikiza machafuko. Mahali pasipo na ugaidi, watapiga sana propaganda kuwa kuna magaidi huku wakitumia vyombo vya habari mpaka ikubalike ili wapate fursa ya kusema wanaingiza FBI wao na Marine wao na drone zao kusaidia kupambana na magaidi. Wakishaingia hawatoki. Na kwa upande mwingine, ukishapandikizwa huo ugaidi, ujue hautakwisha. Kila siku itakuwa watu ni kulipuana tu. Ndio hali ilivyo Yemen, Pakistan,
Makala
AN-NUUR
SHEIKH Rajab Chambuso (katikati). Afghanistan, Iraq, Somalia, Libya na sasa Kenya nayo inaelekea huko huko. Westgate Mall Shopping Centre attack na maguruneti, hayatakoma. Hivi hatukumbuki ile kampeni yao ya kudai kila wakati kuwa Afrika Mashariki kuna kitisho cha kushambuliwa na magaidi wakionya watu wao wasitembelee miji ya nchi hizo? Tumesahau yale madai kuwa mtoto wa shule ya msingi aliingia katika moja ya balozi zao na kigeleni cha mafuta ya taa akitaka kufanya ugaidi? W a l e v i j a n a waliokatisha masomo yao wakiwa kidato cha sita, hawakufanya hivyo ila baada ya kuhudhuria darsa zinazoendeshwa na watu ambao unaweza kusema kuwa hawa ni mawakala wanaotumiwa k u p a n d i k i z a vurugu/ugaidi. Wanachoaminishwa vijana hao ni kuwa kusoma ni kupoteza muda bure. Muhimu kwao ni kwenda kupigana/kupambana na makafiri. Kwa hiyo, wao huacha shule kwa imani thabiti kuwa wanalofanya ni jambo la dini. Lakini mwisho wa yote ni kutumiwa kuleta vurugu itakayoangamiza Uislamu wenyewe na nchi. Zipo taarifa za uhakika kuwa walipoingia vijana hawa Madina kati ya mwezi wa sita na saba mwaka huu, biashara ya mayai ya kuku wa kienyeji ilikuwa kubwa sana. Wenyeji walikuwa hawana uwezo wa kupata kifungua kinywa kwa mayai. Lakini kuingia wao, ikawa hakuna yai linalotagwa ila, limepata mnunuzi. Hawa ni vijana waliokuwa shuleni na vyuoni wakisoma kwa mkopo wa serikali na kwa kutumiwa pesa za matumizi na wazazi wao. Na wazazi wao wanajulikana uwezo wao wa kiuchumi. Huu uwezo wa kwenda kuishi na kujitegemea huko Madina, waliupata wapi? Hata hivyo, pamoja na kuhoji mambo haya, kama nilivyosema awali, sote kwa pamoja kwa hakika tunapaswa kulani kwa nguvu zote
Mahitaji ya Vifaa yanayohitajika kufikia hatua ya Zege la Jamvi PLOT No. 152 Block A, Masjid Jumuiyatil Islamia Ubungo Darajani.
Na Mahitaji 1 2 3 4 5 6 7 8 9 Nondo 12 MM Nondo 8 MM Binding Wire 20 MAWE 200 CM KOKOTO 70 CM Mchanga 40 CM Cement Mbao Cypruss Misumari JUMLA NDOGO Deni la Mkandarasi (mjenzi) JUMLA KUU 35,657,000.00 Nb: haya ni Mahitaji kwa ajili ya Zege la Jamvi Kwa mawasiliano zaidi Tupigie Mwenyekiti 0754 462 050 Katibu 0719 760 777 Mwenyekiti Kamati ndogo ya ujenzi ( Goha) 0787 318 116. International Commercial Bank No A/c 00001/01/601059/01 au A/c 0000/01/ 0009/94/02. Au tutembelee katika Msikiti wetu uliopo Ubungo Darajani. Wabillah Taufiq Size Pcs Pcs Kg Lori Lori Lori Mifuko 16 Kg Idadi 120 60 1 20 7 4 350 120 10 @ 18,000 8000 52000 250000 750000 13500 9000 3000 Tshs 2,160,000.00 480,000.00 52,000.00 5,000,000.00 5,250,000.00 4,725,000.00 1,080,000.00 30,000.00 19,657,000.00
220,000 880,000.00
Makala
AN-NUUR
Na Sheikh Abdallah Bawazir NDIO utaratibu wetu sisi waumini wa dini iliyoletwa hapa duniani na Mtume Muhammad (s.a.w.), kumtanguliza kiongozi wetu kila tunapotaka kutaja tabia njema au mtu yeyote mwenye tabia njema. Kwa sababu hivyo ndivyo tulivyofundishwa na Mola wetu na aidha yeye Mtume Muhammad (s.a.w.), ndiye mkamilifu wa tabia njema. Hayo ndio mafundisho yetu katika Uislamu wala hayahitaji mjadala. Hata hivyo, sio ajabu kumpata mtu na wala mtu huyo si Muislamu kamwe, lakini akawa ana tabia fulani njema na nzuri kinyume cha Muislamu mwenyewe ambaye ilikuwa ni wajibu wake kuwa na tabia hizo, kwa kuwa ndio mafundisho ya dini yake. Kusamehe ni tabia mashuhuri ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.), hasa pale anapokuwa na uwezo na amri ya kuweza kumuadhibu a n a y e s t a h i k i kuadhibiwa. Mfano hai wa hilo katika maisha yake, unapatikana katika kipindi alipoiteka Makka pasina umwagaji wa damu na kuwa chini ya himaya ya dola yake kikamilifu. Aliwasamehe watu waliomkosea hata
MZEE Nelson Mandela. Rais wa Misri Gamal Abde Nasser, yeye pia alizaliwa mwaka huo huo wa 1918 mwaka aliozaliwa Mandela. Lakini Gamal alifariki mapema mwaka 1970 akiwa na umri wa miaka 52 tu. Baadhi ya viongozi waliobahatika kuupata umri wa Mzee Madiba au karibu yake ni Habib Buurqiba 1903 2000 wa Tunisia, Aden Osman 1908 wa Somalia, Dakta Azikiwe 1904 1996 wa Nigeria na Ahmed Ben Bella wa Algeria 1916 2012. Aidha Mzee Mandela amebahatika kufariki Dunia katika hali hii, akiwa bado anapendwa na kuheshimiwa na watu, bila ya kupata mitihani na misukosuko katika kipindi chake kifupi cha uraisi mpaka anajiuzulu mwenyewe kwa ridhaa yake. Bahati kama hii wameikosa wengi miongoni mwa viongozi wa kisiasa wa Bara letu la Afrika na badala yake, walikufa katika hali mbaya na ya dhuluma. Miongoni mwao ni Ahmed Ben Bella wa Algeria, Patrice Lumumba wa Congo au Alhaji Aboubakar Tafawa Balewa, katika dhuluma isiyosahaulika iliyomkuta mwaka 1966 huko Nigeria. Mfano mwingine wa karibu ni dhuluma aliyofanyiwa Dkt. Mohammed Mursi wa Misri, kwa kunyanganywa Serikali kihuni baada ya kushika madaraka kwa mwaka mmoja tu. Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir +255 767 215 898
Inatoka Uk. 12
mdogo. Mwakilishi wa jimbo la Wete, Asaa Othman, alisema ingawa mataifa ya nje yataingilia kati sheria hiyo kwa madai ya haki za binadamu, lakini watu wanaofanya vitendo hivyo ndio wanavunja haki hizo. Akichangia hoja binafsi ya azimio la vitendo vya udhalishaji
jamaa zao kupelekwa k a t i k a v y o m b o v ya sheria. Hoja binafsi hiyo iliyowasilishwa mapema wiki hii na mwakilishi wa viti Maalum Mgeni Hassan Juma, inataka kuanzishwa sheria na mikakati itayosaidia kukomesha vitendo vya udhalishaji watoto vinavyongezeka Zanzibar.
10
Inatoka Uk. 4
Makala
AN-NUUR
11
Inatoka Uk. 12 unaotumika kwenye mikutano ya nchi wanachama wa SAPCO. Amesema kutokana kushindwa kuwakamata wahalifu hao na kuibwa upanga huo, ipo haja ya kulifanyia mabadiliko zaidi jeshi hilo, badala ya kufanyiwa mabadiliko ya kamishna pekee. Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud, amesema kumetokea vitendo vingi vya uhalifu lakini jeshi hilo limeshindwa kuwakamata wahalifu husika. Amesema hali hiyo bado inaonesha kuwa jeshi hilo lina matatizo na kuunga mkono ushauri uliotolewa na Mwakilishi huyo wa kutaka jeshi hilo kufanyiwa mabadiliko ya uongoizi. Kuhusu wizi wa upanga wa dhahabu uliotokea mikononi mwa Jeshi la Polisi Zanzibar, Bw. Aboud alisema uchunguzi unaendelea
Habari/Tangazo
AN-NUUR
13
TH
GRADUATION
The Principal of the University College of Education, Zanzibar (UCEZ), cordially invites all graduands of the academic year 2012/2013 to the 13th Graduation. The Ceremony will be held on Saturday 18th January 2014 at the University College premises. The Second Vice-President of Zanzibar HON. EMBASSADOR SEIF ALI IDD will be the Guest of Honour. All graduands are required to confirm their participation to the Academic Office not later than on Friday 10th January 2014. Graduands are reminded to pay Tzs. 10,000/= (non-refundable) before Thursday 16th January 2014 for graduation gowns. Please note that travel, meals and boarding expenses will be met by the graduands themselves. All graduands are requested to report at the College by 3:00 pm on Friday 17th January 2014 for rehearsal and logistical briefings. Graduands who will not participate in rehearsal will not be allowed to take part in the event. For more information contact the University College on the following address: The Academic Office, University College of Education Zanzibar P.O. Box: 1933 Zanzibar. Tel: +255242234102 Email: amacez@zitec.org Website. www. ucez.ac.tz Mobile: 0776-463405/ 0773-181786
12
AN-NUUR
MAKALA
12
AN-NUUR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na Kamishna mpya wa jeshi la polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame, baada ya mazungumzo yao ofisini kwake Migombani.
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kutunga sheria itakayotoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa, mtu atakayepatikana na h a t i a ya k u m b a k a au kumlawiti mtoto
Inaendelea Uk. 9
nyuma wakati wa kuanzishwa kwangu. K w a s a s a naendelea kutoa elimu bado, ingawa nimechoka sana kutokana na uchakavu wa majengo yangu.
Naomba msaada kwa Serikali na wasamaria wema kunifanyia alau ukarabati tu na ikiwezekana kujengwa upya niwe na sura mpya kama hii inayoonekana hapa chini.
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.