Está en la página 1de 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

(15) MATAJIRI WA KIISLAMU!


Mtume(saw) amesema, Kutoa katika Hijja ni sawa na kutoa katika Jihadi, . Uwezo wa baadhi yetu ni uwezo wetu. Waislamu ni kama jengo au kiwiliwili kimoja. Tupelekane Hijja na tusaidiane kuisimamisha nguzo ya Hijja! Kadiri tutavyokwenda wengi Hijja, ndivyo na Allah Atavyotupa utukufu na nguvu nchini mwetu. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa.Gharama zote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117

Ilunga hajapata matibabu


Yupo hospitali ya Columbia Asia- Bangalore Ubalozi wa India Dar waombwa kusaidia Waislamu watakiwa kufanya Subra kidogo
KAMA ilivyokuwa kwa kaka yake Abdulwaheed, naye Ally Sykes ameondoka kimya kimya. Ally Sykes mzalendo muasisi wa TANU ambae sahihi yake ndiyo iko katika kadi ya TANU ya Baba wa Taifa, amefariki Nairobi Jumapili iliyopita alikokwenda kwa ajili ya matibabu. Siku ile ile ya Jumapili milango ya mchana mchanga kabisa kabla ya Adhuhur, taarifa ikawasili Dar es Salaam kuwa Ally Sykes amefariki dunia. Siku ya pili Jumatatu magazeti yote yalikuwa yametoka yakiwa hayana taarifa yoyote ya kifo cha Ally Sykes. (Soma Tanzia Uk. 6)

ISSN 0856 - 3861 Na. 1072 RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24-30, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Bingwa wa ukombozi aondoka kimyakimya

Kamati ya Mzee Moyo kufanya kongamano


Na Mwandishi Wetu

MARHUUM Ally Sykes

Litafanyika Bwawani kesho Kufunguliwa na Maalim Seif

SHEIKH Ilunga Hassan Kapungu

KAMATI ya Maridhiano ya Mzee Nassoro Hassan Moyo imeandaa kongamano kubwa litakalofanyika katika ukumbi wa Salama hoteli ya Bwawani.

Habari kutoka kamati ya maandalizi zinasema kuwa kongamano hilo litafunguliwa na Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Shariff Hamad. Habari zaidi zinasema kuwa pamoja na mada itakayotolewa

Inaendelea Uk. 2

2
AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
MAONI YETU
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Habari/Tangazo
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013


ya miradi hiyo ya gesi au mafuta, ni sawa na kuwaadhibu kwa makosa yaliyoasisiwa na serikali yenyewe kwa wananchi wake. Tumewajengea imani na uvumilivu, tumeshindwa kutimiza yale yaliyowafanya wawe na imani na uvumilivu kwa serikali yao. Ni wajibu wa serikali sasa kujifunza kutimiza kikamilifu ahadi za maendeleo kwa watu wake kwa wakati, lakini zaidi kutumika kikamilifu rasilimali zilizopo kwa kuzingatia kwanza maslahi ya watu zinapotoka rasilimali hizo.

AN-NUUR

KAMA kungekuwa na rekodi nzuri ya kutekelezwa ahadi za maendeleo katika mikoa ya Kusini mwa nchi yetu tangu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, basi leo hatudhani kama haya yanayotokea Mtwara sasa yangekuwepo. Kwa miaka mingi tangu awamu ya kwanza ya uongozi wa Mwalimu Nyerere, mikoa ya Lindi, Mtwara na (Ruvuma) Tunduru imekuwa katika wakati mgumu kimaendeleo, licha ya kusheheni hazina kubwa ya maliasili isiyoendelezwa na kuwa mahiri kwa kilimo cha mazao ya biashara na ya chakula. Lindi na Mtwara ni maarufu kwa zao la korosho, matunda hasa mananasi, maembe na machungwa. Lindi na Mtwara mahiri kwa uzalishaji wa chumvi, kuna hazina kubwa ya mambo ya kale na ya kihistoria ambayo yanaweza kuwa chanzo kikubwa cha utalii na fedha za kigeni. Miji ya Kilwa, Mikindani, visiwa vya Maa, makaburi ya wapigania uhuru wa Msumbiji, mapango na visima vya maji huko Kipatimu ni vielelezo na ushahidi tosha wa kuwepo uhalisia wa vivutio vya utalii katika mikoa hiyo. Ukiacha maeneo hayo, Mkoa wa Ruvuma una hazina kubwa ya madini hasa katika wilaya ya Tunduru. Mikoa yote hiyo kwa ujumla wake ni maarufu kwa historia ya vita vya majimaji vilivyopiganwa kabla ya uhuru. Jiografia ya mikoa hiyo ni kigezo cha msingi katika maendeleo ya mikoa hiyo na Taifa kwa ujumla, na kwa hakika ilistahili kuwa mbali hadi kufikia karne hii tuliyo nayo sasa. Bandari ya Mtwara na Lindi zingekuwa kichocheo kikubwa zaidi cha maendeleo na uchumi wa mikoa hiyo na ile ya jirani. Kadhalika mikoa hiyo inapakana na nchi jirani za Msumbiji na Malawi, ujirani ambao ni muhimu kwa maendeleo ya kibiashara kati ya watu wa Tanzania hususan wa mikoa hiyo na wale wa nchi hizo. Hata hivyo licha ya kuwepo vichocheo hivyo muhimu vya kiuchumi kwa watu wa mikoa hiyo na Taifa kwa ujumla, bado serikali kwa kipindi chote cha kuwepo kwake, inaonekana kushindwa kutumia kikamilifu fursa zilizopo kiasi cha kuifanya mikoa hiyo kwa miaka mingi kubaki nyuma kimaendeleo kinyume kabisa na utajiri na fursa zilizopo. Maeneo mengi ya mikoa ya kusini yamekuwa hayapitiki, umeme hakuna, maji tabu, shule za akina Kayumba, vituo vya afya nk. Imefika wakati hata

Mtwara wana hoja japo wakikosea njia

kwanza kutizama historia ya watu wa mikoa hii. Hawa ni watu waliochoka na kukata tamaa. Na haitasaidia sana kwa serikali kukimbilia kudai kuwa watu hawa wanachochewa. Kama ni kuchochea, basi mchochezi wa kwanza atakuwa ni Serikali yenyewe kwa kushindwa kujenga barabara ya Mtwara- Dar ikawa kama za mikoa mingine na hivyo kuifungua kusini. Serikali ijiulize, ile Mtwara Corridor imefanya nini katika ile dhana ya kuleta maendeleo kusini? Kama hakuna, kwa nini serikali isikirie kuwa huu ndio uchochezi wenyewe? Inapaswa kutizama

imetekeleza kwa kiasi gani ahadi za kimaendeleo walizopewa wananchi hao kwa awamu zote za uongozi zilizopita. Baada ya hapo iwape elimu ya kutosha na kuwahakikishia maslahi yao katika miradi hii ya gesi na mafuta hadi watakapoelewa. Wakirejesha imani yao kwa serikali na kuelewa kusudio la serikali, ndipo michakato iendelee kwa amani na utulivu. Serikali inawajibika kuchukua hatua hiyo kwa kuwa ndiyo iliyowajengea imani na ndiyo iliyowakosesha imani hiyo. Kuwaponda kwa nguvu za dola kwa kukataa au kuzuia michakato

wafanyakazi wa umma, hasa walimu au madakrari wanaona kama ni adhabu kwenda kufanya kazi katika maeneo hayo. Ilikuwa kusari kutoka mikoa mingine kwenda Lindi na Mtwara ilichukua wiki kadhaa kutokana na uhaba wa miundo mbinu. Mpaka hivi tunavyoandika maoni haya, katika kipindi cha mvua, mawasiliano kati ya Tunduru na sehemu nyinginze za nchi hii, ukiwemo mji mkuu wa mkoa, hukatika kabisa. Kama mvua itapiga kwa miezi sita, basi kwa miezi yote hiyo, mtu akiwa Tunduru hawezi kuka Songea maana barabara haipitiki. Pamoja na kadhia zote hizo, bado watu wa Lindi na Mtwara, wamekuwa wavumilivu na kuendelea kutumaini siku moja watakumbukwa na kutoka katika kifungo cha kimaendeleo. Wa m e e n d e l e a k u v u m i l i a huku wakiendelea kuahidiwa na serikali juu ya maendeleo yao. Na kubwa wanalohitaji ni miundombinu. Kila uchaguzi kampeni zilipigwa. Chaguzi zilipita na mambo yalibakia kama yalivyokuwa. Hata hivyo bado walivumilia na kusubiri. Leo imegunduliwa hazina kubwa ya gesi na mafuta huko Mtwara. Serikali imekuwa katika mipango ya kuanza kuivuna hazina hiyo na kuanza michakato yake. Moja ya michakato hiyo ni kuivuna gesi na kuisarisha kwenda Dar es Salaam. Kwa kuwa watu wa Mtwara wamekuwa na hulka ya uvumilivu na serikali nayo kubakia na dhana yake kuwa watu wa Kusini ni wa namna ya kuvumilia, ikaanza michakato bila hata kuanza kutoa sera ya namna ya kuvuna hazina hiyo kwa wana Mtwara. Lakini hata baada ya serikali kuona kuna haja ya kutoa somo kwanza kwa wana Mtwara ili kurekebisha hali, bado wana Mtwara hao wanaona kama ni yale yale ya miaka ya zamani ya ahadi bila utekelezaji. Sasa wanaonekana kutoiamini tena serikali yao. Bado wanaiona bandari tuli ya Mtwara, wanashuhudia wakikopwa korosho zao, wakisari kwa taabu kutokana na miundombinu mibovu ya barabara na hata ile iliyoanza kujengwa, ikishindwa kukamilika kwa wakati. Hivyo ndivyo wanavyoamini kwamba gesi na mafuta vitavunwa katika ardhi yao na kunufaisha wengine na wao kuendelea kubaki hohehahe. Seriali imejitahidi kujipambanua lakini inaonekana bado makovu ya zamani yanawatesa wana Mtwara na mikoa ya jirani. Bado wanakosa imani baada ya kuwa nayo kwa awamu tatu zilizopita. Katika mazingira haya, viongozi wa serikali wanapaswa

Kamati ya Mzee Moyo kufanya kongamano


Inatoka Uk. 1
na Mzee Moyo mwenyewe, kutakuwa na wazungumzaji wengine, wakiwemo wajumbe wa kamati. Hata hivyo, waandalizi wa kongamano hilo walipoongea na mwandishi, hawakutaka kuweka wazi agenda ya kongamano na mada zitakazowasilishwa ila wakasema kuwa yatazungumzwa mambo muhimu kwa Zanzibar na Wazanzibari hasa yenye kugusa masilahi ya Zanzibar katika kipindi hiki cha kutayarisha katiba mpya. Kamati ya Maridhiano inafahamika kuwa ndiyo iliyofanya kazi kubwa kuleta maridhiano ya kisiasa Zanzibar yaliyozaa mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yaliyopelekea kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Chini ya maridhiano na Serikali hiyo, kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kisiasa na kijamii Zanzibar kubwa na la muhimu zaidi likiwa ni kuondoka kwa siasa za chuki na uhasama baina ya wananchi. Ni kwa sababu hiyo, kamati hiyo imepata heshma kubwa hasa ikizingatiwa kuwa huko nyuma zilishafanyika jitihada kubwa za kitaifa na kimataifa kuleta muafaka lakini hazikufanikiwa. Ni kwa sababu hiyo pia inatarajiwa kuwa kongamano la kesho litapa muitikio mkubwa wa wananchi wakiwa na hamu ya kusikia mipango na mikakati ya kuwapeleka mbele baada ya hatua hii ya awali kuonyesha mafanikio makubwa. Wakati huo huo , kuna

taarifa kuwa Sheha wa Tomondo Mohamed Omary Said amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu ya kifua na jicho. Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura. Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mukadam Khamis amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi wamekichukua ili kukifanyia uchunguzi. Inadaiwa kuwa Sheha huyo alimwagiwa tindikali juzi usiku alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na hakuweza kumtambua mtu aliyefanya uhalifu huo.

TAASISI YA KHIDMAT ISLAMIYA INAWATANGANZIA WAISLAMU WOTE SAFARI YA HIJA KWA GHARAMA YA DOLA 4450 TU AMBAZO ZINAWEZA KULIPWA KWA AWAMU (KIDOGO KIDOGO). GHARAMA YA (KUHIJIWA) NI DOLA 1450 TU. Kuondoka ni Tarehe 5 Octoba na kurudi ni tarehe 27 Octoba 2013 MALIPO YA HIJA YANAJUMUISHA GHARAMA ZIFUATAZO: NAULI YA NDEGE KWENDA NA KURUDI DAR- JEDDAH, MADINA - DAR MALAZI MAKKA, NYUMBA MWENDO WA DAKIKA 18 TU MPAKA MASJID HARAM. MALAZI MADINA, NYUMBA MWENDO WA DAKIKA 5 TU MPAKA MASJID NABAWY USAFIRI WA BASI KATI YA JEDDAH MAKKA, MAKKA MADINA USAFIRI WA UHAKIKA WA BASI MASHAIR (MINA, ARAFAT, MUZDALIFA) CHAKULA CHA KITANZANIA MILO MITATU, KUJIHUDUMIA MWENYEWE (BUFFET) BEGI LA KUSAFIRIA, SIMU YA MKONONI (NOKIA MOBILE) PAMOJA NA SIM CARD YA SAUDIA NGUO (IHRAM) KWA WANAUME NA WANAWAKE, GALONI LA LITA 10 MAJI YA ZAMZAM KUCHINJIWA MNYAWA WA UDH-HIYA, ZIYARAH SEHEMU ZOTE MAKKA NA MADINA KHIDMAT ISLAMIYA IMEKUWA IKIANDAA NYUMBA ZA MAHUJAJI KARIBU KABISA NA MASJID HARAM NA MASJID NABAWY). SHEIKH HASHIM AHMED RUSAGANYA, SHEIKH JUMA RAJAB IKUSI NA SHEIKH HARUNA JUMANNE KAPAMA WATAKUWEPO NA KUTOA MWONGOZO KWA MAHUJAJI WAKATI WOTE. AL-HAJJ AHMED SALEH NAHDY (HAMADO) NA AL-HAJJ ZULFIKAR OSMAN (ZULLY) VIONGOZI WENYE UZOEFU WA MUDA MREFU PIA WATAKUWEPO KUSIMAMIA MASUALA YA USAFIRI. LENGO NI KUHAKIKISHA KILA HUJAJI ANATEKELEZA IBADA YAKE INAVYOTAKIWA.DAKTARI ATAKUWEPO KATIKA MSAFARA NA MADAWA YOTE MUHIMU YATAPATIKANA WAKATI WOTE WA SAFARI. KWA MAELEZO ZAIDI NA UANDIKISHAJI WASILIANA NA: SHEIKH HASHIM AHMAD RUSAGANYA NAMBA YA SIMU 0715 915 008, 0784 915 008 SHEIKH ABDALLAH MOHAMED JUMA IMAM MSIKITI WA MTORO 0713 445 545 AL-HAJJ ZULFIKAR OSMAN 0777 411 020, 0713 530 036, 0786 411 020 AL-HAJJ HAFIDH SALIM 0655 616 623, 0682 535 319 SHEIKH HARUNA JUMANNE KAPAMA 0715 985 413 AL-HAJJ ALTAF ABDULLATIF AHMED 0789 373 222, 0779 786 786 AL-HAJJ OMAR AWADH KHAMIS - MSIKITI WA QIBLATAIN - 0715 210 666 ARUSHA: SHEIKH JUMA RAJAB IKUSI TAYSEER STORE DUKA NO.12 MKABALA NA NMB TAWI LA SOKO KUU NAMBA YA SIMU 0786 125 512, 0767 125 513, 0655 125 513 MOROGORO: AL-HAJJ AHMED SALEH NAHDY (AHMADO)- 0715 372 776, 0773 372 776 DODOMA & SINGIDA: AL-HAJJ YUNUSU RUGEIYAMU 0754 334 400, 0786 293 901 DODOMA & KONDOA: SHEIKH ESMAIL H. ALLIY 0713 677 683 MOSHI: IMAM MSIKITI WA SUNNI MAULANA DOGO 0754 918 977 AU AL-HAJJ OMAR AHMED FARAJ 0784 476 220 MWANZA&DAR: Dr. ABDULKARIM MAMBO SALEH (DAKTARI WA DAWA ZA KISUNNA) 0773 594 334 MULEBA, BUKOBA & DAR AL-HAJJ MAULID ATHUMAN KYEJU 0655 883 573 KIGOMA: AL-HAJJ ABASSI ISSA NYOTA 0688 154 004 TANGA: HAJAT ZAINAB MOHAMED 0713 416 454 HANDENI: AL HAJJ MOHAMED ADAM HAJEE 0784 705 750 KATIBU MTENDAJI Dr. MUHSIN MOHAMED HUSSEIN 0784 / 0715 / 0774 / 0755 786 680, MALIPO YAFANYE KWA KHIDMAT ISLAMIYA CHARITABLE SOCIETY BENKI YA NBC (MATAWI YOTE TANZANIA) AKAUNTI NAMBA 0211 0500 3194 KWA DOLA ZA KIMAREKANI AU KATIKA OFISI YETU ILIYOPO MTAA WA MAFIA DAR ES SALAAM OFISI YETU IPO MTAA WA MAFIA, TUNATAZAMANA NA MSIKITI WA MANYEMA Namba ya Simu 0655 409 135 (TIGO), 0684 409 135 (ZAIN), 0713 986 671. Barua pepe (E-Mail) hajjkhidmat@gmail.com , Tovuti (Website) www.khidmatislamiya.com Peace Travel & Tours LTD, ambayo ipo chini ya Khidmat Islamiya ni kampuni inayouza tiketi za safari ya ndege kwenda sehemu yeyote duniani na ni kampuni iliyosajiliwa rasmi na Serikali ya Saudia kushughulikia viza za Umrah kwa mtu mmoja mmoja, familia au kikundi na pia inatoa huduma ya msaada wa kupata viza za nchi mbalimbali duniani. Tovuti: www.peacetraveltz.com

HIJJAH 2013 / 1434

3
Na Mwandishi Wetu UBALOZI wa India jijini Dar es Salaam umeombwa kuingilia kati kuharakisha kupatikana kibali cha kutibiwa Sheikh Ilunga Hassan Kapungu ambaye amelazwa katika hospitali ya Columbia Asia HospitalBangalore, India. Kibali kinachohitajika ni kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa go (kidney transplantation) baada ya Sheikh Ilunga kupata matatizo ya go kushindwa kufanya kazi ambayo kitaalamu hutwa- chronic renal failure. Taarifa kutoka kwa ndugu na jamaa zinafahamisha kuwa Sheikh Ilunga alilazwa katika hospitali ya Columbia Asia Hospital- Bangalore, toka mwezi wa Februari mwaka huu 2013. Hata hivyo pamoja na taratibu zote za kupata nyaraka na vibali vyote husika ikiwa ni pamoja na kile cha Serikali ya Tanzania, yaani, No Objection Certificate (NOC ), bado Serikali ya India haijatoa Visa ya Matibabu ambayo ndiyo itawezesha hospitali kufanya matibabu ya kuweka go. Habari za kiutafiti zinaonyesha kuwa Ubalozi wa Tanzania (Tanzania High Commission) uliopo New Delhi, umesaidia sana katika jambo hili ikiwa ni pamoja na kutoa kwa haraka na kwa wakati ruhusa iliyohitajiwa na Serikali ya India. Pamoja na kuwa hospitali husika imekuwa ikitoa huduma nyingine za afya kwa Sheikh Ilunga kwa kiwango cha hali ya juu toka ameka hospitalini hapo, hata hivyo, kutokana na sheria za kimataifa juu ya upandikizaji wa viungo, kama hili la go, hairuhusiwi kufanya matibabu hayo bila ya kibali maalumu. Hiyo ni kutokana na kuwepo kwa biashara haramu ya viungo duniani na hivyo kuwekwa sheria kali ili kudhibiti biashara hiyo. Habari kutoka hospitalini Bangalore zinafahamisha kuwa tayari taratibu zote za kitabibu na malipo zishakamilika ikiwa ni pamoja na kuwepo mtu wa kutoa figo, ambaye ni dada yake Sheikh Ilunga ambapo vipimo vya kitaalamu vinaonyesha kuwa viungo vyao vinawiana, havina tatizo. Habari za kiuchunguzi za gazeti hili zinaonesha kuwa kutokana na hitajio la Sheikh Ilunga kupatiwa matibabu ya haraka kulingana na afya yake inavyobadilika kila uchao, uongozi wa hospitali (Columbia Asia HospitalBangalore) ulimweka Ilunga katika orodha ya wagonjwa wa kupewa kipaumbele katika matibabu husika toka katikati ya mwezi uliopita wa Aprili.

Habari

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013


wa India, jijini Dar es Salaam, kibali husika kitapatikana haraka iwezekanavyo baada ya kufikishiwa tatizo hili mapema wiki hii ofisini kwake. Kwa sababu hiyo, Waislamu wametakiwa kufanya subra wakisubiri jibu la Balozi na kama kutakuwa na tatizo la kuhitajia mawazo na msaada wa Waislamu wataariwa. Toka amalize ziara ya kuzunguka nchi nzima akitahadharisha kuwa iwapo dhulma haitakomeshwa na nchi kuendeshwa kwa uadilifu, inaweza kuleta balaa katika nchi; afya ya Sheikh Ilinga haikuwa nzuri hadi ilipogundulika kuwa alikuwa na matatizo ya kufeli go. Katika makongamano aliyokuwa akifanya huku akitumia mifano halisi, Sheikh Ilunga alionyesha kuwa kuna mfumo usio rasmi kikatiba na kisheria, ambao unawabagua Wa i s l a m u h u k u u k i t o a upendeleo kwa Wakriosto. Akatahadharisha kuwa, hatuwezi kuzungumzia kuwepo kwa amani ya kweli ya kudumu pamoja na umoja wa kitaifa bila kuangalia madai ya Waislamu kuwa kuna ubaguzi na dhulma.

AN-NUUR

Kutokana na hali hiyo, madaktari wake wanaomtibia katika hospitali hiyo waliandika taarifa maalum ikielezea hali ya ugonjwa wake na hitajio la kufanyiwa matibabu haraka wakitaraji kuwa vyombo husika vitaharakisha kutoa kibali husika. Naye mkuu wa jopo la madaktari wake Dr. Ravindran T. Jumapili iliyopita tarehe 20 Mei, 2013 alitoa taarifa ya kitabibu akionyesha umuhimu wa mgonjwa Ilunga Hassan Kapungu kupatiwa matibabu (Renal replacement therapy) haraka. Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni jana bado majibu ya kitengo husika huko India, yaani, Foreigners Registration Bureau, Bangalore, walikuwa bado hawajatoa kibali. Ndugu waliopo India wanasema kuwa kila wanapofuatilia katika ofisi hiyo, jibu mara zote limekuwa Your case is still pending.

Ilunga hajapata matibabu


Ufupi wa manneo, ikiwa na maana kuwa suala lenu bado linashughulikiwa. Katika kufuatilia suala hili, kamati inayoshughulikia matibabu ya Sheikh Ilunga, juzi ililazimika kutuma mjumbe hadi Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, na kukutana na Mkuu wa Kitengo cha Afya (Medical Attache) ili kutafuta msaada zaidi wa kiserikali ambapo taarifa zinasema kuwa yalifanyika mawasiliano ya haraka katika taasisi husika kule Bangalore. Juhudi hizo zikifanyika huko India, habari zaidi za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa taasisi ya Islamic Propagation Centre yenye Makao Makuu yake jijini Dar es Salaam imemwandikia Balozi wa India, ikimwomba kutumia uwezo wake na kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na India, kuingilia kati suala hili na kuwasiliana na kitengo

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewahimiza wazazi, walezi na walimu kushirikiana kutika kurejesha maadili na malezi bora kwa watoto. Maalim Seif ametoa wito huo wakati akizungumza katika haa ya maulid ya Mtume Muhammad (SAW), yaliyoandaliwa na Madrasat Ghulam Islamia ya Muembe Makumbi mjini Zanzibar. Amesema maadili ya Kiislamu na malezi bora kwa watoto yanaweza kurejeshwa iwapo jamii itakubali kushirikiana katika malezi, sambamba na kushajiisha elimu ya madrasa kwa vijana. Sisi wakati wetu mtoto alikuwa akilelewa na jamii nzima, yaani kama mtoto akikosea au kuondosha nidhamu na heshima kwa mzee mwengine basi alikuwa na uwezo wa kumrudi mtoto yule, na akienda kushitaki kwao, basi mzazi wake atamuongeza kutokana na kosa hilo, lakini leo wapi, mambo yamebadilika, alieleza Maalim Seif huku akitoa historia ya malezi ya zamani. Aidha amesifu juhudi za walimu wa madrasa katika kuwaendeleza watoto kitaaluma, licha ya kukabiliwa na mazingira magumu, na kuwataka walimu hao kujipanga katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa mishahara. Amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi kuthamini mchango wa walimu wa madrasa kwa maendeleo ya watoto wao, na kushajiika kuchangia

Wazazi Zanzibar wahimizwa kusimamia maadili ya watoto


ili kuwawezesha walimu hao kufanya kazi zao vizuri. Akizungumzia kuhusu Umoja wa Wazanzibari Maalim Seif ametoa wito kwa wananchi kushikamana na mafunzo ya dini katika kuendeleza umoja na mshikamano ili kulinda umoja uliopo. Amefahamisha kuwa umoja huo umeijengea heshima kubwa Zanzibar kitaifa na kimataifa, sambamba na kurejesha umoja wa Wazanzibari uliokuwa hatarini kwa kipindi kirefu. Maalim Seif pia alitumia fursa hiyo kuwatanabahisha wananchi juu ya athari za uchafuzi wa mazingira na utumiaji wa dawa za kulevya. Serikali haijazuia uchimbaji wa mchanga lakini imeweka utaratibu maalum na kuruhusu baadhi ya maeneo. Lengo letu ni kulinda mazingira yetu yasiathirike kwa faida zetu wenyewe ikizingatiwa kuwa nchi yetu ni kisiwa na ardhi inapungua kila siku huku idadi ya watu ikiongezeka kila mwaka, alitanabahisha Maalim Seif. Katika risala yao iliyosomwa na ustadh Amour Mgeni, madrasa hiyo yenye wanafunzi wapata 150 imesema imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, ikiwa ni pamoja na kuweza kujenga jengo la madrasa hiyo. Hata hivyo wamesema jengo hilo kwa sasa limekuwa dogo kulingana na idadi ya wanafunzi, na kuwaomba watu wenye uwezo kusaidia upanuzi wa madrasa hiyo, sambamba na kuipatia vikalio na vitendea kazi vya kisasa. Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amevitaka vyombo vya ulinzi nchini kusimamia vyema majukumu yake ili kuhakikisha kuwa bahari na mipaka ya nchi inakuwa salama. Amesema Zanzibar ikiwa nchi ya visiwa, inakabiliwa na changamoto moto nyingi za kiulinzi na usalama kuhakikisha kuwa magaidi hawaingii nchini, sambamba na kukabiliana na vitendo vya uharamia na usafirishaji wa dawa za kulevya. Maalim Seif ameeleza hayo ofisini kwake Migombani alipokuwa na mazungumzo na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali S S Othman. Amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwa ni tishio la vitendo vya kigaidi katika Pembe ya Afrika, jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa ili vitendo hivyo visije kuiathiri Zanzibar. Suala la ulinzi halina mbadala, kitu cha msingi ni kwa vyombo vya ulinzi na dola kushirikiana kuhakikisha kuwa nchi iko salama kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla, alisisitiza Maalim Seif. Kuhusu vitendo vya uharamia vinavyofanywa katika bahari ya hindi, Maalim Seif amesema vinaathiri shughuli za kibiashara na uchumi na vinastahiki kupigwa vita kwa nguvu zote. Kwa upande wake, Mkuu

cha Foreigners Registration Bureau, Bangalore, kutoa kibali kinachohitajika kuwezesha matibabu kufanyika. Wakati huo huo, Waislamu wametakiwa kuwa na subra na kuzidisha Dua kwa Sheikh Ilunga wakati juhudi zikifanyika kuwasiliana na Ubalozi wa India kuhakikisha kuwa anapata matibabu stahiki. Wi t o h u o u m e t o l e w a k u t o k a n a n a Wa i s l a m u wengi kutaka kujua hali yake, wakihoji ni kwanini mpaka sasa Sheikh Ilunga hajawekewa figo wakati mtu wa kutoa sadaka ya go alishapatikana, fedha za matibabu zishalipwa, huku wengine wakitaka kufunga safari kwenda India kumjulia hali. Kutokana na habari zilizotolewa na kiongozi wa kamati inayosimamia matibabu ya Sheikh Ilunga, bado kuna imani kubwa kwamba kupitia kwa Balozi

wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali S S Othman, amesema suala la ulinzi ndio jukumu la msingi kwa vyombo vya ulinzi, na kuahidi kushirikiana na vyombo vya dola na wananchi katika kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi zaidi. Jererali Othman ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Zanzibar, amesifu mashirikiano anayoyapata kutoka kwa viongozi wa nchi na watendaji wengine katika kufanikisha jukumu hilo la kiulinzi. Jererali Othman pia amekutana na Waziri wa Nchi, Osi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Fereji na kubadilishana mawazo juu ya majumu ya osi hiyo. Waziri Fereji amesema katika kukabiliana na majukumu ya osi hiyo, wanahitaji mashirikiano ya karibu na vyombo vya ulinzi katika kukabiliana na na vitendo viovu vikiwemo udhalilishaji wa watu wenye ulemavu, uchafuzi wa mazingira na matumizi ya dawa za kulevya. Amevishauri vyombo vya ulinzi kujiimarisha zaidi ili kuweza kukabiliana na makundi ya kihalifu yakiwemo yale yanayojihusisha na uchimbaji wa mchanga kinyume na utaratibu. Kuhusu UKIMWI, Waziri Fereji amesema licha ya kuwa kiwango cha maambukizi bado ni chini ya asilimia moja, lakini athari kubwa inajitokeza kwa makundi hatarishi likiwemo lile linalojihusisha na biashara haramu ya ukahaba. (Habari kwa hisani ya Hassan Hamad (OMKR)).

4
Na Bakari Mwakangwale
IMEDAIWA kuwa Serikali ndiyo chanzo cha matatizo ya malalamiko dhidi ya Waislamu kutokana na mwenendo wake wa kuwapuuza viongozi wao huku ikiwathamini viongozi wa Kikristo. Hayo yamebainishwa na Ustadhi Mohammed Mwagila, akihutubia Waislamu katika ibada ya swala ya Ijumaa, masjidi Haq, uliopo Buguruni Jijini Dar es Salaam, akizungumzia sakata la Serikali kufuta kinyemela mtihani wa somo la dini. Angalia tatizo la Serikali yetu, kikao cha kuamua suala hilo wamekaa baina ya Serikali na viongozi wa Kikristo, lakini Waislamu wamewekwa kando hata hao Bakwata wanaowatumia mara kwa mara lakini katika hili nao wamewekwa pembeni. Alisema. Ust. Mwagila, alisema kwa hili ni kipimo kingine cha dhulma kwa Waislamu kwani alidai haiwezekani Serikali iamue jambo zito kama hilo liamuliwe na kundi moja katika jamii na lingine liwekwe kando. Alisema, hao walioshirikishwa hawana sifa kisheria za kulifanya kama sehemu ya somo, bali hufundishana kiholela na Serikali inawaruhusu lakini wenye vigezo hivyo Waislamu hawajashirikishwa. Ust. Mwagila, alisema mara kwa mara Serikali imekuwa ikihaha kudai kutatua migogoro ya kidini nchini lakini yenyewe ndiyo inasababisha na kuleta nyufa za migogoro hiyo. Alisema, Serikali inapofanya maamuzi ya jambo zito kama hilo na kundi moja la jamii unategemea nini, kama sio

Wafugaji wa kuku wapewa somo


Na Abdulkarim S. Msengakamba

kuchochea vurugu. Sasa haya yote Serikali inayasimamia yenyewe halafu baadaye inaanza kutafuta mchawi na kudai kuna matatizo baina ya Waislamu na Wakristo, mimi nasema si kweli, tatizo lipo baina ya Serikali na Waislamu na si Wakristo na Waislamu. alisema Ust. Mwagila. A l i s e m a , Wa i s l a m u n a Wakristo ni ndugu kwa muda mrefu, na kudai hata chumvi wanaombana huko mitaani, bali Waislamu wanamadai yao mengi kwa muda mrefu lakini Serikali yao haiwasikilizi. Ama kuhusu huhusu hukumu ya Sheikh Ponda na Waislamu katika kesi hiyo, Ust. Mwagila, alisema pamoja na kuwa hao wapo nje Waislamu watambue kuwa kuna wengine bado wapo ndani ikiwa ni Bara na Visiwani. Pamoja na kuwa sakata la Sheikh Ponda na Mukadam, huku Bara limekwisha, lakini bado Masheik wetu wengine kule Zanzibar wapo ndani mpaka sasa, kwa mwendelezo uleule wa dhulma dhidi ya Waislamu. Tushishangilie tu kwa hili, hapana bado kuna matatizo mengi kina Sheikh Faridi na wenzake bado wapo ndani, vijana kumi wa Kiislamu huku Bara wapo mahabusu, bado tunawajibu mkubwa wa kuwanusuru hawa wenzetu. Alisema Ust. Mwagila. Aidha, alisema baada ya hukumu ya Kesi ya Sheikh Ponda, kuna ya kuzingatia kwamba Mahakama imeweka wazi kuwa Bakwata ni tatizo kwa Waislamu nchini.

Serikali chanzo cha vurugu


Alisema si hivyo tu kwani alidai hata ushahidi ulioletwa Mahakamani haukumridhisha Hakimu aliyedai kama Mhakama ile ingekuwa ya ardhi angelimaza suala hilo, na kuwashauri Waislamu kuwa waende katika Mahakama ya

Makala

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013


na Bakwata, kama ushahidi ulivyobainisha Mahakamani wakati wa kesi ikiendelea. Hivi ni akili gani kutoa heka nne katikati ya Jiji wewe ukapewe ardhi ingine nje ya Jiji, ili hali Bakwata walikuwa na uwezo wa kununua ardhi hiyo kwa kutumia pesa za miradi mbalimbali iliyopo chini yao, na zile ekari nne zikaendelea kubaki. Alisena akionyesha kushangaa Khatibu huyo.

AN-NUUR

ardhi kudai haki yao. Alisema ushauri huo wa hakimu wa Mahakama ya Kisutu, ana imani viongozi wao wataufanyika kazi, na kwamba sasa haitakuwa heka nne tu watadai hekari zote 27, zilizouzwa kinyemela

MWENYEKITI wa The Islamic Foundation Aref Nahdi akipokea hundi ya shillingi milioni tano kutoka Benki ya PBZ Islamic Division, Tawi la Kariako. Aliyekabidhi kwa niaba ya Meneja wa Tawi Attiye Mohamed ni Ndugu Suleiman Ali Suleiman alie na tai. Juma Mmanga katikati ni shuhuda.

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency


Inawatangazia Waislamu wote Kuwa Imeandaa Safari ya Hijja Mwaka 2013 Sawa na Mwaka 1434 Hijria kwa Dola US$ 3550 tu. Umra kwa Mwezi wa Ramadhani itakuwa ni Dola US$ 1995 Fomu zinapatikana katika osi zifuatazo:1. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel 0713 730 444, au 0773 804101 au 0785 930444 na 0773 930444. 2. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel 0777 484982 au 0777 413 987. 3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es salaam 0784 453838 4. Abdallah Salehe Mazrui ( HOKO) Dar es salaam 0715 724 444 5. Salim Is-haq Dar es salaam 0754 286010 au 0774 786101 6. Dukani kwa Abdala Hadh Mazrui wete pemba 0777 482 665 7. Dukani kwa Mohamed Hadh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456911 8. Sheikh Daudi khamis sheha 0777 679692 9. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Wahi kulipia. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930444. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo 0777 484982 au 0777 413 987. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Sheikh Salim Mohamed Salim 0774 412974 au Kupitia A CCOUNT NAMBA 048101000030 NBC Tanbih: Atakae maliza Taratibu zote kuanzia sasa Mpaka 15 July 2013 atapata Punguzo la asilimia 16% atalipia $ Dola 2982 tu. Atakae maliza Taratibu zote kuanzia Tarehe 16-july Hadi Tarehe 15 Augost 2013 atapata Punguzo la Asilimia sita 6% atalipia Dola $3337 tu. Kutakuwa na umra ya utangulizi kabla ya Umra ya Hijja kwa atakae maliza kufanya hivyo. Atakae maliza taratibu zote mwanzo ndie atakae shughulikiwa mwanzo. Ukilipia kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412975. Kumbuka Kikundi cha Ahlul Daawa Kwa Bei nafuu kuliko wote na Huduma bora Kuliko wengi. Nyote mnakaribishwa

WAFUGAJI wa kuku jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani wamehimizwa kujitahidi kutumia vyakula bora na salama kwa mifugo yao ili kupata tija katika ufugaji. Wito huo umetolewa na Dk. Salimu Nassor Mselem, Mkurugenzi wa Farmers Centre katika semina ya ufugaji kuku iliyoandaliwa Kampuni ya Farmers Centre ya Ilala, iliyofanyika katika osi za CCM Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Ufugaji mzuri ni ule unaozingatia ubora wa vyakula pamoja na mabanda ya kufugia. Mabanda hayatakiwi yawe na unyevunyevu na yanatakiwa kufanyiwa usa kwa uhakika na kuua kabisa mazalio ya panya kwa kuziba mashimo yote. Ni muhimu kuchunguzwa

mara kwa mara, ili kuzuia vifaranga kushambuliwa na kuliwa na panya. Alisema. Dk. Mselem alisisitiza umuhimu wa kuwapa kuku vyakula vilivyo na ubora kwa kupimwa na kujua kama vina viwango. Mtaalam huyo alisema wafugaji wanatakiwa kuchanganya vyakula kwa kupondaponda majani ya mchunga na mihogo na kuyaanika, baada ya hapo wayatumie majani hayo kwa kuchanganya na vyakula vingine. Mimi kwanza huyu mwalimu nilikuwa namsikia tu, na kumuona katika vyombo vya habari, leo ndio namuona, kwa kweli namshukuru sana Dk. Mselem amenizindua, nilikuwa sijui mengi juu ya ufugaji wa kuku na vifaranga vyangu vilikuwa vikifa kila mara. Kwa siku hufa sita had nane lakini kufuatia somo la leo nimejifunza mengi namshukuru sana. Alisema mfugaji mmoja wa kuku aliyehudhuria semina hiyo.

5 Urusi yasisitiza kushirikishwa Iran mkutano wa Geneva juu ya Syria

Habari za Kimataifa/Tangazo

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013

AN-NUUR

KATIBU Mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki Moon na Urusi wamekubaliana kwamba mkutano wa amani kuhusu Syria, lazima ufanyike haraka iwezekanavyo hata kama Urusi inapinga shinikizo la dunia kwamba inawapa silaha wanajeshi wa serikali ya Damascus. Aidha Ban amewaambia waandishi wa habari kuwa matarajio ni makubwa na mkutano lazima ufanyike haraka iwezekanavyo ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Bw. Sergei Lavrov, amesisitiza kuwa kufanyika haraka kwa mkutano huo ni bora zaidi. Hata hivyo Lavrov ametahadharisha kuwa jamii ya kimataifa inatakiwa kukubali kuwa Iran ina athari kubwa katika matukio ya Syria na kwamba, inapaswa kushiriki katika mazungumzo ya kutatua mgogoro wa Syria yatakayofanyika Geneva. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran naye amesisitiza kuwa nchi yake ina nafasi yenye athari katika kutatua mgogoro wa Syria na kusisitiza udharura wa kushirikishwa Tehran katika mkutano ujao wa kimataifa kuhusu Syria. Hata hivyo Bw. Lavrov alisema kuwa ni mapema sana kutaja tarehe ya mazungumzo ya Geneva, ambayo kwa sasa yanatarajiwa kufanyika katika nusu ya kwanza ya mwezi wa sita kwa sababu uwasilishwaji halisi wa wajumbe wa Syria bado haujaamuliwa. Mazungumzo haya mapya yanalenga kuwaleta pamoja waasi na wajumbe wa serikali, hatua ambayo ni ngumu ikizingatiwa kwamba baadhi ya wajumbe wa upinzani wamegoma kumtambua Assad kama sehemu ya mazungumzo.

SHIRIKA la Ujasusi la Marekani CIA, limetangaza kuwa, asilimia 75 ya wananchi wa Syria watamchagua Rais Bashar Assad kwenye uchaguzi wa rais utakaofanyika mwaka 2014. Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imeeleza kuwa, kama Rais Assad atajitosa kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa rais hapo mwakani na bila shaka ataibuka mshindi na kuiongoza tena nchi hiyo hadi mwaka 2020. Uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika hilo la kijasusi ndani ya Syria, unaonyesha kuwa Rais Assad bado anaungwa mkono na wananchi wengi wa Taifa hilo. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, machafuko na mapigano yanayoendelea nchini humo yanaonyesha kuimarika zaidi nguvu za kijeshi za nchi hiyo dhidi ya makundi ya kigaidi, na huenda mapigano hayo yakaendelea hadi wakati wa kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo. Nchi za Magharibi na hasa Marekani na Uingereza, pamoja na nchi waitifaki za Saudi Arabia, Qatar na Uturuki zimekuwa mstari

CIA: Wasyria asilimia 75 wanamkubali Rais Assad

Iran yanyonga majasusi wa Marekani, Israel

wa mbele katika kuyapa misaada ya kifedha na kisilaha makundi ya kigaidi

nchini Syria, kwa lengo la kuuangusha utawala huo uliochaguliwa na wananchi.

TEHRAN Iran imetekeleza hukumu ya kunyongwa majasusi wawili waliokuwa wakilifanyia ujasusi Shirika la Kijasusi la Marekani CIA na Shirika la Kijasusi la Israel, Mossad. Majasusi hao walihukumiwa kifo na Mahakama ya Mapinduzi ya mjini Tehran na hukumu yao imetekelezwa alfajiri ya Jumapili iliyopita. Mohammad Heidari, alipatikana na hatia ya kukutana na majasusi wa Israel nje ya Iran kwa mara kadhaa na kuwauzia taarifa za siri kuhusu Jamhuri hiyo ya Kiislamu. Mwingine ni Kourosh Ahmadi, ambaye alikutwa na hatia ya kuwa na mawasiliano na majasusi wa CIA na kuwapa taarifa za siri kuhusu Iran. Iran imekuwa ikiwatia mbaroni majasusi wa Marekani na Israel, ambao baadhi yao wamedaiwa kuwa ni wale waliohusika na vitendo vya mauaji ya kigaidi nchini Iran dhidi ya wanasayansi wa masuala ya nyuklia wa Taifa hilo.

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


NAFASI ZA UALIMU NGAZI YA CHETI 2013/2014
WAISLAMU MNATANGAZIWA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI CHUO CHA UALIMU KIRINJIKO ISLAMIC A. SIFA: Muombaji awe na sifa zifuatazo: (a) Ufaulu wa kidato cha 4 usiopungua alama 27 katika kikao kimoja cha mtihani, asiwe amekaa zaidi ya miaka mitano (5) tangu amalize kidato cha nne. (b) Awe na credits 4 kiwango cha C endapo amekaa mtihani kwa vikao zaidi ya kimoja. (c) Kuhitimu kidato cha 6 ni sifa ya nyongeza. B. MAELEKEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE 1. Fomu ya maombi iambatanishwe na vyeti (leaving and Academic certicates) vya kidato cha 4 pamoja na picha ya hivi karibuni. 2. Tarehe ya usaili na mwisho wa kurudisha fomu imesogezwa mbele hadi tarehe 22/6/2013 saa 2:00 asubuhi kutokana na kufutwa kwa matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa awali. 3. Vituo vya usaili ni hivi vifuatavyo: (a) Kirinjiko Islamic T.C SAME (b) Ubungo Islamic T.C DSM (c) Nyasaka Islamic S.S. Mwanza 4. Kwa wale ambao walisharudisha fomu wanatakiwa wawasilishe result slips za matokeo mapya mapema kwenye osi waliporejesha fomu hizo ili yaunganishwe na fomu zao. 4. Fomu zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu kumi. Soma vituo vinavyopatikana fomu katika ukurasa wa 9 wa Tangazo la Shule za IPC.:

6
HISTORIA ina kawaida ya kujirudia. Ally Sykes mmoja wa waasisi wa TANU, mmoja wa wale watu wasiozidi takriban saba waliokuwa katika kamati ya ndani ya TAA iliyounda TANU, mmoja wa wafadhili wakuu wa TANU, mmoja wa askari na hapa nalitumia neno askari kwa maana yake halisi kwa kuwa ni Ally Syke ndiye TAA hadi TANU ikimtegemea kwa kutekeleza mambo ya hatari dhidi ya Waingereza, amefariki dunia. Ally Sykes ndiye alikuwa akipewa kazi za hatari za kumwaga sumu na upupu dhidi ya serikali. Sumu na upupu huu yalikuwa makaratasi aliyokuwa akichapa nyumbani kwake usiku makaratasi ambayo Wa i n g e r e z a w a l i y a i t a makaratasi ya uchochezi. Waingereza na makachero wake walikuwa wanamjua Ally Sykes vizuri. Waingereza walikuwa wakijua kuwa alikuwa na medali ya mlenga shabaha bingwa aliyopata Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Huyu ndiye Ally Sykes mzalendo muasisi wa TANU ambae sahihi yake ndiyo iko katika kadi ya TANU ya Baba wa Taifa, amefariki Nairobi Jumapili iliyopita alikokwenda kwa ajili ya matibabu. Siku ile ile ya Jumapili milango ya mchana mchanga kabisa kabla ya Adhuhur, taarifa ikawasili Dar es Salaam kuwa Ally Sykes amefariki dunia. Ghaa mji wa Dar es Salaam alikozaliwa na akaendesha harakati zake dhidi ya ukoloni wa Waingereza ukagubikwa na simanzi. Kila simu iliyokuwa ikipokelewa na wengi ilikuwa ni kutaka kuthibitisha kifo kile. Binafsi simu zikaanza kumiminika kwangu za kunipa pole. Hadi kuka jioni habari zikawa zimeenea mji mzima kuwa ni kweli Ally Sykes hayuko tena duniani. Haukupita muda siku ile ile maiti ya Ally Sykes ikawasili Dar es Salaam kwa ndege ya kukodi ikiwa imesindikizwa na mkewe Bi Zainab na baadhi ya wanae wakiongozwa na mtoto wake wa kwanza wa kiume Abraham Sykes. Siku ya pili Jumatatu magazeti yote yalikuwa yametoka yakiwa hayana taarifa yoyote ya kifo cha Ally Sykes. Hii iliwashangaza watu wengi sana isipokuwa mimi. Sikushangaa kwa kuwa nilikuwa najua siasa za historia inayomzunguka Ally Sykes kwa miaka mingi hususan kuhusu mchango wake binafsi na wa kaka yake marehemu Abdulwahid Sykes

MAKALA

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013


kwa jasho, damu na fedha zake, magazeti haya yalipuuza kifo hicho. Kuna watu katika TANU katika kipindi kile walikuwa wanajaribu kuifuta historia ya kupigania uhuru wakitaka kuondoa mchango wa Abdulwahid na Ally Sykes katika historia ya uhuru. Hata hivyo Tanganyika Standard gazeti ambalo ndilo liliokuwa likilinda maslahi ya ukoloni Tanganyika, ndilo lililoandika taazia ya Abdulwahid Sykes. Mhariri wa Tanganyika Standard Brendon Grimshaw hakuweza kustahamili fedheha ile, aliandika taazia ambayo itaishi zaidi ya miaka miaka mia moja na zaidi. Taazia ile ilitikisa kra Makao Mkuu ya TANU Mtaa wa Lumumba na ikawakera wengi. Grimshaw alisema katika taazia yake kuwa TANU imeundwa pakubwa kwa mchango wa ukoo wa Sykes. Narudia tena. Historia ina kawaida ya kujirudia. Mwaka wa 1968 wakati Abdulwahid anafariki Waislamu walikuwa wako katika taharuki kubwa ya kile kilichokujajulikana kama mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) taharuki iliyojaa simanzi kwa kuwa Mufti wa wakati ule Sheikh Hassan bin Amir mmoja wa masheikh viongozi katika TANU alikuwa kakamatwa na kufukuzwa nchini kwa amri ya Nyerere. Wakati haya yakijiri, Tewa Said Tewa na Bi. Titi Mohamed viongozi wa juu wa EAMWS walikuwa wakiandamwa na Nyerere na hapakuwa na uelewano mzuri baina yao. Ajabu ni kuwa umauti umemkuta Ally Sykes katika hali kama ile ile iliyokuwapo wakati kaka yake alipofariki dunia mwaka 1968 wakati nchi ikiwa katika mgogoro wa EAMWS kishindo ambacho kilidumu takriban miezi mitatu. Ally Sykes kafa wakati nchi ipo katika taharuki kwa kile kinachodaiwa uadui baiana ya Waislamu na Wakristo. Kwa hiki kifo cha Ally Sykes bila shaka wahariri wa magazeti walikuwa wameshughulishwa katika kutafuta habari mpya za k u c h o m w a m a k a n i s a na ugomvi wa kuchinja, hawakuwa na muda wa kufuatilia msiba wa muasisi wa TANU marehemu Ally Sykes. Lakini iweje hali iwe kama vile miaka saba tu baada ya uhuru kupatikana nchi iingie na taharuki ya kiasi kile na hivi sasa taharuki ile ijirejee upya tena ikishuhudiwa na waasisi wa harakati za ukombozi? Ilikuwa nimemaliza kuandika kitabu kuhusu Inaendelea Uk. 8

AN-NUUR

Ally Kleist Sykes-1926 2013


Mzalendo Muasisi wa TANU Aliamwandikia Kukabidhi Julius Nyerere Kadi ya TANU Na. 1
hakuwa akipungua nyumbani kwa Mama Abdu Bi Mrurguru binti Mussa Mtaa wa Kirk. Halikadhalika Maria Nyerere hakuwa akipungua nyumbani kwa aidha kwa Bi Zainab mkewe Ally Sykes Mtaa wa Kipata au kwa Bi Mwamvua mkewe Abdulwahid Sykes Mtaa wa Aggrey. Wakati huu Abdulwahid ndiye akiwa rais wa TAA na harakati za kuanzisha TANU zimepamba moto achilia mbali hila na tna za Waingereza kuwatokomeza viongozi shupavu wa TAA kama Hamza Mwapachu, Dk. Vedast Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi nje ya Dar es Salaam kukivunja nguvu chama. Ndiyo maana TANU ilipokuja asisiwa mwaka 1954 Ally Sykes kadi yake ya TANU ikawa namba 2, Nyerere namba 1, Abdulwahid Sykes kadi yake namba 3, Dossa Aziz kadi namba 4, John Rupia kadi yake namba 7. Historia hii haikuja bure ina maelezo marefu ambayo hapa hayataweza kuenea. Kipindi hiki Ally Sykes alikuwa Katibu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA) na vilevile alikuwa mwakilishi wa chama hicho katika Kamati ya Uajiri ya Serikali (Government Establishment Committee). Thomas Marealle ndiye alikuwa rais wa TAGSA na Rashid Kawawa alikuwa mwanakamati. Wanasiasa hawa vijana Ally Sykes akiwa mmoja wao wenyewe walijipa jina, Wednesday Tea Club wakikutana kila siku ya Jumatano kunywa chai pamoja na kutumia wakati ule kupanga mikakati ya kuwangoa Waingereza katika ardhi ya Tanganyika. Kupitia Ally, Abdulwahid na Dossa Aziz; Nyerere akaweza kujuana na wenyeji wa Dar es Salaam maarufu katika hao ni Sheikh Hassan bin Amir, Mshume Kiyate, Jumbe Tambaza, Sheikh Suleiman Takadir, Clement Mtamila, Bi. Titi Mohamed, Tatu biti Mzee na wengineo. Lakini historia ina kawaida ya kujirudia. Kifo cha Ally Sykes kimepuuzwa na vyombo vya habari kama nilivyoeleza awali kuwa hata kifo cha kaka yake Abdulwahid Sykes alipofariki mwaka 1968 magazeti ya TANU (wakati ule The Nationalist na Uhuru) chama alichokiasisi

AL-MARHUUM Ally Sykes katika harakati za kuasisi Waislamu wa Tanganyika) na TANU na kudai uhuru wa kupitia jumuia hii akajenga Tanganyika. shule ya kwanza ya Kiislamu Historia ina kawaida ya Dar es Salaam, shule ambayo kijurudia. Haya ya kupuuza ilisomesha Quran pamoja kifo cha Ally Sykes yalimkuta na masomo ya kisekula. Hii pia kaka yake Abdulwahid Al Jamiatul Islamiyya ndiyo alipofariki mwaka 1968. iliyotoa viongozi wa kwanza Ally Sykes alikuwa mtu kuiendesha TAA na baadae maarufu kupita kiasi. Alikuwa TANU katika harakati za kwanza ana umaarufu wa kudai uhuru. Ally Sykes kuzaliwa. Kazaliwa Dar es kwa mazingira na makuzi Salaam Gerezani, mtoto wa haya akawa maarufu kama mjini. Kisha alikuwa maarufu alivyokuwa baba yake. kwa nasaba. Baba yake Lakini kubwa zaidi na hili Kleist Sykes alikuwa mmoja ndilo kwa bahati mbaya wa watu mashuhuri katika ndilo linalojulikana zaidi kwa siasa zote za Dar es Salaam sasa ni utajiri ambao Allah katika miaka ya mwanzo alimruzuku toka akiwa kijana ya 1900 hadi alipofariki mdogo sana katika miaka ya mwaka 1949. Baba yake 1950 alipoanza biashara kwa alikuwa maarufu kwa kuwa kuanzisha kampuni yake alilelewa na Affande Plantan binafsi iliyoitwa Sykes Sales askari kiongozi katika jeshi Promotion Consultancy. la Wajerumani lilokuja Inajulikana na wengi Tanganyika na Herman Von Ally Sykes na kaka yake Wissman wakati Wajerumani Abdulwahid Sykes ndiyo w a l i p o i n g i a k u i t a w a l a watu wa mwanzo kumpokea Tanganyika. Kleist alikuwa Julius Nyerere alipokuja ndiye katibu muasisi wa Dar es Salaam mwaka 1952. African Association mwaka Nyerere alika nyumbani kwa 1929 chama kilichokuja akina Sykes kwa utambulisho baadae kujibadili na kuwa na hii ilijenga uraki ambao TANU Ally Sykes akiwa ulipitiliza na kuwa udugu mmoja wa hao waasisi. mkubwa wa mapenzi ya dhati Baba yake Kleist aliasisi si baina yao tu bali hata kwa Al Jamiatul Islamiyya Fi wake na mama zao. Mama Tanganyika (Umoja wa yake Nyerere Bi Mugaya

Tangazo

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013

AN-NUUR

Makala

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013

AN-NUUR

Inatoka Uk. 6

Ally Kleist Sykes-1926 2013


Cameron, Mwalimu Thomas Plantan na ndugu zake Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Plantan, Mwalimu Mdachi Shariff, Mwalimu Nicodemus Ubwe, Kassela Bantu, John Rupia, Hamza Kibwana Mwapachu, Othman Chande, Leonard Bakuname, Stephen Mhando, Oscar Kambona, Peter Colmore, Albert Rothschild, A l i M w i n y i Ta m b w e , Alexander Thobias, Japhet Kirilo, Joseph Kimalando, Ian Smith, Roy Welensky, Jim Bailey, Kenneth Kaunda, M e i d a S p r i n g e r, J o h n Hatch, Gretton Bailey, Brig. Scupham, Dome Okochi Budohi, Annur Kassum, Nesmo Eliufoo, Yusuf Olotu, Joseph Kimalando, Julius Nyerere na wengine wengi wakubwa kwa nyadhifa walizokuja kukamata katika Tanganyika huru na wale walioanguka njiani. Ukikaa na Ally Sykes na mkapitia jina moja baada ya jingine utapata habari za wazalendo na watu hawa na historia yao yote na kwa hakika hiyo ndiyo historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya kweli ya TANU. Ally Sykes alikuwa anawajua watu hawa vilivyo. Atakuambia yupi alikuwa kibaraka wa Waingereza na yupi alikuwa mpiganaji wa kweli. Atakueleza nani alikuja katika siasa kwa uzalendo na nani alikuja kwa ajili ya kutafuta maslahi yake binafsi. Ally Sykes kabla hajafa alikuwa keshamaliza kuandika historia ya maisha yake. Mswada huu unaitwa, Under the Shadow of British Colonialism in Tanganyika. Mchapaji alipomaliza kuhariri mswada ule aliomba kitabu kibadilishwe jina kiitwe, D r e a m s U n f u l f i l l e d . Mhariri alinipigia simu kutoka Nairobi akanambia kila akimsoma Ally Sykes alikuwa anamwona Ally Sykes katika majonzi kwa kuwa ndoto aliyokuwanayo wakati akipigania uhuru wa Tanganyika ndoto ile haikukamilika. Aliniomba nimuombe Ally Sykes jina la kitabu libadilishwe. Kwake Ally Sykes suala halikuwa kugawana vyeo ndani ya chama cha siasa na kisha katika Tanganyika huru. Suala lilikuwa kwa Mwafrika kuwa huru katika nchi yake bila ya kubughudhiwa na mtu yeyote yule. Mwaka 1953 ilikuja shinikizo kubwa kutoka kwa Ivor Bayldon kuunda chama kitakachojumuisha

maisha ya kaka yakeAlly Sykes kitabu kilichokujajulikana kama The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 1968) The Untod Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika. Ally Sykes alinikabidhi nyaraka zake katika utati wa maisha ya Abdulwahid Sykes. Nyaraka hizi mpaka Ally Sykes anakufa zilibaki kuwa sehemu ya malalamiko yangu kwake kuwa hazikustahili kuwa mikononi kwake na kazifungia katika safe zake. Nilikuwa nikimwambia mara kadhaa inagawa hakutaka kunisikiliza kuwa nyaraka hizi ni mali ya taifa la Tanzania lazima azikabidhi serikalini kwa kuhifadhiwa na kuwekwa Tanzania National Archive (TNA) kama urithi wa kizazi kijacho. Yeye siku zote akinambia, Mohamed hizi nyaraka ninaogopa nikiwapa serikali watazichoma moto. Alikuwa na sababu ya kusema vile. Nyaraka za Ally Sykes zinakwenda nyuma kiasi cha miaka mia moja kuanzia siku babu yake Sykes Mbuwane alipotia mguu katika ardhi ya Tanganyika kutoka meli ya kvitia ya Wajerumani pale Pangani akitokea Msumbiji. Nyaraka zile zina barua za wanasiasa wa mwanzo katika Tanganyika achilia mbali habari za baba yake. Ukianza kufunua majalada yale hutachoka kupekua karatasi baada ya karatasi. Nyingine zimechoka kwa umri mrefu. Katika majalada yale utakutana na wazalendo na machifu, utakutana na wanasiasa wenye asili ya Kiasia na Waingereza wenyewe waliokuwa watawala. Nyaraka zile utawaona na utawasikia watu hawa wakizungumza na wewe: Dk Joseph Mutahangarwa, Chief Abdieli Shangali wa Machame, Paramount Chief Thomas Marealle wa Marangu, Chief Adam Sapi Mkwawa wa Wahehe, Chief Harun Msabila Lugusha, Dk. Wilbard Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dk Vedas Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K. Viran, Stephen Mhando, Dossa Aziz, Ivor Bayldon, Yustino Mponda, Ivor Bayldon, Rashid Mfaume Kawawa, Bhoke Munanka, Rashid Kheri Baghdelleh, Robert Makange, Saadani Abdu Kandoro, Malkia Elizabeth, Chief Secretary Bruce Hutt, Gavana Edward Twining, Gavana Ronald

wananchi wa rangi zote katika Tanganyika. Ally Sykes alikuwa akisema laiti kama wangekubali kumeza chambo kile historia ya Tanganyika ingekuwa nyingine na TANU isingeliasisiwa pale New Street mwaka 1954 katika nyumba ile ambayo ilijengwa na kukamilika mwaka 1933 wakati wa uongozi wa baba yake; na Nyerere asingelikuja kuwa kiongozi wa nchi hii. Laiti Bwana Abdu na Hamza Mwapachu wangelikubaliana na ule mpango wa akina Ivor Bayldon na Nazerali uongozi wa nchi huu ungelitoka ndani ya Baraza la Kutunga Sheria la wakoloni, usingelitoka k w e t u s i s i Wa a f r i k a wazalendo wenye uchungu na nchi hii na huenda rais wa Tanganyika angelikuwa Chief David Kidaha Makwaia na Nyerere angelibakia kuwa mwalimu wa shule pale Pugu. Ivor Bayldon baada ya kushindwa kuwapata wanachama wa TAA alikuja baadae mwaka 1955 kuunda United Tanganyika Party (UTP) chama kilichokuja kupinga TANU. Hii ndiyo namna nyaraka za Ally Sykes zinavyozungumza na wewe unapozisoma na pale yeye mwenyewe anapokupa maelezo hutaacha kupigwa na butwaa na mshangao. Nilipata kumuuliza Ally Sykes kama anajua ni fedha kiasi gani alizopata kutumia k a t i k a TA A n a TA N U jibu alonipa ni kuwa hajui wala hajuti. Hizo fedha si kitu kikubwa. Kubwa ni njama ambayo niliundiwa na Waingereza wawili Dk Hughes na Dk Frank kutaka kuniua wakati nikifanya kazi Kibongoto Infectious Disease Hospital, Moshi. Unajua Waingereza kwa kweli walikuwa wamechoka na hili jina letu. Kila Gavana aliyekuja kutawala Tanganyika alikuwa lazima atapambana na jina hili. Baba yetu aliitwa kuhojiwa na kila gavana aliyekuja kutawala Tanganyika kuanzia mwaka 1927 hadi 1947. Kati ya mwaka 1929 hadi 1947 Mzee Kleist aliitwa kuhojiwa mbele ya tribune mara tatu kuhusu harakati za wafanyakazi, yeye akiwa katibu wa Railway African Civil Service Union. Waingereza walikuwa wamechoka sasa na sisi wakaamua kuniua kwa kuniambukiza kifua kikuu (TB). Hawa madaktari wawili walikuwa wakiniita mimi raki yake Nyerere ambaye kwao wao alikuwa adui mkubwa sana. Wakati

AL-MARHUUM Ally Sykes ule kunasibishwa na Nyerere halikuwa jambo jema. Hicho kilikuwa kitu cha hatari na cha kutisha sana. Mimi sikuwa nakataa kuwa Nyerere alikuwa rafiki yangu. Kwa Waingereza hiyo ilikuwa kama vile kujinasibisha udugu na Adolf Hitler. Hii ilikuwa mwaka 1956 na ingawa mimi nilikuwa nimepewa uhamisho kufanyakazi Kibongoto, Moshi ili kuniweka mbali na TANU pale New Street bado nilikuwa nikijitahidi kukijenga chama pale nilipokuwapo. Mimi na Bwana Abdu, Dossa, Mzee Rupia, Nyerere na Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir tulikuwa tukiitumikia TANU kwa nguzu zetu zote na ni wakati huu ndipo nilipompiga muuguzaji wa kike Mzungu Ocean Road Hospital kwa ajili ya ubaguzi wake na matokeo yake nikasimamishwa kazi na niliporejeshwa nikapelekwa uhamishomi Mtwara kama adhabu Mtu usingeweza kuchoka kumsikiliza Ally Sykes anapohadithia historia ya mapambano dhidi ya ukoloni. Ilipokuwa sasa inakaribia kupatikana kwa uhuru anasema, Allah akanifungulia milango zaidi kwa kuwa sasa nikishirikiana na raki yangu Peter Colmore na kampuni yake ya High Fidelity Productions kutoka Nairobi tukawa tumeshika biashara yote kubwa ya uwakilishi wa makampuni makubwa yaliyokuwa Afrika ya Mashariki - Coca Cola (East Africa) Ltd; The Cooper Motors Corporation Ltd; The Shell Company of East Africa Ltd, Aspro Nicholas Ltd; Gailey and Roberts Ltd; Bata Shoes Company Ltd; Kenya Broadcasting Service, Cotton Lint and Seed Marketing Board, Raleigh Industries of East Africa Ltd; na tulikuwa wawakilishi Kenya wa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) lakini mafanikio yana matatizo yake hii nilikujajua baadae sana uhuru ulipopatikana. Sisi tuliokuwa mstari wa mbele tukawa hatuhitajiki tena na husda na tna ikaingia baina yetu sisi waasisi wa TANU na Nyerere Haikuwa rahisi kuacha kumsikiliza Ally Sykes akiieleza historia ya TANU, uhusiano wake na Nyerere na yote yaliyotokea hadi akafutwa kabisa katika historia ya uhuru wa Tanganyika,. Hatuwezi kummaliza Ally Sykes. Ally Sykes Inaendelea Uk. 11

Makala

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013

AN-NUUR

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


NAFASI ZA KIDATO CHA TANO 2013/2014
1. 2. 3. 4. 5. 6.

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, Combinations za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA. Muombaji awe na Crediti 3 au zaidi na angalau D ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana F au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano. Kwa wale ambao walisharudisha fomu wanatakiwa wawasilishe result slips za matokeo mapya mapema kwenye osi waliporejesha fomu hizo ili yaunganishwe na fomu zao. Waombaji wapya wenye sifa wanashauriwa kuendelea kuchukua fomu.Tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu itatangazwa baadaye. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
Arusha Kilimanjaro Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA. - 0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin 0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel 0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU 0715 681701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole 0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627

Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Dar es SalaamMorogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -

6. Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha.

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

Wabillah Tawiq MKURUGENZI

Kampeni za kumchafua Ponda zilivyoshindwa!


Na Said Rajab
MAHATMA Ghandi, baba wa taifa la India, alipata kusema: Uongo hauwezi kuwa ukweli kwa sababu ya kuupigia debe sana, wala ukweli hauwezi kuwa uongo kwa sababu hakuna anayeuona. Leo ningependa, japo kwa uchache, kumzungumzia Sheikh Ponda Issa Ponda, kama mfano wa kuigwa katika kupigania haki zinazoporwa za Waislamu wa Tanzania na kusukuma ajenda muhimu za Waislamu hapa nchini. Kwanza niwatanabaishe wasomaji wangu, miye sikumfahamu Sheikh Ponda kupitia vyombo vya habari. Namfahamu kwa karibu sana na tumeshawahi kufanyakazi za Kiislamu pamoja mara nyingi tu. Kuna jambo moja kuhusu Sheikh Ponda, nataka kulizungumza kwa dhati kabisa ya moyo wangu. Bila ya kuongeza chumvi, na namuomba Mwenyezi Mungu aniepushe na hilo, Sheikh Ponda Issa Ponda ni wa pekee sana katika mapambano ya kudai haki. Ni mtu mwenye sifa zote za kiongozi aliyekamilika.Yuko tayari kujitoa muhanga kwa maslahi ya wengi. Anaongoza kwa kuonyesha mfano badala ya kuagiza tu, na kamwe hasalimi amri kwa sababu ya woga au kunusuru shingo yake. Sheikh Ponda ni mkweli, muadilifu, muaminifu, muungwana, anamwogopa Mwenyezi Mungu, ana msimamo usioyumba katika dini, ana ufahamu mkubwa kuhusu masuala ya kitaifa na kimataifa, na zaidi ya yote, Ponda mkikubaliana kufanya jambo mnafanya! Hata siku moja hawezi kukuzunguka, kukugeuka, kukuhadaa wala kukutapeli. Mimi namfahamu Sheikh Ponda hivyo, na naamini bado hajabadilika. Kusema ukweli kabisa, Sheikh Ponda ni mtu mwenye tabia njema sana! Sifa zake hizi zimemfanya awe kipenzi cha Waislamu wa Tanzania. Matatizo yanayompata Ponda, kwa sababu ya msimamo wake usioyumba wa kupinga dhulma dhidi ya Waislamu, umemfanya awe shujaa wa Waislamu Tanzania. Sheikh Ponda, mara zote amekuwa mstari wa mbele katika kusukuma ajenda zinazowagusa Waislamu kama jamii. Nakumbuka uchaguzi mkuu uliopita, Maaskofu walitoa ilani yao ya uchaguzi, kwa jina la waraka, wakiwaelekeza waumini wao cha kufanya katika uchaguzi huo. Sheikh Ponda alikuwa miongoni mwa viongozi walioandaa muongozo wa Waislamu katika uchaguzi huo, ili kukabili waraka uliotolewa na maaskofu. Kiroja kilichotokea, baadhi ya Waislamu, wakiwemo masheikh, wakaanza kuushambulia muongozo ulioandaliwa na Waislamu na wakaacha waraka wa maaskofu! Kwao, ni rahisi zaidi kuuponda muongozo wa Waislamu wenzao kuliko waraka wa maaskofu. Katika uchaguzi ule, walikuwa pamoja na maaskofu katika ajenda yao. Katika suala la Sensa, ajenda ya Waislamu, baada ya kukaa Shura zao kadhaa, ilikuwa kususia zoezi hilo, iwapo kipengele cha dini hakitaingizwa kwenye dodoso za Sensa. Sheikh Ponda alikuwa mstari wa mbele kuwaunganisha Waislamu katika ajenda hii. Waislamu walikuwa na sababu za msingi sana kususia Sensa! Lakini, kama ilivyo ada, tuliona pia masheikh maslahi wakiwashambulia Waislamu waliogomea sensa, huku wakipotosha kwa makusudi sababu hasa zilizowafanya Waislamu wagome kuhesabiwa. Masheikh hawa, vigeu vigeu, mara zote wamekuwa silaha kali ya maadui dhidi ya Waislamu wenzao. Ndiyo maana hawana mvuto kama Sheikh Ponda mbele ya jamii ya Waislamu, ingawa wanatamani kupata heshima kama anayopata Ponda. Pia katika dhulma iliyofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) dhidi ya wanafunzi Waislamu katika somo la Maarifa ya Uislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alikuwa mstari wa mbele kupigania haki za wanafunzi Waislamu. Ponda aliongoza mapambano hayo, na Waislamu walikuwa tayari kuandamana kuelekea ofisi za (NECTA) kutoa kilio chao na mabomu ya machozi yalipigwa. Waislamu wamelalamikia sana mchezo mchafu unaofanyika NECTA. Lakini, cha ajabu, baadhi ya wenzetu, walikuwa wakipinga ukweli huu kwa sababu ya maslahi binafsi kutoka NECTA. Waliendesha propaganda za kuisafisha (NECTA), kwa kuwaumiza Waislamu wenzao. Sheikh Ponda hawezi kufanya ujinga kama huo hata kidogo! Tofauti yao na Ponda iko hapo. Na wao wenyewe wanajua hivyo, na ndiyo maana wanamchukia. Wa m e k u w a w a k i m z u s h i a uongo na Propaganda chafu ili kumvunjia heshima mbele ya jamii. Sasa NECTA imeboronga matokeo ya mwaka jana, mpaka Serikali imeamua kuyafuta na kuagiza yaandaliwe upya! Je? madai ya Waislamu kuhusu madudu yanayofanyika NECTA yalikuwa kweli au uongo? Mbona kimya kuhusu agizo la serikali NECTA? Mmeona ukweli wa madai ya Waislam? Hebu tuangalie hili la Kiwanja cha Waislamu Markaz Changombe, ambacho Bakwata wamekiuza kinyemela kwa kampuni ya Agritanza, bila ya ridhaa ya Waislamu. Baada ya jambo hili kufahamika kwa Waislamu, Sheikh Ponda, kama kawaida yake, aliona ni jukumu lake kufuatilia haki hii iliyoporwa ya Waislamu. Mara tu Sheikh Ponda na wenzake walipoanza kupigania haki hii kwa njia za kiungwana, propaganda chafu zikaanza kwenye vyombo vya habari. Mara Ponda mchochezi, Ponda anavuruga amani, Sheikh gani yule?, Bwana Maandamano, Mwanaharakati gani yule?, Ponda siyo k i o n g o z i w a Wa i s l a m u , Hana elimu, Mwizi na majina mengi ya kipuuzi kama hayo. Lakini ukweli siku zote utabaki ukweli. Haitatokea duniani uongo ukafuta ukweli, bali ukweli ndiyo unaofuta uongo. Propaganda zote hizo zilikuwa na lengo na kuficha uovu uliofanyika kiwanja cha Changombe Markaz, kama ilivyokuwa kwa uovu uliofanyika NECTA na suala la Sensa. Vy o m b o v y a H a b a r i vikachora picha ya kutisha ya Sheikh Ponda kama ni mtu hatari sana kwa amani na usalama wa nchi. Ponda alikuwa akiletwa Mahakamani kwa ulinzi mkali wa polisi wenye silaha, wakisaidiwa na mbwa, farasi na magari ya maji ya upupu, huku akiwa amefungwa pingu. Vyombo vya Habari vingine vikaanza kumuhukumu kabla hata ya Mahakama, vikizingatia zaidi hisia za chuki binafsi na propaganda badala ya ukweli. Lakini baada ya Dua nyingi z a Wa i s l a m u , M a h a k a m a ikabaini ukweli ulivyo. Ikaona uhalali wa madai ya akina Ponda (Waislamu), hata wakaamua kuvamia kiwanja kile, ingawa utaratibu huo haukuwa sahihi. Ikamuachia huru Ponda na wenzake na kuwashauri Waislamu kudai kiwanja hicho kupitia Mahakama ya Ardhi. Wapiga propaganda dhidi ya Ponda wakaumbuka! Sasa nani mchochezi hapo, Sheikh Ponda au wao? Nani anayevuruga amani, wapiga propaganda au anayedai haki? Nani mwanaharakati wa haki za Waislamu, yule anayejicha chumbani au anayejitokeza hadharani kuandamana? Nani kiongozi wa Waislamu, Sheikh Ponda anayeombewa Dua na Waislamu, au wale wanaolaaniwa na Waislamu? Hapa mwizi Ponda, au yule anayeuza mali za Waislamu kinyemela? Mwenye elimu ni yule anayeangalia tu Waislamu wakiporwa haki zao, au Ponda aliyejitoa muhanga kupigania haki hizo? Propaganda chafu ni moja ya njia mbaya zinazotumiwa na watu waoga, wasio waaminifu na waliokosa maadili, ambao maslahi yao binafsi yameguswa au kuharibiwa, na sasa wana uchungu na hasira dhidi ya wale wanaohisi wamevuruga maslahi yao. Nao wanataka kuwaumiza kihisia, kama walivyoumia wao. Kwa watu wasiomuogopa Mwenyezi Mungu, propaganda chafu hutumika kuwachafua wengine ili wasipendeze mbele

10

Makala/Tangazo

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013

AN-NUUR

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto)


ya jamii, hata kama hawana kosa. Ndani ya Quran, Mwenyezi Mungu amebanisha kwamba Mitume wake wote na wema waliotangulia, ambao walizitaka jamii zao kuishi kwa maadili mema ya kumcha Mungu, walishutumiwa kwa uchochezi, uongo, wizi, majivuno, uzinifu na mambo mengine mabaya. Maisha ya Nabii Yusuph (as), Mussa, Suleiman na hata Muhammad (saw) yamejaa propaganda chafu za watu wabaya dhidi yao. Vile vile, Maryamu (as), mama yake Nabii Issa, Aisha (as) mke wa Mtume wetu, wakiwemo masahaba, pia walichafuliwa kwa propaganda za waovu. Kwa hiyo siyo jambo jipya, na Mwenyezi Mungu amewatahadharisha Waislamu waadilifu: Mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu na mtasikia udhia mwingi kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na kwa wale walioshirikisha. Na kama mkisubiri na kujilinda na anayokataza Mwenyezi Mungu, (mtakuwa mmefanya jambo zuri) Qur(3:186). Kwa hiyo tunajifunza jambo moja la msingi kutokana na propaganda hizi chafu wanazorushiwa kina Sheikh Ponda na Waislamu wengine wanaopigania haki za Waislamu. Kwamba, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kila mipango miovu iliyopangwa dhidi ya waumini hawa itaanguka, na kila propaganda chafu dhidi yao itaruka patupu. Kila propaganda waliyopanga itawarudia wenyewe! Itawafanya wajute hapa duniani na kesho Akhera, labda watubu mbele ya Mwenyezi Mungu toba ya kweli. Mwenyezi Mungu amebainisha hatima inayowasubiri wale waliowachafua Mitume wake na waja wema kwa propaganda chafu: Wa l e w a n a o w a u d h i Wa n a u m e Wa i s l a m u n a Wanawake Waislamu pasipo wao kufanya kosa lolote, bila shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilizo dhahiri Qur(33:58:

Unawatangazia Muhadhara. Siku: Ijumaa 24/05/2013 baada ya swala ya Ijumaa. Jumamosi 25/05/2013 Muda: Saa 3:30 asubuhi (Kwa wanawake tu) Muhadhiri: Sheikh Abdulrahman Bakar Mhina - Imamu Mtambani. Wabillah Tawiq

Masjid Mtambani

11
Na Said Rajab
SHAMBULIO la bomu katika Kanisa Katoliki, Parokia mpya ya Olasiti jijini Arusha, lililosababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine kadhaa, limewashitua Watanzania wengi na kuwajaza hofu kubwa kuhusu tishio la ugaidi hapa nchini. Shambulio kama hilo katika jiji la Boston, Massachusetts nchini Marekani, ambalo limepoteza maisha ya watu watatu na kujeruhi wengine 171, kwa walio wengi ni uthibitisho wa mapambano ya mataifa ya magharibi, kutokomeza wale wanaofanya vitendo hivyo duniani. Kufuatia mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani na jinsi yalivyotangazwa sana, wimbi la hofu likaufunika ulimwengu mzima, ambapo watu wakaaminishwa kwamba mashambulizi zaidi ya kigaidi, yatatokea maeneo mengine tofauti duniani. Vita ya ulimwengu dhidi ya ugaidi ikatangazwa, lengo likiwa kuwasaka magaidi na wale wanaowahifadhi. Muongo mmoja umepita sasa tangu mashambulizi ya Septemba 11. Watu wengi katika nchi za Magharibi wanachukulia tishio la mashambulizi ya kigaidi katika nchi zao kwa umakini mkubwa, kama vile ilivyokuwa tishio la kutokea mashambulizi ya kinyuklia wakati wa vita baridi. Kuna propaganda nyingi sana kuzunguka suala hili la ugaidi na kuliweka katika mtazamo wake sahihi kwa kweli ni muhimu. Kwa sababu kila mtu anaongea lake, wanasiasa, wanahabari, wanaharakati, wasomi, viongozi wa dini na watu wa kawaida. Matokeo yake tunapoteza focus ya jambo lenyewe. Ugaidi, matumizi ya vitisho au vurugu ni mbinu tu inayotumiwa na watu, makundi na hata serikali, na imekuwepo katika kipindi chote cha historia. Ugaidi haukuanzia Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani. Historia inaonyesha ugaidi au vurugu, siyo mbinu inayotumiwa na watu wa kundi fulani tu, au dini fulani peke yake, au watu wenye mrengo fulani wa kisiasa. Kwa mujibu wa historia, mbinu hii imetumika kuanzia zama za kale, mpaka sasa ili kukidhi malengo fulani. Wakati katika muongo uliopita, Osama bin Laden, Al Qaeda, Ayman al - Zawahir na Taleban,

wamekuwa wakilaumiwa sana kwa mashambulizi ya kigaidi, uhalisia ni kwamba ugaidi ni tishio dogo mno kwa watu wengi popote walipo duniani, hususan Marekani. Ripoti ya Utafiti ya START (Study of Terrorism and Responses to Terrorism) inayoitwa 9/11, Ten Years Later, imebainisha kwamba, ukiondoa matukio ya Septemba 11, pungufu ya watu 500 wamekufa kutokana na mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani, kati ya mwaka 1970 na 2010. Tangu Septemba 11 mwaka 2001, jumla ya raia 238 wa Marekani wamekufa kutokana na mashambulizi ya kigaidi. Na kwa mujibu wa Tume ya Usalama wa Bidhaa za Watumiaji nchini humo, Wamarekani wa kawaida wako hatarini zaidi kupondwa na Televisheni au Fenicha na kupoteza maisha, kuliko walivyo hatarini kuuawa na gaidi. Kusema ukweli, mtazamo wa Serikali ya Marekani, hauko katika uwiano sahihi, kuhusu kitu gani kinachoua Wamarekani wengi zaidi. Tumeshuhudia muongo mmoja uliopita, Marekani ikisambaza nguvu zake za kijeshi ulimwenguni kote, huku ikiimarisha usalama wa nyumbani na ikitunga sheria za ajabu za kupambana na tatizo dogo la ugaidi. Wamarekani wengi zaidi wanakufa kwa ajali za gari kila mwaka, wengine wanazama kwenye mabafu (bathtub), wengine wanafia kwenye majengo yaliyoshika moto, na wengine kupigwa radi, kuliko wale wanaokufa kwa mashambulizi ya kigaidi. Lakini vyombo vya habari, hususan televisheni zinazorusha matangazo yake masaa 24, ikiwemo habari zinazowekwa kwenyea mitandao ya kijamii, ndizo zinazokuza tishio hili dogo mpaka likaonekana janga. Angalia jinsi habari za bomu la Arusha zilivyoandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari! Ikajengwa katika akili za watu kana kwamba, makanisa yote hapa Tanzania yanawindwa na magaidi. Na Serikali lazima iyawekee ulinzi! Sasa hata ikitokea pancha ya baiskeli kanisani itaitwa bomu, watu watataharuki, mashuhuda watapatikana, habari

Ugaidi katika mtazamo sahihi


zitaandikwa, tena zikiungwa mkono na Tahariri na watu watakamatwa na kuhojiwa polisi! Ushindani huu wa soko la habari duniani, umeleta uandishi mbaya wa habari na sintofahamu, ambayo imelikuza mno tatizo la ugaidi kuliko lilivyo. Hadithi tamu za kusisimua kuhusu ugaidi zimewafanya watazamaji, wasomaji na wasikilizaji wa vyombo vya habari, kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na propaganda hii, ikijenga katika akili zao kwamba ugaidi ni tishio kubwa, ingawa uhalisia wake hauko hivyo! Siku ya Septemba 11 mwaka 2001, mamilioni ya watu nchini Marekani na duniani kote waliangalia Live wakati jengo la World Trade Centre likishuka chini kwa kishindo, huku watu wakiruka kutoka ghorofa ya 114, wakijaribu kujiokoa na moto mkali. Kuangalia mfululizo wa matukio haya, katika mazingira halisi imewatisha watu wengi sana. Mashambulizi ya kisanii kama haya, huwa hayaondoki kwenye kra za watu daima. Hofu ya ugaidi yanayojengwa, inaweza hata kudumaza umakini wa watu katika kushughulikia majanga asilia, ambayo mengi yao ni makubwa zaidi ukiyapima kuliko ugaidi. Kwa mfano, na siyo lengo langu kudharau vifo hapa, zaidi ya watu 227,000 walipoteza maisha mwaka 2004 katika janga la tsunami lililotokea bahari ya Hindi, ikilinganishwa na watu 3000 waliopoteza maisha kwenye tukio la septemba 11 nchini Marekani. Lakini cha ajabu, mashambulizi ya septemba 11 yamejenga hofu kubwa duniani na kuleta athari ambayo imeitikisa dunia nzima kuliko matukio mazito ya maafa yaliyowahi kutokea duniani. Pamoja na hili, sekta ya burudani nchini Marekani, kupitia lamu na maigizo, imelichukua suala la ugaidi na kuzidi kujenga imani potofu kwa watu duniani kuhusu ugaidi. Filamu nyingi kama hizo, zimebeba maudhui inayosisitiza kwamba Waislamu ndiyo wanaohusika na ugaidi na wanashambulia shabaha za Magharibi. Lakini ukirudi kwenye ukweli, takwimu za jarida la Europol zinaonyesha kwamba kati ya mwaka 2006 mpaka

Makala/Tangazo

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013


69 wanakufa kila saa moja linalopita kutokana na magonjwa ya moyo, wakati Wamarekani 66 wanakufa kila saa moja linaloenda kutokana na saratani. Ukiuweka ugaidi katika mtazamo wake halisi, kusema ukweli, ni tishio dogo mno kwa uhai wa binadamu, isipokuwa limekuzwa kupita kiasi na watu wenye ajenda zao. Miye sikutaka kuandika yote hayo, kwa sababu naamini wafuatiliaji makini wa siasa za ulimwengu wanayajua. Mara kwa mara gazeti hili limekuwa likiandika masuala hayo kwa kina. Lakini sasa yametokea kwetu Arusha, na watu wamesema sana kwa mapito tofauti. Kuna haja ya kukumbushana na kuwekana sawa kimtazamo, kuhusu tafsiri sahihi ya matukio haya. Rais Jakaya Kikwete amesema wiki iliyopita kule Dodoma katika sherehe za kusimikwa Askofu wa Kanisa la Anglikana kwamba matukio haya ya uvunjifu wa amani yana mkono wa nje. Yuko sahihi kabisa. Lakini mimi wasiwasi wangu ni ile nje ya Rais Kikwete maana yake wapi? Ulimwengu wa Magharibi au ulimwengu wa Waislamu? Kwa sababu watu wamejazwa hofu duniani kote, kwamba matukio kama hayo yakitokea, basi washukiwa lazima wawe Waislamu, kama tulivyoona Arusha ambapo wamekamatwa Waarabu wasiohusika, lakini hakuna Mzungu hata mmoja aliyekamatwa, kwa sababu vyombo vya usalama vinadhani Mzungu hauwezi kuhusika na ugaidi.

AN-NUUR

2008, asilimia 99.6 ya shughuli zote za kigaidi barani Ulaya zilifanywa na wasio Waislamu. Na rekodi rasmi za FBI zinaonyesha kwamba asilimia 94 ya mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani, kuanzia mwaka 1980 mpaka 2005, pia yalifanywa na wasio Waislamu. Hakuna shaka kwamba Marekani inahitaji kizingizio ili iweze kutanua zaidi ushawishi wake duniani kote katika karne hii ya 21. Mabeberu wa Marekani wanahitaji kizingizio ili kuhalalisha uwepo wa majeshi yao katika nchi tofauti duniani, lengo likiwa kusukuma mbele ajenda ya Marekani kupora rasilimali za dunia. Kabla hata vumbi la Septemba 11 halijatulia, mashambulizi hayo yakawa kizingizio cha kuzivamia Afghanistan na Iraq. Ugaidi na tishio la ugaidi vimetumika kuhalalisha ubabe wa Marekani duniani kote, na itabaki kuwa ni kwa maslahi ya Marekani kuendeleza hofu hii. Hisia hii ya hofu imetumika kama kizingizio cha kuendesha uchunguzi dhidi ya baadhi ya raia wa Marekani, ikiwa ni pamoja na kufanya mashambulizi ya drones katika nchi za Waislamu. Marekani ina matatizo mengi ya ndani, ambayo yanapoteza maelfu ya maisha ya Wamarekani, na matatizo hayo siyo ugaidi. Mauaji ya mtu mmoja hutokea nchini humo kila dakika 36 zinapopita. Wamarekani

FAIR LAND DISTRIBUTION


NAFASI ZA KAZI Inawatangazia nafasi ya kazi upande wa wauzaji (Salesman) Sifa za muombaji Awe kijana wa kitanzania Awe na umri kati ya miaka 25-45 Awe tayari kuweka dhamana ya mali isiyohamishika Awe na wadhamini watatu ( 3) wenye ajira zinazotambulika kiserikali Awe na elimu siyochini ya kidato cha nne Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu katika fani hiyo. MAWASILIANO Zaidi: Piga Simu: 0789 272 737 Maombi yote yatumwe katika mtandano. Email: fairlandcom@yahoo.com Au kwa Barua S.L.P 4804- DSM MAOMBI YAAMBATANISHWE NA PASSPORT SIZE.

Inatoka Uk. 8 aliishi maisha kamili. Allah alimruzuku kila kitu na akampa dunia. Mguu wake ulikanyaga pale alipotaka. Mimi binafsi nimeshuhudia nguvu zake kwa macho yangu mwenyewe. Wazungu wakimtetemekea na akiwatuma kazi na wakimtumikia kwa adabu na unyofu wa hali ya juu. Mmoja wa jamaa za Ally Sykes, Mzee Ahmed Rashad Ali alipata kunambia kuwa Ally Sykes akiwatuma Wazungu toka ujana wake na anapowaita kuja kula nyumbani kwake wakija na adabu zao kamili. Juu ya haya yote Ally Sykes alikuwa na ibra moja hakuwa mtu wa kujiona. Hukuweza kupima nguvu na uwezo wake kwa kumtazama. Nilisikitika sana mazikoni pale Makaburi ya Kisutu. Wale waliompuuza Ally Sykes na kuufanya mchango wake si lolote si chochote ndiyo walipewa heshima ya wao kuwa mbele pale makaburini katika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho na kusoma hotuba. Raki zake aliokuwa nao siku zote, Abdallah Awadh, Ali Mbarak, Shomari, Abdu Faraj, Boi Juma Risasi, Harudiki Kabunju, Hussein, Abdu Kifea, Abdallah Jabir, Muharram Kocha, Muharram

Ally Kleist Sykes-1926 2013


Mkamba, Abdubari, Salim Hirizi kuwataja wachache waliwekwa mbali na jeneza na kaburi na watu wa Itifaki wa Ikulu nafasi yao ikachukuliwa na wanasiasa na viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ilikuwa aibu kubwa kwa CCM kuonekana hawapo katika kumzika Ally Sykes mwanachama wa TANU kadi namba mbili na mzalendo wa kweli aliyemwandikia na kumkabidhi kadi namba moja ya TANU Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ally Sykes alimpenda na kumuheshimu sana kaka yake na katika maisha yangu ndiyo mtu pekee niliyemsikia kila akimtaja kaka yake anatanguliza neno, Bwana. Kwake yeye Abdulwahid alikuwa Bwana Abdu kila alipomtaja. Ally Sykes amezikwa pembeni mwa kaburi la kaka yake Bwana Abdu. Kwa kifo cha Ally Sykes, hakika nguzo ya watu wa Dar es Salaam imeanguka. Tuamwomba Allah amlaze Ally Kleist Sykes mahali pema peponi. (Taanzia hii imeandikwa na Mohamed Said, 0717 474 954 22 Mei 2013)

12

AN-NUUR
MAKALA

MAULID!!! MAULID!!! Masjid Allah Karim Kazimzumbwi Kisarawe Inawaalika waislamu wote katika Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) Kazimzumbwi Kisarawe, Tarehe 25/05/2013, siku ya Jumamosi Saa 2:30 Baada ya Swalatul Ishaa , Inshaalah. Wafadhili wa maulidi Hii ni. 1. Sheikh Juma Sadiki Muyenga 2. Mohamed Rak Nurmohamed Satya 3. Ndugu wa Familia ya Madenge
Nyote Mnakaribishwa

12

RAJAB 1434, IJUMAA MEI 24 - 30, 2013

Na Shaban Rajab

MHANDISI wa Kiingereza, ambaye alisilimu takriban miaka 22 iliyopita, Sheikh Omar Kirwood, amestaajabu mandhari adhimu ya Wilaya ya Maa, jambo lililomlazimu kuwaeleza Waislamu wa eneo hilo kuwa kamwe wasije kufanya makosa wakawauzia wageni ardhi yao. Kwa kweli nimetembea, lakini hapa nimeona kisiwa chenu ni almasi, shikilieni ardhi yenu, msithubutu kuuza ardhi yenu kwa wageni, mkaja juta muda si mrefu, alisema Sheikh Kirwood kwa Kiingereza na kutafsiriwa kwa Kiswahili. Sheikh Kirwood, alifika Mafia pamoja na masheikh wengine kutoka sehemu mbalimbali nchini, kuhudhuria hadhara ya maulid inayofanyika kila mwaka Mafia, ambayo pamoja na mambo mengine, hutumika kuhamasisha maendeleo ya Waislamu wilayani humo. Safari hii, hadhara hiyo ilianzia katika kisiwa cha Jibondo, kisiwa maarufu kwa hifadhi kubwa ya samaki katika ukanda wa bahari ya Hindi. Majira ya asubuhi ya Mei 18 msafara wa Waislamu ulipokelewa na wenyeji wao Waislamu wa Jibondo ambako yalifanyika Maulid kuanzia saa 3:00 katika Madrasat Munawara iliyo chini ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Jibondo hadi 8:00 mchana. Baada ya kumaliza Maulidi, Umma wa Waislamu wa Maa na Kilwa walipanda mashua na kurejea Maa na kuendelea na Maulidi katika Msikiti Mkuu wa Wilaya ya Maa Markaz Masjid Kabyr, Kilindoni Maa. Pamoja na sherehe za Maulid hayo yaliyojumuisha Madrasa 17 za vitongoji vya Maa, yalifanyika pia mashindano ya kuhifadhi Quran, yaliyosimamiwa na Majaji kutoka Dar es Salaam ambapo washindi walikabidhiwa zawadi zao. Baadae Masheikh kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, walitoa mhadhara kwa Waislamu. Hadhara hiyo ilihutubiwa

Ardhi Maa ni almasi msiuze - Sheikh Omar


Azimio kujenga Markazi ya kisasa lakiwa

Madaktari bingwa kutoka Kuwait watua Muhimbili


Na Mwandishi Wetu MADAKTARI 22 kutoka Kuwait wametua nchini kutoa huduma za upasuaji katika hospitali ya Taifa Muhimbili. Madaktari hao wamekuja nchini kwa uratibu wa taasisi ya Africa Muslims Agency ya jijini, ambapo wamenza kutoa huduma za upasuaji hospitali ya Muhimbili na katika zahanati ya Africa Muslims Agency Tabata kwa siku tano kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Akizingumza na Annuur Muhimbili Jumatatu wakati wa kukaribishwa madaktari hao, Mkuu wa Idara ya Daawa katika taasisi ya Africa Muslims Agency, Mbwana Urari, alisema Madaktari hao wamekuja nchini kufuatia ziara aliyoifanya Rais Jakaya Kikwete nchini Kuwait hivi
ambao wamekuja Tanzania kufanya operesheni kwa kushirikiana na hospitali ya Taifa Muhimbili. Alisema, madaktari hao wakiongozwa na Dk. Hisham Abu Rizk, ni bing wa wa

Sheikh Omar Kirwood (kulia) na Sheikh Othman Maalim (katikati) wakiwa na mwenyeji wao Katibu Mtendaji wa Markaz Kabyr, Sheikh Shuaib Salum Aboud mjini Maa. (Picha na Juma Hussein Ngido)

na Maalim Ally Basaleh, Sheikh Othman Maalim, Sheikh Mahmud Nurdin, Umar Kirwood kutoka Uingereza na wengine. Ni katika muda huo Markaz Masjid Kabyr ilibainisha mpango wake wa kujenga Markazi ya Kisasa ikiwa ni pamoja na Msikiti wa ghorofa tatu ambao utakuwa na shule, English/Arabic Medium, madrasa, ofisi na kituo cha teknolojia ya habari (Information and computer centre). Ta y a r i s e r i k a l i y a Saudia imeahidi kufadhili mpango huo na Waislamu wa Maa ambapo Sheikh Umar Kirwood ambaye ni mhandisi wa ujenzi, amekamilisha michoro ya jengo hilo la kisasa la kituo hicho. Ilielezwa katika hadhara hiyo kuwa Madrasa nyingi za Maa zinakabiliwa na upungufu wa vitabu vya Misahafu na Juzuu. Kufuatia hali hiyo, Sheikh Othman Maalim aliahidi kuzipatia Madrasa hizo misahafu 1000, huku Katibu Mtendaji wa Markaz Kabyr Sheikh Shuaib Salum Aboud akiahidi kutafuta vitabu zaidi.

karibuni ambako ndio makuu ya taasisi hiyo. Alisema, Rais Kikwete alipokuwa nchini humo, aliahidiwa misaada mbalimbali kwa Tanzania na moja ya misaada hiyo ni kuwasili kwa madaktari bingwa wa upasuaji wapatao 14 na madaktari wengine sita,

upasuaji wa magonjwa ya watoto, upasuaji wa macho, koo, sikio na Pua, upasuaji wa kawaida (general surgery) wataalam wa dawa za usingizi na uuguzi ambapo wameanza kazi yao Mei 20 na watakia tamati Mei 25. Aidha madaktari hao pamoja na kuwa Muhimbili, pia wataendelea na kutoa huduma ya macho katika

zahanati ya Africa Muslim Agency iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, huduma ambayo nayo itakuwa ya siku tano. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Marina Njelekela, alisema wamepokea kwa mikono miwili ujio wa madaktari hao na kwamba kuwasili kwao kutasaidia huduma ya upasuaji hospitalini hapo. Alisema madaktari hao wapo katika makundi manne, wanaofanya upasuaji kwa watoto, upasuaji wa kawaida, upasuaji wa pua na koo, masikio
na upasuaji wa macho. H o s p i t a l i y a Ta i f a Muhimbili tunawashukuru sana kwa ujio wao kwasababu kuna wagonjwa wengi wanaosubiri upasuaji kutokana na idadi ndogo ya madaktari t ulio

nao. Tumefunga baadhi ya vyumba kwa ajili ya kuwapa

nafasi madaktari hawa kufanya upasuaji. Alisema Mkurugenzi huyo. Aliongeza kuwa madaktari hao watafanya upasuaji wa wagonjwa 150 katika hizo siku tano watakapokuwa hapa nchini tangu Jumatatu hadi Ijumaa ambapo Jumamosi wataondoka kurudi Kuwait. Dk. Njelekela alisema kuwa wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ni wale ambao wapo katika kliniki na wanakuja katika hospitali ya Taifa kwa ajili ya mahitaji ya upasuaji. Naye Kaimu Daktari Bingwa wa Upasuaji Muhimbili, Bw. Laurence Rwanyuma, alisema kuwasili kwa madakri hao kutatoa fursa kwa madaktari wa hospitali hiyo kubadilishana utaalam na maarifa na wataongeza huduma ya upasuaji kwa wagonjwa.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

También podría gustarte