Está en la página 1de 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Ponda mgonjwa, mzima!


ISSN 0856 - 3861 Na. 1050 MUHARRAM 1434, IJUMAA DES. 21 - 27, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kipya Uk. 8

Taarifa za Wakili, Magereza zagongana Jaji Warioba:

Kwa nini Muungano wa mkataba iwe nongwa?

Kukataa kudhulumiwa ni Ibada Mohammed


Uk. 2 Hili ndilo wanalofanya Waislamu Kama ni kuvunja amani inafanya serikali Iache ukandamizaji, dhulma za mkoloni

SHEIKH Ponda Issa Ponda

Karume, Maalim vinara wa amani


Uk. 6
MAKAMO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

NAPENDA kuwauliza viongozi wa serikali, CCM na wale wa Tume ya Jaji Warioba: kwa nini wakitajiwa neno muungano wa mkataba kwenye maoni na wananchi wa Zanzibar huwa wanahamaki ? Mbona baadhi yao ndio walioshabikia na kuongoza harakati za Sudan ya Kusini kujitenga na Sudan? Kule si mlidai kuwa ni haki yao kujiamulia wanavyotaka! Mbona sasa hamtaki Wazanzibari kujiamulia wanavyotaka? (Soma Uk. 9)

Mbona mlishabikia Sudan Kusini kujitenga?

Jaji Joseph Sinde Warioba.

RAIS mstaafu wa Serikali ya Mapindizu Zanzibar (SMZ), Dkt. Amani Abeid Karume.

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari
AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012

AN-NUUR

MAONI YETU

TAKRIBAN kipindi cha miezi miwili sasa, kumekuwa na tatizo kubwa la kukatika katika umeme nchini hususan katika jiji la Dar es Salaama. Katika maeneo mengi ya jiji, umeme umekuwa ukikatika kwa siku nzima na wakati mwingine usiku na mchana. Imekuwa ni bahati kupita siku, kwa maana ya kutwa nzima au usiku na mchana bila kupatikana hitilafu ya kukatika umeme katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Wakati hali ya umeme ikiwa mbaya kipindi hiki, Watanzania wanaikumbuka kauli aliyowahi kuitoa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete. Mara baada ya kukaa kwa muda osini, aliwahakikishia Watanzania kwamba, safari hii Taifa halitaingia katika zoezi la mgawo wa umeme kama ilivyokuwa siku za nyuma. Alisema kuwa hata kama mvua hazitanyesha, hilo haliwezi kuathiri uzalishaji wa umeme nchini kwa kuwa hivi sasa, shirika la Usambazaji Umeme nchini halitegemei tena umeme wa kuzalishwa kwa nguvu za maji. Aliwahakikishia Watanzania kuwa kutakuwa na umeme wa uhakika unaotokana na gesi ukisaidiwa na ule unaozalishwa kwa nishati ya mafuta. K a u l i h i y o y a Wa z i r i Muhongo, iliwapa imani na faraja kubwa Watanzania, kwamba sasa wameondokana na ile adha ya miaka mingi ya mgawo wa umeme, hali ambayo imekuwa ikiwaadhiri sana kihuduma na kiuchumi na katika zao shughuli mbalimbali. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, tumeshuhudia ile adha ya kukatikakatika umeme ikirejea tena kwa kasi ya ajabu. Awali Osi ya Mawasiliano TANESCO walielezwa kuwa, umeme umekuwa ukikatika kutokana na utaratibu wa kawaida wa kusafisha na kukarabati mitambo wa kuzalisha gesi ya kampuni ya Pan African Energy, kule Mtwara. Kampuni hiyo husambaza gesi ya kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO. Tukaambiwa kwamba zoezi la kufanya usa na kukarabati mtambo huo, ni la kawida tu na si kwamba kuna hitilafu

Watanzania wajulishwe kuwepo mgawo wa umeme usio rasmi

yeyote. Taarifa za wasemaji hao zilibainisha kuwa usa na ukarabati huo utakapokamilika, basi huduma ya umeme itarejea katika hali yake ya kawaida. Baadae tatizo la kukatikakatika umeme likajitokeza kwa mara nyingine hata baada ya usa na ukarabati. Safari hii tukaambiwa kuwa kulikuwa na hitilafu iliyojitokeza katika mtambo huo wa gesi wa Pan African, lakini marekebisho yanafanyika na huduma ya umeme itarejea kama kawaida mara tu baada ya kurekebishwa hitilafu hiyo. Baada ya kiasi cha muda kupita tangu hitilafu hizo kujitokeza, sasa tumerejeshwa tena kwenye adha ile ile ya kukatikakatika umeme. Imekuwa ni muhali kupita siku bila kukatika umeme. Hata hivyo haijafahamika kwa yakini tatizo safari hii ni nini. Tunahoji, iko wapi tofauti ya adha ya mgawo rasmi wa umeme wa siku za nyuma na mgawo huu tulio nao usio rasmi wa sasa? Tunadhani kuwa, si vibaya kuwatangazia Watanzania kuwepo mgawo rasmi wa umeme nchini hivi sasa, ili wapate kufahamu na kujiandaa kukabiliana na hali hiyo na mapema, kuliko kupigia kimya mgawo huu wa kimya kimya. Aidha hatudhani kwamba katika kipindi hiki cha kukatika hovyo umeme, ni muafaka kwa TANESCO kututangazia nia yao ya kutaka kuongeza bei ya umeme. Watanzania kwa muda mrefu wamekuwa wavumilivu huku wakiteswa kwa kubebeshwa ongezeko la mara kwa mara la bei ya umeme, lakini huduma yenyewe ikiendelea kuwa duni. Kimantiki, kumuongezea mwananchi mzigo wa bili sio mwarobaini wa kutatua matatizo ya kiuendeashaji TANESCO. Hatalaumiwa Prof. Muhongo, kwa kuwa bado ana kazi ngumu ya kuisasha TANESCO, ili kuwa shirika kamili la kuzalisha umeme wa uhakika nchini, badala ya kuwa shamba la bibi la vigogo kwa muda mrefu sasa. Watanzania wamechoshwa na porojo na taaraifa za mara kwa mara za kukatika umeme ambazo hazina tija kwao zaidi ya kuzuia hasira zao. Wanachotaka ni umeme wa uhakika.

Na Bakari Mwakangwale ametuambia katika Qur an kwamba msidhulumu na S E R I K A L I i m e t a k i w a wala msikubali kudhulumiwa kuyapatia ufumbuzi madai kukataa kudhulumiwa kwetu ya Waislamu nchini, ili sisi ni ibada. Alisema Shkh. kuleta usawa miongoni Mohammed Said. Alisema, Mwenyezi Mungu mwa wanajamii badala ya kuendeleza dhulma dhidi yao hataki kudhulumu na kwamba kama walivyofanya wakoloni ukidhulumu unajihatarisha kabla ya Tanganyika kupata wewe mwenyewe, na hii ni hatari huku akitolea mfano Uhuru. Wito huo umetolewa na wa machafuko ya Rwanda m w a n a h i s t o r i a m a a r u f u na Burundi, kwamba vinara nchini Sheikh Mohammed wa dhulma nchini dhidi ya Said akiongea na Waislamu Waislamu wajiulize nchi hizo katika ukumbi wa Sabasaba nini kilichowakisha pale. A l i s e m a , Wa i s l a m u Jijini Dar es Salaam, walikuwa na mategemeo wakiadhimisha na kutathimini hali ya Waislamu katika miaka makubwa baada ya kupata 51, ya Uhuru mwishoni mwa Uhuru, kwani walikuwa mstari wa mbele kupambana wiki iliyopita. Mohammed Said alisema, na Muingereza, mpaka pale p a m o j a n a Wa z e e w a walipo hakikisha anafungasha Kiislamu kuwa na shauku virago na kuondoka, huku y a k u j i l e t e a m a e n d e l e o wakiwa na malengo yao katika hususani katika suala la Tanganyika huru. Alisema, hali hiyo elimu, katika Tanganyika huru waliyoipigania, lakini ilijidhihirisha muda mfupi Rais wa awamu ya kwanza b a a d a y a U h u r u k w a n i Julius Nyerere, aliwasaliti h a w a k u c h e l e w a m n a m o kisha kuiuwa Jumuiya ya mwaka 1962, waliitisha Waislamu ya Afrika Mashariki mkutano wa Taasisi zote za na kuwaundia Bakwata, Kiislamu nchini, wakiwa na ambayo inawasumbua mpaka agenda moja tu ya kusomesha watoto wao. hivi sasa. Waislamu walikuwa na Alisema, takribani ni miaka mategemeo makubwa sana 50 sasa, ile hofu aliyokuwa nayo Mzee Bilali Waikela, kuwa baada ya Uhuru wao, mwaka moto wa Waislamu utakuja 1962, Sheikh Hassan Bin kuwaka, leo yanatokea kwani Amir, alisimama akasema Waislamu wameanza kukataa Uhuru ndio huu tumeupigania kuwa daraja la pili na kujaribu tumeupata, lakini ili Uhuru kudai haki zao mara kwa mara huu uwe na maana lazima sisi tusomeshe watoto, kwani wanazodhulumiwa. Alisema, Serikali ingekuwa Waingereza walitudhulumu inatumia akili ingerekebisha k a t i k a e l i m u . A l i s e m a hali hii mapema, lakini Mohammed Said, akinukuu inarejea na kutumia mbinu maneno ya Shkh. Hassan Bin z i l e z i l e w a l i z o t u m i a Amer. Alisema, lengo la kuweka wakoloni kuwabagua na mikakati hiyo ya kielimu kuwakandamiza Waislamu, n a k i l a w a n a p o j a r i b u ilikuwa waje wapatikane kuweka wazi dhuluma dhidi viongozi wa nchi ambao yao huambiwa wanaleta w a t a o n g o z a n c h i k w a kuchanganyikana na ndugu chokochoko za kidini. A l i s e m a , Wa i s l a m u zao Wakristo, wito ambao w a n a t a k a k u f a n y a alikuwa akiutoa Shikh. Hassan m a a n d a m a n o k u p i n g a Bin Amir, kila alimopita d h u l m a k a t i k a B a r a z a nchini kote. Aliwatanabahisha la Mitihani, wanatishwa kuwa watashushiwa jeshi Waislamu akisema, Mfumo liwashughulikie, juu na chini Kristo si mgeni bali mfumo huu ili kuwaziba midomo, akaasa umeanza kazi zamani kabla ya kwamba endapo dhulma hii Uhuru chini ya wakoloni na haitokomeshwa nchi itaingia baada ya Uhuru chini ya Mwl. katika janga la matatizo Nyerere, ambaye alisimamia mambo mawili, kuwanyima makubwa. Wa i s l a m u t u n a s e m a Waislamu elimu na kuizika hatuna chokochoko, bali historia halisi ya Waislamu tunaitanabaisha Serikali katika kupigania Uhuru wa kuwa mnatudhulumu, na Tanganyika. Alisema, Julius Nyerere sisi (Waislamu) Allah (s.w)

Kukataa kudhulumiwa ni Ibada Mohammed

hakupenda wala kufurahia kuona Waislamu kusoma, (Rais wa Kwanza wa Tanganyika) hakuupenda, kwani alidai zilianza chokochoko, kupitia kwake (Nyerere), akitumia vyombo vya dola, ambavyo alikabidhiwa na wananchi ili atawale kwa haki na usawa. Alisema, mwaka 1963, Waislamu waliitisha mkutano ambao ulikuwa ni moja kati ya mikutano mikali iliyowahi kupata kutokea, ambao athari zake mpaka sasa zinaonekana. Alisema, mjumbe mmoja k u t o k a m k o a n i Ta b o r a , aliyemtaja kwa majina ya Bw. Bilali Rehani Waikela, aliyekuwa katibu wa EAMWS, jimbo la Magharibi, akija Jijini katika mkutano huo, mara tu baada ya kushuka katika stesheni ya Dar es Salaam, alipokewa na Waislamu na kumueleza kuwa anaitwa na Shikh. Hassan Bin Amir. Anasimulia Mohammed Said, kwamba Bw. Waikela, alikwenda moja kwa moja kuonana na Shkh. Amir, kama kuitikia wito ambapo (Waikela) alielezwa kwamba Nyerere, anataka kuivunja J u m u i y a y a Wa i s l a m u (EAMWS). Wa i k e l a , a l i p o s h u k a Stesheni, alipokewa na Waislamu, wakamueleza unaitwa na Sheikh (Hassan Bin Amir). Alipoka Shkh. Hassan, akamwambia, Rehani Bilali Waikela, nimekuita hapa, Nyerere (Julius) anataka kuivunja East Africa Muslim Welfare Society, taarifa zimenikia. Alisema Mohammed Said, akinukuu maongezi ya Wazee hao. Akifafanua zaidi kisa hicho Mohammed Said, alisema Sheikh Amir, aliendelea kumweka wazi mjumbe huyo kutoka Jimbo la Magharibi kwamba, ili kuiuwa Jumuiya hiyo ya Waislamu, Nyerere, anawatumia miongoni mwao ndani ya Jumuiya hiyo. Sheikh Mohammed Said, alisema katika kikao hicho cha wawili hao, Shkh. Hassan Bin Amir, alimweleza Bw. Rehani Waikela, kwamba Nyerere, anawatumia wenzao hao kuleta chokochoko ili kuvunja Jumuiya hiyo (EAMWS) kisha awaundie Waislamu Jumuiya nyingine ambayo itakuwa na Waafrika

Inaendelea Uk. 3

Ponda mgonjwa, mzima!


Na Bakari Mwakangwale

Habari

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012

AN-NUUR

HALI ya afya ya Sheikh Ponda Issa Ponda, imegubikwa na utata kufuatia taarifa za Serikali kudai kuwa ni mgonjwa huku baadhi ya jamaa zake wakidai kuwa ni mzima na hawana taarifa za kuugua kwake. Sheikh Ponda, pamoja na watuhumiwa wengine wanakabiliwa na mashitaka kadhaa huku dhamana zao zikiwa zimezuiliwa na DPP, na kuendelea kusota mahabusu katika Gereza la Segerea Jijini Dar es Salaam, mpaka sasa. Serikali kupitia kwa wakili wake, Tumaini Kweka, aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, Desemba 18 mwaka huu kwamba, Sheikh Ponda, alishindwa kuka Mahakamani hapo kwa kuwa ni mgonjwa. Wakili Kweka baada ya kutoa taarifa hizo, ambazo hata Wakili wa Sheikh Ponda na wenzake amedai zimewashtua, aliiomba Mahakama kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine ya kusikilizwa. Kutokana na taarifa hizo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Victoria Nongwa alilazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 31 mwaka huu. An uur ilipohojiana na Wakili wa Sheikh Ponda, Bw. Juma Nassoro, alisema alikuwa anafahamu kuwa Ponda alikuwa na homa ya kawaida lakini hakuwa na taarifa za kuugua kwa mteja wake hadi kushindwa kuka Mahakamani, na kwamba taarifa hizo amezisikia akiwa Mahakamani hapo. Alikuwa ana homa zaidi hatujui ila juzi Jumapili iliyopita) aliagiza chandarua na taarifa nilizonazo ni kuwa uongozi wa Magereza ulikataa kuipokea, wakidai kuwa hakuna utaratibu huo Magerezani. Sasa sina taarifa za kuzidiwa hadi kushindwa kufika Mahakamani leo (Jumanne). Alisema Wakili Nassoro. Wakili Nassoro alisema huwa ana utaratibu wa kwenda kuongea naye kabla ya kesi, lakini safari hii hakuweza kufanya

hivyo kutokana na kuwa na majukumu mengine na hakuwa na shaka na afya yake. Hiyo ndiyo taarifa rasmi ya Serikali, Sheikh (Ponda) anaumwa sisi tuchukulie hivyo, lakini taarifa zingine zinasema haumwi, taarifa hii hata mimi imenistua sana, siku chache za nyuma nilimuona akiwa ni mzima wa afya nikitegemea kuwa leo (Jumanne) atakuja, lakini hakutokea, nitakwenda kumuona. Alisema. Ustadhi Mohammed Ayoub, ambaye alionana na Sheikh Ponda, siku moja kabla ya kwenda Mahakamani, alipohojiwa na An nuur juu ya taarifa hizo za kuugua na kushindwa kufika Mahakamani, alisema hata yeye taarifa hizo zimemstua. Alisema, yeye alionana na Sheikh Ponda siku ya Jumatatu wiki hii, na hakuona kama alikuwa na hali ya kuumwa na kushindwa kufika Mahakamani, lakini alidai lolote linaweza kutokea kwani siku moja inaweza kubadilisha afya ya mtu. Alisema, anaweza akahisi hali ya mtu kama ni mgonjwa, lakini pia alidai Sheikh Ponda hakumueleza kama ni mgonjwa kiasi hicho, zaidi ya kuulizana hali za kawaida na kuongea kisha tuliagana naye akiwa na matumaini ya kwenda kesho yake Mahakamani. Nilimpelekea chakula, Jumatatu alikuwa yupo vizuri tu, kutoka selo alikuja mwenyewe anatembea na kupokea chakula tena aliniambia anahitaji kanzu ingine kwa ajili ya kwenda Mahakamani Jumanne, hizi taarifa za kuumwa kama zilivyoripotiwa sina hakika nazo. Alisema Ustadh Mohammed. Kwa upande wa mke wa Sheikh Ponda, Mama Mariyam, alisema ilimlazimu kwenda kuonana na mumewe siku ya Jumatano wiki hii, kufuatia taarifa za kuripotiwa kuumwa kwake siku ya Jumatatu Mahakanai na Jumanne, kupitia vyombo vya habari, lakini alimkuta akiwa na afya njema, licha ya kuwa mgonjwa. Sheikh yupo katika dozi,

na anaendelea na dozi, zaidi ni malaria ya kawaida tu, si kama ilivyokuzwa hivyo na vyombo vya habari maana nimeweza kuongea naye, angekuwa hoi sidhani kama angeliweza kutoka na kuonana naye. Alisema Mama Mariyam. Taarifa zaidi kutoka ndani ya gereza hilo la Segerea, zilisema Sheikh Ponda ni mzima, kwani alikuwa ni mmoja wa mahabusu aliyeweza kushiriki kutoa maoni ya mchakato wa Katiba mpya, baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kuwatembelea mahabusu na wafungwa katika Gereza hilo wiki hii kupata maoni yao, ambapo yeye (Ponda) alipewa muda mrefu wa kuchangia, tofauti na wengine.

Kukataa kudhulumiwa ni Ibada Mohammed


Inatoka Uk. 2
katika maadhimisho hayo, kushika maneno mawili katika risala hiyo kwamba Waikela, alimkumbusha Nyerere (Rais) kama Mkristo, kuwa alielewa f i k a k w a m b a Wa i s l a m u hawakusoma kwa ajili ya kujikita kupigania Uhuru. Lakini pili, Shkh. Mohammed Said, akimnukuu Bilali Waikela, alisema katika mkutano huo, (Waikela) alimweleza Rais Nyerere, huku akimnyooshea kidole akimtaka kutopenyeza chokochoko, huku akimueleza kutosahau waraka kuhusu juhudi za Waislamu katika kuikomboa Tanganyika. Mwalimu nakwambia (akimnyooshea kidole) moto wa Waislamu ukiwaka wewe huna maji ya kuuzima. Alisema Shkh. Mohammed Said, akimnukuu Bilali Waikela. Shkh. Mohammed Said, alisema haya yanayojiri sasa hivi kwa Waislamu kungamua kwamba wanadhulumiwa na kudai kutendewa haki, na kuinyooshea kidole Serikali kuwa inawadhulumu ndiyo dalili za kauli ya Mzee Waikela, baada ya miaka 51, kupita. Akijibu risala ile ya Waislamu, Mwl. Nyerere, alisisitiza na kuendelea kudai kwamba Tanganyika huru itampa haki kila mtu, pamoja na kwamba alitoka katika ukumbi ule akiwa kichwa chini, kufuatia maneno makali ya Waikela. Shkh. Mohammed Said, alibainisha kwamba, Mwl. Nyerere, alikuwa hapendi kuambiwa au kusikia kwamba Waislamu ndio walioleta Uhuru wa nchi hii, ndio maana hakupenda kueleza ukweli ni nani alishirikiana nao katika kuleta Uhuru, kwa maana alijitahidi kuipoteza historia sahihi na kuweka yale ambayo aliyoyataka yeye yajulikane. Ukisoma historia ya Uhuru wa Tanganyika utakuta ni Mwl. Nyerere tu, mwanzo mpaka mwisho, hukuti mahala historia ikisema kuwa walio muingiza katika siasa na kumpokea ni Wazee wa Kiislamu wa Dar es Salaam, waliompigia debe ni wazee wa Kiislamu, amekuja kuyasema haya alipo amua kungatuka. Alisema Shkh. Mohammed Said. Alisema, mwaka mmoja yalitokea maasi nchini, Mwl. Nyerere, akapata sababu ya kuwakamata Masheikh wa Kiislamu na kuwafunga, ingawa kesi ilipokwenda Mahakamani hakuna hata mmoja aliyeshtakiwa kwa kutaka kuiangusha Serikali ya Mwl. Nyerere. Alisema, kitendo cha kuwakamata Masheikh, wakiwemo viongozi wa Jumuiya ya Waislamu ili ipate kudhoofika, malengo yake yatimie, na katika moja ya kikako cha Waislamu mjini Arusha, ndipo hoja ya kuiua Jumuiya hiyo iliporejea tena na wanaki walitamka kuwa wanataka EAMWS, ife na ianzishwe ingine itakayo Inaendelea Uk. 4

Sheikh Ponda Issa Ponda

watupu. Alisema, katika mkutano huo wa mwaka 1963, uliofanyika katika Shule ya Aghakan ya Wasichana, Jijini Dar es Saalm, kama alivyodokezwa, pakaibuka hoja ya kuivunja Jumuiya hiyo ya Waislamu ya EAMWS, jambo ambalo lilileta mjada mkali. A k a s i m a m a Wa i k e l a (Bilali), akwauliza swali wale waliotaka kuivunja, kwamba hili la kujitenga wamelipata wapi, kwa sababu Qur an inasema, shikamaneni. Kwa hoja hiyo ubishi ule ulimalizika, lakini Waikela aliwaambia, kwa hoja hiyo kuna mkono wa Serikali. Alisema Shkh. Mohammed Issa. Alisema, katika mkutano huo, Bilali Waikela, aliwataka wajumbe wa mkutano kumuita Rais Nyerere, kwa ajili ya kufungua mkutano huo kisha asomewe risala ambayo itamueleza msimamo wa Uislamu kuhusu suala la ubaguzi. Siku ya ufunguzi, Nyerere alifika, risala ilisomwa na Bilali Waikela, alimwambia, hivi mara hii umeshasahau mchango wa Waislamu katika k u i k o m b o a Ta n g a n y i k a kutoka katika mikono ya Waingereza?, alisema Shkh. Mohammed Said. Alisema, risala hiyo ilikuwa na maneno mengi, lakini Shkh. Mohammed Said, aliwataka Waislamu

4
Inatoka Uk. 3 kuwa na Waafrika watupu. Mkutano ulikuwa mkali, taarifa zinaeleza kuwa makachero wa Serikali walikuwa wengi sana, na ndio walikuwa wakiwalisha maneno wale wanafiki ili kuivunja Jumiya ya Waislamu ya Afrika Mashariki na ili kufanikisha malengo hayo, Mwl. Nyerere aliamua kumuondoa Shkh. Hassan Bin Amer, Dar es Salaam na kumpeleka Zanzibar kwa udhalili mkubwa, akiwa na kanga tu. Alisema Kabla ya hapo, alieleza kwamba, mwaka 1964, Sheikh Hassan Bin Amir, alikwenda nchini Misri na ujumbe mkubwa toka Tanganyika na kukutana na Gamal Abdul Nasser, ambaye alijitolea kujenga Chuo Kikuu Cha Markazi, Jijini Dar es Salaam, jambo ambalo lilitia hofu kwa Wakatoliki. Kilichomchoma moyo Mwl. Nyerere, ni mafanikio waliyoyapata viongozi wa EAMWS, katika ziara yao na ahadi ya kujengewa Chuo Kikuu Cha Kiislamu, kwani mwaka 1968, yeye (Nyerere) ndiye alikuwa mgeni wa heshma pale Markazi, mbele ya Shkh. Hassan Bin Amir, Tewa Said Tewa, Mwl. anaweka jiwe la msingi ili pajengwe Chuo Kikuu Cha Waislamu. alisema Shkh. Mohammed Said. Alisema, baada ya taarifa hizo, Kanisa Katoliki walipatwa na hofu wakamwambia Rais Nyerere, nguvu ya Waislamu katika kupigania Uhuru unaijua na kwamba hawa watu (Waislamu) hawana elimu hivyo wanakwenda mbio kujenga Shule na sasa wanataka kuleta Chuo Kikuu, je nafasi ya Ukristo itakuwa wapi. Alisema EAMWS, walifanikiwa kuiuwa n a h a t i m a y e Wa i s l a m u waliundiwa Bakwata, na kukawa na kazi ya kuineza katika mikoa yote, na katika baadhi ya mikoa ilipata upinzani pamoja na ushawishi wa pesa, baadhi ya Wazee wa Kiislamu akiwemo Bilali Wakela, (Tabora), alizikataa pesa zile kiasi cha Shilingi elfu arobain za wakati huo. Lakini kunawatu walichukua pesa zile na Bakwata ikaanzishwa kwa lazima na kuenea Mikoani, na mpaka leo tunayo inatuhangaisha. Tumeikataa Bakwata toka mwaka 1968, lakini tunalazimishiwa nayo hamjuilizi ni kwa nini, na tutaendelea kuikataa mpaka kiama. Alisema Shkh. Mohammed Said. Kwa upande wake Profesa Ibrahim Lipumba, akiongea katika Maadhimisho hayo ya miaka 51, ya Uhuru wa Tanganyika, yaliyoandaliwa na Shura ya Maimam Tanzania, alisema miaka 51 ya Uhuru kwa Watanzania wote imekuwa ni miaka ya adhabu, yale matunda ya Uhuru yaliyotegemewa hayajapatikana. Alisema, ukifanya utati utabaini kwamba ni wachache ndiyo ambao wamefaidi na walio wengi wanaathirika hivyo alisema mabadiliko ni muhimu ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka na inaonekana kwa wote, na kuhakikisha kwamba rasilimali za nchi zinatumiwa kuweza kuleta neema kwa wananchi wote. Akizungumzia sakata la kiwanja cha Markazi, Prof. Lipumba alisema, pamoja na kulifatilia suala hilo kuanzia hatua za awali, mpaka kwa Rais (Kikwete), amebaini kwamba Waislamu wenyewe ndio wanaojimaliza. Tokea kuibuka kwa kadhia hii nimejaribu kukutana na jamaa mbalimbali lakini jambo ambalo nimejifunza ni kwamba sisi wenyewe ndiyo tunao jimaliza. Imeelezwa hapa kwamba waqfu haufai kuuzwa bali huendelezwa kwa lile lengo lililo kususdiwa katika eneo hilo. Alisema Prof. Lipumba. Alisema, ukweli ni kwamba imebainika kuwa eneo limekuwa likiuzwa vibaya na wauzaji ni Bakwata, Taasisi ya Waislamu, aliyenunua ni Muislamu na linalotisha zaidi ni rushwa na ufisadi ulivyokithiri ndani ya vyombo vya dola, hadi kukia huyo aliyenunua kiwanja pia ananguvu na uwezo wa kuamlisha Polisi waweze kukilinda kiwanja hicho. Alisema, kesi hiyo ni kesi ya madai kwamba Waislamu wanasema hicho ni kiwanja chao kwa mujibu wa sharia ya dini yao hakipaswi kuuzwa mnunuzi anasema yeye amenunua na anahati kamili. Kiutaratibu, Profesa Lipumba alisema, kesi hiyo ilipaswa ipelekwe Mahakama ya ardhi, yenyewe iamue kama mnunuzi alikuwa anahaki ya kukinunua kiwanja hicho, kwani kesi iliyopo si ya jinai. Alisema, hata matamko ya Kamanda Kova (Suleiman), alipokuwa akieleza kwa nini Ponda na wenzake

Habari

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012

AN-NUUR

Kukataa kudhulumiwa ni Ibada Mohammed


wamekamatwa, alikuwa hazungumzii suala la kiwanja bali alijaribu kuliunganisha suala hilo na kadhia ya Mbagala (kunajisiwa Qur an) na kuchomwa Makanisa. Alisema, suala hilo linakila dalili ya usadi na rushwa kubwa katika kulishughulikia, lakini katika hilo Profesa Lipumba, alisema jambo l a m s i n g i Wa i s l a m u wanatakiwa kuwa ni watu wa msimamo vinginevyo unaki utawamaliza. Alisema, dhamana ni haki ya kila rai, lakini alidai Sheikh Ponda, kawekewa pingamizi makusudi kwa maslahi ya watu wachache, hivyo aliwataka Waislamu kuwa na msimamo na kuwa pamoja naye kisha kutafuta kila njia ili aweze kutoka, na kesi inayomkabili iweze kuwa ni kesi ya madai. Sasa tutakapo shindwa tutawaeleza kwamba jukumu tulilolichukua limetushinda kwa hiyo tunawarudishia wenyewe muweze kulishughulikia mtakavyoweza. Kwa hivyo zitafutwe njia zitakazo kuwa ni salama tuweze kulimaliza suala hili. Alisema Prof. Lipumba. Prof. Lipumba, aliwataka Waislamu, kuwa kitu kimoja kwani alisema endapo

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. patakuwa na nguvu ya pamoja hawatoweza kuchezewa lakini akatanabaisha kwamba ikiwa watakuwa wepesi kugawanywa na kukosa msimamo basi wataendelea kugawanywa na kudharauliwa.

MKUZO ISLAMIC HIGH SCHOOL


P.O. Box 346, Songea Tel: +255 - 716791113, +255683155902 Email: mkuzoipc@rocketmail.com

Waislamu wote mnatangaziwa nafasi za kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Kiislamu Mkuzo iliyopo Songea mkoani Ruvuma. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28/12/2012 na usaili utafanyika tarehe 29/12/2012 katika vituo vya mtihani vilivyoorodheshwa kwenye fomu ya maombi. Wahi kuchukua fomu mapema, nafasi zimebakia chache. NB: KWA WALE WALIOCHAGULIWA WAFUATE MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE (JOINING INSTRUCTION) KATIKA VITUO WALIVYOFANYIA USAILI. Kwa maelezo zaidi piga simu: 0716 791113, 0683155902. MKUU WA SHULE

NAFASI ZA KIDATO CHA I - 2013

Wanazuoni Afrika wahimizwa kutumia sayansi, utandawazi


Na Bakari Mwakangwale WANAZUONI wa Kiislamu nchini naAfrika kwa ujumla wametakiwa kutumia vyema mazingira ya utandawazi na kuhakikisha kuwa hauathiri maadili ya waumini wao. Aidha wamekumbushwa kuwa huu ni wakati wa sayansi na teknolojia hivyo waitumie katika kufikisha ujumbe wa Allah na kulea jamii kuiletea maendeleo. Wito huo umetolewa na Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika uzinduzi wa Mkutano wa Pili wa wanazuoni Barani Afrika, uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Karume, viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dkt. Bilali, alisema dunia hivi ni ya utandawazi na hakuna jamii itakayoweza kuepuka hilo au kuishi kama kisiwa hivyo ni jukumu la wanazuoni wa Kiislamu kuangalia ni jinsi gani utandawazi hauathiri maadili. Lakini pia ni jinsi gani watanufaika na Utandawazi katika maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yaliyokiwa na mwanaadamu hivi sasa. Alisema Dkt. Bilali. Akiunga mkono malengo mbalimbali ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Barani Afrika, Makamu wa Rais, alisema ni wazi kwamba Waislamu wanapaswa kulipa kipaumbele mbele suala la elimu kwa Waislamu kama walivyo amrishwa katika Qur an na Sunnah. Moja ya malengo yenu ni elimu, suala la elimu na msisitizo wake katika Uislamu hakuna asiyelijua, ni suala la kwanza kufundishwa baba yetu Adam, kwa kuwa Mwenyezi Mungu kabla ya kumpa elimu ya ibada, alimpa elimu ya kuvijua vitu vyote na hivyo hivyo kwa Mtume Muhammad (s a w), amri ya kwanza aliambiwa Iqra yaani soma. Alisema Dkt. Bilal huku akisherehesha aya za Qur an. Alisema, Bara la Afrika lina waumini wengi wa dini mchanganyiko hivyo ni vyema kujenga maelewano mazuri baina ya wafuasi wa dini hizo. Aw a l i , k a m a t i y a maandalizi, ya Umoja huo wa wanazuoni wa Bara la Afrika, ilianisha malengo yake kuwa ni kurejea katika sunnah kwa uelewa wa

Habari za Kimataifa/Tangazo

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012

AN-NUUR

Kura ya maoni yapokewa kwa wingi na wananchi Misri


CAIRO Awamu ya kwanza ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya nchini Misri, imemalizika mwishoni mwa wiki, ambapo Kamati Kuu ya Uchaguzi ya Misri imetangaza matokeo ya awali ya kura hiyo, ambayo yameonyesha kuwa asilimia 57 ya wapiga kura wameipigia kura ya ndiyo rasimu hiyo. Taarifa zinasema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Misri, wamepiga kura ya ndiyo rasimu hiyo ambayo msingi wake mkuu ni Uislamu. Katika awamu yake ya kwanza, kura hiyo ilifanyika kwenye mikoa 10 ya Misri ambayo ni Cairo, Alexandria, ash Sharqiyyah, al Gharbiyyah, ad Daqhaliyyah, Asyut, Suhaj, Aswan, Sinai Kaskazini na Sinai Kusini. Awamu ya pili ya kura hiyo itafanyika siku ya Jumamosi Desemba 22 katika mikoa 18 mingine ya Misri. Hali ya usalama kwa sehemu kubwa ilikuwepo katika mikoa hiyo kumi kulikofanyika awamu ya kwanza ya kura hiyo, isipokuwa tukio moja tu la kuchomwa moto osi ya chama cha al Wafd katika mji wa ad Doqi. Imeelezwa kuwa idadi ya watu walioshiriki kwenye kura hiyo ya maoni, ilikuwa kubwa kiasi kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ililazimika kuongeza muda wa kupiga kura mara mbili. Katika zoezi hilo karibu askari wa usalama na polisi 250,000 walikuwa najukumu la kulinda usalama katika zoezi hilo muhimu na la kihistoria. Mahakimu karibu 12,000, kati ya mahakimu 26,000 wa Misri walisimamia zoezi hilo. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa, kwa jinsi zoezi hilo lilivyofaanyika, ni uthibitisho wa wazi kuwa wananchi wa Misri wamebadilika na wanataka mageuzi ya kweli. Essam al Arian, mmoja wa viongozi waandamizi wa chama cha Uhuru na Uadilifu, tawi la kijeshi la kundi la Ikhwanul

Muslimin, amesema kuwa nchi hiyo itatulia na wananchi watashikamana na kuwa kitu kimoja. Kauli hayo ya al Arian yamekuja kufuatia fujo na machafuko mengi yaliyoikumba Misri, katika kipindi cha hivi karibuni kati ya wanaounga mkono wapinzani wa rasimu hiyo ya katiba mpya. Wapinzani hasa baadhi ya makundi ya kiliberali na kisekula wakiongozwa na watu mashuhuri kama Amri Musa na Mohammed al Baradei, walikuwa wakiwataka wananchi wasusie au wakapige kura ya hapana dhidi ya muswada huo. Wa t a a l a m u w a m a m b o wanasema kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kupitishwa katiba hiyo na iwapo itapitishwa, litakuwa ni pigo jingine kubwa kwa mashabiki wa utawala wa zamani na aliyekuwa swahiba wa nchi za Magharibi, Hosni Mubarak, kadhalika na kwa wale wanaopigia chapuo mirengo ya kiliberali na kisekula nchini Misri. Wakati huo huo, msemaji wa serikali ya Misri ameripoti kuwa mazungumzo ya kitaifa ya nchi hiyo, yameanza baada ya kufanyika kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya. Alaa al Hadidi, ameeleza kuwa mazungumzo hayo yanafanyika kufuatia matokeo mazuri ya kura hiyo ya maoni, na mapendekezo yaliyotolewa na matabaka mbalimbali ya raia nchini humo. Msemaji huyo wa serikali ya Misri amesema kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Hisham Qandil, amefanya mazungumzo na wataalamu wa kiuchumi, ambapo pande hizo zimejadili juu ya mitazamo ya raia wa Misri kuhusu mipango ya kiuchumi ya serikali ya Cairo. al Hadidi, ameongeza kuwa viongozi wa nchi hiyo hivi sasa wanafanya juhudi zote ili kuboresha huduma na ustawi wa jamii, kutimiza matarajio na malengo ya mapinduzi ya wananchi ya Januari 25 mwaka jana.

AU yakabiliwa na ukata
Udhamini wa Gadaf wakumbukwa
kumi na mbili. Umoja huo wa Afrika una nafasi kubwa katika kupunguza utegemezi wa nchi wanachama na kulinda mipaka ya nchi za Afrika iliyokuwepo wakati nchi hizo zinapata uhuru. Vilevile jumuiya hiyo ina mchango mkubwa na majukumu mazito ya kutekelea siasa za ulinzi wa bara la Afrika na kutatua migogoro inayotokea baina ya nchi wanachama. Mambo mengine yanayopewa kipaumbele katika siasa za Umoja wa Afrika, ni kufanya jitihada za kuzuia uingiliaji wa nchi yoyote katika masuala ya

wema waliotangulia, kuweka ukuruba baina ya Maulamaa kutoka maeneo mbali mbali ya Bara la Afriaka. Umoja huo ulioanzishwa mwezi Julai mwaka 2011, mjini Bamako, Mali, pia una malengo ya kuanzisha mamlaka ya marejeo ya kielimu, kivitendo na Kidawa kwa ajili ya kuelekeza juhudi za kiilimu na Kidaawa barani Afrika. Mkutano huo ambao ni wa pili toka kuanzishwa kwa Umoja huo, ulibeba kauli mbiu ya Kulingania kwa mwenendo wa Manabii, ambapo ulihudhuriwa na wanazuoni na walinganiaji wa Kiislamu kutoka nchi takriban 24, kusini mwa jangwa la sahara na nje ya Bara la Afrika.

MKUU wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bi. Nkosazana Dlamini Zuma, amesema kuwa umoja huo unakabiliwa na upungufu wa bajeti ya matumizi yake. Bi. Zuma amesema Umoja wa Afrika (AU) unataka kutembeza bakuli kwa wafadhili wapya kwa ajili ya kutafuta fedha za kudhamini bajeti yake, badala ya kuendelea kutegemea nchi wanachama. Bi. Zuma alisema moja ya malengo ya AU ni kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya Afrika kuwekeza barani humo na kuzidisha mabadilishano ya kibiashara na nchi za Kiafrika. Kwa kawaida bajeti ya Umoja wa Afrika hudhaminiwa na nchi wanachama. Kwa sasa Benki ya Afrika na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika katika Umoja wa Mataifa zina nafasi muhimu katika kudhamini gharama za matumizi ya AU. Kabla ya kungolewa madarakani dikteta wa zamani Kiongozi wa zamani wa Libya marehemu Muammar Gadda, nchi yake ndiyo iliyokuwa mdhamini mkubwa wa bajeti ya Umoja wa Afrika kabla ya kuondolewa madarakani na kuuliwa. Kwa msingi huo, AU imepoteza mmoja wa wadhamini wakuu wa bajeti yake baada ya kungolewa kwake madarakani. Ripoti zinasema kuwa, bajeti ya Umoja wa Afrika kwa mwaka wa fedha wa 2012 ni dola bilioni mbili na milioni mia mbili na

IDADI kadhaa ya wanasiasa wa Marekani wanataka upigwe marufuku ununuaji na uuzaji wa silaha nchini humo, baada ya kutokea jinai ya kutisha katika shule ya msingi ya Sand Hook, katika mji wa Newtown jimboni Connecticut. Duru za habari zinasema kuwa, kitendo cha kuuawa makumi ya wanafunzi na wafanyakazi wa shule hiyo, ni jinai kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo, hivyo wanasiasa na wananchi wanataka katiba iangaliwe upya kwa lengo la kurekebisha kipengee kinahohusiana na uuzaji na ununuaji wa silaha

Marekani sasa wataka ununuzi silaha upigwe marufuku

nchi mwanachama, kutekeleza maamuzi ya jumuiya hiyo katika masuala makubwa kama yale yanayohusiana na makosa ya kivita, mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya binadamu, kutoa misaada katika operesheni za kurejesha amani na kusimamia utekelezaji wa demokrasia na utawala wa sheria. Kwa jinsi hali ilivyo, majukumu mengi ya Umoja wa Afrika yanailazimu jumuiya hiyo kuwa na bajeti ya kutosha, ili iweze kutekeleza vyema mipango yake na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

nchini humo. Katika miaka ya hivi karibuni, kadiri ya miswada kumi imewasilishwa bungeni ikiwa na lengo la kupiga marufuku ununuaji na uuzaji wa silaha lakini bila ya mafanikio yoyote.
Hata hivyo kutokana na mauaji hayo na shinikizo la wanasiasa pamoja na makundi ya kijamii, kuna uwezekano wa kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo kuhusiana na suala la umiliki wa silaha. Watu 28 wakiwemo wanafunzi, walimu na wafanyakazi waliuawa baada ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 20, kuwafyatulia risasi zaidi ya mia moja shuleni hapo.

6
KAMA tulivyoona katika sehemu ya kwanza ya makala hii Maalim Seif alipokonywa vyeo vyote alivyokua navyo katika chama cha CCM na katika serikali na mwishoe kuingizwa gerezani katika miaka ya 1980 kutokana na msimamo wake wa kupinga vitendo vya kuwanyanyasa na kuwagawa Wazanzibari. Maalim Seif alisema potelea mbali liwalo na liwe lakini hawezi k u o n a Wa z a n z i b a r i wanagawiwa. Baadhi kufanywa wenye haki miliki ya Zanzibar na huku wengine wakifanywa maadui. Wengine wakifanywa raia daraja la kwanza na wengine daraja la pili. Ujio wa vyama vingi vya siasa ulimpa fursa Maalim Seif kuendeleza mapambano dhidi vitendo vya kuwagawa na kuwaonea Wazanzibari. Lengo lake na wenzake katika kuanzisha chama chama cha CUF si kulipiza visasi kwa uovu aliofanyiwa yeye na wenzake ndani ya CCM, bali ilikuwa ni kupata chombo cha kuwaingiza Wazanzibari na kuwapeleka kule wanakokutarajia bali ni kuunda jukwaa la kuwaunganisha Wazanzibari baada ya kulikosa alipokuwa katika CCM. Ushahidi wa hili uko wazi kwani pamoja na kuwekwa gerezani kwa miaka mitatu, hakupatapo kupanda juu ya jukwaa na kukilalamikia kitendo hicho cha udhalilishaji na uonevu alichofanyiwa. Tofauti na viongozi wengi wa kisiasa ambao ni kawaida sana kuyafanya mateso wanayoyapata kupitia harakati zao kama mtaji wao katika majukwaa yao kisiasa kwa kulalamika, nimefanyiwa uovu huu ama ule hali hii lakini ni tofauti kwa Maalim Seif. Maalim Seif ajapatapo kupanda jukwaani na kusema nimeteswa, nimehilikishwa, nimewekwa gerezani. Jambo hili limekuwa likiwapa matumaini Wa z a n z i b a r i m a p e m a sana na kufahamu kwamba Maalim Seif hazingatii wala hahesabu maovu afanyiwayo, bali huangalia njia gani za kupita ili kuwahakikishia

Makala

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012 Maalim Seif aliwausia Wazanziabri hao subra kwa kuwaambia ipo siku watashinda. Kuna mamia ya wanafunzi wa Kizanzibari waliofukuzwa masomoni kwa kutuhumiwa kuunga mkono chama cha CUF. Halkadhalika Maalim Seif aliwausia subra wanafunzi na wazazi wa wanafunzi hao kwa kuwaambia ipo siku watashinda. Yote haya yalifanywa kwa lengo la kumkomoa Maalim Seif na wafuasi wake na kujaribu kupambana na chama cha CUF kisiimarike na kisikubalike. Vi t i m b i l u k u k i n a unyanyasaji vilifanywa ili kumkatisha tamaa na wafuasi wake wasifikie lengo wanalolitarajia. Vitimbi hivyo ni ikiwemo kuwaharibia wafuasi wa CUF mali zao kama vile nyumba zao. Moja ya kadhia hizo ni kushuhudiwa kubomolewa nyumba za wananchi waliodhaniwa ni wafuasi wa CUF ambazo walizijenga kwa vibali na sheria kamili za ujenzi huko katika eneo la Mtoni Unguja. Wako Waliopata wendawazimu na maradhi mengine yasiyofahamika hadi kupoteza maisha kwa kitendo cha kushuhudia nyumba zao zikibomolewa bila sababu yoyote. Ni nani aliyezisahanu enzi za melody? Melody walikuwa ni vikosi vya askari, wanamgambo na vijana wanamaskani ( m a j a n j a w i r i ) waliofundishwa chuki dhidi ya wafuasi wa chama cha CUF. Mara kwa mara zilikuwa zikitolewa amri za kutotoka nje kafyuu na askari kupiga madoria katika kila kona za miji na vijiji ambavyo ni ngome za CUF hususan kisiwani Pemba. Kila alieonekana nje alipigwa vibaya hadi kuzirai. Halkadhalika sera maalum za usimamiaji wa utekelezaji wa shughuli za serikali ziliundwa ambazo zilikusudia kuwabagua, kuwaonea na kuwanyima haki na huduma muhimu wale waliounga mkono upinzani. Baadhi ya vipengele vya sera hizo vilitamka wazi uovu kama vile: 1. Serikali ifanye kila njia iwasomeshe vijana wa CCM ambao mwamko wao umo ndani Inaendelea Uk. 7

AN-NUUR

Wazanzibari wanafika kule wanakohitaji kuka akifahamu visasi ni njia ya kutoa mwanya kuwagawa zaidi Wazanzibari na kuunga mkono dhamira mbaya za maadui. Maonevu na vitimbi dhidi ya Maalim Seif na wafuasi wake vilianza mara tu baada ya kuanza mipango ya kuanzishwa kwa chama cha CUF.

Karume, Maalim vinara wa amani


Viongozi na wafuasi waliounga mkono chama cha CUF walinyanyaswa na kufanywa kama si raia wa nchi hii. Kuna mamia ya waliofukuzwa kazini kwa sababu za kuunga mkono chama cha CUF na kunyimwa haki zao zote. Baadhi ya barua wakizoachishiwa kazi zilijieleza wazi wazi umeachishwa kazi kwa

MAALIM Seif Sharif Hamad.

DKT. Amani Abeid Karume.

kosa la kushiriki siasa, wakati barua nyengine zikitafuna maneno kwa kuandika umeachishwa kazi kwa kuwa serikali imelazimika kupunguza matumizi. Wafanyakazi hao walijaribu kufuata taratibu za kisheria kama kupeleka malalamiko yao mahakamani, lakini jitihada zao hizo hazikuzaa matunda yoyote.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mjini, Borafya Silima

7
Inatoka Uk. 6 ya damu ili ikapo mwaka 1998 pasiwe na mpinzani yeyote katika Makao Makuu na katika Wizara au Taasisi ya Serikali, 2. Inaonekana kwamba jeuri kubwa inayotumiwa ni kupitia elimu waliyo nayo wapinzani, kwa kuwa muda mwingi walijishughulisha na kusoma. Hivyo basi Wizara ya Elimu ibuni hila na sababu mbali mbali ili kuwanyima elimu hata ya Sekondari watoto wa wapinzani, 3. Serikali iendelee na kampeni yake ya kuwapunguza wapinzani kisiwani Unguja kwa kuwavunjia nyumba zao katika zile sehemu ambazo hazikupimwa rasmi na Serikali ibuni visingizio mbali mbali na suala hili lifanywe kwa awamu ili kupunguza mshituko nk. Huwezi kuamini kama serikali ya watu inaweza kuwapangia watu wake sera kama hizi. Mateso na utenzaji nguvu dhidi ya watu wasio nahatia yalikuwa ni mambo ya kawaida sana. Vikosi vya ulinzi na usalama, wanamgambo na vikosi vya janjawiri walitumika kuwapiga watu wasio na hatia marungu, mapanga, nondo na risasi za moto. Vitendo hivi vilifanyika mara kwa mara na vilikithiri nyakati za uchaguzi. Watu kwa mamia waliuliwa, waliachwa walemavu, mayatima na wajane. Waliokuwa wakitekeleza vitendo hivyo walipongezwa na kupandishwa vyeo. Yote hayo yalifanywa ili kumkomoa Maalim Seif na chama chake cha CUF. Hata hivyo kwa kuwa mapambano dhidi ya utawala dhalimu uliokuwepo hayakuepukika, Maalim Seif alizidi kuwausia subra wafuasi wake na kuwapa ahadi za ushindi dhidi ya dhulma hizo. Baada ya jamii ya kizanzibari kuwa katika dimbwi la kukata tamaa huku ikiwa imekatika vipande vipande Maalim Seif siku zote alikuwa akikiria njia mbali mbali za kupitia ili kumaliza migogoro iliyopo na kuwaunganisha Wazanzibari. Aliridhia na kusimamia kwa vitendo kukiwa na kutekelezawa

Makala

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012 kitaifa. Kwa kundi hili ni kheri fujo, chuki, uhasama na mapamnano kuliko amani, utulivu na umoja. Hii ni kwa sababu uhai wa kundi hili na maslahi yao na matumbo yao ni kupitia migawanyiko ya Wazanzibari. Kundi hili ni zalio la mabaki ya waumini wakuu wa siasa za kikomandoo. Hawa ndio wale waliojikusanya katika maskani kama ile ya KISONGE na kujipamba kila leo mbele ya sura za Wazanzibari kwa pambo la kusherehekea chuki, farka na ubaguzi. Harakati za watu hawa zinatokana mtandao maalum wa kikundi kinachoungwa mkono na watu wazito serikalini. Hawa huwa hawajifichi hata wakiwa ndani ya chama chao. Wao hujiita wanaharakati na waumini wa ukomandoo. Nyakati za mikutano yahadhara ya CCM hawa hutaka waonekane na wanaCCM wenzao. Kikundi cha takriban watu 50 hivi, akinamama na wasichana, wakiwa wamevalia sare za CCM, ambao kawaida hujiweka safu za usoni za mikutano hutumika kuiibua harakati hii. Hawa ni kama kwamba huchochewa ghafla na mtu, nao wakaibuka kwa kuimba kwa kibwagizo cha Komando! Komando! Komando! Kibwagizo hiki ni cha kuwahadaa watu na kuihadaa hadhira, ili iweze kuamini kuwa watu hao ni waumini wa dhati wa Raisi Mstaafu wa Zanzibar wa CCM mwaka 19902000, Salmin Amour, aliyejipachika mwenyewe jina la Komando, kutokana na hulka yake ya kukosa uvumilivu dhidi ya wapinzani hasa, CUF, na kuthibitisha imani hiyo pale alipowapeleka jela bila ya hatia, Viongozi 20 wa Chama cha Wananchi, CUF. Bila shaka, watambuzi tambueni huo ndio maana ya matusi ya ujumbe wao dhidi ya Maalim Seif,Amani Karume na wapenda umoja wa Wazanzibari. Vibaraka wanausambaza wazi wazi pasi na kicho. Vibaraka wahadhina wanachohitaji na kutamani ni eti CCM Zanzibar kutawaliwa na Komando katika himaya zake, au ukomando katika

AN-NUUR

Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar na mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi

Karume, Maalim vinara wa amani

KIJANA aliyepigwa risasi eneo la Kilimahewa wakati wa mkutano wa kampeni Oktoba 11, 2000.

kwa Muafaka I, muafaka II, na Muafaka III, miafaka ambayo alipigwa teke na chama cha CCM na serikali zake zote mbili huku wakimuacha Maalim Seif, viongozi wenzake na chama chao cha CUF kama mateka wa Miafaka hiyo. Alighilibiwa mara kadhaa kupitia Miafaka hiyo, lakini kwa nia yake sa juu ya kutafuta umoja wa Wazanzibari hakuchoka kuingia katika miafaka hiyo. Maalim Seif aliendelea kuhangaika huku na kule hadi pale yeye na Rais Mstaafu Amani Karume walipofanikiwa kuasisi serikali ya Umoja wa kitaifa iliyotokana na maridhiano ya kisiasa baina yao kwa niaba ya Wazanzibari. Hapa ndipo safari ndefu ya mapambano ya Maalim Seif ilipoanza kutoa dalili njema. Hali ya kisiasa Zanzibar ilikua nzuri, amani na uulivu wa kweli ulirejea, chuki, visasi, ugomvi, mifarakano ilififia pole pole hadi kumalizika kabisa ndani ya kipindi kifupi sana. Wazanzibari wakaungana na kujionakama kitu kimoja. Hata hivyo kuna kundi ambalo halikupendezwa na hali ya utangamano iliyopo Zanzibar hivi sasa tokea kuundwa kwa serikali ya umoja wa

Makala/Tangazo

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012

AN-NUUR

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kipya


kweli. Hapo nyuma Chama Cha WananchiCitizen United Front (CUF) -- kilitokea kuwavutia wengi kiasi kuwa ni tishio kwa CCM. Lakini kilikutana na dhoruba kali kikaenda mrama. Chama hicho kilibambikwa sifa ya kuwa ni chama cha Waislam na hata cha Kiislam. Gazeti moja uchwara lilikishutumu kuwa kinataka kuwasilimsha waTanzania wote nchii iwe ya Kiislam. Ingawa mtu yeyote mwenye akili timamu angeweza kutambua kuwa hilo lisingewezekana lakini matope hayo yaliganda mwilini mwa CUF. Uwongo kama huo haungepata nguvu kama dini iliyokuwa inasingiziwe isingekuwa Uislam; yaani kama ingekuwa Ukristo kwa mfano basi tope hizo zingetiririka na kama vile zimeoshwa na maji. MFUMOKRISTO ulivyojizatiti nchini katu hapataweza kuzuka chama kinachotaka kuleta haki kwa wote na kikawa na nguvu. Vita hivyo vimeendelea hadi hivi leo kiasi kwamba ingawa mgombania urais wa CUF alifikia kujipatia kura zilizomwezesha kushika nafasi ya pili, akishindwa na yule wa CCM mnamo mwaka 2005, chama chake hakikuweeza kupata hata mbunge mmoja kutoka Tanzania Bara. Hujuma kubwa sana ilipita. Kama kweli CUF kilikuwa na bado kina nia ya kuleta haki kwa wote basi waliopata hasara kubwa ni Waislam wa nchi hii. Ni wao ndio wamekuwa wakilalamika kwa siku nnyingi kuwa wanadhulumiwa haki zao. Vita dhidi ya CUF sasa imekuwa kali hasa baada ya Makanisa kujitokeza wazi wazi, sio kukiunga mkono CCM tu, bali pia na kwa nguvu zaidi kukifanyia kampeni CHama cha DEmokrasia na MAendeleo (CHADEMA). Kama inavyofahamika mmoja wa viongozi wa juu kabisa katika chama hicho ni mtumishi wa Mungu katika Kanisa Katoliki. Kuna matukio mawili ambayo wasomaji wanaombwa kukumbuka na kutafakari. Kwanza ni siku ile Rais wa nchi hii alipokemewa hadharani na Muadhama Polycarp Cardinal Pengo. Huyu Rais akiwa kaalikwa kama mgeni Muheshimiwa katika hadhara ya kidini ya Kanisa Katoliki aliambiwa akumbuke kuzungumza vizuri na viongozi wa Kanisa kama alikuwa anataka kuendelea kuiongoza Tanzania. Huyu kiongozi wa Kanisa alisema alikuwa na majeshi ya kupiga kura na kura hizo atazipata yule aliyekubalika na Kanisa. Pili ni katika kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita. Mgombea urais wa CHADEMA alikuwa ni Dkt Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema. Zaidi na la kutafakari kwa makini ni kwamba Muheshimiwa huyu ni padri mkubwa tu katika Kanisa Katoliki. Aliwahi kulifanyia kazi Kanisa hilo katika nyadhifa za juu sana. Wasomaji watakumbuka kwamba Dkt Slaa aliacha kazi ya utawa na kuingia mitaani ambako labda hakuoa ama alioa mke wa kwanza. Lakini wakati wa kampeni ilifahamika kuwa sio tu kamtelekeza huyo mama bali pia alikuwa kapata mwingine ambaye ilisemekana kuwa alikuwa mke wa bwana mwingine. Alipotaka kufunga ndoa na huyu mama wa pili leo hii kesi ipo mahakamani. Lakini la kutia mkazo hapa ni ile hatua ya Makanisa, yakiongozwa na Kanisa Katoliki, kumpigia debe kwa nguvu sana huyu Dkt Slaa akipigania kuwa Rais wa nchi hii. Yaani ilika wakati ambapo padre awe kiongozi wa serekali na nchi kwa jumla. Lakustaajabisha sana ni kuwa viongozi wa Makanisa hawakujali tabia ambayo inaweza kuitwa ya ufuska ya padri huyu ambayo ni kinyume kabisa na maadaili na matakwa ya Kanisa hasa Kanisa Katoliki. Sio hivyo tu bali kuna baadhi ya maaskofu walika kiasi cha kumtetea ati hayo yalikuwa yake binafsi. Kweli!!! Hapa kafikia kiwango cha kuvunja miiko ya Kanisa, yaani kajishughulisha na mambo kinyume na mafundisho ya dini lakini bado Makanisa wanaona wamepata mtu wao ambaye anastahili kuwa Rais wa nchi !!! Ama ukistaajabu yale ya Musa utayaona ya Firaun!! Kwa idadi ya kura alizozizowa Dkt Slaa bila shaka kulikuwemo na wananchama wengine wa CCM ambao walimpa kura zao. Hakika katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi ilisemekana kuwa kulikuwa hata vigogo wanasiasa Serekalini ambao lazima wawe wanaCCM, ambao walionekana wazi wazi kukifanyia kampeni CHADEMA, hata kukinunulia mafuta gari zao (CHADEMA) zitembee. Yaani waliungana wazi wazi na Makanisa kuwa upande mmoja. Mpaka leo viongozi wa CCM wa aina hii, kama kweli walikuwapo, hawajadhurika. Madhumuni ya kuandika yote haya ni kuwaamsha wale Waislam waliowanachama hai na washupavu wa Chama Cha Mapinduzi mpya. Wakumbuke kuwa CUF wamehujumiwa kwa muda mrefu kwa kusingiziwa kuwa ati ni chama cha Waislam ama cha Kiislam. Wengi wa wale waliotekeleza hujuma wamo wanachama wa CCM ama mashabiki wa chama hicho. Turudie kukumbushana kuwa hata pale CHADEMA ilipoonyesha musuli katika uchaguzi uliopita kilipata msaada mkubwa kutoka kwa baadhi ya mashabiki na hata wanachama wa CCM. Lazima tukubali kuwa Chama Cha Mapinduzi kilijengwa madhubuti na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye kila siku alijua anachokifanya huku akiangalia huko mbele kutakuwaje. Ni kweli kunawakati alikasirikia uongozi wa hicho Chama chake na kusema kuwa angeweza kujitoa. Kazi nyingine kubwa aliyoifanya ni kusimika Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA). Hakukijenga chombo hiki kwa maslahi ya Waislam, wengi wa hawa Waislam wamengamua hilo siku nyingi. Lakini hali ilivyo sasa wale Waislam waliowanachama wa CCM na wanaikubali BAKWATA, hata kama ni kwa maslahi binafsi, wanayo nafasi ya kweli kuweza kuutetea Uislam wakiwa ndani ya CCM. Makanisa yana diriki kuitetea CHADEMA, vigogo vya CCM, kwa kujicha ama kujitokeza hadharani kukipigia debe CHADEMA; sasa kitakacho wazuia Waislam ndani ya CCM kutetea HAKI kwa Waislam ni nini? Muheshimwa Ustazi Lt Yusuf Makamba hayupo tena kunadi siasa na dini visichanganywe. Kwake dini yenyewe ilikuwa ni Uislam tu. Alikuwa akiwaogopa Wakristo. Waislam hawataki upendeleo; wanataka dhulma ikomeshwe. WANACHOTAFUTA NI HAKI YAO TU. WANA-CCM WALIO WA I S L A M WATA M B U E HIVYO.

Na Khalid S Mtwangi PAMOJA na kelele na fujo wanazofanaya wafuasi wa vyama vingine vya siasa, hakika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama kikongwe kupita vyama vingine vyote nchini. Sio hilo tu bali pia ndicho kinacho ushawishi mkubwa miongoni mwa wananchi na hasa wafanya kazi Serekalini na katika vyombo na mashirika ya umma. Kweli kufuatana na mengi yanayotokea katika ulingo wa siasa na kandikwa ktika magazeti ni wazi kuwa wamo wasaliti katika baadhi ya wafanya kazi Serekalini; mpaka sasa hujuma zao hazijafua dafu ingawa, kwa wanaCCM na wapenzi wao, ni muhimu kuwa macho sana kabla na hasa wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Uwezekano wa kuwepo hujuma upo; makanisa yanamkono mrefu sana kama ilivyonekana katika uchaguzi uliopita. CCM kuwa na ushawishi mkubwa kiasi hicho pengine si kwa uhodari wa viongozi na wanachama wake tu bali historia ya nchi hii imekisaidia sana chama hicho kuweza kutamba kiasi hicho. Kimekuwa na nguvu sana mijini tangu mwanzo wa TANU (Tanganyika African National Union). Ni sababu hiyo ndio Waislam wengi hujivunia mchango wao mkubwa katika kukiasisi na kukiendeleza mpaka kikawa CCM. Wakazi wa mijini wengi walikuwa ni Waislam na wao ndio ilitokea kuwa walidhurika zaidi na ukoloni kuliko wananchi wenzao waliokuwa wakiishi vijijini ambao, bahati mbaya, walikuwa wakitekwa akili sana na mapadri na makasisi. Ni wale wakristo wa chache wasomi waliokuwa wakiishi mijini ndio waliungana na wananchi wenzao Waislam kupigania uhuru. Hata hivi leo chama hicho kina idadi kubwa sana ya Waislam. Ni bahati mbaya kwa kufahamu au kwa kudanganywa, hawa wanautumikia vizuri sana ule MFUMOKRISTO unaoendesha nchi hii. Ni kweli kuwa hivi sasa CCM hakina mvutio kama ilivyokuwa zamani. Sheria iliporuhusu kuwemo vyama vingi vya siasa wananchi walipata nafasi y kuchagua aina ama sera za siasa zinazowapendezesha na wanazoona zitawaletea maendelao mapema na ya

TANZANIA MUSLIM PROFESSIONALS ASSOCIATION


P.O. BOX 72045, Dar es Salaam, TANZANIA. TEL+255 0655 654900, +255 754 208585, +255 752 245446. Email: info@tampro.org, Web: www.tampro.org

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA 2012


Jumuiya ya Wataalaam wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) inawakumbusha WANACHAMA WAKE kuwa Mkutano Mkuu wa Kumi na Tatu (13) utafanyika siku ya Jumanne na Jumatano, Tarehe 25-26 Desemba, 2012. Mkutano huo utaanza saa 2:30 asubuhi mpaka 11.00 jioni, katika Hoteli ya Lamada, Ilala Boma, Dar es Salaam. Siku ya Jumanne kutakuwa na semina juu ya Wajibu wa Wataalamu Katika Jamii na Uendeshaji wa NGOs. Pia, siku hiyo kutakuwa na ripoti za matawi, Mpango Mkakati wa TAMPRO na salaam za wageni wa Taasisi mbalimbali. Siku ya Jumatano, Mkutano Mkuu utahusika na ajenda zifuatazo: Ufunguzi, Kuthibitisha akidi na Uanachama, Kupokea ajenda, Kuthibitisha kumbukumbu za kikao kilichopita, Yatokanayo, Kuthibitisha wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini, Taarifa ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya TAMPRO, Kupokea na Kujadili Taarifa ya Utendaji na Fedha 2012 ya TAMPRO, Kupokea na Kujadili Mpango Kazi na Bajeti ya Mwaka 2013 ya TAMPRO, Mengineyo, Kufunga. Wanachama Wote Mnaombwa Kuhudhuria PAZI MWINYIMVUA (KATIBU MKUU)

9
Na Mwandishi Maalum WA K AT I h a r a k a t i z a mchakato wa Katiba na madai makubwa ya wananchi ya kutaka suali la Muungano wa Zanzibar na Tanganyika lipatiwe ufumbuzi ukiendelea, kuna mengi ya kujiuliza na kuiuliza Serikali juu ya Utendaji wake na usimamiaji wake wa demokrasia, uhuru na haki za binadamu hasa hapa visiwani, Zanzibar. Nadharia ya Muungano wetu iko wazi kiasili. Iko wazi kwamba ni Muungano wa nchi huru mbili- Tanganyika na Zanzibar, zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kiilivyo, muungano huu ulipaswa uwe na misingi ya usawa kwa pande zote mbili zilizoungana bila kujali ukubwa na udogo wa mshirika mwenza wa Muungano huo. Cha ajabu, Muungano wetu haukubakia na sura yake ya awali, yaani wa usawa kati ya pande mbili. Awali, Muungano ulikuwa na sura ya Kaka mkubwa kwa mdogo. Ikawa Zanzibar inafanywa ni kijisehemu cha mkoa tu wa Tanzania huku Tanganyika ikifa bila kufanyiwa maziko na hakuna anaelijulia kaburi la maiti hiyo ya miaka 51, inayonuka bila kuonekana mzoga wake ulipo. Ukweli ni kwamba, Zanzibar ni zaidi ya kaka mdogo kwa muungano wa sasa. Zanzibar ndani ya Muungano imebanwa na kukandamizwa kila hali na kila muandishi mzalendo ameshaandika sana juu ya hili na sina haja ya kulirudia tena. Kinachonishangaza tu kwa sasa, ni kuona kila harakati anayoifanya Mzanzibari ya kujikwamua na madhila ya Muungano hata kwa njia ya kidemokrasia, mapambano hayo huishia kwa matumizi makubwa ya nguvu za dola zinazopelekea maafa makubwa, tena ni kwa Wazanzibari tu kila siku, ambao hawana haki ya kuhoji haki zao katika Muungano wao. Tukiamua kutaja mabavu na uharamia wa Serikali zetu mbili iwafanyiazo Wazanzibari, ili kuwaziba mdomo wasidai haki zao, basi tutapata kitabu kizima. Achilia matukio ya kukandamizwa na hata kuandamwa watu wenye mitazamo hasi dhidi ya Muungao kutoka Zanzibar, manyanyaso na mateso kwa raia na viongozi wa dini wanaopinga Muungano, mauaji na vipigo wakati wa chaguzi zilizopita, hayo ni machache tu kuyataja. Imekuwa kama utamaduni

Makala/Tangazo

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012


kwa Zanzibar ni kama hewa yenye sumu, hakuna aliekuwa hajaivuta na hakuna aliekuwa haikumuathiri hata ukimsikia akijinadi kuwa muumini wa Muungano uliopo kiasi gani. Akiondoka hapo jukwaani hukohoa damu kama sisi wengine akiwa chumbani mwake. Lazima atakohowa tu! Hewa iliyochafuka haikwepeki hata ukijitahidi kiasi gani. Na kwa Zanzibar ndani ya Muungano, hakuna hewa safi, tusifichane. Si mimi, si Mansuri, si Shamsi wal si Mwinyi Haji, nguvu ya soda tu, sote tunakohowa damu kwa kudhuriwa na hewa mbovu ya Muungano! Na kwa hatua hii uliyokia Muungano wetu na matendo yafanywayo na Serikali zetu dhidi ya Wazanzibari, yaweza kukia mahali baadhi ya watu wakafananisha na ukoloni. Nasema hivi kwa kukozesha sentensi, kwa sababu hakuna sifa hata moja ya kuonesha kuwa kuna tena Muungano wa usawa na nia njema. Kilichopo ni ujanja wa Tanganyika walioutumia kuvaa joho linaloitwa Tanzania. Nasema hivi nikiwa na ushahidi kuwa nchi zote zilizoungana, hazitumii mabavu wala dhuluma dhidi ya upande mshirika wa Muungano huo, eti tu kwa sababu kuna watu wadai haki zao katika Muungano huo. Na kwa maana hii Muungano wetu umepoteza sifa kwani badala ya kutumia katiba, haki, na demokrasia ya maoni huru inatumia mabavu kwa kila jambo lifanywalo Zanzibar hata ikiwa hakuna haja ya kufanya hivyo. Kuna nini Zanzibar? Tuachiwe tupumuwe!

AN-NUUR

Sudan Kusini kujitenga sawa, Muungano mkataba nongwa!


kwa vyombo vyetu vya Dola kufanya kadiri wanaloweza kuzamisha na kukwamisha kila juhudi, kuzima kila pumzi, na kuliziba kila ombwe alipigalo Mzanzibari kudai haki yake kikatiba. Na hili ndilo linalowapa viongozi nguvu ya kujisifu kuwa nchi hii iko huru, ina demokrasia, na ipo kwa ajili ya watu. Ni kweli, ipo kwa ajili ya watu, lakini sio Wazanzibari. Imekuwa kama mila na desturi kwa Serikali zetu, kila ujapo uchaguzi ngome ya jeshi ya kivita hufunguliwa Zanzibar. Tumeona 1995, 2000, na 2005, tuliletewa vifaru, mizinga na maroketi achilia magari ya kawaida ya maji ya kuwasha ya polisi na virungu vyao, katika vijisiwa hivi vidogo vyenye watu wasiozidi milioni moja na kuacha kupeleka majeshi kule bara ambako kuna watu zaidi ya milioni 40. Hivi haya ndio matunda ya Muungano? Hivi tuseme hapa Serikali inatupa Taswira kuwa Zanzibar ni nchi huru katika Muungano? Siamini. Siamini kwa sababu hakuna haja ya kuwalazimisha watu wakubaliane na msimamo fulani, ilhali wako huru kuchaguwa wanalolitaka. Na kufanya hivi ni bishara sa ya kuwa Muungano kati yetu haukuwa wa hiari, wala wa manufaa kwa pande zote mbili na kwa maana hiyo unapoteza sifa na maana ya kuitwa Muungano. Muungano wetu umekuwa ukitumika kuimaliza Zanzibar kwa kutumia vyombo vya dola kufanya mabavu dhidi ya wananchi. Mifano mengine michache tu, kutekwa nyara kwa Ustadh Farid kulikohitimishwa ni kutiwa ndani kwa kesi zinazoendelea mahakani zisizopunguwa sita, ni matokeo ya kuungana kwetu kwa nia safi na wenzetu. Jengine, Maoni ya katiba yalioko hivi sasa Zanzibar, kila Wazanzibari wakijieleza kwa uhuru, hukandamizwa, hutishwa na hata Mheshimiwa Jaji Warioba mwenyewe hasa ukitaja Muungano wa mkataba. Hapa hakuna haki. Kwa nini iwe sisi tu, sio Tabora, Shinyanga na hata Tarime ambako hata Serikali inaogopa kuka kwa fujo za Wakurya? Isitoshe, mchakato wa katiba Zanzibar hivi sasa umeshapandikizwa viluilui vya tina kutoka kwa watu Serikalini kuhakikisha kuwa Zoezi na jaribio la kuukataa Muungano halifanikiwi kwa njia yoyote ile. Yote haya ni matunda ya Muungano ambao ni sawa na yale tuyaonayo wakati wa uchaguzi ya kuletwa watu kutoka bara kwa meli kuja kupiga kura Zanzibar. Yaani hivi tu kila siku! Wanaoutaka Muungano Zanzibar wapo wengi, lakini sio huu uliopo. Ukiachilia wasioutaka kabisa, basi wengi wanahisi uletwe mkataba mpya tukubaliane upya. Kwa upande mwengine, wako wanaotaka ubakie hivi hivi ulivyo lakini hawa ni wale wale, wao kwa wao, na akina mburumatari ambao bila ya kusema hivi watakosa vyeo walivyonavyo. Lakini wakiondoka leo madarakani hujutia maamuzi yao haya ndani ya roho zao. Madhila ya Muungano

JAJI Joseph Sinde Warioba.

Masjidi Mtambani, unawaalika Waislamu wote kuhudhuria katika mawaidha maalum, yatakayotolewa na Mwanahistoria maarufu nchini, SHEIKH MOHAMMED SAID. SIKU: Ijumaa Leo, Desemba 21/2012 Muda: mara baada ya Swala ya Ijumaa. Mada: Harakati za Al-Marhum, Mufti Hassan Bin Amer. Kuanzishwa kwa BAKWATA. Imama, Masjidi Mtambani.

TANGAZO

10
WA K AT I h a r a k a t i z a mchakato wa Katiba na madai makubwa ya wananchi ya kutaka suala la Muungano wa Zanzibar na Tanganyika lipatiwe ufumbuzi ukiendelea, kuna mengi ya kujiuliza na kuiuliza Serikali juu ya Utendaji wake na usimamiaji wake wa demokrasia, uhuru na haki za binadamu hasa hapa visiwani, Zanzibar. Nadharia ya Muungano wetu iko wazi kiasili. Iko wazi kwamba ni Muungano wa nchi huru mbili- Tanganyika na Zanzibar, zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kiilivyo, muungano huu ulipaswa uwe na misingi ya usawa kwa pande zote mbili zilizoungana bila kujali ukubwa na udogo wa mshirika mwenza wa Muungano huo. Cha ajabu, Muungano wetu haukubakia na sura yake ya awali, yaani wa usawa kati ya pande mbili. Awali, Muungano ulikuwa na sura ya Kaka mkubwa kwa mdogo. Ikawa Zanzibar inafanywa ni kijisehemu cha mkoa tu wa Tanzania huku Tanganyika ikifa bila kufanyiwa maziko na hakuna anaelijulia kaburi la maiti hio ya miaka 51, inayonuka bila kuonekana mzoga wake ulipo. Ukweli ni kwamba, Zanzibar ni zaidi ya kaka mdogo kwa muungano wa sasa.Zanzibar ndani ya Muungano imebanwa na kukandamizwa kila hali na kila muandishi mzalendo ameshaandika sana juu ya hili na sina haja ya kulirudia tena. Kinachonishangaza tu kwa sasa, ni kuona kila harakati anayoifanya Mzanzibari ya kujikwamua na madhila ya Muungano hata kwa njia ya kidemokrasia, mapamabano hayo huishia kwa matumizi makubwa ya nguvu za dola zinazopelekea maafa makubwa, tena ni kwa Wazanzibari tu kila siku, ambao hawana haki ya kuhoji haki zao katika Muungano wao. Tukiamua kutaja mabavu na uharamia wa Serikali zetu mbili iwafanyiazo Wazanzibari, ili kuwaziba mdomo wasidai haki zao, basi tutapata kitabu kizima. Achilia matukio ya kuuwawa watu wenye mitazamo hasi dhidi ya Muungao kutoka Zanzibar, manyanyaso na mateso kwa raia na viongozi wa dini wanaopinga Muungano, mauaji ya kinyama ya dola dhidi ya Raia wa Zanzibar, hayo ni machache tu kuyataja. Imekuwa kama utamaduni kwa vyombo vyetu vya Dola chini ya uelekezi wa Serikali kufanya kadiri wanaloweza kuzamisha na kukwamisha kila juhudi, kuzima kila pumzi, na kuliziba kila ombwe alipigalo Mzanzibari kudai haki yake kikatiba. Na hili ndilo linalowapa viongozi nguvu ya kujisifu kuwa nchi hii iko huru, ina demokrasia, na ipo kwa ajili ya watu. Ni kweli, ipo kwa ajili ya watu, lakini sio Wazanzibari. Imekuwa kama mila na desturi kwa Serikali zetu, kila ujapo uchaguzi ngome ya jeshi ya kivita hufunguliwa Zanzibar. Tumeona 1995, 2000, na 2005, tuliletewa vifaru, mizinga na maroketi wachlia mbali

Makala/Tangazo

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012


Madhila ya Muungano kwa Zanzibar ni kama hewa yenye sumu, hakuna aliekuwa hajaivuta na hakuna aliekuwa haikumuathiri hata ukimsikia akijinadi kuwa muumini wa Muungano uliopo kiasi gani. Akiondoka hapo jukwaani hukohoa damu kama sisi wengine akiwa chumbani mwake au hata chooni. Lazima atakohowa tu! Hewa iliyochafuka haikwepeki hata ukijitahidi kiasi gani. Na kwa Zanzibar ndani ya Muungano, hakuna hewa sa, tusichane. Si mimi, si Mansuri, si Shamsi wal si Mwinyi Haji, nguvu ya soda tu, sote tunakohowa damu kwa kudhuriwa na hewa mbovu ya Muungano! Na kwa hatua hii uliyokia Muungano wetu na matendo yafanywayo na Serikali zetu dhidi ya Wazanzibari ni zaidi ya ukoloni, au mateso ya ubaguzi wa rangi wa kule Afrika kusini enzi za makaburu. Nasema hivi kwa kukozesha sentensi, kwa sababu hakuna sifa hata moja ya kuonesha kuwa kuna tena Muungano wa usawa na nia njema. Kilichopo ni ujanja wa Tanganyika walioutumia kuivamia Zanzibar na kuichukuwa kama himaya yao. Na kwa hio Zanzibar imetwemwa na mkoloni mweupe, ikamezwa na mkoloni mweusi, yaani kwa kimombo, from the frying pan, to the re au from gallows to the ring squad! Nasema hivi nikiwa na ushahidi kuwa nchi zote zilizoungana, hazitumii mabavu wala dhuluma dhidi ya upande mshirika wa Muungano huo, eti tu kwa sababu kuna watu wadai haki zao katika Muungano huo. Na kwa maana hii Muungano wetu umepoteza sifa kwani badala ya kutumia katiba, haki, na demokrasia ya maoni huru inatumia mabavu kwa kila jambo lifanywalo Zanzibar hata ikiwa hakuna haja ya kufanya hivyo. Kunani Zanzibar? Tuachiwe tupumuwe!

AN-NUUR

Ya Muungano, na utawala wa mabavu Zanzibar - kulikoni?

WAUMINI wa dini ya Kiislamu visiwani Zanzibar wakiwa katika haa ya pamoja. mijeda yenye magwanda hadi majumbani, katika vijisiwa hivi vidogo vyenye watu wasiozidi milioni moja na kuacha kupeleka majeshi kule bara ambako kuna watu zaidi ya milioni 40. Hivi haya ndio matunda ya Muungano? Hivi tuseme hapa Serikali inatupa Taswira kuwa Zanzibar ni nchi huru katika Muungano? Siamini. Siamini kwa sababu hakuna haja ya kuwalazimisha watu wakubaliane na msimamo Fulani, ilhali wako huru kuchaguwa wanalolitaka. Na kufanya hivi ni bishara safi ya kuwa Muungano kati yetu haukuwa wa hiari, wala wa manufaa kwa pande zote mbili na kwa maana hio unapoteza sifa na maana ya kuitwa Muungano. Muungano wetu umekuwa ukitumika kuimaliza Zanzibar kwa kutumia vyombo vya dola kufanya mabavu dhidi ya wananchi. Mifano mengine michache tu, kutekwa nyara kwa Ustadh Farid kulikohitimishwa ni kutiwa ndani kwa kesi za kubambikiwa zisizopunguwa sita, na zote hazina nyuma wala uso, ni matokeo ya kuungana kwetu kwa nia sa na wenzetu. Jengine, Maoni ya katiba yalioko hivi sasa Zanzibar, kila wazanzibari wakijieleza kwa uhuru, hukandamizwa, hutishwa na hata Warioba mwenyewe hasa ukitaja Muungano wa mkataba. Hapa hakuna haki.Kwanini iwe sisi tu, sio Tabora shinyanga na hata Tarime ambako hata Serikali inaogopa kufika kwa fujo za Wakurya? Isitoshe, mchakato wa katiba Zanzibar hivi sasa umeshapandikizwa viluilui vya tina kutoka kwa watu Serikalini kuhakikisha kuwa Zoezi na jaribio la kuukataa Muungano halifanikiwi kwa njia yoyote ile. Yote haya ni matunda ya Muungano ambao ni sawa na yale tuyaonayo wakati wa uchaguzi ya kuletwa watu kutoka bara kwa meli kuja kuvoti Zanzibar. Yaani hivi tu kila siku. Alimradi Serikali imeapa kupiga, kuuwa, kugaragaza kuulinda Muungano ambao wananchi hasa Wa Zanzibar wamechoshwa nao. Tusimumunye maneno! Wanaoutaka M uungano Zanzibar wapo wengi lakini sio huu uliopo. Ukiachilia wasioutaka kabisa, basi wengi wanahisi uletwe mkataba mpya tukubaliane upya. Kwa upande mwengine, wako wanaotaka ubakie hivi hivi ulivyo lakini hawa ni wale wale, wao kwa wao, na akina mburumatari ambao bila ya kusema hivi watakosa vyeo walivyonavyo. Lakini wakiondoka leo madarakani hujutia maamuzi yao haya ndani ya roho zao

MWENGE EVENING SECONDARY SCHOOL (MESS) KWA KUSHIRIKIANA NA SMS MICROSOFT INTERNATIONAL COMPUTER, LANGUAGES AND ACADEMIC SOLUTIONS
Tunatangaza kuanza kutoa fomu za kujiunga na masomo kwa mwaka 2013 katika kozi zifuatazo: Sekondari ya jioni (Miaka mitatu) Wanaorudia mitihani (Re-sitters) Lugha za kimataifa - Kiingereza, Kiarabu na Kifaransa Kompyuta (Computer studies) Masomo ya Chekechea (Nursery School) WALENGWA: Wafanyabiashara, Wafanyakazi katika sekta binafsi na serikali, wanafunzi waliomaliza darasa la saba , wenye kipato kidogo, wake kwa waume na watoto wadogo kwa kozi ya chekechea. MASOMO: Basic mathematics, English, Civics, Physics, Geography, Kiswahili, History, Maarifa ya Uislam na Computer (kwa wale wa Sekondari) Fomu zinapatikana bure katika vituo vifuatavyo; Shuleni Mwananyamala; Kituo cha njiapanda ya Makumbusho, ndani ya majengo ya Islamic Club (Jirani na Msikiti wa gorofa). Msikiti wa Ijumaa Mwenge Osi za Vijana Osi za TAMPRO (Magomeni Mapipa) Masjid N-nuur, Sinza, Palestina (Muone Dada Aisha) Osi za gazeti la An nuur (Manzese, Tip Top) Osi za gazeti la Kisiwa (Kariakoo, jirani na shule ya Al-Haramain) Pia fomu zinapatikana katika tovuti zifuatazo; www.zidamaafoundation.org, www.eamuslim. com na www.lulunewspaper.com mwengevening@gmail.com/barsett@yahoo.com 0788 307 607, 0713 459 470, 0787 533 123, 0654 533 123 CHAGUA KUSOMA KWETU HUTAJUTIA UAMUZI WAKO NYOTE MNAKARIBISHWA!

NAFASI ZA MASOMO 2013

11
ASSALAMU alaikum Warahmatullahi Wabarakaatuh Nikiwa Mtanzania na mzalendo wa nchi hii, sina budi kueleza kile nilichokishuhudia na kinachoendelea kushuhudiwa na wasafiri wa reli ya kati kutoka Kigoma mpaka Dar es Salaam. Kwa muda mrefu wasari kutoka mkoa wa Kigoma kwenda Dar es Salaam wamekuwa wakiteseka na hali ya usari wa garimoshi kati ya mikoa hii. Ukataji wa tiketi umekuwa ni kero kwa watu wa Kigoma. Ili kuipata tiketi ya Kigoma Dar, wasari wanalazimika kulala stesheni au kuamka kuanzia saa tisa usiku, ili kuwahi foleni ya tiketi.

Nini kimesababisha mzozo mpya Misri?


Na Said Rajab
habari hususan vya Magharibi, kuonesha kwamba vinaungwa mkono na wananchi wengi. Hatua hiyo ilisababisha Dk. Mursi kulegeza msimamo wake wa kujiongezea madaraka ili kutuliza hali ya mtafaruku. Vipi Katiba mpya imechangia mgogoro huu? Dk. Mohammed Mursi aliibuka mshindi na kuwa Mkuu wa Nchi kupitia Katiba na mfumo ule ule uliokuwepo wakati wa Mubarak. Tangu aingie madarakani amekuwa akijaribu kuimarisha nafasi yake ya Urais, na kutunga Katiba mpya imekuwa ndiyo msingi wa jitihada hizo. Hata hivyo, Dk. Mursi anakabiliana na upinzani mkali katika kufanya jambo lolote linaloonekana kumuwezesha kama Rais. Alipoingia madarakani, Mahakama ilivunja Bunge na kisha kulipiga marufuku Bunge Maalumu la Katiba (Constituent Assembly) ambalo lilipewa kazi ya kuandika Katiba mpya. Mgogoro wa sasa wa Kikatiba nchini Misri umewatia moyo sana wapinzani wa Dk. Mursi, ambao wanaona fursa nyingine ya kumdhoosha kiongozi huyo, ikiwa ni pamoja na kutafuta kuungwa mkono kwa kuuponda utawala wake. Mhimili wa Mahakama nchini Misri una ushawishi wa kiasi gani? Mahakama na Dk. Mursi wamekuwa katika uhasama mkubwa tangu awe Rais. Kabla ya kuwa Rais, chama cha Uhuru na Haki kinachoongozwa na Ikhwan Muslimin kilishinda nusu ya viti katika bunge la Misri. Mahakama Kuu nchini Misri ambayo imejaa majaji waliokuwepo tangu kipindi cha Hosni Mubarak, ina historia ya kutoa hukumu zenye utata. Kitu kilichowapa nguvu majaji hawa ni jeshi kuunga mkono hukumu zao. Mazingira yaliyopo sasa nchini Misri ya Mahakama kila wakati kutoa hukumu za kuipinga Serikali, yanahalalisha hoja ya Dk. Mursi kufanya mabadiliko makubwa ya Kikatiba nchini humo. Jeshi limekuwa na jukumu gani nchini Misri? Uingiliaji wa jeshi katika uendeshaji wa nchi na ushawishi usiowiana wa vyombo vya dola umedhoosha m a m l a k a y a R a i s . Ta n g u kupinduliwa kwa Hosni Mubarak, jeshi limehakikisha kwamba uendeshaji wa kila siku wa nchi unakuwa mikononi mwa Serikali ambayo haina mamlaka kamili. Maamuzi yote mazito, ikiwemo sera ya nje yamebaki mikononi mwake. Jeshi limekaa pembeni na limeacha kumpa msaada Rais Mursi ambaye anaungwa mkono na umma. Hata pale Maandamano ya wapinzani yalipochukua sura ya vurugu, jeshi halikuchukua hatua madhubuti kuzima vurugu hizo na badala yake likajifanya liko upande wa wananchi! Kwa hiyo jeshi la Misri limechangia kumdhoosha Rais Mursi kwa kusuasua wakati Ikulu ya nchi na Makao Makuu ya Ikhwan Muslimin yalipovamiwa. Nadhani hiyo ndiyo sababu Dk. Mohammed Mursi akalegeza msimamo wake wa kujiongezea madaraka. Je? Dk. Mohammed Mursi atanusurika kwenye mgogoro huu? Desemba 10, 2012 Dk. Mohammed Mursi alilegeza msimamo wake kuhusu madaraka aliyojiongezea kwa kufuta ile Presidential Decree, ikionekana kama hatua ya kukubaliana na upinzani. Lakini ratiba ya kura ya maoni iliendelea kama ilivyopangwa na bila shaka Dk. Mursi atapata kura za kutosha kuifanya katiba mpya kuwa rasmi. Wakati vyombo vya habari vikubwa duniani vikiwapa wapinzani nafasi kubwa zaidi

Hata hivyo msari akika sio kwamba atakuwa wa kwanza, atawakuta wengine wameshaunga foleni. Jiulize, wewe iliyetoka saa tisa usiku umekuta waliokutangulia, wao wameka saa ngapi hapo stesheni? Kero zaidi ni kwamba, sio wote wanaokuwa kwenye foleni hiyo ndefu watapata tiketi. Wanaweza kuchukuliwa wachache halafu wakatangaza kuwa tiketi za Kigoma-Dar zimekwisha. Hata kama msafiri kalala hapo anakosa. Msafiri huyo akikosa tiketi, atalazimika kwenda

Tatizo la usari wa garimoshi Kigoma-Dar


kukata tiketi ima Dodoma au Morogoro na akika hapo, atatozwa nauli nyingine na faini juu halafu ataanzia kutoka Dodoma au Morogoro na akiwa hana sehemu ya kukaa hadi Dar. Naomba kuuliza hivi ni kitu gani raia wa Kigoma wamekifanya hadi kuadhibiwa kiasi hicho? Vikongwe na wajawazito nao pia kundini kwa nini? Pia stesheni ya Kigoma haina umeme, je, huku si kuzibua mianya ya wizi ufanyike? Ushahidi wa hilo ni tarehe 9. 12. 2012, treni imetoka Dar kuka Kigoma saa mbili

Barua/Makala

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012


vilemba vya ukoka watu wa Kigoma sasa ziishe. Utaratibu wa kukata tiketi uwe kama ule wa Dar kwenda Kigoma, kwani unaweza kata tiketi wiki mbili kabla. Kwa nini na Kigoma msifanye hivyo?. Mwisho kabisa ni kwa viongozi wenye dhamana ya kukatisha tiketi Kigoma. Msari yupo stesheni kuanzia saa kumi, halafu wenyewe wanakuja kufungua osi zao saa nne asubuhi, halafu ikika saa saba unaambiwa tiketi za kwenda Dar zimekwisha. Hali hiyo ipo zaidi kwa abiria wa daraja la tatu. Hebu tendeni haki, waoneeni huruma abiria, vikongwe na wajawazito, tendeni haki. Khalifa wa Allah

AN-NUUR

usiku. Iliondoka kurudi Dar es Salaam saa sita usiku. Hebu jiulize, hakuna umeme, hakuna mbalamwezi, kwa nini mwizi asikuibie? Hebu mamlaka na wizara husika zigeuze upande mwingine wa shilingi na kutatua kero hizi. Kwa watu wa Kigoma kusherehekea miaka 51 ya uhuru katika hali hiyo, ni sawa na kujikejeli wao wenyewe au kuvikwa kilemba cha ukoka na viongozi waishio Dar es Salaam. Hebu Kigoma iangaliwe katika tatizo hili kwani raia wanateseka. Habari za kuwavika

DK. MOHAMMED Mursi, ambaye ni Rais wa Misri tangu mwezi Juni mwaka 2012, alitoa amri ya kirais (Presidential Decree) Novemba 22 mwaka huu, ambayo kwa kiasi kikubwa ilidhibiti madaraka ya Mahakama nchini humo. Amri hiyo ya Dk. Mursi ilisema Maamuzi ya Rais ni ya mwisho na hayatapingwa na yeyote wala chombo chochote nchini Misri, mpaka Katiba mpya iridhiwe na Bunge jipya lichaguliwe. Amri hiyo ya Rais ilisababisha mtafuruku mkubwa miongoni mwa wapinzani wa kisekula ambao walishindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu uliopita. Kubadilishwa kwa mwendesha mashitaka, Abdel Majid Mahmoud, ambaye alishutumiwa vikali kwa kushindwa kuleta hukumu kali zaidi dhidi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak na washirika wake, pia kulisababisha watu wengi wanaoiunga mkono Mahakama kuandamana. Kulikuwa na ghasia kubwa wakati wa Maandamano kwenye mitaa ya Cairo, ikiwemo kuvamia Makao Makuu ya Ikhwan Muslimin na Ikulu ya Rais. Uchaguzi wa bunge la nchi hiyo uliofanyika mwezi Juni mwaka 2012, ulisababisha asilimia 75 ya viti vya bunge kuchukuliwa na vyama vya Kiislamu, huku vyama vya Kisekula vikianguka vibaya. Maandamano yale ya ghasia yalichochewa zaidi na vikundi vya Kisekula ambavyo vilishindwa kwenye uchaguzi wa awali wa bunge. Vikundi hivyo haviungwi mkono na wananchi wengi wa Misri, ingawa viliweza kutumia kikamilifu mitandao ya kijamii (Social Media) na vyombo vya

RAIS wa Misri, Dk. Mohammed Mursi ya kusikika na kusukuma ajenda yao, Dk. Mursi yeye anaungwa mkono na wananchi wengi wa Misri. Wamisri wengi zaidi walijitokeza mitaani kuiunga mkono Ikhwan Muslimin, kuliko wale waliowaunga mkono masekula, ambao ndiyo wapinzani wakubwa wa Dk. Mohammed Mursi. Wapinzani wanataka nini hasa? Ushirika mkubwa wa upinzani nchini Misri The National Salvation Front umeweka bayana kwamba unapinga jaribio la Dk. Mohammed Mursi kujilimbikizia madaraka kama ilivyokuwa kwa Hosni Mubarak. Waliingia mitaani na kuendelea na wito wao wa kumpinga Dk. Mursi na Katiba yake, wakisisitiza wazi upinzani wao dhidi ya baadhi ya vipengele vya Kiislamu kwenye katiba hiyo. Dk. Mursi aliwakaribisha wapinzani kushiriki kwenye majadiliano kuhusu suala hilo Desemba 7, 2012 ambapo walikataa. Lakini Dk. Mursi alipolainika na kufuta kipengele cha kujiongezea madaraka, kwa ajabu kabisa ya uongozi wa upinzani, ulimlaani vikali kwa kufanya kile ambacho walikuwa wakidai! Wakasema jambo hilo halikubaliki kabisa na wakaitisha maandamano na ghasia zaidi! Viongozi wa upinzani nchini Misri wanasema kuondoa kipengele cha kujiongezea madaraka ni geresha tu ya kuficha malengo halisi ambapo wanadai umma unahitaji kuendelea kumpinga Rais anayewapuuza watu wake. Kiuhalisia, upinzani ambao uliangushwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu uliopita, sasa unafanya juhudi za mlango wa nyuma kudhoofisha utawala wa Dk.Mohammed Mursi. Wanatamani kuingia kwenye nafasi za uongozi kupitia mgogoro huu wa kutengeneza.

AN-NUUR
12

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 21-27, 2012

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

Tapeli wa kusilimu jela


Na Jumanne MangiMbeya
YULE tapeli wa kusilimu aliyeandikwa katika gazeti hili siku zilizopita, sasa anatumikia kifungo gerezani. Amefikwa na hatma hiyo baada ya Waislamu kumkisha mahakamani kwa shitaka la utapeli aliokuwa anaufanya kwa Waislamu. Iliwahi kuripotiwa mara kadhaa kuwa mtu aliyejitambulisha kuwa anaitwa Peter John alikuwa akisilimu mara kwa mara. Taarifa zilianzia Ifakara mkoa wa Mororgoro kuwa alifika msikitini na kusilimu na baada ya kushtukiwa taarifa zilipelekwa An nuur ambapo zilisaidia Waislamu wa mkoa wa Mbeya kumnasa alipoenda na usanii wake uleule wa kusilimu. Waislamu wa jiji la Mbeya katika msikiti wa Uyole Njia Panda wakiwa makini na taarifa za wenzao wa Ifakara, waliweza kumnasa bwana Peter John mnamo tarehe 09/10/2012. Chini ya usimamizi wa Imamu wa msikiti huo Ust. H a m i s i Yu s u f , w a l i a m u a wampeleke polisi ambapo Imamu alisimama kama shahidi huku kwana Nurudin Hemedi maarufu kama wa kuchovya akiwa ni mlalamikaji kwa niaba ya Waislamu. Shitaka lilikuwa ni kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Kesi ilianza kusomwa tarehe 14/11/2012 ambapo mshitakiwa alijaribu kuwasingizia Waislamu kuwa ndio waliompeleka msikitini kwa madai ya kuwa alikuwa ameritadi na hivyo walitaka wambambikizie kesi ya wizi wa amplier. Hata hivyo, hakuweza kufurukuta kwa ushahidi uliotolewa. Habari zinafahamisha kuwa mnamo tarehe 28/11/2012 , mbele ya hakimu mfawidhi mahakama ya mwanzo jijini Mbeya, bwana Peter John ambaye jina lake halisi ni Ismail Hassan alisomewa hukumu ya kwenda jela mwaka mmoja kuanzia tarehe 28/11/2012 ili iwe ni fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo ya kutumia maeneo ya ibada kufanya utapeli wao. MBUNGE wa jimbo la Ubungo John Mnyika akichangia hoja katika Ukumbi wa PTA (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam wakati Waislamu walipokutana ukumbi wa Sabasaba Jijini Dar es Salaam, wakiadhimisha na kutathimini hali ya Waislamu katika miaka 51, ya Uhuru mwishoni mwa wiki iliyopita.

Na Bakari Mwakangwale

Fuateni mila ya Ibrahim


Akizungumzia kisa cha yeye na mumewe, (Ustadhi Rajabu) kukamatwa na Polisi, kisha kufikishwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Mwanayamala Mwinjuma, Jumatatu wiki hii, alisema ni kufuatia wanafunzi wake wa kike kutoweka nyumbani kwao wakikimbia kufanyiwa mila za kibila lao. Alisema, wanafunzi hao wa familia moja aliowataja kwa majina ya Mwajuma na Fatma, ambao ni mapacha wa Mzee Mohammed, walitoweka kwao siku ya Jumapili, asubuhi wiki iliyopita baada ya kutofautiana na wazi wao kuhusu mpango wa kufanyiwa mila za kike kwa mujibu wa kabila lao. Ukht. Zuena, alisema mabinti hao ambao wana umri wa miaka 16, ambao ni wanafunzi wa Shule za Sekondari Salma Kikwete na Ananasifu, walidai kuwa walikuwa wanatakiwa kwenda kwao Kibaha, Mkoa wa Pwani, kwa ajili ya shughuli hiyo, jambo ambalo walilipinga kwa kutumia aya na hadithi. Kwa mujibu wa Mwalimu wao (Zuena) ilidaiwa wazazi wao baada ya kuona mabinti hao wamengangania na msimamo wao huo, walipewa amri ya kuchagua ama kufanyiwa mila au kubakia na Uislamu wao. Ukht. Zuena, alisema wanafunzi wake waliamua kuchukua uamuzi kuondoka na kumuambia mama yao kuwa bora wabaki na Uislamu wao kuliko kufanyiwa mila nje ya Uislamu, na zaidi alidai waliacha ujumbe ndani wa maandishi wenye msisitizo wa aya za Qur an, zinazo kataza kufuata mila nje ya Uislamu. Walinieleza nia yao ya kuondoka ikiwa watazidi kuwalazimisha na wapi wataenda kuepuka suala hilo, walisema walimuaga mama yao kuwa wameamua kuondoka ili wabaki na Uislamu wao, mama yo alidhania masihara, lakini alipoingia

WA Z A Z I w a K i i s l a m u wametakiwa kuacha kuamini mila potofu za makabila yao na badala yake watambue kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ya mwanaadam kwa kufuata Qur an na Sunnah. Hayo yamebainishwa na mwalimu wa madrasat Tawhiid (kwa Mzee Kikoti) Mwananyamala Kisiwani, Jijini Dar es Salaam, Ukhuti Zuena Ally, akiongea na An nuur, katikati ya wiki hii, baada ya kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi, kufuatia wanafunzi wake wa kike kugoma kufanyiwa mila za kabila lao. Ukht. Zuena, pia amewataka walimu wa madrasa, wawe tayari kusimamia kimatendo mafundisho wanayowapa wanafunzi wao sambamba na kukabiliana na changamoto kutoka kwa wazazi, ili kuweza kukia lengo la kuandaa vijana wenye maadili mema katika jamii. Ukht. Zuena, alisema wao kama walezi (walimu) kwa upande wa imani wana jukumu la kuwaelimisha watoto maadili mema kwa kuzingatia muongozo wa Qur an na Khadithi za Mtume (s .a .w) na si nje ya hapo, na kuhakikisha wanatekeleza kimatendo. Alisema, kwa kutumia vitu viwili hivyo (Qur an na Khadithi) lazima wazazi wakubali mabadiliko kwa watoto wao ya kimwenendo kutoka katika kuamini mila za makabila yao na kufuata mila sahihi ya dini yao (Uislamu). Wa z a z i w a k u b a l i a n e n a mafundisho tunayowapa watoto wao katika Madrasa, ikiwa tu yanazingatia mafundisho sahihi ya Uislamu kwa kufuata Qur an na Sunnah, na kuachana na mila potofu za makabila kwani nyingi humdhalilisha mwanamke, tofauti na mila ya Uislamu inayolinda linda heshima ya Mwanamke. Alisema.

ndani kukuta ujumbe wa maadishi akajua si utani tena. Alisema Alisema, siku hiyo alifuatwa na baba wa watoto, mjomba na kaka yao wakimshutumu kuwa yeye ndiye chanzo cha watoto wao kugomea kufanyiwa mila ya kuchezwa (wari) huku akitoa maneno makali na kudai kwamba watoto wake wasipoonekana watakishana pabaya. Ukht. Zuena, alisema siku ya Jumatatu, akiwa nyumbani kwake na mumewe, alifuatwa na Polisi akiwa pamoja na wazazi wawili wa wanafunzi wake, na kuelezwa kuwa wanahitajika kituo cha Polisi Mwananyamala Mwinjuma. Alisema, waliondoka pamoja nao, na walipoka kituoni walikuta madai ya kuwatorosha watoto wawili wa kike, Mwajuma na Fatma, kinyume na matakwa ya wazazi wao. Nilikataa hoja hizo, bali niliwaambia nawafundisha wafuate mila ya Nabii Ibrahimu, na si vinginevyo, ambayo ipo wazi katika Qur an, ndiyo tunatakiwa kuifuata na ninadhani wanafunzi wangu wameelewa hivyo. Alisema. Alisema, shauri hilo lilihamishiwa kituo kikubwa cha Ostabey, baada ya hapo kushindwa kupatikana muafaka, baada ya mwanafunzi mmoja kujitokeza ili atoe maelezo, kwa nini hawataki kufanyiwa mila, hata hivyo hakupewa fursa ya kujieleza na alipotaka kusema aliishia kupata vibao kutoka kwa mjomba wake. Hata hivyo, alisema, walipoka katika kituo cha Polisi Ostabey, na kuwekwa rumande kwa muda mrefu, hatimaye muafaka ulipatikana baada ya watoto hao kurejea kwao. Kwa mujibu wa Ukht. Zuena, amedai kwamba baba wa watoto hao ameamua kuwaondoa katika Madrasa yake, akidai anawafundisha watoto wake vitu ambavyo yeye hakufundishwa na Sheikh wake.

UTAFITI uliofanywa na taasisi ya Ant ya Hispania, umebaini kuwa Qurani Tukufu imenvunja rekodi kwa mauzo. Taarifa hiyo inasema kuwa Quran ndicho kitabu kinachouzwa kwa wingi zaidi nchini humo katika nusu ya pili ya mwaka huu wa 2012. Uchunguzi huo unaonesha kuwa vitabu vinavyohusu dini ya Uislamu, ndivyo vilivyouzwa kwa wingi zaidi nchini Hispania katika nusu ya pili ya mwaka huu. Uchunguzi wa kituo hicho umesema kuwa, nakala za kitabu kitakatifu cha Qurani, zinanunuliwa kwa wingi katika maduka ya vitabu nchini humo na kuwa kitabu kinachouzwa kwa wingi zaidi. Baada ya Qurani Tukufu, kitabu cha Sira ya Ibn Hisham kinachozungumzia sira na historia ya Mtume na Uislamu, kinafuatia kwa kuuzwa kwa wingi zaidi nchini humo. Uchunguzi huo pia umebaini kuwa baada ya kuonyeshwa filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) nchini Marekani, uuzaji wa vitabu vinavyohusu dini ya Uislamu uliongezeka sana mwezi uliopita huko Hispania ikilinganishwa na miezi mingine. (IQNA)

Quran yavunja rekodi kwa mauzo Hispania

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

También podría gustarte