Está en la página 1de 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1231 SHAABAN 1437, IJUMAA , MEI 27 - JUNI 2, 2016

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST


(10)KILA ENEO LIPELEKE MAHUJAJI

Allah Ameagiza tuelimishane kuhusu Hijja,


ikieleweka, tutakwenda kutoka kila Mkoa,
Wilaya, Tarafa na Mtaa (Al-Hajj:27). Waislamu
tuhimizane; na matajiri watumie mali zao
kuhakikisha matakwa haya ya Mola wao
yanatimia. Gharama zote kwa Hijja 2016/1437
ni Dola 4,600. Umra ya Ramadhani ni Dola
2,700. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa
huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi:
Tanzania Bara: 0679895770/ 0688895777;
0765462022; 0712735363. Zanzibar:
0777468018; 0777458075; 0777845010;
BEI TShs 800/=, Kshs 50/= 0777497300.

Mauwaji Masjid Rahman Mwanza.....

Fitna kubwa yaja


Mchezo wenu, mauti kwa Tanzania Hofu ya IS Amboni

Yale yale ya Lukuvi


Kanisani juu ya Zbar
Msimshike sharubu Jecha

MHE. Samuel Sitta.

JUU picha iliyowekwa katika mitandao ya kijamii ikidaiwa ni magaidi wa IS


waliopiga kambi katika mapango ya Amboni Tanga. Chini, FFU katika harakati
za kulinda usalama wa raia na mali zao.

MHE. William Lukuvi.

Aliyozungumza Mhe.
Lukuvi kanisani, si ndio hayo
hayo ya IS yanayowapa fursa
wenye MCC kuja na USARAF
zao kufanya vikao Arusha?
Soma Uk. 18.

AN-NUUR

Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Suratu An-faal:73

Fethullah-Gulen
NA wale ambao
wamekufuru baadhi yao
ni maraki wa baadhi.
Mkitolifanya hilo, itakuwa
tna katika ardhi na
uharibifu mkubwa. [ALANFAAL 73]
Katika aya iliyotangulia
Al-Anfaal 72 ilikuja aya
kwa kuthibitisha kwamba
Answarina na Muhajirina
atamrithi mmoja wao
mwingine pamoja na
kutokuwepo uhusiano
wa udugu kati yao. Kisha
imekuja aya hii ambayo
tunataka kuitolea maelezo
na hukumu ya kwamba
Waislamu na makari
hakuruhusiwi kurithi mmoja
wao kumrithi mwingine na
kwamba makari baadhi yao
maraki wa baadhi. Maana
atarithi mmoja wao kumrithi
mwingine. Anaweka wazi
ndani yake Mtume (s.a.w.)
aya hii :
Na alisema: Mimi
nimeepukana na kila
Muislamu anayeishi kati
ya Mushirikina. Wakasema

Ee Mjumbe wa Mwenyezi
Mungu kwa sababu gani.
Akasema Myoto yao
haioni. Maana pamoja na
kuamini kwao kwa hakika
moto ambao wanauwasha
hautoi mwangaza na
hawapambanuki wajuzi wa
mwili wenye kutofautiana
baadhi yao na baadhi
nyingine.
Tunaweza kutoa tathmini
ifuatayo: Moto wenye
kuwashwa jangwani
una umuhimu mkubwa
kwa upande wa kutaka
kufahamu juu ya athari na
kujuwa mahali na kadhalika.
Na huenda ukatathimiwa
mfano huu kwa kipembe
cha kutupambanuka kati ya
moto wa adui na moto wa
raki.
Pakiwa mahali pa
kuwasha moto pa kari na
muumini au machimbuko ya
mwangaza mbele zao yako
pamoja, kutakuwa vigumu
kutenganisha kati yao
pamoja na kujuwa kwamba
kunapasa kuwa mahali
pa kuwasha moto kwa
muumini pawe peke yake
na mahali pa kuwasha moto
kwa kari pawe peke yake,
ili mambo yasichanganyike
juu ya wenye kuwatafuta.
Jambo muhimu kuliko
yote hapa ni kwamba
mwenye kupondoka
akaiacha dini na muumini
nje ya ukanda wa
kuvumiliana kwa pande
mbili na kukubali mmoja
wao hali ya mwingine
iwapo zitadhooka
tofauti za msingi zilizo
kati yao katika upande
wa dini na tabia na kra,

zitaondoka tofauti ambazo


kunapasa kuwepo kati yao
na lau iliendelea hali hii,
unaharibika ule upande
ambao unataka kuanzisha
na unaendeleza ulimwengu
wake pekee juu ya machumo
yake ya kihistoria. Kama
ambavyo kurithiana
hakupiti kati ya muumini
na kari. Hakuna kanuni ya
kurithiana kwa sababu ya
kutofautiana kati ya dini
mbili. Na lau tungesimama
kuendelezea jambo hili kwa
lugha ya wanawazuoni
wa Fiqhi, tungesema: Kwa
hakika kutofautiana kwa
dini kunazuia kurithiana
katika upande wa
mapenzi ya kibinadamu
na kuelewana ikiwa
hakukupatiakana kulinda
juu ya utengano wa mistari
na iwapo kutopatikana
kuchanganyika pasi na
hesabu yoyote au ahadi na
kulifumba jicho kuhusu
baadhi ya misingi ya
kikanuni tutakuwa kwa
matendo yetu na ufanyaji
wetu ambao tumetaraji
kutokana na ufanyaji huo
kuyatengeneza mambo
sababu ya tna na uharibifu
wakati tna na usadi
mkubwa unaohesabiwa
ni tna na usadi wenye
kuchimbuka kutokana
na matendo ambayo
yalifanyika katika msingi
wake kwa niya ya kutengana
kufanya kheri kwa sababu
shari zenye kutokana na nia
njema zimekuwa na sifa ya
kuendelea na makundi ya
watu yasiyokuwa na uelewa
wakati wanapoingia katika
eneo hili kunakuwa kugumu
juu yake kurudi nyuma.

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

UWANJA WA VIJANA-JIONGEZEE MAARIFA


JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA:51
U

38:30

185

12

8:26

7:7

114:5

76:14

MASAUALA
1. Itaje suara na Aya ya ngapi Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja
mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia. Jawabu: 38:30
2. Itaje Sura na Aya ya ngapi? Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada
ya matunda yataning'inia mpaka chini. Jawabu: 76:14
3. Itaje Sura na Aya ya ngapi? Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada
ya matunda yataning'inia mpaka chini. Jawabu: 76:14
4. Malaika yupi akitumwa Wahyi kwa Mitume? Jawabu: Jibril
5. Malaika anayotoa roho? Jawabu: Israel
6. Malaika yupi atakayowauliza waliokufa kwenye Makaburi yao? Jawabu:
Munkar, Nakir
7. Hawali, hawanywi wala hawamuasi Mwenye-enzi-Mungu ni wenye kufwata
amri tu na kutekeleza nani hao? Jawabu: Malaika
8. Ipi nyumba ya Mungu? Jawabu: Msikiti
9. Mitume wakitumiwa kitu gani? Jawabu: Wahyi
10. Kuhani yupi katika nchi ya Syria alipomuona Mtume (SAW) alimtambua kuwa
ndio aliotajwa katika vitabu vilivyopita kuwa ndio Mtume aliobashiriwa? Jawabu:
Bahira

CHEMSHA BONGO: 52

Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.
M

64:5

608 AD

10:16

4:4

35:5

68:17

Bin

610 AD

1,000

74:6

10,000

6:8

3,OOO

5:22

2:99

MASAUALA
1. Itaje Sura na Aya ya ngapi isemayo Kwani haikukujieni khabari ya walio kufuru.
2. Itaje Sura na Aya ya ngapi isemayo Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo
wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo
kuwa asubuhi.
3. Itaje Sura na Aya ya ngapi isemayo Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.
4. Mara ngapi katika mwaka Malaika Jibril akitalii Quran na Mtume Muhammad
(SAW)?
5. Nani aliokuwa Muadhini wa mwanzo katika Uislamu?
6. Kabla ya Vita vya Badr , Sahaba gani alitoa kauli ya kumuunga mkono Mtume
Muhammad (SAW) kwa maneno yafwatayo Ewe mjumbe wa Allah, sisi sio kama wale
watu wa kaumu ya Mtume Mussa AS walionena Wewe na Mola wako watapigana nasi
tunakungoja hapa, Sisi tutakuambia nenda popote pale Allah alipokuamrisha, Tunaapa
kuwa aliokutuma kwa haki basi sisi tutakuwa na wewe bega kwa bega, tutapigana
upande wa kulia, wa kushoto, usoni na nyuma, hatutokimbia.
7. Taja idadi ya Waislamu na Wakiristo pale Tariq bin Ziyad alipoongoza kampeni
ya kupambana na wasio Waislamu nchini Spain?
8. Syd Umar bin Khatab aliuanzisha mji upi kati ya hii: Fustat, Kufa, Basra?
9. Mahujaji wanapotoka Arafa huelekea wapi kwa usiku mmoja? Makka, Muzdalifa,
Mina?
10. Mwaka gani Syd Umar bin Khatab alisilimu, 610, 608, 622 AD?

Jee Unajua?

Baadhi ya Masheikh na watoa mada wakiwa katika picha ya pamoja katika


semina kwa viongozi wa dini juu ya namna ya kudumisha amani katika jamii na
Taifa kwa ujumla. Semina hiyo iliandwaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Kimisr
nchini Tanzania na kufanyika Ngangilonga mjini Iringa hivi karibuni.

Mwandamo wa mwezi

Leo ni Tarehe 20 Shaaban mwaka 1437 AH, sawa na tarehe 27 May, 2016.
Tarehe 6 June tunategemea kuangalia mwezi kwa Ramadhan na Tarehe 7 June 2016
tukijaaliwa tutaanza Ramadhan Rasmi. Kutokea hii leo Ijumaa ya tarehe 27 May
2016 hadi kuka kuanza mfungo wa Ramadhani tumebakisha siku 10.

1. Mti wa Mkaratusi uitwao Eucalyptus Deglupta ni kati ya miti ambayo yenye


kuvutia duniani, mti huu hujiotea wenyewe katika sehemu za Kaskazini mwa dunia,
kwa jina jengine huitwa Mindanao gum au rainbow gum: http://www.wonderslist.
com/10-wonderful-trees-in-the-world/
2. Kati ya viumbe khatari duniani ni Mbu, Nyuki wa Afrika, Papa mweupe,
Dubu wa maeneo ya barafu, Nyati wa Cape, Kiboko: http://www.enkivillage.com/
top-10-most-dangerous-animals.html
3. Ingawa mbwa ni msaidizi na unamtumia kwa kukusaidia lakini mbwa hao
hao unaowapiganisha na kupata kizazi chengine cha bwa ili wawe wakali zaidi huja
wakawa hatari na hata kukuuwa wenyewe, mbwa kama Causcasian Orcharka, Pitbul,
German Shepahard, Rottweiler, Alaskan Malamutes ni mbwa walio khatari sana
kwani ukiwakosea kutowafunza vizuri au kuwachia pasi kuwafanisha mazowezi
mwishowe huja wakakushambulia wewe unayemfuga: http://list25.com/25-mostdangerous-dog-breeds/5/
4. Mwanadamu atapokisha baina ya siku 46 na 73 bila ya kula, hatoweza kuishi
kabisa na akikisha siku hizo atafariki tu. Inakadiriwa kwa kawaida bila ya kula
wala kunywa mtu akikisha baina ya siku 28, 36, 38 na 40, atafariki. http://www.
scienticamerican.com/article/how-long-can-a-person-sur/
5. Ukikisha siku 3 pasi kunywa maji utafariki ingawa wengine hukisha hadi
siku baina ya 8 na 10: https://www.google.com/?gws_rd=ssl#q=how+long+can+you
+live+without+water
6. Walaji wa mkate wa mwanzo duniani ni watu wa Misri: http://www.
encyclopedia.com/topic/bread.aspx
7. Muhogo una kemikali iitwayo linamarin kemikali ambayo unapokula muhogo
mbichi hugeuzwa na kuwa cyanogenic glycoside ambayo inaweza kukuuwa, vyema
kuuchemsha muhogo kabla ya kuula: http://www.alternet.org/food/worlds-10-mostdangerous-foods-people-actually-eat
8. Kati ya sumu hatari sana kwa maisha ya mwanadamu ni Polonium ambayo
inasadikiwa ndio iliotumiwa kumuua kiongozi wa Palestina Yasir Arafat, sumu
nyengine ni Botolinun, Arrow poson, VX, Tetrodotoxin, Strychnine, Cyanide
inasadikiwa ndio aliokunywa Hitler na kufa, Sarin, Amatoxin, Ricin: http://www.
enkivillage.com/deadliest-poisons.html

3
MWANZA kumetokea tukio
ambalo sio la kawaida. Ni
tukio lililogubikwa na maswali
mengi yasiyo na majibu. Lakini
pengine maswali hayo kwa sasa
tuyaweke kando.
Kama walivyosema Masheikh
wa Umoja wa Wanazuoni wa
Kiislamu (Hay-at Ulamaa),
Baraza Kuu na Baraza la Sunna
(BASUTA), mauwaji na jinai
kama hiyo haiwezi kufanywa na
Waislamu, kwa sababu yoyote
ile iwayo. Ila kuna jambo moja
hapa tunatakiwa tulitizame,
nalo ni mlolongo wa matukio.
Yaweza kuwa ni bahati nasibu
tu (hayawiani), lakini wakati
mwingine, sayansi ya bahati
nasibu (science of coincidence)
inakataa.
Kiasi mwezi mmoja uliopita,
ilikuwa ni Aprili 29, 2016,
vyombo vya habari vya
Magharibi vilisambaza habari
kwamba kamanda mmoja wa
Al-Shabaab ameingia Afrika
Mashariki kuanzisha tawi la IS.
Huyu alitajwa kuwa ni Abdul
Nadir Mumin aka Orangebearded Jihadi general, Msomali
raia wa Uingereza.
An Orange-bearded British ISIS
leader sets up base in Somalia as
part of terror group's expansion
plans.
Ndivyo lilivyoripoti gazeti la
Mirror la Uingreza.
Sky News wao wakasema, A
British Islamic State leader has set
up a base in Somalia to extend its
inuence in the Horn of Africa for
the rst time.
Kisha ndani ya habari hiyo
wakasherehesha wakisema:
He is seeking to boost the ISIS
brand in East Africa, a region that
is ripe for the groups expansion but
has yet to be exploited.
Taarifa hiyo ikadakwa na
magazeti ya Uingereza, Marekani
na kwingineko Ulaya, nao
wakaisambaza huku wakinukuu
walichosema ni footage obtained
by Sky News.
Kilichosisitizwa na vyombo
hivyo vya habari vya Magharibi
ni kuwa eneo hili la Afrika
Mashariki lina fursa nzuri za
kusitawi ugaidi wa IS ambazo
hazijatumiwa. Ni kama ardhi
bikra ambayo haijawahi
kulimwa toka iumbwe dunia.
Kulingana na jinsi taarifa zile
zilivyoshabikiwa na kupigiwa
zumari na vyombo vya habari
vya Magharibi, sisi tukaandika
tukionyesha wasiwasi wetu.
Kuna nini? Kuna pangwa
nini? Lakini pia tukahoji,
inakuwaje Afrika Mashariki hii
kuwe na mazingira mazuri ya
kustawi ugaidi wa IS wakati
tayari tumeundiwa vikosi
vya kupambana na magaidi
ambavyo vimewezeshwa kisilaha
na kitaaluma za kikachero na
wataalamu wetu wa ukachero
na Counter terrorism, Marekani?
Hatujakaa sawa, zikarushwa
habari nyingine kwamba tayari
Afrika Mashariki kuna magaidi

Maoni yetu

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Fitna kubwa yaja


Mtego wa panya

States Army Africa (USARAF),


walikuwepo.
Kama tulivyotangulia
kusema, inawezekana matukio
haya yamefuatana tu kwa
bahati nasibu, lakini ukitizama
mlolongo wa matukio haya ya
kigaidi katika nchi nyingine toka
hii crusade ilipoanza, upo
utata mwingi na maswali mengi
ya kuhoji.
Tuliwahi kusema katika moja
ya habari zetu kwamba mara
nyingi watu hawa wanaotoa
tahadhari wamekuwa kama
waganga wa kienyeji na
wapiga ramli wanaoshirikiana
na wachawi. Wanakuambia
IS wameingia Tanzania na
wanakusudia kupiga, na
si muda unapigwa! Kama
tutalitizama tukio hili la Mwanza
na yaliyokuwa yakiripotiwa
na vyombo vya habari vya
Magharibi juu ya ujio wa IS
Afrika Mashariki/Tanzania,
katika sura ya ushirika huu
wa wapiga ramli, wachawi na
mashetani yao, yaweza kuwa
msaada mkubwa katika kujua
MUFT wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir (wa pili kushoto) nini kinatokea na nini ufumbuzi.
akiwa na Amir Sheikh Mussa Kundecha, Sheikh Amran Kilemile Kinyume cha hapo, ni balaa tupu
mbele ya safari.

wakitoa tamko la kulaani mauaji ya Waislamu Msikitini


Mwanza, jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki.
wa IS ambao wanapanga
kushambulia Kenya kwa kimeta.
Hiyo ilikuwa ni mwanzoni mwa
mwezi huu wa Mei. Gazeti la
Daily Mail la Uingereza likiripoti
tukio hilo likasema:
Large-scale' ISIS anthrax attack
is foiled by police: Three people 'who
plotted biological attack in Kenya'
are arrested.
Kisha likaweka vichwa vidogo
vilivyosema: Married couple
and woman arrested in Kenya over
anthrax attack plot. All three are
'part of an ISIS-linked East Africa
terror group network'. Accused
of planning 'large-scale' and
'biological' attacks in Kenya. (Mei
4, 2016)
Nukta ya msisitizo hapo
wakasisitiza kuwa wahusika ni
ISI-linked East Africa terror group
network.
Kilichofuatia ni wanafunzi
wa watatu, Waislamu wakisoma
Shahada ya udakitari (medicine)
kukamatwa wakituhumiwa
kuwa ndio wahusika na
wanachama wa ISI-linked East
Africa terror group network.
Ilipoka tarehe 18 Mei, 2016
mitandao ya kijamii ya wanaMagharibi hao na vyombo vyao
vya habari vikaibuka na taarifa
kwamba kuna magaidi wa IS
katika mapango ya Amboni,
Tanga.
Pro-Islamic State in Iraq and al
Sham (ISIS) militants reportedly
based in Tanzania released a Swahili
and Arabic language video on May
18. The video, titled Warriors of
Tanzania sent another message to
their relatives, shows at least four
militants wielding assault ries in a
cave, possibly in the Amboni Caves

in Tanga region, Tanzania. Reported


al Shabaab militants engaged
Tanzanian soldiers in the Amboni
Caves in February 2015, killing
one and wounding four others. It
is unknown if these two groups are
related.
Ndivyo ilivyoripotiwa katika
mtandao wa Strategic Intelligence
Service: Counter Terrorism &
Internal Security Intelligence.
(Tazama: David Goldman, ISIS
In Tanzanian Caves; Terror
Threat Multiplication, Strategic
Intelligence Services, May 18,
2016.)
Katika habari hiyo ikawekwa
picha ikionyesha vijana
waliocha nyuso na kushikilia
bunduki aina ya AK-47, huku
nyuma yao katika mlango wa
pango, kukiwa na bedera ya
IS. Habari hizo zikaambatana
na tahadhari kuwa IS hao
wanapanga shambulio lao la
kwanza Tanzania. Kwa hiyo,
hata lilipotokea hili la Mwanza,
vyombo hivyo vikaripoti kuwa
shambulio hilo limekuja baada
ya kusambazwa video ya
kuonyesha uwepo wa IS katika
moja ya mapango Tanzania na
kutoa ilani kuwa watapiga.
Lakini ni kipindi hicho
hicho, wakati zinaripotiwa
habari za IS waliojichimbia
katika mapango ya Amboni,
kulikuwa kukiendelea kikao
cha makamanda wa majeshi ya
Ardhini Afrika (Mei 16-19, 2016),
jijini Arusha. Na tukaambiwa
kuwa agenda kuu ni hatari
ya ugaidi Afrika na kwa hiyo
wakufunzi na wataalamu
wetu wa mambo ya mapambano
ya ugaidi, Marekani-United

Fitna inayotukabili
Ambalo ni muhimu kulisema
hapa na kusisitiza ni mambo
mawili. Moja, ni juu ya tna
inayotukabili. Mwaka 2011
zilisambazwa habari katika
vyombo vya habari ikidaiwa
kuwa Boko Haram walikuwa
wameuwa Wakristo 375 kwa
kuwachoma moto. Boko Haram
burns 375 Christians, ndivyo
ilivyoripotiwa huku habari hiyo
ikiambatanishwa na mamia
ya maiti zilizoonekana dhahiri
kwamba zimeungua moto.
Ilikuwa ni picha za kutisha,
huwezi kuzitizama mara mbili.
Kama ilivyotarajiwa. Ilijenga
chuki na kuwatia hasira
Wakristo. Kilichofuatia? Mwaka
huo huo, Wakristo wakalipiza
kisasi. Ilikuwa katika siku kuu
ya Eid el Fitri, kundi la vijana wa
Kikristo likawavizia Waislamu
wapo katika sijda, wakawavamia
wakiwa na silaha mbalimbali,
wakauwa wengi na wengine
kuwachoma moto. Hiyo ilikuwa
Agosti 28, 2011 katika mji wa
Birom. Kutokana na chuki
ya kisasi, kijana mmoja wa
Kikristo akakata mguu wa maiti
moja kwa panga akala nyama.
Alipohojiwa akasema ni hasira ya
kisasi. (Tazama: Birom Christians
eat Roasted esh of Muslims they
Killed in Jos, Nigeria. BBC Captures
and Records Cannibalism Episode.)
Kuonyesha kiwango cha sumu
ya chuki iliyokwishapandikizwa
katika jamii ya Wanigeria
(Wakristo/Waislamu),
zilipotolewa habari hizo katika
mitandao ya kijamii, mwananchi
mmoja aliyejitaja kwa jina moja la
Kebelle, akatoa maoni akisema:
THIS IS GOOD

Inaendelea Uk. 4

Maoni yetu/Habari

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Osi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Fitna kubwa yaja


Mtego wa panya
Inatoka Uk. 3
NEWS.............I NEED
TO HEAR MORE OF
THIS PLS. @POSTER
ALWAYS UPDATE US
WHENEVER CHRISTIAN
ROAST THOSE ANIMAL
VAMPIRES-kebelle
Swali hapa ni je, ni
kweli Boko Haram/
Waislamu waliwachoma
moto Wakristo 375?
Jawabu ni hapana.
Ilikuwa uwongo mtupu
na propaganda.
Picha iliyotumiwa na
kudaiwa ni Wakristo
waliochomwa moto na
BH, ilikuwa ya watu
walioungua moto
katika ajali ya lori la
mafuta (petrol) ambalo
lilipinduka Kinshasa,
Congo tarehe 6 Julai,
2010. Kama ilivyowahi
kutokea hapa Tanzania,
watu walikimbilia
kuchota mafuta,
likalipuka, mamia
wakafa kwa kuungua.
(Tazama: A massacre, or
an oil tanker explosion?
2. Boko Haram massacre
image fake. 3. Congo risks
more killer fuel accidentExpert.)
Waliosambaza
habari hizo za urongo
zilizoilipua Nigeria, ndio
hao hao ambao hivi leo
wanatuletea picha za
magaidi wa IS katika
mapango ya Amboni,
Tanga. Na pengine la
kusisitiza hapa ni kuwa
matukio kama hayo ya
urongo kwa Nigeria,
yalikuwa mengi sana.
Labda hapa nitoe mfano
mwingine.
Mwezi Februari 2012
vyombo vya habari vya
Magharibi na Nigeria
viliripoti kwamba
kuna Boko Haram
wameshambulia kwa
bomu kanisa la Church of
Christ in Nigeria (COCIN)
huko Miya Barkate,
Jos-katika Jimbo la
Bauchi. Ikaelezwa kabisa
kwamba msemaji wa BH
akitajwa kwa jina la Abul
Qaqa kwamba amekiri na
kutamba kwamba ni wao
BH waliolipua kanisa

hilo.
Hata hivyo
kilichotokea ni kwamba
waliofanya hujuma hiyo
walikuwa vijana wa
kanisa hilo wakitajwa
kwa majina ya Lamba
Goma, Filibus Danasa,
Joshua Ali, Danjuma
Sabo, Joseph Audu,
Simon Gabriel, Bulus
Haruna, Yohanna Ishaya
na Daniel Ayuba. Na
kwa bahati ya mambo
ni kuwa wananchi wa
eneo hilo waliwaona
na wakawazingira na
kuwapiga sana kabla
ya kuokolewa na polisi.
(Tazama: When Boko
Haram Became ChristiansFebruary 27, 2012)
Japo matukio hayo
ilikuja kubainishwa
kuwa yalikuwa mambo
ya kupanga, lakini tayari
yalikuwa yashafanikisha
kilichokusudiwa.
Hivi sasa Nigeria hali
ni mbaya. Na sumu
ya tna inaendelea
kupandikizwa. Mafatani
hawajachoka mpaka
yao yatimie. Mwezi
Machi mwaka huu
wakati wa siku kuu ya
Pasaka walitoa taarifa
wakiichagiza Marekani
kwamba kwa nini bado
haijawashugulikia
Waislamu vya kutosha.
Barack Obama anakulaje
siku kuu ya Pasaka huku
Wakristo wakimalizwa
Nigeria? Iliandikwa hivi:
U.S. at Easter: When
Christians Are Slaughtered,
Look the Other Way.
Kwamba, wanashangaa
Marekani, White
House na Pentagon,
wanasherehekea
vipi Pasaka huku
Waislamu wakichinja
Wakristo Nigeria?
Ikashereheshwa kuwa
tayari zaidi ya Wakristo
10,000 washachinjwa
na makanisa 13,000
kulipuliwa (Muslims
Slaughter Over 10,000
Christians and Destroy
13,000 Churches in
Nigeria.). Anaandika
habari hiyo Raymond
Ibrahim (March 27, 2016.)
Picha tunayopewa

katika tukio la
Mwanza, ni Waislamu
wanachinja Waislamu,
kama ilivyo Somalia,
Syria na Libya. Katika
sura hii, yawezekana
mitaani wakawepo
watu ambao wanaweza
kudhaniwa kuwa ni
katika kundi la hao
wanaodaiwa kuvamia
msikiti na kuuwa watu.
Tujue hiyo ni tna
inapandikizwa. Tuwe
makini. Na kisingizio
kitakuwa chepesi kabisa:
Kulipiza kisasi. Watu
watauliwa mahali halafu
inatangazwa kuwa ni
kulipiza kisasi dhidi
ya kundi lililohusika
kuuwa Masjid Rahman.
Ikishatokea hivyo,
utasikia tena wengine
wameuliwa na hao hao

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016


wanaodaiwa kuwa IS.
Hoja labda itasemwa ni
kuuwa wanaki au watu
wasio taka Jihad. Tayari
balaa litakuwa lishaingia
na hakuna kuhani wa
kuliondoa.
Mtego wa Panya
Mtego wa panya.
Hili nalo ni somo
jingine la kuzingatia. Ni
kweli, mtego wa panya
uvunguni mwa kitanda,
unamhusu nini ngombe
na mbuzi, japo wote
wapo katika nyumba
moja? Lakini badala ya
panya, mtego umekamata
nyoka mkiani. Nyoka
amemuuma mwenye
nyumba kafa. Watu
wamekusanyika kwa
maziko, matanga na
khitma, lazima kipatikane
kitoweo. Kachinjwa

ngombe na mbuzi.
Balaa la namna hii
likishaingia katika nchi,
hakuna wa kusalimika.
Tazama Nigeria, Kenya,
Somalia, Libya, Syria n.k.
Kwa hiyo isijedhaniwa
kuwa hili ni tatizo la
Waislamu na IS. Huu
ni ubeberu. IS ni njia
ya kupita tu. Ni mbinu
mkakati. Mkisha nasa
katika mtego huu,
matukio ya hapa na
pale ya kuuliwa watu,
Waislamu kwa Wakristo,
yatakuwa ni yenye
kuendelea, wala hamtajua
anayewafanyizia ni nani.
Mtabaki mkiimba tu BH,
Al Shabaab!
Huu ndio uzoefu
unaoonekana popote pale
walipo kumbwa na balaa
hili. (Soma uchambuzi
zaidi uk. 10)

Sherehe kubwa mazazi ya


Mtume zafanyika Hedaru
SHEREHE kubwa za
kuadhimisha mazazi
ya mtukufu wa daraja,
Mtume Muhammad (saw)
zimefanyika Jumamosi
mwishoni mwa wiki hii
katika mji wa Hedaru
Wilayani Same, mkoni
Kilimanjaro.
Sherehe hizo zilizoanza
Ijumaa iliyopita chini ya
mwenyeji wa shughuli
Sheikh Yusuf Kidago
wa Ahbaabur Rasuul,
zilifanyika katika Msikiti
Mkuu wa Hedaru kwa
kufanyika maonyesho
ya elimu kwa wanafunzi
wa madrasa mbalimbali,
ambapo baadae jioni

zilifuatiwa na zafa kubwa


iliyoongozwa na Sheikh
Jafaar Sadiq, mtoto wa
Sheikh Muhammad Albeidh
kutoka Malindi Kenya.
Madrasa mbalimbali
za ndani na nje ya nchi
zilikogesha sherehe,
wakiwemo wanafunzi wa
chuo cha Shamsul Maarif
cha Tanga, Madrasatul
Sabilillah ya Dar es Salaam,
Majumuat Jiil Salama
kutoka Mombasa Kenya na
nyingine nyingi za mkoani
Kilimanjaro.
Masheikh mbalimbali
wa ndani na nje ya nchi
walihudhuria katika
sherehe hizo wakiongozwa

na Mudir wa Shamsul
Maarif ya Tanga Sheikh
Samir Sadiq.
Wengine ni Sheikh Said
Ali Hassan kutoka Kenya,
Sheikh Muhmoud Mustafa
Al Shiraz kutoka Mombasa
Kenya, Sheikh Hilal
Kipozeo, Sheikh Shaaban
Mbwera, Imam Msaidizi wa
Masjid Jumuia Kisumu Dar
es Salaam.
Masheikh wengine
waliokuwepo katika sherehe
hizo ni Sheikh Hassan
kutoka Mombo, Sheikh wa
Wilaya ya Longido, Sheikh
Abdallah Jamzuri kutoka
Lukozi, Maalim Adam
kutoka Bakwata. ahbaabur.
blogspot.

USTADH Yufuph Kidau (watatu kulia) akiwa na Masheikh kutoka mikoa mbalimbali
na nje ya nchi wakiongoza Zafa mjini Hedaru hivi karubuni.

Makala ya Kimataifa

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Wapalestina kote duniani waadhimisha siku ya


Nakba, miaka 68 tokea kuvamiwa kwa ardhi yao
UTANGULIZI:
Wananchi wa Palestina tarehe
15 ya mwezi huu wa Mei
mwaka 2016, wameadhimisha
kumbukumbu ya miaka 68,
tangu lilipotokea janga kubwa
la kibinadamu la kukaliwa
kwa mabavu ardhi yao, huku
wenyewe wakifukuzwa na
kulazimika kuyaacha makazi
yao, kulikofanywa na utawala
wa Kizayuni wa Israeli.
Siku hii inajulikana kama
siku ya Nakba au siku ya
nakama,janga,maafa na msiba
mkubwa kwa wananchi wa
Palestina wasio na hatia.
Ripoti iliyotolewa na
Kamati Kuu ya Kitaifa ya
kumbukumbu za Siku ya Nakba
imeeleza kuwa, haki ya kurejea
wakimbizi wa Kipalestina
katika ardhi yao ya asili haiwezi
kupingika wala haina mbadala.
Tarehe 15 Mei kila mwaka,
Wapalestina duniani kote
hufanya maandamano
kukumbuka Siku ya Nakba,
ambayo inakumbusha
masaibu ya kufukuzwa kwa
nguvu mamia ya maelfu ya
Wapalestina kutoka katika ardhi
yao, kulikofanywa na vikosi
hivyo dhalimu vya Wazayuni
wa Israeli mwaka 1948.
Wazayuni pia walifuta karibu
ramani za miji na vijiji 500 vya
Wapalestina na kusababisha
Wapalestina wanaokadiriwa
mamilioni kuwa wakimbizi kwa
karne kadhaa kwenye nchi jirani
za kiarabu.
SIKU YA NAKBA
Hivyo basi, Mei 15 kila
mwaka Wapalestina duniani
kote huadhimisha siku hiyo
ya Nakba, inayowakumbusha
dhulma ya kihistoria
iliyowapata,ambayo masaibu
yake yanaendelea kuwanyima
raha hadi leo hii.
Uhalifu huo ulisababisha
kuihama ardhi yao kilazima,
ikiwa ni matokeo ya uhalifu
wa wanamgambo dhalimu wa
Israeli dhidi ya raia wasio na
hatia wa Palestina mwaka 1948.
Kufukuzwa huko kwa
Wapalestina toka katika
ardhi yao ya asili, kumekuwa
kunajulikana kama Al
Nakba (Maafa), huku zaidi
ya Wapalestina laki nane
(800,000) wakiwemo wanaume,
wanawake, na watoto,
wakilazimishwa kuyahama
makazi yao kufuatia tamko
la kuundwa kwa Israeli
mwaka 1948,litokanalo na kile
kilichojulikana kama harakati za
kizayuni.
Wapalestina walikimbilia
katika maeneo mengine ya
Palestina ambayo yalibakia
katika udhibiti wa ndugu zao
wa kipalestina na Waarabu au
nchi jirani za Kiarabu, huku
wakiacha kila kitu zikiwemo
mali, biashara, na akiba yao ya
vyakula ikiwemo nafaka.

WANAJESHI wa Israel wakivamia na kuwapiga raia wa Palestina.


Mara baada ya kufukuzwa
kwa Wapalestina kutoka katika
nchi yao, mfululizo wa sheria
za kidhalimu zilipitishwa na
serikali ya Israeli, zinazolenga
kuzuia wakimbizi wa
Kipalestina kutoka na kurudi
majumbani mwao.
Kufukuzwa kwa wapalestina
kutoka katika ardhi yao ya
asili,haikuwa tu ni dhulma
bali kumelenga pia kuwafuta
na kuwaondoa kabisa katika
historia.
Hadi kukia mwishoni
mwa mwaka 1948, theluthi
mbili ya Wapalestina ilikuwa
imefukuzwa kutoka katika nchi
yao, kufuatia shambulio kijeshi
la Israeli.
Hali iliyopelekea kukimbia
mauaji yaliyofanywa na
wanamgambo wa kiyahudi
katika maeneo mbalimbali
ya Palestina, kama vile Deir
Yassin na Tantura.
Kiuhalisia vikosi hivyo vya
kiyahudi vilipunguza idadi ya
wapalestina kwa kuteketeza
zaidi ya vijiji na miji mia tano
(500).
Hivyo, kila mwaka ikapo
siku ya Nakba, Wapalestina
hukumbuka na kuomboleza
vitendo hivyo vya ugaidi wa
Israeli uliotekelezwa dhidi ya
Wapalestina zaidi ya laki nane
(800,000).
Idadi hiyo kubwa ambayo
wengi wao hawakuwa na uwezo
wa kujitetea, kwani walitokana
na familia za wakulima wa
kawaida wasio na silaha, ambao
walikuwa wamefukuzwa kwa
nguvu na kulazimika kuihama
ardhi yao ya asili.
Serikali ya Israeli iliyoingia
madarakani hivi karibuni,
imepokonya ardhi ya wakimbizi
wa kipalestina,bila kuheshimu
haki zao au tamaa na matakwa
yao ya kurudi nyumbani katika
ardhi yao ya asili.
Viongozi wa kiyahudi

wametamka waziwazi kwamba,


kuna haja ya kutumia nguvu
za kijeshi ili kuwafukuza
Wapalestina wengi vyovyote
iwezekanavyo.
Kulikuwepo na mpango
mkakati maalumu uliowekwa
na wanamgambo wa kiyahudi
ujulikanao kama Haganah
militias Plan Dalet,uliolenga
kutekeleza uhalifu huo wa
kuwafukuza kwa nguvu
wapalestina kutoka katika ardhi
yao,kwa mujibu wa kauli ya
Waziri Mkuu wa kwanza wa
Israeli David Ben Gurion.
"Ni lazima kutumia njia
mbalimbali zikiwemo ugaidi,
mauaji, vitisho, kuwaondoa kwa
ngvu na kukata huduma zote
za kijamii ili kuwafukuzia mjini
Galilaya, ambao ni mji wa mbali
wa Kiarabu."
Mahali pengine duniani
hali hii huchukuliwa kuwa ni
uvamizi wa kutumia silaha,
kufuatia kuporwa kwa ardhi ya
wapalestina wasio na hatia,kwa
kutumia silaha mbalimbali
zikiwemo bunduki na mabomu
kutoka kwa familia zisizo na
silaha.
Kuna wakimbizi wa
kipalestina zaidi ya milioni saba
(7) katika nchi jirani za Kiarabu
na duniani kote hadi kukia
leo hii, ni ukweli usiopingika
kwamba ndio idadi kubwa zaidi
ya wakimbizi duniani iliyobaki.
Hadhi ya wakimbizi na haki
zao mbalimbali ikiwemo haki ya
kurudi nyumbani katika ardhi
yao ya asili, ni miongoni mwa
masuala muhimu katika mzozo
unaoendelea kati ya Israel na
Palestina.
Hii ni kwa sababu wakimbizi
wote wanafurahia haki ya
kutambuliwa kimataifa, kwa
kurejea katika ardhi yao ya asili
ambayo wao walilazimishwa
kuihama na kukimbilia nje.
Haki hii imekubalika
waziwazi wazi kupitia mikataba

ya amani ya hivi karibuni katika


nchi mbalimbali kama vile
Cambodia, Rwanda, Croatia,
Bosnia-Herzegovina, Guatemala,
Ireland ya Kaskazini, Kosovo,
Sierra Leone, Burundi, na Darfur
nchini Sudan.
Umoja wa Mataifa unatilia
mkazo haki hii ya Wapalestina,
kupitia Azimio lake namba 194
la mwaka 1948, lakini Israeli
kwa kukwepa mkono wa
sheria haikukubali kurudi kwa
Wapalestina katika ardhi yao ya
asili, wakati Mayahudi kutoka
mahali popote duniani walipo
wanaweza kurudi na kuishi
nchini Israeli.
Nakba ni maafa makubwa
zaidi kuliko uhalifu wa aina
yake wa mwaka 1948, ni janga
la kihistoria ambalo bado
wapalestina wanalichukulia
kuwa ni ukweli na uhalisia,
si tu kukumbuka tukio hilo
ili kuadhimisha kilichotokea
miaka 68 iliyopita, bali ni maafa
yanayoendelea kuiharibu
Palestina na Wapalestina
wenyewe hadi leo.
Hivyo basi, siku ya Mei
15 kila mwaka,huwa si tu ya
maadhimisho ya miaka 68 au
zaidi ya maafa ya Nakba, bali ni
mwaka mmoja zaidi wa kudumu
kwa ukatili wake. Historia ya
maafa ya Nakba haikuwa ni
historia tu ya siku na miaka
iliyopita, bali ni historia ya sasa
tunayoishi nayo.
Nakba imesababisha
mamilioni ya wakimbizi wa
kipalestina hadi leo kusambaa
duniani kote, huku wengi wao
wakiwa ni wakimbizi kwa zaidi
ya mara mbili au tatu, kutokana
na uvamizi wa makazi yao na
ardhi yao unaoendelea nchini
Palestina.
Uvamizi huu wa kidhalimu
na uhalifu huu, unaendelea
kufanywa na Israeli kinyume
na sheria, ukiwemo upanuzi
wa mara kwa mara wa makazi
haramu ya walowezi,kupora
ardhi ya Wapalestina na
kuharibu mali na maisha yao.
Hivyo basi,Wapalestina
popote duniani, jumuiya
ya kimataifa na wale wote
wapenda haki na amani
duniani, huadhimisha siku hii
ya Mei 15, ikiwa sio tu siku ya
maombolezo na maadhimisho
ya yale yaliyotokea mwaka 1948,
bali pia ni siku ya kuungana na
wananchi wa Palestina katika
kudai uhuru wao, haki zao na
kumaliza uvamizi wa kimabavu
katika ardhi yao.
Contact us: P.O Box 20307,
612 UN Road Upanga West,
Dar es Salaam Tel: 2152813,
2150643 Fax: 2153257 Email:
pict@pal-tz.orgWebsite: www.
pal-tz.org

Hoja ya Juma Kilaghai

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Hakuna ugonjwa usio na dawa! (3)


KATIKA makala iliyotangulia
tulisema kuwa tati
zinaonyesha kwamba kuna
wakati saratani ni matokeo
ya mchakato wa ukarabati wa
seli zilizoharibika ndani ya
mwili. Tukaendelea kusema
kuwa kila mwanadamu ana
seli ndani ya mwili wake
ambazo huitwa Trophoblasts
ambazo zinafanana sana na
seli za saratani na kuwa seli
hizi hutumwa katika eneo
ambalo kuna uharibifu wa seli
za mwili kwa sababu moja
ama nyingine, kwa nia ya
kusaidia ukarabati. Tulisema
pia kuwa tatizo linalozaa
saratani ni pale ambapo
uharibifu wa seli husika ni
endelevu na hivyo kupelekea
kuwa na mlundikano mkubwa
uliopinduka mpaka wa
Trophoblasts.
Tuliona kuwa moja ya
tiba mujarabu za saratani ni
ile inayotumia vimengenya
(enzymes) ambayo ilibuniwa
na Dk. William D. Kelly wa
Marekani na kuthibitishwa na
Dk. Nicholas Gonzales wa New
York huko huko Marekani.
Tuliona kuwa Dk. Kelly aliamini
kuwa saratani ni zao la mwili
kushindwa kuchakata vizuri
vyakula vya jamii ya protini
kutokana na upungufu wa
vimengenya vinavyozalishwa
na kongosho, hususan vile
ambavyo kazi yake ni kuchakata
na kuyeyusha protini (proteolitic
enzymes). Mantiki ya D. Kelly
ilijikita kwenye ukweli kuwa
kama mwili una vimengenya
vya kutosha, na hasa vile
vinavyotumika kumengenya
protini, basi kusingekuwa na
uwezekano wa kuwepo kwa
mlundiano uliopindukia mipaka
wa Trophoblasts ambao baadaye
ungezaa saratani.
Vyakula vilivyopikwa
havina vimengenya hai. Hii
ni kwa sababu vimengenya
vingi hufa (hupoteza uhai
wake) vinapowekwa kwenye
joto la nyuzi joto kati ya 42 na
47 katika kipimo cha Celcius.
Vyakula vingi huivishwa na
maji ambayo huanza kuchemka
baada ya kukia nyuzi joto
100 katika kipimo cha Celcius.
Hii ina maana kuwa mgonjwa
wa saratani anayetaka kujitibu
kwa programu ya Dk. Kelly
atalazimika kula sehemu kubwa
ya chakula chake katika hali
ya ubichi. Vyakula vinavyofaa
kuliwa katika hali hii ni pamoja
na asali gha, mayai mabichi,
njugu za aina mbalimbali
kama karanga, korosho, lozi
(almond), kimea (sprout),
matunda na mboga mboga
za majani. Mbogamboga za
majani zinaweza kuliwa kama

Tiba za saratani Sehemu ya pili

saladi na inaposhindikana kama


smoothy, yaani kimiminika
kinachotokana na kuzisaga.
Hata hivyo vyakula vyenye
kiwango kikubwa kabisa cha
vimengenya vinavyomengenya
protini ni matunda ya aina ya
nanasi na papai. Kwenye nanasi
kuna kimengenya kinachoitwa
bromelain. Kimengenya hiki
kipo kwa wingi zaidi kwenye
kigogo cha katikati ya tunda la
nanasi hivyo basi tunapohitaji
kulitumia nanasi kama dawa
ni vizuri tukajumuisha kigogo
hicho katika matumizi.
Papai nalo lina kimengenya
kinachojulikana kama papain.
Mtu anayetaka kutumia
kimengenya hiki kama tiba,
anaweza akakipata kupitia
unywaji wa kutosha wa juisi ya
papai.
Katika makala ya leo
tutazungumzia aina nyingine
ya tiba ya saratani ambayo
mgunduzi wake aliitazama
saratani katika jicho tofauti
kidogo. Tiba hii ni ile
inayojulikana kama The
Budwig Diet Protocol ambayo
ilivumbuliwa na Dk. Johanna
Budwig. Dk. Budwig alizaliwa
nchini Ujerumani mnamo
mwaka wa 1908 na alifariki
mnamo mwaka 2003 akiwa na
miaka 95. Katika wasifu wake
mwanamke huyo anatajwa
kama mmoja wa wanasayasi
watati wa masuala ya saratani
wa juu kabisa kuwahi kutokea
katika bara la Ulaya, Mkemia
wa masuala ya kibailojia
(Biochemist), Mtaalam bingwa
wa damu (Blood Specialist),
Mtaalamu wa tiba za kifamasia
na Mwana zikia. Moja ya
mambo yanayomtambulisha Dk.
Budwig kama mwanasayansi
mkubwa ni kule kuchaguliwa
kwake mara 7 kama mshindani
katika tuzo za Nobel. Mwaka
1952 kule nchini Ujerumani
aliajiriwa na serikali kuu ya nchi
hiyo kama Mtaalamu namba
moja wa Serikali katika masuala
yaliyohusiana na mafuta (ya

kula) na dawa za kifamasia.


Katika uhai wake Dk. Budwig
alitambulika pia kama mmoja
wa wanataaluma wakubwa
duniani kuhusiana na mafuta ya
kula.
Kupitia tati zake Dk. Budwig
alibaini kuwa moja ya chanzo
kikubwa sana cha maradhi
kilikuwa ni mafuta ya kula.
Tati zake zilibainisha kuwa
mafuta ya kula ya viwandani
(commercially processed fats
and oils) yalikuwa yanaharibu
kiwambo cha seli za mwili
(cell membrane) na kuwa hali
hiyo ilikuwa chanzo kikubwa
cha maradhi ya kimfumo.
Kwa mujibu wa Dk. Budwig
katika seli ya mwili yenye
siha njema, kiini cha seli (cell
necleus) huwa kimebeba umeme
chanya na kiwambo huwa
kimebeba umeme hasi. Dk.
Budwig alisema kwa kuwa
mafuta ya kula yaliyosindikwa
viwandani yalikuwa pia
yamepoteza umeme hasi
ambao yalikuwa nao kabla
ya kusindikwa, yanapoliwa
na kuka katika ngazi ya seli
badala ya kuimarisha wingu
la chembechembe zilizobeba
umeme hasi katika kiwambo
cha seli, yalikuwa yanaharibu
wingu hilo na kusababisha
umeme unaozalishwa kwenye
seli kuwa mdogo. Kuporomoka
kwa kiwango cha umeme
kinachozalishwa kwenye seli
ndio chimbuko la seli kushindwa
kufanya kazi vizuri na hatimaye
kusababisha maradhi.
Dk. Budwig alisema
kuwa mafuta yaliyoharibika
yanapoingia ndani ya mwili
yanakuwa yamepoteza uwezo
wake wa kuungana na protini
zilizoko mwilini na hivyo
kupoteza uwezo wake wa
kuyeyuka ndani ya vimiminika
vilivyomo mwilini bila matatizo.
Kwa mujibu wa Dk. Budwig
kitendo cha mafuta kushindwa
kuyeyuka ndani ya vimiminika
vilivyomo mwilini kulikuwa
kunapelekea mafuta hayo

yashindwe kutiririka kwa wepesi


ndani ya mishipa ya damu na
hivyo kuzaa tatizo la mzunguko
wa damu.
Bila mafuta tunayokula
kuchakatwa ama inavyopaswa
ndani ya mwili, vitendo vyote
muhimu ambavyo ni lazima
vitokee mwilini vinaathiriwa na
kuathiriwa huku huathiri hali
ya kisiha ya viungo mbalimbali.
Athari hizi ni pamoja na
kuzalisha uhai mpya ndani ya
mwili na kuzaliwa kwa seli
mpya. Miili yetu huzalisha
zaidi ya seli milioni 500 kia
siku. Kupitia tati zake Dk.
Budwig alibainisha kuwa ili
seli igawanyike vizuri na kuzaa
seli mpya, ni lazima umeme
unaotengenezwa na seli husika
ukie kiwango fulani la sivyo
haitagawanyika ipasavyo na
kama hili halitafanyika, mwili
unaanza kufa. Kwa maneno
mengine mafuta yaliyosindikwa
viwandani yalikuwa
yanasababisha seli za mwili
kuzalisha umeme wa kutosha
na hivyo basi kujenga mazingira
ya magonjwa hatari ya kimfumo
kuibuka mwilini.
Dk. Budwig alipambana kujua
jinsi ambavyo mwili ambao
tayari ulikuwa umevamiwa na
maradhi ya kimfumo ungeweza
kujikarabati na kuirudisha
siha yake. Baada ya jithada za
muda mrefu aligundua kuwa
iwapo mgonjwa angetumia
mchanganyiko wa mafuta
yanayoitwa omega-3 na jibini
ya nyumbani (cottage cheese)
wingu la umeme hasi kwenye
viwambo vya seli mbalimbali
za mwili lingeweza kurejeshwa
na kufanya seli za mwili
kutengeneza umeme unaoweza
kukidhi viwango vya kuufanya
mwili kuwa na siha njema. Dk.
Budwig alipendekeza matumizi
ya mafuta ya mmea unaoitwa
ax ambayo yana kiwango kingi
cha omega -3.
Ubora wa tiba ya Dk. Budwig
umethibiti kwa uwazi kabisa.
Uzuri wa tiba hii ni kwamba
inatibu magonjwa takriban yote
ya kimfumo ikiwa ni pamoja
na baridi ya yabisi (arthritis);
magonjwa ya moyo; magonjwa
ya ngozi kama Psoriasis,
Eczema, nakadhalika; Upungufu
wa Kinga Mwilini; Magonjwa
ya mishipa ya fahamu; Kisukari;
Magonjwa ya mapafu; Vidonda
vya tumbo; Magonjwa ya Ini;
Tezi dume; Kiharusi; Saratani za
ubongo; Mkakamo wa mishipa
ya damu na magonjwa mengine
mengi ya kimfumo.
(Juma Killaghai ni mtaalam
wa lishe, ni mtaalam wa stadi za
tiba, na pia ni mkemia mtati
wa bidhaa zinazotokana na
viumbe hai (Organic Natural
Products Research Chemist).
Kwa mawasiliano unaweza
kumpata kwa namba
0754281131;0655281131)

7
Na Bakari Mwakangwale

UCHUMI imara miongoni


mwa jamii ya Kiislamu
unaweza kuita ni
janga linalosababisha
kukwamisha mipango
na malengo yao katika
kutimiza ndoto za kuweza
kumiliki Vyuo Vikuu,
vyuo vya kati, Mabenki
na hata Hospitali kubwa.
Misikiti mingi, hususani
Jijini Dar es Salaam, ikiwa
kama Taasisi imekuwa na
malengo ya muda mrefu
na mfupi katika mipango
yao, licha ya kumiliki ardhi
nje ya Jiji, lakini malengo
yao ya muda mrefu ikiwa
ni kuwa na vitu kama vile
Vyuo Vikuu, Hospitali
za Kiislamu, yamebakia
katika makaratasi, kikwazo
kikubwa kikitajwa kuwa ni
uchumi duni.
Je, ni kweli Umma wa
Kiislamu kupitia Taasisi
zao za Misikiti, Mabaraza
na Jumuiya mbalimbali
za Kiislamu zinashindwa
kujipanga na kuweka
mikakati ya kutimiza
malengo hayo? Nini tatizo!
Uislamu una utajiri
mkubwa ikiwa tu wenye
Uislamu wao wataweza
kufata misingi ya
kukabiliana na umasikini.
Hii ni changamoto kwa
Waislamu, wanapaswa
kuvumbua utajiri uliomo
ndani ya Uislamu ambao
umelala, kwani Waislamu
wenyewe ndiyo rasilimali
na utajiri weneyewe. Lakini
wanatumika vipi hapo ndipo
kwenye matatizo.
An nuur, wiki hii
imetembelea Msikiti wa
Makuti (Masjid Makuti),
uliopo kati ya Mtaa wa
Lindi na Tukuyu, Ilala Jijini
Dar es Salaam na kuweza
kupata historia ya Msikiti
huo na maendeleo yake kwa
ujumla. Kupitia historia ya
Masjidi Makuti, An nuur,
imebaini kuwa Msikiti
huo mkongwe kabisa,
unamilikia ardhi nje kidogo
ya Jiji la Dar es Salaam,
katika maeneo ya Buyuni,
Chanika, yenye ukubwa
wa zaidi ya mita za mraba
4000. Hii ni kwa mujibu wa
Imamu Mkuu wa Masjid
Makuti, Sheikh Abdallah
Nassoro Matulanga, aliyetoa
historia ya Msikiti huo na
kueleza kuwa matarajio ya
matumizi ya kiwanja hicho
ni mengi ikiwemo kujenga
Hospitali kubwa ya Kiislamu,
sambamba na kujenga kituo

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Masjid Makuti, Ilala

PICHANI juu ni Masjid Makuti, Ilala. Katikati, wanafunzi wakiwa


darasani.

cha elimu kwa ujumla, ila


tatizo linalo wakwamisha ni
hali ya kiuchumi tu.
Anaeleza kwamba historia
ya Masjidi Makuti, inaanzia
Mei 23, mwaka 1949,
kutokana na juhudi za AlMarhum Sheikh Kibwana
Chanzi, aliyefatilia eneo hilo
Serikalini, ambapo kiwanja
cha Msikiti huo kiliweza
kupatikana.
Baada ya upatikanaji wa
kiwanja hicho ulijengwa
Msikiti wa Makuti, kwa
maana kwamba kuta zote
zilizunguushiwa Makuti na
kuezekwa kwa Makuti, na
ndio asili ya jina la Msikiti
huo na kudumu mpaka sasa
kama Masjid Makuti. Msikiti
huo, uliendelea kuswaliwa
katika hali hiyo ya Makuti,
mpaka Julai 8, mwaka 1965,
baada ya kupata kibali kutoka
Halimashauri ya Jijiji la Dar es
Salaam na kubomoa Msikiti
wa Makuti na kuboreshwa
kwa kuujengwa kwa matofali
ya saruji. Toka wakati huo
umebakia hivyo mpaka
sasa kama unavyoonekana,
wakati huo Imamu alikuwa
Marehem, Sheikh Ally
Athumani, ambaye alifariki
mwaka 1992.
Awali Msikiti huo ulikuwa

na ukubwa wa viwanja nane,


lakini vilikuwa vimetekwa
lakini kwa juhudi za
Wadhamini wa Msikitiki huo
walifanikiwa kuvirejesha
katika miliki ya Msikiti na
kuweza kutumika katika
shughuli mbalimbali za
Kiislamu ikiwemo kujenga
vyumba vya biashara,
Madrasa na Shule za Awali
na Msingi za Kiislamu (Ilala
Islamic Nursery &Primary
School), zilizoanza mwaka
2004.
Kwa upande wa Madrasa,
zipo Madrasa za aina mbili,
kuna Madrasa ambayo inatoa
elimu ya Dini (Fiqih, Nahau,
Balagha n.k) ambayo ipo
chini ya Ustadhi Mohammed,
na timu yake ya walimu
watano, wakisaidiana kutoa
elimu hiyo ya dini, lakini pia
kuna Madrasa maalum ya
kuhifadhisha Qur an kwa
watoto walio na miaka 5-14.
Imam Matulanga, anaeleza
kuwa kabla ya Shule hizo,
Madrasa ndio zilitangulia na
kulikuwa na utaratibu wa
kuwasaidia kwa kuwalea na
kuwasomesha watoto yatima
hususani wanaozunguka
eneo hilo la Msikiti. Akielezea
namna ya kuwapa watoto hao
yatima alisema, wanawapata
kupitia kwa wazazi wao wa
kike, baada ya kuthibitisha

kwa kuwapatia cheti cha


kuzaliwa mtoto na cheti
cha kifo cha baba hapo na
baada ya uhakiki huo ndipo
wanaweza kumuingiza katika
daftari husika.
Kuanzia hapo tunachukua
jukumu la kumsomesha
kuanzia Shule ya Awali
mpaka hatua ya Sekondari
na ikiwa atafanya vizuri
bado tutakuwa na jukumu
la kuendelea kumsomesha
kwa ngazi ya kidato cha
Tano na Sita, na wale ambao
wanakuwa hawajapata
nafasi ya kidato cha tano,
huwatafutia vyuo vya
Ualimu au kulingana na
ufaulu wake. Alisema Imam
Matulanga.
Anasema, utaratibu huo
chini ya Msikiti, ulianza kwa
kuwakusanya watoto hao
kisha kumwajiri mwalimu wa
kuwafundisha, na kuendelea
nao katika utaratibu huo
mpaka pale ilipoanza Shule
ya Ilala (Ilala Islamic).
Kuanzishwa kwa Shule hizo
Msikitini hapo kuliongeza
chachu ya utaratibu huo
kwani baada ya kuanzishwa,
miongoni mwa watoto hao
waliokuwa na sifa za kuanza
Shule, walijiunga moja kwa
moja wakiwa ni miongozi
mwa waanzilishi.
Baada ya ujio wa shule
hiyo waligawana majukumu
ambapo upande wa Shule
wamechukua jukumu la
kuwasimamia katika elimu na
wao kama Msikiti wamebakia
na jukumu la kugharamikia
gharama zingine kama sare,
chakula , vitabu pamoja na
madaftari.
Kwa mujibu wa Imam
Matulanga, alisema mpaka
sasa kupitia utaratibu huo,
Msikiti umekwisha wasaidia
watoto yatima wapatao 43, na
ambao wamemaliza elimu ya
Sekondari, mpaka hivi sasa ni
watoto tisa.
Pamoja na kuwakisha
katika hatua hizo, lakini kama
Msikiti huwa wanaendelea
kuwasimamia na kuwasaidi
ikiwa wamefaulu kuendelea
na kidato cha Tano ama
wale wanaopata ufaulu wa
chini huwatafutia vyuo vya
kujiendeleza kama Ualimu
ambapo mpaka sasa wapo
walio hitimu na wanafanya
kazi katika Shule za Serikali
na zile za binafsi.
Masjidi Makuti pia una
vitega uchumi vyake katika
eneo hilo la Msikiti ambavyo
ni vyumba vipatavyo 25,
vilivyokodishwa kwa watu,
sambamba na mradi wa
kufyatua matofali.

8
KAMA msomaji ulivyoweza
kuona, makala niliyonukuu
katika toleo lililopita
hayaongelei lolote kuhusu dini
ya mtu, lakini yamesababisha
shutuma kwa mwandishi wake,
waumini wa dini inayodhaniwa
kuwa ni ya mwandishi na
dini yenyewe. Hali hii ni
mapambano dhidi ya udini,
au ni dhihirisho la uwepo wa
udini nchini mwetu?
Kiongozi mmoja wa dini
nchini Tanzania, Mwadhama
Polycarp Kadinali Pengo,
aliwahi kusikika akisema:
Kama wanaokemea usadi
wangekuwa wanaukemea kwa
dhati wenyewe wakiwa sio
masadi, nchi hii isingekuwa na
usadi.
Katika hali inayofanana na
hiyo, tunaweza kusema: Kama
wanaokemea udini wangekuwa
wanaukemea kwa dhati wao
wenyewe wakiwa sio wadini,
nchi hii isingekuwa na udini.
Nukuu ya pili: Raisi Mstaafu
wa awamu ya pili wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Alhaji
Ali Hassan Mwinyi, aliwahi
kusikika akisema:
Sura ya mtu ni kioo cha
mwingine. Usemi huu aliusema
alipokuwa akiwajibu waliokuwa
wakimtuhumu bila uthibitisho
kuwa alikuwa na upendeleo.
Alisema hivyo akiwa na maana
kuwa huenda bila kujijua, hao
wanaomtuhumu wanajitangaza
wenyewe kuwa endapo
wangekuwa kwenye nafasi
yake (Mwinyi), wangekuwa na
upendeleo.
Kuna mambo anayoyaona
mtu kikira kwa wengine
kwa sababu tu yapo kwake
mwenyewe, na sio kwa sababu
yapo kihalisia kwa huyo
anayetazamwa. Kwa kawaida
mtu muaminifu sio mwepesi
kuwatilia shaka watu wengine
kama ambavyo asiye muaminifu
huwatilia shaka. Ni rahisi,
kwa mfano, mwizi kumdhania
mtu mwingine kuwa ni mwizi
kuliko asiye mwizi anavyoweza
kudhania. Katika hali kama
hiyo, kuna wanaowatuhumu
wengine kwa udini kwa
sababu tu wao wenyewe ni
wadini wanaodhamiria kucha
udini wao lakini wakajikuta
wakiutangaza bila kujijua.
Kuna usemi kuwa,
unapomnyooshea mtu kidole,
vitatu huelekea kwako. Mara
kwa mara tunawashutumu
watu kwa shutuma ambazo
sisi wenyewe tunazo kwa
kiwango kikubwa kuliko hao
tunaowashutumu.
Aidha, katika Injili ya Luka
6.41 hadi 6.42, imeandikwa:
Unawezaje kukiona kibanzi
kilicho katika jicho la mwenzio,
usione boriti iliyo katika jicho
lako mwenyewe? Au, unawezaje
kumwambia mwenzako, Ndugu,
ngoja nikuondoe kibanzi katika
jicho lako, na huku huioni
boriti iliyoko katika jicho lako

AN-NUUR

Makala

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Udini- 6

Kilichosababisha niitwe mdini

RAIS mstaafu awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

mwenyewe? . Toa kwanza


boriti iliyoko jichoni mwako, na
hivyo utaona sawasawa kiasi
cha kuweza kuondoa kibanzi
kilicho katika jicho la ndugu
yako. Maneno kama hayo
yanapatikana pia katika Injili ya
Mathayo 7.4 hadi 7.5.
Njia nzuri na nyepesi
ya kumbadilisha mtu ni
kujibadilisha mwenyewe
kwanza. Sio rahisi kumtaka
mwingine afanye jambo ambalo
wewe mwenyewe hutaki, wala
kutamani kulifanya.
Kwa upande mwingine,
yimiza wajibu wako kabla ya
kudai haki, na utoe haki kwa
mtu kabla ya kumtaka atimize
wajibu. Haki na wajibu ni
pande mbili za sarafu moja.
Hakuna haki bila wajibu kama
ambavyo hakuna wajibu bila
haki. Kuwapo au kutokuwapo
kwa migogoro na migongano
hutegemea kwa kiasi kikubwa
upande tunaoanza kuutazama
katika kuielewa sarafu hiyo.
Ukianza kudai haki kabla ya
kutimiza wajibu wako, na
mwingine akakutaka utimize
wajibu kabla hajakupatia haki
hiyo ndipo mgogoro hutokea.
Kwa upande mwingine, Ukianza
kutimiza wajibu kabla ya kudai
haki na mwingine akaanza
kukupa haki kabla ya kukutaka
utimize wajibu, hakutakuwa na
mgogoro.
Hebu turejee maelezo
yafuatayo kuhusu tamko la
Maaskofu nchini Tanzania
kupitia Jukwaa la Wakristo
Tanzania katika mkutano
wao uliofanyika Kurasini Dar
es Salaam tarehe 06.12.2012.
Najiuliza: Matamko kama haya
humlenga nani na ni kwa faida
ya nani? Kutokana na umuhimu
wa viongozi wa dini kama

walivyo maaskofu, nakuomba


ndugu msomaji uzingatie
yafuatayo:
Kwanza, kabla hujasoma
maelezo haya ni vema utumie
muda mfupi kumuomba
Mwenyezi Mungu kwa imani
yako akuongoze kuutambua
ukweli. Usishawishiwe na
kitu kingine katika kuyasoma
isipokuwa kujua ukweli.
Katika kuujadili, usiongozwe
na kitu kingine isipokuwa kile
unachoamini kuwa ni ukweli au
kinachokuwezesha kujua ukweli,
na katika kuufanyia kazi, daima
uzingatie ukweli.
Pili, muombe akujalie moyo
wa subira na uvumilivu,
akuepushie jazba na mihemko.
Akupe uwezo wa kusikiliza
na kutafakari hoja za wale
unaotofautiana nao kimaoni na
kiimani. Akuwezeshe kuupokea,
kuupenda na kuufurahia
ukweli hata kama katika hali ya
kawaida ukweli huo unauma.
Uamuzi wa kuandika maelezo
haya ulikuwa mgumu sana
kwangu kutokana na ukweli
kwamba ninayokusudia
kuandika yanatofautiana
na matamko ya maaskofu,
watu ambao huaminiwa na
kuheshimiwa sana na jamii
nzima wakiwemo wenye dini
tofauti na yao. Hata hivyo,
kutoyasema nako kunaitesa
dhamira yangu hivyo nimeamua
kuyasema.
Kabla sijaanza, ni muhimu
niwakumbushe ndugu wasomaji
kuwa Historia na hata vitabu
vitakatifu huthibitisha kuwa
uongozi katika dini sio utakatifu
wala ukamilifu. Miongoni mwa
wahalifu wakubwa waliowahi
kutokea duniani wamo pia
waliokuwa viongozi wa dini,
hivyo hatuna sababu ya kuamini
kila lisemwalo au kuelekezwa na
viongozi wa dini bila kulitafakari

kwa akili zetu wenyewe. Kuna


mifano mingi ya viongozi wa
dini kujihusisha na uhalifu lakini
ni vizuri nitaje ile ambayo wengi
wetu tumeishuhudia na bado
tunaikumbuka.
Kwanza, miongoni mwa
washitakiwa katika Mahakama
ya Kimataifa ya mauaji ya
kimbari ya mwaka 1994 nchini
Rwanda ni maaskofu na
mapadri, na baadhi ya mauaji
hayo yamefanyikia makanisani
kwa maelekezo yao.
Pili, hivi karibuni Ulaya,
Kanisa Katoliki lilikumbwa
na kashfa ya viongozi wake
kulawiti na kudhalilisha
kingono watoto waliokuwa chini
ya uangalizi wa kanisa hilo.
Kwa muda mrefu watumishi
wa kanisa hilo wamekuwa
wakiwalinda na kuwachia siri
wahalifu hao hadi watu wengine
nje ya kanisa walipochua siri
hiyo.
Tatu, bado Watanzania
hawajasahau masaibu
waliyopata baada ya kutapeliwa
na kampuni ya kikanisa ya
DECI, maarufu kama kampuni
ya kupanda na kuvuna pesa.
Viongozi wake ambao ni
wachungaji waliwadanganya, na
wengine bado wanawadanganya
watu kuwa DECI ni jibu la
umaskini kutoka kwa Mwenyezi
Mungu baada ya wao kukesha
wakiomba na kufunga kwa
muda mrefu wakimlilia
awaondolee waja wake baa la
umaskini.
Tujiulize: Kama
tungetahadharishwa mapema
kabla ya matukio haya, ni
wangapi miongoni mwetu
wangeamini kuwa yanaweza
kutokea? Ukweli ni kwamba ni
wachache sana, na ndio maana
hata watuhumiwa wa utapeli
wa DECI walipokamatwa
watu waliandamana wakitaka
waachiwe na kuiona serikali
iliyowakamata kuwa ndiyo
isiyowatakia mema wananchi
wake. Baadhi ya wanasiasa
wanaotafuta umaarufu kwa
njia za mkato waliungana na
waandamanaji hao wakidai
serikali inaifungia DECI
kwa sababu ni mshindani
wa biashara za kibenki
zinazomilikiwa na serikali au
zenye maslahi kwa serikali.
Nimetaja mifano hiyo kwa
lengo moja tu la kuthibitisha
ukweli kwamba uongozi katika
dini sio utakatifu hivyo hakuna
sababu, na kwa kweli ni ujinga
wa kiwango cha juu sana,
kupokea maelekezo, hasa ya
kidunia, ya viongozi wa dini bila
kujiridhisha kwa akili zetu kuwa
maelekezo hayo ni sahihi.
Nimetoa mifano inayohusiana
na viongozi wa dini ya Kikristo
sio kwa sababu viongozi wa dini
nyingine ni watakatifu, bali kwa
sababu lengo la makala haya
ni kujibu tamko lao walilolitoa
kwa kutumia nafasi yao ya
uongozi katika dini ya Kikristo.
Ni msisitizo tu kwa wasomaji
kuhusu umuhimu wa kusoma
matamko kama haya kwa
uangalifu kabla ya kuyaamini.

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Dharura kukosa sukari, siyo kupata sukari


Na Juma Jumanne

ASILI ya biashara ni halali


isipokuwa namna ya
ufanyikaji biashara pamoja
na aina ya bidhaa ndiyo
inayoweza kuifanya ikawa
haramu. Mwenyezi Mungu
ameihalalisha biashara na
kuiharamisha riba. Biashara
ikifanyika kwa mujibu wa
maelekezo ya Allah ni ibada
na mwenye kuifanya hupata
malipo. Aghalabu, wengi
katika watu wanapotaka
kufanya biashara huishia
kuangalia faida na hasara ya
biashara anayotaka kufanya.
Kama inalipa basi mtu
hufanya maamuzi ya kuingia
kwenye biashara husika.
Lakini Muislamu hutakiwa
kwenda mbali zaidi ya hapo.
Kabla ya kuangalia faida na
hasara ya biashara anayotaka
kufanya, anatakiwa kwanza
aangalie uhalali wa hiyo
biashara anayotaka kuifanya.
Hichi ndicho kigezo kikubwa
kabisa ambacho Muislamu
hukiangalia na siyo kukimbilia
kuangalia faida na hasara.
Hata hivyo, kigezo hichi
anatakiwa aangalie pia mtumiaji
wa bidhaa anapoka dukani
au mahali popote kwa ajili
ya kununua bidhaa. Namna
iliyo bora ni kuangalia uhalali
wa bidhaa yenyewe kisha
kuulizia bei yake. Siyo unauliza
bei kwanza bila kuangalia
uhalali wa hicho unachotaka
kununua. Ukiulizia bei kabla
ya kuangalia uhalali wa bidhaa,
kisha ukaangalia uhalali
wake, muuzaji atakuchukulia
kwamba umeogopa bei na siyo
uharamu wa hicho ulichoulizia.
Uwezekano wa kula haramu
katika mazingira yetu haya ni
mkubwa zaidi kuliko maeneo
ambayo mfumo wa Allah ndio
unaoshika hatamu. Kwa mantiki
hiyo, tunapaswa kuwa wadadisi
zaidi ili kujiridhisha kabla ya
kutumia ama kufanya kitu
chochote. Tunaweza kufanya
haya kwa kuwauliza maulamaa
wetu.
Ni takribani wiki tatu sasa
toka nchi yetu iingie katika
gogoro la kuadimika na ama
kukosekana kabisa kwa sukari,
hali iliyopelekea kupanda bei ya
sukari ghaa. Baada ya ufuatiliaji
kujua sababu za kutokea hali
hii, ikabainika kwamba kuna
wafanyabiashara wamenunua
sukari wakafungia kwenye
maghala (godowns) na hawataki
kuuza.
Serikali baada ya kubaini

RAIS Dkt. John Magufuli.

WAZIRI Mkuu Mh. Kassim Majaliwa

hilo, ikatangaza kwamba kwa


atakayeendelea kukaa na sukari
na asiitoe atanyanganywa na
kugawiwa wananchi bure.
Tahadhari hii aliitoa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe
Magufuli akiwa kwenye ziara
maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Kama haitoshi, tumeambiwa
kwamba sukari inayoagizwa
kutoka nje haina ubora, hivyo
ni hatari kwa afya zetu. Kuzuia
sukari hiyo, ndiyo namna ya
kudhibiti sukari feki iliyokuwa
ikiingizwa hapa nchini. Hapa
nampongeza Rais wetu kwa
kuthamini afya za wananchi
wake.
Tayari kauli ya Mheshimiwa
Rais imeshaanza kufanyiwa kazi
na watu wamenyanganywa
sukari ikagawiwa wananchi na
taasisi mbalimbali. Naungana
na serikali katika nukta moja tu,
nayo ni kuchukizwa na adha
wanayopata watu kwa kukosa
sukari. Adha iliyosababishwa
na wafanyabiashara kufungia
sukari ndani na kudai hawana
sukari. Hili jambo siyo zuri. Siyo
jambo zuri kwa sababu sukari
ina watumiaji wengi ambao
maisha yao ni ya chini sana.
Kupanda kwa bei kunawaumiza
kwa kiwango kikubwa.
Hata hivyo, pamoja na
tahadhari alizotoa Dr. JPM,
binafsi sikuamini kama kweli
watu watanyanganywa
sukari. Niliamini baada ya
kupitia magazeti na kuona
maneno yaliyosomeka; Sukari
Iliyochwa Yagawiwa Bure.
Maneno haya yanapatikana
katika ukurasa wa mbele kabisa
wa gazeti la Nipashe la jumatatu

tarehe 09 Mei, 2016 katika toleo


lake nambari 0578844.
Halikadhalika, gazeti la Uhuru
nalo kwenye ukurasa wake wa
mbele yakasomeka maneno:
Vigogo Wabanwa Kila Kona,
Shehena Nyingine Yanaswa
Ikipelekwa Machoni; TRA
Yataisha Sukari Ya Magendo,
Yaigawa Bure. Kwa mujibu wa
gazeti hili toleo nambari 22439
la jumatatu tarehe 09 Mei, 2016
kuna maelezo ya kina kuhusu
kukamatwa kwa sukari katika
maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Linaeleza gazeti la Uhuru
kwamba, jumla ya mifuko
800 ya sukari yenye ujazo
wa kilo 50 imekamatwa
ikipelekwa machoni. Sukari
hiyo ni sehemu ya mali ya
mfanyabiashara Haruni Zakaria,
anayetuhumiwa kucha tani
4,579.2, zilizokamatwa hivi
majuzi na Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU).
Ipo pia sukari inayodaiwa
kuingizwa kimagendo nchini
ikitokea Brazil na kuingilia
bandari ya Lindi ikitokea
Zanzibar. Sukari hii iligawiwa
taasisi 13, ambayo inadaiwa
kukia thamani ya Tsh. Mil.
373.5, ikiwa ni mifuko 5,319
yenye uzito wa tani 133.
Kinachonipa tabu hapa
kama Muislamu ni ule uhalali
wa mimi kula sukari hiyo.
Utata huu ndio ulionipelekea
kumpigia simu mmoja katika
Masheikh zetu ili kujiridhisha
kuhusu matumizi ya sukari
hiyo. Hii ndiyo kawaida yangu
kufanya, pindi ninapokutana na
mazingira ambayo hayaeleweki.
Napenda sana kujua kabla ya
kuendea jambo ili nilifanye nafsi

ikiwa imetulia.
Baada ya kumpigia simu yule
Sheikh akasema kwamba yupo
darasani lakini nikamkatisha
kwa kumtaka radhi kwa swali
fupi tu. Akawa amenikubalia
nikamuuliza. Jibu nililopata ni
fasaha na fupi sana. Kwamba
hiyo ni dhulma, hakuna adhabu
ya namna hiyo katika Uislamu.
Nilipokea jibu hili kwa mikono
miwili nafsi ikiwa imetulia
kabisa kwa sababu hata mimi
nilikuwa natarajia kupata majibu
kama hayo.
Kilichonisukuma kuandika
makala hii ni ule ukweli
ninaoujua katika jamii
yetu. Tumekuwa wepesi
wa kuchangamkia mambo
bila kutumia mizani sahihi.
Dhulma hii tusiifanye
kuwa fursa. Hatujui sababu
zilizopelekea wafanyabiashara
hawa kuchukua maamuzi
waliyochukua. Hata kama wana
makosa, bado hukumu hiyo siyo
sahihi. Huwezi kuwafananisha
na wezi au majambazi.
Wanazuia chao.
Pengine tunaweza kusema
kwamba hii ni dharura watu
wamekosa sukari watafanyaje?
Hii siyo hoja ya msingi. Kama
hawataki kuuza waachwe wakae
na sukari yao, itafutwe namna
nyingine ya kuagiza sukari nje
ya nchi. Tambua kwamba huo
unaokula ni moto, na itakuwa ni
majuto kuanzia kaburini mpaka
siku ya qiyaama.
Ikiwa ni suala la kucha
sukari ili ipande bei, basi
oparesheni hii itagusa maeneo
karibu yote ya bidhaa za msimu.
Wafanyabiashara wengi wana
kawaida ya kununua nafaka
mapema ambapo inakuwa ni
nafuu sana na kuweka kwenye
maghala. Bei wanazokuja kuuza
ni karibu mara mbili ya bei
walizonunulia.
Sisi Waislamu, Allah
aliyetukuka ametukataza
kudhulumu wala kudhulumiwa.
Ametukataza kula mali kwa
dhulma. Enyi mlio amini!
Msiliane mali yenu kwa dhulma,
isipo kuwa iwe biashara kwa
kuridhiana wenyewe..
[4:29] .Ametukataza kula kama
walavyo wanyama. Tusifurahie
kupewa sukari ya bure. Hiyo
bure unayoona wewe, kesho
itakutokea puani. Kweli
wamekosea lakini bora tuikose
hiyo sukari kuliko kula haramu.
Bora adha hii ya duniani siyo ya
akhera.
Juma Jumanne (0659 789 468)

10

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Mauwaji Masjid Rahman Mwanza

Tusifanye mchezo na uhai wa watu


Mchezo wenu, mauti kwa Tanzania
Na Omar Msangi

WIKI iliyopita kulifanyika


mauwaji ya kinyama na kutisha
ambapo watu wasiofahamika
walivamia msikiti wa Rahmani
jijini Mwanza, na kuuwa
watu watatu. Taarifa ya polisi
imesema kwamba watu wasio
zidi 15 wakiwa wamecha
nyuso zao, walivamia msikiti
huo wakati wa swala ya Isha
na kuanza kuwashambulia
waumini baada ya kuzima
taa. Waliouliwa wametajwa
kuwa ni Feruzi Ismail Elias,
Mbwana Rajab na Khamisi
Mponda, huku wengine
wakijeruhiwa. Taarifa hiyo ya
polisi iliyotolewa na Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza
ikasema kuwa vyombo vya
dola vinafanya upelelezi ili
kuwabaini wahalifu hao na
kuwakisha katika vyombo vya
sheria.
Kwa upande wa vyombo
vya habari, ukiacha habari za
ziada zilizotokana na kuwahoji
watu waliokuwa eneo la
tukio, ndugu wa marehemu
pamoja na viongozi wa dini na
serikali ya Mtaa, walio wengi
wamewasilisha taarifa kama
ilivyotolewa na Kamanda
(SACP) Ahmed Msangi.
Hata hivyo, wapo baadhi ya
waandishi wamelisherehesha
tukio hilo na kulipa sura ya
ugaidi na kuja na maelezo
kwamba waliohusika na jinai
hiyo ni magaidi wa IS.
Habari zinadai kwamba,
watu waliohusika na mauwaji
hayo wana uhusiano na kundi la
kigaidi la Islamic State (IS).
Aliandika mwandishi
mmoja wa gazeti la kila siku na
kuongeza akisema kuwa kuna
habari kuwa mtandao wa IS
upo katika mikoa ya Mwanza,
Arusha, Tanga na Dar es
Salaam.
Anachosema mwandishi
huyu ni kwamba Tanzania
wapo magaidi wa IS na hawa
ni wale tunaoambiwa kuwa
wanachinja watu kule Syria,
Iraq, Libya bila kumsahau Jihad
John. Lakini pia anasema kuwa
waliofanya mauwaji Mwanza sio
IS wenyewe, bali watu walio
na uhusiano na IS. Kwa hiyo
anachotuambia mwandishi huyo
ni kuwa, hapa Tanzania kuna
makundi mawili ya kigaidi: IS
na watu walio na uhusiano na
IS. Na wote hao inavyoelekea
wapo nchini bila hata vyombo

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mwanza, (SACP) Ahmed Msangi.


vyetu vya dola kujua ila sasa
ndio mwandishi wetu huyu
Sitta Tumma anatufahamisha na
kuvistua vyombo vya dola!
Swali ni je, mwandishi wetu
huyu, taarifa hizi za uwepo
wa IS Dar es Salaam, Mwanza,
Tanga na Arusha kazipata
wapi? Ushahidi gani anao?
Anaweza kutuonyesha japo IS
mmoja au yalipo macho yao?
Lakini muhimu zaidi, anajua
anachokisema? Anawajua
IS ni nani, na nini hatari ya
kutangaziwa kuwa mnao IS
nchini kwenu?
Somo kutoka Syria
Huu ni mwaka wa tano,
machafuko na mapigano
yanaendelea Syria. Wapo watu
wanaitwa Islamic State (IS),
tunaambiwa kwamba ni magaidi
wanaotaka kusimamisha Dola
ya Kiislamu. Toka ilikuwa ni
mzozo wa wa-Syria wenyewe
kwa wenyewe, sasa imeingia
Marekani na NATO kwa
kisingizio kwamba inawapiga
magaidi wa IS. Kutokana na
mapigano hayo, zaidi ya watu

400,000 washauliwa huku


mamilioni wakibaki wakimbizi
na miji kuharibiwa.
Wakati Marekani ilidai
kuwa ipo Syria ili kuwasaka na
kuwaangamiza IS, hivi karibuni
Waziri wake wa Mambo ya
Nje, John Kerry ametishia
kwamba Syria kutakuwa na
vita isiyokwisha kama Bashar
Assad hataondoka madarakani
na kama yale yanayotakiwa
na Marekani katika eneo hilo
hayatatimia. Kerry aliyasema
hayo katika mkutano wa Vienna
(17-nation International Syria
Support Group) uliowakutanisha
wajumbe kutoka nchi 17
kuzungumzia suala la Syria
(Tazama: Kerry Threatens WarWithout-End on Syria.)
Ni kutokana na hali kama hizo
zinazojitokeza katika suala la
Syria/Iraq/IS, mwandishi Finian
Cunningham anasema kuwa
kinachodaiwa kuwa Marekani
inapambana na magaidi wa IS/
Al qaida, ni unaki mtupu. IS
wanatumiwa kama kisingizio
cha kukamilisha regime change
Syria na ndio maana kila siku

IS wanaonekana kupata nguvu


mpaka lengo litimie.
Anyone who has not been
brainwashed by Western media
propaganda knows full well that
the suering of Syria has been
caused by Washington and its
allies sponsoring a covert war for
regime change in that country. The
US pays lip service to defeating
terrorism.
Anasema Finian Cunningham
akimaanisha kwamba, kwa mtu
ambaye hajavurugwa akili yake
na propaganda za vyombo vya
habari vya Magharibi, anajua
kwamba kinachoitwa vita dhidi
ya ugaidi, inatumiwa tu kama
kisingizio cha kuzivuruga nchi
zinazolengwa na mabeberu. Na
kwamba mabeberu hao hawajali
machungu yenu, iwe ni kufa
watu, kutiwa vilema au miji
yenu kuharibiwa kama ilivyo
hali Syria.
Anamalizia kwa kusema
kuwa, kwa walio na akili
timamu, watajua kwamba
huyo anayejidai kupambana
na magaidi, ndio huyo huyo
anayepalilia same terror groups
for its criminal political objectives.

Sura tusiyoijua
tukio la Mwanza
Three Massacred in Suspected
Terror Attack in a Tanzania
Mosque, ndivyo ilivyoripotiwa
katika mtandao wa kijamii
uliopewa jina la Shmuel Yosef
Agnon juu ya tukio la Masjid
Rahmani Mwanza. Lakini kabla
ya kusema lolote, ikawekwa
picha inayoonesha vijana watatu
wakiwa wamecha nyuso zao
wameshika AK-47, nje ya pango
ambalo inadaiwa kuwa ni
moja ya mapango ya Tanzania.
Kisha ikaelezwa kuwa mauwaji
ya Mwanza yamefanyika
baada ya kusambazwa video
ikitahadharisha uwepo
wa magaidi wa IS katika
mapango ya Tanzania na
kwamba duru za ki-intelijensia
zilishatoa tahadhari. Lakini
pia ikaambatanishwa na picha
ya polisi wetu kama kusema
kwamba wanapambana na IS
lakini hawawezi. Shmuel Yosef
Agnon, alikuwa mwandishi
wa Kiyahudi (1888-1970). Ni
kwanini mtandao huo ukaitwa
kwa jina lake, ni swali la
kutafakari. (Soma: Strategic
intelligence had warned of an
imminent threat citing a video
shot by Islamic State in Tanzanian
caves.)
Mwandishi Ludovica
Inaendelea Uk. 11

11

MAKALA

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Tusifanye mchezo na uhai wa watu

Inatoka Uk. 10

Iaccino akiandikia gazeti la


International Business Times
UK, na akitajwa kuwa ni
mwandishi maalum wa masuala
ya Afrika na Mashariki ya Kati,
akiripoti tukio hilo, naye akataja
uwepo wa magaidi katika
mapango ya Tanga. Kwamba
tukio la Masjid Rahman
limekuja baada ya magaidi wa IS
waliojichimbia katika mapango
Tanga kusambaza video ikisema
kuwa watafanya shambulio hivi
karibuni.
Ludovica Iaccino anasema,
The attack occurred days after a
video emerged of masked people
alleging they were the East African
branch of the Islamic State (Isis/
Daesh) group. The people claimed
they were in Tanzania's coastal
region of Tanga.
Nukta ya kuzingatia. Hapa
mwandishi Ludovica Iaccino
anazungumzia East African
branch of the Islamic State.
Ukimwambia akuonyeshe
hao IS Tawi la Afrika Mashariki,
hatakuonyesha. Lakini
akishaandika hivyo, watakuwa
wanalikariri mpaka wengine
wetu huku watalidaka katika
magazeti yao na tutaamini au
tutajidanganya na kujipumbaza
kuwa wapo East African branch
of the Islamic State.
Amesema kweli Nabeel
Naiem akimaliza mahojiano
yake na Al-Maydeen TV juu
ya IS na makundi mengine
yanayodaiwa ya Jihad Syria
aliposema:
They fool you, they keep fooling
you and they enjoy fooling you, not
because theyre smart, but because
youre foolable.
Kwamba mabeberu hawa
na vyombo vyao vya habari,
wanakudanganyeni kwa
propaganda zao na wanafurahia
kukufanyeni wapumbafu, sio
kwa sababu wao ni wajanja sana,
lakini kwa sababu mnakubali, na
hata kufurahia kudanganywa.
Kwanza, niseme kwamba
taarifa kama hizi kwamba kuna
magaidi katika mapango yetu
bila sisi wenyewe wenye nchi
kujua, ni matusi na dharau
kwetu kama nchi na hasa
kwa vyombo vyetu vya dola.
Kwamba wanaweza kutoka
magaidi huko watokako, iwe ni
nchini au nje ya nchi wakapiga
kambi Amboni, hatuna habari
mpaka watuambie akina
Ludovica Iaccino!
Ila la kufahamu hapa ni
kwamba tusije wadhania
Ludovica na wenzake ni
wajinga. Wajinga ni sisi
tunaowanukuu katika magazeti
yetu, bila kutafakari. Wao
wanajua wanalolifanya. Wapo

MAPANGO ya Amboni, Tanga.


kazini.
Yupo mwandishi mwingine
wa Kimarekani David Paul
Goldman, naye kaweka katika
mtandao wake picha hizo za IS
pangoni na kuandika: ISIS In
Tanzanian Caves; Terror Threat
Multiplication.
Sasa soma kilichoandikwa

baada ya kichwa cha


habari na picha hiyo ya
pangoni (Tumenukuu
hapa kwa Kiingereza
kama walivyoandika):
Wanachotuambia akina David
Goldman ni kuwa magaidi
wa ISIS wapo katika mapango
yetu lakini vyombo vyetu vya

ISIS In Tanzanian Caves;


Terror Threat Multiplication
Event Summary
Amid reports of signicant
infrastructure concessions,
SOCMINT, HUMINT, and
OSINT reports of Tanzania
increased presence of Islamic
States (ISIS terrorists) indicates
the country may soon suer
security risks.
A visibly poor video shot
in Tanzanian caves show's
armed youths brandishing
Kalashinkovs and the Islamic
States ag backed by picture/
image evidence validated the
presence of Daesh in Tanzania.
Nonetheless, Harakat AlShabaab Mujahideen (HSM)
also has active cells in the East
African country.
The ISIS video is evidence
that jihadist have set up shop
in Tanzania, a rather docile
member of the East African
community.What are the
ramications of this emergence
of the Daesh in Tanzania?
Analysis
For the past 3 years, reports
of jihadists making inroads
in Tanzania have been either
ignored or the threat neutralized,

as analysts would assume (based


on subsequent events including
arrests of suspected cells). There
are no available records of
counter terrorism operations in
Tanzania. The security forces are
not aptly trained and equipped
to counter the threat posed by
violent extremists.
2016 will be a momentous
year for Dar, to be certain. ISIS
is looking forward to the long
awaited 1st terror attack in
East Africa's key towns (Both
Tanzania and Kenya face the
risk). The uncertainty about the
long term implications of an
implosion of violent extremism
in Tanzania clearly is worrying.
The video of Jihadist training
and heavily armed inside
Tanzania marks, with the clarity
that hindsight brings, the new
inection point, that begs the
following questions;
1.
Is Tanzania capable of
countering violent extremism?
2. Is the country's
intelligence aware of the risks/
threats posed by these jihadist?
3. What are the short term
Cont. Pg. 12

usalama havina habari. Na


wanatutahadharisha kuwa si
muda mrefu ISIS watafanya
shambulio lao la kwanza (Masjid
Rahman???)
Lakini ili tuone umuhimu
ya kuita wataalamu kutoka nje
(FBI, Marines???) kutusaidia
kupambana na magaidi hao
wa ISIS ambao wapo katika
mapango yetu kwa muda sasa,
lakini wenyewe hatuna habari,
David Paul Goldman anahoji:
Is Tanzania capable of
countering violent extremism? Is
the country's intelligence aware
of the risks/threats posed by these
jihadist?
Kwamba je, Tanzania wana
uwezo wa kukabiliana na kitisho
cha magaidi (violent extremists na
jihadists) hawa?
Sasa mwandishi, Mtanzania
mwenzetu unapoandika habari
kama wanavyoandika hawa
akina David Goldman, kwanza,
kama alivyosema Finian
Cunningham, unajitukana wewe
mwenyewe. Unautangazia
ulimwengu jinsi ulivyokuwa
brainwashed, lakini pia
namna ulivyo-foolable. Pili,
unavitukana vyombo vyetu
vya Dola na kuitukana serikali
yetu kwa ujumla. Ulitakiwa
tu ujiulize, kunaweza kuwa
na makundi ya kigaidi katika
mapango ndani ya ardhi ya
Tanzania na vyombo vyetu
vya usalama visijue? Na kama
ingekuwa hivyo, tusingekuwa
na Tanzania tuliyo nayo hivi leo.
Lakini pengine swali la
kujiuliza ni hili, hawa akina
David Goldman ni akina nani
na lengo lao ni nini? Wiki
iliyopita nilieleza juu ya Amina
Abdallah Arraf al Omari na yote
yaliyoelezwa juu yake kuhusiana
na vita inayoendelea Syria
ya kumngoa Bashar Assad.
Nikaonyesha kuwa hapakuwa
na mtu anaitwa Amina
Abdallah Arraf al Omari kama
alivyoelezwa na kusiwa, bali ni
jambo lilibuniwa ukatengenezwa
mtandao ukidaiwa ni wa Amina
na huko zikawa zinawekwa
taarifa za Amina bandia. Sasa
hawa akina David Goldman
wanaotujia na video za IS katika
mapango ya Amboni, wanafanya
kazi kama ya akina Tom
MacMaster na Britta Froelicher
na mtandao wao wa A Gay Girl
In Damascus.
Iko picha moja katika mtandao
anaonekana aliyekuwa Rais
wa Marekani George W Bush
kavaa kilemba akiwa na madevu
kama ya Osama. Kwa mtu
mshamba wa IT ataona ni Bush
kweli kavaa kilemba. Hivyo
hivyo, kwa mwandishi ambaye
hana upumbafu na utaahira wa
Inaendelea Uk. 12

12

MAKALA

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Tusifanye mchezo na uhai wa watu

Inatoka Uk. 10

kujitakia, hawezi kuona picha


na video za akina David za IS
wa Amboni akachukua kuwa ni
ushahidi kwamba kuna magaidi
wa IS Dar es Salaam, Tanga,
Mwanza na Arusha.
Nani ISIS
Kwa anayetaka kujua
ukweli, si jambo gumu kujua
IS ni nani na kwa nini IS.
Hivi sasa tunaambiwa kuwa
IS wanashikilia baadhi ya
miji ndani ya Iraq na Syria.
Wanadhibiti visima vya
mafuta, wanauza, wanapika na
kupakua. Lakini tunaambiwa
kuwa Marekani na washirika
wake NATO kwa zaidi ya miaka
minne sasa, wanapambana na
IS hawajaweza kuwashinda.
Picha inayojengwa ni kuwa
hao ni magaidi hatari sana na
ukiacha kuwa Marekani pamoja
na mabavu yake, inahangaika
nao, lakini pia wana uwezo
wa kuingia mji wowote Ulaya
wakapiga na kuondoka bila
ya kukamatwa. Hivyo ndivyo
tunavyoambiwa na kutarajiwa
tuamini. Na ndio sababu
unakuta habari kama hii ya Sitta
Tumma kwamba IS wanaweza
kuwepo Dar es Salaam bila
Kamanda wetu Simon Sirro
kujua wala Idara zetu za
Usalama!
Hivi sasa si siri tena
kwamba al-Qaeda ilianzishwa,
mwanzo kama Mujahidina
wa kupambana na Mrusi kule
Afghanistan kwa niaba ya
Marekani, lakini baadae ikawa
inatumiwa kama bogeyman
la kufanikisha mipango ya
mabeberu. Ilibuniwa kupigana
proxy wars miaka ya 1980s,
na leo tunaikuta Al Qaeda hiyo
hiyo ikiwa katika makundi
tofauti tofauti kule Syria,
ikiwemo IS, ikifanya kazi ile ile
ya umamluki wa proxy war.(Tazama: Al Qaeda: Heroes of the
Empire By Ulson Gunnar- a New
York-based geopolitical analyst and
writer.)
Dubwana hili al-Qaeda, sasa
laonekana kuzeeka na kuchoka
na lililopitwa na wakati (worn
out and tired), ghaa linabuka
bogeyman jingine likichinja
watu na video kusambazwa
katika YouTube. Hawa
tunaambiwa ndio magaidi
wapya-IS (al Qaeda 2).
Yapo mambo mawili
inatakiwa tuyatathmini
hapa. Kwanza ni hizi video
zinazosambazwa ikidaiwa
kuwa ni IS wanachinja watu.
Ukizitizama ni za ubora wa hali
ya juu, zilizopigwa kitaalamu

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro .


unaweza kusema za viwango
aris al-Irq al-Jamhriyy).
vya Hollywood-quality.
Kwamba kitawaonyesha cha
Hizi ni picha zinazoonyesha
mtemakuni Wamarekani.
kutengenezwa kitaalamu
Kufumba na kufumbua,
kutoka upigaji hadi editing.
Marines wakakiyeyusha. Libya
Jambo la pili ni picha
ilikuwa hivyo hivyo kama
tunayopewa kwamba hawa
walivyofanya kule Panama
IS ni wataalamu wa vita
walipotaka kumngoa Manuel
na wenye silaha kali, na
Antonio Noriega Moreno. Ila leo
hawapungukiwi na silaha kiasi
tunaambiwa eti IS wamekuwa
cha kuwachezesha mchaka
wababe sana wanamtoa jasho
mchaka Marekani na NATO
Uncle Sam!
kwa zaidi ya miaka mitatu. Yote
Kupitia ugaidi wa IS, Iraq
hayo mawili hayawezi kuwa ya
na Syria zinasambaratishwa na
magaidi kama tunavyoambiwa.
inaelezwa kuwa kinachotakiwa
Wakati Marekani inaivamia
ni kukia mahali pafanyike
Iraq mwaka 2003, kulikuwa
ugawaji wa mipaka mipya,
na maneno mengi juu ya
kuwe na vinchi vidogo
ukali wa kikosi cha Saddam
vidogo dhaifu (Shia, Sunni
Hussein kikijulikana kama
na ya Wakurdi) ili iwe
Republican Guard (Kiarabu:
rahisi kudhibitiwa na Israel

ISIS In Tanzanian Caves;


Terror Threat Multiplication

From Pg. 11

and long term implications of


militants insurgency?
What may begin as a small
ISIS movement in Tanzania
is likely to morph into a
national security threat whose
catastrophic ramications
will certainly stop Tanzania
at it's tracks. The video is a
recruitment and 'presence
validation" for both the
hundreds of online Tanzanian
youths who've shown sympathy
and the government of
Tanzania.
While East Africa is not a
security union, the eye's of the
world will fall on Tanzania,
not for the threat posed by ISIS

jihadist who published a video


validating their presence in
the country, but for those who
failed to stop them from setting
up camp in the caves and what
the same security ocers will
do to preempt the threat these
terrorists pose.
It's also highly likely, in the

wake of these events, that


Tanzania security intelligence
services will have to call for
more cooperation with Kenya
and Uganda to prevent an
ISIS implosion in future.
(Tazama: Strategic Intelligence

Service: Counter Terrorism &


National Security Intelligencekama ilivyowekwa na David
Goldman Mei 18, 2016)

halikadhalika kuporwa mafuta.


Na hii inaendana na ule mkakati
maarufu "A New Israeli Strategy
Toward 2000" au A Clean Break:
A New Strategy for Securing the
Realm.
Ukiusoma mkakati huo ni
kuwa nchi za Mashariki ya Kati
zinatengenezewa mazingara
ya kupigana zikamuane damu
mpaka zidhooke. Lakini
pia itajengwa chuki baina
yao ionekane kuwa Shia
hawawezi kukaa nchi moja
na Sunni, Umoja wa Mataifa
uingilie kati, zigawanywe,
Mashia kwao na Sunni kwao.
Kukamilisha mkakati huu,
watatumiwa watu watakaojidai
kuwa wanasimamisha Dola ya
Kiislamu-Sala (IS, lakini ni
mamluki-mercenaries).
IS inapoletwa huku kwetu
inafanya kazi mbili. Kwanza
kupiga propaganda kuwa IS
ndio tishio la dunia hivi sasa
na hivyo kuna kila sababu
jumuiya ya kimataifa kuungana
kuwapiga vita. Kwa hiyo
unahalalisha yanayofanyika
Iraq na Syria au mahali pengine
popote ambapo mabeberu
watataka kuingia kwa kutumia
kisingizio kwamba wanawasaka
IS. Pili kama alivyohoji David
Goldman, akionyesha wasiwasi
kwamba Tanzania haina uwezo
wa kukabiliana na IS, inatumika
kujenga hoja ya kuyakaribisha
majeshi ya mabeberu kuja
kutukalia (kutusaidia).
Unapopiga porojo kwamba
Dar es Salaam na Mwanza wapo
IS, unachofanya ni kuwaita
majeshi hayo. Lakini kabla ya
hapo ni kuita kufanyiwa vitendo
zaidi kama vilivyofanyika
Masjid Rahman ili kipatikane
kisingizio cha kutosha kupatiwa
msaada huo wa kijeshi. Na
hutajua waliofanya. Utabaki
tu kuimba ni watu wenye
uhusiano na IS wala hutaweza
kuwakamata au kuwadhibiti.
Utabaki tu kuvilaumu vyombo
vya dola au kuvihimiza kufanya
hili na lile.
Hebu jiulize, Nigeria super
power ya Afrika, ndiyo ya
kuchezewa na Abubakar
Shekau?
Ukilitafakari hilo kwa
kina utajua kuwa Shekau ni
Bogeyman tu, kama ambavyo
tunaambiwa kuwa Obama
kamshindwa Abu Bakr alBaghdadi al-Husseini alHashimi al-Qurashiy!!!

13

MAKALA
Na Azza Ally Ahmed

ENYI makundi ya Waislamu,


vijana kwa wazee, wanawake kwa
wanaume, matajiri na masikini,
Ramadhaan inakaribia. Umeka
wakati wa kufanya maandalizi
kwa ajili ya kuupokea na
kutekeleza ibada ya nguzo ya nne
ya Uislamu ambayo ni funga ya
mwezi Mtukufu wa Ramadhani,
inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kuna haja kwa kila Muislamu
kutia nia ya kutenda ibada hii na
kuukaribisha kwa moyo mweupe
na upendo wa hali ya juu, huruma
na Mapenzi ya dhati mwezi huu.
Ifahamike tu kwamba ndani
ya mwezi waa Ramadhani kuna
fadhila nyingi na matunda yake
yameshabainishwa na Mwenyezi
Mungu Muumba na Mtume wake.
Kuna falsafa kubwa na pana kwa
wanadamu katika Swaum ya
Ramadhani hapa duniani na hata
kesho akhera. Katika Ramadhani
kuna nafasi kubwa na ya kipekee
ya mja kutubu na kusamehewa
madhambi yake au uovu alioufanya.
Ramadhani ni fursa ya kuomba
na kukubaliwa maombi, ni
fursa ya kurehemewa ni fursa
ya kusameheana na kuombana
msamaha.
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
ni semina, ni darsa na shule kwa
Waislamu na hata waso Waislamu.

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Karibu Ramadhan
Kuna funzo la kujenga moyo
wa huruma si kwa matajiri wala
masikini, kujenga moyo wa
kusaidia hasa masikni na mafukara,
kujenga moyo wa kutoa, moyo wa
upendo, umoja, kujenga afya na
subra kushinda njaa sio suala rahisi
inahitaji subra ya hali ya juu na
mengine mengi.
Pamoja na kueleza hayo
machache yaliyobainishwa, lakini
zaidi ni kwamba fadhila za kufunga
Ramadhani ni kubwa kiasi kwamba
Mwenyezi Mungu ndiye anayejua
na kukadiria kiwango cha malipo
yake, kwani Mola amewahakikishia
kwamba ni Yeye tu ndiye
atayekwenda kuilipa kwa haki
inayotakiwa kulipwa.
Hekma ya ahadi hii ya
Mwenyezi Mungu ni kwamba
ameifanya funga kuwa ibaada
ya siri kabisa baina ya mja na
Mola wake, hakuna mwanadamu
anayeweza kuthibitisha kwamba
fulani amefunga na funga yake
imepokelewa au kukataliwa au
fulani hajafunga wala funga yake
haijapokelewa kwa kuwa kakosa
hiki au kile.
Amesema Mtume (s.a.w),

AN-NUUR

Kila amali njema anayoifanya


mwanadamu italipwa mara
kumi .
Allah (s.w) amesema, Ila
kufunga kwa sababu funga ni
kwa ajili Yangu, na ni Mimi
mwenyewe nitakayeilipa)
kutoka kwa Abu Hurayrah na
kupokewa na Al-Bukhaariy na
Muslim].
Uzuri wa ibada ya funga
ya Ramadhani ni kwamba
inakuja kwa utaratibu na
ustaarabu wake. Mgeni huyu
haki bila kubisha hodi, bila
ya kuwaletea taarifa. Daima
analeta ujumbe wake kwamba
anakuja kutembelea Umma huu,
anazielewa silka na tamaduni za
ugenini.
Ameshaondoka mjumbe wake
Rajab na karibuni ataondoka
mjumbe mwingine Shaaban,
ili kumpisha mgeni karimu
Ramadhan. Basi niwasihi ndugu
zangu tumfungulie mlango wa
tabasamu kubwa huku mioyo
yenu ikiwa wazi kwa faraja

pamoja na kupokea mafunzo


yote atakayokuja nayo na
kutuachia.
Mtume (s.a.w) ametuelezea
kuhusu fadhila za mwezi
huu: Umekujieni mwezi wa
Ramadhaan, ni mwezi wa
Baraka. Imefanywa Swaum
kwenu kuwa ni Fardh, milango

ya Pepo hufunguliwa na milango


ya moto yote hufungwa na
Masheitwan hufungwa.
Umo katika mwezi huu usiku
ulio bora zaidi kuliko miezi elfu
moja. Atakayenyimwa kheri zake
hakika kanyimwa [yote ya kheri].)
(Imepokewa na Imaam Ahmad).
Unadhifu wa matendo ya
Ramadhaan ni kuitimiza amri ya
Swaum bila ya kutafuta hoja. Kwani
Waumini wa kweli husema:
(Tumesikia na tunatii) [SuratulBaqarah: 285].
Itakuwa ni hasara kubwa
kutotilia maamani ujio wa
Ramadhan, tukajifanya hatuoni
wala husikii hadi kushindwa hata
kumfungulia mlango nyumbani na
katika familia zetu.
Hala hala Waislamu jitahidini
kuukirimu Ramadhan na kuwa
sababu ya kuondolewa katika usajili
wa watu wa waovu. Allah ajaalie
wote wenye afya njema kuitekeleza
ibada hii adhimu, ili iwe nusra leo
na kesho Akhera.

Kusameheana mke na mume sababu ya kudumu ndoa zetu

Na Sheikh Kamali Ahmed Hassan


SHUKURANI za dhati anastahiki
Mwenyezi Mungu peke yake,
rehema na amani zimkie yule
ambaye hapana Nabii baada yake.
Toka kwa Aisha (r.a) kama
alivyozungumza Ummu Salama,
kwamba alikuja na chakula katika
sahani yake kwa Mtume (s.a.w)
na Maswahaba wao waliokuja
na chakula Umu Salama akaja
Aisha kwa hasira akapiga sahani
ile kwa jiwe laini na kuivunja
na ikasambaratika, hapo hapo
akakusanya Mtume (s.a.w) vipande
viwili vya sahani na akasema
kuwaambia Masahaba wake,
Kuleni ameona wivu mama yenu.
Kisha akachukua Mtume (s.a.w)
sahani ya Aisha na kuipeleka kwa
Umu Salama na akampa Aisha
ile ya Umu Salama. Hebu tazama
uzuri wa tabia za Mtume (s.a.w)
pamoja na upole, kisha tazama
uzuri wa hukumu zake na huruma
katika jambo hili. Tizama namna
alivyotumia njia ya kutosha kutatua
makosa haya toka kwa Aisha (r.a),

kwa maneno yake kuwa ameona


wivu mama yenu. Naye huku
akiifahamu nafsi ya Aisha na
kuiombea udhuru Mtume (s.a.w)
na wala hakumuadhibu Aisha kwa
kosa hili na wala yeye hakumtukana
Mtume (s.a.w).
Ni kwa nini? Kwa sababu Umu
Salama yeye ndiye aliyekuja katika
nyumba ya Aisha kwa kumletea
Mtume na Maswahaba zake
chakula, hivyo akakadiria Mtume
kitendo hiki na kuamiliana naye
kwa upole na hekima na Bi. Aisha
(r.a) kwa yale yanayomtokea mtu
miongoni mwa madhara ya wivu
kwa uzoefu wake Mtume (s.a.w)
kwa yale yaliyomo katika moyo wa
mwanamke.
Mtume hakumpa adhabu yoyote
Bi. Aisha, bali alibainisha tu kuwa
yeye ni mwenye wivu pamoja na
kuvunja sahani na kufanya vitendo
vyake hivyo mbele ya Maswahaba.
Mtume amesiwa na Mwenyezi
Mungu na hakika ipo juu ya
tabia yake tukufu. Hebu angalia
matumizi ya hekima na tazama
muamala mzuri na laiti haya
yangekutokea wewe, ungekuwa
mume, ungekuwa katika hali gani?
Baadhi ya wanaume
huyachukulia matatizo kama haya
ni chanzo cha kumaliza tatizo kwa
talaka.
Sikiliza juu ya msimamo huu,
imepokelewa kuwa mtu mmoja
alikuja kwa bwana Omari Bin
Khatwabi (r.a) ili ashitakie matatizo
ya ubaya na tabia za mke wake,
akasimama mlangoni kwake
anasubiri kutoka akamsikia mtu
huyu mke wa bwana Omar akiinua
ulimi wake akigombana naye akiwa
kimya wala hamjibu akiondoka
yule mtu akirudi kwake huku
akisema ikiwa hii ni hali ya bwana

Omari pamoja na ukali wake na


nguvu zake naye akiwa ni kiongozi
wa waumini, basi vipi hali yangu
mimi?
Hapo hapo alitoka Bwana Omari
akamuona anaondoka, akamwita
akasema Una mahitaji gani ewe
mtu?
Akasema Ewe kiongozi wa
waumini nilikuja kukushitakia juu
ya ubaya wa tabia za mke wangu
na unyanyuaji wake wa ulimi
kwangu, mimi nikamsikia mkeo ni
hivyo hivyo kwako, nikarudi huku
nikisema Ikiwa hali hii ipo kwa
kiongozi wa waumini na mkewe,
basi vipi hali yangu mimi?.
Akasema bwana Omari, Ewe
ndugu yangu hebu sikiliza yale
aliyowapa Mwenyezi Mungu, mimi
ninavumilia kutokana na haki zake
kwangu, kwani yeye ndiye mpishi
wa chakula changu, na ndiye
muokaji wa mikate yangu, na mfuaji
wa nguo zangu, mnyonyeshaji
watoto wangu, na hayo yote si
wajibu kwake na huutuliza moyo
wangu na kuuepusha na haram,
basi mimi ninavumilia kutokana na
hilo.
Yule mtu akasema (Ewe kiongozi
wa waumini na ni hivyo hivyo
mke wangu. Akasema Omar, Basi
vumilia ewe ndugu yangu kwani
hayo ni ya muda mdogo tu, na
kama mtu atawachukia wanawake
basi hakika mtakichukia kitu hali
ya kuwa kajaalia Mwenyezi Mungu
ndani yake kheri nyingi.
Basi aya hii ni liwazo la ahadi
ya Mwenyezi Mungu kwa kila
mwanamume aliyeonywa kwa
kila anachokichukia kwa mkewe
kusubiri juu ya mtihani huo,
atampa kheri na malipo makubwa
na fungu nono ambalo hakuna
ajuae isipokuwa Mwenyezi Mungu
mtukufu.

Hivyo ndivyo yalivyo maisha


ya wanandoa, kuyataja mazuri
na kuyafumbia macho mabaya
na makosa madogo madogo
ambayo yanaweza kusamehema,
ili kuepusha talaka nyingi ambazo
zinatokea kutoka kwa wanaume
kwa sababu ambazo zinavumilika.
Pale wanaposimamia watu wa
kheri au mahakimu au wengineo
juu ya sababu za talaka ni sababu
ndogo ambazo hazitajwi. Na hivyo
hivyo matatizo mengi ni madogo
tu ambayo humalizwa kwa kwisha
maisha yenyewe ya ndoa, tena kwa
masikitiko makubwa.
Imepokelewa kuwa Aisha (r.a)
amesema alipita mwanamke
mmoja kwa Mtume (s.a.w)
akiwa amemkasirikia, akasema
kumwambia Mtume, Hivi wewe
ndiye unayedai ni Mtume.
Akatabasamu Mtume (s.a.w). Ucha
Mungu gani wa muelekeo kama
huu kwa Mtume ambaye haifanyi
nyumba kuwa ni pepo.
Pale anapokasirika mke mmoja,
ni wajibu kwa wengine kuwa
wapole kwani hali ya hasira ni
sawa na hali ya ulevi, mtu hajui
analolifanya na analolisema kwa
wakati ule.
Basi ninatamani kwa kila
mume na mke kuepukana na kila
maneno mabaya na kuleta hasira
na kukasirisha. Ninatamani kila
mmoja kuyataja yaliyo mazuri kwa
mwenziwe, yenye kupendeza na
kuyafumbua macho yote ya upande
wa mapungufu ya kibinadamu kwa
wote wawili.
Email : eg_islamic_center39@
yahoo.com

14

AN-NUUR

MAKALA/MASHAIRI

JICHO MOJA
Bismilahi awali , shairi ninaanzia
Namshukuru jalali , wasaa kunipatia
Sasa niko afadhali , tungo ninarudia
Jicho Moja Kwenye Dini , Ni Kusahau Akhera.
Sio mashihi Dajali , usije ikadhania
Yeye bado kuwasili , muda haujatimia
Hebu tumia akili, mwishowe utang`amua
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Maana ya jicho moja , kuangalia dunia
Akhera hauna haja , jicho umejifumbia
Jambo hili ni kiroja , akili zimefubaa
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Mungu katupa mawili , macho ya kuangalia
Akhera jicho awali , la pili ni la dunia
Yote yaone kwa mbali , mambo kushughulikia
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Ni mtume Muhamadi , mafunzo katupatia
Dunia hauna budi , nawe kushughulikia
Na Allah umhimidi , kama kesho wajia
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Wenye jicho moja wale , wanatambia dunia
Haramu, halali wale, matumbo kujishibia
Wanadhaia milele , duniani kubakia
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Dunia wameipenda , mola wamemkataa
Sheria wanaziponda , Allah alowatungia
Za kwao wameziunda , wayapate manufaa
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Macho mawili hakika , hao wamejitambua
Dunia wanaitaka , na akhera yao pia
Wanaishi kwa mashaka , wasimuudhi jalia
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Vipi unajicho moja , mtu akikuambia
Nawe ukaleta hoja , kwamba hakuangalia
Ndugu yangu kuna haja , haraka kujikagua
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Wale wenye moja jicho , warudi kwake Nabia
Kulifumba lao jicho , wajue wajisumbua
Kilema chao cha jicho , wenyewe watajutia
Jicho Moja Kwenye Dini Ni Kusahau Akhera
Kalamu naweka chini , nami kujikiria
Hivi kweli nitawini , mawili kuyatumia
Yailahi ya manani , ndiye wa kusaidi
JICHO MOJA KWENYE DINI NI KUSAHAU
AKHERA
ZABIBU IDDI NG`ONDA
MWANZA

FITNA! FITNA! FITNA!!!


Mengi sitaki kunena, mintarafu mauwaji,
Yalojiri wiki jana, katika la Mwanza jiji,
Wilayani Nyamagana, tafakuri yahitaji!
FITNA HII HATARI, TUSIPOKUWA MAKINI!
Kwa watu mufakirina, kuna mengi ya kuhoji,
Yanohitaji wa kina, si rahisi ujibuji,
Uso majibu mwanana, bali ubabaishaji!
FITNA HII HATARI, TUSIPOKUWA MAKINI!
Tumuombe Subhana, wa siri Mkashifuji,
Aikashifu bayana, kunga yao wauwaji,
Waijue alamina, na dhati ya mauwaji!
TUWENI NAYO MAKINI, FITNA HII HATARI!
ABUU NYAMKOMOGI

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Chuki kamwe haitakuwa na maslahi kwenu - 2


Na Shaban Rajab
MWENYE tabia ya chuki
husababisha kufungulia
milango ya kuchukiwa
na watu. Japokuwa
watakuwepo watu au
kikundi cha watu au
watu wa imani fulani
watakaoona na kuamini
kuwa wananufaika na
matokeo ya vitendo vya
chuki vya kiongozi wao.
Hata hivyo ukweli
utabakia pale pale kwamba
kila mtu atapendwa na
ataheshimiwa na wengine
kwa kuamini katika haki
bila kujali matabaka
ya watu. Vivyo hivyo
mtu huyo anategemewa
awapende na ahifadhi
heshima za wengine pia
na ajiepushe kabisa na
kila jambo linalokwenda
kinyume na maingiliano
mazuri au linaloweza
kusababisha kuharibika
kwa maelewano na
wengine.
Maradhi ya chuki na
uadui ni miongoni mwa
maafa makubwa dhidi
ya ufanisi na utulivu wa
nafsi, yanayotokana na
tabia mbaya ya hasira ya
kushindwa katika medani
ya kutafuta maisha au
kushindwa katika kile
unachokitafuta katika
kuboresha maisha.
Lakini kubwa zaidi ni
mtu kukosa uvumilivu
wa kiimani, kushindwa
kuheshimu imani za watu
wengine kwa kra kwamba
yako ni bora na inastahili
kufuatwa na kila mtu.
Imani yako haistahili
kufunzwa kwa hoja, na
akitokea mtu akahoji
kabla ya kukubali, huyo

atachukiwa na hata
kutafutiwa namna ya
kumdhibiti.
Kushindwa huku
katika hoja za kujifunza
mtu, humfanya mhusika
kupata hamaki na
kuchukia na kujenga
uadui. Mtu mwenye
moyo dhaifu na mwepesi
wa kuhamaki havumilii
kusikia akikosolewa
au akichambuliwa hata
kidogo.
Hamaki ni matokeo ya
chuki iliyojengeka kiasi
cha kuwa kama moto
uliofunikwa chini ya
majivu, ambao unaweza
kutoa cheche za uadui
zitakazounguza na
kuteketeza ufanisi na
utulivu wa nafsi.
Bila shaka kutozijali
hisia za watu huleta
matokeo mabaya ya
kudharauliwa na wengine
na kuonekana ni mtu
duni usiyefaa katika jamii
za watu wastaarabu na
wasomi.
Kama vile ambavyo
kusamehe kunaonyesha
utukufu na umakini wa
nafsi ya mtu pia kunaleta
usalama na umoja na
utulivu wa nafsi, vivyo
hivyo, uadui na uhasama
kunapelekea kuwa na,
chuki ambayo huzaa
mfarakano na ugomvi.
Ingawa uhasama hufanywa
ili kutuliza misukosuko
ya ndani ya nafsi, lakini
madhara anayopata mtu
kwa kulipiza ubaya kwa
ubaya huwa ni makubwa
zaidi kuliko madhara
anayopata kwa njia
nyingine, kwani maudhi
licha ya kuwa ni shida
kuvumilia, mwisho wake
huondoka, lakini uhasama
unapoota mizizi huchoma

moyo wa mtu kama miba


ya sumu na humdhuru
daima.
Isitoshe, uadui hauwezi
kuondoa ubaya. Bali
hulipanua na kulichimba
zaidi donda. Kwa kawaida,
uhasama humfanya
hasimu ajitetee zaidi
na alipize kisasi zaidi,
akitegemea kupata utulivu
wa nafsi, kumbe ndio
anajirimbikizia machungu
ambayo humletea
maradhi ya saratani ya
akili na kupelekea kuwa
na maamuzi yasiofaa
na yaliojaa visasi na
chuki. Kutotumia akili
na kutokiria matokeo
mabaya ya kufanya
ugomvi, akikiria kwamba
anamkomoa mtu kumbe
anajikomoa mwenyewe.
Watu wengi
wanashindwa kuelewa
kwamba kushikwa na
hasira sana ni dalili ya
kutopevuka kiakili, kwani
huenda mtu anayekosoa
huwa hana nia ya
kumtukana au kumdharau
mwenzake. Uchambuzi
uliokusudiwa kuudhi
na kudharau, kama una
ukweli na unaonyesha
kosa lenyewe, basi huwa
ni zinduo na funzo kwa
mwenye akili badala
ya kuwa chukio. Lakini
uchambuzi usiokuwa na
msingi na ukweli usitiwe
maanani, kwani unatokana
na husuda na ubaya.
Kitendo cha kuchambua
bila ya msingi wowote ni
kitendo cha kitoto, chuki
na wivu chenye lengo la
kujitukuza kuwadharau
wengine. Hata hivyo,
tusikereke na watu kama
hao, bali tuwafunike kwa
shuka ya kuwapuuza bila
kuzozana nao.

KAMATI YA KUENDELEZA UISLAMU darpwani


S.L.P 55014 Simu: +255 673 497970 , +225 713 631 419 , +255 716 058 538
Website:www.kkuttz.com Email: kkudarpwani@gmail.com

Assalam aleikum warahmatullah wabaratuh


Kamati ya Kuendeleza Uislamu Dar Pwani inawatangazia Waislamu wote wake kwa waume kuwa
Kutakuwa na Program maalumu ya ufahamishaji wa program mbali mbali za kamati katika misikiti
mbalimbali ya Dra es salaam na pwani kama inavyoonekana hapa chini;
NA

TAREHE

DHUHRI

07.06.2016

ISTIQAMA KAWE

TAQWA - MWANANYAMALA

L-ASRI

2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20

08.06.2016
09.06.2016
10.06.2016
11.06.2016
12.06.2016
13.06.2016
14.06.2016
15.06.2016
16.06.2016
17.06.2016
18.06.2016
19.06.2016
20.06.2016
21.06.2016
22.06.2016
23.06.2016
24.06.2016
25.06.2016
26.06.2016

HAQ ILALA
TUNGI TEMEKE
MUHLISINA KIGAMBONI
LILAH MKURANGA
TAQWA CHALINZE
ISLAMIA KISARAWE
MWANALUGALI KIBAHA
NUR MLANDIZI
MOZA BAGAMOYO
MSIKITI MKUU KIBITI
TAQWA RUFIJI
TAQWA KIGAMBONI
KEKO FENICHA TEMEKE
KIBAMBA CCM KINONDONI
MAKUTI(RAHIIM) TANDALE
IKHWAN ILALA
KWA GUDE-KIWLNI/ILALA
NGUVU KAZI CHANIKA
MSIKITI MKUU MAFIA

HIJRA - TEMEKE
CHIHOTA TEMEKE
MJIMWEMA KIGAMBONI
MUHAMMAD MKURANGA
ASADI CHALINZE
FARAJI KISARAWE
MSIKITI WA MKOA KIBAHA
QADRIYA - MLANDIZI
FIRDAUS BAGAMOYO
MSIKITI WA SOKONI - KIBITI
JAMAA RUFIJI
SAKINA KIGAMBONI
BADRI TEMEKE
AL AMIN MANZESE/KINONDONI
NUR - KIGAMBONI
ISTIQAMA ILALA
MASHINE YA MAJI GMBOTO/ILALA
HIJRA - TEMEKE
KIGAMBONI - MAFIA

Waislamu wote mnaombwa kuhudhuria katika program hii ili kuelewa kwa upana Nini kamati ya
kuendeleza uislamu na Inafanyaje kazi zake.
Mnaomba kuhudhuria bila kukosa.
Wabillahi Tawfiq
Kaimu Amir - Rajabu Ngalongela

15

AN-NUUR

SAFU YA BEN RIJAL

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Wanyama waliotajwa katika Quran: Mbwa-5

Na Ben Rijal
KATIKA makala haya yatamurika
juu ya mbwa ajulikanavyo katika
uga wa sayansi na vijana waliolala
katika pango na ushuhuda wa
kisayansi. Kila lugha humwita
mbwa kwa jina lake. Kiengereza
humwita dog, Albania qen,
Africana hond, Kiarabu kalbu,
Bemba wao humwita Imbwa,
Wabengali Kukur, Bosnia
anajulikana kwa jina la Pas,
Cambodia Jakay, Wachima Gou,
Wadenish Hund, Watu wa Fiji
humwita kolil, Wayunani Kyon,
Gujarati kutto, Hausa kare
(http://www.dogbreedinfo.com/
languages.htm).
Mbwa katika kila kona ya dunia
ana majina yake na katika lugha
nyengine wameenda mbali zaidi
kwani mbwa wa kiume ana jina
lake na wa kike ana jina lake,
anapokuwa mdogo ana jina lake
anapokuwa na mimba ana jina lake,
ila kwetu Kiswahili mbwa ni mbwa
tu, mtoto wa mbwa, mbwa jike,
mbwa ana mimba, hana jina jengine.
Kwa kitaalamu katika uga
wa sayansi jina la mbwa huitwa
Canis lupus familiaris au Canis
familiaris wakiwa katika familia
ya Canidae. Tuliposoma katika

makala mbili zilizopita tulimsoma


mbwa katika Quran aliofwatana
na vijana kuukimbia utawala
wa mfalme aliokuwa dhalimu
akiabudu masanamu, vijana kama
tulivyokwisha ona ndio wanaoleta
mabadiliko duniani, wazee mara
nyingi huwa waoga kwenye suala
la mabadiliko ila vijana ndio
husimama kidete na kuona potelea
mbali.
Mapinduzi mengi duniani hata
barani Afrika yaliongozwa na
vijana wakiwa na umri mdogo iwe
Marehemu Muamar Ghadda wa
Libya, Jerry Rawlings wa Ghana,
Thomas Sankara wa Burkina Fasso
na wengineo, hao wote walikuwa na
umri mdogo na kuona kuwa kuna
haja ya kuleta mabadiliko na hao
watatu niliowataja hakika waliweza
kufanikisha mabadiliko makubwa
katika nchi zao ingawa Gadda
alikaa muda mrefu kwenye utawala,
lakini Captain Thomas Sankara
alichukua muda mfupi kabisa muda
wa miaka 4 na kuibadilisha nchi ya
Burkina Faso na kupiga maendeleo
ya haraka na kuwashtua mabeberu
kuona kasi yake ya mabadiliko na
kutafuta vibaraka na vikaragosi
na kumngoa kwa mapinduzi
yaliowarejesha nyuma Wabukinabe.
Vijana wa pangoni
Kwanini vijana wa Pangoni
waliamua kuukimbia utawala
wa kidhalimu? Sababu ni moja
tu nayo imani yao ilio thabiti.
Hawakuwa tayari kuyasujudia
masanamu kama walivyotakiwa
na mfalme Diqyanus. Vijana

hawa waliona kinachofwatwa


na huyo mfalme sicho wakawa
wanakipinga. Mfalme huyo baada
ya kufahamu kuwa kuna vuguvugu
la vijana wanakwenda kinyume
na imani anayoifwata, ilibidi
kuwaita ili waungame kama kweli
wanamkhalifu kiongozi wao.
Ujasiri wa vijana
hawakutetemeka bali kwa pamoja
wakasimama na msimamo wao
wa kusema ni ndio hawaabudu na
kuwasujudia masanamu. Mfalme
akawatisha kuwa atawaua akawapa
siku moja wakakae wabadili imani
yao hio na kurudi katika ibada
ya wazee wao waliopita ambayo
inaendelezwa na mfalme huyo.
Vijana wakaweka bunge lao la
kujadili nini cha kufanya kwa umoja
wao msimamo wao haukuwa wa
kutetereka ila walisimama na imani
yao kutoyasujudia masanamu, iwe
itavyokuwa, potelea mbali, bora
kufa waliona kuliko kufanya hivyo,
wakakia uamuzi wa kukimbia.
"Vijana hao walipo kimbilia
kwenye pango walisema: Mola wetu
Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako,
na tutengezee uwongofu katika
jambo letu. (18 :10)
Vijana hao wakaamua kukimbia
na mbwa wao ajulikane kwa jina
Kitmir ila tu walimuomba Mola wao
wapate rehma na kuwa na moyo
thabiti katika harakati zao za kuwa
na imani ya Mungu ni mmoja.
Hakika idadi yao haikuwa
inatambulikana. "Watasema:
Walikuwa watatu, wa nne wao
ni mbwa wao. Na wanasema:
Walikuwa watano, wa sita wao ni

mbwa wao. Wanavurumisha ovyo.


Na wanasema: Walikuwa saba, na
wa nane wao ni mbwa wao. Sema:
Mola wangu Mlezi ndiye anaye jua
sawa sawa hisabu yao. Hawawajui
ila wachache tu. Basi usibishane
juu yao ila kwa mabishano ya juu
juu tu hivi. Wala usiulize khabari
zao kwa yeyote yule. Idadi sio
muhimu kuijuwa lilokuwa ni
muhimu kuweza kufahamu namna
walivyookoka.
Na walikaa katika pango lao miaka
mia tatu, na wakazidisha tisa. (18:25).
Ni miaka waliokimbia na kuingia
kwenye pango na kulala kwa kifupi
walilala kwa karne 3 na zaidi.
Sema: Mwenyezi Mungu anajua
zaidi muda walio kaa. Ni zake tu siri
za mbingu na ardhi. Kuona kulioje na
kusikia kwake! Hawana mlinzi isipo
kuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote
katika hukumu yake (18:25)
Walilala siku zote hizo. Jee
tutawezaje kuthibitisha hayo? Jee,
kuna njia yoyote ile ya kisayansi
itatuambia hivyo? Muislamu
anayakubali moja kwa moja hayo
lakini bado kwa wale wenye tembe
ya kuona hayo hayawezekani, ndio
sasa naonelea kujaribu kuja na hoja
za kisayansi.
Aina zote za wanyama hulala
kwani kulala ni kipumzisho
baada ya harakati nyingi kiumbe
anazozifanya na hasa katika
kutafuta kijio chake, viumbe
vyote hulazimika kupata kijio
ndio waweze kuishi, mwanadamu
hufanya kazi mbalimbali katika
kutafuta kupata kijio, wengine

Inaendelea Uk. 16

Jee, tuwe kunguru au tafrani za panya?-3


KATIKA makala mbili zilizopita
tulijaribu kutafuta mwelekeo wa
kuzungumzia uvaaji wa Kata K
bila ya kugusia chimbuko lake na
kushamiri uvaazi huu duniani.
Katika makala haya ya kumalizia
tutalizungumzia chimbuko na
kukhitimisha uvaazi uliokuwa sio
wenye nidhamu na muruwa.
Mvaaji wa Kata K hujulikana
kwa jina la Sagger aidha katika
baadhi ya sehemu duniani uvaaji
huu huitwa Kivazi cha mchupo.
Kivazi cha Kata K chimbuko lake
ni kule Marekani ambapo kulikuwa
na wafungwa wengi mno ambao
wakikia kuamua kujiua kwa
kutumia mikanda ya suruali baada
ya kuona ni adha ya kuselelea
gerezani na hasa ukizingatia
wengi wao walikuwa ni jamii ya
Wamerekani Weusi ambao baadhi
yao walitiliwa chonza na kufungwa
(kubambaziwa kesi).
Wakuu wa Magereza kuona
kuwa idadi kubwa ya wafungwa
huamua kujitia kitanzi kwa kutumia
mikanda ya suruali, ikakia kuwa
wafungwa hawapewi mikanda na
hupewa masuruali mabwanga na
wanapoyavaa huwa yanaonyesha
chupi, kwa kweli haikuwa ni ya

kuwafurahisha lakini ilikuwa ni


jambo limeamuliwa na hawana budi
nalo. Kwa hio, wengine wakijaribu
kuzipiga pindo suruali zao, lakini
wengi wakiamua yawe yatayokuwa
watazivaa kama walivyopewa ikiwa
kila wakati zinaonyesha suruali zao
za ndani.
Wengine walikuja na nadharia
kuwa waliokuwa wakivaa Kata
K ni mashoga kuwatambulisha
wengine kuwa wao ni wenye
kufanya amali hio, maelezo haya
hayana uzito, kwa kuwa wana
historia katika tati walizozifanya
walikuja kugundua kuwa uvaaji
huu ulikuwa ni suluhisho huko
magerezani watu kutojiua kwa
kupewa mikanda.
Wanawake katika baadhi ya
sehemu duniani nao wameingia
katika uvazi huu wa Kata K
na kuonyesha nguzo zao za
ndani za siri na hata huku kwetu
tumeanza kushuhudia uvazi huu
kwa wanawake. Ukweli ni kuwa
wanawake wenye kujiuza miili
yao, ndio walio wengi katika
kivazi hichi. Hakika uvaazi huu
unakirihisha na una udhi kikweli
kweli na unahitaji kupigwa
marufuku na kuadhibiwa wale

wavaao, kwani unatupeleka nje ya


maadili yetu.
Maudhi yamewakisha
wapi wanaongoza?

Mwanamama alio kiongozi


katika kitongoji cha Ocala, Fla huko
Marekani alichoshwa na kuona
uvazi wa Kata K umeshamiri
katika eneo analoishi, kwa hio
akafanya awezavyo kuona uvazi
huu unapigwa marufuku katika
eneo lake na katika mwaka wa 2014
katika mwezi wa July, eneo la Ocala,
Fa ulipigwa marufuku uvaazi huu
na yoyote yule atayekutikana kavaa
vazi hilo alipigwa faini ya $ 500
sawa na Shillingi milioni mmoja za
Kitanzania au kwenda korokoroni
kwa mwezi mmoja.
Katika mji wa Wildwood, N.J.
Mayor wa mji alifanya awezavyo
kuona uvazi huu katika eneo
analoliongoza hauvaliwi. Huko
Marekani ambapo ndio chimbuko la
kivazi hichi nako kimeshawachosha
wazee kuona wana wao wanavaa
kivazi hichi kisichokuwa na
heshima. Kwetu wazee wapo kimya
kama sio jambo lenye kukirihisha.

Inaendelea Uk. 16

MSANII akishangiliwa na
kivazi cha Kata K

16

SAFU YA BEN RIJAL

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Jee, tuwe kunguru au tafrani za panya?-3


Inatoka Uk. 15
Kitu gani kilichofanya Kata K
kupendwa na vijana? Vijana wengi
wameathirika na mziki na mziki
waupendao ni ule wa kupwayuka
ujuliknao kwa jina la Hip hop na
ule wa Reggae ambao umeshamiri
katika nchi za West Indies hasa hasa
katika nchi ya Jamaica. Mziki wa
Hip hop ni burudani kwa vijana
wengi ambao hata wanapoziimba
hizo nyimbo hujua kuziimba
lakini hukosa kujua maana ya
hizo nyimbo nyengine huwa
wanajitukana wenyewe.
Katika miaka ya 90 uvaaji wa
Kata K ulianza kuvaliwa na
waimbaji wa Hip Hop na kasi yake
ikawa kubwa. Ilipoka mwaka wa
2010 waimbaji maarufu kina Justin
Bieber, Liam Payne, Ross Lynch na
wengineo walikuwa wanapotokea
katika majukwaa ya muziki, huwa
na kivazi cha Kata K.
Katika miaka ya 90 waliokuwa
wakivaa Kata K wakivaa suruali
za ndani za zile suruali ambazo
wapiganaji wa masumbwi huvaa
wakati wa mapigano lakini kukia
mwaka wa 2010 mtindo wa Kata
K ukawa na kivazi maalumu
nacho ni kivazi cha madengirizi
(Jeans) za kubana. Uvaazi huu
kwasasa sio umeshamiri nchini
Marekani tu inasemekana
umehamia na Uiengereza katika
mwaka wa 2016 utati uliofanywa
nchini humo imekuja kuonekana
asilimia 35 ya watoto wa kiume
huvaa kivazi ya Kata K wakiwa
wengi ni wenye umri wa kati ya
miaka 13 na 16 na vijana wa kike
wakao asilimia 65 wenye umri
baina ya miaka 13 na 18 wamekiri
kuwa kivazi cha Kata K ni kivazi
muruwa na chenye kuwavutia.
Mziki wa Video
Mziki wa Video (Music video)
umekuwa maarufu duniani
kote, raha ya mziki huu kama
wasemavyo vijana ni kumuona
mwana muziki anavyoimba kwenye
video, mbali na zamani ukiwa
unamsikia tu mwanamuziki bila ya
kumjua na nini anafanya nini?
Kuandaa mziki wa video ni
ghali, huunganishwa picha
zilizopigwa sehemu mbalimbali
na kumfanya msanii anaonekana
amebadilisha nguo na kuwepo
sehemu mbalimbali, nyimbo mmoja
inaweza kumuonyesha msanii yupo
katika sehemu mbalimbali hata nchi
mbalimbali na amebadilisha nguo
hata kukia mara kumi.
Wasanii wengi katika miaka
hii hupendelea kukisha jumbe
zao kwa kutumia mziki wa video
ili kuleta mvuto zaid. Mwaka
wa 1996 ulikuwa ni mwanzo wa
kudhihirishwa mziki wa video
kupitia uvazi wa Kata K kupitia
nyimbo ya Back Pockets on the
Floor ilioimbwa na kutengenezwa
na Green Brothers wa Highland
Park wa mjini Michigan. Onyesho
hili kupitia mziki wa video
uliwavutia wengi na kuushabikia.
Aidha katika mwaka wa 2007
msanii Dewayne Brown wa mji wa
Dallas uliopo Texas akaja na kibao
Pull Your Pants Up, ilipoka

mwaka wa 2012 mwimbaji wa rapu


kijana wa miaka 9 Amor Lilman
aliandika nyimbo Pull Ya Paints
Up na kuingiza katika mziki
wa video (https://www.youtube.
com/watch?v=dF_wiHSeRY4) na
kuwatia wazimu vijana wenzake na
kushabikia Kata K kwa kiwango
cha juu.
Nasaha kwa vijana
Sio kila kiingiacho mjini sio
haramu. Kwa kweli kuna mambo
tunahitajika tujitahidi kwa kadri
tuwezavyo kujiepusha nayo hasa
kwa vijana wa Kiislamu. Dini ya
Kiislamu ina mipaka yake mpaka
Utupu wameutolea kielelezo chake
(Dnition) na kuugawa baina ya
mwanamume na mwanamke.
Mwaname utupu unahesabiwa
baina ya kitovu na magoti, kuanzia
kwenye kitovu hadi kwenye magoti
huhesabiwa ni utupu na hapo hata
kufanya ibada hakukubaliki. Kwa
mwanamke utupu kwake ni mwili
mzima isipokuwa uso na viganja
vyake viwili. Sababu ya mwanamke
kuekewa mipaka hiyo ni kuwa
kila sehemu yake ni yenye mvuto.
Uislamu umejaribu kumlinda
mwanamke wala sio kumdhalilisha.
Avaapo kata K kijana wa
kiume hakika huwa anajidhalilisha
yeye, wazee wake na dini yake
ambayo imemuweka na kumjenga
kuwa mtu alio na muruwa. Hakuna
sababu hata mmoja ya watu kutaka
kuona suruali ya ndani iliovaliwa
na kijana wa kiume, aidha kwa
wanawake ndio kabisa ndio
anahitajiwa ajisitiri vilivyo.
Tati katika nchi za Mrekani na
Ulaya zimeonyesha kuwa baina ya
mwanamke aliojistiri kinavyotakiwa
na Uislamu na wale wasiojistiri,
idadi ya wanaobakwa ni kubwa kwa
wale wasiojistiri ila tu wanawake wa
Kiislamu wanaojistiri huhujumiwa
kwa zile chuki za ubaguzi lakini sio
kwa uvazi wao.
Katika toleo la kwanza juu
ya mada hii tulitoa Kisa cha
kunguru na kile cha panya, wote
hawa wawili katika hikaya za
hikma tulizozisoma huko nyuma
zimetuonyesha kuwa ukijaribu
kuiga kila kitu mwishowe
utaambulia patupu. Kwani kunguru
alitaka kuwaiga kila ndege walivyo,
mwishowe alijikuta hata ile asili ya
mwendo wake aliipoteza na panya
alileta tafrani walipokuwa safarini
na kila alipokuwa anakatazwa
na sungura hakuwa ni msikivu,
matokeo yake walikuja wakazama
wote. Na sisi wazee kama tutajikalia
kimya pasi kuwakataza vijana wetu
na vitu kama hivi Kata K tujuwe
ka kuwa sio wao tu watapotea
kwani na sisi tutaingia kwenye
mkumbo huo wa kutojua nini
tamaduni zetu na nini Uislamu
wetu utuongozavyo.
Makala haya yalijaribu
kuonyesha uvaazi huu umetokea
wapi na kuonyesha dhahiri kuwa
hao waliokuwa gerezani wakivaa
mtindo huu ilikuwa sio kwa
mapenzi yao ila yaliwakuta tu
kutokana na amri za wakuu wa
magereza. Tumeona aina mbili
ya kivazi hichi nayo ni kuwa

Uvazi gani huu usio na ihtiramu na nidhamu?


wafungwa wakivaa kutopewa
mikanda wasije wakajiua na jengine
ni kuwa ilikuwa ni aina ya ushoga
ingawa kauli hii haina nguvu. Iwe
itavyokuwa, kwa nini lilobaya

tulivae ikiwa vivazi vizuri na


vilivyo muruwa vimejaa?
Fwatana na mie katika makala
ijayo juu ya kujichora mwili Tatoo
chimbuko lake na kuenea kwake.

Wanyama waliotajwa katika Quran: Mbwa-5

Inatoka Uk. 15

hulima, wengine husomesha,


wengine huwinda, wengine
huendesha magari almuradi
mihangaiko. Hayo yote azma yake
ni kuweza kupata kijio.
Kuna aina ya wanyama huwa
katika harakati kubwa mchana
ikapo usiku hulala (Diurnal).
Kundi hili ni binadamu, ngombe,
mbuzi, ngamia na wengineo na
kuna baadhi ya wanyama wao
hulala mchana na usiku ndio huwa
saa zao za harakati (Nocturnal).
Wanyama hao wakiwemo popo,
bundi, komba n.k. Viumbe hawa
unapojaribu kuwabadilisha wa
mchana wawe wa usiku na wa
usiku wawe wa mchana, inakua ni
vigumu na hata ukiwalazimisha
baadaye huja wakaathirika.
Vijana wa pangoni (Ashab Kahf)
wao walilala takriban karne 3,
Quran inatuambia Quran:
Na unaliona jua linapo chomoza
linainamia kuliani mwao kutoka
hapo pangoni; na linapo kuchwa
linawakwepa kushotoni, na wao
wamo katika uwazi wa pango.
Hizo ni katika ishara za Mwenyezi
Mungu. Ambaye Mwenyezi Mungu
anamwongoa basi huyo ni mwenye
kuongoka. Na anaye muacha
kupotea basi hutampatia mlinzi
wala mwongozi. (18:17).
Nawe utawadhania
wamacho, na hali wamelala. Nasi
tunawageuza kulia na kushoto. Na
mbwa wao amenyoosha miguu
yake ya mbele kizingitini. Kama
ungeli watokea hapana shaka ungeli
geuka kuwakimbia, nawe umejaa
khofu. (18:18).
Hapa sasa tutaangalia Quran
inavyotueleza na Sayansi
inavyotuambia. Tuanze kuangalia
usingizi na makataa yake.

Tunapolala kuanzia usingizi


unapokuwa na lepe, ukasinzia,
kisha ukalala, hapo usingizi huwa
na makataa yake ambayo mwenye
kulala huyapitia.
Tunapolala kila siku huwa
tunapitia hatua 5 au 6 za usingizi,
ikiwa lile kataa la usingizi
haujakolea, usingizi wa kati na
ule ulio mzito uliojaa mikoromo
ambayo wataalamu huita alpha,
beta na gama.
Usingizi ulio mzito uliokolea
mara zote hufanya harakati za
mwili kuwa polepole pamoja na
mapigo ya moyo, na hata presha
ya damu nayo huwa ya wastani.
Unapokuwa katika hali hii inakuwa
katika kitu kinaitwa hypnosis
lakini hisia zako zinakuwa zipo
na ndipo aliolala hivyo ukimgusa
hushtuka, hata wale waumini wa
dini ya Bhuda na mazowezi ya
Yoga, hufunga macho na kuifanya
nafsi kutoka katika kiwiliwili na
kufunga macho na kuvuta pumzi
kwa nguvu kwa kufanya hivyo
huyashusha mapigo yao ya moyo
na kupiga taratibu hapa huwa,
juu ya hayo afanyayo huwa sawa
kama yupo macho kama hajafanya
kitu. Mambo haya huangaliwa
katika Yoga kupitia aidha katika
masomo ya physiology, psychology
na psychosomatic therapeutic.
Tunapoyapitia hayo katika elimu
hizo ndivyo tunavyokuja kuelewa
usingizi na itasaidia makala haya
kuweza kuyakihitimisha somo la
hawa vijana wa pangoni na usingizi
mzito waliolala na kuyafahamu
haya mambo ya kimambo leo na
sayansi.
Fwatana na mie wiki ijayo
kuweza kuikamilisha mada hii.

17
Na Khatib Juma Mziray
WIKI iliyopita nilimalizia kwa
kusema kuwa kuna msomaji
amesoma makala ya Ugaidi ni
nini nani gaidi? akaniandikia
ujumbe mreefu, akilaumu
kuwa, tumekuwa tukishusha
hadhi ya gazeti letu kwa
kuandika makala za kusimama
upande mmoja wa imani ya
dini; na kushambulia upande
wa pili wa dini ya wasiokuwa
Waislamu.
Anasema kuwa, pamoja na
kuwa naye ni Muislamu, lakini
haaki mwenendo wa makala
zangu.
Nilitafuta jina lake katika
mtandao nikakuta anaitwa
Kalindula Huseni.
Hata hivyo kwa maneno
aliyoandika ninatilia mashaka
jina hilo na Uislamu wake.
Lakini makala ninazo
andika, ninaandika na rejea
za nukuu za vitabu au gazeti;
nilidhani angenikanusha kuwa
nimeandika nukuu za uwongo;
lakini haikuwa hivyo.
Niseme tu kuwa,
mimi siandiki makala za
malumbano; naandika
makala za kuhabarishana na
kufahamishana; ila kuna watu
wana mtazamo wao siwakatazi
mtazamo wao. Kwa mfano hebu
soma maneno haya:
Kunyongwa Sadam Hussein
ni sehemu ya historia ya Biblia
*Ni zao la Babeli lililolainiwa.
Hilo ni gazeti la Kikristo la
Msema kweli toleo Na. 488. La
tarehe ya Januari 7-13,2007. uk.1.
Si nia yangu kwa leo kuandika
jinsi mwandishi wa gazeti hilo
alivyo furahia na kushadidia
kufa kwa Sadam Hussein wa
Iraq, la; ninachofanya hapa ni
kuunganisha kisehemu kidogo
na makala yangu hii:Imebainika kuwa
kunyongwa hadi kufa kwa Rais
wa zamani wa Iraq, Dikteta
Sadam Hussein kunaendelea
kukamilisha historia ya Biblia
Takatifu, juu ya wafalme wa
Babeli waliolidhihaki Taifa la
Israeli na baadaye kukumbana
na laana ya Mungu. Uk.1.
Kwa bahati mbaya mwandishi
hakutwambia kuwa hawa
wafalme wanao wadhihaki
wanadamu hapa duniani na
kuwaanzishia vita na kuwaua,
kuwatesa kuwafanya vilema,
kuwafanya masikini kwa
kupora mali zao na kuwafanya
wakimbizi; laana ya Mungu ikoje
katika Biblia? Au hawa ni kwa
sababu si wana wa Mungu wa
Israeli?
Bw. Sadam alinyongwa
Jumamosi, Desemba 30, 2006
baada ya Mahakama Kuu nchini
Iraq kumtia hatiani kwa mauaji
ya wanavijiji 148 wa dhehebu
la Shia kutoka Dujail, baada ya
jaribio lililoshindwa la kumuua
la mwaka 1982. Uk.1.
Mwandishu huyu
anachotwambia hapo, ni
kuwa, kesi ya Rais Sadam
Hussein si ya kuwa na silaha
za maangamizi; ambayo ndiyo
ilikuwa kauli mbiu ya Rais Bush
na washirika wake 32. Ila ni ya
mauaji ya Mashia 148 waliotaka
kumuua na kumpindua mwaka

Makala

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Wakimbizi Ulaya -2

wa 1982.
Kwa maana hiyo, mwandishi
anatwambia kuwa Mashia
hao walikuwa ni wa haini wa
serikali ya Iraq; na hukumu
ya wahaini tunajua kuwa ni
nini. Sina maana ya kufurahia
kuuliwa kwa watu hao; ila kwa
mwandishi huyu kufurahia
kuuawa kwa Rais Sadam Husein
kwa kuwaua washia wahaini
148, sijui kuwa anafurahia nini
kwa malaki kama si mamilioni
ya wa Iraq waliouawa na
wanaoendelea kuuawa na
kulemazwa, kufanywa mayatima
na masikini bila ya kosa; kutokana
na uvamizi wa majeshi ya nchi 32
washirika wa Marekani; ambao
wamewatinisha kwa kuwaachia
kirusi cha Ushia na Usunni.
Lakini mwandishi hakutwambia
kuwa toka mwaka wa 1982 mpaka
kuvamiwa kijeshi Iraq ni wakimbizi
wangapi waliokuwa walikimbilia
nchi za Ulaya Magharibi.

Qadar, hii ina dhana gani?


Nabii Yusufu A.S. Alipouzwa
Misri, Mwenyezi Mungu alijua
kuwa Qadari yake ina malengo na
itafanya kazi aliyoikusudia.
Na yule aliyemnunua huko
Misri alimwambia mke wake:
Mtengenezee makazi ya hishima
(mtumwa) huyu; huenda akatufaa
au tukampanga kuwa mtoto wetu.
Na kama hivyo Tulimmakinisha
(Tulimkalisha) Yusufu katika nchi
(ya Misri) kwa raha ili kumfundisha
hakika ya (kila) maneno. Na
Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye
kushinda juu ya jambo Lake
(Alitakalo; lazima liwe); lakini watu
wengi hawajui.) Quran 12:21.
Habari za Nabii Yusufu
zinajulikana vizuri kwa wasomaji
wa Quran, na Biblia; kisa chake
kinatokana na kupendwa na baba
yake, Nabii Yaqub, (Yakobo). Kiasi
kwamba nduguze walimwonea
wivu ulioishia kumuuza huko
Misri. Ndiyo maana Mwenyezi
Mungu anatwambia kuwa Qadar,
yake ilikuwa:Na kama hivyo Tulimmakinisha
(Tulimkalisha) Yusufu katika nchi
(ya Misri) kwa raha ili kumfundisha
hakika ya (kila) maneno (Quran
12:21. )

AN-NUUR

Qadar, iliyofanya Nabii Yusufu


kuuzwa nchi ya Misri ilibeba maana
ya Ujumbe huo wa Mwenyezi
Mungu n.k. Kadar, hii inayofanya
watu wa kimbilie Ulaya ina dhana
gani inayofanana na hiyo ya Nabii
Yusufu?:
Husda mbaya, wivu mbaya,
uroho wa mali na cheo; ndio
uliowafanya kaka zake Nabii
Yusufu waamue kumuua au
kumuuza.
Nchi za Marekani, Ulaya
Magharibi na baadhi ya nchi za
Mashariki ya Kati; zina roho mchafu
wa aina hiyo. Kama vile nduguze
Yusufu walivyoshirikiana kumuuza,
ndivyo na nchi hizo zilivyo, na
zinavyoshirikiana kuzipiga na
kuzipindua nchi za Asia, Mashariki
ya kati, Afrika na dunia kwa
jumla; ambazo wananchi wake
wanakimbilia Ulaya Mashariki.
Na huko wanachaguliwa,
wanaofaa kubaki huko watabaki,
wasifaa kubaki huko watarudishwa
makwao; hatujui vigezo vya
kuwafanya wabaki Ulaya au
warudishwe makwao ni nini. Labda
ni elimu inayohitajika Ulaya, au
waliokuwa na mapesa yao huko
kwenye makenki ya Ulaya.
Hata hivyo, vyo vyote iwavyo,
wao ni watumwa, waliojipeleka
wenyewe; watapata raha kama ujuzi
wao utawasaidia, na kukubalika
kwa Mapharao wa Ulaya; kama vile
Yusufu alivyokubalika kwa Pharao
wa Misri kutokana na ujuzi wake
uliompelekea kufanywa Waziri wa
hazina wa serikali ya Misri.
Hata hivyo moja ya Qadar,
iliyopelekea Nabii Yusufu A.S.
kupelekwa Misri; ni kukisha
Ujumbe wa Mwenyezi Mungu
kwa Ufalme uliokubuhu katika

kufuru pamoja na raiya zake.


Kiasi kwamba kwa Qadar,
hiyo imetuachia historia na
mafundisho ya kuzingatia, ili
tuepukane na uovu uliozagaa
hapa duniani.
Qadar, ya wakati wa Nabii
Yusufu, A.S. ilimpeleka Yusufu
Misri akiwa mtoto, akakulia
Misri; ndipo Qadari ikawafanya
nduguze na baba yao Nabii
Yakobo na kizazi chake wote
wakahamia Misri.
Kwa mujibu wa Biblia kitendo
hicho, aliambiwa Nabii Ibrahimu
A.S. kuwa, katika wazawa

wake, wako watakaokwenda


utumwani muda wa miaka 400.
Mwanzo 15:13. Alafu watatoka
huko; ndio hao Yakobo na kizazi
chake.
Ndipo Nabii Musa
aliponusurika kuuawa akiwa
mchanga, na baadaye akalelewa
kwa mfalme (Pharao) na kuwa
sababu ya kuanguka kwa ufalme
wake na kukombolewa kwa
Wana wa Israeli kutoka Misri.
Kuna jambo ninalo liweka
kwa wasomaji, ili walitafakari
wakiendelea kusoma makala hii.
Kwa historia ya wafalme,
walikuwa wanapenda kuoa
wanawake wazuri, tena si kuoa,
bali huagiza kuwa watafutwe
wanawake wenye sura nzuri
wapelekwe katika kasri ya
mfalme; wale atakao wapenda
basi hao ni wakeze.
Ndiyo maana Nabii Ibrahimu
A.S. Alipokuwa anaingia Misri
akiwa na mkewe Mama Sara,
alimwambia kuwa wakika
Misri asije kuwaambia kuwa ni
mkewe; bali awaambie kuwa
ni dada yake; maana kulingana
na uzuri wake aliokuwa nao,
mfalme atataka awe mkewe; na
akijua kuwa ni mke wa Ibrahimu
atamuua Ibrahimu ili amchukue
Sara. Soma Biblia mwanzo 12:1418.
Kwa maana hiyo, ni kuwa,
kizazi cha wa Misri na cha wana
wa Israeli, kwa miaka hiyo
mianne kimezalisha machotara
wa mataifa hayo mawili; kama
tunavyoona na kusikia habari
za Ethiopia, kuhusu Mafalasha
(wana wa Israeli wa Ethiopia).
Tofauti ya Qadar, ya
wakimbizi wanaoenda Ulaya,
na ile ya Nabii Yusufu; ni kuwa,
wanaokimbilia Ulaya kutoka
Aka Kaskazini, Mashariki ya
Kati na Asia; ni watu wazima na
familia zao; wenye elimu zao na
maarifa mbali mbali.
Kama vile Qadar ya wakati
wa Nabii Yusufu A.S. ilifanya
ndugu zake wawe ni kisababishi
cha Yusufu kuka Misri; ndivyo
na Qadar, ya wananchi wa nchi
hizo za Asia, Mashariki ya Kati
na Afrika ya Kaskazini; kuwa
wakimbizi imesababishwa
na nchi za Marekani, Ulaya
Magharibi na baadhi ya nchi
za Mashariki ya Kati kwa
kushirikiana na kuanzisha vita
katika nchi hizo zinazotoka
wakimbizi.
Miaka mianne, Qadar,
iliyompeleka Nabii Yusufu A.S.
Misri, ilikamilisha kuanguka
kwa ufalme wa (Pharao) wa
Misri.
Hatujui kuwa Qadar hii ya
wakimbizi wanaokimbilia Ulaya
imebeba dhana gani.
Hata hivyo, kwa sasa
imetuonyesha udhaifu wa
imani na huruma, kwa nchi
za Kiislamu, kwa kushindwa
kuwahurumia wakimbizi,
tena wa imani moja ya dini
na wao; wameshindwa na
Papa Mtakatifu amechukua
familia zenye watu 12 kwenda
kuwalelea Vatikani kwa mfuko
wa Vatikani; ninaamini kuwa
Qadar, hiyo itatujuza mengi
Inshaalla.
(Khatibu Juma Mziray 0757
01 33 44.)

18

MAKALA
Na Abuu Zahrah

UKITAKA kuyaelewa yale ya


Jecha Salum Jecha na kauli
ya Rais Shein katika sherehe
za mapinduzi hivi karibuni,
rudi katika mzizi wa jambo.
Rudi katika yale yaliyotokea
kupindua Katiba iliyotokana
na maoni ya wananchi, kama
yalivyokusanywa na Waziri
Mkuu na Jaji Mstaafu, Mzee
Joseph Sinde Warioba.
Wazanzibar/Wananchi
walitaka Muungano wa Serikali
Tatu na mpaka leo ndio kilio
chao. Lakini Muswada ule
ulitupiliwa kwa mbali, ukaja
mjadala mpya kabisa kiasi cha
kushutumiwa Tume ya Warioba
na kuonekana kama wasaliti
fulani hivi.
Labda tujiulize, lile la Katiba
lina tofauti gani na aliyofanya
Jecha katika Uchaguzi Mkuu?
Mapendekezo yaliyosomwa
na Mzee Warioba Bungeni,
yalikuwa ya Serikali kwa
sababu Tume ilikuwa ya Rais na
mapendekezo yao waliyakabidhi
serikalini ndio yakapelekwa
Bungeni.
Leo Rais Shein anatamba
kuwa yeye ni Rais halali kwa
mujibu wa Katiba. Na anaongeza
kusema kuwa kufutwa uchaguzi
ilikuwa kwa mujibu wa sheria
na hivyo hata kurejewa uchaguzi
ni kwa mujibu wa sheria. Watu
wa CUF na wengine wenye
kufuatilia mambo haya kwa
mujibu wa Sheria na Katiba ya
Zanzibar, wanasema hapana.
Hapa utaona kuwa ni yale
yale ya wajumbe wa Tume
ya Jaji Warioba walivyokuwa
wakitetea na kusema kuwa
walikuwa wamewasilisha maoni
ya wananchi, kujali masilahi
ya nchi na mustakbali mwema
wa muungano. Waliokuja
kuyapindua nao walidai kuwa
wanatetea maoni, matakwa na
masilahi ya wananchi.
Mtu pekee aliyekuja
kuwa mkweli na kufumbua
fumbo la Katiba ya UKAWA
na Mapinduzi ya CCM, ni
Mheshimiwa William Lukuvi.
Pengine kwa kuona kuwa
Maaskofu, Mapadiri na waumini
wenzake hawatalielewa fumbo
lile na hivyo kudandia Bogi la
kutaka serikali tatu, ilibidi awe
muwazi.
Alisema hofu ni Uislamu.
Muungano wa Serikali Tatu,
utaifanya Zanzibar kuwa huru
zaidi na hivyo ni hatari kwa
Waislamu kuchukua nchi na
kuleta hatari ya ugaidi mpaka
Bara. (Lakini sasa tunaambiwa
ugaidi upo Amboni! Inawea
kusemwa Tanga, ndio hao hao,
Waswahili.) Hilo akalirudia
aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba, Samwel
Sitta alipokuwa akiongea
na Watanzania wanaoishi
Uingereza alipotakiwa kueleza
kwa nini walipindua Katiba ya

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Hofu ya IS Amboni

Yale yale ya Lukuvi


Kanisani juu ya Zbar
Msimshike sharubu Jecha

MHE. William Lukuvi.


Wananchi. Pamoja na maelezo
yake mengi ya kuzunguka, lakini
mwisho akawataka Watanzania
wale wajiulize, je, wangetaka
kuona Zanzibar inayotawaliwa
na Sheikh mwenye madevu na
kilemba? Hawaoni hatari yake?
Huu ndio msingi wa
mapinduzi ya Jecha katika
uchaguzi, akaufutilia kwa mbali.
Mengine ni porojo, ndio maana
yanachukua sura ya mdahalo wa
viziwi.
Labda kama alivyofanya
Mheshimiwa Lukuvi, tulifafanue
hili. CUF ni UKAWA. UKAWA
ndio wanataka Muungano wa
Serikali Tatu, kuwapa nchi,
ni kutafuta Shari na hatari
aliyoizungumzia Mheshimiwa
William Lukuvi. Kwa hiyo,
hoja inayosimama hapa ni ya
Dr. Shein. Kwamba ilikuwa
lazima uchaguzi urudiwe
na kuhakikisha kuwa CCM
inatapa ushindi wa kishindo.
Mantiki yake ni kuwa ndiyo
njia pekee ya kuhakikisha
kuwa Tanzania inaondokana na
hofu aliyozungumzia Lukuvi
Kanisani.
Ilisikika kauli ya CCM

AN-NUUR

wakiomba radhi juu ya lile


bango la kibaguzi lililoingia
uwanjani siku ile mbele ya
Rais Magufuli, Rais Shein
na Marais wastaafu. Lakini
nini kosa la watu wale?
Kile kilichoandikwa katika
bango lile, kinatofauti gani
na aliyosema Samwel Sitta?
Hivi maneno ya bango lile,
tuseme ndiyo mazito kuliko
yale aliyosema Mheshimiwa
William Lukuvi Kanisani na
kisha akayakariri ndani ya
Bunge, tena kwa kujiamini!
Swali la kujiuliza ni
hili: Inakuwaje hatuyaoni
na kuyasemea yale ya
Waheshimiwa sana William
na Samwel? Mbona hatusikii
ikisemwa kuwa ikishika
CHADEMA atarudi
Mjerumani na siasa zake za
ki-Hitler au kusimika sera
za akina Angela Dorothea
Merkel za Christian
Democratic Union (CDU)?
Kwa nini hofu iwe ni kurudi
Mwarabu/Hizbu, Sheikh
mwenye midevu na kilemba?
Kama hayo hatuyaoni,
basi tusubiri Jumuiya ya
Kimataifa na wenye MCC

wampiganie Maalim haki


yake ya kutangazwa!
Pengine ike mahali
tutumie akili japo kidogo tu
tujiulize, watu walioipiga
Afghanistan, wakaivamia
na kuiharibu Iraq, kisha
wakaisambaratisha Libya na
sasa wapo Syria, watasilikiza
kilio cha wanaotaka Maalim
atangazwe au watajali zaidi
yale ya William Lukuvi
aliyetoa kauli ya kulihami
Kanisa na hatari ya Katiba
ya CUF/UKAWA inayotaka

Muungano wa Serikali Tatu?


Aliyozungumza Mheshimiwa
Lukuvi si ndio hayo hayo ya IS
yanayowapa fursa wenye MCC
kuja na USARAF zao kufanya
vikao Arusha?
Hao wenye MCC wana mengi
wanayataka katika madini yetu,
mafuta na gesi, watahangaika na
ya kumpa haki yake Maalim

waache mikakati yao na walio


madarakani kupata mradi
wao?
Tatizo la msingi la Zanzibar,
sio Dr. Shein kuwepo Ikulu
au kumpisha Maalim.
Tatizo la Zanzibar ni kubwa
zaidi ya hapo. Na maadhali
hatutaki kuliona, litaendelea
kututafuna kama nchi na
kama jamii.
Jiulize tu, hii hali
iliyopo Zanzibar hivi sasa
kiuchumi, kijamii na kila
hali, na mustakbali wake
utakavyokuwa kama siasa
zikiendelea katika mkondo
wake huu huu, wale
waliokuwa wamebeba bango
la sera za akina Samwel Sitta
za Sheikh mwenye madevu
pale uwanja wa Amani
katika sherehe za Mapinduzi,
wananufaika na lipi?

KUMRADHI

KATIKA toleo lililopita katika gazeti hili, maelezo


ya picha hii yalinukuliwa kimakosa. Usahihi wake
ni: Mahujaji wakiwa katika uwanja wa Arafa. Na
sehemu nyeupe inayoonekana kwa juu ni Jabar Rahma.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.

19

Ukurasa wa Watoto

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Uislamu ni usa: Usa wa nguo

Nguo yenye najisi ni


chafu. Haifai kuswalia.
Muislamu havai nguo
yenye najisi.
Sauda ni dada yake
Ali.
Sauda anasoma
darasa la tatu.
Sauda ni mtoto hodari
sana.
Anaweza kufua nguo
zake vizuri na kuzipiga
pasi.
Sauda hupendeza
akivaa nguo zake sa.
Mtoto msa
hupendeza.
Mtoto msa
hupendwa na watu.
Mtoto msa huwa na
afya njema.
Mtoto msa huwa na
furaha.
Muislamu anatakiwa
kuwa msa wa tabia,
mwili na nguo.
Hakika Allah
huwapenda wanaotubu
na wanaojitakasa.

WIKI iliyopita
tulijifunza juu ya usa
wa meno na kinywa.
Katika somo letu,
watoto walihimizwa
kupiga mswaki mara
kwa mara. Hasa
wanapoamka asubuhi
na kila baada ya kula.
Leo tunaangalia usa
wa nguo.
Watoto wanatakiwa
kuvaa nguo sa.
Kama hawajaweza
kufua wenyewe wazazi
na dada zao wawafulie.
Ali hajaweza kufua
nguo vizuri lakini ni
msa.
Ali hachafui nguo
zake ovyo.
Mama yake humfulia
vizuri nguo zake na
kuzipiga pasi.
Ali akivaa nguo sa
hupendeza.
Ali akienda haja huwa
mwangalifu asichafue
nguo zake kwa najisi.

HAIIBA TIMAMU TEA

CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

UVIMBE TUMBONI UMEYEYUKA KAMA MCHEZO!


Na. Sabrina Jaffo
Hivi karibuni vipimo vya hospitali vilibainisha kuwa nilikuwa na uvimbe mkubwa
kwenye kizazi. Hii ilikuwa ni baada ya kuugua kwa muda mrefu. Baada ya uvimbe
huo kubanika nilishauriwa kufanyiwa upasuaji ili uweze kuondolewa. Nashukuru
kuwa kabla sijafanyiwa huo upasuaji rafki yangu mmoja alniashauri nitumie chai
ya Haiiba Timamu. Iliniambia kuwa siyo tu kuwa gharama zitakuwa ni ndogo sana
ukilinganisha na upasuaji, lakini matibabu yangechukua muda mfupi na
yangeondoa tatizo langu bila kuniachia jeraha. Nashuuru nilimwelewa kwa sababu
ni kweli kwamba baada ya kutumia dawa kwa majuma manne uvimbe wote
umeondoka na sisikii maumivu yoyote.
https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

SHINIKIZO LA DAMU
(HYPERTENSION/HIGH BLOOD
PRESSURE)
UGONJWA WA MOYO
KIHARUSI
JONGO (GOUT)
MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM)
MAUMIVU SUGU YA KICHWA
BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS)
MAGONJWA YA INI
SARATANI MBALIMBALI
UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA
VIUNGO VYA UZAZI VYA MWANAMKE
(FIBROIDS, POLYPS NA CYSTS)
KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY
INCONTINENCE)
ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI
PUMU
UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI
KASI YA KUZEEKA
MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO
WA DAMU
MKAKAMO WA NGOZI;
UDHAIFU WA MACHO
KUPOTEZA KUMBUKUMBU
KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA
MAKOVU KWENYE MAPAFU
UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI,
YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA


INAPATIKANA
HERBAL IMPACT
MOSQUE STREET, NO. 1574/144
(MKABALA NA MSIKITI WA
SUNNI), KITUMBINI, DAR ES
SALAAM
TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU
NAMBA:
0754281131/0655281131/06862
81131/0779281131

AN-NUUR

20

MAKALA

20

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 20 - 26, 2016

Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa

AN-NUUR

SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 27 - JUNI 2, 2016

Madrasa bora kujengwa


Na Bakari Mwakangwale

MCHAKATO wa kujenga
Madrassa zilizo bora na za
kisasa nchini kwa ajili ya
mafunzo ya Qur an na kozi
maalum kwa Walimu wake,
umeanza katika Wilaya ya
Ruji, Mkoani Pwani.
Madrassa hiyo itakayojulikana
kwa jina la Imamu Kassim Ally
Integrated Academy ni moja kati
ya Madrassa zipatazo 50, zilizo
katika mchakato wa kujengwa
katika Vijiji mbalimbali nchini
chini ya Taasisi ya Kiislamu ya
Kalam Education ya Jijini Dar es
Salaam.
Ustadhi Juma Nchia,
amebainisha hayo, akieleza
mipango mikakati ya kumaliza
tatizo la vijana wengi wa
Kiislamu waliopitia Madrassa na
kubahatika kusoma na kuhifadhi
Qur an, lakini wanashindwa
kuishi kitauhiid.
Alisema, ndoto za Kalamu
Education kwa mwaka 2016-

2025 ni kujenga Madrassa


zipatazo 50 za kisasa katika
Vijiji mbalimbali nchini ili
kuleta uamsho kwa jamii ya
Kiislamu kwa kuwaanda vijana
tokea ngazi ya chini na kuwalea
kitawhid tofauti na ilivyo sasa.
Ustadhi Nchia, alisema tayari
kituo cha kwanza kimeanza
kujengwa na kitajulikana kama
Imamu Kassim Ally Khan
Integrated Academy, kinacho
jengwa hivi sasa Wilayani
Ruji.
Alisema, baada ya
hapo vitafatia vituo vya
Profesa Kigoma Malima
kitakachojengwa Wilayani
Mkuranga pamoja na Burhan
Mtengwa ambacho kitakuwa
Wilayani, Kisarawe.
Alisema, vituo hivyo pia
vitakuwa mahala bora kwa
mafunzo ya Walimu wa
Madrassa ili kuwajenga kuwa na
mfumo maalum wa ufundishaji
na wao wakiwa mfano kwa
wanafunzi wao.

Somesheni Quran
Na Bakari Mwakangwale

UPO umuhimu wa kusomesha


na kuhifadhisha Qur an katika
Mashule ya Kiislamu ili
kuwasaidia vijana wa Kiislamu
kukabiliana na changamoto za
Kiutandawazi zilizopo katika
jamii kwa sasa.
Hayo yamesemwa na
Ustadhi Ally Asaa, akiongea
na Mameneja na wamiliki wa
Mashule za Kiislamu Katika
semina iliyoandaliwa na
Jumuiya ya kuhifadhisha Qur
an, katika Ukumbi wa City
Garden, Jijini Dar es Salaam,
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akiwasilisha mada yake ya
Umuhimu wa kuisomesha na
kuihifadhisha Qur an katika
Mashule ya Kiislamu, Ust.
Asaa, alisema bila kuifanya
Qur an kuwa ndio msingi wa
kuwajenga kimaadili wanafunzi
wa Kiislamu katika Mashule ya
Kiislamu itakuwa ni vigumu
kuwaepusha na majanga ya
Utandawazi yaliyopo katika
jamii hivi sasa.
Yatosha au ni lazima

kuisomesha na kuhifadhisha
Qur an pale ambapo Mashule
yetu tumeyaita ni ya Kiislamu,
kwa maana hiyo kuna umuhimu
na ulazima kuhakikisha somo la
Qur an linasimamiwa ipasavyo
ili kuwaandaa vijana wa
Kiislamu kuweza kuishi kwa
mujibu wa Qur an na Sunnah.
Amesema Ust. Asaa.
Alisema, umuhimu wa

Madrassa Imamu Kassim Ally Integrated Academy inatazamiwa


kuwa hivi ikikamilika ujenzi wake.
Pia, alisema Walimu hao
watapata fursa ya kujifunza
ujasiria mali kwa kupewa
kozi fupi za Kilimo, Biashara,
ufugaji pamoja na uongozi na
malezi kwa lengo la kuwasaidia
kuinua vipato vyao na kujikimu
kimaisha.
Kwa upande wake Wakili
Juma Nassoro, akizungumzia
tatizo hilo, alisema mazingira
kuisomesha Qur an, Mashuleni
unazidi kuonekana pale
unapoiangalia jamii na hali ya
Ulimwengu ilivyo kwa sasa
unabaini kuwa bila ya Qur an,
ni vigumu kuwaepusha watoto
na majanga ya Utandawazi
yaliyopo Ulimwenguni hivi sasa.
Hakuna Uislamu nje ya
Qur an, ama hakuna Uislamu
bila ya Qur an kwa hiyo ikiwa
Shule zetu ni za Kiislamu basi
hazitotimia bila ya kufundishwa
na kuhifadhishwa kwanza Qur
an. Alisema.

RAIS mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na baadhi ya Masheikh


katika semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya kuhifadhisha Qur an, katika
Ukumbi wa City Garden, Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.

aishiyo mtu hujenga wasifu


wake.
Ikiwa Sheikh au Ustadhi
ambaye amepewa dhima ya
kuwasomesha na kuwaanda
vijana kimaadili kwa
kuwafundisha Qur an, anaishi
kama muhuni, hata wanafunzi
wake hawawezi kuogopa
kupituka mipaka ya kimaadili.
Amesema Wakili Nassoro.
Wakili Juma alisema
msimamo wa wazazi katika
malezi kwa watoto pamoja na
kuwa wanasoma Madrassa nako
kuna tatizo hivyo elimu yake ya
Madrassa inakuwa haimsadii.
Alisema, katika hali hiyo
ndipo panapohitajika mafunzo
maalum kwa Walimu wa
Madrassa ili kuwapa mbinu
za ufundishaji sambamba na
uboreshaji wa Madrassa na
kufanya vyote hivyo vilete tija
kwa jamii.
Mabadiliko kwa jamii
ya Kiislamu na Walimu wa
Madrassa ni jambo tunu
kulishughulikia, KALAMU,
tumeliona hilo kwa lengo la
kuleta mabadiliko katika sekta
ya Madrassa zetu ili zilete tija
kwa jamii kuanzia ngazi ya chini
kwa watoto wetu. Amesema.
Wakati huo huo ujumbe
kutoka katika Taasisi ya Islamic
Help, Sheikh Sultan Niaz Ul
Hassan Qadr akiongozana Imam
Ijaz Ahmad Shami, ambaye ni
mwanzuoni maarufu Uingereza,
Jumatano wiki hii walitembelea
Osi za Kalamu Education
Faundation, na kufurahishwa na
juhudi za Taasisi hiyo.
Ujumbe huo umefurahishwa
na mpango wa mafunzo ya
Walimu wa madrassa sambamba
na ujenzi wa vituo 50, vya
Integrated Academy, haswa
katika maeneo ya Vijijini.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

También podría gustarte