Está en la página 1de 20

Mansour awaliza Waislam

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.com

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1194 DHULQAAD 1436, IJUMAA , SEPTEMBA 11-17, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Tanganyika si Guantanamo
ya kutesa Masheikh
Maalim kumrejesha Sheikh Msellem
Apokewa kwa Tala' al Badru 'Alayna, Pemba
Msiwape kura wasiotaka maelewano - Moyo

MAALIM Seif Sharif Hamad (kushoto) na Mhe Edward Lowassa.

MAELFU ya wakazi wa Zanzibar waliohudhuria mkutanao wa uzinduzi wa kampeni za Urais, Ubunge na Uwakilishi wa UKAWA ulifanyika
juzi Jumatano katika Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar.

Makala

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Mafundisho ya Quran-Baqara: 150

Fethullah-Gulen

N A
p o p o t e
utakapokwenda
u e l e k e z e u s o wa k o
upande wa Msikiti mtukufu
na popote mtakapokuwa
elekezeni nyuso zenu
upande wake tumefanya
hivyo ili watu wasiwe na hoja
juu yenu, isipokuwa wale
ambao wamefanya dhulma
miongoni mwao kwa hiyo
msiwaogope na niogopeni
mimi, na ili niitimize neema
yangu juu yenu na ili mpate
kuongoka. [Al-Baqarah
150].
Baada ya kufika Mtume
(s.a.w.) Madina na kuitukuza
alipitisha muda wa miezi
16 au 17 na hali ya kuwa
anaelekea katika swala zake
upande wa Msikiti wa mbali.
Ilikuwa Al-Kaaba wakati huo
imejazwa masanamu (kama
kawaida ya washirikina).
Alipokuwa Mtume (s.a.w.)
amepelekwa kwa dini ya
kumpwekesha Mwenyezi
Mungu na kutoonyesha
umuhimu wowote upande

wa masanamu, kwa sababu


hiyo alizuiliwa kwa kipindi
maalum kuelekea katika wala
zake upande wa Al-Kaaba ili
aonyeshe msimamo wake wa
thabiti na mkazo upande wa
masanamu.
Kwa uhakika kuna
uhusiano imara kati ya hakika
ya Ahmad na kati ya hakika
ya Al-Kaaba, na alikuwa
Mtume (s.a.w.) anahisi
kufuatana na maumbile
yake ambayo amemuumba
juu yake Mwenyezi Mungu
tokea tangu jambo hilo na
anapenda kuelekea upande
wa Al-Kaaba na ana shauku
kubwa ya jambo hilo, na
kuelekea huko na kufanya
shauku kumewekwa wazi na
Quran tukufu:
Kwa hakika tunaona
kugeukageuka kwa uso wako
kuelekea mbinguni. [AlBaqarah 144]
Ama lengo la Mtume
(s.a.w.) kutokana na
kugeuzageuza uso wake
kuelekea mbinguni, ni kutaka
kwake aweke, Mwenyezi
Mungu mtukufu hukumu
mpya katika maudhui ya
kukibadilisha Qibla. Ndiyo
alikuwa anangojea khabari
kutoka mbinguni. Kwa sababu
hiyo tunaona aya baada
ya hapo na mwisho wake
inamfikishia habari njema
kwa kusema: Tutakuelekeza
Qibla unachokiridhia. [AlBaqarah 144].
Jambo la wazi ni kwamba
ni vigumu kuifahamu hakika
hii na haifahamu isipokuwa
mtu kama Mtume (s.a.w.)
ambaye alikuwa anauelewa
uhusiano huu ulio imara kati
yake na kati ya Al-Kaaba.

Ukweli kwa kuelewa kwa


maumbile yake.
Ndiyo, ilikuwa hakika ya
Al-Kaaba na uhusiano na
Mtume, isipokuwa ni kwamba
masuala ya kumpwekesha
Mwenyezi Mungu ambayo
ndiyo sababu ya kupelekwa
kwake, yalikuwa na umuhimu
mkubwa sana katika utukufu
wa Al-Kaaba na kule kuwa
kwake ni Qibla cha swala,
kwa sababu hiyo alielekea
Mtume (s.a.w.) wakati yuko
Makkah katika swala zake
upande wa Msikiti wa mbali
na akaendelea juu ya utaratibu
huo muda mwingine huko
Madina vile vile.
A m a , M a ya h u d i k wa
hakika wao, walianza kudai
kutokana na kuwa Qibla
cha Waislamu ni upande wa
Msikiti wa mbali kwamba
wao ndiyo asili na kwamba
Wa i s l a m u wa n a wa f u a t a
wao, ili wafanye kupitia
maudhui hayo hoja kwa
dini yao. Na lau angetaka
Mtume (s.a.w.) angekigeuza
Qibla akakielekeza kwenye
Al-Kaaba wakati wa kufika
kwake tu Madina.
Isipokuwa yeye hakuwa
akifanya mambo kwa
matakwa yake na raghba
yake, bali alikuwa wakati
wote amefungamana na
Mwenyezi Mungu mwenye
kufanya ikhlasi kwake katika
kila jambo. Katika mambo
yake anangoja maamrisho
kutoka kwake, hali ya kuyapa
nguvu maamrisho hayo juu
ya matakwa ya moyo wake
kwani alikuwa ni mtu wa
kilele anayetazamia vipeo
vya mbali vya kibinadamu.
Isipokuwa yeye hakusahau

kuwa kwake ni mja; Mjumbe


anayetekeleza maamrisho ya
Mwenyezi Mungu mtukufu.
Kama ambavyo Mtume
(s.a.w.) kutokana na kuelekea
kwake katika swala yake
upande wa msikiti katika
swala aliwasha nuru ya
uongofu katika nyoyo za
watu wengi katika Mayahudi,
mifano ya Abdillah Bin Salam,
na inawezekana kwamba
sifa ya Mtume huyu ilikuwa
imetajwa katika vitabu vyao.
Kwa hali yoyote ile kwa
hakika walikuwepo baadhi ya
Mayahudi ambao waliongoka
kwenye Uislamu na baada ya
miezi 16 au 17 katika kuelekea
huko upande wa Msikiti wa
mbali makusudiwa yalitimia
na haukubakia mikononi mwa
watu hawa ushahidi wowote
ambao wanaweza kuutumia
dhidi ya Waislamu. Maana
hakukuwa ni jambo lililo
katika uwezo wa Mushirikina
kusema:
Nyinyi mnaelekea
upande wa Al-Kaaba ambayo
imejazwa kwa masanamu
yetu ikiwa ni hivyo basi dini
yetu ndiyo asili.
Na hakukuwezekana kwa
Mayahudi kusema: Nyinyi
mnaelekea kwenye Qibla
chetu ikiwa ni hivyo, basi dini
yetu ndiyo asili.
Katika mfano wa mazingira
kama haya, ilikuja amri
ya Mwenyezi Mungu kwa
kuelekea upande wa Msikiti
mtukufu akauthibitisha
muungano kati ya dhati ya
Mtume (s.a.w.) na dhati ya
Al-Kaaba yenye kutukuzwa.
Kuna ishara nyingi katika
Agano la Kale katika mambo
yanayofungamana na Nabii

Isaya (AS) zinaashiria


kwamba matukio yatapita
kama yalivyopita kwa
sababu baadhi ya Mayahudi
walikuwa wanasema kwa
kujengea juu ya ishara hizo
Hakika Qibla cha Mtume
anayekuja kitakuwa Makkah
Ama Muhammad ataacha
kuwa anaelekea katika swala
zake upande wa Baytul-Almu
Qaddasi Na maneno haya
yanatoa mwangaza juu ya
baadhi ya pande za maudhui
haya.
Na ili niitimize neema
yangu juu yenu. [Al-Baqarah
150]
Maana: kwa hakika
kuelekea kwenu katika swala
upande wa Msikiti wa mbali
kulikuwa ni neema isipokuwa
neema ya asili iliyokuwa
kubwa sana ilikuwa katika
kukutana wapenzi. Maana
kukutana kwa Mtume (s.a.w.)
mwakilishi wa umma wa
Kiislamu na Al-Kaaba, na
kutoka hapo kupanda baada
ya hapo kuelekea Sidrat
Al-Mutaha ili afuzu kwa
kuipata neema ya Mwenyezi
Mungu uso kwa uso na hili
linawezekana tu kwa kuelekea
upande wa Al-Kaaba. Na
cheo ni kama hivyo, atakuwa
Mwenyezi Mungu mtukufu
ametimiza neema yake na
huo ni utukufu, ameuchagua
M w e n y e z i M u n g u k wa
utukufu huo umma huu
ambao ameeneza juu yake
neema zake.
(Imenukuliwa kutoka
Kitabu: Miyangaza ya Quran
katika mbingu ya hisia,
cha Muhammad Fethullah
Gullen kilichotafsiriwa
kwa Kiswahili na Sheikh
Suleiman Amran Kilemile)

Tanganyika si Guantanamo ya kutesa Masheikh


Na Mwandishi Wetu

ANGANYIKA sio
Guantanamo ya
kutesea Masheikh na
watuhumiwa wa ugaidi.
Amesema hayo
mgombea urais kupitia
CUF, Mheshimiwa Maalim
Seif Shariff Hamad.
Na kwa maana hiyo,
atahakikisha kuwa
kanuni za Utawala Bora
zinatumika kukomesha
Guantanamo hizo za
kidhalimu.
Maalim Seif Shariff
Hamad amesisitiza jambo
hilo, ambalo limekuwa
likisemwa na kukaririwa
na mgombea urais kupitia
CHADEMA, Edward
Lowassa.
Akasema kuwa, viongozi
wa sasa wa serikali ya
CCM wameiuza Zanzibar
kwa Bara hali inayopelekea
hata kudharauliwa kwa
Mahakama Kuu ya
Zanzibar.
Mgombea huyo
wa Urais, Zanzibar,

ameyasema hayo katika


uzinduzi wa kampeni za
kugombea urais Zanzibar
kupitia chama cha CUF.
Mkutanao huo ulifanyika
juzi Jumatano katika
Uwanja wa Demokrasia,
Kibanda Maiti, Zanzibar.
Akitumia msemo ule
ule wa Mheshimiwa
Lowassa, Maalim Seif
amesema, serikali ya CCM
imeifanya Tanganyika ni
Guantanamo ya kutesea
Masheikh na akaahidi
kuwa katika mambo ya
mwanzo kufanya akiingia
madarakani, ni kukomesha
mtindo huo wa kunyakua
Masheikh na Wazanzibari
kwenda kuwatesa Bara.
Hiyo ni mara ya
k wa n z a k wa M a a l i m
Seif kugusia suala la
Masheikh wa Zanzibar
toka walipokamatwa na
kupelekwa rumande katika
magereza za Bara zaidi ya
miaka miwili sasa.
Alisema, hilo ni
suala jepesi, linalohitaji
tu uzalendo na uelewa

wa mambo kwani hata


kwa Katiba na Sheria za
sasa, Mahakama Kuu ya
Zanzibar ina hadhi sawa
na ile ya Tanganyika.
Akashangaa inakuwaje
s e r i k a l i ya Z a n z i b a r ,
i n a y o j i n a d i k u wa i n a
Rais, kufikia mahali pa
kuidharau hata Mahakama
Kuu yake kiasi cha kaucha
watu wake kunyakuliwa
kwenda kuhukumiwa na
Mahakama za Tanganyika.
Akasisitiza kuwa
Masheikh waliowekwa
r u m a n d e
B a r a
watarudishwa na kama
wana tuhuma za kujibu,
basi watafikishwa katika
mahakama za Zanzibar.
Akasisitiza kuwa, ili
kuweka mambo sawa ya
kimuungano na kuondoa
mkanganyiko ulioko hivi
s a s a , k a ma wa ta in g ia
madarakani, watarejesha
Rasimu ya Katiba ya Jaji
Warioba ambayo ndiyo
yenye maoni ya wananchi.
Na kwamba watapigania
kurejea kwa Tanganyika

yenye mamlaka kamili na


Zanzibar yenye mamlaka
kamili, zikiunganishwa na
serikali ya muungano.
Kama mtanichagua kitu
cha kwanza, nawaahidi
wananchi wa Zanzibar
n i k u p a t a s e r i k a l i ya
muungano yenye serikali
tatu Zanzibar kuwa
na mamlaka kamili
na kurejesha rasimu ya
Jaji Warioba amesema
Maalim.
Katika jumla ya mambo
aliyosisitiza Maalim Seif ni
pamoja na lile la utawala
bora ambapo alisema kuwa
mtindo wa janjaweed,
wa t u wa n a o va a s o k s i
usoni kuficha nyuso zao
wakapiga watu, mwisho
wao ni Oktiba 25.
Akasema, anataka
kuijenga Zanzibar yenye
amani ambapo mwananchi
atakuwa akitembea kifua
mbele bila ya hofu.
Mambo ya watu kuvaa
soksi usoni wanapiga watu
mwisho Oktoba 25, siwezi
kukubali Wazanzibari

wanadhalilishwa ndani ya
nchi yao. Alisema.
Kwa upande wake Mzee
Hassan Nassor Moyo
amewataka Wazanzibar
wasifanye kosa kuwapa
k u r a wa t u wa s i o t a k a
maelewano.
N a w a o m b a
Wazanzibari mnaopenda
amani, kura mtilieni
Maalim Seif.
Viongozi wote Zanzibar
wasiotaka maelewano
msiwape kura zenu.
Alisema na kusisitiza
Mzee Moyo huku
akishangiliwa kwa nguvu.
Akiwa Kada mkongwe
wa CCM, Mzee Moyo
amekuwa akisisitiza
kuwa huu ni wakati kwa
Wa z a n z i b a r i k u s a h a u
yaliyopita, wafute siasa
z a c h u k i , b a l i wa l e t e
maelewano ili kujenga
Zanzibar yenye mamlaka
kamili na maendeleo ya
kweli.
K wa m t i z a m o h u o ,
alifanya kazi kubwa
Inaendelea Uk. 3

Habari

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Waislamu wanahitaji mabadiliko


Na Bakari Mwakangwale

AMA ni mabadiliko,
wanayahitajia zaidi
Waislamu.
Na muda wenyewe wa
kuyaleta ni huu katika
uchaguzi mkuu.
Hayo yamesemwa na
Masheikh waliopo katika
Gereza la Segerea, Jijini
Dar es Salaam, wakiwataka
Wa i s l a m u k u z i n g a t i a
mustakabali wao kisiasa
wakati huu wakielekea
katika uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 25.
Masheikh na Waislamu
hao wanaotuhumiwa kwa
ugaidi, wametuma salamu
hizo kupitia mpasha habari
wa gazeti hili wakisisitiza
k u wa , j a p o h i v i s a s a
kuna kibwagizo kuwa
Watanzania wanahitaji
mabadiliko, lakini
Waislamu wanayahitajia
zaidi.
Bali na kama alivyosema
Mwalimu Nyerere,
haielekei kuwa mabadiliko
hayo watayapata ndani ya
CCM.
Kwa hiyo, ni wakati
kwa Waislamu kupima na
kuona kama mabadiliko
hayana dalili kuja kupitia
chama hicho kikongwe,
wayatafute nje ya CCM.
Na mabadiliko yenyewe
ni kuona kuwa nchi
inaongozwa kwa misingi
ya haki na uadilifu ambapo
dhulma na uonevu dhidi ya
Waislamu unakomeshwa.
Masheikh
hao
wamesema, kwa kuzingatia
h a l i h i y o Wa i s l a m u
wanatakiwa kuwa makini
zaidi kwa kuangalia
Chama na viongozi
wa t a k a o wa c h a g u a n a
kwamba katika uchaguzi
wa mwaka huu, mbele
yao hakuna chaguo zaidi
y a C C M n a U K AWA
kwa ngazi zote kuanzia
Udiwani, Ubunge pamoja
na Uraisi.
Wakizielezea pande hizo
mbili (CCM na UKAWA)
wamesema, kwa upande
wa Chama Tawala (CCM)
hakuna Muislamu asiyejua
madhila ya Chama hicho
kwao, kwani utawala wa
sheria umekuwa kipofu
na kiziwi usio sikia wala
kuona hujuma na dhulma
wanayofanyiwa Waislamu.
Nyinyi mnajua zaidi
yaliyotufika chini ya CCM,
Waislamu tumedhalilishwa
vya kutosha na kunyimwa
haki zetu za msingi katika
awamu zote za utawala wa
chama hicho.
L a k i n i
p i a
tumejidhulumu nafsi zetu
wenyewe kwa kukiuka
maagizo ya Mtume (s.a.w)
kuwa Muislamu wa kweli
haumwi na nyoka mara
mbili katika shimo moja.

Sisi tumekuwa kila


m wa k a wa u c h a g u z i ,
CCM inakuwa na uhakika
kuwa ina mtaji wa kura za
Waislamu.
Umesema ujumbe toka
S e g e r e a u k i wa h i m i z a
Waislamu kwamba angalau
katika kura zao waonyeshe
kuwa hawapo na CCM
hata kama wakiingia kwa
mabao yao ya mkono
lakini wawe na uhakika
kwamba Waislamu hawapo
nao.
W a m e s e m a
wa t u h u m i wa h a o wa
Ugaidi walio rumande
kwa mwaka wa pili sasa.
Wa m e s e m a , h i v i
sasa nchi inapita katika
kipindi cha mabadiliko

na hiyo haipingiki kwani


n i l a z i m a ya t o k e e n a
kwamba tayari Waislamu
wamejitokeza kwa wingi
katika kujiandisha hivyo
kilichobaki ni wapi
waelekeze kura zao kwa
lengo la kuweka viongozi
watakao watendea haki
kwa mujibu wa sheria na
Katiba.
Wa k i u l e z e a u m o j a
wa vyama vya upinzani
U K AWA , w a m e s e m a
kuwa, wapo wanaoona
kuwa umoja huo
umemsimamisha Mh.
Edward Lowasa, ambaye
alikuwa ndani ya CCM
hiyo hiyo.
Lakini wakasema kuwa
ni ukweli usiopingika kuwa

Mfumo wa Serikali ya
CCM, uliopo madarakani
ndio unaoendeleza
dhulma na ubaguzi
dhidi ya Waislamu kama
ulivyowanyima OIC na
Mahakama ya Kadhi.
Hakuna kiongozi
mwenye ubavu wa kuzuia
linalotakiwa na mfumo
uliopo ndani ya Serikali
ya CCM, suluhisho sahihi
ni kuondoa mfumo na
kuleta mfumo mbadala
utakaotenda haki sawa kwa
makundi ya wapiga kura
wote, bila kujali itikadi zao
kama ilivyo sasa.
Tusiposhiriki kuleta
mabadiliko, tutaendelea
kubaki kuwa ni raia wa
daraja la pili na idhilali

haitokoma.
Kimesema chanzo
hicho, kikinukuu salam za
Masheikh kwa Waislamu.
Masheikh hao kupitia
chanzo hicho, kikawataka
Masheikh Mussa
Kundecha, Mohammed
Issa pamoja na Ramadhani
Sanze, kusimama na
kuunganisha nguvu za
Waislamu katika kuelekea
katika uchaguzi Mkuu
pamoja na kulingania zaidi
suala la umoja na amani.
Tuna waomba sana
nyie viongozi, unganisheni
nguvu za Waislamu, si
s a h i h i k u wa a c h a n j i a
panda katika kipindi hiki.
Kimesema chanzo hicho
kikifikisha salamu hizo
kupitia An nuur.

Tanganyika si Guantanamo ya kutesa Masheikh


Inatoka Uk. 2
kupitia Kamati ya
Maridhiano kufanikisha
kuwakutanisha Maalim
Seif na aliyekuwa Rais wa
Zanzibar, Mheshimiwa
Amani Abeid Karume, hali
iliyowezesha kuundwa
kwa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Zanzbar
Hata hivyo, amekuwa
akipigwa vita na
wahafidhina ndani
ya c h a m a h i c h o h a l i
iliyopelekea kuvuliwa
uanachama wake.
Maelfu ya wafuasi na
wa p e n z i wa C U F , n a
U K AWA wa l i j i t o k e z a
k we n ye u z i n d u z i wa
kampeni za urais kupitia
CUF, uliofanyika Kibanda
Maiti Zanzibar, juzi
Jumatano.
Katika uzinduzi huo,
pamoja na kuhudhuriwa
na maelfu ya wananchi,
viongozi mbalimbali, pia
tukio hilo limehudhuriwa
na mgombea urais wa
Jamhuri ya Muungano
wa Ta n z a n i a k u p i t i a
CHADEMA chini ya
mwamvuli wa UKAWA,
Edward Lowassa na
mgombea mwenza Juma
Duni Haji.
Katika salamu zake,
Lowassa aliwataka
Watanzania, wapenzi wa
UKAWA kuondokana na
hofu ya kuibiwa kura,
b a l i wa j i a m i n i k u wa
watashinda.
Wakati umefika tukatae
dhana ya kuibiwa (kura),
wa n a n c h i wa m e a m u a
mabadiliko na lazima
tuachane na dhana eti
wapinzani wakichukua nchi
kutatokea vurugu, hayo ni
maneno yasiyokuwa na
msingi wowote. Alisema
Lowassa.
Wakati huo huo, Maalim
Seif Shariff Hamad

jana alipata mapokezi


makubwa Pemba, ambayo
yanasemekana kuwa
hayajawahi kutokea katika
historia ya kisiwa hicho.
Umati wa watu kutoka
kona mbalimbali za Pemba,
ulimiminika kumlaki
toka uwanja wa ndege na
kumsindikiza kwa miguu
hadi uwanja wa Tibirizi,
Chake Chake.

Katika waliotia fora


katika mapokezi hayo, ni
wapiga dufu wakiimba
kasida ya Tala' al Badru
'Alayna, ambayo aliimbiwa
Mtume Muhammad (s.a.w)
alipoingia Madina akihama
kutoka Makkah.
Kwa upande mwingine,
palikuwa na kundi kubwa la
wazee na watu wa makamo
wakivalia kanzu safi na

makoti wakimzunguka
Maalim huku Masheikh
wakitangulia kuomba Dua.
Katika Dua hiyo
ya kuomba ushindi na
kuiombea Zanzibar baraka
na ustawi, waliombewa
pia wale wahafidhina
waliodaiwa kutoitakia
mema Zanzibar kwamba
Mungu awazindue waione
haki na waweze kuifuata.

Bi. Aisha Sururu (Katikati) akiongea na wanawake katika semina ya kinamama


wa Kiislamu iliyofanyika Markazi Changombe jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mansour awaliza Waislam


Ni jinsi Masheikh walivyodalilishwa
Huku viongozi wa CCM, wakishangilia

Na Alghaithiyya, Zanzibar

AT U w a l i p i g a
kimyaa, wengine
wakibubujikwa na
machozi.

H i y o i l i k u wa wa k a t i
Mansour Himid akielezea
uovu na udhalilishaji
waliofanyiwa Masheikh huku
baadhi ya viongozi wa CCM
na SMZ wakishangilia.

Akasema, kuirejesha
CCM madarakani, ni sawa
na Wazanzibari kukubali
kuendelea kudhalilishwa na
kufanyiwa vitendo vya utovu
wa adabu.
Akizungumza katika
mkutano wa ufunguzi wa
kampeni za CUF, Mansoor
Yussuf Himid ambaye ni
Mshauri wa Katibu Mkuu wa

Inaendelea Uk. 5

Tahariri/Tangazo

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Waislamu kuambulia patupu UKAWA


Y
UPO bwana mmoja
katutumia ujumbe
akisema kuwa
i t a k u wa n i j a m b o l a
hatari Waislamu kuweka
rehani haki zao kwa kina
Lowassa na Magufuli.
Katika kujenga hoja yake
akasema kuwa uraia katika
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, una haki
zake zilizoainishwa
kikatiba. Kwamba kila
raia wa kundi lolote
katika jamii ana haki
zote zinazofungamana na
uraia wake. Kinga ya haki
za kiraia na kijamii, ni
Katiba ya nchi. Kiongozi
anaweza kuwa na nafasi
yake katika dhamana
ya utawala. Lakini yeye
hawezi kuwa hakikisho
la haki za raia.
Akisherehesha zaidi
akasema kuwa hivi sasa
nchi imeingia katika
kampeni za kumchagua
Rais wa tano wa nchi
hii. Katika kipindi hichi,
wagombea kupitia vyama
vyao watanadi Ilani zao
ambazo zitajumuisha
ahadi mbalimbali pamoja
n a s e r a . Wa g o m b e a
watakuwa na ahadi nyingi,
lakini lazima izingatiwe
kuwa hawataweza
kutekeleza jambo kinyume
na Katiba halikadhalika
sheria za nchi. Kwa maana
hiyo, mgombea yoyote
asiaminike iwapo atatoa
ahadi ya kufanya jambo
ambalo lipo nje ya Katiba
na kinyume na sheria
zilizopo.
Kwa upande mwingine,
haki zote za kiraia
zilizoainishwa kikatiba,
zisinadiwe wala kuwekewa
ahadi na mgombea kwa
sharti la kumpigia kura.
Haki hizo hazihitaji
kuwekewa ahadi, bali
kutekelezwa na yeyote
atakayeingia madarakani
kwa sababu zilishatolewa
na katiba.
Kwa maneno mengine,
Rais yeyote, kutoka chama
chochote, anakuwa na
wajibu wa moja kwa moja
kutekeleza haki za kiraia
na kijamii. Na kwa maana
hiyo basi, Waislamu kama
jamii, hawana sababu ya
kufungamanisha haki
zao kikatiba na kisheria
na ahadi za mgombea
urais. Kufanya hivyo ni
kuziweka rehani haki zao
kwani hakuna uhakika
wa moja kwa moja kuwa
mgombea huyo atashinda.
Tuseme
kuwa
tunakubaliana naye
mia kwa mia. Na labda
tuongeze kuwa la

muhimu kwa Waislamu


ni kuzitambua haki zao na
kama uongozi uliotangulia
ulikuwa hauwatekelezei,
wajiulize, kosa lipo
wa p i ? K a m a k o s a a u
mazingira yaliyopelekea
wadhulumiwe na
kuhujumiwa yatakuwa
ni yale yale, hata
kama utakuja utawala
mwingine, kwa maana
ya kuingia madarakani
chama kingine, bado hali
ya Waislamu haitabadilika.
Na hili ndilo tungependa
kulijadili hapa na kutoa
maoni yetu.
Kosa liko wapi? Katika
kujiuliza swali hilo, lipo
jambo moja la kuzingatia.
Kama walivyosema
Wa s wa h i l i , u n a w e z a
kumuongoza ngombe
mpaka mtoni, lakini
kunywa maji ni hiyari
yake. Na hapa tunadhani
ndipo lilipo kosa la msingi.
Nchi imeweka katiba na
sheria zinazotambua
haki za kila raia na
inayotamka wazi kuwa
ni marufuku kuwabagua
watu, iwe kwa dini zao,
rangi zao, makabila yao
au mahali wanapotoka
n.k. Katiba pia imeweka
wazi na kutambua haki
ya kuwa ama Muislamu,
Mkristo na kufanya yote
yanayohitajika ndani ya
dini uliyochagua. Sasa
nchi/serikali ifanye
nini zaidi ya hapo?
Kuwalazimisha Waislamu
wakatae kubaguliwa na
k u d h u l u m i wa ? K a m a
Wa i s l a m u w e n y e w e
ndio wanapenda na ndio
starehe yao, CCM na
Serikali wao wafanye nini!
Kwa nini wengine wao
hawalalamiki kuhujumiwa
haki zao? Kama Waislamu
walikuwa wakidhulumiwa
na CCM na serikali yake
hata katika yale mambo
a m b a y o n i h a k i ya o
kisheria na kikatiba, basi
ni Waislamu wenyewe
wamependa. Nchi/Serikali
imewafikisha kisimani
kwa Katiba na Sheria
n zuri, lakin i h a iwe z i
kuwalazimisha kunywa
maji.
Mtadhulumiwa vipi
halafu mkubali. Si dini yenu
inasema, msidhulumu
wala
msikubali
kudhulumiwa? Si dini
yenu inasema, mumsaidie
mwenye kudhulumiwa na
pia mumsaidie dhalimu?
Wa i s l a m u w a j i u l i z e ,
wamemsaidia vipi huyu
CCM na serikali yake
wanayedai kuwa ni
dhalimu toka kadhia za

kunyimwa elimu, MoU,


mauwaji ya Mwembechai,
mabucha ya nguruwe,
OIC, Mahakama ya Kadhi
na hili la kukamatwa na
kuteswa Masheikh? Mbona
hawathubutu kuwafanyia
hayo wachungaji,
mapadiri na maaskofu.
Kwa upande huo ni kama
alivyojisemea Alhaji Alli
Hassan Mwinyi, Mbunge
Muislamu katuhumiwa,
kakamatwa na pembe za
ndovu akamfunga, lakini
akamuonea haya Padiri
mwenye kosa hilo hilo,
akamuachia huru! Kwa nini
Muislamu huyu afungwe
na Padiri asamehewe?
Hivi Mzee Ruhsa
angefanya kinyume chake,
akamfunga Mbunge
Mkristo akamuachia huru
Sheikh mwenye kosa
sawa na la Mbunge huyo
Mkristo, angethubutu
k u j a k u ya s e m a h a y o
hadharani? Redio na
Televisheni zikirusha
live kama alivyofanya
la Aburabi? Na kama
angethubutu, unadhani
angemaliza muda wake
salama?
Waislamu wamefanya
nini kuifanya CCM
itambue kwamba
inavyofanya sio vizuri. Si
ni ndio Masheikh hawa
hawa wanaitwa katika chai
na majukwaa ya kisiasa na
kuisifia CCM na viongozi
wake? CCM wathubutu
kuwafanyia hayo
maaskofu waone? Lakini
wanajua, watawafanyia
h a y o Wa i s l a m u n a
hata mabaya zaidi ya
hayo, hakuna lolote
litakalotokea. Wataendelea
kukalia viti vyao kwa raha
mustarehe!
Sasa kosa hapa la nani?
La CCM au la Waislamu?
Na kama hali ndio hii,
hata akija Lowassa,
si itakuwa mambo ni
ya l e ya l e ? M a t h a l a n i
Wa i s l a m u w a k i s e m a
kuwa watamchagua
Edward Ngoyay Lowassa
kwa sababu ameahidi
kwamba akiingia Ikulu
atatumia Katiba na Sheria
za Nchi kuhakikisha kuwa
Masheikh walio ndani
wanapata haki zao, kama
akishindwa kutekeleza
na akawabamiza zaidi
Waislamu, watafanya nini?
Kama ndio hawa hawa
ambao wanadai kutendewa
isivyo na Serikali ya CCM
na wakajikuta hawana la
kufanya?
Toka amesimulia yule
Ustadh Jamal yaliyomkuta
Shimoni huku wenzake
waliojitaja kuwa ni Sabato
na Pentekoste wakiendelea
na shughuli zao mitaani
huria, Masheikh na
Waislamu kwa ujumla
wamefanya nini? Masheikh
k i m y a a ! ! ! Wa n a o n a
muhimu kwanza wampate
Mufti wao! Ili afanye nini?
Labda akamalizie biashara
i l i y o a c h wa n a M u f t i

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015


aliyetangulia ya kuuza
eneo la Wakfu, Kinondoni
Muslim!
Tujiulize, hivi ingekuwa
ni kijana wa Kikristo
amesimulia kuwa
amekutana na Polisi
a k a wa a c h i a we n z a k e
wawili waliojitambulisha
kuwa ni wa Madhhabi
ya Shafii na mwingine,
Ibadh, ila yeye kwa vile
kavaa Msalaba shingoni,
akaruswa kichura
kuingizwa katika difenda
kuelekea Guantanamo
Via Shimoni, Maaskofu
wangekuwa kimya mpaka
leo? Wabunge Wakristo,
vyama vya siasa, taasisi
zisizo za kiserikali (NGOs)
na vyombo vya habari,
wote hawa, wangekuwa
kimya mpaka sasa?
Kampeni hizi za akina
Lowassa na Magufuli
zingekuwa zikiendelea tu
na hali ikiwa shwari kabla
serikali haijasema kuwa
imemfanya nini askari
yule?
Kuna yule mwanamke
Muislamu aliyekamatwa
kwa kuwa mtuhumiwa
wa ujambazi alijificha
upenuni mwa nyumba
yake, akiwakwepa polisi.
A k a t e s wa k i k a t i l i n a
katika namna mbaya ya
kumdhalilisha. Kuachwa
akiwa katika hali zake
bila ya maji wala cha
kujihifadhi, mpaka siku
zake zikaisha! Tuseme
Tanzania Media Women's
Association (TAMWA),
Ta n z a n i a G e n d e r
Networking Programme
Mtandao(TGNP Mtandao),
Tanzania Women Lawyers
Association (TAWLA),
Legal and Human Rights

Centre (LHRC) na wengine


kama hao hawajasema.
Inaweza kueleweka. Na
akina mama wa Kiislamu
je? Kuna Baraza la akina
mama wa Kiislamu,
kuna vitengo vya akina
mama katika BAKWATA,
Baraza Kuu, na wasomi,
wataalamu WaislamuTa n z a n i a M u s l i m
Professionals Association
(TAMPRO) wakiwemo
wanasheria wanawake
ndani yake! Kipi
kinawashinda kulichukua
suala hili, kulijengea hoja
na kulishughulikia!
Ukijiuliza maswali haya
ndio utajua ukweli kwamba
aje Lowassa au Magufuli,
Waislamu hawana chao
maana wenyewe ndio
wamejiweka kihivyo. Kila
atakayekuja atabamiza
a p e nd a v y o , wa k i b a k i
kushangilia na kupiga
kofi.
Kama Lowassa
ni mabadiliko, na
mabadiliko ni Lowassa,
basi mabadiliko haya
hayatakuwa na maana
yoyote kwa Waislamu
muda wa kuwa Waislamu
wenyewe hawajabadilika
kwanza. Tutawalaumu
bure akina Magufuli na
Lowassa kumbe tatizo ni
sisi wenyewe.
Na hii ndiyo kanuni
ya Quran. Mabadiliko ya
Lowassa au muendelezo
wa sera za CCM chini ya
Magufuli, yatatunufaisha
vipi wakati nyoyo zetu na
hali zetu ni zile zile tukiwa
chini ya makucha ya CCM
ya N ye r e r e , M w i n y i ,
Mkapa na Kikwete?

Bismillahir Rahmanir Rahiim

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL


P.O.BOX 55105 , TEL: NO 2450069,
Mob: No 0687 820895 & 0716 960456 Dar Es Salaam.

PRE-FORM ONE PROGRAM

ITAANZA TAREHE 21/09/2015 - 27/11/2015


Program hii itaendeshwa hapa UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL kwa
wanafunzi wa Kiislamu wanaojiandaa kujiunga na kidato cha kwanza Januari, 2016
Masomo yafuatayo yatafundishwa na kutahiniwa:
1. Elimu ya Dini ya Kiislamu
2. Mathematics.
3. Arabic language
4. English language
5. Introduction to Computer
ADA: Tshs 100,000/= kwa program yote (Italipwa yote kabla ya kuanza masomo.)
Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni BURE baada ya kulipa ada.
Muda wa masomo:
Jumatatu - Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi8:30 mchana.
Jumamosi kuanzia saa 2:00 Asubuhi8:30 mchana
Masomo yataanza rasmi tarehe 21/09/2015
Jiandikishe kuanzia 11/09/2015 ofisi ya Mkuu wa Shule
Ubungo Islamic High School kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:00 mchana .
Wahi mapema nafasi hii adhimu
Wabillah tawfiiq
MKUU WA SHULE

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Ujerumani kutumia Euro


bilioni 10 kwa wakimbizi

HARAMA za kifedha
zitakazotumika
kuwahudumia watu
wanaotafuta hifadhi nchini
Ujerumani, zinaweza
kufikia Euro zisizopungua
bilioni kumi ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu,
kiwango ambacho ni mara
nne ya kile kilichotumiwa
na serikali ya Berlin mwaka
jana kwa ajili ya wakimbizi.
Ofisi ya takwimu ya
Ujerumani imeripoti kuwa
Euro bilioni 2.4 zimetumika
kuwahudumia wakimbizi
wapya 203,000 waliongia
nchini humo mwaka jana.
Mkutano kuhusu
Wa k i m b i z i u l i o f a n y i k a
mwezi Julai kwa
kusimamiwa na Bunge la
Ujerumani ulikadiria bajeti
ya Euro bilioni 5.6 kwa ajili
ya kuwapokea wakimbizi
450,000, huku wimbi la
hivi karibuni la wakimbizi
kutoka eneo la Mashariki
ya Kati na Afrika likipita
makadirio ya awali.
Wakimbizi wasiopungua
laki nane wanatazamiwa
kuwasili Ujerumani hadi
kufikia mwishoni mwa
mwaka huu. Katika siku
za hivi karibuni maelfu ya
wakimbizi kutoka Syria
wamefanikiwa kuondoka
Hungary baada ya kukwama
nchini humo kwa siku
kadhaa na sasa wanaelekea
Austria na Ujerumani nchi
ambazo zimetangaza kuwa
tayari kuwapokea.
Wakati hali ikiwa hivyo,
Shirika la Kuhudumia
Wa k i m b i z i D u n i a n i
UNHCR, limezitaka nchi za
Ulaya zichukue wakimbizi
laki mbili.
Nchi za Umoja wa Ulaya
lazima zikubali kuwapa
hifadhi wakimbizi laki mbili
kama sehemu ya Mkakati
wa pamoja wa kukabiliana
na mgogoro wa wakimbizi
duniani.
Hiyo ni kauli ya Mkuu wa
Shirika la Umoja wa Mataifa
la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) Antonia Guterres,
ambaye amezitaka nchi za
Umoja wa Ulaya kutumia
nguvu zao zote kutatua
mgogoro uliopo.
Hayo yamejiri wakati
ambapo mwishoni mwa
wiki maelfu ya wakimbizi
kutoka Hungary wameingia
nchi jirani ya Austria.
Sehemu kubwa ya
wakimbizi hao ambao ni
kutoka Syria, wanatazamiwa
kuelekea Ujerumani.
Austria imesema wakimbizi
6,000 wameingia nchini
humo na wengine wengi

wanatarajiwa kuwasili katika


kile kinachotajwa kuwa na
mgogoro mkubwa zaidi
wa wakimbizi barani Ulaya
tangu vita vya Yugoslavia
katika muongo wa 1990.
Ulaya inakabiliwa
na wimbi kubwa zaidi la
wakimbizi ambapo watu
300,000 wakiwa wameyaweka
maisha yao hatarini kuvuka
Bahari ya Mediterenia na
kueleka katika nchi za bara
hilo mwaka huu pekee.
Wakimbizi hao ni kutoka
nchi za Afrika na Mashariki
ya Kati.
Z a i d i ya wa t u 2 , 6 0 0
wamefariki dunia wakijaribu
kuvuka bahari hiyo, akiwemo
mtoto wa Syria aliyeitwa
Aylan Kurdi, aliyekuwa
na umri wa miaka mitatu,
ambaye picha ya maiti yake
iliyoonekana akiwa amelala
pwani nchini Uturuki baada
ya k u s o m b wa n a m a j i ,
imeibua huzuni kubwa katika
nyoyo za watu kote duniani.
Rais Vladimir Putin wa
Urusu amesema mgogoro huo
wa wakimbizi umesbabishwa
na sera mbovu za Umoja
wa Ulaya, kuingilia mambo
ya ndani ya nchi za Afrika
Kaskazini na Mashariki ya
Kati.
Rais Vladmir Putin alisema
I j u m a a i l i y o p i t a k u wa ,
mgogoro wa wahamiaji
unaolikabili bara Ulaya kwa

Qatar, Saudia
zilikubaliana
kuibomoa SyriAssange

sasa umetokana na sera


mbovu za kigeni za nchi
za bara hilo, hususan zile
ambazo ni wanachama wa
Umoja wa Ulaya (EU).
Kiongozi huyo alisisitiza
kuwa, uingiliaji wa
Wamagharibi katika mambo
ya ndani nchi za Mashariki
ya Kati na Kaskazini mwa
Afrika ni moja ya sababu
za kuibuka mgogoro wa
wahajiri katika nchi za EU.
Rais Putin alisema viongozi
wa Ulaya wameingia kwenye
mtego wa Marekani kwa
kukubali kufuata kibubusa
sera zake, hususan katika
ulimwengu wa Kiislamu na

kwa mantiki hiyo migogoro


ya kisiasa katika nchi za
Syria, Libya, Somalia, Yemen
na kwingineko imewafanya
raia wa nchi hizo kukimbilia
usalama wao barani Ulaya.
"Wanawatwisha watu
sera zao kwa lazima bila ya
kujali itikadi zao za kidini,
utamaduni wao na muundo
wa jamii. Hilo lazima litaleta
matatizo makubwa", alisema
Putin.
R a i s h u y o wa U r u s i
ametahadharisha kuwa, EU
na Marekani zisipobadili sera
zao za kigeni, mgogoro huo
utakuwa mpana zaidi katika
siku za usoni. Irib.

wanzilishi wa tovuti
ya whistleblower
Julian Paul
Assange, ametoa siri ya
makubaliano yaliyofanywa
na nchi za Qatar, Uturuki na
Saudi Arabia ya kuiangusha
serikali ya Syria.
Assange alifichua siri hiyo
katika televishen ya Urusi
akisema kuwa, makubaliano
hayo yalipitishwa na
kusainiwa kwa siri mwaka
2012 na nchi hizo tatu, huku
nchi za Magharibi kama
vile Ufaransa, Uingereza na
Marekani wakiunga mkuno
makubaliano hayo.
Aidha alisema washirika
wa Marekani katika nchi za
Mashariki ya Kati walisaini
makubaliano hayo kwa
ajili ya kukuza uhasama
dhidi ya serikali ya Syria,
kiasi kwamba serikali ya
Saudi Arabia ili kuonyesha
uhasama wake, ilifikia
hatua ya kukiuka hata
mapendekezo ya waanzilishi
wa fikra hiyo ambao ni
serikali ya Marekani katika
suala hilo.
Uthibitisho wa kuwepo
makubaliano hayo ni
miungoni mwa nyaraka
nyingi za siri, ambazo
z i m e o n ye s h a u o v u wa
b a a d h i ya m a t a i f a n a
serikali za Mashariki ya
Kati zinazotafuta nguvu
kibabe ikiwemo msimamizi
wao mkuu (utawala Saudi
Arabia).

kile walichofanyiwa
Masheikh wetu hivi nani
hajui kama Masheikh wetu
wamedhalilishwa na ku
amesema huku akionesha
uchungu.
Wa k a t i M a n s o o r
akiyasema hayo, uwanja
ulikuwa kimya watu
wametulia wakimsikiliza kwa
makini namna anavyojenga
hoja na kuonesha kwamba
alichokuwa akikizungumza
kikiingia akilini mwao.
Mansoor amehoji
watu wenye kujiita
wana Mapinduzi, lakini
wakashindwa kuyatekeleza
m a l e n g o ya M a p i n d u z i
ambayo yameasisiwa na
aliyekuwa Rais wa Kwanza
wa Zanzibar Marehemu
Mzee Abeid Amani Karume
ambapo alitaka wananchi
wote kuishi bila ya ubaguzi.
Ni jambo la kushangaza
ndugu zangu, vikosi vya
ulinzi na usalama ambao
wamepoteza roho zao
kwa ajili ya Mapinduzi na

kutaka kujitawala, leo hii


wao ndio wanahusika katika
kuwadhalilisha Wazanzibari,
wao ndio wamekuwa
wakiwadhalilisha,
wakiwakashifu na
wakiwanajisi Wazanzibari,
inasikitisha kuona vikosi
hivyo hivyo leo hii
wakiwatesa Wazanzibari,
wakiwapiga wakiwavua
nguo ndugu zetu wa kike
na kuwakadhifu hadharani,
inasikitisha sana na baadhi
ya viongozi wanapanda
majukwaani wakifurahia
na kucheka, tunaelekea
wapi ndugu zangu? Alihoji
Mansoor.
Mansoor alisema viongozi
wa aina hiyo hawafai kupewa
nafasi tena ya kurudi
madarakani kwa sababu
wakirejeshwa wanaweza
kuyafurahia tena yale
matendo mabaya waliokuwa
wakifanyiwa Wazanzibari ya

kudhalilishwa utu wao.


Alisema kwa sasa haoni
kama kuna kiongozi wa
CCM ambaye ataweza
kurejesha heshima na hadhi
ya Zanzibar.
Hivyo amewataka
Wazanzibari kumuunga
mkono Maalim Seif
wampitishe kwa kumpa
kura nyingi ili aweze
kuirejesha hadhi na heshima
ya Wazanzibari ambayo
imepotea kutokana na mfumo
mbovu uliopo unaoongozwa
na chama cha mapinduzi.
Mansoor alisema jambo
la msingi kwa wote na
Watanzania ni kurejeshwa
kwa mamlaka kamili ya
Zanzibar na mamlaka ya
Tanganyika ambapo alisema
viongozi wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi UKAWA
ndio watakaoweza kutetea
Muungano wa usawa na
haki.

Rais Vladmir Putin

Mansour awaliza Waislam

Inatoka Uk. 3
Chama Cha Wananchi (CUF)
Maalim Seif Sharif Hamad
a l i wa t a k a Wa z a n z i b a r i
kutokubali kuendelea
kuwaunga mkono watu
a m b a o wa n a h u s i k a n a
udhalilishaji wa Masheikh.
Mansoor alisema ni
jambo la kusikitisha
k u o n a wa p o b a a d h i ya
viongozi wanapanda
majukwaani na kufurahia
kile kinachotendeka dhidi
ya Masheikh wa Jumuiya
ya Uamsho ambao kesi
ya o i m e k u wa i k i p i g wa
kalenda kila siku badala
ya kusikilizwa na kupewa
hukumu kwa mujibu wa
makosa yao.
Ndugu
zangu
Wazanzibari, msije kukubali
hata siku moja kuwarejesha
madarakani viongozi wote
wanaochangia au kufurahia
udhalilishaji wanaofanyiwa
Masheikh zetu, leo hii
anasimama kiongozi
j u k wa a n i n a k u f u r a h i a

Makala

Viongozi Bakwata Mwanga


mtajibu nini kwa Mola wenu

IANZE kwa
kumshukuru
Allah (S.W.) kwa
kukumbuka kuanzishwa
k wa s h u l e ya a wa l i
katika Msikiti Mkuu wa
zamani wa Same mjini.
Uanzishwaji wa shule hii
ulitokana na Ijitimai ya
kitaifa iliyofanywa Mkoa
wa Kilimanjaro Wilayani
Mwanga chini ya uongozi
wa Tablighi ya kituo cha
Gongolamboto jijini Dar
es salaam. Niliteuliwa
na Amiri wa Mkoa
wa K i l i m a n j a r o B w .
Atumani, kuhamasisha
Waislamu wa Wilaya ya
Same, na kusambaza kadi
za mualiko.
Tulifanikiwa katika
Msikiti wa Same kukodisha
basi lililojulikana kwa jina
Sirori la Bw. Habibu
Mndeme (marehemu).
Tulijaza gari tukiwa na
viongozi wa Bakwata wa
Wilaya, akina mama, kina
baba na vijana. Ijitimai
hiyo ilifanyiwa katika
eneo ambalo ni kiwanja

cha ekari arobaini 40, ambalo


lilikuwa ni la kujenga Kituo
c h a Ta b l i g h i , S h u l e n a
Chuo cha dini ya Kiislamu.
M a h u d h u r i o ya l i k u wa
makubwa kiasi kwamba
Station Master aliombwa
na akakubali kuwa treni
iliyobeba Waislamu kutoka
Mombasa isimame chini
ya eneo hili liliopo karibu
na barabara ya kwenda
Langata, na ikasimama
Waislamu wakashuka.
Walihudhuria Waislamu
wa nchi mbali mbali
waliwemo wa Zambia n.k.
K u l i k u wa k u m e j e n g wa
sehemu ya kuwekwa jiwe
la msingi, na mgeni wa
heshima wa kuweka jiwe hilo
alikuwa mi Mufti Hemedi
bin Juma (Al-marhum).
Nilipiga picha za shughuli
zote zilizofanyika kwa muda
wa siku tatu. Lakini sasa
maktaba yangu inanisuta na
kuwasuta Waislamu.
Kundi la Matablighi
la kima mama walifanya
kazi kubwa sana tena sana
Allah S.W. Awalipe ujira
wao Inshaallah. Wakina
mama wa Msikiti wa Same
c h i n i ya k i o n g o z i wa o
Fatuma Kasagho tuliporudi
Same, nilikuwa Katibu wa
Msikiti huo, aliniambia
kuwa niwaelekeze jinsi
ya k u a n z i s h a S h u l e ya
chekechea hapo Msikitini,

m a a n a wa l i y o ya s i k i a
katika Ijitimai yanatosha,
kwani kumbe kuwapeleka
watoto wa Kiislamu katika
chekechea za Kanisa ni
kuwaritadisha. Palitokea
msuguano na uongozi
wa Msikiti kwa upande
mmoja na Mtaa na Wilaya
kwa upande mwingine,
Bakwata, wakisema
kuwa wao hawako
tayari kendesha shule.
Hawana pesa, hawana
uwezo. Hata hivyo
kina mama wakasema
k u wa wa t a j i t e g e m e a
wao kama kina mama
katika kuendesha shule
hiyo, kama kina baba

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

JIWE LA MSINGI LILOWEKWA NA MUFT HEMED LILIVYO KWA SASA

MAJENGO YA SHULE YALIYOJENGWA WAKATI WA


MWANGA.
watawasaidia ni hiyari walijenga majengo zaidi ya
yao.
matatu yakafikia hatua ya
I l i p o f i k a m w a k a kupauliwa, lakini viongozi
wa 1 9 9 1 M a m a h u y o wa B a k wa ta Mwa n g a
kiongozi, aliwahamasisha wakasema eneo lile ni la
kina mama wakawatoa kwao ukazuka mvutano
watoto wote waliokuwa wa kesi kiasi kwamba
wakisoma katika Kanisa Tablighi waliacha eneo
na tukaanzisha Shule hiyo lile baada ya kesi ya miaka
ambayo imesimamiwa mingi, wakaenda kuomba
na kina mama mpaka leo eneo jingine.
ina robo karine. Nasema
Baada ya miaka
Alhamdulillah kisha k a d h a a , n i l i k u w a
Alhamdulillah. Maktaba n a h a m u ya k we n d a
yangu inanisuta! Kwa kuona kilichoendelea.
sababu ninazo kumbu Nilikuta pori na zile
k u m b u z a p i c h a z a kuta za yale majengo
Wahadhiri mbalimbali waliyojenga Matablighi
waliohadhiri wakati huo; z i k i w a z i m e a n z a
na ya aliyekuwa Mufti kuyeyushwa na mvua.
wakati huo Sheikh Hemedi Bakwata waliopigania
bin Juma, wakati akiweka eneo hilo kuwa ni lao
jiwe la msingi la kituo hakuna walichofanya.
hicho; na kanda za kasseti Nilizichukua picha hizo
nilizorekodi zinanisuta, hapo. Baada ya robo karine
kuwa kwa robo karine, nilienda tarehe 27/08/2015
eneo lile ambalo Matablighi kushuhudia maendeleo

HARAKATI ZA MARKAZ
yaliyofanywa na Viongozi
wa Bakwata Mwanga.
Innalillahi wa innailaihir
rajiuun. Hakuna kitu.
Nikajiuliza, kwa nini
wa l i wa p o r a e n e o l i l e
Tabligh mpaka kupeleka
kesi mahakamani?
Katika eneo lile,
nilikuta kimebaki kile
kisehemu kilichojengwa
kwa ajili ya kuweka jiwe
la msingi, kwa kuwa
kijengwa kwa matofali ya
sementi, nacho kimechoka
hata lile jiwe la msingi
limeanza kubomoka kama
linavyoonena katika picha
na mandhari yake. Na
yale majengo yaliyokuwa
yamejengwa kwa matofali
ya kuchoma na Matablighi,
yamebomolewa yote
kiasi kwamba hata
misingi yake haionekani,
ambapo Matablighi
walishapeleka mbao za

kupaulia, na baadhi ya
majengo walishaweka
fremu na kuezeka kama
inavyoonekana kwenye
picha.
Na eneo limekuwa ni
makorongo, na sehemu
ya eneo na jiwe la msingi
ni uwanja wanachezea
mpira watoto wa shule.
Nilipouliza kwa robo
karine sasa, Bakwata wana
mpango gani na eneo
lile walilowanyanganya
Tabligh, sikupata jibu.
Labda tu niwakumbushe
viongozi wa Bakwata wa
Wilaya ya Mwanga kuwa,
kila kitu tulichofanya
na wanachofanya
kinarekodiwa, na mwenye
sifa ya kujua kila kitu-Allah
Subhana wa Taaallah. Na
siku ya Qiyama sio picha
nilizopiga katika ile Jitimai
wala hizi nilizopiga kwa
mara ya pili na ya tatu
zitakazoonyesha kama
ushahidi wa kilichotendeka
na kinachotendeka mahali
pale; bali ni kila aliye
kwamisha mradi ule wa
kituo cha Tablighi atajibu.
Kama ni kwa Qibri chake,
ukubwa wa cheo chake,
ukubwa wa elimu yake,
umaarufu wake kwenye
dola na uwezo wa
kuwachangisha Waislamu
pesa za kuendeshea
kesi zilizokwamisha
maendeleo yao kama haya
ya robo karine, yote hayo
yatawekwa wazi siku ya
hukumu.
Nimalizie kwa kusema
kuwa, 1992 ilianza
kutafutwa Ardhi ya
kujenga Kituo cha Kiislamu
Same Kirinjiko, 1994,
eneo likapatikana. Kazi
ya kufeka eneo ilianza,
na ujenzi ikaanza 1996
na Shule ikaanza 2000.
Sasa ni kituo kikubwa cha
Kiislamu kikiwa na shule
ya msingi, sekondari na
chuo cha ualimu. Vijana
wa Kiislamu wanahitimu
kila mwaka katika ngazi
mbalimbali.
Maktaba yangu
inanisuta! Kuwa, katika
Wilaya ya Mwanga juhudi
z i l e z i m e k wa m i s h wa
na Bakwata. Wasiwasi
wangu mkubwa ni
pale niliposhiriki futari
M wa n g a m wa k a j a n a
na kiongozi aliyetualika
futari hiyo akatoa ahadi
k u wa i t a f u t we A r d h i
yenye wasaa ya kujengwa
shule na chuo cha
Kiislamu, ataleta marafiki
zake wasaidie kujenga
chuo hicho lakini hadi
sasa sijasikia chochote.
Sijui kuwa katika futari
ya mwaka huu kulikuwa
na mrejesho gani. Allah
S.W. atuzindue katika kiza
hiki totoro cha kiuongozi
wilayani Mwanga
Inshaallah.
(Khatibu Juma Mziray.
0757 01 33 44. 31/08/2015)

MAKALA

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Tusilazimishe ndoa kama hatupendwi!


Na Juma Jumanne

I A N Z E t u k wa
kusema Innaa
Lillah Wa-Innaa
Ilayh Rajiun. Hivi ndivyo
alivyotufundisha Allah
(swt) katika Suratul
Baqara [02:156] aliposema,
Wale ambao ukiwasibu
msiba husema: Hakika
sisi ni wa Mwenyezi
Mungu, na kwake Yeye
hakika tutarejea. Aya
hii imewalenga wale
wenye kusubiri pindi
wanapopatwa na msiba.
Kumradhi kwa msemo
nilioanza nao.
Waislamu tumeingia
katika mtihani mzito wa
kulazimishwa kupenda
jambo moja kubwa
ambalo Allah Mtukufu
ametuwekea kama njia ya
kuingia katika maisha ya
milele. Nasema hivi kwa
sababu jambo lenyewe lipo
lakini tunaliogopa mno,
nalo ni kifo. Hali inatisha,
inasikitisha, inaumiza,
inachosha, inamaliza upeo
wote wa kufikiri!!? Kifo ni
njia pekee ambayo Allah
(swt) ameiweka ili iwe
njia pekee ya kukutana
naye na kumuona ikiwa
t u t a f a n i k i wa k u p a t a
mwisho mwema. Siyo
wote watakaofanikiwa
kumuona Allah (swt).
Allah Mtukufu
anasema, AMETUKUKA
ambaye mkononi mwake
umo Ufalme wote; na
Yeye ni Mwenye uweza
juu ya kila kitu. Ambaye
ameumba mauti na uhai
ili kukujaribuni ni nani
miongoni mwenu mwenye
vitendo vizuri zaidi. Na
Yeye ni Mwenye nguvu na
Mwenye msamaha. (QurAn 67:01-02).
Ndugu zanguni, kwa
hali iliyopo, hatuna sababu
ya kuipenda dunia. Mimi
sikusuii kupenda dunia
lakini nikuulize swali
moja wewe unayetamani
kuishi sana. Ukane imani
yako uishi, au udhihirishe
imani yako uuwawe?
Kumbe mavazi, ndevu,
na majina yetu sasa ni
tiketi ya kifo, kuteswa,
kudhalilishwa!!? Kupigwa,
kuteswa, kudungwa
sindano tunaona ni jambo
dogo siyo? Hizo sindano
wanazodungwa ndugu
zetu hatujiulizi zina nini?
Tusubiri nasi yatukute.
Vyombo vyetu leo
vinavyojiita vya usalama
havina haja tena ya kufanya

upelelezi, bali wanaishia


tu kuangalia mwonekano
wa nje. Ukionekana
umebeba jembe, basi
moja kwa moja wanasema
huyu ni mkulima? Mtu
unajiuliza maswali mengi
yasiyokuwa na majibu
kwa sababu hali inatisha.
Mambo yanayofanyika
ni mazito na ukijaribu
kunasibisha hali hii na
namna tunavyochakarika
mtaani, ni vitu viwili
tofauti.
Lakini tutambue
kuwa, kwa hakika
h a k u n a m wa n a d a m u
atakayeepukana na
kifo. Hawa madhaalimu
wanaowatesa ndugu zetu
watambue kuwa yupo
Mfalme wa haki! Yupo
Jabaar. Yupo Qahaar!!
Wa t u t e s e , wa t u f a n ye
wanavyotaka lakini
watambue kwamba
watawaua Waislamu lakini
Uislamu utabaki kwa kuwa
aliyeuleta hana sifa ya
kufa! Hana sifa ya kusinzia
wala kula. Wasubiri punde
tu watakutana na adhabu
za Allah aliye juu.
Allah Mtukufu
anasema, Kabla yenu
zimepita nyendo nyingi;
basi tembeeni katika
ulimwengu muangalie
vipi ulikuwa mwisho wa
wanao kanusha [Qur-an:
03:137].
Misri siyo mbali, wafike
washuhudie aliyejifanya
mungu anavyodhalilika.
Wa m u o n e F i r a u n
aliyejiita mungu. Firaun
aliyewatesa wana wa Israili
kwa kuwapa kazi ngumu,
kuwaulia watoto wao
na kila aina ya madhila.
Yeye na jeshi lake wote
waliangamizwa.
Pamoja na hali
kama hii, lakini bado
Waislamu wanaipenda
C C M . Wa n a wa p e n d a
wana-CCM! Japo
hujidai tunawachukia,
cha ajabu tukikutana
kwenye siasa tunagonga
cheers! Tunawasaidia
kufanikisha azma yao
ya k u e n d e l e a k u k a a
Ikulu. Kinachotufanya
tujipendekeze kwa hawa
madhaalim ni kipi haswa!?
Anayetoa riziki yupo, au
hayupo!!? Ipi tofauti yetu
na mwanamke anayejidai
hampendi mumewe ilhali
wa t o t o wa n a e n d e l e a
kupatikana!!? Anajidai
kumsema vibaya mumewe,
lakini mimba zinaingia na
watoto wanapatikana.
N i n y i Wa i s l a m u
mnaoipenda CCM hii,
ni kwa sababu ya elfu

MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (katikati) siku alipowakabidhi Ilani


ya Uchaguzi wa chama hicho kwa mgombea wake wa Urais, Dk. John Magufuli.
tano mnazopewa kipindi eti ashindwa kuzungumza Hata kama angetumia
cha kampeni au mna atakavyotatua changamoto siku nzima kuzungumza
pale uwanjani, kwetu sisi
ajenda nyingine. Hivi ni za wananchi.
H i v i
n d i v y o wenye kujua hali iliyopo,
kweli tamaa zetu ndio
waandishi wa gazeti hili tungeona hana jipya tu.
zimetufikisha hapo!!!?
Lakini pia, kusema
Siku moja nipo maeneo walivyoandika. Lakini
mimi
niseme
tu
kuwa,
suala
kwamba
kauli za viongozi
ya stendi, nasubiri mzigo
k u t o k a M b e y a , k w a la kutumia muda mchache w a d i n i z i l i o n e s h a
pembeni yangu alikuwepo s i y o t a t i z o k w a n g u , kununuliwa, sina haja ya
dereva bodaboda akasema kwa sababu kusema na kujua wamenunuliwa kwa
yeye yupo tayari kupigia kutenda ni vitu viwili bei gani. Kwenye nukta
kura jiwe kuliko kuipigia tofauti kabisa. Hata kama hii niwakumbushe tu
C C M . K wa m s i s i t i z o Lowassa angesimama waandishi hawa kwamba,
na kusalimia tu, kisha hawakusikia kauli za
akasema:
Kwa
n a m n a akakaa kitako bado nampa Benjamini William Mkapa?
nilivyoichoka CCM, hata b i g u p . K wa n i C C M K u w a i t a w a p i n z a n i
k i k i k o s e k a n a c h a m a wameanza lini kusimama wapumbavu na malofa
p i n z a n i i k a w a j i w e na kuzungumza, mpaka ndiyo sawa siyo?
limesimamishwa dhidi wametuundia TOT ya
Serikali yetu ya
ya CCM, mimi nalipa jiwe mipasho kutupumbaza C C M i n a u g o m v i n a
kwa maneno yao, lakini
kura yangu.
Waislamu. Kwa namna
S i k u t a k a k u d a d i s i hakuna kitu!? Mara ngapi wanavyowashughulikia
CCM
wanasimama
na
sana kwa kuwa, hakuna
jipya alilosema zaidi ya ilani yao na wanayofanya W a i s l a m u , l a i t i
kuongeza nguvu katika ni vingine kabisa? Lakini wa n g e e l e k e z a n g u v u
k i l e n i n a c h o k i a m i n i . suala la kutozungumzia hizo kwa vibaka, wezi,
Maslahi binafsi, ulafi, namna atakavyotatua majambazi, makahaba
unafiki na mengineyo changamoto pia halina na mfano wa hayo, hali
n d i y o ya n a y o t u f a n ya nafasi kwenye kampeni ingekuwa shwari kabisa.
tuendelee kuipenda CCM. hii. Sisi tunachotaka ni
Chama Cha Mapinduzi,
Tusilazimishe ndoa kama utatuzi wa changamoto C C M h a t a k a m a
na
siyo
kujua
namna
hatupendwi, hatupendwi
z i t a k a v y o t a t u l i w a . wakiandika ilani ndefu,
tu. Ya nini tujipendekeze.
Leo nakubali kupiga Hata kama akisimama urefu wa barabara zote
kampeni, siyo kumpigia kutangaza tu kwamba, za lami ilizojenga, bado
Lowassa bali kampeni m s i i p i g i e k u r a C C M , sitawaelewa. Nafasi yao
ya kutoipigia kura CCM. b i n a f s i n a m u e l e w a kwenye kampeni hizi
Aliyosema Ustadh Jamal kwa kuwa mimi siyo ni kutangaza mafanikio
Yasin itoshe kuwa kampeni mhamiaji bali raia wa ya ilani zao zilizopita na
ya kuifuta CCM.
nchi hii. Waliyofanya
K a t i k a g a z e t i l a CCM na wanayoendelea sababu za kushindwa
Mzalendo toleo nambari kutufanyia Waislamu kutatua yale waliyoahidi,
2308 la Jumapili Agosti 30 h a y a h i t a j i i k a m p e n i n a s i y o k u w a n a n g a
wapinzani. Wapinzani
Septemba 5, 2015, kwenye jamani!!
Kusema kwamba Dk. wanayo haki ya kuponda
ukurasa wa mbele kabisa
wanasema; Rekodi ya Dk. M a g u f u l i a m e t u m i a chama tawala. Hatukatai
Magufuli Dar yamshinda muda mrefu (dakika 58), kama wamefanya, lakini
Lowassa. Akaendelea ndio tayari ameshatatua siyo kama ilivyotakiwa
kusema kwamba, Lowassa changamoto hizo? Mambo kufanywa. Wamefanya
a t u m i a d a k i k a n a n e aliyokuja nayo mgombea
kuzungumza, ilani ya wa CCM yana upya gani? chini ya kiwango kwa
ukawa yakosekana, lakini Tumechoshwa na maneno, m u d a m r e f u s a s a .
kama haitoshi wakasema tunataka kuona utendaji. Watupishe!

WENYEZI Mungu
hawaadhibu watu
m p a k a a wa l e t e e
mjumbe. Hivyo ndivyo
Quran inavyotwambia.
Kwa upande mwingine,
katika mazingira ya dharura,
jambo lililo haram, laweza
kuruhusiwa, lakini kwa
k i wa n g o c h a k u o n d o a
dharura ila isiwe ni jambo la
kufurahiwa na kuachwa liwe
la kawaida na kuzoeleka.
Kwa kipindi kirefu hapa
n c h i n i , Wa i s l a m u , h a s a
wafanyabiashara, walikuwa
katika kilio cha kuendesha
biashara zao kupitia benki
ambazo ni za mfumo wa
riba. Hata hivyo, jitihada
zilizofanywa na baadhi ya
Waislamu, kwa rehema za
Allah (SWT), imepatikana
Benki ya Amana ambayo
imeondoa dharura hiyo.
Hivi sasa mfanyabiashara
Muislamu akifanya biashara
zake kupitia benki za mifumo
ya riba, itakuwa ni kwa
kutaka mwenyewe na hivyo
ajiandae kumjibu Mola wake
juu ya dhambi hiyo.
Ili kujua ni kwa namna gani
Benki za Kiislamu zinafanya
kazi, na zinawasaidia
vipi na kuwawezesha
wafanyabiashara, fuatilia
mahojiano haya na
Mkurugenzi Mtendaji
wa Amana Benki upate
kuelimika.
Asalaam aleikum Dr.
Muhsin; ni mara yetu ya
kwanza kukutana na
ningependa nichukuwe nafasi
kukupongeza kwa kuteuliwa
na bodi ya Amana Benki
katika uongozi na usimamizi
wa Benki hii ya Kiislam
Tanzania. Tunashukuru kwa
kutupa muda wako kwa
ajili ya kuongea nasi. Lengo
letu ni kutaka kuwasaidia
watanzania walio wengi
waelewe nini Amana Benki
na uendeshaji wake katika
kuzingatia Sharia za Kiislamu
na mchango wake katika
mfumo wote wa kibenki
nchini.
Jibu: Waleikumsalaam,
Ahsante sana, na karibu sana
Amana Benki.
Kwanza kabisa napenda
nianze kwa kuchukua fursa
hii adhimu kuwashukuru
kwa dhati kabisa wadau
wetu wote kwa muitikio wao
ambao wamechangia katika
ukuaji wa Amana Bank tokea
kuanzishwa kwake mwezi
November 2011 mpaka hivi
sasa tunapokaribia miaka
mi nne.
Natoa shukrani za dhati
kwa wateja wetu ambao
wametupa muitikio mzuri
kwa kutumia huduma zetu.
Pia nawashukuru wanahisa
wetu kwa uwekezaji wao
na uvumilivu wao katika
kipindi cha mwanzo wa Benki

Makala

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Biashara
ya
riba
sasa
basi
Amana Benki yatoa ufumbuzi

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Kiislamu Amana, Dr.


Muhsin Masoud.
ambacho kwa kawaida huwa
ni kigumu kwa wawekezaji.
Natambua mchango
mkubwa wa wakurugunzi
wa Amana Benki kwa
mawazo yao na muongozo
w a o . Wa f a n y a k a z i w a
Amana Benki nawapongeza
sana kwa weledi wao
ambao umeiwezesha Benki
kuweza kufikia hatua hii
na pia nawataka waongeze
juhudi na ubora wa utendaji
katika uwanja huu ambao
una ushindani mkubwa wa
kibiashara. Naishukuru sana
Benki Kuu ya Tanzania na
serikali kwa ujumla kwa
kuwezesha uanzishaji wa
taasisi ya kifedha inayofuata
misingi ya Kiislamu na
naviomba vyombo vyetu
hivi vitusaidie kutengeneza
mazingira mazuri zaidi
ya kutuwezesha kufanya
shughuli zetu kwa ufanisi
mkubwa.
Swali: Je ni kitu kipi
kinakupa muongozo katika
uendeshaji wa shughuli za
Amana Benki?
Jibu: Ni Dira yetu. Dira
yetu inatuelekeza tujizatiti
kuwa ni chaguo la kwanza
na kuongoza katika
utoaji huduma za kibenki
zinazofuata Sharia za Kiislam
katika masoko yetu. Dira hii
inafuatiwa na dhamira yetu
ya kutoa huduma za kisasa
na za kipekee zinazofuata
Sharia za kibenki za Kiislamu
kikamilifu kwa kuzingatia
maadili na kwa njia iliyo wazi
kwa kutumia teknolojia ya
kisasa. Pamoja na kuzingatia
dira na dhamira hizi, Benki

yetu pia inazingatia misingi


mitano mikuu katika
kuendesha shughuli zake
ambayo ni Uadilifu, Taaluma,
Uwazi, Uaminifu na Usikivu.
Tumejikita pia katika sifa
kuu nne katika utendaji
wetu wa kila siku ambazo
ni uzingatiaji wa ubora wa
hali ya juu wa kiutendaji
na utoaji wa huduma kwa
kuzingatia wito uliotukuka.
Sisi wafanyakazi wa Amana
Benki tunazingatia sifa
hizi katika utendaji wetu
na mahusiano yetu na kwa
wadau wetu wote.
Kwa kuzingatia Dira,
Dhamira na misingi mikuu,
tumejikita katika kuijenga
Amana Benki katika maadili
ya hali juu na kuipanua
huduma hii kwa kuanzia na
maeneo yote ya Tanzania na
nje ya mipaka ya Tanzania kwa
kuzingatia mkakati wa muda
wa miaka mitano ambao
unafanyiwa marekebisho
kila baada ya mwaka mmoja.
Tunajenga Benki ambayo
inazingatia matakwa ya Jamii
na uboreshaji wa mazingira.
Swali: Tueleze kwa ufupi
kuhusiana na mfumo huu wa
fedha wa Kiislamu.
Jibu: M fumo wa fedha
wa Kiislam ni mfumo
unaofuata misingi ya Sharia
(Fiqh al muamalat) ambao
unajumuisha benki za
Kiislam, bima za Kiislamu
(Takaful) na masoko ya
dhamana (sukuk). Mfumo
huu umeendelea kuenea
kwa kasi sana katika miaka
ya karibuni sio tu katika
nchi za Kiislamu, lakini

umeenea duniani kote. Hali


hii imepelekea mfumo huu
kuingia katika mjumuisho wa
kifedha (financial inclusion)
katika uchumi wa mataifa
mbali mbali likiwemo
Tanzania. Kinyume kabisa na
mfumo wa kisekula ambao uti
wake wa mgongo ni misingi
ya riba, mfumo wa Kiislamu
pamoja na mambo mengine
kama ilivyo katika Sharia,
umeharamisha misingi ya
riba katika utendaji wake:
Enyi mlio amini! Msile
riba mkizidisha juu kwa juu,
na mcheni Mwenyezi Mungu
ili mpate kufanikiwa. Quran
3:130
Hadi sasa, nchi nyingi
katika maeneo ya Asia,
Afrika, Mashariki ya Kati,
Bara la Ulaya, na Amerika,
zimeamua kuutumia mfumo
huu kufuatia umadhubuti
wake juu ya mfumo wa
kisekula na kupelekea
kukubalika katika jamii
mbali mbali zilizo na zisizo
za Kiislamu. Kwa mujibu
wa mkutano wa kumi wa
uchumi wa Kiislamu WIEF
(World Islamic Economic
Forum) uliofanyika Octoba,
2014 Dubai UAE, thamani
ya mfumo wa fedha wa
Kiislamu umefikia dola
trilioni nane ($8 Trillion)
ambayo ni sawa na 11% ya
uchumi wa dunia ikiwa na
ongezeko la 6.3% kwa mwaka
wakati mfumo wa kisekula
ukiwa na ongezeko la 5.3%
kwa mwaka.
Swali: Nini hasa tofauti
kati ya mifumo wa fedha wa
Kiislamu na ule wa kisekula?
Jibu: Katika jamii yetu
kuna hali ya mkanganyiko
miongoni mwa watu wengi
juu ya mfumo wa fedha wa
Kiislamu ambapo wapo
wanaoona kwamba mfumo
huu hauna chochote cha zaidi
isipokuwa ni kubadilisha na
kuupachika jina la Mfumo
wa Kiislamu, na riba na
kuiita faida. Hii ni hoja
ambayo inaharibu mawazo,
fikra na mitazamo ya baadhi
ya watu. Tofauti iliyopo
katika mifumo hii ni pamoja
na:Benki za Kiislamu hazitoi
mikopo ya fedha taslim kama
ni sehemu ya uwekezaji
wake, bali inajikita katika
ununuaji wa bidhaa na utoaji
wa huduma kwa kutoa nafasi
kwa wateja wake kulipa
kidogo kidogo. Wakati benki
zisizo za Kiislamu hutoa
mikopo ya fedha taslim kwa

njia ya riba, kitu ambacho


kinawapelekea baadhi ya
wakopaji kuzitumia fedha
walizokopa kinyume na
malengo ya mkopo ule.
Hali hii ndio inayopelekea
wakopaji wengi kushindwa
kulipa madeni yao na kuingia
katika matatizo na kuziingiza
benki katika matatizo pia.
Benki za Kiislamu
zinajikita na uuzaji wa bidhaa
tu ambazo zimethibitika
kutokuwa na madhara kwa
jamii wakati benki zisizo za
Kiislamu hujishughulisha na
kuwezesha shughuli mbali
mbali bila kuzingatia athari
itakayoipata jamii kupitia
shughuli zile, mfano wa
shughuli hizi ni pamoja na
utoaji mikopo kwa kampuni
zinazouza na kusambaza
aina mbali mbali za ulevi
na sigara pamoja na mikopo
kwa kampuni zinazoendesha
michezo ya kamari.
Swali: Je mfumo huu wa
fedha wa Kiisalamu, ni kwa
ajili ya Waislamu pekee?
Jibu: Pamoja na kwamba
ni matarajio ya Waislamu
wengi kuwa na mfumo wa
kifedha unaokidhi mahitaji
yao ya kila siku; lakini kwa
sababu mfumo huu umekua
n i we n ye k u k i d h i k wa
ufanisi mkubwa mahitaji
ya k i b i a s h a r a , n a k wa
sababu biashara ni shughuli
zinazofanywa na jamii zote,
hivyo basi, benki za Kiislamu
zipo kwa ajili ya watu wote,
sio Waislamu pekee.
Swali: Je, kuna mahusiano
gani baina ya benki na mteja
katika kupokea fedha?
Jibu: Benki za Kiislamu
hupokea fedha kwa mikataba
miwili; mkataba wa kuweka
akiba na mkataba wa
uwekezaji. Katika mkataba
wa uwekezaji, mteja wa benki
anakuwa ni mshirika katika
uwekezaji ule. Hushirikiana
na benki katika biashara,
na hupata faida na hasara
kulingana na ukubwa
wa ushiriki wake na kwa
k u z i n g a t i a m a t o k e o ya
biashara inayofanywa. Ikiwa
matokeo ni mazuri na faida
huwa nzuri na ikiwa matokeo
ya biashara sio mazuri,
mteja nae hupata gawio
dogo. Pia ieleweke kuwa
wateja wanapata gawio kwa
kuzingatia faida ya uwekezaji
kabla ya kutoa gharama za
uendeshaji wa benki.
Swali: Ni utaratibu gani
Amana Bank inatumia katika
kuwekeza fedha za wateja
wake?
Jibu: Katika Benki za
Kiislamu, asilimia tisini
(90%) ya uwekezaji wake
unahusisha kuuza na
kununua mali au kutoa
huduma kufuatia maombi
husika ya mteja wake. Kwa
Inaendelea Uk. 9

Makala

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Inatoka Uk. 8
mfano mteja anapokwenda
benki na mahijati ya mkopo
kwa ajili ya ununuzi wa
malori kwa ajili ya biashara
zake, benki za Kiislamu
hazitampatia fedha taslim,
bali zitanunua yale magari
na kumuuzia mteja yule kwa
faida pamoja na kumpa fursa
ya kufanya malipo kidogo
kidogo.
Swali: Amana Bank
inaithibitishiaje jamii
kwamba inafuata misingi ya
Sharia za Kiislamu kikamilifu
katika shughuli zake?
Jibu: Benki za Kiislamu
zina mfumo wa usimamizi
wa mambo ya Sharia ambao
upo katika ngazi mbili, ngazi
ya juu na ngazi ya chini.
Katika ngazi ya juu, kuna
bodi maalum ya usimamizi
wa Sharia inayoundwa na
wataalam waliobobea na
wenye weledi wa Sharia
katika miamala (Fiqh al
muamalat). Bodi hii ndiyo
inayotoa miongozo juu ya
utayarishaji wa huduma
na mikataba, kuthibitisha
taratibu za uendeshaji, bidhaa
na huduma zinazotolewa,
mikataba na maadili ya
kushughulika na mteja.
Lakini bodi hii pia huendesha
mapitio na ukaguzi wa Sharia
(Sharia Compliance Reviews)
na kutoa maamuzi kufuatia
ukaguzi huo. Katika ngazi
ya chini na ya ndani ya
benki, kunakuwa na kitengo
maalum kinachohusika
na usimamizi wa Sharia
katika shughuli za kila siku
ikiwa ni pamoja na kufanya
ukaguzi wa miamala yote na
kuwasilisha ripoti kwa bodi
ya Sharia kwa maamuzi.
Swali: Ni yapi mafanikio na
changamoto zinazozikabili
benki za kiislam Tanzania?
Mkurugenzi mtendaji
Jibu:
Mafanikio yaliyopo ni
pamoja na;Kwanza kabisa ni Benki
Kuu ya Tanzania (BOT) kutoa
leseni ya uendeshaji wa
benki za Kiislamu Tanzania.
Baada ya kuona umuhimu wa
kuwepo benki za Kiislamu
hapa nchini, Benki Kuu ya
Tanzania haikusita kutoa
ruhusa licha ya kutokuwepo
kwa Sheria wala kanuni
mahsusi zinazotoa miongozo
ya uendeshaji wa benki za
Kiislamu hapa nchini.
Pili, Mchakato wa
u t a ya r i s h a j i wa k a n u n i
mahsusi (regulatory
framework) za uendeshaji wa
benki za Kiislamu Tanzania
unaendelea. Benki Kuu
tayari imechukua hatua za
matayarisho ya kanuni hizo
mahsusi katika kunyanyua
mfumo huu na kurahisisha
uendeshaji wake kwa
manufaa ya watumiaji na taifa
kwa jumla. Mchakato huu

unajumuisha pia utayarishaji


wa Bodi Kuu ya Usimamizi
wa Sharia (Central Sharia
Supervisory Board) kwa
benki za Kiislamu.
Tatu, kuwepo kwa semina
mbali mbali zinazohusu
mfumo mzima wa fedha
wa Kiislamu zinazolenga
kutoa mafunzo ya mfumo
h u u k wa wa d a u m b a l i
mbali ambapo kwa kiasi
kikubwa zimeisaidia jamii
kupata mwamko na kuona
uzuri wa mfumo huu huku
benki zenyewe za Kiislamu
zikifaidika kwa kuongeza
ujuzi unaosaidia kuboresha
utendaji wao.
Nne, Kuanzishwa kwa
bima ya Kiislamu (Takaful) ni
sehemu kubwa ya mafanikio
ya m f u m o m z i m a wa
fedha wa Kiislamu; bima
ya Kiislamu itasaidia jamii
kwa kiasi kikubwa kufikia
malengo hasa ya ukamilifu
wa mfumo huu kwa kuwa

hata benki za Kiislamu


zitakua zimefanikiwa
kuendesha shughuli zake
kwa kushirikiana kwa karibu
sana na kampuni za bima ya
Kiislamu.
Tano, kuanzishwa kwa
programu za masomo
ya mfumo wa fedha wa
Kiislamu (Islamic Finance
Courses) katika ngazi za
cheti, diploma, shahada ya
kwanza na shahada ya pili
katika vyuo vikuu vilivyopo
hapa nchini, mfano wa vyuo
hivyo ni pamoja na Chuo
Kikuu cha Zanzibar (Zanzibar
University) na Chuo Kikuu
cha Waislamu Morogoro
( M u s l i m U n i ve r s i t y o f
Morogoro). Hatua hii
itawezesha kupatikana kwa
wataalam wengi wenye ujuzi
wa utendaji na uenezi wa
mfumo huu.
Na mwisho, ni jinsi
jamii ilivyoupokea mfumo
huu kwa mikono miwili
jambo ambalo limepelekea

ukuaji wa kasi hata zaidi ya


matarajio ya wengi katika
wadau wa fedha nchini.
Mfano, sisi Amana
Benki ikiwa ndio benki
ya kwanza ya Kiislamu
Tanzania, tumeweza kukua
na kufungua matawi sita
yaliyopo katika miji ya Dar es
Salaam, Arusha na Mwanza
na ipo mbioni kufungua tawi
la saba kabla ya mwisho wa
mwaka 2015 katika eneo
la Mbagala Zakhiem Dar
es Salaam. Amana Benki
katika kipindi hiki kifupi
imeweza kukuza amana
za wateja kutoka TZS 30.3
billion mwaka 2012 hadi
kufikia TZS 152.2 billion
mpaka mwezi Juni 2015 na
kukuza portfolio ya mikopo
kutoka TZS 16.8 bilioni 2012
mpaka kufikia 101.8 bilioni
2015. Vile vile tumefanikiwa
kutengeneza ajira kwa kuwa
na wafanyakazi wafikao 122.
Kwa upande wa pili, benki
za Kiislamu zinakabiliwa na
changamoto kama zifuatazo:Kwanza, mchakato wa
kutunga sheria na kanuni za
kuendesha benki za Kiislamu
nchini unakwenda pole pole
sana. Hili linafanya benki za
Kiislamu zisiwe na uwezo wa
kupata msaada stahili kutoka
kwa Benki Kuu ya Tanzania
pale unapohotajika.
Pili, kutokuwepo kwa
bima ya Kiislamu ambayo
ni sehemu ya mfumo mzima
wa Kiislamu na ni msaada
mkubwa katika utimilifu wa
uendeshwaji wa mfumo huu
nchini. Kwa mfano, benki
za Kiislamu ambazo kwa
asilimia kubwa zinajikita
katika uuzaji wa bidhaa,
bidhaa hizi huhitaji kukatiwa
bima kupitia kampuni za bima
za Kiislamu; kutokuwepo
kwake kunapelekea bidhaa
hizi kukatiwa bima isiyo ya
Kiislamu chini ya dharura
na kupelekea baadhi ya
jamii kutilia mashaka juu ya
uhalali wa baadhi ya miamala
inayofanywa na benki za
Kiislamu hapa nchini.
Ta t u , k u w e p o k w a
baadhi ya wanajamii ambao
hawana uelewa wa kutosha
kuhusiana na mfumo
huu, lakini wanajaribu
kuuzungumzia vibaya kwa
kusema mfumo huu na ule
usio wa Kiislamu ni sawa

sawa bali umebadilishwa


jina tu. Hali hii imepelekea
wanajamii wengine
kuukwepa kabisa mfumo
huu. Hili wanalolifanya
watu wa namna hii ni kosa
kubwa ambalo linapelekea
kuwazuia watu wasiende
katika kheri. Qurani 36:
17 inakataza binadamu
kusema na kutenda asiyo
na ujuzi nayo kwani hakika
siku ya Kiyama atakua na
jukumu kwa aliyoyatenda na
aliyoyasema.
Swali: Ni kitu gani
u n g e p e n d a k u wa s h a u r i
wasomaji wetu juu ya Amana
Bank.
Jibu: Napenda nimalizie
mazungumzo haya mafupi
kwa kuwaahidi wadau wetu
wote na hususan wateja
wetu kuwa kila siku Amana
Benki tunajikita zaidi katika
u b o r e s h a j i wa h u d u m a
zetu ili kukidhi mahitaji ya
wateja wetu. Nawaomba
sana wadau wetu wote
wasisite kabisa kutukosoa
pale ambapo hawataridhika
na huduma zetu; kwa hakika,
sisi ni benki sikivu na tupo
tayari kusikiliza maoni kwa
ajili ya kuboresha.
Nawahakikishia wadau
wetu kuwa tunaliendesha
jahazi hili katika maadili
yaliyotukuka na yanayofuata
uwazi, weledi na usikivu wa
hali ya juu kutoka kwa wadau
wetu wote; wateja, wanahisa,
wakurugenzi, serikali na
jamii yote kwa ujumla. Benki
yetu inatumia teknolojia ya
kisasa ambayo inatuwezesha
kufanya miamala yetu kwa
uharaka na umakini wa hali
ya juu. Vilevile ningependa
ieleweke kuwa benki hii
inafuata misingi ya Sharia
za Kiislamu lakini haibagui
katika uwekezaji, ajira na
kutoa huduma kwa wateja.
Amana Benki inatoa huduma
zake kwa watu wote.
Ningependa vile vile
niwashauri wasomaji wetu
wajitahidi sana waweze
kufika katika matawi yetu
mbali mbali yaliyopo jijini
Dar es Salaam, (Tandamti
na Lumumba yaliyoko
Kariakoo, Golden Jubilee
Tower lililoko katikati ya
jiji, Nyerere Road lililoko
Jengo la DRTC, Barabara ya
Nyerere), Tawi la Mwanza
lililopo katika barabara ya
Kenyatta na Tawi la Arusha
lililopo Hugo House ili
waweze kupata maelezo
zaidi kuhusu Amana Bank
na namna itakavyoweza
kuwaendeleza kiuchumi.
Karibuni sana Amana
Benki mufaidike na huduma
za kisasa zinazozingatia
maadili mema na zisizo
husisha riba.
Amana Bank Idara
ya U s a n i f u b i d h a a n a
Usimamizi wa Sharia (2015)

10
Na Omar Msangi

IKI iliyopita
kulifanyika Dua
ya kuiombea
Zanzibar amani na
utulivu katika kipindi cha
uchaguzi. Waislamu mbali
mbali wakiongozwa na
Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad, walikusanyika
katika viwanja vya
Maisara mjini Zanzibar
kwa ajili ya kuomba dua
ya kuiombea Zanzibar
amani na utulivu, hasa
katika uchaguzi mkuu
ujao.
Akizungumza katika
hafla hiyo, Katibu Mtendaji
wa Kamisheni ya Wakfu na
Mali ya Amana Zanzibar
Sheikh Abdallah Talib,
alisema mara nyingi amani
ya Zanzibar hutoweka
kutokana na sababu za
kisiasa hasa inapofika
wakati wa uchaguzi mkuu,
hivyo juhudi za makusudi
zinapaswa kuchukuliwa
katika kuendeleza amani
ya nchi wakati wote.
Akasisitiza kuwa suala
la kudumisha amani
na utulivu ni mchakato
unaopaswa kuendelezwa,
ili kuinusuru nchi kuingia
katika machafuko
yasiyokuwa ya lazima, na
kwamba kila mwananchi
ana jukumu la kuhakikisha
k u wa a m a n i ya n c h i
haichezewi.
Naye Amir wa Taasisi za
Kiislamu Zanzibar Sheikh
Ali Abdallah akasema
dua hiyo ya kitaifa
imefanyika nchi nzima
katika viwanja mbali mbali
Unguja na Pemba. Dua
hiyo iliyotanguliwa na
sala ya Alasiri viwanjani
hapo, ilihudhuriwa na
viongozi mbali mbali
wa dini ya Kiislamu,
serikali na vyama vya
siasa wakiwemo Mufti
Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kabi, Katibu
wa Mufti Sheikh Fadhil
Soraga, Mkuu wa Mkoa
wa Mjini Magharibi Mhe.
Abdallah Mwinyi Khamis
na Mgombea Urais wa
Zanzibar kupitia Chama
Cha ADC Mhe. Hamad
Rashid Mohammed.
Kuomba dua ni jambo
jema sana na kwa hakika
ni ibada. Na kila mja
anavyoomba Dua kwa
Mola wake, ndivyo Allah
anavyomridhia. Kinyume
na mwanadamu ambaye,
hata kama atakuwa
mkarimu vipi, lakini
ombaomba ikizidi, hata
kama anayemuomba ana
shida kweli, hufika mahali

Makala

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Zanzibar
ilete
toba
Sio kuomba amani, baraka, neema
Mufti Kabi awasaidie viongozi SMZ

MAKAMU wa Kwanza Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na Katibu
wa Muft, Sheikh Soraga wakitoka katika dua iliyofanyikia katika viwanja vya
Maisara Zanzibar hivi karibuni.
akakereka.
uharamia huo wa kupiga hapana shaka inahatarisha
H ata h i v y o p a moja watu na kuvuruga amani amani na utulivu, halafu
na ukweli huo, lazima ya Zanzibar. Sasa hili la viongozi hao hao wa
tuwe wa wazi na tuseme kuomba dua kumtaka serikali wanakusanyika
u k w e l i k wa m b a d u a Mungu alete amani au Maisara kumwomba Allah
h i i y a Z a n z i b a r i n a la k u a mbia n a u k we li (SWT) alete Amani katika
walakini, tena mkubwa. wanasiasa kuwa waache nchi!
Nitafafanua. Kwanza hii uharamia huo? Mahali
Ambacho tungetaka
imeitwa kuwa ni dua ya pengine Sheikh Talib kusikia, ni Serikali ya
kuiombea Zanzibar amani anasema kuwa suala la U m o j a wa K i t a i f a ya
na utulivu katika uchaguzi ulinzi wa amani ni la kila Zanzibar kuja na kauli
mkuu ujao. Pili, Katibu Mzanzibar. Sawa kabisa. thabiti kwamba yaliyopita
Mtendaji wa Kamisheni ya Lakini katika mazingira yamepita, hakutakuwa
Wakfu na Mali ya Amana haya ya Janjaweed na tena na visa vya vikosi
Zanzibar Sheikh Abdallah vikosi, mwananchi wa kupiga watu au kuja na
Talib, amesema amani kawaida afanye nini? Kwa njama za magoli ya
ya Zanzibar hutoweka nini hamuwaambii ukweli mkono katika uchaguzi
kutokana na sababu za wanasiasa?
huu, mambo ambayo
kisiasa inapofika wakati
Turudi nyuma mauwaji ndiyo huvuruga amani.
wa uchaguzi mkuu.
y a 2 0 0 1 . Wa t u w a l e Serikali ikisha hakikisha
Sasa turudi nyuma toka waliouliwa kosa lao nini? hayo, ndio sasa iwatake
zimeanza siasa za vyama Ile kutumia haki yao ya wananchi, kila mmoja kwa
vyingi, tujiulize, nani kikatiba na kidemokrasia nafasi yake kuhakikisha
walikuwa wakiwavamia kuonyesha kutokuridhika kwamba amani inadumu.
w a t u n a k u w a p i g a k w a o n a u c h a g u z i Na Dua, Itqaaf zifanyike.
o v y o k u a n z i a z o e z i ulivyoendeshwa, ndio
Wakati Masheikh wale
la kuandikisha wapiga hukumu yao kupigwa akiwemo Mufti Mkuu wa
kura, wakati wa kupiga risasi na kufanyiwa kila Zanzibar Sheikh Saleh
kura na hata baada. Nani aina ya udhalimu?
Omar Kabi, Katibu wa
wa l i k u wa wa k i va m i a
Pa m o j a n a k u we p o M u f t i S h e i k h F a d h i l
akina mama majumbani Serikali ya Umoja wa Soraga, wananyanyua
m wa o k u wa i b i a v i t o Kitaifa, bado juzi hapa mikono na Maalim Seif
vyao vya dhahabu na wakati wa uandikishaji k u o m b a A l l a h ( S W T )
kuwabaka? Nani walikuwa wapiga kura, ya Janjaweed aimiminie neema, amani,
wakiwatuma watu hawa na yalijitokeza tena ambapo utulifu na Baraka Zanzibar,
kuwalinda wasifikishwe watu walipigwa sana Masheikh wenzao wapo
katika vyombo vya sheria? katika baadhi ya maeneo gerezani Bara kwa zaidi
K w a b a h a t i n z u r i na ushahidi ukitolewa ya miaka miwili sasa.
M a k a m o wa K wa n z a kuwa watu waliofanya Masheikh wale wamesema
wa Rais, Maalim Seif uovu huo ni katika wale m e n g i y a l i w e m o y a
Shariff Hamad na Hamad wale vikosi. Unaposema kudhalilishwa na hata
R a s h i d w a l i k u w e p o . v i k o s i m a a n a y a k e kunajisiwa.
Wote hawa walipokuwa unasema serikali. Sasa
S h e r i a ya K i i s l a m u
pamoja katika upinzani, kama huku sikumfanyia a m b a y o M u f t i w a
wanajua na wakisema stizai na kumcheza shere Zanzibar anaijua vyema,
h a d h a r a n i h a b a r i ya Allah Subhana Wataallah inasema kuwa lau watu
vikosi na janjaweed nini! Kwamba serikali wangesikilizwa tu kwa
waliokuwa wakitumiwa i t oe v i k osi v i h u ju mu madai yao, kuna watu
na SMZ (CCM) kufanya wananchi, hali ambao wangedai damu na mali za

watu. Bali ni juu ya mwenye


kuleta madai, kuleta
ushahidi kuthibitisha
madai yake. Ni mwaka
wa pili sasa, serikali
haijaweza kufikisha
ushahidi mahakamani
kuthibitisha tuhuma zake
dhidi ya Sheikh Msellem
Alli na wenzake. Ambayo
tafsiri yake yaweza
k uwa Mashe ik h wa le
wamekuwa wakiteswa
na kuadhibiwa kwa
dhulma. Wala hawafikirii
taabu wanayopata wake
na watoto wa Masheikh
hawa kwa kukosa huduma
muhimu za maisha. Kisa
wakuu wa kaya wapo ndani
kwa tuhuma ambazo kwa
miaka miwili, Mahakama
haijaweza kuzithibitisha!
Katika dhulma kama
hii, unanyanyua mikono
kumwomba Allah ili
akupe nini?
Tu l i t a r a j i a k a t i k a
mkusanyiko ule, badala
ya Mufti kuongoza Dua,
angemuuliza Makamo wa
Kwanza wa Rais, Maalim
Seif Shariff Hamad, kwa
kosa gani Sheikh Msellem
yupo ndani mpaka sasa?
Kuwa Mufti maana yake
kutoa fatwa, na maadhali
hiki ni cheo na wadhifa
unaotambuliwa katika
mfumo wa uongozi wa
S e r i k a l i ya Z a nz i b a r ,
tulitarajia Mufti Sheikh
Saleh Omar Kabi atoe
fatwa juu ya suala la
Sheikh Msellem na
wenzake na awashauri
viongozi wa serikali juu ya
kadhia hii.
Kunyanyua mikono
kuomba Dua kwa
Allah yaweza kutuletea
balaa zaidi. Afadhali
tungejikalia kimya na
dhulma zetu mpaka hapo
tutakapoamua kuzibadili
nyoyo zetu. Na Quran
i n a s e m a wa z i , A l l a h
habadili yaliyo kwa waja
mpaka wenyewe wabadili
yaliyo katika nafsi zao.
Kama ndani ya nafisi zetu
imeondoka huruma, huku
dhulma na kuonea watu
kukitamalaki, hiyo amani
na utulivu, ije ili akae wapi.
Angalau Edward
Lowassa amekuwa japo na
ujasiri wa kutamka kwamba
kama akichaguliwa
atalishughulikia suala
la Masheikh wale kwa
kutumia sheria zilizopo.
Sisi ambao ndio wenyewe,
wenye watu wetu, wenye
Masheikh wetu, tunaona
ni nuksi hata kuwataja
tu! Halafu tunakusanyika
kumwomba Mungu
atumiminie Baraka
tele, tunawiri ili tuzidi
kuwadhulumu zaidi waja
wake!

11

Makala

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

CCM yavunja rekodi usajili dirisha dogo


Na Juma Jumanne

UNAENDELEA
kushuhudia mengi
katika kampeni hizi
za uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25,
2015. Ni vioja, ni uwongo,
unafiki, na mfano wa
hayo kwa namna ya ajabu
kabisa ambayo haijawahi
kutokea. Kinachofanyika
sasa, pengine tukiite
mipasho kama ile ya
wa s a n i i wa t a a r a b u .
Kuna watu wanaonekana
kuwa na vipaji hivyo
vya uimbaji wa taarabu,
lakini wamejikuta wapo
kwenye siasa labda kwa
ajili tu ya kupata unga.
Bila shaka kwa
wafuatiliaji wazuri wa
v y o m b o v ya h a b a r i ,
watakuwa wamemsikia
vema kabisa, kiungo mpya
wa yanga aliyesajiliwa
kupitia dirisha dogo.
Mchezaji huyu ambaye
alifanyiwa rasmi majaribio
kwenye mechi ya kirafiki
iliyorushwa moja kwa moja
kupitia vituo vitatu vya
matangazo, TBC 1, Star Tv
na Azam Tv, anaonekana
hana kiwango licha ya
kusajiliwa kwa gharama
kubwa kuziba pengo
la mchezaji aliyehamia
i l i y o k u wa t i m u ya k e
ya zamani. Hakuweza
kuonesha kiwango
kilichotarajiwa na wengi
wanaomfahamu, hususan
wafadhili jambo ambalo
l i n a we z a k u wa v u n j a
moyo mashabiki wa timu
hii ambayo imekuwa
kinara kwa takriban miaka
hamsini sasa.
A k i wa k a t i k a t i m u
yake ya zamani, mchezaji
h u y u n d i ye a l i k u wa
team captain na
aliongoza vizuri kabisa
japo hawakufanikiwa
kuchukua kombe hata
moja. Alikuwa mchezaji
mzuri, mwenye nguvu
na stamina barabara
ikizingatiwa kwamba
ni Padri, hivyo yeye
na wanawake ni kama
mashariki na magharibi.
Siyo kama wachezaji
wengine ambao mara
nyingi hujichanganya na
wanawake na kupoteza
viwango vyao.
Kwa watu weledi wa
mambo ya propaganda,
wanatambua vyema
kwamba, aliyecheza pale
siyo Willy, bali katumika
kama mdoli tu. Ni kama
mtu anapopandwa na
mashetani husema vitu vya
ajabu, vya kuchanganya
na mara nyingine anaweza
kujipigiza, kukimbia
ovyo na mfano wa hayo.
Hayo yote, anafanya yule
aliyejificha ndani ya mwili

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa (kushoto) na


aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Harun Lipumba.
wa huyo mtu.
Imefika mahali watu
wanaanza kurudi
nyuma, hususan wale
wa l i o m wa m i n i h u y u
anayeitwa Dokta. Wanaona
labda yupo sahihi na
ameongea mambo
ambayo kweli yametokea.
Binafsi sipingani na
baadhi ya kauli zake ila
ninachokataa hapa ni
kwamba, hajasema yeye.
Kwa wale waliomsikiliza
kwa makini watakubaliana
nami kwamba, yale
maneno yaliyokuwa na
yanayoendelea kumtoka
yana rangi ya kijani
i l i y o i va k a b i s a a a . ! !
Jiulize mwenyewe, majani
kijani kibichi yanatoka
wa p i m a j i r a h a ya ya
kiangazi!?
Lakini kuna wapo
waliofika mbali kabisa
wakasema kwamba, isije
ikawa kuondoka kwa
Slaa na kutamkishwa
maneno kama haya
kunatokana na ugonjwa
kama ule unaowasumbua
Waislamu? Nilipotaka
kujua ni ugonjwa gani
huo, nikakutana na swali
badala ya jibu! Nikaulizwa
ina maana hujui ugonjwa
unaowatafuna ninyi
Waislamu? Nikapata hamu
ya kujua gonjwa hilo, ndipo
nilipoambiwa kwamba,
huo utaasisi wenu na
u-manhaj umeusahau!?
Lakini kubwa zaidi ni
kwamba, mchezaji huyu
alikuwa na matarajio ya
kuwa team captain kwa
mara nyingine. Suala la
kumpa u-kepteni mchezaji
mpya ambaye hajazoea,
hajajua fomesheni ndilo
haswaa msingi wa

usajili feki uliofanywa


bila kuangalia uwezo wa
mchezaji ambaye tangu
hapo ni veterani.
Wa k a z i d i k u s e m a
kwamba, kwahiyo
kinachoendelea siyo
Richmond tu, kuna mambo
kama yenu Waislamu
yameingilia katikati! Kwa
hali hiyo, usishangae
yanayoendelea kwa kuwa
mgombea anayetokea
chama chenye rangi kama
ya maneno uliyoyaona
kutoka kwa Dokta Slaa
ni baba mmoja, mama
mmoja. Hapo nilichoka
mwenyewe..!!
Lakini amini usiamini,
kwenye mfumo wa
kinachoitwa demokrasia
hakuna mwanasiasa
msafi. Wanatofautiana
tu viwango vya kuiba.
Waangalie wanaomtetea
Magufuli wakoje,
wamefanya nini, hali zao
kimaisha na mengineyo.
I k i wa k we n ye s a k a t a
la akaunti ya Escrow
wamehusika mpaka
viongozi wa dini, sembuse
hawa wasiomjua mungu!
Wananchi msiyumbishwe
n a wa t u wa n a o t e t e a
matumbo yao.
Ndugu zanguni ikiwa
maneno haya yana ukweli
au uzushi, tubaki kwenye
agenda yetu. Wenyewe
ndio wanasema! Na mimi
siyo mzungumzaji sana,
hivyo huwa napata fursa
ya kusikia na kujifunza
mengi. Ushauri wangu
ni kwamba, tusikubali
kuburuzwa kila wakati
jamani. Hawa watu ni
waongo mno. Leo Slaa
ndio anapata ujasiri
wa kugusia mambo ya

Waislamu? Haongei yeye.


Ukiangalia kwa jicho pevu,
ndio utaweza kumuona
shetani aliyempanda
kichwani.
Wa t u k a m a h a w a
wapo kila kona ya dunia.
Mathalani, aliyekuwa
waziri wa zamani wa
serikali, Bw. Nalaila
Kiula ametamka maneno
ambayo ni wazi kabisa
huyu mtu ameishiwa au
amefilisika kifikra! Sisi
tunafahamu kwamba,
hizi ni tuhuma ambazo
bado hazijathibitishwa.
Kumbe yeye na uoni
wake mdogo ameshajua
kwamba hawa masheikh
wa Uamsho ni magaidi!?
Hata maana yenyewe ya
ugaidi haijui, anafuata
tu mkumbo. Hawa ndio
watu ambao maombi yao
na dua zao huzielekeza
CCM pindi wanapopatwa
na matatizo. Wanaipenda
CCM kuliko hata Mungu
wao wanayemwamini.
Naye mwenyekiti
wa Chama cha Kijamii
(CCK), Bi. Constantine
Akitanda, amediriki
kusema kwamba, kwa
kauli ya kutaka kuwaachia
watuhumiwa wa Uamsho
wanaodaiwa kusababisha
uvunjifu mkubwa wa
amani Zanzibar, Lowassa
a m e d h i h i r i s h a k u wa
akiingia madarakani
atasababisha mfarakano
mkubwa zaidi katika jamii.
Akaendelea kusema
k u wa , h a l i ya a m a n i
imerejea Zanzibar
na sasa wananchi
wanafanya shughuli zao

za maendeleo bila hofu


ya vitendo vya kigaidi
kama ilivyokuwa awali.
Hivyo, mtu anapokuja na
kutoa ahadi ya kuwaachia
watuhumiwa waliokuwa
wanazusha hofu kubwa
visiwani, ni lazima
atazamwe kwa shaka.
Hawa ndio watu wetu,
japo unaweza kujiuliza
kwamba, huyu ni raia wa
Tanzania au mhamiaji!
A m a n i
i p i
anayoizungumzia iliyopo
Zanzibar? Kubakwa
mwanamke, tena mchana
wa Ramadhani kwenye
zoezi la vitambulisho
vya wapiga kura ndiyo
amani hiyo!? Angetuweka
wazi kwenye nukta hii
ili twende sawa, tujue ni
akina nani anaowakusudia
kwamba wanaishi kwa
amani sasa! Ni vitendo
vipi hivyo anavyodai
kwamba, ni vya kigaidi?
Sisi tumekaa kusubiri
hukumu kwa masheikh
zetu, kumbe wenzetu
tayari wanafahamu
kinachoendelea!!
Naye Maria Sarungi,
mmoja katika Watanzania
maarufu katika mtandao
wa t w i t t e r , a n a s e m a
kwamba, Kama vyombo
vya habari vya Tanzania
vingekuwa kama vya
Marekani, kichwa cha
habari kutoka mkutano
wa Jangwani kingesema;
Mgombea Urais atangaza
kuwasamehe wabakaji na
magaidi. Mwanamama
huyu ndio kachelewa
pengine kuliko wote. Bila
shaka akipewa wadhifa
wa uraisi, jambo la
mwanzo kufanya litakuwa
kuruhusu Maria na Janeti
kuoana kanisani kwa
kigezo cha limesemwa na
linafanyika Marekani!
Wosia wangu kwa mara
nyingine ni kwamba, kila
mtu ana haki ya kusema
lakini siyo kila kisemwacho
ni sahihi. Tutumie vema
neema ya akili ili itusaidie
sisi na jamii kwa ujumla.
Kampeni yetu ni kuitoa
CCM madarakani kwa
sababu haitutendei haki.
Kama Lowassa hafai, basi
waliomuweka kwenye
wadhifa wa Uwaziri Mkuu
ndio hawafai zaidi. Hata
k ama Lowassa ak iwa
bubu, hata asiposema
chochote, hata akisema
atatuua sote, sisi lengo letu
CCM itoke tu, kwa kuwa
tumeshajifunza kwamba
maneno na matendo
yenu wanasiasa wa CCM
hayawafikiani na uhalisia.

12

MAKALA

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Mabadiliko: Nafasi ya Lowassa katika siasa za Tanzania


Na Anil Kija

MTUME Paulo anasema


mahali fulani kuwa inabidi
watu waombe kulingana na
mapenzi ya Mungu, kitu
ambacho kinaleta utata wa
mantiki katika hatua mbili,
ya kwanza ni kama mtu
anaweza kujua mapenzi
ya Mungu ni yapi katika
jambo fulani ili aelekeze
maombi yake hapo. Jibu
katika hatua hiyo ni hapana,
kwani njia rahisi zaidi ya
kujua kama kitu hiki au
kile kinaendana na mapenzi
ya Mungu ni kuangalia
sheria, na mara nyingi tatizo
linakuwa siyo hilo. Suala
ni mwelekeo wa baraka;
nini Mungu anachobariki
wakati huo.
Tatizo la pili ni kuwa
maombi hayawezi
kutenganishwa na hisia za
kile ambacho kila mmoja
wetu kama binadamu
anakitaka, na ndani ya kila
mmoja kuna hisia ya faida na
hasara, kwa kuangalia jambo
fulani kwa upande wowote
ule. Ndiyo maana maombi
kwa mfano ya kushinda
mchezo wa soka ni aina
ya kichekesho, lakini kwa
upande fulani ni sahihi,
kwani huwezi kuwa na
dhana kuwa Mungu haipendi
timu pinzani, lakini ni wazi
anaweza kutoa baraka kwa

timu yenu kwa siku hiyo.


Inategemea mtiririko wa
baraka zake.
Inapokuja katika suala
la uchaguzi mkuu nchini
hapo Oktoba 25, kuna suala
gumu la kuelewa mtiririko
wa baraka uko upande gani,
kati ya wahafidhina ambao
h a wa we z i k u t a z a m i wa
kuleta mabadiliko, na
wanaoyataka. Tofauti moja
ya kina ni kuwa licha ya
migawanyiko yao, makundi
yao na fitina zisizoisha,
wahafidhina wana uzoefu wa
dola, na kiwango kikubwa
cha utii, ndiyo maana watu
wengi wanawaamini kulinda
amani na utulivu. Lakini
historia, na hata maandiko,
hayaonyeshi kuwa utulivu
ndiyo lengu kuu daima.
Hivyo uwezekano wa
mabadiliko upo, lakini
m a b a d i l i k o ya n a a i n a
m b i l i k wa m a n t i k i ya
mfundishaji wa Uyunani ya
Kale, Aristotle (aina sita za
serikali, tatu njema na tatu
mbaya). Aina ya kwanza
ya mabadiliko, ambayo kila
mtu anataka, ni mabadiliko
c h a n ya a m b a y o n d i y o
mema, nchi kwenda mbele
kwa mwelekeo bora zaidi,
na aina ya pili ni mabadiliko
hasi, ambayo kwa lugha
ya maandiliko ni hukumu.
Nchi ipewe kiongozi wa
kuifikisha gizani, iangamie.
Kwa maana hiyo,

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CHADEMA-UKAWA, Mhe. Edward Lowassa.


swali halisi kwa mtiririko
wa m a a n d i k o n i k a m a
kilichopo hapa nchini hivi
sasa ni mabadiliko (chanya)
ambayo ni baraka, au ni
hukumu ambayo ina maana
ya mabadiliko hasi, nchi
iparaganyike, ianze au
ipanue mitafaruku kwa

n j i a i s i y o ya k a wa i d a .
Mabadiliko hasi ya moja
kwa moja yanaanza na uasi,
kwa mfano ule uasi wa
Katiba Mpya ulioongozwa
na Kanisa Katoliki kuelekea
mwisho wa 2010, baada
ya mgombea wao, kasisi
muasi Dk. Wilibrod Slaa

kushindwa katika kura ya


urais. Tungeparaganyika.
Mabadiliko ambayo
yanatafutwa sasa yana asili
yake katika uasi huo, lakini
yamebadilika sura na kurudi
katika hali ya kawaida,
kuwa dhamira yake siyo

Inaendelea Uk. 16

Lowassa na Yakobo: Baraka za utajiri


kwa vipindi tofauti vya kazi ya Mungu

Mhe. Edward Lowassa.

OJA ya sifa
za kizazi cha
I b r a h i m u
hadi wakati wanatoka
Kanaani na kuingia
Misri, ni utajiri mkubwa
hasa wa mifugo, ishara
ambao inaonekana pia
kwa baadhi ya watu
wenye sifa ya kuwa
karibu kabisa na Mungu,

kwa mfano Ayubu, na


ukiacha Mfalme Daudi,
mwanawe, Sulemani.
Ni suala lisilopingika
kuwa utajiri ni baraka
z a M u n g u k wa m t u
fulani, ila kutokana na
hisia moja au nyingine
ya Injili, mara nyingine
huonekana vinginevyo.
Ziko fikra zilizopanuka

duniani, kuwa utajiri ni


wizi, ufisadi, uharamia
tu.
Hata hivyo, ukiangalia
kwa makini katika
maandiko unakuta kuwa
hata pale uharamia, wizi
au 'ufisadi' unapokuwepo,
bado utajiri ni baraka kwa
sababu mhusika anaishi
maisha ya raha. Suala
ni kuwa baraka hizo
zinaanzia wapi, kama
Mungu anamkirimu mtu
a mb a ye n i mw iz i a u
haramia, au anabarikiwa
licha ya kuwa mwizi au
haramia. Fikra ya kikuhani
ingependelea kuwa mtu
anapofikia hatua ya kuwa
mwizi au haramia baraka
iondolewe, hukumu yake
ishuke, lakini maandiko
hayaonyeshi hivyo.
Ukifuatilia maandiko,
unakuta kuwa Mungu
anatumia baraka ya utajiri

katika maeneo mawili:


kwanza kuwastawisha
walio karibu naye ili
kujenga vizazi vya
wanaoamini, wasiingiliane
na
wasioamini
wakaharibikiwa. Hii ni
azma ya familia tajiri
kuoana wao kwa wao, na
kama imani yao inatosha,
hulka ya wazazi inaendelea
miongoni mwa wana wao,
na siyo kuharibikiwa
kwa kuchanganyika na
wa s i o a m i n i , wa s i o t i i
amri muhimu za maisha.
Ndiyo maana Ibrahimu
a k a m t u m a m k u u wa
watumisi wake kutwaa
binti kule Irak.
Ibrahimu alikuwa
hataki mwanae Isaka
aoe miongoni mwa
wa-Kanaani, akiwa
na uhakika kuwa hali
hiyo itateteresha imani
ya Mungu (wa kweli)

katika nyumba ya Isaka.


Mtumishi akafika Padan
Aramu kwa ndugu yake
Ibrahim aitwaye Nahori,
akapokelewa na binti
mwenye adabu na heshima
kisimani kabla hajafikia
nyumbani, kumbe ndiye
mteule wa kurudi naye.
Rebeka alikuwa ndugu
wa I s a k a k a m a j i n s i
Sara alivyokuwa kwa
Ibrahimu.
Yakobo alifaulu kuinua
nyumba yenye itikadi
njema kwa njia ambayo
baba zake hawakufaulu,
yaani Ibrahimu na Isaka.
Nyumbani kwa Ibrahimu
ilibidi Hajira aondoke
n a m wa n a e I s h m a e l i
kwani wasingeweza
kukaa nyumba moja na
Sara (na Isaka), na katika
nyumba ya Isaka ambayo
mke alikuwa mmoja,

Inaendelea Uk. 16

13
Na Rashid Abdallah

Mahakama Kuu
inaelekea kuhalalisha
uongo katika
kampeni za kisiasa.
Hivyo ndiyo lilivyonadi
gazeti la mtandaoni
kutoka Marekani la
The Huffington Post la
tarehe 16/06/2014. Nalo
gazet i l a Kienger eza
la the Guardian la
April 2014 likaandika;
Mahakama kuu kuamua
ikiwa kampeni za uongo
ni halali.
Hii ilikuwa ni kesi
iliyozua mjadala
mkubwa na kuteka watu
wengi mno, mahakama
kuu nchini Marekani
(Supreme Court) ndio
waliokuwa wanasikiliza
kesi hii, kubwa zaidi ni
kuwa mahakama hiyo
i a m u e i k i wa k u s e m a
uongo kuruhusiwe kaika
kampeni.
Kwani sheria ya Ohio
An Ohio law inakataza
wagombea kusema uongo
wakati wa kampeni, lakini
shirika la SBA-List (The
Susan B. Anthony List)
linalojishughulisha na
kampeni za kupinga utoaji
mimba nchini Marekani
na linawaunga mkono
wanasiasa wanaounga
mkono kampeni hiyo,
mwaka 2010 lilipeleka kesi
mahakama kuu kupinga
sheria hiyo ya Ohio.
Nianze kwa kunukuu
maneno ya mchangiaji
mmoja wa mada hii katika
mtandao kuwa ; Marekani
inaenda mbali zaidi
kwani baada ya uhuru
wa kuzungumza, sasa
wanaelekea kuruhusu na
uhuru wa kusema uongo.
Nami niseme kwamba
hii ni hasara ya uhuru
uliopindukia. Naamini
uhuru ukipindukia
mipaka, basi unaleta balaa.
Hata Rais Barack Obama
aliwahi kusema kuwa;
Hatuwezi kuwa na uhuru
wa asilimia mia moja
kisha tukajihakikishia
usalama wa asilimia mia
moja.Hata mimi nasema
kuwa uhuru kwangu una
mipaka.
Tu y a a c h e h a y o y a
Marekani turudi nyumbani
k i s h a t u ya l i n g a n i s h e
hayo na haya ya kwetu
sisi, hasa ukizingatia
kuwa tayari kampeni
za uchaguzi wa October
25, zimeanza. Wasikiliza
kampeni yatupasa tuwe
makini kwani kuna watu
ni wachanganyaji wazuri
wa n z i m a n a m b o v u
b i l a ya k u g u n d u l i k a .
Wanachanganya ukweli na
uongo na wanachanganya

MAKALA

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Mchezo wa kuwapatia watu


kula kila baada ya miaka 5

akili za wasikilizaji pia.


Propaganda ni kitu kibaya
zaidi kuliko uwongo. Siku
zote uongo ni uongo na
hauna chembe ya ukweli.
Lakini propaganda ni
jambo ambalo linakuwa
na chembe ya ukweli na
uwongo pia kwa maslahi
ya kisiasa, ni kama
kuchanganya tui kidogo
(juisi ya nazi) na maziwa
kidogo, usipokuwa
mtaalaumu utashindwa
kungamua kuwa haya si
maziwa safi.
W a n a s i a s a

wanaochanganya tui na
maziwa, mbovu na nzima,
ukweli na uwongo kwa
wa k a t i m m o j a , wa p o
hata hapa kwetu. Kama
k a m p e n i wa n g e k u wa
wanazifanya kwa uongo
mtupu, ingekuwa rahisi
sana kwa wananchi
kugundua na mwisho
kuachana nao. Lakini
mara nyingi wananchi
t u n a d a n g a n y wa k wa
sababu kampeni
zinaendeshwa kwa
propaganda, yaani
uwongo hapo hapo na

ukweli hapo hapo. Kwa


hiyo inakuwa ngumu
sana kwa mwananchi wa
kawaida kugundua lipi
lilikuwa na ukweli na lipi
ni la uwongo. Watakuja
wabunge, wawakilishi
na wagombea wengine
majimboni mwenu,
watakuja na mengi
mazuri katika masikio
yenu lakini hayotokuwa
y o t e n i ya k w e l i i l a
mengine yatakuwa ya
uongo ili kufanikisha
kile wakitakacho. Wapo
watakaokuwa wanatoa

hongo pesa, vitenge na


mambo mengine ilimradi
tu wazisuuze roho zenu
m u p a t e k u wa c h a g u a .
Ili kuwa na uhakika na
unaekwenda kumchagua,
ni bora kuacha kupokea
rushwa, kwani sayansi
inatuambia kuwa moyo
wa binaadamu una
kawaida ya kuathirika
ya yule anayeutendea
wema. Hivyo ukichukua
pesa ya mtu mwisho wa
siku moyo unaweza kuwa
mzito kutomtilia kura japo
hafai kwa sababu tayari
umeshaathirika na wema
ulionfanyiwa.
Dunia ni mchanganyiko
wa mambo yote machafu
na mazuri , ni kama
ungo uliobeba kila
kitu, kwani wakati sisi
tukitahadharisha juu
ya uongo wa baadhi ya
wanasiasa kwa wananchi
na tukiwaeleza kuwa wawe
makini na watu hao, kuna
watu wao wanaanzisha
kabisa kampeni ili uongo
uruhusiwe katika siasa.
Ndivyo dunia ilivyo.
Naamini kampeni hii
ya kupinga sheria ya
Ohio kwa kule Marekani
kama ingekuja Tanzania
b a s i wa p o wa n a s i a s a
ambao wangeivalia
njuga na kuitetea kwa
sauti pana huku mizizi
ya shingo ikiwatoka na
jasho likiwakatika, kama
vile ambavyo Marekani
haikukosa wa kuitetea,
afadhali kuwa hadi sasa
SBA-List hawajashinda
kesi ile na hapa kwetu
tusingekosa SBA-List wa
Kitanzania.
Utendaji wa wagombea
ni moja ya kipimo kizuri
cha wananchi kumpima
mgombea wao, ushiriki
wake katika masuala ya
kijamii na wala si ule
ushiriki wa kinafiki wa
siku za karibu na uchaguzi.
Ya w a p a s a m u t a l i i
vizuri tangu mwanzo
aliwaongozaje hadi leo hii
anataka tena ridhaa yenu
ili awaongoze tena.
Wapo pia wagombea
wanaoendeshwa na
misimamo ya vyama vyao,
misimamo ambayo ni
kinyume na matakwa yenu,
mukimrudisha mtu kama
huyu bungeni au katika
baraza la wawakilishi
kisha akaendelea kufanya
vile vile, hatutokuwa na
wa kumlaumu isipokuwa
ni sisi wenyewe ambao
tumemrudisha tena
uongozini. Mwanasiasa
bora ni yule anayejali
matakwa ya watu wake
na sio misimamo ya chama
chake ambayo inakwenda
Inaendelea Uk.14

14
Inatoka Uk. 13
kinyume na matakwa
yao. Mwanasiasa huyo
ni yupi? Wewe unamjua
zaidi. Ukiwa mpiga kura
u t a k u wa u n a m j u a n i
yupi anayekujali na yupi
anayejali tu kinachosemwa
kutoka makao makuu
yake.
Kila jimbo linajua kuwa
mbunge wetu alikuwa
ni mtu wa kuishi Dar es
Salaam tu au alikuwa na
ushirikiano na sisi. Wale
wa kuishi Dar halafu
akichomoza sura yake
wakati wa uteuzi na chama
chake kikampitsha sasa
anataka apitishwe na
wananchi, hukumu ya
mtu kama huyu munaijua
nyinyi hata akaja na
maneno ya namna gani
yatakuwa tu ni sehemu ya
propaganda za kisiasa la
wala si ukweli.
Wale wanaosema siasa
ni mchezo mchafu wanazo
sababu. Moja ni kuwa
wanasiasa wana tabia
ya kuchanganya ukweli
na uongo. Anaweza
kuwaahidi mambo mengi
yaliyompita kichwa au
asiyoweza kuyatekeleza
ilimradi tu achaguliwe
kisha ndio imepita hiyo.
Kampeni zimeanza

MAKALA

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Mchezo wa kuwapatia watu


kula kila baada ya miaka 5

BAADHI ya wajumbe waliopo katika timu ya kampeni ya mgombea Urais kwa tiketi
ya CCM wakiwa katika picha ya pamoja. Kulia ni Dk. Harrison Mwakyembe na
katikati ni Makongoro Nyerere siku ya uzinduzi wa kampeni wa hicho hivi karibuni.
lakini nyinyi ni mashahidi w a n a t o a a h a d i k i l a na watu wao wanaahidi,
kuwa viongozi waonataka wapitapo kila wanapo ahadi kumi hadi ishirini.
r i d h a a y a k u o n g o z a simama na kuzungumza Hivi ni kweli wanaweza

k u z i t e k e l e z a ? Au n i
sehemu ya mchezo
wao mchafu ili kuingia
madarakani? Yatupasa
tufikiri na tutulize akili
zetu ili kumpata kiongozi
bora.
Nimalizie kwa
kuwatakia kampeni za
a m a n i v ya m a v y o t e .
Jeshi la polisi liwepo
kulinda watu na wala si
kuendeshwa na vyama.
Amani ni jambo muhimu
katika nchi yetu, nchi kama
hii na ilivyo na watu wengi
mambo yakiharibika basi
yanaharibika kweli kweli.
Hivyo kila chama
kiheshimu chama
chengine, matusi yasiwepo
na wala kusiwepo
na kampeni za uongo,
waeleze wanachi ambalo
utaweza kulitekeleza na
wala usitie chumvi kwa
ambalo una uhakika liko
nje ya uwezo wako.
Wananchi tuzidi kuwa
makini na wagombea
waongo wanaojazia
yasiyowezekana, wasio
na akili na uwezo wa
kuongoza. Umakini
unahitajika kumpata
kiongozi bora, vinginevyo,
kupiga kura itabakia
mchezo wa kuwapa watu
kula kila baada ya miaka
mitano.

Usawa kati ya mwanamume na mwanamke katika ibada na majukumu

Na Dk. Akili Mohamed Akili

HUKURANI zote
anastahiki Mwenyezi
Mungu, Mola mlezi
wa ulimwengu na rehema
na amani zimfikie mbora
wa Manabii na Mitume
Muhamad (saw) na jamaa
zake na shahaba zake wote.
Ama baada ya utangulizi
h u u m f u p i k wa ya k i n i
Mwenyezi Mungu mtukufu
amemuumba mwanamke
akiwa ni binadamu mwenye
haki zote kuanzia utukufu,
uhuru na kumiliki na pia
kufikiri, kufanya kazi na
mengineyo.
Amesema Mwenyezi

Mungu mtukufu, Kwa


h a k i k a Tu m e m t u k u z a
binadamu (mtu), aya ya 70
Israi. Na wala Mwenyezi
Mungu hakubagua kuwa
utukufu ni kwa wanaume
peke yao na akasema juu ya
uhuru kwa wote kwa mambo
yasiyodhuru wengine kwa
wanamume na wanawake.
Hapana kulazimisha katika
dini (Albakarat 256).
K wa mb a k u n a u h u r u
kamili katika imani au kukosa
imani, lakini atakayeamini
atapata maisha bora hapa
duniani na akhera na lililo
bora ni uhuru wa kila jambo
la kimaisha ya akhera na aya
tukufu haikutenga uhuru
kwa wanamume tu. Na
amesema Mwenyezi Mungu
juu ya kusaidiana watu wote
wanamume na wanawake,
walio Waislamu na wasio
Waislam. Na saidianeni kwa
wema na kumcha Mungu,
na wala msaidiane kwa
madhambi na uadui Surat
Almaaida aya ya 2.
Basi wanamume na
wanawake katika asili ni
sawawasa kwa wastani wa
mambo yote aliyoyalazimisha
Mwenyezi mMungu kwa
watu, ili tu wapate maisha
bora hapa duniani, basi na
wajenge nchi na waingie

peponi kwa wale wanaoitikia


wito wa ibada sawasawa
akiwa ni mwanamke au
mwanamume. Na wataingia
motoni kwa wale wenye
kumuasi Mungu na wala
pepo haikuandaliwa kwa
ajili ya wanamume tu peke
yao na yametiwa nguvu
juu ya hayo pale aliposema
Mwenyezi Mungu mtukufu,
Yeyote mwenye kufanya
mema awe mwanamume au
mwanamke, naye akiwa ni
muumini basi tutampa uhai
mzuri na tutawalipa ujira
wao kwa uzuri zaidi kwa yale
waliyoyatenda Annahli 97.
Na neno lake, Na
akawajibia Mola wao mlezi,
kuwa mimi sipotezi matendo
ya mtendaji miongoni mwenu
awe ni mwanamume au
mwanamke al Imrani 195.
Na amesema Mtume (saw),
Kwa hakika wanawake
ni ndugu wa wanaume
Ameitoa Abuu Daudi kwa
mapokezi sahihi.
Umekuja Uislamu na
k u m u w e k a m wa n a m k e
k a t i k a s e h e m u ya k e ya
kawaida na kumrudishia
haki zake na utu wake
pamoja na daraja lake ambalo
alinyanganywa chini ya kiza
cha dhulma na uharibifu kwa
desturi mbaya.

Ukati nguvu Uislamu


juu ya mmoja na makuzi
yao kati ya wanamume na
wamawake. Na kumuumbia
mwanamume kuwa na mkewe
na kusambaza kutokana na
wao, wanaume wengi na
wanawake na muogopeni
Mwenyezi Mungu ambaye
atuwaulizenu juu ya
kuunga udugu, kwa yakini
hakuacha kuwa Mwenyezi
Mungu kwenu ni mwenye
kuwasubiri Surat Nisai aya
ya 1.
Na umekataa Uislamu
msimamo wa washirikina
na kungangania alama zao
na kutofahamu nafasi ya
mwanamke katika maisha
na kuwa shina katika
nidhamu ya maisha sawa na
mwanamume. Bali yeye ni
chanzo kikuu cha kuendelea
familia na kwa hivyo basi,
Uislamu umemtazama
kama ni zawadi toka kwa
Mwenyezi Mungu na Qurani
ikamtanguliza katika kumtaja
kuliko mwanamume.
Amesema Mwenyezi
Mungu, Humpa amtakae
mwanamke na humpa
amtakae mwanamume
au humchanganyia
mwanamume na mwanamke,
na humfanya amtakae
ngumba (49-50) Shura.

Kwa hakika katika jamvi


la heshima na utukufu
na mapenzi kwa vile
anavyoiandaa jamii kinafsi
ili kuipokea kila mtoto kwa
utulivu na nafsi iliyoridhia
na kuaminia misaada ya
Mwenyezi Mungu amesema
mwenyezi mungu mtukufu
(na wala msiwaue watoto
wenu kwa kuogopa umasiki,
sisi tunawaruzuku wao na
nyinyi Israi 31.
K a m a
U i s l a m
ulivyomtukuza mwanamke
tangu akiwa bado kijana na
kumpa mambo yake muhimu
na matakwa yake maalum
katika maisha yake, nayo
ni kuitengeneza nyumba
yake na kumchagua mume
akasema (saw) Asiozeshwe
mwanamke mkubwa ha
ashauriwe na mwanamke
mdogo hadi atoe idhini
m we n ye we Wa k a s e m a
ewe Mtume wa Mwenyezi
Mungu na ni ipi idhini
yake? Akasema Ni kule
kunyamaza. Ameipokea
Imam Muslim.
Na Uislamu umemuwekea
mwanamke kila kitu chake
cha lazima na kumpa haki
zake nyingi kama vile,
uhuru wa kumiliki kwa njia
ya usawa na mwanamume.
Inaendelea Uk. 15

15

MAKALA

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Ni nani anayekataa funga ya siku tisa za Dhul-Hijjah?

Na Abdallah A. Bawazir

UNA hatari iliyo


jitokeza na ambayo
inaonekana kukua
katika karne yetu hii ya
baadhi ya watu kujinadi
kwamba wao ni wapenzi
wa Sunna lakini hatimaye
wanaipinga Sunna hiyo hiyo
wanayo dai kuipenda na
kuitetea. Funga ya siku tisa
za mwanzo katika mwezi wa
Dhul-Hijjah {Mfunguo tatu},
ni Sunna maarufu mbele
ya Wanazuoni wetu walio
bobea katika somo la Sunna
na Fiq-hi miongoni mwa
wanazuoni walio tangulia
na walio ishi au wanao
ishi katika karne yetu hii.
Kwani Sunna hii imethibiti
kwa Hadithi ya Bwana
M t u m e { S wa l l a A l l a h u
Alaihi wa sallama} iliyo
sahihishwa na Wanazuoni
wajuzi na weledi wa somo
la Hadithi. Na miongoni
mwao ni Almarhuum Sheikh
Muhammad Nasirid diin AlAlbaaniy.
Katika wakati huu kuna
wajasiri walio ondoa khofu
nyoyoni mwao na haya
nyusoni mwao, wakashamiri
kutaka kuikataa Hadithi ya
Bwana Mtume kwa lengo la
kutaka kuifuta Sunna hii ya
kufunga katika siku tisa za
mwanzo za Dhul-Hijjah.
Funga hii ni maarufu vile
vile katika madhehebu ya
Fiq-hi, katika madhehebu
ya Imamu Shafiy, Hambali
na kadhalika sio taabu sana
kuujua umuhimu wa Sunna
hii kwa sababu imo katika
vitabu vingi maarufu vile vya

zamani na hivi vya sasa.


Al-marhuum Sheikh
Abdul-Aziz Bin Baazi
aliulizwa kuhusu mtu anaye
ikataa Sunna hii, akajibu
kama ifuatavyo:
Huyo ni mtu mjinga
(hajui Sunna) inatakikana
afundishwe.
Kwa sababu hilo liko wazi
katika Hadithi nambari 2437
katika Sunan Abi Dawood
kwamba Bwana Mtume
{Swalla Allahu Alaihi wa
sallama} alikuwa akifunga
siku tisa za Dhul-Hijjah.
Lakini kwa upande
mwingine, huenda ikawa
kuna baadhi ya wasomi
walio tatizika katika Sunna
kwa sababu ya Hadithi

nyengine sahihi inayo ashiria


kugongana na Hadithi hii.
Yaani ile Hadithi yenye kauli
ya Bi. Aysha {Radhiya Allahu
An-haa} isemayo:
Sikupata kumuona
Bwana Mtume {Swalla Allahu
Alaihi wa sallama} kamwe
katika hali ya kufunga katika
siku kumi za mwanzo za
Dhul-Hijjah.
Wa n a z u o n i we t u
wa m e u z u n g u m z i a s a n a
mgongano wa Hadithi mbili
hizi katika vitabu vinavyo
sherehesha Hadithi hii.
Lakini kwa mwenye kufikiri
kidogo tu, atagundua kuwa
hapa hakuna mgongano wa
kumfanya mpenda Sunna
asifunge siku hizo kwa

sababu ifuatayo:
Hadithi yenye kauli ya
Bi. Aysha inakanusha na
Hadithi tunayo itegemea sisi
hapa inathibitisha na katika
kaida {kanuni za fani ya
Hadithi} zetu sisi ni kwamba
katika mgongano wa aina
hii, Hadithi inayopewa
umuhimu wa kwanza na
kufanyiwa kazi ni ile Hadithi
inayothibitisha na wala siyo
ile inayo kanusha.
Sasa inaonekana kuwa
ni kawaida hapa nchini
kwetu kila unapo karibia
m we z i wa D h u l - H i j j a h
kama hivi, Masheikh
wetu wakubwa kubishana
kuhusu funga ya Arafa.
Wengine wanasema siku ya

sheria haki na wajibu,


kama vile haki ya kufungu
mkataba na masharti yake
na haki ya kushitakiwa,
kutetea haki zake mbele
ya mahakama.
Amesema Mwenyezi
Mungu Na wao wana
haki sawa na mfano wa
wanamume kwa wema
Albakarat 228.
Na imekuja katika
hadithi tukufu kwamba
Mtume (saw) amesema,
Kwa hakika wanawake
ni ndugu wa wanamume.
Ameipokea Imamu Abuu
Daudi na Tirmidhi.
H i v y o
b a s i ,
mwanamume na
mwanamke ni sawa mbele
ya Mwenyezi Mungu na
huenda mwanamke mcha
Mungu ni bora mbele ya
Mwenyezi Mungu kuliko
mwanamume. Kwa

hakika mbora wenu mbele


ya Mwenyezi Mungu ni
yule mwenye kumuogopa
sana Mwenyezi Mungu
Hujurat 13. Hivyo pepo
haikuandaliwa kwa ajili
ya wanamume tu pasi na
wanawake.
Kwa yakini Qurani
tukufu imekuwa mfano
bora kwa wanawake pale
a l i p o s e m a M we n ye z i
Mungu mtukufu, Na
amepiga mfano Mwenyezi
Mungu kwa walioamini,
p a l e m k e wa F i r a u n i
aliposema Mola nijengee
mimi k wa k o n y u mba
peponi na uniokoe mimi
d h i d i ya F i r a u n i n a
matendo yake na uniokoe
mimi dhidi ya watu wenye
dhuluma, na Mariam
bint Amrani, ambaye
amehifadhi tupu yake na

tukampulizia sisi kutokana


na Jibril na akathibitisha
maneno ya Mola wake
mlezi na vitabu vyake na
kuwa miongoni mwa watu
wema. Atahrimi 11-12.
Kwa yakini umekuja
Uislam na tabia
nzuri, na vyanzo vya
kumyanyua mwanamke,
na kumuhifadhi yeye
na heshima zake, na
kumrudishia haki zake
zilizotekwa tangu muda
mrefu, na kumpa haki
zake zote kwa ukamilifu
mbele ya watu wote, ili
watu wote wajue utukufu
n a u k u u wa d i n i ya
Kiislam na uadilifu wake
kati ya viumbe. Mwenyezi
Mungu ndiye ambaye
anayeongoa katika haki
na njia iliyonyooka.

Usawa kati ya mwanamume na mwanamke katika ibada na majukumu

Inatoka Uk. 14

Amesema Mwenyezi
Mungu mtukufu,
Mwanamume ana fungu
lake katika mali ya wazazi
na ndugu wa karibu na
mwanamke ana fungu lake
katika mali za wazazi na
ndugu wa karibu, ikiwa
mali ni kidogo au nyingi,
ni fungu maalum Nisai 7.
N a
U i s l a m u
ameheshimu umiliki
huu na kuutukuza kwa
kumpa uhuru mwanamke
wa kutumia. Amesema
Mwenyezi Mungu
wapeni wanawake
mahari zao za wajibu na
wakitamani wenyewe kwa
nafsi zao, basi kuleni kwa
vizuri kabisa Nisai 4.
Na Qurani imemuweka
sawa mwanamke na
mwanamume mbele ya

kufunga Arafa ni ile siku


ya kisimamo katika uwanja
wa Arafa huko Makka. Na
wengine wanasema kwamba
funga hiyo inategemea
mwezi mwandamo hapa
kwetu hata kama siku hiyo
itatofautiana na siku ya
kisimamo cha huko Makka.
Wakati mwengine mjadala
huu unakuwa mkubwa kiasi
cha kuwapelekea baadhi
yao kuandaa muhadhara ili
kutetea siku moja hiyo tu
katika mwaka. Si hivyo tu
bali baadhi yao wanatenga
khutba maalumu siku ya
Ijumaa juu ya Mimbari
ili kutetea siku moja hiyo
katika mwaka. Mjadala huu
upo mpaka leo hii, inabidi
tuwaulize Masheikh wetu
hawa wanao vutana maswali
yafuatayo:
Mosi, ni upi msimamo
wao juu ya funga ya
siku tisa za Dhul-Hijjah?
Wanakubali kwamba hiyo
ni Sunna au hawaikubali?
Kama hawaikubali, basi
itabidi wayakubali maneno
ya Al-Marhuum Sheikh Bin
Baazi kwamba wanahitaji
kuelimishwa. Lakini kama
wa n a k u b a l i p i a i t a b i d i
t u wa u l i z e s a b a b u i l i y o
wafanya wao washabikie
sana funga ya siku moja tu
ya Arafa na kuzipuuza siku
nane za kabla ya siku ya
Arafa?
Pili, Vitabu vya Fiq-hi na
vitabu vya Hadithi karibu
vyote au vilivyo vingi,
vinaeleza kwamba tofauti
iliyopo baina ya funga mbili
hizi; funga ya siku nane kabla
ya Arafa na funga yenyewe
ya Arafa, ni kwamba funga
ya siku nane ni Mustahabu
{Sunna} na funga ya
Arafa yenyewe ni Sunna
Muakkada {iliyo kokotezwa}
tu. Lakini zote ni Sunna na
zote zimethibiti kutoka
kwa Bwana Mtume {Swalla
Allahu Alaihi wa sallama}.
Kwa maana hiyo basi, hii
tofauti ya ziada Masheikh
zetu hao wameipata wapi?
Kwani kuna kauli inayosema
k wa m b a k a t i k a m w e z i
wa Dhul-Hijjah funga ya
Sunna ni ya Arafa peke
yake? Yaani, Bwana Mtume
alikuwa akifunga siku moja
tu ambayo ndio Arafa?
Kwa nini Masheikh
zetu badala ya kuzozana
katika mihadhara yao na
Mimbari zao kwa ajili ya
kuitetea siku moja tu ya
Arafa, hawakubaliani na
sisi kuwahimiza watu katika
m we z i wa D h u l - H i j j a h
kufunga siku tisa zote za
mwanzo na Arafa ikawa
h u m o h u m o ? H a wa o n i
kwamba kwa utaratibu huu
mizozo na mabishano baina
yetu yatakuwa yamefikia
mwisho na kuisha?
(Kwa mawasiliano 0773
215 898)

16

MAKALA

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Mabadiliko: Nafasi ya Lowassa katika siasa za Tanzania

Inatoka Uk. 12

kuvunja nchi, bali kuondoa


umaskini uliokithiri. Ila
dhamira hiyo bado ipo katika
lindi la ukungu wa fitna,
kwani inasulubiwa kuhusu
kukubalika (yaani, miongoni
mwa makuhani) kwa kiongozi
wake Edward Lowassa kuwa
hakidhi viwango vya usafi
vilivyowekwa na mtiririko
wa fitna katika CCM. Aliwahi
kuhusika na mkataba wa
kuzalisha umeme binafsi,
tunaambiwa ulileta taabu.
Kumbe taabu yenyewe
ilisababishwa na wabaya
wake, waliokataa
kuidhinisha mkopo mdogo
tu kukamilisha mradi wa
kutwaa mtambo, ukachelewa
takriban miezi sita. Licha ya
kuwa fitna inalenga tukio
hilo (kwa uwongo kuwa
ulikuwa mpango mbaya, wa
mtambo wa megawati 100
ambako serikali inalipa kwa
miaka miwili, wakisahau
ulikuwepo tayari mtambo
wa megawati 100 ambako
serikali inalipa kwa miaka
20), suala halisi ni utajiri wa
Lowassa, Ndiyo nanga ya
mabadiliko nchini; chanya
au mbaya?
Ndiyo hapa linakuja suala
la utajiri wa Lowassa, kuwa
unatokana na ufisadi kama
wahafidhina wanavyosema,
au ni baraka za Mungu
hasa kutokana na uhitaji wa
mabadiliko katika wakati
unaokuja. Kuna vielelezo
viwili vya suala hilo, au
tuseme baada ya kupangua
hoja ya msingi, kuwa kama
utajiri wa Lowassa unatokana
na ufisadi, kwanini waliokaa

Inatoka Uk. 12

bado wazazi, au Rebeka,


aliwatofautisha wanae,
na wakatofautiana kabisa.
Yakobo alioa wake wawili
a m b a o n i n d u g u wa
tumbo moja, wakafuatana
na wajakazi wao, Yakobo
akiwa amepata utajiri
m k u b wa wa m i f u g o .
Wajakazi nao wakazaa na
Yakobo kwa kuruhusiwa
na wake zake, wakafikia
wana 12.
B i l a u t a j i r i Ya k o b o
asingeweza kuinua kizazi
cha wana nao (mabinti
zake hutajwa kwa nadra)
na hapakuwa na tofauti
kati yao kuhusu nani
mwana wa mke mkubwa
au mdogo, mwana wa mke
au mjakazi. Ila kwa vile
'Shetani anaishi milele,'
tofauti zao zilianzia kwa

madarakani miaka yote


hawana utajiri kama
wa kwake, na hajawahi
kutuhumiwa kwa wizi halisi?
Ujanja wa hapa na pale (ten
percent), kungemfikisha
alipo, au ujasiriamali?
Ukiangalia kwa karibu
unaona kuwa utajiri wa
Lowassa ni sehemu ya agenda
ya k i m a a n d i k o k u h u s u
mabadiliko, kwani Mungu
anainua mali binafsi akiwa
na Ibrahimu, na Lowassa
ni kielelezo cha hilo na
kupitia kwake mfumo wote
ubadilike. Dhana ya Misri,
ya Farao, ni kuitegemea dola,
watu wote wawe watiifu.
Wawe mali ya serikali,
watumwa wa serikali,
wakulima wabaki katika
ardhi ya serikali hawana
chao.
Wahafidhina hudai miiko
ya uongozi inawafanya
v i o n g o z i wa w e k a r i b u
na watu; dhana potofu.
Hali halisi ni kuwa miiko
hiyo inahamisha hisia ya
ujasiriamali kutoka katika
azma ya kufanya kazi fulani
yenye faida, kuipeleka azma
hiyo katika kituo cha kazi,
mtu akusanye kwa siri ajenge
nyumba (labda hata ya
kifahari), na ya kupangisha,
na hata kwa mwandani
wake mmoja au wawili.
Anabaki "kiongozi msafi," ila
akifanya ujasiriamali halisi na
kufaulu, wakipata mwanya
wowote wanasema ni mwizi.
Mwalimu alidai kuwa utajiri
wa Lowassa ulitokana na
kuwa mkuu wa Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano
pale Arusha; majuzi mfitini

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CHADEMA-UKAWA, Mhe. Edward Lowassa (katikati)


mmoja alidai unatokana na aulinde mfumo, wakati wa kuzalisha kama sasa.
umasikini unatokana na Hivyo hisia ya kina ya
uwaziri mkuu.
Huyu mfitini, anayejiamini mfumo wa Misri, wa dola kutaka mabadiliko ambayo
sana kuwa ni mwadilifu, hodhi, iliyoshika kila kitu, ni aina ya maombi, huleta
aliwahi kutibiwa katika k u n e e m e s h a wa t a wa l a . uwezekano wa mabadiliko
hospitali ya mkwewe (kwa Baada ya kukwama miiko
kufikiwa katika njia isiyo
mujibu wa taarifa za wakati ya uongozi, wahafidhina
huo) kwa maradhi ya mguu w a n a j i t a m b u l i s h a k wa ya m p a r a g a n y i k o wa
kwa takriban wiki moja. Bili kutokuwa na uhusiano wa moja kwa moja. Kuna
iliyofikishwa serikalini na kibiashara na makampuni hatari ya mikasa kwani
malipo yakaidhinishwa ni binafsi, hasa ya nje. Ndiyo dhambi za Watanzania
shilingi milioni 100 - huo siyo yanayoyasumbua mashirika na hasa katika kuua siyo
ufisadi! Ni ujanja ujanja tu y a u m m a n a w a t e t e z i Albino tu, ila watu wa
aina tofauti ili mtu afikie
wa kila siku, na unakubalika wake bungeni, wasiotaka
utajiri, ni nzito. Huwezi
kwa sababu mtu wa aina y a k a g u s w a . Ya k i i n g i a
kuhakikisha kuwa hakuna
hiyo anajitwalia kidogo tu mikononi mwa watu binafsi
hukumu ila maombi
na haweki mfumo hatarini. yatalipa kodi, tusipoteze
Lowassa na Rostam Aziz, s h i l i n g i t r i l i o n i m b i l i ya mabadiliko chanya
kwa vile ni wafanyabiashara kulipa madeni TANESCO, na kumtumia Lowassa
halisi, wanaweka mfumo ya ubadhirifu na kulinda aliyefaulu kutetemesha
mfumo, aondoe mwiko
hatarini, waubadilishe.
uwekezaji.
Mgombea wa CCM
K u i n g i z a m t a m b o wa kutobinafsisha, atue
a n a p a n i a k u o n d o a kutakuwa ujasiriamali, bila mizigo. Uhakika haupo ni
watu wachache wabovu, ulinzi maalum wa uwezo uwezekano.

Lowassa na Yakobo: Baraka za utajiri


kwa vipindi tofauti vya kazi ya Mungu

baba yao kumpenda sana


Yusufu, kama mwana
mwenye heshima, adabu,
msikivu na hata haiba ya
kupendeza. Kijicho hicho
kikawa nyenzo ya utukufu
wa Mungu, wakataka
kumuua ila ikaishia
kumuuza kwa msafara wa
wa-Ishmaeli, akanunuliwa
Misri, akastawi.
Kielelezo kuhusu ubaya
wa ndugu zake Yusufu na
jinsi Mungu alivyokuwa
na nia na ubaya huo, ili

Yusufu aondolewe katikati


yao na kuandaa ujio wa
ukoo wa Yakobo nchini
Misri. Ni hapo historia
yote ya unabii na sheria
pale Musa anapoinuliwa
miaka 800 baadaye
(kuanzia 2300 BC hadi
1500 BC) inaposimama.
Kuinua na kuteketeza
himaya au kibri katika
maisha ya watu, siyo
mzunguko hasi wa mema
na mabaya, wa vicheko
na vilio, ila mtiririko
wa kuvunja nguvu za

Ibilisi, ambaye baada ya


Gharika Kuu anachukua
sura ya Mungu Jua wa
Babeli aliyeabudiwa pia
Misri (na kwingineko
duniani). Ndiye mjenzi
wa ule mnara wa Babeli,
akatukuzwa, na ndiye
hasa anayehitaji sadaka
ya binadamu amuongezee
m t u n g u v u , a t a wa l e .
Ndiyo hapo inakuja ibada
ya sananu (huruhusu
sanamu zifanywe kwa
mfano wake), na historia
ya wokovu. Katika kila

mfumo wa jamii kuna


msuguano na mtiririko wa
matukio ya kupambana
kwa jema na baya, jema
likiwa ni kutenda mema
peke yake bila fidia kutoka
k wa M u n g u ; b a ya n i
kutenda utakalo, kutoa
sadaka upate nguvu.
K u n a u h u s i a n o wa
karibu kati ya utajiri wa
Lowassa na hawa wakuu
wa zamani, kuwa utajiri
wao uliwawezesha
kuwa huru, kutoogopa
kutofautiana na mfalme,
Farao wakati Ibrahimu
akiwa Misri, na Abimeleki
wakati akiwa Kanaani.
Katika mazingira yetu,
mfalme alikuwa ni
Mwalimu Nyerere
wakati akiwa hai, na
fikra ya Mwalimu akiwa
Inaendelea Uk. 17

17

MAKALA

NDOA

1.Bismillahi nakaa, ndugu zangu sogeeni


Ninayo ya kutongoa, si mengi kukuchosheni
Machache ya manufaa, naomba yasikizeni
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
2.Kuchapo twaona ndoa, zafungwa misikitini
Sherehe zimeenea, kila kona mitaani
Kwa wingi twahudhuria , mashahidi si utani
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
3.Mtume katuusia, enyi ndugu ikhwani
Wake wema kuchagua, tuwapendao nyoyoni
Tuishi nao kwa nia , ya kudumu maishani
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
4.Mashekhe Makadhi pia, wajibu wamebaini
Khutuba watusomea, waadhi, nasaha ndani
Twapaswa kuzingatia, tukaishi furahani
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
5.Kuozwa mke sheria, kutoka kwa Rahmani
Kaka usije zembea, kujifanya hayawani
Kaa na mwenza tulia, si kwema vichochoroni
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
6.Bi Harusi nawe poa, mpende wako mwandani
Sasa umeshaolewa, ukome vibarazani
Hakuna ila umbeya, na matusi ya nguoni
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
7.Ndoa inahitajia, subira iwe usoni
Mmoja akikosea, muombane samahani
Visasi kutobakia, na kumlani shetwani
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
8.Kila siku kumbukia, hili liwe akilini
Ndoa ni kama mauwa, yalopandwa upenuni
Usipo yamwagilia, yatachanua kwa nini
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
9.Harusi twaziombea, kwa wetu Mola Manani
Zisiingie madoa, tukaishi kwa huzuni
Zihifadhi Ya Jalia, na ibilisi fattani
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
10.Namalizia kwa dua, mikono tunyanyuweni
Amina kuitikia, ni wetu utamaduni
Allah tutakabalia, waja wako tuauni
Tusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha
SULUHU A. HAMZA
C/O ZAINAB H. MTIMA (0777 357 031)
ZANZIBAR 0776 720 588

KUOMBA DUA

1.Dua tumuombe Mola, Muumba asiye shaka


Hana sifa ya kulala, wala bado hajachoka
Kafika kila mahala, dunia kaizunguka
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
2.Tuombe kwa zetu shida, Mola atatuauni
Twahitajia msaada, sisi kwake masikini
Tufanye ni kawaida, asubuhi na jioni
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
3.Hata tukiwa rahani, kuomba tusisahau
Inazidisha Imani, ya Mola kutodharau
Hili liwe akilini, na wakati ndio huu
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
4.Mtume katuhimiza kila jambo ni kwa dua
Hilo tusijepuuza, ovyo tukajiendea
Chochote unachoanza, Mola kumuelekea
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
5.Unapotoka nyumbani, dua iwe ya awali
Kujikinga na shetani, wasije kukukabili
Mengi majanga njiani, Mungu ayapishe mbali
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
6.Unapokwenda kazini, kutafuta cha halali
Au la msikitini, swala tano kuziswali
Na iwe hata sokoni, dua kuacha muhali
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
7.Popote unapokwenda, dua ndio ngao yako
Muumba atakulinda, uepuke masumbuko
Dua ikisha kushinda, mwenzangu huna mashiko
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
8.Ukiingia chooni, dua usijeiacha
Uepukane na jinni, huko yeye hujificha
Huo ni utamaduni, uwe nao kutwa kucha
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
9.Enyi ndugu Islamu, lengo ni kukumbushana
Dua kuomba muhimu, uwe nacho au huna
Sote tushike hatamu, haya kwetu ni bayana
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
10.Hapa nimehitimisha, sinalo la kuongeza
Machache nilofikisha, anza leo kujifunza
Mikono nimeiosha
, ni kwenu kutekeleza
Dua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada
SULUHU A. HAMZA
C/O ZAINAB H. MTIMA (0777 357 031)
P. O. BOX 1898
ZANZIBAR
0776 720 588

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Lowassa na Yakobo: Baraka za utajiri

Inatoka Uk. 16
amekufa, au uongozi
wa chama tawala
k a m a wa l i n z i wa
fikra hiyo. Lowassa
amekuwa kiongozi
huru mjasiriamali,
mfanyabiashara
aliyefaulu; wengine
hudunduliza kidogo
wakichota serikalini.
Kuna uwezekano
mkubwa wa Mungu
kukamilisha kazi ya
kupangua kabisa
dhana potofu za
Azimio la Arusha za
kuitenga Tanzania
na mitaji duniani, na
kuwabana viongozi
wategemee ajira ili
wawe watiifu kwa
chama na serikali,
yaani Nyerere na
warithi wake. Ndiyo
msingi wa ubadhirifu,
wizi uliokithiri na
huku viongozi wote
wanajiamini ni
wasafi, kwani wizi wa
kudokoa hatma yake
ni maisha bora katika
n g a z i ya f a m i l i a .
Akili za walioenda
s h u l e k wa j u m l a
zinajielekeza katika
udundulizaji na
kupinga uwezekaji,
ubinafsishaji.
Endapo hali hiyo
itafikiwa, utakuwa
muujiza wa Mungu
kumwinua mtu
mmoja awe na nguvu,
alete mafuriko
ya wafuasi akiwa
CCM apangue hila
za mwenyekiti wa
chama kuhusu nani
awe mgombea, aweke
aliyefaa zaidi, na yeye
aende kugombea
upinzani. Ni aina
ya mnara wa Babeli
kisiasa, na chanzo
chake ni u-Yakobo
wa Lowassa, kama ile
hadithi ya Uyunani
ya mtu akigusa kitu
huwa dhabahu. Ni
kuanza na ng'ombe
uuze wachache
uweke hizo fedha
benki, ukope nyingine
uunde kampuni ianze
kujilipa, kila wakati.
Kuna uwezekano
pia wa kuunda
kampuni za madini
hasa kutokana na
hali ya kutapakaa
kwa madini mkoani
Arusha na Manyara,
nje ya ushiriki katika
maeneo mengine
ya biashara, kama
kununua mashamba

na kukata viwanja
vya bei mbaya baada
ya miaka kumi, n.k.
Au kununua viwanja
sehemu za mijini na
kujenga maghorofa
baadaye, iwe ni mtu
binafsi au kwa ubia na
wengine, n.k. Ni vitu
ambavyo ukivifikiria
vinawezekana, lakini
baraka za Mungu ni
kumwezesha mtu
mmoja afanye hivyo,
ili aipangue milki ya
CCM.
Mungu aliitingisha
Misri akitumia silaha
ndogo, ya Sara
mke wa Ibrahimu
ambaye Ibrahimu
alimwambia kokote
wa t a k a p o k we n d a
aseme ni ndugu
yake Ibrahimu, ili
watoe posa kwake,
na siyo kumwua
na kumchukua
Sara. Ila alijua kwa
uficho Mungu
angejitambulishwa
kwao
hima,
wamrudishe Sara.
U t a j i r i wa m t u
mmoja unampa
nguvu, mradi kuna
kitu kama utawala
wa sheria na siyo
udhalimu wa moja
k wa m o j a , k u wa
huru na utawala, na
kwa kushiriki kwake
kisiasa, kuweza
kuweka tofauti kati
ya itikadi iliyopo,
na inayotakiwa.
Lowassa anaogopwa
na watu wa CCM
kuwa anaweza
kurudia sera za
awamu ya pili za Rais
Ali Hassan Mwinyi
ambazo Waziri wa
Fedha Saada Mkuya
Salum anajizuia tu
kuzitamka waziwazi,
kuondoa mizigo ya
mashirika ya umma
begani mwa serikali.
Nje ya baraka ya
utajiri, kazi hiyo
isingefanyika,
na kwa maana
hiyo upo kabisa
u we z e k a n o k u wa
inaweza kufikisha
mabadiliko, au iwe
ni mchango muhimu
wa mabadiliko
makubwa kwa idadi
ya wabunge, kupooza
utukufu wa CCM.
Kibri cha CCM
n i k u k a t a a wa t u
wengine kuwa huru
kukaa kwetu na
kununua mali, pamoja
na kushirikiana na
wageni kununua mali
kutoka kwa wenyeji,
wa m p e m we n ye j i

mtaji wa kufanya
biashara, kilimo
bora, siyo kuishi
katika umaskini,
na wao wafanye
biashara wastawi.
Ndiyo huu mfumo
jadi wa ardhi kuwa
mali ya serikali ili
watumwa wa serilali,
wakulima, wabaki
katika ardhi hiyo
wasiwe na uwezo
wa kumwuzia mgeni
kwa bei ya soko, na
akinunua ana haki tu
ya kutumia, huweza
kunyang'anywa
na kina Magufuli
wakati wowote
kama alivyotangaza
majuzi. Mungu
anachokitaka hapa
nchini ni unyeyekevu
wa kukubali kuwa
wengine wana haki
wakitaka kuishi
hapa nchini, ambayo
inategemea mfumo
wa mali binafsi ili
wanunue bila hatari
ya kunyang'anywa
na warithi wa Farao
na Abimeleki. Mungu
akiwa mmoja, hiyo
inawezekana.
U b a g u z i wa k i n a
unatokana na ibada
ya sanamu, ya kila
taifa na mzimu wake.
Suala ni kama
Mungu atafanikisha

mabadiliko ya
mfumo kwa kuingia
mali binafsi, na siyo
tu mabaliko ya Baraza
la Mawaziri waingie
U K AWA , h a l a f u
wa e n d e l e z e f i t n a
ile ile, wakatae mali
binafsi, waendeleze
umaskini. Kwa
upande fulani
baraka ya Mungu
kwa Lowassa
kufikia madarakani
inategemea dhamira
hiyo. Kama ana nia ya
mabadiliko ya kweli,
kupangua mfumo
huu wa jadi, na kuacha
kibri cha kufukuza
makampuni ya nje,
wawe na haki sawa
hapa nchini kama
raia wengine. Endapo
atabania dhamira
yake atake kufuata
mfumo uliopo licha
ya baraka za Mungu
kwake, kuwa mtu
huru kuupangua
mfumo kwani
haitegemei CCM,
kuna hatari ya utabiri
mbaya kwake ambao
ulitajwa mwezi
Januari na mtabiri
Hassan Yahya pamoja
na Sheikh Sharrif
Mwitongo kutimia.
Ni kuambiwa
'kahubiri Ninawi.'
wewe useme 'sitaki....'

MASOMO KIDATO CHA KWANZA 2016


(PRE FORM ONE COURSE) 2015

TA A S I S I YA E L I M U YA W E C
Inawatangazia nafasi za masomo ya
Kidato cha kwanza na masomo ya
awali PRE-Form One Course itaanza
01/10/2015 hadi 1/12/2015. Tarehe ya
kuripoti ni 27/9/2015. Katika shule zake
zilizopo Kibaha Pwani.
Masomo yatakayofundishwa
(Pre form One):
Hisabati
Kiingereza
Kompyuta
Sayansi
Biashara
Shule zina mandhari nzuri ya
kusomeshea na Maabara za kisasa.
ADA (Pre-form one course ) Bweni
shs.150,000/= Kutwa shs 80,000/=
Madaftari na kalamu zitatolewa
bure shuleni.
Kwa mawasiliano: 0754-395186,
0656-313889, 0659-573004, 0786-959522,
0789-887799, 0784-489476, 0765-198360,
0719-904904, 0768-904904.

18
Na Mwadini Ali

ILA ninapomuangalia
Samia Suluhu Hassan,
ninapata shida
kufikiria ni kwa namna gani
atafanikiwa kushawishi
u m m a wa Wa z a n z i b a r i
kumpigia kura Daktari John
Pombe Magufuli itakapofika
tarehe 25 mwezi ujao wa
Oktoba. Siku hiyo ndiyo
siku ya upigaji kura katika
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Kutakuwa na
kura ya kumchagua Rais wa
Jamhuri, Mbunge wa kuingia
Bunge la Jamhuri na Diwani
wa kufanya maamuzi kwenye
Baraza la Madiwani katika
Halmashauri mbalimbali.
Lakini katika siku hiyo, pia
Watanzania wa upande wa
Zanzibar, ambao unapokuja
uchaguzi mkuu wa Jamhuri
huwa wanakuwa na kura
mbili Rais na Mbunge
watapata haki ya kupiga kura
nyingine tatu za uchaguzi
mkuu wa Zanzibar. Kura
hizo ni ya kumchagua Rais
wa Zanzibar, Mjumbe wa
Baraza la Wawakilishi, ambalo
ndilo Bunge kwa wao kwa
ajili ya kuyaamua masuala
yanayoihusu Zanzibar peke
yake, pamoja na kura ya
Diwani, ambaye huingia
katika mabaraza ya madiwani
yakiwa nje ya mfumo wa
Muungano.
Sasa wakati Samia, mwenye
asili ya Makunduchi, Wilaya
ya Kusini, Mkoa wa Kusini
Unguja, anazunguka mikoa ya
Tanganyika kumuombea kura
Dk. Magufuli, atawajibika
kurudi kwao Zanzibar
kufanya kazi hiyo hiyo.
Samia ambaye elimu yake ni
ya kiwango cha Shahada ya
Uzamili (Masters Degree)
aliyoipatia nchini Marekani,
katika masuala ya uongozi
wa fedha, baada ya kuanza
kusomea takwimu kiwango
cha cheti, ameteuliwa na
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuwa mgombea mwenza.
K wa k u wa m g o m b e a
mwenza, jukumu lake ni
kusimama sambamba na Dk.
Magufuli anayegombea urais.
Magufuli akichaguliwa, moja
kwa moja atakuwa amteua
Samia kuwa ndiye makamu
wa k e wa R a i s . K u f i k i a
hatua hiyo, Samia atakuwa
na wajibu wa kujipa muda
kuzunguka kwenye majimbo
ya Zanzibar kumpigia chapuo
Dk. Magufuli ambaye sio
tu ni mgeni machoni pa
Wazanzibari, bali kwa hakika
hafahamiki kisiasa.
Kweli anasikilikana
akisema hili na lile akiwa
katika majukumu yake ya
k i k a z i k wa wa d h i f a wa
uwaziri, tangu alipoteuliwa
kwa mara ya kwanza naibu
waziri wa ujenzi baada ya
kuingia serikali ya awamu ya
tatu chini ya Benjamin Mkapa
na baadaye kupandishwa
kuwa waziri kamili, lakini
hakujisumbua kuwa karibu
na Wazanzibari.
Inawezekana kwa kujua
mazingira ya Zanzibar na
ugeni wa Dk. Magufuli, ndipo
C C M wa k a mt e u a S a m i a
kushika ugombea mwenza
wakitarajia kwa uanajike
wake, atamudu kuuvuta
umma umkubali daktari huyo
na kushuhudisha mapenzi
yao kwake kwenye sanduku
la kura. Ni utabiri uliokwenda

MAKALA

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Samia ana kazi ngumu


kumnadi Magufuli Zbar
Mwenyewe ashajipalia mkaa...
Baada ya yale ya Katiba Dodoma

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John


Magufuli (kulia) akiwa na mgombea mwenza Bi Samia
Suluhu Hassan.
m r a m a . N i n a v y o ya o n a
m a m b o , n a k wa k u wa
Samia ni mwanamke kama
wanawake wengine, lakini
pia kwa jinsi ninavyoijua
siasa ya Zanzibar, uchaguzi
wa Chama cha Mapinduzi
utawarudia wenyewe
wajumbe wa Mkutano Mkuu
au viongozi wakuu wa chama
hicho.
Hakuna historia hata
nduchu ya mwanamke wa
Kizanzibari kupata umbele
katika mwenendo wa siasa
za Zanzibar. Hao waliotajwa
na kutajika, basi si katika
kupanda majukwaani wao
wenyewe na kuhutubia
umma. Hata kidogo.
Wanawake hao ambao naona
ni wachache wa kuhesabu
vidoleni, walipata umaarufu
kupitia migongo ya waume
zao walipokuwa katika
kilele cha mafanikio kwenye
nyadhifa za kisiasa Zanzibar.
Wanasiasa waliosifika
Zanzibar, walijenga taswira
nzuri katika jamii kwa kuwa
walikuwa wakifuatana na
wake zao kwenye shughuli za
kisiasa, hasa zilizowafikisha
kupanda majukwaani
kuhutubia. Kwa hivyo wake
zao walitambulika tu kwa
sababu ndio mbeleko za
waume zao. Hilo moja.
Lakini
jingine
litakalomletea shida Samia
katika kumtafutia kura
Dk. Magufuli, ni ukweli
kwamba yeye mwenyewe
amejiangusha, kiasi cha
kufikia hatua kwa sasa
kuonekana amepotea njia
katika kupigania haki za
wanawake wenzake, bali kwa
zaidi ya hapo, mustakbali wa
nchi yake.
Samia alikuwa mwanamke
makini na shupavu
alipokuwa akifanya kazi
za harakati wakati akiwa
kwenye mashirika ya hiyari
ambako alijikurubisha mno

na wanawake kuyatambua
m a t a t i z o ya k i j a m i i n a
kushiriki kupanga mikakati
ya namna ya kuyashughulikia.
Kwa wakati wote, alikuwa
bega kwa bega na wanawake.
Hichi kilikuwa ni kipindi
cha miaka ya 1990 wakati
hajagusa ulingo wa siasa
kabisa. Ingawa alikuwa
serikalini, lakini kazi zake
akiwa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Mpango wa
Chakula Duniani (WFP)
zilimuweka karibu zaidi
na jamii. Alipata bahati ya
kuwa Meneja Msimamizi
wa mradi katika shirika
hilo kati ya mwaka 1985
na 1987. Akarudi serikalini
na kuwa Ofisa Mipango
katika Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar. Baadaye akachupa
na kushiriki kwa kasi safari
hii shughuli za kijamii. Ni
h a p a a l i p e wa d h a m a n a
ya kuongoza Mtandao wa
Mashirika ya Hiyari (NGOs)
alikofanya kazi kwa miaka
kadhaa kama Mkurugenzi
Mtendaji (1988/1999).
Wanaomjua wanasema leo
kuwa Samia alipokuwa kule
chini, alikuwa mwanamke
shupavu kwa hoja na
mipango. Akijishirikisha na
alikuwa mwenye huruma
na maono ya mbali katika
kupigania haki za wanawake
na mafukara. Ni mtizamo
huo uliwachochea wanawake
wenzake kumshawishi
kuingia kwenye siasa wakati
miaka hiyo ya 1990 inafikia
ukingoni. Taarifa zinasema
alianza kujisogeza kwa
wanasiasa wa kiutawala na
Alhamdulillah, alionekana
wakati wa kuelekea uchaguzi
m k u u wa Z a n z i b a r wa
mwaka 2000.
Mwanamke mmoja
ambaye yungali kwenye asasi

za kiraia akisaidia kuwajenga


wanawake na watu wa hali
za chini moyo wa kutambua
matatizo yao na kujitahidi
kujikwamua, ameniambia
alikuwa mmoja wa wanawake
waliokuwa mstari wa
mbele kumshawishi Samia
kupigania nafasi za kuingia
Baraza la Wawakilishi kupitia
Viti Maalum.
Ni vipi jina lake liliingia
akilini mwa Amani Abeid
Karume, aliyeshika urais
mwaka 2000, sijapata kujua.
Lakini hapo ndipo alipoingia
Baraza la Mapinduzi baada
ya kuteuliwa kuwa Waziri
wa Kazi, Maendeleo ya Jinsia
na Watoto.
Ikumbukwe ni wakati CCM
iliposhutumiwa kuidhibiti
Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC), ikatumia mwanya
kuvuruga uchaguzi na
kujitangazia ushindi kwa kila
ilichokitaka. Kunapotokea
janga kama hilo na ukasikia
mtu amepenya na kuteuliwa
nafasi kubwa kama uwaziri,
ujuwe kuna mengi yalikuwa
yanaendelea kabla. Au labda
ni ukweli pia kwamba katika
mazingira hayo hayo, hata
asiyefikiriwa hupenya na
kupata nafasi kubwa ya
kisiasa au ya utendaji kwenye
asasi ya serikali.
Samia aliingia uchaguzi
wa 2005 akitafuta jimbo sasa.
Alipofanikiwa akarudishwa
Baraza la Mapinduzi, safari
hii akiteuliwa kuongoza
Wizara ya Utalii, Biashara
na Uwekezaji chini ya Rais
Karume. Sifa zake ni nyingi
kiutendaji mote alimopita.
Pengine shida kwake
ilianzia alipoingia siasa
za kibunge uchaguzi wa
2010. Aligombea ubunge
jimbo la kwao Makunduchi,
akashinda. Akateuliwa Waziri
katika Ofisi ya Makamu wa
Rais, chini ya serikali ya Rais
Jakaya Kikwete. Ukafika
m u d a wa t a i f a k u i n g i a
katika utafutiaji wa katiba
mpya ya jamhuri, ikiwa ni
utekelezaji wa azma ya Rais
kuipatia jamhuri Katiba
itakayodumu kwa miaka
50 mingine ijayo. Bunge la
Jamhuri likatunga Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba,
2011 ambayo imeelekeza
kuwepo Bunge Maalum la
Katiba litakalojadili Rasimu
ya K a t i b a i t a k a y o k u wa
imeandikwa na Tume ya
M a b a d i l i k o ya K a t i b a .
Bunge hili lilipokutana
mjini Dodoma, baada ya
kuandaa Kanuni, lilifanya
u c h a g u z i wa v i o n g o z i .
Akapatikana Samuel Sitta
kuongoza bunge, na Samia

akawa naibu wake. Hapo


ndipo Samia alipoingizwa
mjini. Bunge lile lilifanya kazi
ambayo haikuwafurahisha
wengi, wala kukidhi
viwango na matarajio ya
wananchi ya kupata Katiba
kwa kuwa CCM ilidhibiti
kila kitu na kufanikiwa
kuivuruga Rasimu ya Katiba
iliyoandaliwa na Tume ya
Jaji Joseph Warioba, na
kupandikiza mapendekezo
yake.
Kwa sehemu kubwa, Katiba
iliyotoka kutokana na bunge
lile, inazidi kuikandamiza
Zanzibar. Kwanza imeondoa
pendekezo la kuwepo
Muungano wa mfumo wa
serikali tatu, na kadhalika
imerudisha utamaduni uleule
wa kuzuia mabadiliko ya
mifumo ya uongozi ukiwemo
wa kuiwezesha Zanzibar
kutumia fursa zaidi za
kujenga uchumi kwa manufaa
ya watu wake. Matokeo haya
yamechangiwa sana na Samia,
kama kiongozi msaidizi wa
Bunge Maalum lile, ambaye
alisimamia mkakati wa
chama chao akishirikiana na
wajumbe wenzake wa CCM
waliopuuza matumaini ya
Wazanzibari kupata katiba
inayotambua haki yao ya
kujiongoza.
Mwisho wa bunge lile
ukawa mwanzo wa wakati
mgumu kwao kujitokeza
k wa u m m a k wa k u j u a
walichokifanya na CCM
wenzao wa Tanganyika, ni
kinyume cha matarajio ya
Wazanzibari na mustakabali
wa nchi yao.
Suala la Katiba mpya
limehanikiza akilini
mwa Wazanzibari wengi.
Linachukuliwa kama
u k a n d a m i z a j i wa h a k i
za Zanzibar. Hapohapo
inaaminika suala hilo ndilo
lililochochea utawala wa
CCM kuwakamata masheikh
walio chini ya Jumuiya ya
Uamsho na kuwasweka
gerezani miaka mitatu
sasa bila ya mashitaka yao
kutolewa ushahidi.
Hakuna
namna
walioshiriki kujenga katiba
inayoonekana kuzidi
kuikandamiza nchi huku
ikidhoofisha na kuhilikisha
viongozi wa Kiislamu
kwa kuwanyima haki zao
za kifamilia na faragha,
wa t a u n g wa m k o n o l e o
wa n a p o t a k a r i d h a a ya
wananchi.
Samia hajafanikiwa kufuta
mtizamo huo. Hisia za chuki
dhidi ya CCM zinaongezeka
nguvu. Samia alipofika
Zanzibar kumtambulisha Dk.
Magufuli baada ya kuteuliwa
Dodoma, aliona mapokezi
yalivyokuwa. Hakuna
kilichobadilika.
Hata leo hali ndiyo
i m e k u wa n g u m u z a i d i .
Kwa hivyo basi, ninaamini
haitakuwa rahisi kwake
kupenyeza chembe ya
imani kwenye nyoyo za
Wazanzibari, kuwashawishi
wavoti kwa ajili ya Dk.
Magufuli na CCM

19
Na Mwandishi Wetu

limu ni maarifa
anayopata mtu ambayo
kwayo, humuwezesha
kuvitazama na kuvijua vitu
kwa uhalisia wake. Elimu
ndiyo imekuwa nyenzo
pekee ambayo athari yake
inaonekana katika nyanja
zote za kimaisha; kiuchumi,
kijamii, kisiasa, kiteknolojia
na nyingine nyingi.
Maendeleo yanayotajwa na
kuonekanwa leo, msingi
wake mkuu ni elimu. Ndiyo
maana Allah (swt), kitu cha
mwanzo kabisa kumpa
Adam (as) ni elimu. [Quran: 02:31]. Vile vile, mtume
Muhammad (saw) wakati
anapewa wahyi, aliambiwa
soma. [Qur-an: 96:01].
Kwa mujibu wa ayah
hizo mbili, tunapata picha
k wa m b a e l i m u n i k i t u
muhimu kuliko vitu vingine
vyote. Elimu humtofautisha
kati ya mwenye nayo na
asiyekuwa nayo. Wawili
hawa, kamwe hawawezi
kufanana. Allah Mtukufu
ameuliza swali ndani ya
Qur-an, kwamba; Sema: Ati
watakuwa sawa wale wanao
jua na wale wasio jua? [Quran: 39:09].
Uhalisia unakataa
kwamba, anayejua na
asiyejua watakuwa sawa.
Ndiyo maana hata Malaika
walipoulizwa majina ya vitu
walisemaje?, Wakasema:
S u b h a n a k a , We we
umetakasika! Hatuna ujuzi
isipokuwa kwa uliyo tufunza
Wewe. Hakika Wewe ndiye
Mjuzi Mwenye hikima [
Qur-an 02:32]. Lakini Adam
(as), kwa kuwa alishapewa
elimu ya vile vitu, kwake
jawabu lilikuwa jepesi pale
alipotakiwa kutaja majina ya
hivyo vitu.
Wanadamu kwa utashi
wao wamezigawa elimu
katika makundi mawili
makuu, ambayo ni elimu ya
dini na elimu ya mazingira/
muongozo. Nadiriki
kusema hivyo kwa sababu,
Mtume Muhammad (saw)
alipoamrishwa kusoma,
hakuambiwa asome dini
au elimu ya mazingira, bali
aliambiwa soma kwa jina la
Mola wako. Haya makundi
mawili tuliyoyatengeneza
sisi, ni kitu kimoja. Ni
k a m a wa l e wa n a o s e m a
tusichanganye siasa na dini!
Kwa kutambua hilo, nami
nimeipa makala hii anuani,
Elimu Zetu Zinatusaidiaje,
kwa maana ya elimu
zote mbili. Kwa kiwango
kikubwa kabisa elimu hizi
mbili kama tulivyozigawa
sisi, zinaishi maisha
ya kutegemeana. Lakini
pamoja na kutegemeana
huko, moja ina umuhimu
zaidi kuliko nyingine, nayo
ni elimu ya muongozo. Elimu
ya kumjua Allah Mtukufu ni
ya muhimu zaidi kwa kuwa
ndiyo inayoweka nidhamu
ya namna mwenye elimu
inayoitwa ya mazingira,
aweze kuishi kwa maelekezo

MAKALA

AN-NUUR

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Elimu zetu zinatusaidiaje?

Baadhi ya wanafunzi Waislamu wa shule za msingi Wilaya ya Temeke waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya
msingi, wakiwa katika dua maalumu iliyoandaliwa na Baraza la Wazee wa Buza, iliyoongozwa na kusimamiwa
na Mzee Mikidadi Khalfan na kufanyika Masjid Lillah jijini Dar es Salaam mwisho wa wiki iliyopita.
yake Allah (swt).
Elimu hii ya muongozo
ni kama tumbo/fuko la
uzazi (womb), ambalo
humtengenezea mtoto
mazingira sadifu kwa
kuruhusu maingiliano ya
kimfumo ambayo hayana
athari kwa mtoto. Vile vile,
tumbo hili la uzazi hufanya
kazi ya kuzuia muingiliano
ambao una madhara kwa
kiumbe (mtoto). Kwa sura
hii, unaweza kuona ni jinsi
gani elimu ya muongozo
i l i v y o k u wa n a n g u v u ,
ukilinganisha na elimu ya
mazingira.
Kwa upande mwingine,
elimu ya mazingira nayo
ina mchango mkubwa sana
endapo itatumiwa vema,
ikiwa chini ya ulinzi wa
elimu ya dini. Masuala
yote yahusuyo teknolojia
na mengine mengi, ni zao
la elimu hii inayoitwa ya
mazingira. Lakini pia,
ifahamike kwamba,
ugunduzi wa hizi teknolojia
tunazojivunia leo, ni matokeo
ya tafiti mbali mbali za
k i s a ya n s i z i l i z o f a n y wa
kwa kutumia vitabu vya
elimu ya dini, hususan
Q u r - a n . Wa l i c h o f a n y a
watafiti ni kuoanisha yale
yaliyoandikwa kwenye Quran na kuyaingiza kwenye
utendaji kwa majina yao.
Tutaona kwa kina kwenye
makala zingine inshaallah,
m i f a n o h a i ya m a m b o
ambayo tunayaita elimu
ya mazingira, kumbe yapo
ndani ya Qur-an.
Hata hivyo, pamoja na
ukweli kwamba hawafanani
wanaojua na wasiojua, wenye
elimu na wasio na elimu
kuna nukta ya msingi hapa
ningependa tuiangalie kwa
makini sana. Mwenye kujua
anayekusudiwa hapa, ni yule
ambaye amelijua jambo na
akafuatisha kwa vitendo
kwa kukatazika na kuamrika
(kutekeleza maamrisho).
Elimu haishii kujua tu, bali
utendaji ndio utakaotoa
tafsiri sahihi kwamba wewe

una elimu na ujuzi kadhaa wa


kadhaa. Matumizi ya elimu
ya mtu ndiyo yanayoweza
kumtofautisha na mwingine
asiyekuwa na elimu.
H e b u t u a n g a l i e k wa
uchache umuhimu wa elimu
katika jamii na madhara ya
kutokuwa/kutoitumia vema
elimu. Kama tulivyosema
hapo awali kwamba, elimu
ni ile ambayo humuwezesha
mtu kuvijua/kuvitizama
vitu kwa uhalisia wake.
Ikiwa ukweli ndio huo,
basi mwenye elimu husika
ataweza kufanya/kutenda
jambo kwa uadilifu kwa
kutoa tafsiri sahihi kutokana
na weledi aliokuwa nao
kwenye taaluma aliyonayo.
Kinyume chake, ni ufisadi,
uwongo, ubadhirifu, dhulma,
kurubuniwa, rushwa,
upotoshaji na mengine
yenye kufanana na hayo.
Faida ya elimu inapatikana
katika maeneo mbali mbali,
lakini kwa uchache tuangalie
zifuatazo:
Nyenzo Kuu ya Kufikia
Lengo:
Kama Waislamu, bila
shaka tunatambua vema
lengo la kuumbwa kwetu,
nalo ni kumuabudu Allah
(swt). Kama tulivyoona hapo
awali kwamba, kitu cha
mwanzo kupewa Adam (as)
na Mtume wetu Muhammad
(saw) ni elimu. Lengo lao na
letu ni moja tu, kumuabudu
Allah Mtukufu. Hivyo basi,
namna pekee na rahisi kabisa
ya kufikia ndoto tulizonazo,
lengo la kuumbwa kwetu na
malengo mengine, ni kwa
kupitia ELIMU. Elimu zote
mbili zina nafasi kubwa mno
katika kujua halali na haramu
n a k u we z a k u v i e p u k a .
Elimu ya mazingira kwa
mfano, inasaidia kujua
aina mbali mbali za vijenzi
vilivyotumika kutengeneza
vyakula tofauti tofauti. Hii
huwapa fursa Maulamaa
wetu kuweza kutolea fataawa
mbali mbali kwa hoja na
dalili kadha wa kadha.
Uadilifu: Aghalabu, watu

wenye elimu hususan ya


muongozo hufanya mambo
kwa uadilifu tofauti na
wale wasiokuwa na elimu.
Watu wasiokuwa na elimu
wanayo nafasi kubwa mno
ya kuleta tafsiri za kupotosha.
Mathalani, usawa na uadilifu
vinaweza kutumiwa kwa
moja kuchukua nafasi ya
kingine. Si lazima kila
mwenye kufanya jambo kwa
usawa anakuwa amefanya
uadilifu, lakini mwenye
kufanya uadilifu anakuwa
amefanya vyote viwili kwa
wakati mmoja, kwa maana ya
usawa na uadilifu. Kufanya
uadilifu, kunategemea na
uelewa (elimu) katika hilo
unalofanya.
Umakini Katika Kufanya
Maamuzi: Weledi wa mtu
h u w e z a k u p i m wa k wa
namna anavyopokea mambo
na kuyatolea maamuzi. Mtu
mweledi, mwenye kuitendea
ve m a e l i m u ya k e h a n a
kawaida ya kukurupuka.
Kwa hali hiyo, maamuzi
yake yatakuwa yana asilimia
kubwa ya ufanisi na usahihi.
Mtu wa namna hii haoni
haya kusema sijui kwa jambo
ambalo halijui, tofauti na
mjinga ambaye hujitutumua
kujibu kitu asichokijua.
Elimu ni Maisha: Nyenzo
kuu ambayo inatumiwa leo hii
katika kufikia malengo mbali
mbali ni elimu. Mipango
mizuri, utendaji mzuri yote
yanatokana na matumizi
sahihi ya elimu. Ndio kama
a l i v y o s e m a m wa n d i s h i
m m o j a k wa m b a , e l i m u
siyo maandalizi ya maisha,
bali ndiyo maisha haswaa.
[ John Dewey, 1859-1952,
philosopher, psychologist,
education reformer].
Elimu humjengea mtu
uwezo wa kufikiri zaidi na
hivyo kuweza kugundua
mambo mengi ambayo
humpatia wepesi katika
shughuli zake mbali mbali
za kila siku. Maendeleo
yote tunayoyaona leo hii, ni
matokeo ya elimu mbali mbali
walizosoma wanadamu.
Miundo mbinu mizuri ya

barabara, vyombo vya usafiri,


mawasiliano na mengine
mengi tunayofurahia, hii yote
ni elimu.
Kuwa na Msimamo:
Watu wenye elimu, ndio
ambao wanakuwa na
misimamo kwenye imani
zao, kwenye mambo mbali
mbali ya kijamii. Ni kwa
sababu wanatambua vema
wanachokisimamia, hivyo
hawatetereki kwa lolote kwa
kule kutambua pande zote
za shilingi. Wanafahamu
madhara ya kufanya na
kutofanya jambo kadhaa.
We n ye e l i m u h a wa i s h i
kwa dhana, bali wanatafiti
kwanza hakika ya jambo
kama lina tija au vinginevyo.
Huepusha Migogoro
Isiyokuwa na Sababu za
Msingi: Migogoro mingi
husababishwa na kutokuwa
na elimu. Namna nzuri ya
kusuluhisha, pia ni jambo
ambalo linahitaji elimu. Ndio
maana kuna vituo maalum
vya mambo ya ushauri
nasaha kwa kujua nafasi ya
elimu.
Kushinda Ushirikina: Watu
wengi ambao hujihusisha na
mambo ya ushirikina ni wale
wasio na elimu. Angalia,
kwa mfano mauaji ya albino,
mauaji ya vikongwe hususan
wenye macho mekundu
n.k. Wanafanya haya kwa
kutumiwa au wenyewe,
wakiamini wanaweza kupata
wanachokitaka kama vile
mali na mengineyo. Elimu
h u s u s a n ya m u o n g o z o
ndiyo yenye nafasi kubwa
ya kumuepusha mtu na
mambo machafu kama haya
ya ushirikina. Allah Mtukufu
ameahidi kusamehe dhambi
zingine zote zisizokuwa
ushirikina kwa amtakaye.
E l i m u H u m u we z e s h a
Mtu Kwenda na Wakati.
Mabadiliko ya kiteknolojia
yanakwenda kwa kasi
ya a j a b u . We n ye e l i m u
ndiyo wanaonufaika na
mabadiliko haya, na ndio
wanaoyachangamkia
kutokana na kuwepesisha
baadhi ya kazi. Matumizi
ya internet kwa mfano,
ya n a wa n u f a i s h a we n ye
elimu peke yao. Namna rahisi
na nafuu kabisa ya kusoma
siku hizi ni kupitia mitandao.

AN-NUUR

20

MAKALA

20

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

AN-NUUR
(25) MWENYE UWEZO AHIJI KILA MIAKA MITANO

DHULQAAD
1436,
IJUMAA
SEPTEMBA
11-17,
2015
Kwa
muislamu
Hijja
ni wajib
mara moja
katika
umri wake isipokuwa aliyepewa afya njema
na mali. Huyu ananyimwa Rehma za Allah
akipitisha miaka mitano bila kurudia Hijja.
Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni
Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300.
Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma
nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania
Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.
Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010.

Bado Serikali ina hamu kuwa na Ponda


Na Bakari Mwakangwale

SERIKALI inaonekana
kuelemewa na hoja za
upande wa utetezi katika
kesi ya Sheikh Ponda Issa
Ponda, baada ya kukwama

kuwasilisha hoja zake,


katika kesi inayoendelea
Mjini Morogoro, ili
kutolewa hukumu.
SERIKALI inaonekana
kubanwa mbavu katika
kesi inayomkabili Sheikh

Ponda Issa Ponda, baada ya


kushindwa kuwasilisha hoja
zake katika Mahakama ya
Mjini Morogoro, kwa ajili ya
kutolewa hukumu.
Hali hiyo imejidhihirisha
Ijumaa ya wiki iliyopita,

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto) akiteta jambo na Wakili wake Juma Nassoro/

Wapalestina wataka bendera yao ipeperushwe UN


W A P A L E S T I N A
wamewasilisha rasmi
mapendekezo yao kwa
Umoja wa Mataifa (UN)
wa k i t a k a b e n d e r a ya o
ipeperushwe katika makao
makuu ya umoja huo jijini
New York, Marekani.
Makao makuu ya Kanisa
Katoliki duniani, Vatican pia
wamewasilisha pendekezo
kama hilo.
Va t i c a n n a Pa l e s t i n a
zinatambuliwa kama
wanachama watazamaji
wa UN, lakini Palestina
inapigania kutambuliwa
rasmi kama nchi huru
yenye mamlaka kamili ya
kujitawala.
Pendekezo la Palestina la
kutaka bendera yake ipepee
katika makao makuu ya UN
limeungwa mkono na nchi
21 zikiwemo nchi kadhaa za
Kiarabu na Kiafrika.

Viongozi wa dunia
wanatarajiwa kukutana
katika kikao cha kila mwaka
cha Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa kuanzia mwezi
ujao na iwapo pendekezo
la Palestina likapigiwa

kura kabla ya mkutano huo


na likipitishwa, bendera
ya Palestina itakuwa kati
ya nyingine 193 za nchi
wanachama wa UN kufikia
mwishoni mwa Septemba
mwaka huu. (irib).

BENDERA ya Taifa la Palestina

baada ya Julai 7, 2015,


Mahakama ya Mjini
Morogoro, kuamuru pande
mbili, upande wa Jamhuri
n a u p a n d e wa u t e t e z i
kuwasilisha hoja zao ndani
ya siku 21, yaani hoja za
utetezi na hoja za upande wa
Jamuhuri (Serikali).
Kwa mujibu wa Wakili
wa S h e i k h P o n d a , B w .
Juma Nassoro, ameeleza
kuwa siku hiyo ya Ijumaa
(Septemba, 4, 2015) kesi hiyo
inayomuweka mahabusu
mteja wake kwa mwaka wa
pili sasa, ilikuwa ipangiwe
tarehe ya hukumu, jambo
ambalo limekwamishwa na
upande wa Jamhuri.
Alisema, hali hiyo
imesababishwa na upande
wa mashitaka (Serikali ya
J a m h u r i ya M u u n g a n o
wa Tanzania) kushindwa
kuwasilisha hoja zao kwa
maandishi kama ambavyo
Mahakama inayosikiliza
kesi hiyo Morogoro,
ilivyoziamuru pande mbili.
Akifafanua zaidi Wakili
Nassoro, alisema Julai 7,
2015 baada ya wao (upande
wa utetezi) kukamilisha
kutoa ushahidi, Mahakama
iliamuru kuwa pande zote
mbili wapeleka hoja za
majumuisho ya kesi ndani
ya siku 21, kuanzia siku hiyo,
ambazo zilikoma Agosti 28,
2015.
Alisema, baada ya hapo
hatua iliyokuwa inafuatia
ni kesi kupangiwa Tarehe
ya hukumu, kwa matarajio
kwamba, kila upande
utakuwa umejumuisha hoja
zao (Final submissions) kama
Mahakama ilivyoamuru
Julai, 7.
Sisi tuliwasilisha
majumuisho yetu ndani ya
siku 21, kabla ya Agosti
28, 2015, kama Mahakama
ilivyo amuru Julai 7,
tukitegemea pia upande
wa Jamhuri (Serikali)
nao wangewasilisha kwa
muda huo au kabla, lakini
upande wa Jamhuri wao
hawakufanya hivyo, badala
yake leo (Ijumaa iliyopita)
wameomba waongezewe
muda zaidi. Amesema
Wakili Nassoro.
Kufuatia hali hiyo,
upande wa utetezi uliiambia
Mahakama kuwa baada
ya S e r i k a l i k u s h i n d wa
kuwasilisha hoja zao kwa
maandishi kwa muda wote

huo wa wiki tatu, hawana


nafasi tena ya kupeleka
maelezo yao.
Wakili Nassoro, alisema
hawana nafasi hiyo kwa
sababu utaratibu haukuwa
wao (upande wa utetezi)
wapeleke hoja kisha wao
(Serikali) wajibu hoja bali
amri ilikuwa ni pande zote
wapeleke hoja zao kwa
m a a n d i s h i k wa wa k a t i
mmoja na hapakutakiwa
majibu yoyote.
Kwa manaa hiyo kama
wataruhusiwa, maana yake
ni kwamba wao (Serikali)
watakuwa wanajibu hoja
zetu za upande wa utetezi,
kwa maana hiyo sisi
hatutokuwa na nafasi ya
kujibu tena.
Mahakama, baada ya
malumbano ya kisheria kwa
pande hizo mbili (Serikali na
utetezi) iliamua kuahirisha
kesi kwa mara nyingine
mpaka Septemba 18, 2015,
ili iweze kutoa uamuzi
iwapo upande wa mashitaka
(Serikali) wafaili maelezo yao
au Mahakama itoe hukumu.
Wa k i l i N a s s o r o ,
alilalamikia mwenendo
huo wa Serikali na kusema
kwamba, inaonekana wazi
kuwa upande wa mashitaka
wanakusudia kuchelewesha
hukumu hiyo kwa maslahi
yao kwani akadai inaonyesha
hawataki kuona hukumu ya
kesi hiyo ikisomwa kwa
sababu wanazozijua wao.
Hawakuwa na sababu
yoyote ya msingi ya
kutokuwasilisha hoja zao
ndani ya muda uliowekwa
na Mahakama na badala
yake wameamu kuchagua
kutokuwasilisha ili waweze
kuongezewa muda jambo
ambalo linafanya hukumu ya
kesi kuchelewa ili hali Sheikh
Ponda, yupo mahabusu
kwa miaka miwili sasa bila
sababu za msingi. Alisema
Wakili Nassoro.
Hivi sasa kesi hiyo
ipo katika mchakato wa
kusubiri hukumu, baada
ya Mahakama kusikiliza
mashahidi wa pande zote
mbili ambapo upande
wa Jamuhuri (Serikali)
ulisimamisha mashahidi tisa,
wakati upande wa utetezi
ulipeleka mashahidi wawili
tu.
Kadhia ya Shkh Ponda,
i m e k u wa n a m l o l o n g o
mrefu wa kisheria, ambapo
pamoja na kwamba hadi sasa
hajahukumiwa, lakini yupo
ndani kwa miaka miwili
sasa, kutokana na dhamana
yake kuzuiliwa na DPP.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

También podría gustarte

  • Press Realse 28
    Press Realse 28
    Documento4 páginas
    Press Realse 28
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1262
    Annuur 1262
    Documento20 páginas
    Annuur 1262
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1264
    Annuur 1264
    Documento20 páginas
    Annuur 1264
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1232 PDF
    Annuur 1232 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1232 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Documento15 páginas
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1231 PDF
    Annuur 1231 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1231 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Documento15 páginas
    HOTUBA YA BAJETI OFISI YA RAIS Final
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1225
    Annuur 1225
    Documento20 páginas
    Annuur 1225
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1217
    Annuur 1217
    Documento20 páginas
    Annuur 1217
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1229 PDF
    Annuur 1229 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1229 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Documento20 páginas
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • ANNUUR 1228d
    ANNUUR 1228d
    Documento20 páginas
    ANNUUR 1228d
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1230 PDF
    Annuur 1230 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1230 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1226 PDF
    Annuur 1226 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1226 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1227 PDF
    Annuur 1227 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1227 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1223
    Annuur 1223
    Documento20 páginas
    Annuur 1223
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1224
    Annuur 1224
    Documento20 páginas
    Annuur 1224
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1219
    Annuur 1219
    Documento20 páginas
    Annuur 1219
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Press Release - Muungano Na Mazingira
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Documento4 páginas
    Press Release - Muungano Na Mazingira
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1215 PDF
    Annuur 1215 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1215 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    100% (1)
  • Annuur 1218 PDF
    Annuur 1218 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1218 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1220
    Annuur 1220
    Documento20 páginas
    Annuur 1220
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • ANNUUR 1216d
    ANNUUR 1216d
    Documento20 páginas
    ANNUUR 1216d
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Documento27 páginas
    Hotuba Ya Maalim Seif - January 9 2016
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1210a
    Annuur 1210a
    Documento20 páginas
    Annuur 1210a
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1214
    Annuur 1214
    Documento20 páginas
    Annuur 1214
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Karume Shujaa
    Karume Shujaa
    Documento11 páginas
    Karume Shujaa
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1213 PDF
    Annuur 1213 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1213 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1212
    Annuur 1212
    Documento20 páginas
    Annuur 1212
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • ANNUUR 1209aaa
    ANNUUR 1209aaa
    Documento20 páginas
    ANNUUR 1209aaa
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones