Está en la página 1de 16

ISSN 0856 - 3861 Na.

1145 DHULHIJJA, IJUMAA , OKTOBA 3-9, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamu
www.annuurpapers.co.tz
UNAPOTAKA kupiga
kura fikiria, wazia na
pimia juu ya uzito wa
mchoro wako mmoja tu
wa kalamu utavyokuwa
na athari kwa nchi yako,
watu wako na watoto na
wajukuu wako.
Fumba macho, rudisha
nyuma f i kr a zako,
kumbuka wema na ihsani
za waliokuzunguka,
BI BLI A yas ema I r ak
ina pepo shujaa wa vita.
Walipigana na malaika
wa Mungu siku 21. Ilibidi
Malaika Mkuu Mikaeli
ashuke kuingilia kati. Rais
Bush asoma Biblia kabla ya
kutangaza vita.
Hivi sasa yaelekea Bush
na makamanda wake wa
kupigana vita dhidi ya ugaidi,
ndio Malaika Mkuu wa
kuangamiza Waislamu. (Uk. 6)
EID MUBARAK!
Mhariri na Watendaji
wa gazeti la AN-NUUR
wanawatakia Waislamu
wot e Ei d Mubarak
njema.
EID MUBARAK!!!
KAULI ya Mwenyekiti
wa Kamati ya Uandishi
wa Katiba, Mh. Andrew
Chenge, kuwa Mahakama
ya Kadhi hai st ahi l i
kuingia katika Rasimu
ya Katiba, ni sawa na
kuwaambia Waislamu
kuwa Qur an ni kitabu
kidogo.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu wa Jopo la
Masheikh na Wanazuoni
Ni Hapana kwa Rasimu
Asema kiongozi Baraza Kuu
Baraza la Idd Kichangani Jumapili
Shura ya Maimamu yajipanga
Masheikh wapo Golgotha
ni yale yale ya Constantino
Alisema kweli George W Bush ni Crusade
Haishangazi leo kwa akina Sheikh Farid
Eid Mubaraka Wajumbe...
Bunge la Katiba kutoka Zanzibar
Chenga twawala, lakini twafungwa
Kura yako Maangamizi Daima
uliokuwa nao pamoja
katika maisha yako na
uwafkirie khatma njema
ya muda mrefu.
Kumbuka jukumu lako
kwa Mwenyenzi Mungu
na fkiria kama hicho ni
kitendo cha mwisho cha
maisha yako ili ukitie
katika mizania nzuri ya
maamuzi yako.
(Uk. 7)
Amesema kweli Mataka
Quran imedhalilishwa
Kamati ya Chenge imedharau Waislamu
Wakristo wanaweza kuhukumiwa na Pilato
Na Bakari Mwakangwale
Inaendelea Uk. 2
wa Kiislamu Tanzania,
Sheikh Hamisi Mataka,
akiongea katika kipindi
cha Baraza l a Kati ba,
kinachorushwa na Radio
MUM ya Chuo Kikuu Cha
Waislamu Morogoro.
S h e i k h M a t a k a
akizungumzia kauli hiyo
ya Mh. Chenge, alisema
kwamba unapos e ma
Mahakama ya Kadhi
ni Mahakama ndogo
maana yake unawaambia
SHEIKH Farid Hadd. SHEIKH Ayman al-Zawahiri.
MWENYEKITI wa Bunge la Katiba, Samwel Sita (kushoto) na Mwenyekiti wa
Kamati ya uandishi Bunge la Katiba, Mtemi Andrew Chenge.
2
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.t E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofsi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
AWALI ya yote tuchukue
fursa hi i kuwat aki a
Wai sl amu wot e Ei d
Mubarak. Lakini pia
tuwatakie kila la kheri
mahujaji wetu waliopo
Makka, wakitekeleza
ibada ya Hija, ambayo ni
nguzo ya tano ya Uislamu.
Idd el Hajj ni sikukuu
ya Ki i sl amu ambayo
hus her ehekewa ki l a
mwaka katika siku ya
kumi ya mwezi wa Dhul
Hijjah, mwezi ambao ni
wa Hajj.
Kwa Waislamu sikukuu
hii hujulikana zaidi kama
I dd- al - Adhha, yaani
si kukuu ya kuchi nj a
au Idd-al-Kabir, yaani
sikukuu kubwa.
Idd Hajj husheherekewa
kama kumbukumbu ya
sadaka ya I brahi mu,
ambaye alipewa mtihani
na Mwenyezi Mungu
na kuamriwa kumchinja
mwanaye kipenzi Ismail.
Mti hani huu ul i l enga
kupima imani ya Nabii
Ibrahi m na mwanaye
I smai l , ambaye naye
Mwenyezi Mungu alimpa
Unabii.
Nabii Ibrahim aliridhia
a mr i ya Al l a h wa
kumchinja mwanaye, naye
Ismail akaridhia baba yake
kutekeleza maamrisho
aliyopewa na Mola wake.
Lakini wakati Ibrahim
anaanza kutekeleza amri
hiyo, alisikia sauti ya
takbira.
Mwe nye zi Mungu
alishashuhudia utii wa
waja wake hawa, Malaika
Jibril akamzuia Ibrahim
asimchinje mwanaye na
akampatia kondoo kutoka
kwa Allah (sw) amchinje
na kuwa sadaka badala ya
mwanaye.
Kwa kisa hiki, kimekuwa
ni funzo kubwa la utii
kwa Allah (sw) na ibada
kubwa kwa Wai sl am.
Hapo ndipo lililozaliwa
somo la kuchinja katika
Hija na kwenye sikukuu
ya Eid el Haji.
Hi k ma y a k e n i
kujikurubisha kwa Allah
Eid Mubarak
(SW) kama anavyosema
katika kauli yake: Basi
swali na uchinje kwa ajili ya
Mola wako. (Al-Kawthar:
2)
Leo t uchukue fursa
hi i kukumbushana na
kuelekezana Waislamu
j uu ya umuhi mu wa
kutekel ezwa i bada ya
kuchinj a katika Eid el
Udhhiya.
Kama tunavyofahamu,
sherehe ya Idd huanza na
swala ya Eid Msikitini au
eneo la wazi (uwanjani).
Baada tu ya swal a ya
Ei d kubwa, Wai sl amu
wenye uwezo wanapaswa
kuchi nj a mnyama wa
sadaka siku hiyo.
Mafundisho yanasisitiza
kwamba kuchinja kondoo
ni bor a zai di l aki ni
aki kos ekana, mbuzi ,
ng' ombe ngami a na
mnyama mwingine halali
kuliwa anaweza kufaa
katika kutekeleza ibada hii.
Tusisahau kuwa sehemu
ya nyama ya sadaka hii
huga wi wa ma s i ki ni
wasio na uwezo, majirani
na marafiki na nyingine
hutumiwa katika karamu
ya familia.
Kuchinj a ni moj a ya
ibada za Kiislamu ambayo
inatukumbusha Tawhid ya
Allah (SW) na baraka zake
kwetu, pamoja na kutupa
mafunzo ya utiifu wa baba
yetu Ibrahim kwa Mola
wake na kumpwekesha
Allah. Hivyo ibada ya
kuchi nj a ni muhi mu
sana kwa Muislamu na
inatupasa tuizingatie kwa
makini na kuitekeleza.
Nyama zao hazimfkii
Allah wala damu zao,
lakini unamfikia uchaji
Allah wenu. Namna hivi
tumewadhalilisha kwenu
i l i mumt ukuze Al l ah
kwa al i vyokuongoeni .
Na wabashirie wafanyao
mema. (Al-Hajj: 37).
Na kafara ni kuchinja
kwa kujikurubisha kwa
Allah (SW). Kuihuisha
Sunnah moj awapo ya
Tawhi d, wakati Al l ah
alipompa wahyi Ibrahim
(as) amchinje mwanawe
Ismail. Kisha Allah (SW)
akampa fdia ya kondoo,
akamchinja badala yake.
Al l ah ( SW) anasema:
Basi tukamtolea fidia
kwa dhabihu mtukufu
(Aswaafaat: 107).
Mu i s l a m k u we z a
kuwalisha nyama familia
yake pamoja Na jamaa zake
siku ya Eid na kueneza
rahma mi ongoni mwa
masikini na mafakiri.
Kutoa shukurani kwa
Allah (SW) kutujaalia kuwa
na wanyama wafugwao
k a ma a n a v y o s e ma :
Na ngamia wa sadaka
tumekufanyieni kuwa ni
kudhihirisha matukuzo
kwa Al l ah; kwa hao
mna kheri nyingi. Basi
litajeni jina la Allah juu
yao wanaposimama kwa
safu. Na waangukapo
ubavu kuleni katika hao
na walisheni waliokinai
n a wa n a o l a z i mi k a
kuomba. Ndi o kama
hivi tumewafanya hawa
wanyama dhalili kwenu ili
mpate kushukuru.
Nyama zao hazimfkii
Allah wala damu zao,
lakini unamfikia uchaji
Allah wenu. Namna hii
tumewadhalilisha kwenu
i l i mumt ukuze Al l ah
kwa al i vyokuongoeni .
Na wabashirie wafanyao
mema. (Al-Hajj: 36-37).
Hata hivyo tuwe na
tahadhari kuwa wanyama
wa n a o p e n d e k e z wa
kuchinjwa, lazima wawe
wanono na wenye afya,
wasiokuwa na maradhi
au kilema au kasoro za
kumfanya awe duni.
N i v y e m a p i a
t ukakumbus hana na
m a p e m a k wa m b a
kuchinja ni asubuhi ya
siku ya Idd baada ya swala.
Hairuhusiwi kuchinja kabla
ya swala kama alivyosema
Mt ume ( Saw) Kut oka
kwa Anas (ra) kwamba,
Mtume (Saw) amesema,
Atakayechinja kabla ya
swala atakuwa amejichinjia
kwa ajili yake mwenyewe.
Na Atakayechinja baada
ya swala atakamilisha
kafara (kichinjo) yake na
atapata (atatekeleza) Sunna
ya Waislam (Bukhari na
Muslim).
I n a p e n d e k e z w a
Mui s l a mu k uc hi nj a
mwe n y e we , l a k i n i
a k i mwa k i l i s h a mt u
k u m c h i n j i a p i a
i naruhusi wa. Hakuna
hitilafu katika jambo hili
baina ya Maulamaa.
Mchinj aj i anatakiwa
kuigawa nyama aliyochinja
kat i ka s ehemu t at u.
S e he mu ya k wa nz a
watatumia familia, sehemu
ya pili itatolewa sadaka na
sehemu ya tatu itagawiwa
marafiki, maj irani n.k.
kama anavyosema Allah
(Sw), Ili washuhudie
manufaa yao na walitaje
jina la Allah katika siku
maalumu juu ya nyama hao
aliowaruzuku. Basi kuleni
katika hao na mlisheni
mwenye shida aliye fakiri
(Al-Hajj: 28).
Pia inaruhusiwa pia
kui gawa nyama yot e
sadaka. Inaruhusiwa pia
kubakisha sehemu.
Ai dh a t un a pe n da
kuwakumbusha Waislamu
na kuwapa nasaha ya
kufunga siku ya Arafah ya
Dhul-Hijjah 1435 Inshaa-
Allaah. Fadhila zake ni
kufutiwa madhambi ya
mi aka mi wi l i ; mwaka
uliopita na unaofuatia.
Pi a t unakumbus ha
kuwa katika siku ya Eid
kubwa, ni vyema ki l a
Muislamu akafunga kwa
muda kuanzia asubuhi
hadi baada ya swal a.
Inapomaliza swala ya Eid
aendelee kula na kunywa
na kusherehekea sikukuu
yake. Itakuwa dhambi
kuendelea kufunga baada
ya swala.
Eid Mubarak
Amesema kweli Mataka
Inatoka Uk. 1
Waislamu kuwa Quran
yao ni kitabu kidogo jambo
ambalo si sahihi.
Sheikh Mataka alisema
Mahakama ya Kadhi sio
Mahakama ndogo kama
anavyodhani Mh. Chenge,
pengine na kamati yake
kwani inapaswa ichukuliwe
kama Mahakama maalumu
na kwa mambo maalum ya
kiimani.
Mahakama ya Kadhi
inahukumu kwa mujibu
wa Qur an na Sunna, hivyo
unaposema Mahakama
ya Kadhi ni ndogo na
Katiba haishughuliki na
Mahakama ndogo huku
ni kuwadharau Waislamu
lakini ndani yake pia kuna
namna ya kuidharau zaidi
Qur an. Alisema Sheikh
Mataka.
Al i sema, maj i bu ya
Mh. Chenge, juu ya suala
hilo ni jibu la kiufundi
kwa Wai slamu, kwani
mtu akitaka kulikwepa
jambo kiufundi atatumia
ufundi katika jibu lake
akitegemea kueleweka
zaidi, lakini kinyume chake
afahamu kuwa kwa jibu
hilo ameidharau Qur an.
Ki l a s i ku j i bu l a
kiufundi haliwi ni jibu
halisi, bali ni jibu la kumtoa
mtu katika mtengo fulani
alionasa, maelezo ya Mh.
Chenge, si maelezo sahihi
kwa umma wa Kiislamu.
Alisema Sheikh Mataka.
Alisema, hoja ya Mh.
Chenge, haina mantiki
kwani ni hoja dhaifu katika
jambo zito kama hili linalo
gusa imani ya moja ya
kundi kubwa katika umma
wa Watanzania, ambao
nao ni miongoni mwa
watumiaji wa katiba hiyo.
Shkh. Mataka, alisema
kwa kuwa sual a hi l o
ni hitajio la kiimani na
kiibada hivyo Waislamu
wa t a e nde l e a kui da i
Mahakama ya Kadhi na
ana imani kwamba siku
moja watafanikiwa kama
ilivyo Kenya, Uganda na
nchi nyingine jirani na
Tanzania zenye Mahakama
za Kadhi zinazotambulika
Kikatiba.
Mataka alisema huko
nyuma wakati Waislamu
wa na da i uwe po wa
Mahakama hiyo walielezwa
kuwa haiwezekani kwa
sababu Katiba iliyopo
hai i tambui , cha aj abu
akasema katika muda huu
wa kutengeneza Katiba
mpya zinakuj a sababu
na hoja zisizo na mantiki
tena kwa viongozi wenye
heshima.
Tanzani a i nget aka
kuangalia na kulimaliza
suala la Ukadhi ingeangalia
nchi jirani kwamba ni jambo
ambal o l i nawezekana
kuingizwa katika Katiba.
Mahakama ya Kadhi
imetajwa katika katiba ya
Kenya, na ibara ya nane
katika Katiba ya Uganda,
kwa ni ni wasi angal ea
mfano katika nchi hizo.
Alisema na kuhoji Sheikh
Mataka.
Kwa upande wake
akichangia katika kipindi
hicho, Bw. Magesa Japhet,
Inatoka Uk. 1
3
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Habari
Ni Hapana kwa Rasimu
WAISLAMU hawatokuwa na
kura ya NDIYO katika zoezi
la kuipigia kura Rasimu ya
Katiba iwapo maoni yao ya
uwepo wa Mahakama ya Kadhi
hayatoingizwa katika Katiba
mpya.
Mwishoni mwa wiki iliyopita,
Mwenyeki t i wa Kamat i ya
Uandishi ya Bunge la Katiba,
Mh. Endrew Chenge, aliwasilisha
Rasimu ya mwisho ya Katiba,
ambapo ilibainika kuwa maoni
ya Waislamu juu ya Mahakama
ya Kadhi hayajaingizwa katika
Katiba inayopendekezwa.
Rasimu hiyo ni ya mwisho
katika mtiririko wa kupatikana
Katiba mpya, ambapo katika
hatua zote za awali za Rasimu,
maoni ya Waislamu mengi,
likiwemo pia la Mahakama ya
Kadhi hayakuonekana.
Kwa muj i bu wa t arat i bu,
kinachosubiriwa sasa ni Rasimu
hiyo kurudi kwa wananchi kwa ajili
ya kupigiwa kura jambo ambalo
tayari Waislamu wameweka
msimamo wa kuikataa rasimu
hiyo kwa kupiga kura ya hapana.
Akizungumza na An nuur,
msemaji wa Jumuiya na Taasisi
za Kiislamu nchini, Sheikh Rajabu
Kati mba, al i sema kutokana
na maamuzi hayo ya Bunge
na kutiliwa mkazo na Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, Waislamu
hawatoiunga mkono rasimu hiyo
ya Katiba.
Kwa hili hatuna kura ya ndiyo,
tutakuwa na kura ya hapana na
hili linaanza kufanyiwa kazi katika
Baraza la Eid, (kesho kutwa)
tutawaeleza Waislamu msimamo
juu ya hatua hiyo ya Bunge na
Serikali yake, tutawaeleza maoni
yetu yamekataliwa na sisi tuikatae
Rasimu hiyo katika kupiga kura.
Alisema Katimba.
Alisema, nj ia na mikakati
iliyotumika kugomea Sensa ya
watu na makazi baada ya Serikali
kugoma kui ngi za ki pengel e
cha Dini ndizo zitakazotumika
kuwaeleza Waislamu kupiga kura
ya hapana.
Katimba alisema kuanzia sasa
Jumuiya na Tasisi za Kiislamu,
zinaratibu hotuba za Ibada ya
swala ya Ijumaa zitakazo kuwa
na uj umbe mmoj a, ambazo
zitasomwa mfululizo kila Ijumaa,
kati ka muda utakaopangwa
zikielezea kupuuzwa kwa maoni
ya Waislamu katika Katiba mpya.
Alisema, uzuri wa bahati kauli
na msimamo huo wa Bunge
Maalum na Serikali, umekuja
wakati Shura ya Maimamu, ikiwa
katika vikao na Maimamu kutoka
Mikoa mbalimbali nchini hivyo
moja ya maazimio waliyo ondoka
nayo (Maimamu) ni mikakati
kuhusu Waislamu kupiga kura
ya hapana.
Wajumbe kutoka Mikoa yote
iliyojumuishwa Kikanda kwa
Tanzania bara na Visiwani, kazi
itafanyika na ujumbe utafika
tutakutana nao mitaani katika
masanduku ya kura. Alisema
Shkh. Katimba.
Al i sema, kat i ka kupi nga
Rasimu hiyo ya Chenge, wataanza
kusambaza vipeperushi na vitabu
mbalimbali nchi nzima kama
ilivyokuwa katika sakata la Sensa
Na Bakari Mwakangwale
na kazi itakayo anza katika Baraza
hilo la Eid, ambalo litafanyika
siku ya Jumapili (kesho kutwa)
katika Msikiti wa Kichangani TIC
Magomeni jijini Dar es Salaam,
kuanzia majira ya saa nane mchana.
Kat i mba amesema, i ki wa
wajumbe katika kamati ya uongozi
wa Bunge hilo wamejiridhisha
kuwa madai ya Waislamu kuhusu
Mahakama ya Kadhi ni ya msingi,
kwa nini wasubiri mpaka Januari
mwakani.
Aki t oa t amko l a Seri kal i
Bungeni baada ya maoni ya
Waislamu kuhusu Mahakama
ya Kadhi kutokuwemo katika
Rasimu iliyowasilishwa na Mh.
Andrwe Chenge, Waziri Mkuu
Mzengo Pinda, alisema Januari
mwakani Sheria ya Kiislamu sura
ya 375 itafanyiwa marekebisho ili
kutambua uamuzi wa Mahakama
ya Kadhi, ikiwemo maeneo saba
yanayolalamikiwa na Waislamu.
Waziri Mkuu (Mh. Pinda)
akisema kuwa itaboreshwa hapo
baadae, anamaanisha kwamba
Mahakama ya Kadhi sio jambo
muhimu kwa mtazamo wao lakini
kwetu sisi Waislamu ni muhimu
sana lazima watambue hivyo
na ni muda mrefu Waislamu
wameonyesha umuhimu wa suala
hili lakini wanapuuzwa. Alisema.
Alisema, ukiyatafakari maelezo
ya Waziri Mkuu Pinda, na maelezo
ya Mh. Chenge, ni mael ezo
ambayo yanagongana na kuashiria
lengo ni kuwatoa Waislamu katika
msimamo wao au kuwafanya
daraja la kupitishia mambo ya
wengine.
Shkh. Katimba, alisema kwa
mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti
wa Kamati ya Uandi shi wa
Rasimu ya Katiba ya Bunge hilo
(Mh. Chenge) alieleza bayana
kwamba kila kitu kilicho muhimu
kimeingizwa katika Rasimu hiyo
ya Katiba.
Kwa hiyo Jumuiya na Tasisi
za Kiislamu tunaona kuwa hili ni
changa la macho, hamna chochote
watakacho kipata Waislamu,
kwani hizo zimekuwa ndio kauli
zao kwani walianza katika ilani
yao ya CCM ya uchaguzi waliahidi
hi vyo hi vyo l aki ni hakuna
utekelezaji, sasa sisi tunasema
msimamo wetu upo pale pale,
Hapana kwa Rasimu. Alisema.
Jumamosi ya wiki iliyopita,
Sheikh Hamid Jongo kutoka kundi
la 201, anaewakilisha dini ya
Kiislamu, aliomba mwongozo
akionyesha wasiwasi wake kwamba
huenda ubora wa Katiba mpya
ukawa mashakani endapo maoni
ya Waislamu kuhusu Mahakama
ya Kadhi hayatoingizwa katika
Katiba mpya.
Sisi tulileta marekebisho
yetu, Waislamu tunataka tujue
yataingizwa au hayaingizwi kama
hayaingizwi, basi (Waislamu)
tunao msimamo wetu ambao
pengine ule ubora wa katiba
inayopendekezwa utabomokea
hapa. Alisema Sheikh Jongo.
Amesema kweli Mataka
Inatoka Uk.2
aliwataka Wakristo wenzake
kutotaka jambo ambalo kwao
halipo wala dini yao haijaamuru
kuhukumiana kwa mujibu wa
Biblia.
Tusione kwa kuwa Waislamu
wanataka haki yao ya msingi
ambayo imo katika kitabu chao
(Qur an) na sisi ndio tuanze
kujipenyeza kudai kitu ambacho
hatunacho kiimani, kwa nini
isifke mahali tukaungana nao
kuitaka Serikali wapewe haki
yao. Alisema Bw. Japheti.
Bw. Japheti, aliyedai kuwa
amefanya utafti wa kina juu
ya suala hilo na kuona halina
tatizo kuingizwa katika Katiba
ya nchi, akaitaka Serikali
kuziruhusu Mahakama hizo
kikatiba na kuzigharamikia
hata kwa asilimia 75 tu, kama
sio kwa asilimi mia moja.
Al i sema, haoni sababu
kwa Ser i kal i kushi ndwa
kuzigharamikia Mahakama
hizo ikiwa ni huduma kwa
sehemu ya raia wake, ili hali
inatumia mabilioni ya pesa bila
sababu za msingi.
Alisema, kutokana na utafti
alioufanya, amebaini kuwa
tatizo watu wengi husasani wa
upande wa pili hawajaelimishwa
na endapo wataelimishwa vizuri
nini maana ya Mahakama ya
Kadhi, hukumu yake na mipaka
yake lingechukuliwa kuwa ni
jambo la kawaida na ni haki ya
Waislamu na hata uwepo wake
Kikatiba hakuathiri imani ya
watu wengine.
Aki zungumzi a kaul i ya
Askofu Mapunda, aliyedai
kuwa endapo Mahakama
ya Kadhi itaingizwa katika
Katiba basi, hata Wakristo nao
watahitaji pia Mahakama yao
ya Kikristo, alisema hakuna
sababu ya kufanya hivyo kwani
wao Wakristo Dini yao haina
amri ya kuhukumiana Kikristo.
Mimi kama Mkristo na
msomaj i mzuri wa Bi bl i a
nataka kuuthibitishia umma
unaonisikiliza kwamba katika
Biblia kunzia kitabu cha kwanza
kinachoitwa Mwanzo na cha
mwisho kinaitwa Ufunuo wa
Yohana hakuna mahala popote
ambapo sisi Wakristo katika
imani yetu tumelazimishwa na
Mungu ama panapozungumza
Wakristo wanatakiwa kuwa na
Mahakama zao. Alisema Bw.
Japheti.
Akifafanua Bw. Japheti,
alisema kwamba hata hukumu
ya Kristo (Yesu) pale msalabani
hakuhumiwa na Kanisa au
kwa sheria za Kikristo, bali
alihukumiwa na kina Pilato
(watawala) kwani alidai wakati
ule (mtawala) ndiye aliyekuwa
Jaji (mwamuzi).
K wa h i y o K r i s t o
h a k uh uk umi wa k a t i k a
Mahakama ya Ki kr i s t o,
ha kuna ma ha l a popot e
ambapo Wakristo wanatakiwa
wa h u k u mi we Ki k r i s t o
kama ambavyo Wai sl amu
wanaelekezwa katika Qur an
yao. Sisi (Wakristo) tunaweza
kabisa tukahukumiwa na hizi
Mahakama za Seriakali, wala
dini ya Kikristo haizumgumzi
c ho c ho t e vi pi Mkr i s t o
ahukumiwe Kikristo. Alisema
Bw. Japheti.
Kwa mana hiyo alisema,
uki soma kat i ka Mat hayo
utakuta inasema Tiini mamlaka
kwa kuwa hakuna mamlaka
iliyowekwa yenyewe mamlaka
zote zimewekwa na Mungu.
Kiongozi huyo (Askofu
Mapunda) nadhani alikuwa
anajaribu kujenga hoja ili hii
Mahakama ya Kadhi isiweze
kuingizwa katika Katiba, lakini
hakuna sababu yoyote ile ya
msingi ya kuzuia Mahakama
hiyo isiruhusiwe kikatiba ili
Waislamu wakahukumiana kwa
mujibu Quran yao inavyotaka.
Alisema.
Bw. Japheti, akitilia mkazo
kua Wakristo hawana lazima ya
kuhukumiana Kikristo, alitoa
changamoto kwa kiongozi
yoyote wa j uu wa Kanisa
hata kama ni Papa, ajitokeze
kumthibitishia kwa maandiko
kama Wakristo wanatakiwa
kuwa na Mahakama zao zilizo
amliwa na Mungu au Yesu kwa
ajili ya kuhukumiana Kikristo,
na endapo akijitokeza atakuwa
t ayari kuwa mj akazi wa
kiongozi huyo bila malipo kwa
maisha yake yote yaliyobaki.
Hili ni sawa na suala la
kuchi nj a, kwani wenzet u
kuchinja ni ibada lakini kwa
Mkristo nichinje nisichinje
hainiathiri, kwa nini tusimuachie
yule ambaye kuchinja kwake ni
ibada akafanya shughuli hiyo ili
kujenga umoja na mshikamano
wa Ki tai fa. Al i sema Bw.
Japheti.
4
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Habari/Tangazo
TAASISI ya Taqwa Orphans Trust
Tanzania imepokea hundi yenye
thamani ya dola za kimarekani
13,690 pamoja na nguo mpya
za watoto kutoka kwa wahisani
wao taasisi ya Qamer ya nchini
Canada, kwa ajili ya sikukuu ya
Idd el Hajj.
Msaada huo ulitolewa katika
hafa ya kuwakutanisha watoto hao
yatima na wahisani wao kutoka
nchini Canada, iliyofanyika katika
ukumbi wa Al-Hilal jijini Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita na umewalenga watoto
yatima wanaoishi majumbani
pamoja na walezi wao.
Mkurugenzi Mtendaj i wa
taasisi hiyo, Dk. Salha, wakati
wa kupokea msaada huo alisema
kuwa, jambo la kuwalea yatima
ni la kila mtu na linalompendeza
sana Mwenyezi Mungu, hivyo kila
Muislamu anatakiwa kujitahidi
kuchukua nafasi hiyo popote pale.
Qamer Foundation imechukua
dhamana ya kuwalea watoto 34
kati ya watoto 100 wanaolelewa
na taasisi ya Taqwa, ikitoa mahitaji
yao yote ya nyumbani, shule na
madrasa pia.
Akitoa maelezo ya taasisi hiyo
na shughuli zinazofanywa na
taasisi hiyo, Dk. Salha alisema kazi
yao kubwa ni kuhakikisha watoto
Taqwa watoa Eid Mubarak
kwa yatima Dar es Salaam
Na Azza Ally Ahmed
mwao pamoja na michango ya
wanachama na watu mbalimbali,
ambao wanasaidiana kuwalewa
watoto hao kwa mapenzi na
huruma ili na wao wajisikie wapo
na wenzao.
Aidha amewataka kina mama
na wafadhili kujitokeza zaidi
kuwafadhili watoto hao, hata kwa
kumlea mtoto moja au kupeleka
chochote anachojaaliwaa mtu
katika ofsi zao.
Alikumbusha kuwa watoto hao
wanawalea hali ya kuwa wako
katika familia zao na ndugu zao,
na sio katika vituo vya kuwalelea
watoto yatima.
Alisema wanachofanya ni
kuwapelekea misaada na mahitaji
muhimu inayohitajika katika
malezi yao pale wanapolelewa.
Naye mwakilishi na mwanzilishi
wa Qamer Foundation kutoka
nchi ni Canada, Ukht Bi l ki s
Abdulkadir, aliwataka Waislamu
kulitilia mkazo suala la kuwasaidia
na kuwalea watoto yatima na
kudai kuwa ni jambo la kila mtu
na sio kuachia taasisi au watu
fulani.
Alisema Waislamu, mtu moja
moja au vikundi ni vyema wakawa
na tabia ya kujiwekea malengo,
hata kwa kuchangishana shilingi
mia mia kwa kuwa hiyo mia
inaweza kufanya jambo kubwa
katika kuwasaidia yatima hao bila
ya mtoaji kujua.
wanapata chakula, wanawatafuta
wahisani ili kusaidiana kuwalea
watoto hao kuhakikisha wanapata
matibabu pamoja na mahitaji yao
muhimu ya shule.
Dk. Salha alisema pesa
wanazotoa kwa watoto hao
ni fedha zinazotoka mifukoni
JUMUIYA ya Ist i qama for
Devolopment ikishirikiana na
Zanzibar Children Fund (ZCF)
wiki hii kwa mara nyengine tena
wameendelea kutoa misaada
mbalimbali ya kijamii ikiwemo
fedha taslimu na masurufu
mengine, ikiwa ni kwa lengo
l a kuwasai di a wanaj ami i
kufanikisha maandalizi ya
kusherehekea sikukuu ya Iddi-
elhaji.
Kiongozi mkuu wa jumuiya
hi z o S he i k h Mo ha mme d
Suleiman Altiwaniy mapema
aliweza kuongoza hafa hiyo kwa
kuwakaribisha wageni waalikwa
ambao ni pamoja na maafisa
tawala, masheha, madiwani
kutoka Wilaya zote nne za kisiwa
cha Pemba, ujumbe kutoka ofsi
ya mufti, ujumbe kutoka ofisi
ya wakfu na mali ya amana,
mai mamu, wanachama wa
jumuiya ya Istiqama na wanajimii.
S h e i k h M o h a m m e d
amefahamisha kuwa misaada
wanayoendelea kutoa kwa jamii
ni kwa ajili ya kujenga ushirikiano
mapenzi mshikamano na umoja
miongoni mwao kama Mwenyezi
Mungu alivyoamrisha.
Mwenyezi Mungu ametutaka
tushikamane na tushirikiane,
hakika Waislamu wanapokaa
pamoja na kuacha tofauti zao,
umoj a wao na mshi kamano
Istiqama watoa misaada Pemba
Na Mwaandishi wetu wao huongezeka mara dufu pia
nakushukuruni kwa kukubali
kukaa pamoj a kwa mambo
yakusai di a na kunyanyua
Waislamu kisiwani Pemba.
Sheikh Mohammed.
Mapema akifungua hafa hiyo
mgeni rasmi Ndugu Ahmed
Khalid, ambaye ni Afsa Tawala
wa Wilaya ya Micheweni, alisema
wamefurahishwa mno wao kama
viongozi wa serikali kwa jinsi
ya mshikamano ambao ndugu
zao wa Istiqama wanauonesha
kwa jamii huku akikumbushia
jinsi walivyoweza kutoa msaada
kwa janga la moto lililowahi
k u wa k u mb a wa k a z i wa
Micheweni mwaka jana.
Alisema ihsani ya namna hiyo
ni ya kuigwa na taasisi nyengine
kisiwani Pemba hata zile zisokuwa
za kidini.
Tul i mpel ekea ri pot i i l e
Balozi Seif Ali Iddi ambaye ndie
aliyekuwa kiongozi wa kwanza
kututemblea mara baada ya janga
lile kututokea na alifurahishwa
mno na ripoti ile juu ya namna
taasisi hii ilivyojitolea pamoja
na wengine wote waliotusaidia
Alisema Ahmed
Aidha alisifu jitihada hizo na
kuwasihi kuendelea na moyo
wal i ounesha huku aki ahi di
mashirikiano pindi watakapo
hitaji msaada kwa serikali juu ya
shuhuli zao.
Zaidi ya shilingi milioni ishirini
zimetumika kwa msaada huo kwa
jamii.
BAADHI ya watoto yatima wanaohudumiwa na taasisi ya akinamama
ya Taqwa.
5
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Makala
Rasi mu i l i yot angazwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya
Uandishi wa Katiba, Andrew
Chenge, inatusuta na kuwafanya
wale wengine ambao hawataki
Muungano wowote kati ya
Tanganyika na Zanzibar wawe
na hoja juu yetu. Wanatwambia
kuwa tangu mwanzo walijua
pasingelikuwa na kheri yoyote
inayoweza kupatikana kupitia
mikono ya Chimwaga.
Sisi tujionao kuwa Waliberali
wa Muungano tumeshindwa.
Kushindwa kwetu, hata hivyo,
hakumaani shi ushi ndi kwa
wale wa siasa kali zinazoelemea
upande wa kul i a kwenye
Muungano, ambao sauti yao ndiyo
inayoakisika kwenye Rasimu hii
ambayo tayari imeshapagazwa
lakabu ya Rasimu ya Vijisenti.
Tumeshi ndwa Wal i beral i ,
ambao licha ya upinzani wetu kwa
mfumo uliopo wa Muungano,
tulitaka uendelee kubakia ukiwa
na mageuzi ya kimsingi. Lakini
hawakushi nda wahafi dhi na
ambao wanataka mfumo uliopo
ubakie na bali usonge mbele
zaidi kuelekea serikali moja
kama ilivyokuwa ndoto ya mmoja
wa waasisi wake, Mwalimu
Julius Nyerere. Hawakushinda
hata kama waliyoyataka ndiyo
yaliyomo kwenye Rasimu ya Tatu
na ambayo huenda ikapitishwa
Bungeni na yumkini ikapelekwa
kwa wananchi kwa ajili ya kura
ya maoni.
Kile ambacho Rasimu hii ya
Vijisenti imefanya ni kuuchora
mstari katikati ama wanaotaka
Muungano kwenye tafsiri yake
ya awali ambayo ni Tanganyika
kushika hatamu (Tanganyika
supremacy) au wale wasioutaka
kabisa Muungano huu, na ambao
wanaona jambo bora na la salama
ni ya mataifa haya mawili kwenda
njia mbalimbali na kukutana
kwenye ujirani na ushirikiano
mwengine wa kikanda.
Kwa maneno machache ni
kuwa sasa nguvu zilizopo kwenye
siasa za Muungano zimo kwenye
matapo mawili tu wale wenye
siasa kali za mrengo wa kushoto
kuelekea Muungano na wale
wenye siasa kali za mrengo
wa kulia kuelekea Muungano.
Sisi waliberali wa Muungano
tunapaswa sasa ama kuchagua
moj a kati ya makundi hayo
mawili au kujikubalisha kufa
na kuachana kabisa na siasa
za Muungano. Ingawa nal o
pia halimaanishi kwamba nchi
itakuwa salama. Panapokosekana
watu wanaopigania wastani wa
mambo, mambo yote huharibika.
Afdhalul-umuri ausatuhaa.
ubora wa mambo ni wastani wake,
ndivyo tunavyousiwa!
Rasimu ya Jaji Joseph Warioba
ilikuwa imesimama katikati baina
Rasimu ya 'vijisenti itakavyouvunja kabisa Muungano
Na Mohammed Ghassani
ya uliberali na mrengo wa kulia
panapohusika suala la Muungano.
Bado iliupa Muungano nafasi ya
juu kwenye kila jambo, lakini
pia ikapuruzia baadhi ya utashi
wa nchi washirika. Haikuwa ya
kiliberali moja kwa moja.
Kinyume chake ni kuwa Rasimu
ya Vijisenti imeelemea moja kwa
moja kwenye mrengo wa siasa kali
za kulia. Imechukuwa kila kitu
kwenye Muungano na haikuacha
lolote kwa nchi washirika. Na
hapo panaifanya Zanzibar kufa
dungu msooni, kwa kutumia
maneno ya Arham Ali Nabwa.
Inaambiwa mchezoni haimo na
ilokwishakula iziteme.
Mwandishi wa siku nyingi na
mwanasheria wa Zanzibar, Ally
Saleh, ambaye pia aliwahi kuwa
mjumbe wa tume iliyokusanya
na kuratibu maoni ya wananchi
juu ya katiba mpya (Tume ya
Warioba), anaandika hivi kwenye
waraka wake kwa wabunge wa
Zanzibar waliomo kwenye Bunge
Maalum la Katiba:
Si kweli, na si kweli kabisa,
kuwa Katiba inayopendekezwa
ina maslahi na Zanzibar. Haina,
hai na kat u, hai na abadan,
kamwe haina. Ni katiba ambayo
inatuweka pabaya na pagumu
zaidi na imeendelea kuyachukua
mamlaka ya Zanzibar na kuyatia
katika Muungano. Vipi Katiba
hi i i t akuwa na masl ahi na
sisi (ikiwa) . kuondosha au
kuukataa mfumo wa Shirikisho
ina maana (a) Zanzibar haiwezi
kuwa na hadhi na haki sawa
na Serikali ya Muungano, ( b)
Tumejibakisha pale pale Zanzibar
haina mshirika mwenziwe kwenye
Muungano , (c) Tumerudi pale
pale mshirika wa Zanzibar ni
Tanzania na kwa hivyo hakuna
usawa , (d) Tumeganda pale pale
kuwa Tanganyika inasimamiwa
na Serikali ya Muungano , (e)
Tumesalia papo kuwa Bunge la
Muungano linatunga sheria za
Tanganyika na tunajua kuwa
sheria kama hizo hazina nguvu
Zanzibar , (f) Tumejizuga vile vile
kumwita Waziri wa Muungano
hata asiyesimamia j ambo la
Muungano kama kilimo bila ya
kuwa na hadhi kama hiyo, ( g)
Tumekwama pale pale Mahakama
Kuu ya Tanganyika inaitwa ya
Muungano, ( h) Tumejidanganya
vile vile wafanyakazi wote wa
Tanganyika wanabaki ni wa
Muungano na wale wa Zanzibar
mwisho wao ni Chumbe.
Ally Saleh, kama nilivyo mimi,
ni mliberali wa Muungano.
Anataka Muungano ubaki e
ukiwa na mageuzi ya kimsingi.
Anataka nguvu ya Seri kal i
ya Muungano kwa mambo
yasiyokuwa ya Muungano katika
nchi washirika zipungue kama
si kuondoka kabisa. Anataka
mgawanyiko wa wazi wa ipi
Tanganyika (kama nchi mshirika)
na ipi Tanzania (kama Muungano
wenyewe). Anataka hadhi na
heshima ya Tanganyika, kwa
upande mmoja, na Zanzibar, kwa
upande mwengine, zitambulike
na ziheshimike.
Rasimu ya Vijisenti inafanya
kinyume chake na hapo ndipo
unapolifanya kundi la mrengo
wa siasa kali za kushoto ndani
ya visiwa vya Zanzibar kuwa na
nguvu kwenye hoja yake. Baada
ya Rasimu hii, sasa ni rahisi zaidi
kuushawishi umma kuamua dhidi
ya Muungano kwa ujumla wake
kuliko kuamua juu ya baadhi
ya mambo na kuacha baadhi
ya mengine ndani Muungano
huo, kama ambavyo Rasimu ya
Warioba ilikuwa imefanikiwa
kuweka mizania.
Danganya-toto, kwa mfano,
ya kumfanya Rais wa Zanzibar
kuwa Makamu wa Pili wa Rais
wa Tanzania, lakini wakati huo
huo kuyapeleka madaraka ya
Muungano kwa Makamu wa
Kwanza na wa Tatu (ambao si
lazima wawe Wazanzibari na hata
wakiwa hawawakilishi matashi
ya Zanzibar kwenye Muungano)
kumedhihirisha tu hoja ya wenye
siasa kali za kushoto kuelekea
Muungano, kwamba Dodoma
haitapata usingizi hadi imalize
kila alama ya uhuru, uwezo na
hadhi ya Zanzibar.
Waliberali wa Kizanzibari
wa Muungano kama tulivyo
mimi na Ally Saleh ambao
kila siku tuliamini kuwa njia
ya kati na kati inawezekana
kupitika kuelekea Muungano
mzuri zaidi kati ya Tanganyika
na Zanzibar, tumeambiwa na
Rasimu ya Vijisenti kwamba
hilo halipo wala haliwezekani
kabisa. Tumekhiyarishwa baina
ya kuisalimisha kabisa heshima
ya nchi yetu au kuukataa kabisa
Muungano na Tanganyika.
Wakati Rasimu hii imetunyima
sisi waliberali tunachokitaka, na
ambacho tunaamini ndicho pekee
kinachoweza kuudumisha na
kuunusuru Muungano, imewapa
kila kitu wale wenye siasa kali za
mrengo wa kulia, ambao mtazamo
na siasa zao ni kuelekea nchi moja
na serikali moja na ambao wala si
waumini wa Muungano kwa dhati
yake, bali Muungano kwa jina
lake tu. Kwa dhati kabisa, kundi
hili linaamini kuwa Zanzibar
hai paswi hata kui shi kama
sehemu muhimu na yenye upekee
kwenye Muungano, bali inapaswa
tu kuwa kama vile zilivyo Arusha,
Tanga na Shinyanga.
Tuliokosa si sisi Waliberali tu,
bali pia kundi jengine ambalo
si dogo ndani ya visiwa vya
Zanzibar ambalo liliivumilia
mizania ya Rasimu ya Warioba
licha ya kwamba haikuwapa kila
wakitakacho la siasa kali za
kushoto kuelekea Muungano.
Lile ambalo linaamini juu ya
kut okuwe po ka bi s a kwa
Muungano. Lakini kwa kuwa
kundi hi l i l i l i tegemea sana
matokeo hayo, halikushitushwa
isipokuwa tu limethibitisha na
kupata hoja ya kutusuta sisi
wengine. Na kwa msingi huo,
sasa linapata uhalali zaidi kuliko
kundi la akina miye na Ally Saleh.
Matokeo yake ni kuwa Rasimu
ya Vijisenti inatufanya na sisi
waliberali tuangalie upya siasa
zetu kuelekea Muungano kwa
mara ya kwanza. Je, ni kweli
hapa njia ya kati na kati kuelekea
kwenye Muungano wa heshima,
haki na usawa kama tulivyokuwa
tukiamini siku zote? Je, nasi
tuelemee kushoto kabisa au kulia
kabisa?
Maj i bu ya maswal i haya
yametolewa kwa njia isiyo sahihi
ndani ya Rasimu ya Vijisenti;
na haitakuwa ajabu kwamba
Rasimu hii, kwa hivyo, ndiyo
itakayouvunjilia mbali Muungano
huu uliodumu kwa nusu karne.
Waswahili husema: kheri i
matumboni mwa shari!
(Makala hii imetolewa kwa hisani
ya Mohammed Ghasani kama
ilivyopatikana katika mtandao wa
Mzalendo.)
6
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Makala
Inaendelea Uk. 12
NENO msalaba linatokana
na neno sulubu, kwa maana
ya tabu, mateso, shida n.k.
Hivyo kama ni kazi, ni kazi
ya mateso, kama ni maisha
ni maisha ya mateso, kama ni
kipigo ni kipigo cha mateso
na kama ni kifo au kuuawa ni
kifo au kuuawa kwa mateso ya
aina yoyote, si lazima yawe ya
aina fulani.
Ku u n g a n i s h wa k i l e
kinachoaminika kuwa Yesu
alisulubishwa kwa maana ya
kuwa alipigiliwa msalabani, na
kuunganishwa kuwa msalaba
ni nembo ya ukombozi kwa
dini ya Kikristo, inawezekana
kuwa si sahihi, kwa kuwa,
kuwasulubisha watu kulikuwa
hata kabla ya Yesu kuzaliwa,
na ilikuwa ni sheria ya ukatili
uliotendwa na serikali ya
Kirumi kwa enzi hizo. Ndiyo
maana walikuwa na mahali
maalumu pa kusulubishia
watu palipoitwa Golgotha,
yaani mahali penye mafuvu ya
watu walio teswa na kufa hapo
na kuozea hapo.
Ndi yo ma a na s he r i a
ya Taurat i i kat of aut i sha
unyongwaji wa mtu aliyestahili
kunyongwa na ile sheria ya
Kirumi, pale ilipoandikwa hivi:
Akiwa mtu ametenda dhambi
ipasayo kufa, akauawa, nawe
ukamtundika juu ya mti, mzoga
wake usikae usiku kucha juu
ya mti; lazima utamzika siku
hiyo hiyo kwani aliyetundikwa
amelaaniwa na Mungu; usije katia
unajisi katika nchi yako akupayo
BWANA Mungu wako, iwe urithi
wako. (Kum. 21:22-23.)
Kwa maana hiyo, alama ya
pande nne au jumlisha, sio
msalaba. Neno hilo la msalaba,
limeingizwa na mfalme wa
Rumi ili kuchochea askari
wake wakati waki pi gana
vita kwa kuvamia mataifa
mengine ili wahakikishe kuwa
wanawasulubu wale wote
waliowaita kuwa ni maadui zao,
wasiwahurumie na baadaye
likatiwa rasmi katika Vita vya
Msalaba. Kilichozungumziwa
hapo, ni , kutundikwa mtini au
kunyongwa, iwe ni kwa kamba
au nduano (ndwana).
Vita vya Msalaba vilikuwa
vi t a vya kuwaangami za
Waislamu vya mwaka wa
1096, vilivyo idhinishwa na
Pope Urban II na ambavyo
vinaendelezwa hadi sasa kwa
kutumia misamiati mbalimbali
kama tutakavyoona baadaye.
Mwa k a A . D . 3 1 2
Cons t ant i ne al i kwe nda
kupigana vita na Maximian,
aliyekuwa amejitwalia kwa
hila ufalme wa Italy, na wa
Afrika. Constantine alipokuwa
akisafri kwenda vitani, alisema
kwamba aliona maono ya ajabu:
maana mbinguni ilitokea dalili
au ishara, kama ya msalaba
wa mwanga ukizungukwa na
Masheikh wapo Golgotha
Wanabebeshwa msalaba wa Pope Urban II
Na Khatib J. Mziray
WATUHUMIWA wa kesi ya ugaidi wakiwa katika Mahakama ya
Kisutu jijini Dar es Salaam.
maneno ya moto yaliyongaa.
Maneno yenyewe ni haya: Kwa
msalaba huu utapata ushindi.
Basi Consitantine akaamuru
kwamba mfano wa msalaba
ushonwe katika bendera zote
za majeshi yake. Akaenda
akamshinda Maxsentius, kisha
aliporudi Rumi akasimamisha
sanamu humo mjini mfano
wake yeye mwenyewe; sanamu
aliyechorwa katika jiwe kuu.
Na sanamu huyo alikuwa
na msalaba mkononi; nao
umeandikwa chini anwani yake
ya kusema kwamba msalaba
huo ul i mshi ndi a vi tani .
(Historia ya Kanisa uk.55, cha
Canon H.J.E. Butcher.)
Ndiyo maana Peter the Hermit,
alipozusha poropoganda, za
kuwa, Waislamu wanawauwa
Wakristo kule Yerusalemu,
na akaomba kibali kwa Pope
Urban II; alifanya kazi hii hii
inayofanywa na Marekani, na
mataifa ya Ulaya ya kuzunguka
nchi za Ulaya, na kukusanya
Maaskofu na ma Padre wengi
wakakus anya Wa k r i s t o
wengi wake kwa waume, watoto
kwa wakubwa wakavaa alama
ya msalaba katika nguo zao,
wakenda vitani. Ikimanisha
kuwa wanaenda kuwasulubu
Waislamu wa Yerusalemu,
katika Crusades ya mwaka wa
1096. Na wanaandika wenyewe
jinsi walivyowasulubu, hata
pale Waislamu walipotaka
suluhu, Wakristo na kanisa
na viongozi wao hawakutaka
suluhu, bali sulubu. Canon
anatufahamisha akisema:
Kisha askari hao wakaenda zao
wakafka Antiokia, katika nchi ya
Palestine, wakauzunguka muda
wa mezi minane. Wakautwaa mji
huo, wakawaua wote waliokataa
kui shi ka di ni ya Ki kri sto.
(Historia ya Kanisa, u.k. 85.)
Pia, walikuwako wengi kati
ya Waislamu ambao walitaka
kuishi kwa amani kati yao na
Wakristo, vile vile Wakristo
wenye mashamba eneo za
Mashariki waliona haja ya
kupatana. Lakini, maaskari
waliotoka nchi za Magharibi
wa l i t uma i ni kuwa okoa
Waislamu wote kwa upanga,
wakaacha chuki kat i ya
Waislamu na Wakristo hata
siku hizi zetu. (u.k.87).
Wafundishaji wa Ukristo,
wanatwambia kuwa msalaba ni
alama ya ukombozi, na askari
hao wa Crusades walivaa
mavazi yaliyochorwa misalaba
kama alama ya ukombozi,
lakini kazi waliyofanya ni
hiyo hapo juu; ya kuwaokoa
( kuwauwa) Wai sl amu kwa
kuwakata vichwa kwa upanga.
Ukatili huo unaotokana na
sera za kuasisiwa kwa Kanisa,
chini ya mfumo wa Kirumi, na
viongozi wa Ukristo, ndio huu
huu unaoendelezwa sasa katika
vita vinavyoitwa vya magaidi,
wanavyofanyiwa Waislamu.
Chakusikitisha ni kuwa, kwa
sasa, viongozi wa nchi za
Kiislamu na hata na viongozi
wa Waislamu, wanakusanywa
pamoja na nchi za Ulaya na
kuchangia Vita vya Msalaba
(Crusades) kwa kisingizio cha
kutokomeza magaidi. Labda
hapa nitoe mfano hai wa vita
vya Iraq vilivyomwondoa Rais
Sadam Husseni, tuone jinsi vita
hivyo vilikuwa vya msalaba;
na jinsi viongozi wa Makanisa
walivyokuwa wakifurahia
kuona Waislamu wakiokolewa
kwa kulipuliwa vichwa kwa risasi
na mabomu.
S a d a m H u s s e n i
alisingiziwa kuwa ana silaha
za maangamizi. Rais Bush
akishirikiana na mataifa ya
Ulaya, Umoja wa Mataifa na
baadhi ya nchi za Kiarabu
(Waislamu) wakakokotwa kwa
kutishwa kuwa atakayekataa
kushirikiana na Marekani,
atachukul i wa kuwa huyo
ni gaidi. Na viongozi wa
Makanisa na mashirika ya
kanisa na vyombo vyao vya
habari vikieneza poropoganda
na kusherehesha na kufafanua
lengo la vita hivyo. Kwa ujumla
vikikoleza propaganda, uzushi
na uwongo.
Ni l i a n d i k a ma k a l a
zilizoelezea lengo la vita
hi vyo t arehe 28/ 10/ 2005.
Inawezekana waliozisoma
wakati huo hawakuzingatia
ukwel i huo, ni meonel ea
nizinukuu hapa ili wasomaji
walinganishe hali iliyopo sasa
na mambo yalivyokuwa na
lengo lilivyokusudiwa. Moja
ya gazeti la Kanisa liliandika
kichwa cha habari hiv:
Biblia yasema Irak ina pepo
shujaa wa vita. Walipigana na
malaika wa Mungu siku 21. Ilibidi
Malaika Mkuu Mikaeli ashuke
kuingilia kati. Rais Bush asoma
Biblia kabla ya kutangaza vita.
Chini ya maandishi hayo
iliwekwa picha ya askari wa
Iraki aliyetekwa na askari wa
Marekani wakimnywesha maji
kutoka katika chupa zao za
kijeshi na mmoja wa askari
hao amemwekea mtutu wa
bunduki kichwani; lakini
inavyoonekana ni kuwa askari
huyo wa Iraki alishakufa, na
hizo ni kejeli na mbwembwe
za askari wa vita vya msalaba.
Mwandi shi wa makal a
hiyo alikuwa ni Mchungaji
Teghua akithibitisha kuwa
anachofanya Bush ni cha Kanisa
-Ukristo, na kuwa ametumwa
na Mungu kuwaangamiza
Waislamu (mapepo) wa Iraki.
Alinukuu kitabu cha Danieli
(10:1-19), ili kuonyesha uhalali
wa Rais Bush wa kuivamia
Iraki huku akimwelezea kuwa
ni mkombozi aliyetumwa na
Mungu kuyaondoa mashetani
wa Iraki. Hivyo kuangamizwa
wat u wa I raki ni hal al i .
Mchungaji Teghua aliandika
hivi:
Rais Bush wa Marekani,
ambaye ni Mlokole alikaa kwanza
kusoma Biblia katika kitabu
cha Mwanzo 18:17; BWANA
AKANENA, JE! Ni mf i che
Ibrahimu jambo nilifanyalo
Haikuelezwa na yeyote kuwa
ni nini alichokikusudia Rais
Bush kusoma andiko hilo kisha
kunyanyuka kwenye kiti na
kutangaza vita.
Hat a hi vyo Mchungaj i
Teghua, alifafanua kidogo kwa
kuandika hivi:-
Kama vile alivyosema Bwana
Yesu kuwa siku za mwisho zitakuwa
7
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014 Makala
Barua ya wazi kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar
27 Septemba, 2014
Assalam alaykum
Natumai hamjambo ndugu, kaka na
dada zangu. Inshallah Mwenyenzi
Mungu akupeni afya na uzima
kuelekea kipindi hiki muhimu
cha kupiga kura kuamua Katiba
inayopendezwa na pia Mola akupeni
busara na maamuzi mema.
Nakuandikieni barua hii kama
Mzanzi bar i mwenzenu s i na
zaidi ya hilo. Ni kutokana na
Uzanzibari wangu nimeona kuwa
nijaribu kukuaidhini, kunasihini,
kukushawishini, kukusemesheni,
kukuombeni kuwa msiikubali Katiba
inayopendekezwa na muipigie kura
ya HAPANA.
Taf adhal i ni wekeni mbal i
ushindani, itikadi na mitazamo
ambayo inatutenganisha Wazanzibari
na muamue kwa maslahi makubwa,
mapana na ya muda mrefu ya
Zanzibar. Msitizame tulipojikwaa bali
tizameni tulipoanguka. Msitizame
nyuma mkahesabu visa na mikasa, ila
nyinyi hapo mlipo ndio wenye fursa
ya kuiokoa, kuinusuru na kuihuisha
Zanzibar.
Naam, ni kura ya HAPANA
ndio ambayo itaibakisha, itaiokoa,
i tai si mami sha Zanzi bar. Mj ue
mkipigia kura ya NDIYO maana
yake ni kuwa Zanzibar tuipendayo
inazidi kupungua, kuchukuliwa na
kumezwa kama ambavyo imekuwa
khofu yetu kwa miaka kadhaa ya
Muungano huu.
Nat aka muami ni ndani ya
dhati yangu mimi ni muumini wa
Muungano. Nataka Muungano wa
haki na hadhi sawa baina ya Washirika
wa Muungano Tanganyika na
Zanzibar- ili kila nchi ipate fursa sawa
za kuhudumia watu wake.
Wengi wenu kwa kauli zenu
mara kadhaa mmekuwa mkisema
Muungano hauakisi hali ya usawa,
haki na hadhi sawa, lakini mkawa
mnatumia neno KERO kuwasilisha
fikra zenu hizo, na wengi tukawa
na matumaini kwamba fursa hii ya
kuunda upya Katiba yetu itapunguza
kama si kuondosha kabisa KERO
hizo.
Il a baada ya kui ona Kati ba
inayopendekezwa, nimeona kuwa
andiko hilo halina msaada, halina
muel ekeo na hal i na wema na
Zanzibar. Kulikubali andiko hilo
ni kujitia kitanzi wenyewe na sasa
imekuwa ni kusokotwa, kubanwa
na kudhibitiwa Zanzibar lakini mara
hii itakuwa kwa kujitakia wenyewe.
Huko nyuma tumekuwa tukisema
kuwa kumekuwa na hadaa, sijui
ujanja, sijui ghalat, sijui unyemela
wa kuongeza Mambo ya Muungano
ambayo yamekuwa yakipunguza
madaraka ya Zanzibar, lakini mara
hii tunajichinja wenyewe kwa mikono
yetu.
Hii ilikuwa ni fursa kubwa kwetu
kusimama kama Zanzibar. Zanzibar
ilipaswa kusimama kama kundi
zima ndani ya Bunge na kukaa na
kundi zima la upande wa pili yaani
Tanganyika, na watu wa pande mbili
hizi kuamua umbo, hadhi na sifa gani
tunataka Tanzania iwe.
Hili la pande mbili lilikuwa
lisionewe aibu kwa sababu ndio
ukweli na uhalisia kwamba tuko
pande mbili. Haiwezekani kuwa na
Muungano, ambapo upande mmoja
WAJUMBE wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar walipokuwa
Bungeni Dodoma. (Picha kwa hisani ya mtandano wa IPP)
una kila sifa za kuwa nchi, halafu
upande mwengine uwe na sifa za
kuwa dola na nchi ifchwe ndani yake.
Ilikuwa ni nafasi nzuri kwa
Zanzibar kudai haki zake, stahiki zake,
fursa zake ili iweze kukidhi mahitaji
ya watu wake, maana hata kama
tumo ndani ya Muungano, basi bado
tuna chumi mbili zinazoshindana
na kwa kweli zinazopigania na
kunyanganyiana rasilimali karibu
zile zile.
Ilikuwa ni wakati wa kufanya kila
njia ili Zanzibar ijitengenezee fursa ya
kuwa na mafanikio kama ya Visiwa
vya Seychelles au Mauritius ambavyo
wastani wa kipato cha mwananchi wa
nchi hizo mbili ni zaidi ya dola 14,000
na dola 15,000 mtawalia.
Naj ua hoj a itakuj a basi haya
yangef anywa kwa umoj a, na
mbona umoj a huo haukuwepo,
nakiri kuwa hilo kweli limetokea,
lakini ni kama katika mchezo iwapo
mchezaji mmoja ametolewa ama
kwa kuonewa na mwamuzi au kwa
kitendo chake cha makusudi, haina
maana kuwa waliobakia uwanjani
wakubali kupoteza mchezo, badala
yake hujibidiisha kushinda ili iwe
njia moja ya kumsuta mwenzao
aliyetolewa na sifa kwa kweli inakuja
kwa waliobakia uwanjani.
Kwa kuendelea kuj igandisha
katika ubavu, kuendelea kuamini
kuwa hatuwezi kujitegemea na kwa
hivyo mambo kadhaa kuyabakisha
katika Muungano ni kujiviza akili,
ni kuj idhalilisha kimkakati na
kujidogosha kihadhi.
Si kweli na si kweli kabisa kuwa
Katiba inayopendekezwa ina maslahi
na Zanzibar. Haina, haina katu,
haina Abadan, kamwe haina. Ni
katiba ambayo inatuweka pabaya
na pagumu zaidi na imeendelea
kuyachukua mamlaka ya Zanzibar
na kuyatia katika Muungano.
Vipi Katiba hii itakuwa na maslahi
na sisi? Hebu tutizame mambo
machache:
1. Kuondosha au kuukataa mfumo
wa Shirikisho ina maana kuwa
Zanzibar haiwezi kuwa na hadhi na
haki sawa na Serikali ya Muungano.
Pili, tumejibakisha pale pale Zanzibar
haina mshirikia mwenziwe kwenye
Muungano. Tatu, tumerudi pale pale
mshirika wa Zanzibar ni Tanzania
na kwa hi vyo hakuna usawa.
Nne, tumeganda pale pale kuwa
Tanganyika inasimamiwa na Serikali
ya Muungano. Tano, tumesalia papo
kuwa Bunge la Muungano linatunga
sheria za Tanganyika na tunajua
kuwa sheria kama hizo hazina nguvu
Zanzibar. Sita, tumejizuga vile vile
kumwita Waziri wa Muungano hata
asiesimamia jambo la Muungano
kama kilimo bila ya kuwa na hadhi
kama hiyo. Saba, tumekwama pale
pale Mahakama Kuu ya Tanganyika
i nai t wa ya Muungano. Nan,
tumejidanganya vile vile wafanyakazi
wote wa Tanganyika wanabaki ni
wa Muungano na wale wa Zanzibar
mwisho wao Chumbe.
Fikiria, hii ndio Zanzibar tuitakayo?
2. Tunajipa moyo kuwa kumfanya
Rais wa Zanzibar kuwa ni Makamo
wa Rais wa Muungano kuna manufaa
kwa Zanzibar ilhali hakutakuwa na
msaada wowote.
Tumewapa watu matumaini kuwa
hilo litawezesha Rais wa Zanzibar
akitoka nje atakuwa na hadhi ya
kimuungano wakati tunajua hilo
litaleta utata mkubwa zaidi huko
mbele. Kwanza kwa suala la gharama
pili kutakuwa na mgongano wa
maslahi na majukumu yake kama
Rais wa Zanzibar vs Umakamo wa
Muungano
3 . Ha i we z e k a n i Ra s i mu
inayopendekezwa iwe imenyofoa
mamlaka zaidi yaliokuwa yameanza
kuikaribia Zanzibar kutokana na
Rasimu ya Warioba, halafu isemwe
kuwa kuna maslahi kwa Zanzibar.
(Mfano) kuondoa uwezo wa Zanzibar
kuunda Benki yake. Kurudisha
nguvu za kuigawa Zanzibar kwa
Rais wa Muungano. Kukubali ardhi
kurembwa. Tumerudisha suala la
Tume ya Pamoja ya Fedha ambayo
imeshindikana kwa miaka kadhaa
toka nia hiyo ilipotiwa kwenye Katiba
ya 1977.
4. Uamuzi wa kuyatia madaraka
ya Serikali ya Zanzibar ndani ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano
ilhali hakuna sehemu yoyote ya
Katiba inayopendekezwa ambapo
madaraka ya Serikali ya Tanzania
Bara kama inavyoitwa yameainishwa
ni kuendelea kujidanganya.
Pili, kwa kufanya hivyo tunarudi
tena pale pale ambapo Zanzibar
inaonekana inakiuka Katiba ya
Jamhuri pale inapotaka kufanya
mabadiliko yenye maslahi yake,
ilhali jambo kama hilo halionekani na
wala halipo kwa upande wa mshirika
mwenziwe, maana mshirika ni huyo
huyo Serikali ya Jamhuri na Serikali
ya Tanzania Bara.
Ndugu, kaka na dada zangu ujue
wazi kuwa maamuzi unayotaka
kuyafanya ni makubwa na yana athari
ya muda mrefu kwa vizazi vingi vya
Zanzibar, ambayo pamoja na tofauti
zetu, lakini naamini tunakubaliana
kuwa Zanzibar tuipendayo iwepo. Na
kuwepo kwake lazima iwe na nguvu
na matao yake.
Na kwa dal i l i zote, Rasi mu
inayopendekezwa inapopotoa nguvu
na matao ya Zanzibar. Inaondosha
uzuri na haiba yake kwa kuifanya
kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya
Muungano badala ya kuwa ni nchi
moja kamili ndani ya Muungano huu.
Fikirini, pimeni na muvuke nje ya
itikadi na mitizamo. Fanya uamuzi
ili nafsi yake iwe na amani kwa
sababu umefanya uamuzi wako bila
ya shindikizo, maelekezo au utashi
wa kisiasa, maana wewe kwanza
ni Mzanzibari kisha mengine ndio
yanafuata.
Nawaomba radhi kwa uamuzi
huu wa kuandika barua ya wazi
maana isingewezekana kumfka kila
mmoja wenu, lakini nataka muamini
kuwa barua hii nimeiandika kwa
sababu nimeona kuna wajibu kwangu
kufanya hivyo.
Unapotaka kupiga kura fikiria,
wazia na pimia juu ya uzito wa
mchoro wako mmoja tu wa kalamu
utavyokuwa na athari kwa nchi yako,
watu wako na watoto na wajukuu
wako. Fumba macho, rudisha nyuma
fkra zako,
kumbuka wema na ihsani za
waliokuzunguka, uliokuwa nao
pamoj a katika maisha yako na
uwafkirie khatma njema ya muda
mrefu.
Kumbuka j ukumu l ako kwa
Mwenyenzi Mungu na fkiria kama
hicho ni kitendo cha mwisho cha
maisha yako ili ukitie katika mizania
nzuri ya maamuzi yako.
Piga HAPANA kwa faida ya
Zanzibar na usinitizame mimi kama
Ally Saleh, la. Mimi ni mtu mmoja tu
tena tunaweza kuwa tuna mzigo wa
tofauti zetu, lakini pamoja na yote
mimi na wewe ndio Zanzibar.
Kwa maslahi ya Zanzibar piga
HAPANA.
Ally Saleh
Zanzibar
8
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Makala
Inaendelea Uk. 9
HALI si shwari. Ni hamkani
tupu. Polisi, jeshi, taasisi za
kikachero na viongozi wa serikali
katika nchi mbalimbali duniani,
wapo hai hai kuweka mikakati
ya kukabiliana na kitisho cha al
Qaida, al-Shabab, Boko Haram
na ISIS. Vikao vinafanyika na
kutumia gharama kubwa, nini?
Kujadili kitisho cha ugaidi, iwe
ni Boko Haram, al Qaida, ISIS au
al Shabab.
Kwa upande mwingine, wapo
wale ambao ndio waathirika
wakubwa na wa mwanzo
kuathiriwa na mikakati hii ya
wakubwa ya kupambana na
magaidi. Waathirika hawa ni
Waislamu. Nao miongoni mwao
wapo wal e wal i omezeshwa
propaganda ya Jihad ya Boko
Haram, al Shabab na I SI S,
wakaipokea na sasa wapo tayari
kuacha familia zao kwenda
kushika bendera nyeusi yenye
kalimt Tawheed kusimamisha
Khilafah. Lakini hata kama hilo,
halitawezekana, basi wamebaki
kuwa mas habi ki ambapo
katika ushabiki huo wanajikuta
wakifanya vitendo ambavyo
vinawapeleka Goligotha, wao
binafsi na jamii ya Waislamu kwa
ujumla.
Makundi yote haya mawili,
yanafanya kazi kama mawakala
Tumemeza al Qaida, ISIS
Boko Haram, al Shabab
Sasa tunaletewa Khorasan Group
Na Omar Msangi
tu, iwe kwa kutambua au kwa
kutumiwa bila kujijua.
Hivi sasa Marekani ipo katika
kampeni kubwa ya kuwapiga
IS ndani ya Syria. Lakini katika
kufanya kazi hiyo inaj ikuta
ikikabiliwa na vikwazo viwili.
Kwanza ni kuwa i naf anya
mashambulizi hayo bila idhini ya
Bunge lake yenyewe wala kibali
kutoka Umoja wa Mataifa (U.N.
authorization). Kwa hiyo hakuna
uhalali wa kisheria (lack of legal
justifcation- No viable claim of
self-defense or U.N. approval.)
Pili, ni kuwa itakuwa vigumu
sana kudumisha uungwaji mkono
kutoka kwa wananchi wake iwapo
kampeni hiyo itachukua muda
mrefu. Na hiyo ni kwa sababu
hao ISIS hawaonekani kama ni
kitisho cha karibu na cha uhakika
kwa Marekani (imminent threat to
the homeland). Wanaonekana
tu kuwa ni adui na zimwi, lakini
lililopo mbali. Nini ufumbuzi?
Kutafuta zimwi jipya.
Kundi la Khorasan
Hivi sasa Marekani imekuja na
madai kuwa kuna kundi jipya la
kigaidi linalojiita The Khorasan
Group, ambalo ni hatari zaidi
ya ISIS. Na kwamba kundi hili
linapanga kufanya mashambulizi
Amerika na Ulaya mfano wa lile la
Septemba 11. Katika madai hayo,
wakuu wa Marekani wanasema
kuwa hao The Khorasan Group
wana utaalamu wa kutengeneza
milipuko midogo lakini yenye
nguvu sana na ambayo haiwezi
kugundulika kirahisi na mitambo
ya ukaguzi kwa hiyo wanaweza
kuingia nayo katika ndege za abiria
MAUAJI kushoto kulia. Hakuna
anayehesabu tena ni watu wangapi
wanauliwa. Libya imetoka katika
habari zinazongara za mfumo.
Imeshavurugwa. Waliotumika
wakidhani akiondoka Gadhaf
wa t a s i ma mi s ha Dol a ya
Kiislamu (Khilafah), wameachwa
waki uwana wenyewe kwa
wenyewe. Amani hakuna tena
Libya. Nia na lengo la makafri
mabeberu limefkiwa. Mapigano
yamefanikiwa. Kuisambaratisha
nchi nyingine ya Waislamu ili
kuinyonya kwa urahisi. Sasa
Libya ni Congo (DRC) ya Afrika
Kaskazini.
Vita na mtambo wa mauaji
vinasonga mbele. Waislamu
h a mn a z o h a wa j a k o ma
wa l a k u t a n a b a h i . S a s a
wanatumika tena kuivuruga na
kuisambatarisha Syria. Damu
ya maelfu kwa mamilioni ya
akina mama na watoto wasio na
hatia inamwagwa ili kufanikisha
malengo ya mabeberu makafri.
Waliotangulizwa kufanya kazi
hii chafu ni wanaojiita Waislamu
mujahidina, IS.
Kwa kisingizio cha kuangamiza
n a k u t o k o me z a u g a i d i
unaohatarisha amani duniani,
vita ya kuuwa na kuhujumu
Waislamu inaendelea. Masheikh
wanakamatwa na kufanyiwa
matendo ya kudhalilisha ikidaiwa
kuwa hiyo ni katika vita kwa ajili
ya kudumisha amani na utulivu.
Ni hivyo. Hakuna jipya. Gazeti la
Washington Post linavisifu vita
Mauaji kushoto kulia
Mtambo wa mauaji unasonga mbele
Tumekuwa wacheza mduara wa maadui
Na Omar Msangi
ni pendekezo lenye faida.
Ukienda kule Nchi za Ghuba,
tayari ni wacheza mduara wa
Marekani, kama alivyothibitisha
Waziri wa Mambo ya Nje John
Kerry katika safari yake ya hivi
karibuni kwenda Mashariki
ya Kati kupata mifungamano
mipya. Mashine ya kutotoa
uwongo inafanya kazi nzuri
kuwachanganya watu. Kufikiri
binafsi ni kama kumeuawa. Watu
wanafuata propaganda ya habari
ya nchi za Magharibi ambayo
inashikiliwa kwa asilimia 90
na mashirika sita ya habari ya
Wayahudi. Ukweli huu na hali
halisi vinabidi kurudiwa kila
wakati vinginevyo tutasahau
ni wapi uwongo unaochuruzika
unapotokea.
Tangu 9/11, kati ya watu milioni
10 na milioni 15 wameuawa, iwe
ni moja kwa moja kwa mikono
ya mtambo wa vita wa Marekani
na NATO, au kupitia machafuko
yaliyosukumwa na kuwezeshwa
kifedha kote duniani na Marekani.
Yote kati ka j i na takati fu l a
kupigana na ugaidi, bila shaka.
Ni kisingizio chema sana. Nchi
zote za Magharibi zinashiriki.
(Kipande hiki kimetafsiriwa na
kuhaririwa kutoka makala The
Mass Media and ISIS vs Syria,
vs Ukraine, vs Iraq, vs Gaza: A
Game Of Confusion And Killing By
Propaganda kama ilivyoandikwa na
Peter Koenig)
Balaa lililoletwa na IS
Mapema wiki hii ndani ya
Baraza la Umoja wa Mataifa,
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin
Netanyahu alisema kuwa Islamic
State, kwa maana ya Dola ya
Kiislamu, ndio kitisho kikuu cha
dunia hivi sasa. Akaongeza kuwa
IS na Hamas, ni matawi ya mti
ule ule wa sumu akiutaja kuwa ni
Uislamu akiubatiza kwa jina la
militant Islam.
"ISIS and Hamas are branches of
the same poisonous tree. ISIS and
Hamas share a fanatical creed.
Alisema Netanyahu, ufupi wa
maneno akimaanisha kuwa ISIS
na Hamas, ni matawi ya mti wa
sumu na mti huo akautaja kwa
ishara kuwa ni Uislamu.
Japo ameijumuisha Hamas
hapa, lakini muhimu hapa ni
kuwa hapa ndipo walipotufkisha
ISIS. Kwamba leo hata Netanyahu
ambaye punde t u amet oka
kuchinja Wapalestina takribani
2000, anakuwa na ujasiri wa
kusimama mbele ya Baraza la
Umoja wa Mataifa kudai kuwa
kuna watu katili na wauwaji
kuliko Israel.
Ukiacha kauli hii ya Netanyahu,
lakini kinachofanyika hivi sasa,
ni kufuta rekodi i l i yokuwa
imewekwa na wauwaji katili
wote waliotangulia katika historia
ya mwanadamu wakiwemo wale
wa makuruseda, na kuandika
historia mpya kuwa watu katili
na wauwaji washenzi kuliko
wote, ni hao IS wanaotajwa kwa
jina linalowakilisha Uislamu na
Waislamu. Hii pekee ni msiba kwa
Waislamu.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin
Netanyahu.
Inaendelea Uk. 9
9
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Makala
Tumemeza al Qaida, ISIS
Boko Haram, al Shabab
Inatoka Uk. 8
bila kugundulika. Wanaendelea
kudai kuwa Khorasan Group
wameingia Syria, si kwa lengo la
kupigana bega kwa bega na ISIS,
lakini kutafuta namna ya kutoa
mafunzo kwa wapiganaji wa
ISIS kutoka Ulaya na Marekani
ili iwe rahisi kwa wapiganaji hao
kuingia katika nchi zao kufanya
mashambulizi ya kigaidi.
Kwa kipindi sasa, taarifa hizo
zimekuwa zikilishwa vyombo vya
habari vya Marekani na kuchukua
nafasi kubwa kuliko zile za ISIS.
Taarifa ya Associated Press (AP)
ya Septemba 13 inawanukuu
maofsa wa serikali ya Marekani
wakisema kuwa kumeibuka
muj ahi di na wapya kutoka
Afghanistan, Yemen, Syria na
Ulaya ambao ni tishio la moja kwa
moja kwa usalama wa Marekani.
Wakadai pia kuwa mujahidina
hao wapya wanashirikiana na
magaidi wa Yemen wenye ujuzi
wa kutengeneza mabomu wakiwa
la lengo la kushambulia U.S.
aviation.
I nael ezwa kuwa t of aut i
n a muj a h i di n a we n g i n e
wanaopambana kumng oa
Bashar al Assad, hawa Khorasan
wametumwa na kiongozi wa
al-Qaida Ayman al-Zawahiri
kuwapa mafunzo mujahidina
wenye hati za kusafria (passports)
za Marekani na Ulaya ili iwe rahisi
kwao kuingia katika nchi hizo
kufanya mashambulizi bila ya
kutiliwa shaka.
The fear is that the Khorasan
mi l i t ant s wi l l provi de t hese
sophisticated explosives to their
Western recruits who could sneak
them onto U.S.-bound fights.
AP i l i e l e z a i k i wa o nya
Wamarekani kuwa tofauti na ISIS,
hawa Khorasan Group ni tishio la
moja kwa moja na la sasa hivi kwa
Amerika .
Katika kukoleza kitisho na
propaganda hiyo, taarifa ya
habari ya CBS News asubuhi ya
Septemba 18, ikaja na kauli kama:
sources warn of a more immediate
threat to the U.S. Homeland.
Sources confrm the Al Qaeda cell
goes by the name Khorasantheyre
developing fresh plots to atack U.S.
aviation.
Mchana wa siku hiyo hiyo,
i kat oka kaul i kut oka kwa
Mkur ugenzi wa Nat i onal
Intelligence, James Clapper
akidai kuwa:
In terms of threat to the homeland,
Khorasan may pose as much of a
danger as the Islamic State.
Septemba 20, The New York
Times , nalo likaibuka na kichwa
cha habari kilichonadi:
U. S. Suspects More Direct
Threats Beyond ISIS.
Na kukoleza kwa kibwagizo
kuwa Khorasan, ikiongozwa na
mtu aliyetajwa kwa jina la Muhsin
Inaendelea Uk. 11
Mauaji kushoto kulia
Inatoka Uk. 8
Ho j a h a p a s i o k a ma
yanayosemwa kufanywa na IS
ni kweli au la, lakini hoja ni
namna Waislamu walivyotumika
kufanikisha propaganda hii
kupitia proxy war kutufikisha
hapa. Wapo baadhi ya watu
wanatoa hoja kuwa IS ni wapigania
dini wenye nia ya kusimamisha
Uislamu na wao (IS) wameona
kuwa njia inayofaa ni hiyo ya
vita na mauwaji. Wenye hoja hii
wanasema kuwa hakuna haja ya
kuwasema vibaya IS kwani hiyo
itakuwa sawa na kueleta faraka,
fitna na malumbano yasiyo na
maana miongoni mwa makundi
mbalimbali ya Waislamu.
Pengine nianze kwa kusema
kuwa hoja kama hizi zinatoa
somo moja kubwa na muhimu
sana kwa Waislamu: Kwamba
maadui wa Uislamu hawalali na
wameshafanya kazi kubwa sana.
Tunavyostuka hivi sasa, ni kuwa
inavyoonyesha kumeshafanyika
kazi kubwa sana ya kusambaza
mawakal a ( agent s) ambao
wamefanikiwa kupandikiza sumu
na kukoroga bongo za Waislamu
kiasi cha kuleta kuchanganyikiwa
kukubwa.
Lakini pia kuna mambo mengi
yenye utata mkubwa. Jaaliya kuwa
mahali fulani wanaibuka watu na
kusimama katika mimbari za
Misikiti wakihamasisha watu
kushika silaha kupambana na
wasio Waislamu. Jaaliya kuwa
watu hawa wanatokea kuhubiri
kuwa ni halali Muislamu kupora
mali ya kafiri!!! Mwelekeo na
mahubiri ambayo kwa hakika
yanakuwa sawa na kuwachochea
watu wafanye yale yanayofanywa
na Boko Haram kule Nigeria-
kuwavamia watu (Wakristo na
hata Waislamu wasio kubaliana
nao) na kupora mali zao na kisha
kuwauwa. Swali ni je, ikitokea
watu hawa wakafanya kazi hii
kwa kiasi mwaka mzima bila jamii
kuwachukulia hatua, nini itakuwa
tafsiri ya kitendo hicho cha jamii
na hasa vyombo vya dola kukaa
kimya? Je, inawezekana katika
nchi yoyote kufanyika mambo
kama hayo, serikali isijue? Na
kama itakuwa inajua, swali ni je,
kwa nini watu kama hao waachwe
wadumu na mahubiri yao mpaka
kupata wafuasi kisha baadae ndio
zije operesheni za kamatakamata?
Ni jambo lililo wazi kuwa
hawa IS waliandaliwa, kupewa
mafunzo, silaha na fedha na
hao hao wanaokusanyana leo
kuunda muungano wa kuwapiga
IS hivi sasa. Je, hatuoni kuwa
iwapo tulikuwa tukiwasikia
watu wakitoa mahubiri ya ki-
IS na hatukuchukua hatua, hii
yaweza kutafsirika kuwa na
sisi huku tulibeba jukumu la
kushiriki katika hii Crusade
ya kuangamiza Waislamu, kwa
kuwapa fursa hawa akina Abu
Fulani, ambao ni wenzao na
akina Abu Baghdadi, kukamilisha
uwakala wao unaolenga kusimika
uwepo wa kitisho cha ugaidi ndio
tuanze kuwakamata na kutoa
fursa ya kuingiza waliokuwemo
na wasio kuwemo?
Lakini jingine la kutaja hapa ni
kuwa siri iliyo nyuma katika kuicha
IS ifanye iliyofanya na sasa kuanza
kuipiga ndani ya Iraq na Syria, sio
siri tena. Inajulikana wazi kuwa ni
katika kuzisambatarisha nchi za
Mashariki ya Kati, kuzichangua,
na kuweka mazingira mazuri ya
kupora mali kuzinufaisha Israel
na mabeberu wa Marekani na
Ulaya.
Iwapo jamii yetu itakubali
kuwalea akina Abu Baghdadi
waliotumwa huku kwetu, halafu
baadae ndio ije na mkakati wa
operesheni kamatakamata na
kuchukua hatua za kushadidia
uwepo wa kitisho cha ugaidi, ni
lazima ijue kuwa inachofanya ni
kuita machafuko, mauwaji zaidi
na kukaribisha drones na hatua
nyingine zitakazowapa mabeberu
kisingizio cha kutuvuruga zaidi
na wao kutandaza makucha yao
RAIS wa Syria, Dkt. Bashar al Asaad (katikati).
Inaendelea Uk. 11
WAPIGANAJI wa ISIS.
10
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Makala
I KI WA ni si ku r asmi ya
upigaji kura kwa wajumbe
wa bunge maalum la Katiba
kuridhia ama kutoridhia katiba
inayopendekezwa, Waziri Mkuu
Mizengo Pinda alijitokeza
hadharani kulitolea ufafanuzi
suala la Mahakama ya Kadhi
ambal o l i l i kuwa l i meanza
kulitafuna Bunge hilo baada
ya wajumbe kadhaa Waislamu
kutishia kukwamisha rasimu
hiyo ya katiba.
Alipokaribishwa kuzungumzia
hilo tangu awali wa taarifa
yake nilijua tu kabisa hakuna
mahakama ya kadhi kwenye
katiba kwa ule ule wimbo wa
kutenganisha shughuli za dini na
serikali, kwamba serikali haina
dini, ila wakati wa shida zao
wanarudi kwa viongozi wa dini
kuwalilia kuhusu mambo hayo
hayo ya serikali.
Waislamu wakitaka ushirikiano
wa kiuchumi na mashirika ya
kimataifa kama Organisation of
Islamic Conference (OIC), kupata
fedha za misaada n.k kutoka
Uarabuni, serikali inaingilia kati
na kukemea vikali, Waislamu
wanayakumbuka ya Zanzibar
na OIC , East African Muslim
Walfare Society (EAMWS) pamoja
na aliekuwa mlezi (patron) wake
mkuu Agha Khan.
Ila kabla hatujaangalia kiundani
maelezo na tamko la Waziri
Mkuu Pinda pia maswali tata
yanayojitokeza, naomba nianze na
historia hii fupi ya hapo mwaka
2012 wakati viongozi wa Kiislamu
na waumini wao walipoishinikiza
serikali kuweka kipengele cha dini
katika kuhesabu sensa ili kuondoa
ule mkanganyiko uliofanywa
na baadhi ya Taasisi na shirika
la utangazaji la Tanzania (TBC)
kwamba Wakristo ni wengi kuliko
Waislamu.
Kwa muda mrefu hoja nyingi
za kut aka ki pengel e hi cho
kiwekwe zilitolewa, majadiliano
yakafanyika baina ya viongozi
wa Kiislamu na serikali, ikawa
mikikimiki, wakati wote huu
hakuna ki ongozi mkuu wa
nchi, Rais, makamu wake na
hata Waziri Mkuu alijitokeza
hadharani kulitolea ufafanuzi.
Siku za lala salama ndipo
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Jakaya Kikwete
akajitokeza hadharani katika
hali ya huzuni na unyenyekevu
mkubwa kuwalilia Waislamu
wajitokeze kujiandikisha kwenye
sensa.
Hoja kuu ya Rais Kikwete
katika kuwashawishi Waislamu
Kutoka sensa hadi Mahakama ya kadhi, mchezo ni ule ule
Na Yusufu Ahmadi
kuj iandikisha kwenye sensa
i ka wa kwa mba t a kwi mu
zitakazopatikana ndio zitatumika
katika kupata kitambulisho cha
uraia ambacho pia kitakuwa
kikitumika katika kupigia kura
katika chaguzi mbalimbali za
hapa nchini n.k.
Wapo walioitika wito kwa
kuhesabiwa baada ya ushawishi
wa Rais na kuhofia kutopata
vitambulisho vya uraia , na
wengine kwa hofu ya kuchukuliwa
hatua za kisheria kwani wapo
waliokamatwa kwa hatua za
kususia mchakato ule.
Baadhi ya watu nikiwemo
mimi, tulijiuliza wakati wote ule
wa vuta ni kuvute Rais alikuwa
wapi kulizungumzia jambo hili,
wapo waliosema aliwaachia
wasaidizi wake, hoja ikawa suala
lile lilikuwa ni zito na hata hivyo
wasaidizi wengi wa serikalini
hawaaminiki siku hizi, kwani
kauli zao nyingi zinazotolewa ni
za kugongana.
Mchakato ukapita japo wapo
ambao hawakujiandikisha katika
sensa , ndio maana baadhi ya
watu wanasema hata takwimu
zilizopatikana mfano wa idadi ya
watu kuwa tupo takribani milioni
45 zina kasoro kutokana na baadhi
ya Waislamu kususia.
Leo hii vitambulisho vya Uraia
vinatolewa, aliyehesabu sensa,
hakuhesabu wote wanapewa,
sijui tatizo lilitokea wapi mpaka
takwimu za sensa hazitumiki
katika zoezi hili kama ilivyoelezwa
na Rais Jakaya Kikwete katika
hotuba yake ile.
Kisa kama hicho nakilinganisha
na hiki cha Waziri Mkuu Pinda,
wakati huu ikiwa ni suala zima
la kuingizwa kwa mahakama
ya kadhi kwenye katiba mpya
ambapo Waislam walipiga kelele
sana mahakama hiyo kuwemo
ndani yake huku wengi ne
wakipinga hilo.
Kama ilivyokuwa kwa zoezi
la sensa, ndivyo imekuwa katika
mchakato wa katiba mpya ambapo
hoja mbali mbali kutoka kwa
Waislamu zililitolewa, mivutano
ikatokea ndani ya bunge maalum
la katiba kutaka kipengele cha
mahakama hiyo iingizwe kwenye
katiba.
Waislam wakatoa hoja nyingi
tu, moja wapo ni ile ya kwamba,
kutaka kwao mahakama ya
kadhi kuwemo kwenye katiba ni
kuwezesha hukumu zinazotolewa
na mahakama hiyo zinakuwa
na nguvu za ki sher i a pi a
zinaheshimiwa na mahakama
za kawaida, kwani ilionekana
hukumu hizo zikipelekwa katika
mahakama za kawaida zinakuwa
ni batili.
Muda wote huo wa mvutano
hakuna kiongozi mkuu yeyote
wa nchi aliejitokeza hadharani
kulitolea ufafanuzi, badala yake
Kama i l i vyokuwa kwa Rai s
Kikwete kujitokeza siku za lala
salama za sensa, ndio kafanya
Waziri Mkuu Pinda, kachomoza
hadharani kuzungumzia suala
hilo siku rasmi ya upigaji kura
kama nilivyosema awali.
Kwa mujibu wa Pinda, ambae
ofisi yake ilipewa jukumu la
kul i shughul i ki a sual a hi l o,
aliwaambia wajumbe wa Bunge na
Umma kwamba wamekubaliana
na Masheikh kuwa wataliingiza
sual a hi l o kati ka Sheri a ya
Mahakimu sura ya 11 na Sheria
ya Kiislamu sura ya 375 ambapo
zitafanyiwa marekebisho ili
kutambua uamuzi wa Mahakama
ya Kadhi.
Na kwa mba of i s i ya ke
inaenda kuzipitia sheria hizo
ili kuziboresha na kisha kuja
nazo katika Bunge la Januari
mwakani ili zijadiliwe na kupitiwa
na wabunge kabla ya kuwa sheria
rasmi baada ya Rais Kikwete kutia
saini yake.
Taarifa na ahadi ya Waziri
Mkuu inazua maswali kadhaa
na muhimu ya kujiuliza kwa
Waislamu wote, kwa nini Waziri
Mkuu kama alivyofanya Rais
Kikwete amejitokeza siku ya
kupigia kura katiba iliokuwa
inapendekezwa na Bunge, siku
zote za mivutano alikuwa wapi?
Waziri Mkuu kakiri kuwa suala
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
hilo limo ofisini mwake tangu
mwaka 2005 , sasa ni takribani
miaka saba imepita, ina maana
ofsi yake ilikuwa haijajua tatizo
liko wapi, wiki iliopita ndio kweli
wamefahamu kwamba kwa nini
Waislamu wanataka mahakama
ya kadhi kuwemo kwenye katiba?
Nai kumbukwe sual a hi l i
halijaanza katika utawala wa
awamu hii ya nne, tangu enzi za
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa
lilikuwepo na tume iliundwa, japo
Waziri Mkuu Pinda hakurejea
yaliokuwemo ndani ya tume ile
kujua sababu?
Je, tukisema lengo la Waziri
Mkuu Pinda lilikuwa nikulainisha
tu mioyo ya baadhi ya wajumbe
wa Kiislamu ambao walitishia
kupiga kura ya Hapana kama
mahakama ya kadhi isingeingizwa
kwenye katiba na badala yake
waipigie kura ya Ndio kuepusha
kukwama kwa katiba iliokuwa
i napendekezwa, t ut akuwa
t unakosea? J ambo ambal o
lilifanikiwa kwani walilainika
haswaa.
Je, ni kweli Pinda na serikali
yake wana ni a ya dhati ya
kuwapa Waislamu mahakama
ya kadhi ilio na meno makali
kama anavyosema, au na yeye
anasogeza siku tu mbele ili
amalize muda wake atue mzigo
chini amuachie atakaekuja?
Nimshauri na kumsihi Waziri
Mkuu Mizengo Pinda kama
alivyoambiwa pale Bungeni na
Sheikh Masoud Jongo kwamba
wao (viongozi wa dini ya Kiislamu)
hawawezi kubeba dhamira ya
Waislamu, kazi yao ni kushawishi
tu waumini wao.
Hivyo basi atambue kuwa nia
ya Waislamu kudai mahakama ya
kadhi yenye meno makali sawa
na mahakama zingine kamwe
haitakufa.
Kama tamko lile lilikuwa
ni geresha tu ya kuwafanya
wajumbe wa Kiislamu wapigie
kura ya Ndio ili katiba iliokuwa
inapendekezwa ipite, akumbuke
yeye atapita ila maandiko yatabaki
milele katika mioyo ya Waislamu
ikibeba wito wa mahakama ya
kadhi yenye uhai.
Ni ukweli sasa mahakama
ya ka dhi kwe nye ka t i ba
haiwezekani, na wanaosubiri
J anuari 2015 kwamba ndi o
watapata mahakama hiyo yenye
nguvu kwa kuwemo kwenye
sheria za kawaida, wasubiri tu,
kwangu mimi ni ndoto!
Si walisema Zanzibar itoke OIC
ili Tanzania ijiunge. Kiko wapi!
Kama hatutaamka na kutanabahi,
tutafanywa madaraja ya kupitishia
mambo ya wengine daima.
Ahsanteni.
11
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Makala
Inaendelea Uk. 13
Tumemeza al Qaida, ISIS
Boko Haram, al Shabab
Inatoka Uk. 9
al-Fadhli, posed a more direct threat
to America and Europe.
Inadaiwa kuwa huyu Muhsin
al-Fadhli, alikuwa mmoja wa
viongozi waandamizi wa al Qaeda
akiwa karibu sana na Osama
Bin Laden, na kwamba yeye ni
katika watu wachache waliokuwa
wakij ua mipango ya siri ya
shambulio la Septemba 11, 2001
kabla shambulio halijafanyika.
Pr o pa g a nda i l i e nde l e a
kukolezwa na mwandishi Richard
Engel wa NBC News akiungana
na Brian Williams, kuleta madai
ya adui mpya-The New Enemy,
ambapo Engel akidai kunukuu
vyanzo kutoka duru za kiusalama
za Marekani alisema kuwa:
Khorstan is considered a threat
to the U.S. because, U.S. intelligence
ofcials say, it wants to bring down
airplanes with explosives.
Akimaanisha kuwa maadui
hao wapya wana l engo l a
kulipua ndege za abiria na hivyo
wanakuwa tishio kwa Marekani.
Hebu soma nukuu zifuatazo:
The United States also pounded
a little-known but well-resourced
al-Qaeda cell that some American
officials fear could pose a direct
threat to the United States. (The
Washington Post)
Among the targets of U.S. strikes
across Syria early Tuesday was the
Khorasan Group. The group was
actively plotting against a U.S.
homeland target and Western targets,
a senior U.S. ofcial told CNN on
Tuesday. (CNN)
There were indications that the
militants had obtained materials and
were working on new improvised
explosive devices that would be hard
to detect, including common hand-
held electronic devices and airplane
carry-on items such as toiletries.
Osama Bin Laden.
(U.S. ofcial)
We hit them last night out of a
concern that they were geting close to
an execution date of some of the plans
that we have seen. (U.S.A Atorney
General Eric Holder.)
Ni meweka nukuu hi zi i l i
kutopotosha maana kwa tafsiri
kuonyesha kinachopikwa na
kupangwa hivi sasa. Tunaletewa
gaidi mpya Khorasan Group,
ambaye tunaambiwa kuwa huyu
ni kitisho cha uhakika na cha
sasa hivi kwa Marekani. Na
kwamba hao ni wataalamu wa
kutengeneza milipuko kulipua
ndege za abiria za Marekani na
Ulaya na kwamba wanaweza
kuingia na milipuko hiyo katika
ndege bila kutambulika kutokana
na walivyoitengeneza kitaalamu!
Kinachotafutwa hapa ni kile
tulichoeleza mwanzoni. Moja,
kitisho hicho kitawafanya watu
wa Marekani kuiunga mkono
serikali yao.
La pili, ni kujenga mazingira ya
kupata kibali kutoka Umoja wa
Mataifa kama kilivyopatikana kile
cha kuipiga Afghanistan. Kama
mkakati huo utaonekana kuwa
utazaa matokeo yanayotakiwa,
hapana s haka ut aendel ea
kupigiwa debe mpaka na sisi
huku tutaimbishwa. Vyombo
vya usalama vitakwenda mbio
kuwasaka Khorasan Group. Na
si ajabu zikawekwa taratibu mpya
za ukaguzi wa usalama katika
viwanja vya ndege. Hiyo ikiwa ni
pamoja na kulazimishwa kuweka
mitambo mipya itakayoamuliwa
na mabeberu na tutainunua kwa
bei watakayoweka mabeberu.
Ukiacha ndege zinazuiwa kutua
katika viwanja vyako. Mabeberu
wananeemeka.
Lakini usije ukashangaa pia
kukuta vi j ana wa Ki i sl amu
waki shabi ki a kuwa wao ni
Muj ahi di na wa Khorasan
Group. Unajua sababu yake nini?
Khorsan ni j i na l a eneo
la kihistoria linalounganisha
Kaskazini mwa Iran, Turkmenistan
ya Kusini na Kaskazini mwa
Afghanistan. Ni eneo lililokuwa
toka utawala wa Sasania kule
Iran (Sasanian dynasty), jina
hilo likimaanisha (Ardhi ya Jua)
kwa vile ilikuwa upande wa
Mashariki wa utawala huo. Wakati
wa utawala wa Kiislamu chini ya
Umayyah (Umayyad Caliphate),
Khorsan ilikuwa moja ya maeneo
ya utawala huo iliyostawi sana. Ipo
Hadith yenye utata ambayo inadai
kuwa Mtume (s.a.w) alitabiri
Inatoka Uk. 13
Mauaji kushoto kulia
Inatoka Uk. 9
ya ubeberu. Hili tukilifahamu,
nadhani tunaweza kuwa makini
zaidi tusije kuwa vibaraka na
mamluki wa kuangamiza nchi
zetu kwa mikono yetu wenyewe
tukidhani tunapambana na ugaidi.
Haihitaji kuwa razini
sana kufchua uwongo
Labda tuj iulize, hivi kuna
mt u mwenye aki l i t i mamu
anayeamini yale tuliyoambiwa
juu ya Westgate Kenya au zile
porojo za Bring Back Our Girls
kule Nigeria? Wasichana 270
wamepotelea porini mpaka leo
hawajapatikana-nchi ambayo ina
serikali, polisi, usalama wa taifa
na jeshi!! Usanii wa ki-Hollywood
uliovunja rekodi. Hivi wataalamu
wetu, wanausalama wetu na
viongozi wetu, wanapokutana
(au pengine tutumie maneno
wanapokutanishwa na hawa
viranja wa vita dhidi ya ugaidi
duni ani ) kuj adi l i mambo
yanayofanana na porojo hizi
za Bring Back Our Girls na
kisha kuibuka na kauli kalikali,
wanajisikiaje?
Tuache kuisingizia
mambo Quran, Suna
Jambo la pili linalojitokeza
katika hoj a zinazotolewa na
baadhi ya Waislamu, inaonesha
kuwa wengi wanaojidai kufuata
Quran na Sunna au kuja na hoja
kuwa jambo fulani halipo katika
Quran na sunna, hata hiyo Quran
yenyewe hawaisomi au kama
wanaisoma, huisoma kibubusa.
Inadaiwa kuwa Boko Haram
na IS wanataka kusimamisha
Khilafah, kwa maana ya Dola
ya Ki i sl amu. Laki ni taari fa
tunazopewa kupitia vyombo
vya habari na kupitia mitandao
yao, ni za utekaji nyara, mauwaji,
kuchinja watu, iwe ni Wakristo
au Wai sl amu wanaodai wa
kutokukubaliana nao. Ukiacha
taarifa za vyombo vya habari, kuna
video mbalimbali zinarekodiwa
na wanaodaiwa kuwa viongozi wa
Boko Haram na IS wakitoa taarifa
za harakati zao wakithibitisha
kuwa wamefanya mauwaji haya
na yale na kutoa picha za watu
waliowauwa.
Katika tukio la kutekwa mabinti
wa shule Nigeria, anaonekana
anayedaiwa kuwa kiongozi wa
Boko Haram, Abubakar Shekau
akiwa kasimama na bendera yenye
maandishi ya kalima tawheed
akitangaza kuwa wasichana
aliowateka amewasilimisha kwa
nguvu na kutishia kuwauwa
wanaokataa kusilimu. Kwa IS
ni hivyo hivyo, wanarekodi
picha za video wakichinja watu
na kuziingiza katika mtandao
wakidai ni katika harakati zao za
kusimamisha Khilafah.
Kuna namna mbi l i t u za
kuzipokea habari hizi. Moja, ni
kuamini kuwa yaliyosemwa ni
kweli. Ukijaaliya hivyo, sasa jiulize
je, mambo haya yanakubalika
katika Uislamu? Kwamba katika
kusimamisha Khilafah, unapita
mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji,
mji kwa mji, ukiuwa na kuchinja
watu? Jibu ni hapana.
Namna ya pili ni kujaaliya kuwa
hata kama kuna watu wanajiita IS
wenye lengo la kusimamisha Dola
ya Kiislamu, lakini sio wanaofanya
vitendo hivyo. Wanasingiziwa
tu. Ukijaaliya hivyo, lazima uje
na taarifa mbadala ukionyesha
wanachosema na wanachofanya
IS. Mpaka sasa hakuna taarifa hata
moja kutoka IS inayowaonyesha
wakikanusha kuwa wao sio
wanaofanya mauwaji hayo na
wala zinazoonyesha mambo
mazuri wanayofanya katika
miji waliyodaiwa kuteka. Ila
kilichopo ni taarifa zao wenyewe,
zikiwemo za video walizojirekodi,
wakithibitisha kufanya mauwaji
hayo. Laki ni pi a uki j aal i ya
kuwa taarifa hizo ni uwongo,
akili ya kawaida tu itakutuma
kujua kuwa majina haya kama
IS na madai ya kusimamisha
Khilafah yakiambatanishwa na
matendo mabaya ya mauwaji
ya kikatili, yanatumiwa kama
propaganda ya kuupaka matope
Uislamu na kuutafutia sababu
ya kuuangamiza. Kwa hiyo,
haitakuwa busara kushabikia
msamiati huo.
Sasa leo anapoibuka Muislamu
na kuja na hoja kuwa IS/Boko
12
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
12
Makala/Mashairi/Tangazo
Inatoka Uk. 6
Masheikh wapo Golgotha
kama ilivyokuwa Sodoma
na Gomora, ujumbe huo
aliousoma Rais Bush, ni
muhimu sana hasa kwa
vile ndio uliokuwa ujumbe
wa utangulizi kabla ya
Mungu kuziangamiza
Sodoma na Gomora.
Hivyo bila shaka ni ishara
nyi ngi ne ya Mungu
kuangamiza tena kizazi
hiki kiovu na uovu wake.
(Kizazi kiovu hapo ni
Wairaki, Waislamu na
Uislamu wao.)
Mchungaji Teghua
anachokieleza hapo
ni i mani yao kama
Wakri sto Wal okol e,
kuwa wa- I r aki na
Waislamu popote walipo
wanaonekana katika
imani na macho yao
kuwa ni mapepo yaani
mashetani, hivyo ni wa
kuangamizwa kama
wal i vyoangami zwa
watu wa Sodoma na
Gomor a, na Bus h
( Ma r e k a n i ) n d i o
kachaguliwa kufanya
kazi hiyo.
Ni vizuri ninukuu zile
aya ambazo Rais Bush
alizisoma, na mchungaji
akazinukuu kwa kifupi
ili msomaji asiye na
Biblia aelewe mtazamo
na malengo ya Mlokole
Bush, wachungaji na
Crusades zao:
Ki s h a wa t u ha o
wa k a o n d o k a h u k o
wakaelekeza nyuso zao
Sodoma. I br amhi mu
akaenda pamoj a nao
awasindikize. BWANA
(Mungu) akasema, Je!
Ni mf i che I brahi mu
jambo hili nilifanyalo?
Akiwa Ibrahimu atakuwa
tai f a kuu, hodari na
katika yeye mataifa ya
duni a watabari ki wa?
Kwa maana nimej ua
yakwamba atawaamuru
wanawe, na nyumba
yake baada yake waishike
njia ya BWANA wafanye
haki na hukumu, ili
kwamba BWANA naye
akamtimizie Ibrahimu
ahadi zake. (Mw. 18:16-
19).
Tuj iulize, maneno
hayo hapo j uu, kwa
mujibu wa imani ya
Wakristo, yameandikwa
na Nabii Musa A.S. na
yamepitia kwa manabii
wengi wa wana wa
I srael i , na di ni ya
Kikristo inatokana na
msingi wa kitabu cha
Torati, na Rais Bush na
Mchungaji Teghua ni
wafuasi wa Neno la
Mungu tena walokole,
kwa maana ya kuwa
h a wa n a d h a mb i ;
Je! Kuishika njia ya
BWANA (Mungu) ndio
huko kuwaangamiza
wa Iraki na Waislamu
katika nchi zao?
I n a v y o o n e k a n a
k i n a c h o w a s i b u
W a i s l a m u n a
Masheikh duniani kote
wanaobambi ki wa
t uhuma za ugai di
kisha kudhalilishwa
kwa mateso na hata
kunajisiwa na matendo
mengine ya kishenzi, ni
katika muendelezo wa
vita ileile iliyoasisiwa
na Albano, akina Bush
ni warithi tu.
Ni Golgotha ileile
ya Warumi. Unamtesa
mtu, huridhiki mpaka
unamtia majiti sehemu
zake za siri!!!
P.O. BOX 80059, TEL: 022-2860694, 0754/ 0655-462777, 0754-377897
DAR ES SALAAM (TZ)
QURAN, TAALUMA , MAADILI.
PRE-FORM-ONE 2015.
MASOMO YATAANZA TAREHE 14/10/2014 (SIKU YA INTERVIEW) HADI
14/12/2014.
MASOMO YATAKAYOFUNDISHWA NI QURAN, MATHEMATICS,
MAARIFA YA UISLAM NA KIINGEREZA.
WANAFUNZI WATAKAA BWENI (BOADING).
MAHITAJI: MAVAZI YA KIISLAM, MADAFTARI (HARD COVER), MAS-HAF
AU JUZUU NA MAHITAJI YA KUMUWEZESHA KUKAA BWENI.
ADA KWA MUDA WOTE HUO NI T.SHS 200,000/= TU.
KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA DARASA LA SABA (7) DAARUL-
ARQAM SCHOOLS WATASOMA BURE.
USAILI (INTERVIEW) 2015.
USAILI KWA WANAFUNZI WA SHULE YA AWALI, MSINGI NA SEKONDARI
(2015) ITAFANYIKA SHULENI DAARUL ARQAM KIGAMBONI DSM
JUMANNE TAREHE 14/10/2014 (NYERERE DAY) SAA 2 ASUBUHI. FORM NI
TSHS 10,000/= TU.
SIMU 0717 190 242 AU 0658 190 079.
DAARUL ARQAM SCHOOLS
Leo siku ashirafu, ARAFA iso na shaka,
Mahujaji twawashufu, ALLAH wakimuitika,
Uwanja mtakatifu, "Allahumma labbaika",
ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.
Kutwa nzima watakifu, hapo pasipo kutoka,
Ndaniye itasadifu, jua likishapinduka,
Khutba njema zindufu, thuma swala kuswalika,
ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.
Kasi DHIKIRI sharifu, baadiya zitashika,
Na kumuomba RAUFU, MAGHFIRA kadhalika,
Pamwe na DUA lufufu, mpaka kughurubika,
ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.
ARAFA siku tukufu, kwa walo ndani ya Makka,
Watangaa utukufu, wake na nje ya Makka,
Kwa FUNGA tuusharifu, nasi tusokuwa Makka,
ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.
Tufanye udunduifu, wa fedha nasi kuweka,
Kabla ya wetu ufu, tuweze hijja kufka,
Kaditama kualifu, chini kalamu naweka,
ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.
Tuisharifu kwa FUNGA, siku hii ashirafu.
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.
ARAFA (TUISHARIFU KWA FUNGA)
IDD ! (SALAMU ZA IDD)
Natakadamu za IDD, salamu zipokeeni,
Kesho wala si baidi, nadharini tambueni,
Tutakuwa kwenye IDD, kwa utashi wa MANANI,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Salamu zangu za IDD, vyema zizingatieni,
Kuzitoa sina budi, kuzindua ikhiwani,
Katika yote biladi, ya Bara na Visiwani,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Sinazo tumbi zawadi, za nyote kukutosheni,
Kwa timilifu idadi, yenu pasi nuksani,
Kwa hiyo nimeadidi, badala cha kukupeni,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Chazidi hata nukudi, na vito vyenye thamani,
Si lulu wala zabadi, kadhalika marijani,
Kwa ukumbusho wa IDD, vyote havioni ndani,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Mwapaswa siku ya IDD, kutambua nadharini,
Kwa nuru ya tauhidi, si kwa kiza cha shetani,
Kwamba kwetu sisi IDD, si siku ya kufurani,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Kwa hiyo hapana budi, ALLAH tumdhukuruni,
Takbira na nyiradi, masnunu tuleteni,
Kwa wingi tumhimidi, sikuyo kwa shukurani,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Tusijevuka hududi, kwa kumuasi MANANI,
Kwa twaa tujitahidi, kumtii RAHMANI,
Pamwe na kuikalidi, ruwaza yake Amini,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
IDD siku ajwadi, kwa twaa furahikeni,
Kadhalika mawaridi, majumba yenu pambeni,
Yumkini hata nyudi, kwa ndani yafukizeni,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Maakuli kuadidi, fanzeni hima nyumbani,
Vinywaji kuvifanidi, vya halali sharibuni,
Sharubati za kutadi, mipaka ziepukeni,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Libasi zenu jadidi, za stara valieni,
Jitanibuni na jadi, ya kujivika vimini,
Nanyi Abuu na Iddi, kata 'kei' ziacheni,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Zingatieni hududi, ya flamu runingani,
Kushufu picha za 'nyudi', si wetu utamaduni,
Kikoa tuzikaidi, 'ponograf' kwa kani,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Kadhalika ukuwadi, wa fulani kwa fulani,
Nayo siyo yetu jadi, kuunganisha wahuni,
Wanomuasi WADUDI, kwa zinaa pasi soni,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
IDD ni siku saidi, si ya kwenda uzinzini,
Wala si ya kufsidi, ajisadi ulevini,
Au ya shari kuzidi, na kukesha madansini,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
'Kiasi siku ya IDD, ja kwamba mahasharini,
Ikabuyo i shadidi, akhera yaumu-dini,
Juludiyo 'tajadidi, iyeyukapo narini,
Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.
Sinayo mengi zaidi, kwa twaa sururikeni,
Ikiwa bado ahadi, tutakutana mwakani,
Khamsashara sizidi, kalamu naweka chini,
Salamu zidurusuni, za IDD kwa irishadi.
ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.
13
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
MAKALA/TANGAZO
Tumemeza al Qaida, ISIS Boko Haram, al Shabab
Inatoka Uk. 11
akisema kuwa Bendera Nyeusi
zitasimama kutokea Khursan na
hakuna atakayeweza kuzizuiya
mpaka zisimamishwe pia Ayliya
(Bayt al-Maqdis).
Hadi t h hi yo i nayodai wa
kusi mul i wa na Ahmad, at -
Tirmidhi na Nu'aym ibn Hammad,
inadaiwa kusimuliwa na Abu
Hurayrah.
Kwa kuwepo Hadith hii, hapana
shaka utaona kuwa makafiri
mabeberu wamefanya kazi yao
vizuri. Wanajua kuwa vijana wa
Kiislamu watashabikia jina hili
Khorsan kwa vile lipo katika
Hadith inayotabiri kuwa Uislamu
utasimama kuanzia mahali hapo.
Na ndio maana unaona pia hata
bendera za ISIS ni nyeusi zikiwa
na Kalma Tawheed.
Muhi mu hapa si o kuwa
Hadith hiyo ni sahihi au la, lakini
mambo manne. Moja ni kuwa hao
Khorasan Group hawapo Syria
na hata kama wakitokea kuwepo
watu wakijiita jina hilo, watakuwa
wa kupanga kama yule mtoto
na kigeleni chake cha mafuta ya
taa aliyedaiwa kutaka kulipua
Ubalozi mmoja maarufu Jijini Dar
es Salaam.
Pili, magaidi hawa wapya
wanabuni wa i l i kut af ut a
kisingizio na sababu ya mabeberu
kuendeleza vita yao Syria ili
kumngoa Bashar Assad (another
regime change).
Tat u, makaf i r i hawal al i
na wanapopanga mambo yao
hufanya utafti na kulenga mahali
na kwa namna ambayo kama
akili hazikutumika, inakuwa
vigumu sana kutambua kwa
haraka ulaghai wao. Tizama
walivyochagua jina Khorasan
lililotaj wa katika Hadith ya
Abu Huraira kuwa ndio mahali
bendera ya Uislamu itakapoanza
kusimama!
Nne, baadhi ya watafti kama
Will McCants wa Brookings
Institute, anasema kuwa utabiri
huu unahusu mapinduzi ya
wakati wa Abbasid karne ya 8
(Abbasid revolution), mapinduzi
yaliyoanzia Khorasan, ambapo
himaya ya Waarabu iliporomoka,
utawala wa Kiislamu ukawa
mi kononi mwa wasi okuwa
Waarabu. Lakini hata ukijaaliya
kuwa Hadith hiyo ni sahihi na
inatabiri kuibuka upya kwa
utawala wa Kiislamu katika
zama hizi, bado ukweli utabaki
kuwa hao Khorasan Group
hawapo hivi sasa na hawana huo
ujuzi wanaodaiwa kuwa nao wa
mabomu yanayotishia usalama
wa ndege za abiria za Amerika
na Ulaya.
Mauaji kushoto kulia
Inatoka Uk. 11
Haram, wana l engo zuri l a
kusimamisha Uislamu wasisemwe
vibaya, lazima mtu uhoji uwezo
wa akili ya mtu kama huyo. Ni
kama vile katika baadhi ya kesi
mahakamani hutokezea zikafutwa
kama watu watatuhumu kama
mtuhumiwa hayuko barabara
kiakili na dakitari akathibitisha
hilo. Ila sasa kwa muktadha huu,
jambo hili si jepesi kiasi hicho
kwa sababu madhara yake ni
makubwa mno kijamii. Waislamu
wasi wachukul i e watu hawa
kuwa ni maadhura wakawaacha,
ni lazima watafute namna ya
kuwatibu na kuhakikisha kuwa
hawaleti madhara kwa jamii ya
Waislamu na nchi kwa ujumla.
Hawa watakuwa wamefkishwa
mbali. Watakuwa wamekorogwa
vya kutosha na wale akina Abu
Fulani, walioachiwa wakafanya
kazi yao ya uwakala, baadae
ndio tunakurupuka kuendesha
operesheni za kuwasaka na
kuwakamata!!!
Wapo wasomi waliotimiza
wajibu wao, siri wamefchua
Wasomi na watafiti wengi
wameandika sana juu ya hatari
ya hawa mawakala na vifaa vya
mabeberu-IS na Boko Haram.
Lakini unapowanukuu katika zile
tahadhari zao wanazotoa, baadhi
ya vijana wetu, watakuambia
kuwa unanukuu makafri badala
ya kuleta ushahidi wa Quran
na Sunna. Namna yake ni
kama unakutana njiani na John
anakuambia ndugu yangu, hapo
mbele kuna joka kubwa au kuna
vibaka usipite, unasema mimi
sisikilizi la kafri nafuata Quran
na Sunna! Sasa huu ni ujinga
na kuisingizia Quran. Niliwahi
kutoa mfano nikasema kuwa
wanaotoa hoja hizi wachukue
sumu ya cynide au sumu yoyote,
watizame maelezo yake, wakiona
kuwa anayetoa tahadhari juu ya
sumu hiyo sio Muislamu na wala
maelezo ya sumu hiyo hayapo
kwenye Quran na Sunna, basi
wanywe.
Nihitimishe kwa kusema kuwa
ukitizama hoja nilizozijadili hapa
kama zinavyotolewa na baadhi ya
vijana wa Kiislamu, zinabainisha
mambo makubwa matatu. Moja
ni kuwa mawakala wa mabeberu
makafiri, wamefanikiwa sana
kutukoroga, sasa wanavuna. Kwa
upande mmoja wamefanikiwa
kupandi ki za f i kra pot of u,
sasa Waislamu wanakorogana
wenyewe kwa wenyewe. Pili,
baada ya kuchanganyikiwa huko,
sasa Wai sl amu wanatumi ka
kumal i zana wenyewe kwa
wenyewe kwa manufaa ya kafri.
Wanauwana Syria, Libya, Iraq na
kwengineko. Wamefanikiwa pia
kupandikiza kitisho cha ugaidi
katika nchi zetu, sasa baadhi ya
watu wapo ndani wakisubiri
kesi zao huku kukiwa na madai
ya kudhal i l i shwa Mashei kh
waliounganishwa katika kesi hizi.
Tatu, ni kuwa mjadala huu
unaonye s ha kuwa uj i nga
miongoni mwetu ni mkubwa
sana. Mtu anakuja na hoja kuwa
hawezi kusikiliza la kutoka kwa
kafiri, lakini kavaa kilemba,
kaptura na kanzu iliyotengenezwa
na elimu (kutoka kwa Allah)
iliyofanyiwa utafti na ugunduzi,
ama na Muislamu au wasio kuwa
Waislamu ikawezesha kupatikana
mitambo ya kucheza na Pamba ya
Msukuma mpaka ikatoa nguo.
Lakini kavaa kilemba na kanzu
au kikoi, ambavyo vingi vinatoka
China, Thailand, Indonesia na
nchi zisizokuwa za Waislamu.
Badala ya kuhimiza Waislamu
kusoma taaluma hizi ili hatimaye
viwanda kama vya nguo na
vitu mbalimbali vizalishwe na
Waislamu, ili kukuza uchumi
wa Waislamu; unakuja na hoja
lemavu za kusema elimu ni za
kikafiri ambapo maana yake
ni kuwa utaendelea kununua
kanzu na pensi yako (suruali fupi
ya kufika magotini ila kidogo),
ki l emba na ki zi bao kut oka
viwanda vya makafri na hivyo
kuzidi kuwatajirisha!
Au t us e me mwi s ho wa
mawaidha haya ya elimu za
ki kafi ri ni kuvua na nguo
z i l i z ot oka na na t a a l uma
(zinazosingiziwa kuwa) za kikafri
na kutembea uchi?
14
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Makala
Uchakachuaji wa Aqida ya Kiislamu - 2
Na Said Rajab
KAMA tulivyoona kwenye makala ya
mwanzo, uwepo wa fikra za kikafiri
kwenye jamii, umekuwa kikwazo
kikubwa katika njia ya kuhuisha dini
ya Mwenyezi Mungu. Na kuongeza
chumvi kwenye ki donda, f i kr a
hizo zinasimamiwa na kunezwa na
wanaharakati wa Kiislamu na makundi
yao. Wakati umefika kwa Waislamu
wenye ufahamu, walio waadilifu na
wanaomuogopa Mwenyezi Mungu,
kuendesha harakati za kusimamisha
Uislamu kama alivyofanya Mtume wa
Mwenyezi Mungu. Waondoe fkra hizo
potofu kutoka kwenye nyoyo na fkra za
Waislamu. Wale wanaolingania Uislamu
kama vitendo binafsi vya Ibada (rituals)
lazima wafahamishwe na waelewe
kwamba Uislamu ni mfumo kamili wa
maisha na dini iliyokusanya nyanja zote:
"Si maneno yaliyozuliwa, bali ni hakikisho
la yale yaliyokuwa kabla yake (miongoni mwa
vitabu vingine vya Mwenyezi Mungu) na ni
maelezo juu ya kila kitu..." Qur(12:111).
"Na tumekuteremshi a Ki tabu hi ki
kielezacho kila kitu..." Qur(16:89)

Na lazima Waislamu wazingatie
kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu
ametuagiza kuuchukua Uislamu wote
kama ulivyo na siyo vipande vipande, na
tena amewalaani Waislamu wanaofanya
hivyo:
"Enyi Mlioamini! Ingieni katika hukumu
za Uislamu zote,wala msifuate nyayo za
Shetani; kwa hakika yeye kwenu ni adui
dhahiri" Qur(2:208).
"Je? Mnaamini baadhi ya Kitabu na
kukataa baadhi (yake)? Basi hakuna malipo
kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila
fedheha katika maisha ya dunia; na siku ya
Kiyama watapelekwa katika adhabu kali".
Qur(2:85).
Wai sl amu wanakat azwa kabi sa
kuugawa Uislamu na kuweka vipaumbele
vya kanuni za Kiislamu kwa kuzingatia
akili zao wenyewe au maslahi yao.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ndi ye
anayeweka kanuni za Kiislamu na
kuonyesha ipi iwe ya kipaumbele na ipi
ifuatie.
Wai sl amu wakumbushwe j i nsi
masahaba walivyoingia kwenye Uislamu
na jinsi walivyokubali na kuvifanyia kazi
vipengere vyote na kanuni za dini hii
tukufu ya Mwenyezi Mungu. Waislamu
wafahamishwe kwamba haiwezekani
kuwa Muislamu mzuri au "kujenga Imani
ya Muislamu" bila kuwa watiifu kwa amri
za Mwenyezi Mungu kwanza.
Kwa hiyo, kutii amri ya kusimamisha
Swala ni sawa kabisa na kutii amri ya kutoa
Zaka au kumkata mkono mwizi. Vile vile
kumtii Mwenyezi Mungu kwa kusema
ukweli ni sawa kabisa na kumtii katika
ukusanyaji kodi au kusimamisha sheria
yake katika ardhi. Mwenyezi Mungu
atatuadhibu kwa kuacha Swala au kusema
uongo kama vile atakavyotuadhibu
Waislamu kwa kukubali kutawaliwa
kikafri.
Na wale Waislamu wanaoshabikia
fkra ya kupata faida kama kigezo cha
kutenda mambo, lazima waeleweshwe
vizuri kwamba Uislamu una namna ya
kipekee sana ya kuiangalia faida au tija.
Uislamu unaelekeza kwamba faida au tija
inazunguka kwenye kanuni za Mungu.
Popote palipo na Uislamu wa kweli, basi
faida inapatikana na siyo kinyume chake.
Waislamu wanawajibika kutekeleza
amri za Uislamu, bila ya kuzingatia faida
itakayopatikana au madhara. Faida ni
ile iliyobainishwa na Mwenyezi Mungu
kupitia Sheria zake na siyo fkra zenye
kikomo za kibinadamu.Kwa maneno
mengine, faida kwa Muislamu inapatikana
kwa kumtii kiukweli Mwenyezi Mungu,
ikiwa ni pamoja na kuukumbatia Uislamu
wote. Mwenyezi Mungu anasema:
"Mmelazimishwa kupigana vita (kwa ajili
ya dini). Nalo ni jambo zito kwenu. Lakini
huenda mkachukia kitu, nacho ni kheri kwenu.
Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari
kwenu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua,
lakini nyinyi hamjui" Qur(2:216).
Aya hi yo ya Mwenyezi Mungu
inabainisha wazi kwamba Yeye ndiye
anayeweka sheria na utaratibu wa
vitu ambavyo vinaweza visionekane
kama faida kwa macho ya kibinadamu,
na kwamba Waislamu wanawajibika
kutekeleza sheria na taratibu hizo, bila
ya kuzingatia mtazamo wao kuhusu
sheria hizo.
Kwa kuongezea, Aya hiyo ya Mwenyezi
Mungu inabainisha wazi kwamba uwezo
wa kuamua lipi jema na baya, au lipi ni
sahihi na potofu, au lipi ni haki na lipi
batili, unazidi ule wa kibinadamu. Aya
nyingine inasisitiza zaidi jambo hili:
"Na kama Haki ingelifuata matamanio yao
(kama wanavyotaka), zingeliharibika mbingu
na ardhi na vilivyo ndani yake" Qur(23:71)
Waislamu wanapaswa kuziangalia
hukumu za Kiislamu kama ndiyo
hukumu pekee zilizo sahihi na za haki,
ikiwa ni pamoja na kuzifuata kikamilifu
kiakili, kihisia na kimwili. Hakuna faida
inayoweza kuonekana kwa macho ya
kibinadamu katika kuifuata Hadithi hii
ya Mtume wa Mwenyezi Mungu:
"Jihad iliyo bora zaidi ni kumwambia
ukweli mtawala dhalimu" (Muslim)
Waislamu wanapaswa pia kuwaangalia
Ma s a ha ba wa ka t i wa l i pokuwa
Abissiniyah mbele ya Mfalme Mkristo,
wakitakiwa kutoa maelezo kuhusu Nabii
Issa (as). Baada ya kujadiliana kidogo, jibu
lao lilikuwa wazi:
"Sisi tutasema kile ambacho Mtume
wetu ametuambia kuhusu Issa (as)"
Ha wa kuj a l i ka bi s a kwa mba
wanazungumza na Mfalme Mkristo na
anaweza kujisikia vibaya. Walisema vile
ambavyo Uislamu unamuangalia Nabii
Issa (as).
Kama vile walivyokuwa Masahaba,
Waislamu hatupaswi kabisa kutanguliza
maslahi binafsi wala kuangalia faida
itakayopatikana au kuogopa misukosuko
inayoweza kutokea, pale tunaposimamia
misingi ya Dini ya Mwenyezi Mungu.
Kama kuna faida katika Uislamu, basi
faida hiyo ni kuingia peponi na kuepuka
moto wa Jehanamu. Faida hiyo haipatikani
isipokuwa kwa kuukubali Uislamu na
kuufuata kwa ukamilifu wake:
"Kila nafsi itaonja mauti. Na bila shaka
mtapewa ujira wenu kamili siku ya Kiyama.
Na aliyewekwa mbali na moto na akaingizwa
Peponi, basi amefuzu (amefaulu kweli kweli).
Na maisha ya dunia (hii) si kitu ila ni starehe
idanganyayo (watu)" Qur(3:185)
Wanaharakati wa Kiislamu hapa
nchini na maeneo mengine ya dunia,
wanatakiwa kuweka mazingatio yao
kwenye harakati tu za kusimamisha
Dini ya Mwenyezi Mungu, bila ya kujali
zawadi ambazo watapata, ili waache
ajenda hiyo na kuwa sehemu ya mfumo
unaopinga Uislamu.
Na wale wanaotaka kuunda mgogoro
kati ya dini na akili, kama ilivyo kwenye
Ukristo, lazima waufahamu Uislamu
kuwa ni Dini ya ulimwengu. Mara
matumizi ya akili yanapoondolewa, basi
kunakuwa hakuna hoja ya kuwalingania
watu kwenye Uislamu. Bila ya matumizi
ya akili, ili kufika kwenye ukweli na
kuthibitisha uhalisia wake, Uislamu
utakuwa kama Ukristo au Ubudha tu.
Waislamu hawatajua kwa uhakika
uwepo wa Muumba wao, usahihi wa
Kitabu chao au kuaminika kwa Mtume
Muhammad (saw).Bila ya uhakika katika
Aqida ya Kiislamu, msingi wa Uislamu
utakuwa dhaifu na wenye kutiliwa shaka,
ambapo mawazo potofu yatauchukulia
kama hauna uwezo wa kushughulikia
matatizo ya binadamu.
Kutumia akili hakuna maana kwa
namna yoyote ile kuipa akili mamlaka
yote. Uislamu umeainisha kwa uwazi
kabisa nafasi ya akili kwamba siyo
yenye maamuzi ya mwisho, na wala
isichukuliwe kama haipo. Kutotumia
akili kabisa katika masuala ya Dini
kunagongana na uhalisia wa Aqida ya
Kiislamu na ukweli kwamba Aqida hiyo
imezingatia matumizi ya akili.
Ndani ya Qur'an, kuna Aya nyingi sana
za Mwenyezi Mungu zinazozungumzia
"Ulil Albab", "Ulin Nuha" na "Ulil
Absar", ambazo zinawataka wafkiri na
kutafakari kwa kina kuhusu ulimwengu
huu, ili wafke kwenye ukweli kwamba
uliumbwa na Mwenyezi Mungu na Yeye
tu ndiye anayepaswa kuabudiwa. Allah
(sw) anasema:
"Je! Hawawatazami ngami a j i nsi
wal i vyoumbwa? Na mbi ngu j i ns i
z i l i vyo i nul i wa ? Na mi l i ma j i ns i
i l i vyot hubut i shwa? Na ardhi j i nsi
ilivyotandazwa? Qur(88:17-20).
"Na kama ukiwauliza, "Ni nani aliyeumba
mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi"?
Bila shaka watasema, "Mwenyezi Mungu"
Wapi basi wanapogeuziwa?" Qur(29:61).
Mwenyezi Mungu pia amewaamrisha
watu kufikiri kuhusu muuj iza wa
Muhammad (saw), yaani Qur'an Tukufu:
"Na kama mna shaka kwa hayo
tuliyomteremshia Mtumwa Wetu, basi leteni
sura moja iliyofanywa na (mtu) aliye mfano
wake, na muwaite waungu wenu bighairi
ya Mwenyezi Mungu (wakusaidieni), ikiwa
mnasema kweli" Qur(2:23).
"Je! Hawaizingatii hii Qur'an?Au katika
nyoyo zao kuna kufuli?!"Qur(47:24).
Kwa hiyo, Uislamu unawataka watu
wafikiri kuhusu uwepo wa Mwenyezi
Mungu na Utume wa Muhammad
(saw), ili kufika kwenye ukweli halisi
kwamba Aqida ya Kiislamu ni sahihi.
Mara mtu anapofkia hitimisho hili na
kuamini Uislamu, Qur'an inadhibiti
matumizi ya akili, kama nyenzo ya
kufahamu maandiko ya Mwenyezi
Mungu, lakini siyo kuamua kuhusu
uhalali au usahihi wake. Mawazo ya
Muumini lazima yasalimu amri kwa
sheria za Muumba zilizopo ndani ya
Qur'an na Sunna. Mwenyezi Mungu
anawataka wale waliokubali imani hii
(Uislamu) wanyenyekee na kusalimu
amri:
"Enyi Mlioamini! Mtiini Mwenyezi
Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka
juu yenu. Na kama mkikhitilafana juu ya jambo
lolote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu
na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi
Mungu na siku ya mwisho"Qur(4:59).
"Naapa kwa (haki ya) Mola wako. Wao
hawawi wenye kuamini (kweli kweli) mpaka
wakufanye (wewe ndiye) hakimu (mwamuzi)
katika yale wanayotofautiana, kisha wasione
uzito nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyotoa
na wanyenyekee kabisa"Qur(4:65).
Nimejaribu kufafanua uhalisia wa
akili kwamba inatofautisha vitu ambavyo
vinaweza kuhisiwa na milango ya fahamu
na kueleweka. Akili inajua sifa za vitu
kama vilivyo, kwa mfano ulimwengu huu
una Muumba wake, Muumbaji huyo ni
wa milele, au usahihi wa utume kwa yule
ambaye bishara zinamuelekea.
Lakini si kazi ya akili kuifanya nyama
ya nguruwe iwe haramu au halali, au
nyama ya mbuzi iwe halali au haramu,
au Swala ya Dhuhr iwe na rakaa nne
na Maghrib rakaa tatu. Hakuna nafasi
ya akili hapo! Si kwa kuamrisha wala
kuzuia. Kazi ya akili ni kuelewa tu amri
za Mwenyezi Mungu zinataka nini na
kufuata, siyo kuhoji kwanini ziko hivyo.
Na kwale wanaoshindwa kutambua
ukweli kwamba watawala wa nchi za
Waislamu ni mawakala wa Makafiri,
hilo halihitaji mjadala mrefu kuthibitisha
vinginevyo. Matukio kama ya kuuawa
kwa Waislamu katika nchi za Palestina,
Iraq, Afghanistan, Pakistan, Yemen, Libya
na Somalia, bila ya wao kuchukua hatua
yoyote ya kuwanusuru inathibitisha hilo.
Mbaya zaidi ,watawala hawa mara
zote wamekuwa upande wa maadui
kuwaangamiza Waislamu wenzao. Au
kama hilo halitoshi, basi angalia historia
zao kwa kina, mawazo wanayolingania
katika umma, na jinsi wanavyoshirikiana
na Mabeberu wa Magharibi katika
kueneza Kufru na kukandamiza mwamko
wa Kiislamu miongoni mwa Waislamu
nchini mwao.
Hata mitaala ya elimu wanayotayarisha
katika nchi za Waislamu, imebuniwa
ili kuwatengeneza watu watakaokuwa
watiifu kwa mabeberu wa Magharibi na
ustaarabu wao. Watu ambao hawawezi
kupigania na kufia Uislamu. Ni watu
ambao wanaitwa Waislamu, lakini
hawana Uislamu ndani yao.
Na wale ambao bado wana tatizo
kuhusu mgongano uliopo kati ya Haki
na Batili, lazima wafahamishwe kwamba
mgongano huo ni sehemu ya uumbaji wa
Mwenyezi Mungu. Ni jambo la maumbile
hilo:
"Bali (tulifanyalo ni hili:-) tunaitupa haki
juu ya batili ikalivunja fuvu la kichwa chake;
mara (batili) ikatoweka" Qur(21:18).
Ni jambo la wazi kabisa kwamba
mifumo miwili haiwezi kukaa pamoja na
ukweli huu utapatikana iwapo tutaangalia
uhalisia wa kihistoria. Katika kipindi
chote cha historia, mataifa yaliyokuwa
na fkra na mawazo tofauti, yamekuwa
katika mgongano wa kudumu kati yao, na
kila mfumo uling'olewa kupitia mchakato
wa harakati za mapambano.
Kut okana na ukwel i huo, ki l a
Mtume wa Mwenyezi Mungu na Nabii,
akiwemo Muhammad (saw) alipingwa
vikali na mfumo uliokuwepo, na kila
Mtume na Nabii wa Mwenyezi Mungu
alipambana na mifumo iliyokuwepo na
fkra zilizojenga mifumo hiyo. Kwa hiyo,
hakuna sababu ya Waislamu kudhani
kwamba wanaweza kukwepa uhalisia
huu, au kuamini kwamba ukweli wa
uumbaji wa Mwenyezi Mungu unaweza
kubadilika kwa ajili yao.
Uwepo wa fkra hizo potofu miongoni
mwa Waislamu haukuja kwa bahati
mbaya. Fikra hizo zimebuniwa kwa
ustadi wa hali ya juu na kupandikizwa
kwa uangalifu mkubwa. Waislamu
wakizikubali na kuzikumbatia, basi
Umma hautakuwa wa Kiislamu,
isipokuwa litakuwa taifa la Kikafri
lenye idadi kubwa ya Waislamu.
Uislamu utakuwa dini tu kama
Ukristo au Ubudha, na ' Ahkam
Shariah' ambayo ndiyo kigezo
cha Kiislamu kufanya mambo,
itaondolewa kutoka kwenye maisha
ya Waislamu.
Kwa kuongezea, Umma wa
Wai sl amu utal azi mi ka kutupa
dhamira (mission) yake ya msingi
hapa ulimwenguni, ambayo ni kuishi
kwa mujibu wa mfumo wa Kiislamu
na kuusambaza Uislamu huo kwa
binadamu wengine duniani, kama
ujumbe wa muongozo.
Fikra potofu kama hizo zimejaa
mbegu za kuharibu Umma wetu
wa Kiislamu.Wanaoeneza fkra hizo
mbaya, kwa kujua au kutokujua,
wanatumikia maslahi ya Makafiri
na kuufanya Ukafri uzidi kujikita
kwenye ardhi na fkra za Waislamu.
Na pia wanafanyakazi ya kuuweka
Uislamu mbali na maisha, ikiwa ni
pamoja na kuukwamisha usirudi
kwenye nafasi yake kama mfumo wa
kutawala na kuratibu maisha ya kila
siku ya watu.
Kwa hiyo, fkra kama hizo, lazima
zibainishwe na kushambuliwa, badala
ya kuzikumbatia na kuzipa ladha ya
Kiislamu. Makafri na mawakala wao
miongoni mwa Waislamu, wanaweza
kufanikiwa kuuvuruga Umma wa
Kiislamu kwa kipindi fulani.
Wanaweza kuweka vikwazo katika
njia ya kuhuisha Uislamu, lakini
iwapo kutakuwa na kundi ambalo
linaukumbusha Umm a wa Kiislamu
kuhusu Dini yao iliyosahaulika, na
kufichua njama zilizojificha dhidi ya
Umma huu, na kufanyakazi bila ya
kuchoka ya kurejesha mfumo wa maisha
wa Kiislamu,bila shaka makafiri hao
hawataweza kuzuia kurejea tena kwa
Uislamu:
"Wanataka kuzima nuru ya Mwenyezi
Mungu (ya Uislamu) kwa vinywa chao; na
Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake
ijapokuwa makafri watachukiwa"Qur(61:8-9)
15
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Tangazo
Bismillahir Rahmanir Rahiim
ISLAMIC PROPAGATION CENTRE
NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA 2015
Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo:
Mkuzo Islamic High School - Bweni tu - SONGEA
Kirinjiko Islamic Sec. School - Bweni tu SAME - KILIMANJARO
Nyasaka Islamic Sec.School - Bweni tu - MWANZA
Ubungo Islamic High School - Kutwa tu DAR ES SALAAM
1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi mazuri ya Kiislamu.
2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo:
Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Quran na mafunzo yake, Hadithi za Mtume(s.a.w), Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics, Physics, Chemistry, Biology, Geography,
History, Civics, Book keeping na Commerce.
3. Patakuwa na mtihani tarehe 29/11/2014 saa 2:00 asubuhi katika vituo mbali mbali kote nchini. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote.
4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28/11/2014.
5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani.
Arusha - Ofsi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na
msikiti Mkuu Bondeni : 0763 282 371/ 0783552414.
Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha : 0654 723 418.
- Same Juhudi Studio mkabala na Bank ya NMB Same: 0757 013344.
- Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075
- Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.
- Ugweno Kifula Shopping Centre- Yusuph Shanga : 078458776.
Tanga - Twalut Islamc Centre Mabovu Darajani : 0715 894111/0789 410914.
- Uongofu Bookshop: 0784 982525
- Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007.
- Mandia Shop - Lushoto: 0782257533.
Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685.
- Ofsi ya Islamic Education Panel Mtaa wa Rufji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770.
Musoma - Ofsi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05 : 0784721015/0765024623
Kagera - Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na ofsi za TRA. : 0684 701175.
Shinyanga - Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0752180426
- Kahama ofsi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi : 0753 993930.
Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School : 0712974428/0712033556.
- Ofsi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin : 0655144474.
Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380.
Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718 661992.
Singida - Ofsi ya Islamic Education. Panel karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784 928039.
Manyara - Ofsi ya Islamic Ed. Panel Masjid Rahma: 0784 491196
Kigoma - Msikiti wa Mugera Mwandiga: 0714 717727.
- Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860.
- Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802.
Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.
Mtwara - Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.
Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264/0683670772.
- Mkuzo Islamic High School : 0717348375.
Mbeya - Ofsi za Islamic Education Panel Uhindini 0785425319.
- Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319.
.
Rukwa - Sumbawanga: Masjid TAQWA: 0717082 073.
Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566.
Iringa - Madrastun Najah: 0714 522 122.
Pemba -Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.
Unguja - Madrasatul Fallah: 0777125074.
Mafa - Ofsi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu : 0773580703.
Handeni - Nassoro Mafga: 0782 105735/ 0657 093983
USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!
MKURUGENZI
WABILLAH TAWFIIQ
1
16
AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
16
MAKALA
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works Limited, S.L.P. 4605 Dar es Salaam.

AN-NUUR
16
DHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014
Soma
gazeti la
AN-NUUR kila Ijumaa
T U L I TA F A U T I A NA
Wa z a n z i b a r i k a t i k a
muundo wa serikali, lakini
hatukutafautiana katika
maoni ya kutaka katiba
imtambue Rais wa Zanzibar
sawa na mwenzake wa
pande ya pili. Tukatamka
kwa nguvu zote kwamba
t unat aka rai s mwenye
mamlaka kamili na serikali
mbili zenye usawa.
Hii katiba haijatambua
kilio chetu tukiwa wadau
wenye hadhi sawa katika
muungano na haijathamini
maoni ya Wazanzi bari
hasa upande wa watawala
wal i opi nga mf umo wa
serikali tatu lakini wakaamini
tutarudi wakati wa Mzee
Karume akiwa Makamo wa
Rais wa muungano mwenye
maml aka yake ye nye
nguvu. Ukweli na tuuseme
wazi wazi , t ul i gawi wa
tukagombana wenyewe kwa
wenyewe tukifikiri ahadi
za mamlaka tunayoyadai
tutapatiwa ndani ya mfumo
wa serikali mbili.
Tazama namna rasimu hii
ilivyojizonga na kudharau
ma ml a ka ye t u nda ni
ya muungano. Rai s wa
Zanzibar katajwa tu kama
makamo wa rais tena wa pili,
hana mamlaka yoyote, ni
ceremonial position tu tena
isio na nguvu hata mbele ya
makamo kamili.
Lakini rais wa muungano
kameza hata namna ya
kugawa mikoa visiwani
j ambo ambal o hal i mo
katika muungano na zaidi
hata tawala za mikoa nazo
kinyemela zikatajwa katika
rasi mu huku zi ki wa si
mambo ya mungano ili huko
mbele kupatikane sababu ya
kusema Wazanzibari walio
wengi waliridhia.
Tazama pia jee ana nafasi
gani mbele ya Waziri Mkuu
ambae kwa rasi mu hi i
amebatizwa makamo wa tatu
wa rais? Ukweli hana nguvu
zaidi ya namba yake kutajwa
mwanzo na ya Waziri Mkuu
kutajwa mwisho. Ndio yale
yale tuliokuwa tukiyasema
mwanzo, hadaa na ghilba
tupu. Tumeambiwa rais wetu
atakuwa makamo wa pili,
tukapiga makof lakini hana
mamlaka yoyote hata rais
anapoondoka nafasi yake
huchukuliwa na makamo
wa kwanza na ikiwa naye
Rais wa Zanzibar mwenye mamlaka Kamili
Na Team Zanzibar
RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
hayupo ni makamo wa tatu
ambae ni Waziri Mkuu.
Jee, haya ndio mamlaka
ya rais tulioyadai ndani ya
muungano? Jee, hii ndio
heshima, usawa na haki
tuliojigamba kupata ndani
ya mfumo wa mbili? Fikiri
sasa ingekuwa Mzee Karume
anapangiwa kuwa makamo
wa pili butu wa muungano
angelikifanya nini koti?
Tusiende mbali tukumbuke
m a n e n o m a k u b w a
yalioonyesha kuchoka na
ukosefu wa haki kutingisha
kibiriti kilichojaa kweli
tumekuwa hatukumbuki
basi hata mazito yaliotamkwa
na waliokataa ukoloni wa
kujitakia?
Hebu fkirini vizuri sasa
na tujaalie rais ajae ni Bwana
Sita na Waziri Mkuu wake
akawa ni bwana Chenge aka
Vijisenti, jee huu muungano
tunaouringia utakuwa katika
hali gani? Jee nafasi ya rais na
mawaziri wake wa Zanzibar
watakuwa hali gani?
Tutazame hasa kubwa
l i pi l a kumnyi ma Rai s
wa Zanzibar mamlaka ya
umakamo wa rais kamili?
Kwa nini lilifanyika kazi
wakati wa Mwalimu tena
vyama vikiwa tafauti, huku
ASP na Bara TANU hata
lisifanye kazi sasa? Kubwa
l i pi hasa l a kutunyi ma
nafasi tuliokubaliana awali
na tukaweka msingi wa
muungano na mahusiano
makubwa tulionayo?
Kama ni serikali mbili,
alau zile za Mzee Karume
na Mwalimu, sio za Sita na
Chenge.
Turudi katika misingi ya
awali ya kuungana. Huu
ulioletwa ni usanii wa hali
ya juu, kumfanya Rais wetu
kuwa makamo wa pili lakini
akiwa hana mamlaka hata ya
kuendesha vikao katika hata
shughuli za serikali kwa yale
yanayotuhusu akawa chini ya
Waziri Mkuu, halikubaliki.
Fikiri sasa kwa mara
nyengine logic mbovu yenye
madhara kwa Zanzibar,
kwa nini katika mfumo wa
uongozi wa vyama hakuna
makamo wa pili na wa tatu
lakini uwe katika mfumo wa
serikali? Kuna mwenyekiti
na makamo wake wawili wa
bara na visiwani, wakiwa
na nguvu sawa na heshima
sawa, lakini huku kwenye
serikali madaraka ya rais
alieungana na mwenzake
kuunda muungano l eo
kawekwa nyuma ya Waziri
Mkuu hata hii hamuioni?
Ni s a wa na ma ka mo
mwenyeki t i wa chama
akanyimwa mamlaka ya
kuongoza vikao na badala
yake akapewa katibu mkuu
au nai bu kati bu mkuu,
itafka siku tutawekewa rais
ambae ni mkuu wa mkoa wa
jiji la Dar! Tuamke na tuwe
na uchungu wa nchi zetu
na muungano wetu ili haki,
usawa na heshima itawale,
sio uchu na chuki za baadhi
yetu zituhadae.
Huku ni kut awal i wa
kialiki. Ndio yale yale ya
chenga twawal a, l aki ni
twafungwa tu. Kwa hii ya
vij isenti hapana hapana
hapana.
WAZIRI Mkuu wa Uturuki,
A h me t Da v u t o g l u ,
ameihakikishia Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar
k u wa ma k u b a l i a n o
yaliyofikiwa kati ya nchi
hiyo na Zanzibar, yamo
katika hatua za maandalizi
kutekelezwa kama ilivyo
katika makubaliano juu
ya maslahi ya pande mbili
hizo.
B w . D a v u t o g l u
ameyasema hayo mapema
wiki hii wakati alipokutana
na Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar,
Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad, jijini Instanbul
nchini Uturuki, kwa ajili
ya kuzungumzia masuala
mbalimbali yanayohusu
ushirikiano kati ya pande
mbili hizo.
Maal i m Sei f yupo
j ij ini Istanbul Uturuki
kuhudhuria mkutano wa
Uchumi wa Dunia (WEF)
ambao umewakutanisha
vi o ngo z i wa ki s i a s a ,
wataalamu na wawakilishi
wa sekta za watu binafsi
Uturuki mbioni kuwekeza Zanzibar
Na Khamis Haji, Istanbul kutoka mataifa mbalimbali.
Wa z i r i Mkuu huyo
alisema kuwa baadhi ya
makampuni ya nchi hiyo,
yamo kat i ka hat ua za
kufanya utafti juu ya namna
yatakavyoweza kufungua
miradi ya uwekezaji, ikiwa
ni pamoja na kutekeleza
ahadi ya serikali yake ya
kusaidia shughuli za kijamii
na maendeleo Zanzibar.
Alisema kuwa baadhi
ya maeneo hayo ni Usafri
wa Anga, Sekta ya Utalii,
Miradi ya Kilimo, Afya na
Elimu pamoja na shughuli za
kuwasaidia watoto yatima.
Ka t i ka ba a dhi ya
maeneo tuliyokubaliana
kushirikiana, makampuni
ya Uturuki tayari yanafanya
utafiti utakaoyawezesha
kutekeleza ahadi hizo,
alisema Bw. Davutoglu,
katika mazungumzo hayo
yaliyofanyika katika hoteli
ya Hilton Istanbul Bomanti.
Wa z i r i Mkuu huyo
aliongeza kuwa amevutiwa
s ana na mandhar i ya
visiwa vya Zanzibar, pale
al i poi t embel ea wakat i
al i pokuwa Wazi r i wa
Mambo ya Nje wa Uturuki,
hali ambayo ameielezea
kuwa inaweza kuiingizia
Zanzibar mapato mengi
kupitia sekta ya Utalii.
Kat i ka mazungumzo
hayo, Makamu wa Kwanza
wa Rais alisifu ushirikiano
uliopo kati ya Uturuki na
Zanzibar na kuahidi kuwa,
Zanzibar itahakikisha hali
hiyo inazidi kuimarisha
katika siku zij azo kwa
faida ya nchi mbili hizo.
Aidha, Maalim Seif
al i mpongeza Wazi r i
Mkuu huyo kwa ushindi
mkubwa wa chama chake
katika uchaguzi mkuu wa
nchi hiyo uliofanyika hivi
karibuni, ambapo Rais
Recep Tayyip Erdogan,
al i chagul i wa kushi ka
wadhifa huo na yeye
kuwa Waziri Mkuu.
Mazungumzo hayo pia
yalihudhuriwa na Waziri
wa Biashara, Viwanda na
Masoko, Nassor Ahmed
Mazrui, pamoja na Balozi
wa Tanzania nchini Italia,
ambaye pia anahusika na
nchi ya Uturiki, Balozi James
Msekela.

También podría gustarte