Está en la página 1de 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Ndoto ya Zanzibar itatimia

Hakukaliki! Wakristo, Waislam washikiana mapanga, bunduki

ISSN 0856 - 3861 Na. 1103 SAFAR 1435, IJUMAA , DESEMBA 13-19, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs

Uk. 5

Mauwaji ya kutisha kijiji kwa kijiji Watu waswali na silaha mgongoni Kanisa Katoliki lafurika wakimbizi

HAYATI Nelson Rolihlahla Mandela.

Mandela alikuwa katika orodha ya magaidi ya Marekani hadi 2008


Obama, Cameron walipaswa kuomba radhi
Na Shaban Rajab
K WA wa p e n d a h a k i , Hayati Nelson Rolihlahla Mandela, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1993 ni alama ya kimataifa ya uhuru na ushujaa. W a t a e n d e l e a kumkumbuka kwa yote aliyoyafanya katika kutetea haki na uhuru si kwa watu wa Afrika Kusini bali kwa

Waislam katika msiba wa Uhuru


Na Bakari Mwakangwale WA K AT I Ta i f a likisheherekea miaka 52, ya Uhuru wa Tanganyika, Waislamu wamekuwa katika hali ya misukosuko ya kudai

Baadhi ya wapiganaji wanaosababisha mauaji ya raia Jamhuri ya Afrika ya Kati (Central African Republic-CAR).

Serikali yawasahau wapigania Uhuru Msiba umbeleni kama dhulma haitakoma


maoni yao juu ya nafasi ya Waislamu ndani ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika, iliyofikia kilele Jumatatu ya

Inaendelea Uk. 8

haki ndani ya Tanganyika (Tanzania) huru. Hayo yamebainishwa na baadhi ya Masheikh wakitoa

wiki hii (Desemba 9, 2013). Kwa upande mwingine Inaendelea Uk. 2

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Makala
AN-NUUR

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

Waislam katika msiba wa Uhuru


Inatoka Uk. 1
Taifa limetakiwa kuwa na utaratibu wa kuwakumbuka na kuwaenzi wapigania Uhuru, ili kuleta maana halisi ya sherehe za Uhuru na kuweka historia sahihi ya Tanganyika. Wakiongea kwa nyakati tofauti Masheikh hao wamedai kwamba, ni kweli Uhuru ulipatikana mwaka 1961, lakini baada ya muda mfupi ilionekana kuwa Uhuru huo si kwa makundi yote ya kijamii ndani ya Tanganyika, ambayo kwa sasa ni Tanzania. Akizungumzia hali ilivyo nchini hivi sasa, Sheikh Mohammedi Saidi, alitahadharisha akisema, ikiwa Serikali itaendelea kupuuza madai ya Waislamu, huenda huko mbele hali ya hea ikachafuka. Kwa mwenendo huu, Waislamu watarudi kudai Uhuru, na isidhaniwe safari hii itakuwa katika viwanja vya Mnazi mmoja, huenda mbinu za kudai uhuru huo zikabadilika. Alisema Shkh. Mohammed. Alisema, Waislamu ndio waliopigania Uhuru wa nchi hii, huku wakiwa na mategemeo, kuwa (Uhuru huo) utaondoa dhulma, ubaguzi na madhila mbalimbali miongoni mwa Watanganyika, waliyokuwa wakifanyiwa na Wakoloni. Mohammed, alisema kwa muda mrefu Waislamu wametumia njia mbalimbali za kufikisha madai na malalamiko yao, wakiitaka Serikali kuangalia upya mwenendo wa utawala wake tokea Tanganyika ipate Uhuru mwaka 1961. Alisema, kama hiyo haitoshai Waislamu wakasema hadharani kwa kutembea nchi nzima, wakilalamika kuwa nchi hii inaendeshwa kwa unaowabagua Waislamu ndio maana kila mara Waislamu wanalalamika kutokutendewa haki. Tu s i t a k e k w e n d a katika kadhia ya mauaji ya Waislamu Mwembechai, au sakata la Kilindi, tuweke pembeni, kama hali ndiyo hii uhuru kwa Waislamu upo wapi, ikiwa hali itabaki kuwa hivi kwa kundi moja kuendelea kukandamizwa huko tunakokwenda tutaivuruga nchi. Alisema huku akitaadharisha Shkh. Mohammed. A k i z u n g u m z i a maadhimisho ya mika 52, ya Tanganyika, alisema, n i v y e m a Ta i f a l i k a wa na utaratibu maalum wa kuwaenzi na kuwakumbuka wazee waliopigania Uhuru wa Tanganyika na sasa ni Tanzania. Kama tunataka kusherehekea kweli Uhuru wa Tanganyika, basi ni lazima tuwe tunawaenzi mashujaa wetu waliopigania Uhuru wa Tanganyika, ambao wapo wengi, watafutwe walio hai wawe wanaonekana katika sherehe hizo kwani wengine wapo hai ni bora waenziwe. Alisema Shkh. Mohammed Said. Alisema, ajabu ni kwamba k a t i k a m a a d h i m i s h o ya Uhuru wa Tanganyika, kabla na wakati wa kilele cha siku hiyo hutajwa mtu mmoja tu, ambaye ni Julius Nyerere, lakini waliomuweka mbele hawatajwi wala kusimuliwa. Akimnukuu Mshairi mmoja wa Kimisri, alisema Mshairi huyo anasema Ukilisifia kabati kwa uzuri wake, usifie na ule msumeno uliokata mbao na kutengeza kabati hilo. Unapo msifia huyo Nyerere, basi uwasifie na uwatambue pia wale watu alikuwa nao bega kwa bega mpaka Uhuru ukapatikana, kwani yeye (Nyerere) alikuta watu tayari wanaendelea na harakati za kudai Uhuru. Alibainisha Shkh. Mohammed. Aliwataja ndugu wawili ambao ni Abdulwahid Saykes na Ally Sykes, kuwa wao ndio waliompokea Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kisha kumuingiza katika harakati za Siasa na kupigania Uhuru, huku wawili hao wakiwa ni miongoni mwa wafadhali wa k u u wa TA A , TA N U mpaka Tanganyika inapata Uhuru, mwaka 1961. Hata hivyo Shkh. Mohammed, alisema katika kusheherekea miaka hamsini ya Uhuru wa Tanganyika, wawili hao (Abulwahid Sykes na Ally Saykes), walipewa medani katika viwanja vya Ikulu, na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Alisema, medani hizo zilitolewa baada ya kifo chake (Abdul) na alipokea mwanae Klayst Sykes, ambapo medani ya Ally Sykes, wakati huo yu hai alipokea mwenyewe. Mohammed Said, akahoji kitu gani kilifanya wacheleweshe kuwaenzi ndugu hawa wawili, ambao Chama cheyewe cha TAA, kilicho zaa TANU, kilihuishwa na baba yao mwaka 1927. Zaidi alisema, baba yao ndiye aliyefanya kazi ya kuwakusanya wanachama wenzake na kujenga nyumba ambayo ikaja kuwa ofisi za TAA, TANU na sasa CCM, mwaka 1930. Vipi walikaa miaka yote hiyo bila kuwatambua watu hao, wakaja kuwatambua miaka hamsini, baadae lakini bado haitoshi kuwaenzi vinara hao wawili ikawa basi ili hali wapo wengine wengi tu. Alisema Shkh. Mohammed. Shkh. Mohammed, alisema mbali ya Abdul na Ally, wapo wengine ambao kamwe huwezi kuelezea harakati za Uhuru, ukawaacha watu kama Hamza Mwapachu, Dr. Kyeruzi, Sheikh Hassan Bin Amir, John Rupia, Mwalim S t i ve n M u h a n d o , K i a t e Mshume, Jumbe Tambaza na Haidari Mwinyimvua. Wengine ni Idd Tosir, Bi. Titi Mohammed na Tatu Bint Mzee. Akasema hao ni wachache tu waliokuwa Jijini Dar es Salaam ambapo wote h a o wa l i k u wa p a m o j a , na walimkaribisha Mwl. Nyerere. Kutoka mjini Moshi, aliwataja baadhi yao kuwa ni Yusuph Olotu, Mama bint Malik, Halima Kilengio, na kwa Jijini Tanga, kulikuwa na Hamisi Heri, Rashid Sembe, Mzee Makoko. Akahoji vipi hawa hawakupewa au hata kutajwa tu kwani walikuwa msitari wa mbele katika TANU. Wa n a h a r a k a t i wa l i o p i g a n i a U h u r u n a wanaostahili walau kutajwa ni wengi huwezi kuwataja wote, kule Tabora, yupo Bilal Waikela, Mzee Fundi Muhindi, Saleh Tambwe na Bibi Nyange bint Chande. Lindi, utamkuta Salum Mpunga, Yusuph Chembela, Yusuph Badi, Bi. Saharifa, na Kanda ya ziwa, miongoni mwao ni Abdul Kandoro na Paulo Bomani. Alisema huku akiwataja. Shkh. Mohammed, alisema hivi sasa Waislamu nchini wanatakiwa kuingia tena katika siasa, kwa lengo la kulinda maslahi yao kama ambavyo wafanyavyo wenzao Wakristo toka walivyoingia au kuingizwa katika TAA, TANU mpaka CCM. Suluhisho kwa Waislamu, hawana budi watambue kwamba njia ya kujitoa katika hali waliyonayo sasa ni kurudi katika harakati za siasa kwa kuingia katika vyama wakiwa na agenda yao kama walivyofanya au wanavyofanya wenzao hivi sasa.alisema mwanahistoria huyo. Naye Imam Hamza Shaban, wa Masjid Thaqib, Jijini Mwanza, alisema Waislamu katika miaka hiyo 52, ya Uhuru wanaweza kusema kuwa wapo ndani ya msiba wa Uhuru na wala si Uhuru halisi. Tunapozungumza hivi namaanisha kwamba kundi moja wapo katika Tanganyika, a m b a l o n i l a Wa i s l a m u limekuwa likikandamizwa t o k e a Ta n g a n y i k a i p a t e Uhuru, na kujikuta wamo katika misukosuko ya kudai haki. Amesema Imam Hamza. Imam Hamza alisema, hali

Tumemsifia Mandela lakini muhimu tujifunze kwake


TA N G U a f a r i k i dunia Mzee Nelson Mandela Desemba 5, Alhamisi iliyopita, watu mbalimbali wamekuwa wakimsifu kwa yale aliyofanya wakati wa uhai wake. Hata hivyo nasaha zilizopewa kipaumbele zaidi katika msiba wa Mzee Mandela, nyingi ni viongozi wa dola na watu mashuhuri, hususan katika ile siku rasmi ya maombolezo iliyoandaliwa na serikali ya Afrika Kusini, na kufanyika katika uwanja wa soka wa FNB jijini Johanesburg Jumanne wiki hii. Viongozi wengi wa l i opa ta nafas i ya kumzungumza Madiba, walikuwa wakijitahidi kadiri wawezavyo kumwaga sifa kemkem kwa Mandela. Baadhi ya sifa zilizotajwa zaidi ni kwamba Mandela alikuwa mpenda haki, mwanademokrasia wa kweli, mwadilifu, asiyekuwa na uroho wa madaraka, mchukia rushwa, asiyetaka kusikia vitendo vya kibaguzi na alikuwa muumini wa amani na upendo n.k. Pamoja na viongozi wengi na maarufu kupata nafasi kutoa salamu zao katika msiba ule, lakini nasaha alizotoa Askofu Desmond Tutu, ndizo zilizotuvutia zaidi na zinazoacha somo muhimu. Kwa kifupi Mzee Tutu katika nasaha zake fupi siku ile alisema Mzee Mandela amesifiwa sana kwa matendo yake mema enzi za uhai wake. Lakini jambo la msingi kwa waliosalia, ni kuishi kwa kufuata nyendo zake. K wa m b a k wa s i f a zile zile ambazo wengi walimsifia pale

uwanjani, sifa ambazo k we l i a l i k u wa n a z o Mzee Madiba, basi w e n g i n e n a o wa n a wajibu wa kumuenzi k wa k u j i f u n z a k wa Mandela, kutenda yale aliyokuwa akiyatenda Madiba wakati wa uhai wake kwenye nafasi zao. Bila shaka Askofu Tutu alijua fika kwamba siku ile kulikuwa na idadi kubwa ya viongozi wa dola, taasisi na Jumuia za Kimataifa waliohudhuria katika maombolezo yale. Alitambua kuwa wengi waliomsifia Mandela, inawezekana hawana na wala hawajafanya yanayostahili sifa kama za Mandela katika nafasi zao, zaidi ya kudhulumu. Alijua kuwa wengi wao walisifia ikiwa ni katika kumpamba tu mtu kama sehemu ya kutimiza wajibu, baada ya mhusika kufa. Na haya kwetu sisi tunaona yamekuwa mazoea kwa wengi, kusifiwa marehemu mdomoni kupamba msiba. Kama alivyobainisha Askofu Tutu, tunaona kwamba viongozi, hasa wa l e wa d o l a wa n a wajibu wa kujifunza kwa Mandela katika kuwaongoza watu wao. Wanaweza wasifikie kiwango na uwezo wa Mandela, lakini kwa kujifunza kutoka kwake, wanaweza kufanikiwa katika uongozi wao. Wanaporudi kutoka Johannesburg wajiulize, katika nchi zao hali ya rushwa ikoje, ubaguzi (siku hizi zaidi ni wa kidini, kikabila) ukoje, vipi hali ya ubadhirifu wa mali za umma katika serikali zao, rushwa katika taasisi za serikali, vipi hali ya dhulma n.k. Si vibaya kusifia, lakini ni vizuri zaidi tukajifunza kwa tunayemsifia.

Inaendelea Uk. 3

Taasisi za Kiislamu zatakiwa kuitisha mjadala wa pamoja


Ni wa kujadili matatizo ya Waislamu Tofauti za kiitikadi ziwekwe pembeni
maadili ya dini. Tunahitaji kujifunza mbinu za kibiashara ili kukabiliana na hali ya sasa, ili Waislamu nao wawe sehemu ya mabadiliko ya kibiashara yanayoendelea duniani kote hivi sasa, bila kuathiri misingi yetu ya dini ya Kiislamu. Alisema Bw. Mhezi. Aidha aliwataka Waislamu kubadilisha mienendo yao, hususani njia zinazotumika katika kuwapa vijana elimu mbalimbali, kwamba kuna haja ya kuwepo mikakati madhubuti ya kuwaanda Na Bakari Mwakangwale MABARAZA, Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini zimetakiwa kuitisha mjadala wa pamoja kuyatafutia u f u m b u z i m a t a t i z o ya Waislamu, ili kutoka katika hali ya kuhasimiana na walalamikaji. Wito huo umetolewa na Bw. Habib Mhezi, wakati akiongea na Waislamu na wanachama wa Hajj Trust Saccos LTD, katika Mkutano M k u u wa S a c c o s h i y o uliofanyika katika hoteli ya Starlight Jijini Dar es Salaam, Desemba 1, 2013. Bw. Mhezi, alisema ni jambo bora kuanzishwa majada baina ya makundi mbalimbali ya Kiislamu, kwa lengo la kujadili matatizo yanayowakabili Waislamu na kuyatafutia ufumbuzi wa pamoja na kuacha kuwa walalamikaji miaka yote. Ni vyema pakaanzishwa m a s h a u r i a n o b a i n a ya makundi mbalimbali ya Waislamu, wakutane na kufanya mjadala mpana wa kuunusuru Uislamu na Waislamu, ili kuondokana na dhana mbaya ya kubaki kuwa walalamikaji au watu wa kulaumu kila wakati, bila kutoa njia mbadala ya kutuondoa mahali tulipo. Alisema Bw. Mhezi. Alisema ni wazi kwamba kila kundi lina mtazamo tofauti, lakini jambo la msingi ni kwamba wote ni Waislamu na kukutana kwao iwe ni kwa ajili ya mustakabali wa Waislamu na sio itikadi zao. Bw. Mhezi, alisema haja ya Waislamu kutambua kwamba hakuna mtu wa kuwaondoka katika hali waliyonayo, isipokuwa ni wao wenyewe kwa kuangalia fursa na kuzitumika. Moja ya fursa zilizotajwa ni kuanzisha Saccos zao, ambazo zinafuata maadili na misingi ya Kiislamu na kufuta fikra kwamba vikundi hivyo havifai kwa Waislamu. Bw. Mhezi aliongeza kuwa changamoto zinazowakabili Waislamu ni kutotilia maanani elimu ya ujasiriamali, ambalo huonekana kama ni kinyume na Uislamu. A l i s e m a m a t o k e o ya dhana hiyo ni kuachwa nyuma kimaendeleo na kukabiliana na umasikini wa kipato. Alifahamisha kwamba ujasiliamali ni njia tanzu ya kibiashara na katika Uislamu biashara si ukiukwaji wa vijana wa Kiislamu katika kushika nafasi mbalimbali katika jamii. Alitahadharaisha kwamba kinyume na hivyo, Waislamu wataendelea kubaki kuwa ni walalamikaji wakati wenzao wakijipanga na kushika sehemu zenye maamuzi katika jamii, huku wakitumia fursa kama hizo za Saccos ambazo nyingi hufunguliwa hata Makanisani. Fursa zipo za kuanzisha vikundi ambavyo vitafuata utaratibu na mafundisho ya Uislamu, hili linawezekana, mfano ni huu wa Hajj Saccos, Alisema na kuhoji, Bw. Mhezi. Tatizo la ukosefu wa fedha kwa Waislamu ni kubwa, wengi hawana uwezo hata wa kutekeleza nguzo ya Hijja kutokana na vipato vyao duni, huku kukiwa hakuna chombo cha Kiislamu kilichoweka utaratibu wa kudumu wa kulipatia ufumbuzi tatizo hili. Alifafanua. Aliongeza kuwa kupitia Hajj Trst Saccos, wameweka u t a r a t i b u wa k u l i p a t i a ufumbuzi tatizo hilo, ambapo wanachama wao watapata fursa ya kujiwekea akiba ambayo itawawezesha kwenda Hijja na kutatua matatizo ya kiuchumi yanayo wakabili. Alisema pamoja na kuwapo kwa taasisi na Mabaraza mengi ya Kiislamu nchini, lakini nyingi hazina mpango

Habari

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

Inatoka Uk. 2 hiyo inatokana na mapitio mengi ambayo Waislamu wamekutana nayo tokea Tanganyika ipate Uhuru huku Waislamu wakitendewa ndivyo sivyo katika awamu zote nne za utawala. Alisema, ukianzia mwaka 1961, kumbukumbu inaonyesha Masheikh wengi walikamatwa na wengine waliwekwa ndani. H a wa k u t e n d e wa h a k i kama wananchi wengine, bali wakati mwingine kwa makusudi kabisa walibaguliwa na kuhujumiwa. Na hiyo ilikuwa ni baada ya kufanya kazi kubwa ya kudai uhuru. Ukija mwaka 1964, ni misukosuko tu mpaka 1993, hali bado ni tete kwa Waislamu kila wanapo simama na kueleza kutaka usawa hujikuta wakiandamwa. Masheikh wetu wamepigwa sana na kuumizwa na wengine kusababishiwa vifo mara baada ya kutoka magerezani, wengine kufunguliwa kesi n a k u k o s a u s h a h i d i wa mashitaka wanayopewa. Alisema Imam Hamza. A k i g u s i a m a t u k i o ya mwaka 1998, Imam Hamza alisema Umma utakumbuka k wa m b a Wa i s l a m u waliuwawa Mwembechai. Na kwamba hiyo ilikuwa ni baada ya serikali kusikiliza na kufanyia kazi madai ya Paroko, bila kujali kama yalikuwa ya kweli au la. Akielezea mashitaka yake ambayo yalimuweka rumande zaidi ya miezi mitatu anasema yanakwenda sambamba na yale ya Askofu mmoja Jijini humo, lakini Askofu hajaguswa na mpaka sasa yupo mitaani, huku yeye (Imam) akiendelea kusimama

Waislam katika msiba wa Uhuru


Mahakamani. Inavyoonekana Uhuru huu upo kwa wenzetu tu, hata wakiwa na makosa hawaguswi. mfano huyu Askofu Mpemba ni mmoja wa Maaskofu waliosababisha mauaji Buseresere. Huyu Askofu, hivi sasa yupo huru, pamoja na Jeshi la Polisi kutangaza kumtafuta lakini hajakamatwa na wala h a wa n a m p a n g o h u o . Alisema Imam Hamza. Imam Hamza, alisema utasemaje Waislamu wapo huru ikiwa kila wakiitaka Serikali iwatendee haki, Masheikh wao wanakamatwa na kuwaweka jela na hata kuwanyima dhamana. Alisema, ukifatilia m a t u k i o ya n a y o wa h u s u Wa i s l a m u n c h i n i t o k e a Uhuru upatikane, utabaini kuwa ni kama matukio ya kutengeneza yanayohusu kundi moja la jamii ndani ya Taifa linalodai kuwa ni huru na linaloongozwa kwa kufuata utawala wa sheria. Imam Hamza, alibainisha kwamba haya yanayowakuta Waislamu muda wote tokea wapate Uhuru, ni tatizo la mfumo wa kinchi, ambao haupo katika uadilifu. Akieleza nini cha kufanya kwa Waislamu, Imam Hamza, aliwataka Masheikh kuwa kitu kimoja na kuwaunganisha Wa i s l a m u , k w a n i b i l a mshikamano wa kweli wataendelea kuwa daraja la pili ndani ya Tanzania huru. Kwa upande wake Sheikh Ayoub Muyinge, akitoa maoni yake alisema, anaona mazingira wanayokwenda nayo ni kuwa Waislamu wa Tanganyika, wanaweza kusema kuwa wana uhuru jina tu, na si uhuru halisi waliopigania wazee wao. Shkh. Muyinge, alisema bahati mbaya wazee wa Kiislamu waliopigania Uhuru wa Tanganyika, walikuwa wameandaa silaha kisha wakajilenga wenyewe, bila kufahamu na kujikuta Waislamu wapo nje ya Uhuru walioutarajia, jambo ambalo limeendelea kuwagharimu kwa miaka 52 sasa. Waislamu walifanya j u h u d i k u b wa k u t a f u t a U h u r u w a Ta n g a n y i k a k a m a wa n a h a r a k a t i n a juhudi zikafanyika hatimaye walifanikiwa kupata Uhuru, lakini mambo yaligeuka ghafla, kwa maana hiyo, kama ni biashara tunaweza kusema tumepata hasara. Alisema Shkh. Muyinge.

endelevu ya leo na kesho ya kutatua matatizo ya Waislamu kiuchumi. Akasema kuwa ni wakati muafaka sasa wa kukaa na kujiuliza, Waislamu watabaki katika hali hii mpaka lini. Hivyo akasema kwa mtazamo huo kuna haja kwa Mabaraza, Jumiya na taasisi za Kiislamu kukutana na kufanya mjadala na kuunganisha fikra na kuweka mipango endelevu. Bw. Mhezi, alisema Hajj Saccos imesaidia kutoa ajira mbalimbali kupitia wanachama wake kwa kuwakopesha na kuanzisha miradi mbalimbali ambayo husaidia kuajiri vijana wengine.

Ili Waislamu wajikwamue kutoka katika hali hiyo, Shkh. Muyinge, aliwataka Waislamu watambue nini maana ya Uhuru, na wapo kwa ajili ya nani hapa ulimwenguni. Zaidi, Shkh. Muwinge, akawataka Waislamu kurejea Qur an 2:30, kisha akawataka wajiulize hayo yaliyoelezwa katika aya hiyo yametimia au bado, na kama hayajatima ni kwa nini. Jumatatu wiki hii, Desemba 9, 2013, Watanzania waliadhimisha miaka 52, ya Uhuru wa Tanganyika, ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliongoza shamrashamra hizo zilizo fanyika katika viwanja vya Uhuru, Jijini Dar es Salaam.

Msaada ujenzi wa Msikiti. Mahitaji ya Vifaa yanayohitajika kufikia hatua ya Zege la Jamvi PLOT No. 152 Block A, Masjid Jumuiyatil Islamia Ubungo Darajani.
Na Mahitaji 1 2 3 4 5 6 7 8 9 Nondo 12 MM Nondo 8 MM Binding Wire 20 MAWE 200 CM KOKOTO 70 CM Mchanga 40 CM Cement Mbao Cypruss Misumari Deni la Mkandarasi (mjenzi) Size Pcs Pcs Kg Lori Lori Lori Mifuko 16 Kg Idadi 120 60 1 20 7 4 350 120 10 @ 30,000 8000 52000 250000 750000 220000 13500 9000 3000 21,097,000.00 16,000,000.00 Tshs 3,600,000.00 480,000.00 52,000.00 5,000,000.00 5,000,000.00 880,000.00 4,725,000.00 1,080,000.00

Nb: haya ni Mahitaji kwa ajili ya Zege la Jamvi Kwa mawasiliano zaidi Tupigie Mwenyekiti 0754 462 050 Katibu 0719 760 777 Mwenyekiti Kamati ndogo ya ujenzi ( Goha) 0787 318 116. International Commercial Bank No A/c 00001/01/601059/01 au A/c 0000/01/ 0009/94/02. Au tutembelee katika Msikiti wetu uliopo Ubungo Darajani. Wabillah Taufiq

4
A: KIRINJIKO ISL T.C I: WANAWAKE
Na 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 45 46 47 48 49 50 51 52 53 54 55 JINA SHAMIMU HABIBU MFINANGA YASMINI ALLY IBWENDE MAIMUNA SWALEH NTOLE FATUMA HASANI RASHIDI FARIDA SULEIMAN MREMBO ZAMUA SHABAN NGOYA SAUMU SHABANI ALLY ZANURA JUMANNE HAMISI ZAINA SELEMANI MWANAMVURA SALUMU ZENA MAGASHA YUSUPH SAMILA MARICK SAUMU SHABAN KIRAHO AZIZA RAMADHANI NTUI ZUBEDA BAKAR MJUNGU HIDAYA JUMA IPINGIKA MAIMUNA RASHID OMAR MWAMJAKA BATULI MARIAM IBRAHIM RASHID MAUA SAID NDENGU MURSHIDI SURURU MWAJUMA HEMED KUDRATH H. TENGENEZA SADA RAMADHANI MASANJA SALAMA ABDILLAH MUHAMADI UMMU-KULUTHUM ABDALLAH MAMU SHUFAA SWALEHE HEMED ZUBEDA OMARI SAID AISHA SELEMAN HAMIDA ABDUS-SALAM RAHMA JUMA HASSAN MWAJUMA SAID HADIJA RAMADHANI MWANGA AMINA SALIM HEMA MWAJUMA SHABANI MWINYIMVUA ZUHURA YASSINI SUNZU ASHURA KHAMISI KIUNGULIA AMINA SAIDI LIMEI ASHA HAMADI KIMARO RAHMA SHABANI HAMZA REHEMA KATUMBA HAMISA RAMADHANI JUMA WAMOYONI HUSSEIN BAKARI SALMA RAJAB SHANI KHAMIS ZAHRA RAJABU MNYAMIKE ZULFA KASSIM HASSAN RAHMA MBARAKA HASSAN ZAITUNI ATHUMAN LIDA FATUMA ABDUL MUNISI SOMOE HASSANI BEGE ZAHRA HASSAN MWIRU AMINA SAIDI MMAPALA HAWA HAMIDU OMARI SALAMA MUSSA RAMADHANI 56 57 58 59 60 61 62 63 64 65 66 67 68 69 70 71 72 73 74 75 76 77 78 79 80 81 82 83 84 85 86 87 88 89 90 91 92 93 94 95 96 97 98 99 100 101 102 103 104 105 106 107 108 109 110 111 112 113 114 115

Tangazo

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA UALIMU WA KOZI FUPI (SHORT COURSE) FEBRUARI 2014


ZILABELA M. ATHUMANI NAIMA KASSIM MUSSA SHAMILA AZIZ YUNUS JAMILA ISSA SIMBA JASMINE OMARY MVUNGI KHADIJA RAMADHANI KASONSO REHEMA ALLY ATHUMANI SALMA SHABANI MOHAMMED HAMISA RASHIDI HALFANI JASMINI ABDALLAH SAID JASMINI SALIM NGWILIZI NEMA RICHARD LEKEY MWAJUMA BWAKAME SHEMSA S. NGIMBWA AMINA FADHILI JUMA AMINA RAMADHANI FERUZI FATMA QASSIM ISMAILY JAMILA A. MTUA MTUMWA ZUBERI KHAMISI SAMIA OTHMAN MPONDA HAMIDA SULEIMANI ALLY HADIJA HASSAN ZAHRA YUSUPH SWALEH ASHURA A. AMANI HALIMA HAROUN MWANANJELA ZUHURA ADAM MTATIFIKOLO RAHMA SULEIMAN HALIMA KIGAMBA AMINA SHAIBU MATAJA HUSNA MAULIDI MADODO NAIMA JUMA HATIBU RAIHANA MUHAMEDI MWANGA ABEDA RUBEA SAID NASRA RAMADHANI BOI RUKIA ADAM ABUBAKAR NUSURA MIRAJI HASSAN HAFSWA MOHAMED ASIA H.MSHEKHA HAMIDA MALIKI MWANANJELA ZULFA MUHIBU NANGONGA FATMA ALI HAMAD AISHA ADAMU PUTTA HALIMA YUSUPHU MPAKA MARIAM RASULY MVAMBA ZAINAB MASOUDY HAMIDY ZAWADI SHAFII ZAYANA TWAHA SHABANI ZUENA MUSSA AISHAH ISSA JUMA FATUMA IDDY MUHAMMED MARIAM KHALID KASTELA MWAJUMA FAUSTINE MABITA SALMA HASSANI MOHAMED MWASHA NIA MWASITI SHABAN MZURI HUDAINA NASSORO ABDALLAH FASBIR SALEH MOHAMED SWAUMU KILUA REHEMA BAKARI SAADA RAMADHANI MUSSA 116 117 118 119 120 121 122 123 124 125 126 127 128 129 130 131 132 133 134 135 136 137 138 139 140 141 142 143 144 145 146 147 MARIAM AMAN FATUMA HAMISI MTEPA SALMA SHABANI MAKUTAS ZALKA K. MIRAJI MAIMUNA IDRISA HASSAN ZAKIA IDD NTUNGU AESHI SUDI YUSUPH ASHURA HARUNA MWANANJELA MWANTUMU ALLY ZIKO ZENA HASSANI MLAMBO ZUMLATI ABDI MSHANGAMA HAMIDA SEIFU ABDALLAH MARIAMU JUMANNE DEFU MWANAIDI AZIZI MSANGI ZULFA MOHAMED MWINYIMVUA FATUMA ZAKARIA IKHOTO FAUDHIA AMRAN YUSUPH ASHURA MOHAMED JONGO KHADIJA RAJABU SUWI AMINA HASANI MATOLA MWANAIDI MBARAKA HALIMA YUSUPH SALMA MASOUD AZIZA ALLY MKOLEKE ELISIA JULIUS MWANADIA ABUBAKARI IDDI MWANAKOMBO IMAMU KUNEMA SOMOE SAID MSOKOWALE RAFIA BURHANI HADIA MOHAMED SAIDI MGENI KHALIFA JUMA TATU HASSAN ALLY JINA HAMDAN M. HAMDAN ISSA MBELWA BAKARI RAMADHANI HUSSEIN YASSIN MOSHI HAMZA MOSHI IDD RAJAB RAJABU ALLY ATHUMANI TWALIBU HASSANI NYUMBA FADHIL HAMIS ATHUMAN MOHAMEDI SALUMU MINENGENE HUSSEIN ABDALLAH FUNDI NGHWAGI ROBERT KITABU OMARI KITABU RAMADHANI ABDALLAH SHAABAN ALLY MRISHO ALLY MUSSA HAMISI SHINENI MAULIDI ATHUMANI KONKI RASHIDI JUMA ALLY FADHIL MUSSA YUSUF IS-HAKA MWAJIMBO OMARI HASHIM LEVERIAN MIGINI SEF ABDALLAH MOHAMED ABASI HASANI MANGARE ABDILLAH SWALEH ATHUMAN HILALI SADICK MUSSA KHALID JUMA 26 27 28 29 30 31 MUSSA HAMID SWEBE MUHAMMAD JUMA OTHMAN HIMID ABDULAZIZ ATHUMANI ADAMU SUEDI IBRAHIM MUSTAPHA JUMANNE IDD

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

B: UBUNGO ISL T.C I: WANAWAKE


Na 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 Na 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 JINA JAMILA JIHADI MACHEMBA MARIAM IBRAHIM RAHMA SAID SULTAN KIDEE MOHAMEDI KINGARU SOPHIA ALLY CHIVANGA ASHURA ISSA ABDALLAH WARDA MUSSA ABDALLAH UMMUKULTHUM ADAM JUMA DALIA ABDALLAH CHUNGU PILLY ALLY MSHAMU MARIAMU MAKOTA ARAFA FADHILI MASAWE ZAITUNI MOHAMEDI MPULINGA ZAITUNI AHMED ZAIDI JINA MUHARAMI MUHIDINI SAID MOHAMMED JUMA OMARY IDRISA MAHAMI JAFARI BAKARI TWALIB ISIHAKA LUPINDO SELEMAN SALUM HASSAN RASHIDI SAIDI MTOLELA IDDI SAIDI IDDI ATHUMANI KASIMU DHAHABU MIRAJI HOSENI ATHUMANI HAIDARI RAMADHANI IDD RASHID OMARY BEYA DARSA ABDALLAH IBRAHIM M. SALUM HAMISI RASHIDI MAZURI MASHAKA H. NJIMBWI OMARY ABDALLAH MAGOMBE YUSSUPHU KASSIMU YUSUFU JAFARI ABDALLAH MWALIMU ABUUAFANI OTHMAN SALIM MASOUD R. KAZI

II: WANAUME

II: WANAUME
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25

MAELEKEZO MUHIMU 1. Barua za maelekezo ya kujiunga (Joining instructions) zinapatikana katika kituo muombaji alipofanyia mtihani. 2. Fomu za maombi zinaendelea kutolewa kwa ajili ya chuo cha Ualimu Ubungo tu. 3. Mtihani wa pili utafanyika Chuoni Ubungo tarehe 21/12/2013 saa 2:00 asubuhi. 4. Muombaji unaombwa kuthibitisha kukukubali nafasi kabla ya tarehe iliyotajwa.
5. Baada ya tarehe ya mwisho nafasi ya asiyethibitisha atapatiwa muhitaji

mwingine. 6. Kwa maelezo zaidi wasiliana na 7. Mkuu wa Chuo husika . ( Kirinjiko 0787188964,

8.

Ubungo 0712557099) Wabillaah Tawfiiq MKURUGENZI

5
K a t i k a s e h e m u h i i ya leo tutatazama namna ya uboreshwaji wa mfumo wa muungano ili uwe na nguvu za kisheria, legitimacy (uhalali na kukubalika) kwa wananchi na pia maendeleo yaliokusudiwa katika uundwaji wake. Kwa sasa mfumo wa serikali mbili kuelekea moja, umefeli na kuundeleza ni kuendeleza makosa yaliyoleta chuki, fitna na ukiritimba mkubwa wa maendeleo nchini. S i n a h a j a ya k u r e j e a historia ya muungano huu au uasisi wake kwa sababu ya controversies (mkanganyiko wake) zinazouzonga mfumo mzima wa muungano kuanzia uundwaji wake na miaka karibu hamsini ya uhai wake. Ila tutatazama namna ya kuuboresha na kuhakikisha mfumo ujao utajenga culture (utamaduni) wa kuaminiana, kufahamiana na kurejesha heshima iliokuwa kama ni lengo la kuungana hasa kwa namna ya Wazanzibari walio wengi walivyoufahamu muundo huu na kuamini kama ndio maudhui makuu ya uundwaji wake. Nasema hivi kwa sababu kumetokea taswira za aina mbili za upokewaji wa muungano, upande mmoja hususan ndani ya mamlaka ya Z a n z i b a r wa k i a m i n i uwepo wa nchi ya Zanzibar kama ni jambo muhimu katika maamuzi yoyote ya uwepo wa muungano huu wakati upande wa pili ukijijenga zaidi katika safu za kuhakikisha muungano huu utakuwa kama ni wa nchi moja iliyokamilika. Imani yangu na Wazanzibari walio wengi ni kwamba Zanzibar ni nchi iliyokamilika na kujiendesha kwa misingi ya kimamlaka ya n a y o o n g o z wa n a i l e mamlaka kuu ya Rais pamoja na serikali aliyoiunda baada ya kuridhiwa na uchaguzi unaotegemewa kuendeshwa kwa misingi ya demokrasia. Katiba ya Zanzibar hususan baada ya mabadiliko ya 2010 yameonyesha kwa uwazi bila ya kuweweseka kwamba ni nchi na ikaenda mbali zaidi kuhakikisha mamlaka ya mkuu wa nchi hii hayatakuwa na kigugumizi kwa kuingiliwa na nguvu nyengine ndani ya muungano hasa baada ya kuhakikisha kwamba ni Rais wa Zanzibar pekee mwenye madaraka na uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikoa bila ya ushauri wa ye y o t e k i n y u m e n a ilivyokuwa awali. Uthibitisho wa haya ni kura ya maoni ambayo inatazamwa kama ni mfano wa uchaguzi pekee ulioendeshwa kwa uwazi zaidi huku kundi la wapiga kura (yes vote) likibeba nguvu ya zaidi ya asilimia 66 ya wananchi walioikubali kura ya maoni hiyo. Katika manifesto ya CCM ya mwaka 2010 s u a l a l a m a b a d i l i k o ya katiba halikuwemo na

Makala

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013


huu. Hatuwezi kuendelea kuwa na Wazanzibari ndani ya bunge la muungano wanaopiga kura bajeti za wizara zisizo za muungano huku tukiwa na Baraza l e t u m a h s u s i k wa a j i l i yetu wenyewe. Hatuwezi kuendelea na mfumo wa vyama kushika hatamu zaidi hata ya katiba ya nchi na matakwa ya wananchi katika nchi yenye mfumo wa d e m o k r a s i a . U m m a h a u t a t u v u m i l i a t u k i wa wepesi wa kulalamika pale yanapotufika lakini tukawa wagumu wa mabadiliko yataondosha kero lukuki zinazorudisha nyuma maendeleo ya wananchi. Kauli ya mheshimiwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda ndio iliozaa mabadiliko ya katiba ya 2010, sasa utawezaje kutamani rais mwenye mamlaka kamili bila ya nchi yenye mamlaka kamili? Watetezi wakuu wa mfumo wa muungano huu ndio hao hao waliosimamia, kuyapitisha na kuyaamini mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya 2010 wakijuwa wazi kwamba ile ni road map ya mabadiliko ya mfumo wa serikali mbili. Miaka 50 ya muungano imezaa kero zaidi badala ya suluhisho, hivyo wanaoamini kwamba mfumo wa sasa unahitaji utatuzi tu wa kero tuseme viongozi waliopita hawakuwa na nia ya kweli ya kutatua kero hizo hata washindwe kwa miaka 50? Hawaoni kwamba tatizo si kero kwa vile kero ni zao la mfumo wa sasa na kinachohitaji kurekebishwa ni mfumo mzima unaozidisha kero na hasama kila kukicha? Ndoto ya Wazanzibari katika mfumo mpya wa muungano tuutakao ni wa uwazi wenye nia ya maendeleo sio kiutawala, unaongozwa kwa misingi ya haki, heshima na usawa. Ikiwa tutatakiwa kuchangia kwa nini tusielezwe kwa uwazi formula itayotumika tukizingatia pia udogo wetu na kwamba mchango weu tutayoitia katika muungano ilingane pia na tutakachopata katika mapato tutayoigawiana. Bunge dogo la muungano pamoja na serikali ndogo ya muungano kwa yale tutayokubaliana n a a z m a k u b wa i l e n g e maendeleo sio mlolongo wa watawala. Wananchi baina ya Zanzibar na bara tumeweza kuishi kwa vizuri kabla ya hata ya muungano, historia inaonyesha hakukuwa na mpasuko wa malumbano na naamini kwamba kinachoulinda muungano huu sio katiba au mfumo wa sasa bali historia ya pande mbili zilizojengeka kwa heshima, maelewano na amani. Tunahitaji mabadiliko ya kweli yatayoondosha kero na kelele za muungano ili tuzijenge nchi zetu kwa kutumia muungano kama asasi ya maendeleo na chachu ya mshikamano wa Afrika nzima. (Makala kwa hisani ya Farrell JNR Foum)

AN-NUUR

Ndoto ya Zanzibar itatimia


Haki sawa, heshma katika muungano

wengi tunaamini kwamba mabadiliko ya katiba ya muungano yameibuliwa na mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya 2010 hasa baada ya kuona kwamba katiba mbili haziendani kimantiki hata kisheria na kwa vile kura ya maoni ya Zanzibar ilibeba sehemu kubwa ya wa n a n c h i wa l i o i p i t i s h a hakukuwa na budi zaidi ya kuifanyia marekebisho katiba ya muungano ili iendane na sauti ya asilimi 66 ya Wazanzibari. Muundo ambao mheshimiwa Warioba na tume yake waliokuja nao umethamini kauli ya wananchi wanaounda muungano huu na kwamba ile dhana ya udogo wa sehemu ikawa ndio kigezo cha kuburura maoni yao iliondoshwa kwa vile msingi mkuu wa muungano ni nchi mbili bila kujali ukubwa au idadi ya watu wa nchi ziliungana na ni lazima mabadiliko yoyote yathamini maoni ya pande mbili na huru ya mwenzake ili kupata makubaliano baina yao na kuunda kitu kitachokiubalika na wote. Ndio maana ukakuta hata baada ya mamilioni ya Watanganyika waliotamani serikali moja hayakuridhiwa kuwekwa katika muswada wa kwanza wa katiba kwa sababu yalipingana n a ya Wa z a n z i b a r h a t a wakiwa na idadi kubwa ya watu ikilinganishwa na bara. Maoni yangu ni kwamba Mheshimiwa Warioba ametupa heshima tunayostahili Wazanzibari katika muungano huu na pia matumaini ya kwamba mfumo ujao utaweza kuwa n i k i e l e l e z o k i p ya c h a mabadiliko makubwa zaidi katika mfumo wa muungano utaojengwa kwa misingi thabiti ya kuheshimiana, kuaminiana, haki na usawa. Wengi tunaamini mfumo w o w o t e wa m u u n g a n o katika ndoto ya Wazanzibari iendane na kauli mama ya Zanzibar kama ni nchi na yenye kujiendesha yenyewe kimamlaka. Mifumo butu yenye taswira moja lakini lengo lililojificha halitakubaliwa katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi hasa ukizingatia

kwamba ari ya kuja na mfumo wa mkataba haukuwa na uasisi wa chama chochote bali wananchi wa kawaida ndani na nje ya visiwa hivi walioona mbali zaidi na kuhakikisha mfumo ujao hautakuwa na kigugumizi chochote juu ya uhalali wa kuwepo kwa taifa la Wazanzibari. Hili linawezekana hata ndani ya mfumo wa serikali mbili ikiwa yaliomo ndani ya muungano yatazingatia maoni ya wengi yalioweka wazi msimamo wa Zanzibar kama ni nchi yenye kila nyenzo ya kujitosheleza na kujiendesha y e n y e w e . M h e s h i m i wa Warioba kafahamu maana kamili ya muungano wa mkataba na ndio maana akaja na muswada wa mwanzo ya m f u m o wa s e r i k a l i t a t u n a u k a k u t a we n g i waliopendekeza mfumo wa mkataba hawakuwa na upinzani wa serikali tatu kwa sababu ya yaliyomo ndani ya muswada huo uliopunguza mambo ya muungano kutoka zaidi ya 30 hadi kufikia saba. Ndio ukakuta wanamageuzi wa kweli hawazingatii jina la mfumo wa muungano bali yaliyomo yanayobeba muungano wenyewe na kwa sasa nguvu zimeelekezwa katika kuyafuta yale yatayokwenda kinyume na azma ya mamlaka kamili. Hoja zisizo na mashiko kama gharama za muungano katika mfumo wa serikali tatu zenye kujitegemea zinaelekezwa zaidi kama khofu hususan kwa Wazanzibari kama vile nchi hii haitaweza kujiendesha wenyewe wakati wahubiri hawa wanashindwa, kuwaeleza watu kabla ya muungano huu serikali ilijiendesha vipi? Ukiangalia zaidi kabla ya kifo cha Mzee Karume muungano huu haukuwa na msimiko mkubwa kama baada ya kifo chake na kujichanganya kukubwa kulikounda CCM ambayo ikabeba dhima kubwa zaidi hata ya mamlaka ya kikatiba ya nchi. Katiba ya nchi ikawa chini ya katiba mama ya chama na kidogo kidogo tukaona mapungufu ya muungano yakizidi kukuwa na kila alieweza kupayuka kupinga msukumo wa chama wakawa maadui wa nchi. Mpaka

leo hii sifahamu iweje Rais wa nchi aliechaguliwa na wananchi, akafukuzwa urais huo ambao aliupata kabla ya hata muungano wa ASP na TANU kwa kutazama m a t a k wa ya n c h i ya k e kwanza. Hakuna sababu wala uhalali wowote zaidi ya ghilba za kupitia mlango wa nyuma kuhakikisha lengo si muungano bali nchi moja bila ya hata maoni ya wahusika wakuu. Kauli za Zanzibar tunachangia kiasi gani katika shughuli za muungano zisiwe ndio kisingizio cha mfumo wa sasa, sugar coating makosa na kuficha tathmini za kitaaluma zilizoonyesha namna gani Zanzibar inapoteza fursa kubwa za maendeleo katika mfumo wa sasa kwa sababu rahisi rahisi kama hizi ni ukosefu wa uoni pamoja na dhana nzima ya uongozi wa misingi ya haki. Masuala ya kujiuliza ni namna gani kwa mfano 4% ya mgao kwa Zanzibar uliofanyiwa tathmini miaka ya 60 wakati idadi ya watu laki tatu tu lakini ikabaki hivyo hivyo kwa miaka karibu hamsini wakati sasa kuna zaidi ya watu milioni moja na nusu! Au t u t a z a m e h i z o gharama za uendeshwaji mfano jeshi la wananchi, kati ya nchi ya milioni arobaini ikilinganishwa na mchango wa milioni moja utakuwa katika uwiano gani? Zanzibar ikiwa na eneo dogo mara mia kuliko bara, wapi kunahitajika ulinzi zaidi na hivyo mchango wa Zanzibar utafanyiwa tathmini uwe kiasi gani? Au tutazame kwa upande wa urahisi zaidi, ikiwa tunaambiwa tuchangie sawa baina yetu jee na mapato tutagawiwa kwa misingi hio ya usawa kama ilivyo kwa uchangiaji? M u u n g a n o u n a j e n g e wa mazingira ya kutishana badala uwazi utakaojenga heshima na kuthaminiana b a i n a ya j u m u i a m b i l i zilizokaa pamoja kabla hata ya uhuru wa Tanganyika na hata Mapinduzi ya Zanzibar. Hatuwezi kuendelea na mfumo wa sasa ambao unamuweka mkuu wa nchi moja katika baraza la mawaziri wa muungano na kutompa heshima yake kikatiba kama ilivyokuwa wakati wa kuasisi muungano

6
Na Mwandishi Wetu

Makala/Tangazo

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

Hakukaliki! Wakristo, Waislam washikiana mapanga, bunduki


Jamhuri ya Afrika ya Kati (Central African Republic-CAR) ipo katika hatari ya kutumbukia katika maafa yaliyowahi kuikumba Rwanda. Kama walivyokuwa wakiuwana ndugu wa nchi moja, Watutsi na Wahutu, CAR wao wanachinjana Waislamu na Wakristo. Mgogoro ambao mwanzo wake ulikuwa wa kisiasa, hivi sasa umetumbukizwa chuki za kidini hakuna udugu tena wala ujirani baina ya Muislamu na Mkristo. Wa t u w a n a k i m b i a vijiji vyao wakikimbia mapigano na mauwaji huku wanyonge wakiwemo wazee wakibaki kusubiri majaaliwa yao ambayo ni ama kupigwa risasa au kukatwa shingo kwa panga. Hadi sasa takriban watu 1000 washauliwa huku vurugu zikiendelea katika mji mkuu Bangui na viunga vyake. Ukiacha hali tete iliyokuwa huko nyuma, vurugu na mauwaji ya hivi sasa yameanza baada ya wanamgambo wanaomuunga mkono na watiifu kwa, Rais aliyepinduliwa Francois Bozize, kuvamia baadhi ya vijiji vya Waislamu na kufanya mauwaji. Wa n a m g a m b o h a o m a a r u f u k wa j i n a l a "Anti-balaka", (Balaka ikiwa na maana ya panga kwa lugha ya ki-Sango na Mandja), wanasema wao wapo kwa ajili ya kujilinda na kuwalinda Wakristo kutokana na wapiganaji wa Seleka. Hawa Seleka ni muungano wa makundi ya waasi wakiongozwa na Michel Djotodia ambaye h i v i s a s a n d i ye R a i s wa nchi hiyo baada ya kumpindua Bozize. Yapo madai kuwa baada ya kufanya mapinduzi, wapiganaji hawa wa Seleka wamekuwa wakifanya uvamizi katika vijiji vya Wa k r i s t o n a k u f a n ya mauwaji. Kutokana na hali hiyo, ndio Wakristo nao wakaunda Anti-balaka. Lakini yapo maelezo pia kuwa wanamgambo wanaomuunga mkono Bozize, wameamua kupigana kwa vile

h a wa t a k i k u o n a n c h i ikitawaliwa na kiongozi Muislamu. Michel Djotodia, ni Muislamu kutoka eneo la Kaskazini lenye Waislamu wengi ambalo kwa muda m r e f u l i m e t e l e k e z wa bila huduma muhimu za kijamii na kimaendeleo na hivyo kuwa nyuma sana kimaendeleo ikilinganishwa na sehemu za Kusini walipo Wakristo wengi. Wakristo katika nchi hiyo ni asilimia 50 ya watu wote huku Waislamu wakiwa ni asilimia 15 tu. Waliobaki ni watu wa dini za asili. Jumala yote ya watu wa Afrika ya Kati ni kiasi 4,600,000 (milioni nne laki sita). Hali ilivyo sasa ni i l e ya p i g a n i k u p i g e Baadhi ya wapiganaji wanaosababisha mauaji ya raia Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa maana kuwa AntiBalaka wakivamia kijiji (Central African Republic-CAR). cha Waislamu, Seleka nao wanapiga kijiji cha Wakristo. Miili ya watu waliouliwa inaonekana ikizagaa mitaani, huku baadhi k u o n a k a n a k wa m b a makabila makuu mawili, (katika ile inayotambuliwa Na Omar Msangi Waislamu wa Tanzania ndivyo ambavyo sababu za kuwa ni ya Waislamu) kisiasa zimetumbukizwa ikifikishwa katika Misikiti wamechelewa. WIKI iliyopita niliswali K w a m s e m o w a k e kujenga chuki baina ya na mingine ikikusanywa Ijumaa katika msikiti w e n z e t u j a s i r i , s i s i wananchi Waislamu na n a wa t u wa M s a l a b a m m o j a j i j i n i D a r e s (Watanzania) tumekuwa Wakristo. Mwekundu. Salaam ambapo Khatib waoga na wanafiki wengi. I n a s e m e k a n a k u wa Na ukitaka kujua hilo, aligusia juu ya ghasia na Kwa maneno mengine katika hao walioshika huyu Michel, akiwa na mauwaji yanayotokea na mepesi amehalalsha na serikali, japo Rais ni h a m u ya k u wa R a i s , Afrika ya Kati. kupongeza kinachotokea Muislamu, hakuna hata a l i t u m i a m wa n ya wa Yapo baadhi ya mambo RCA huku akilinganisha mmoja anayezungumzia kuwepo Waislamu wenye alipatia, lakini nadhani hali ile na Jihad. suala la dini au kubadili malalamiko ya muda mrefu yapo mambo ya msingi Kwanza, kwa madai mfumo na utawala uwe wa dhidi ya serikali iliyokuwa aliyapotosha na hivyo yoyote yatakayokuwa, Kiislamu. ikiwakandamiza na kutoa ujumbe unaoweza yawe ni ya kidini au kisiasa L a k i n i h a t a h a o kuwabagua kwa miaka kuwa na athari mbaya na kijamii, hakuna namna askari wa Seleka, hawa mingi, akawakusanya kwa waumini waliokuwa y o y o t e m t u u n a we z a wametokana na makundi vijana wa Kiislamu wenye wakimsikiliza na nchi kwa kupongeza na kuhalalisha ya waasi, wasio na mlengo hasira na kuwatia katika ujumla. hali inayoendelea Jamhuri wala msimamo wa kidini Seleka. N i k w e l i k w a m b a ya Afrika ya Kati hivi kabisa, yaani Union of Yapo madai pia kuwa Wa i s l a m u wa A f r i k a sasa ambapo makundi Democratic Forces for alipata wapiganaji kutoka y a K a t i w a m e k u w a ya watu wenye silaha Unity (UFDR), Union Chad na Sudan. n a m a l a l a m i k o k u wa huvamia vijiji na kuuwa of Republican Forces Hata hivyo, baada ya wanabaguliwa. Na ni kweli watu wasio na hatia. (UFR) na Convention of kupata Urais, ameshindwa pia kuwa eneo la Kaskazini Waislamu wanavamia vijiji Patriots for Justice and k a b i s a k u w a d h i b i t i linalokaliwa na Waislamu vya Kikristo na Wakristo Peace (CPJP)! Kama ni wapiganaji hawa, kwa wengi, limeachwa bila ya wa n a va m i a v i j i j i v ya Muislamu, ni Muislamu hiyo wanajifanyia yoyote maendeleo ikilinganishwa Waislamu. wanayotaka. jina tu. na Kusini. Baada ya kuongoza Inavyoonekana ni kuwa Kama ilivyokuwa Lakini ni kweli pia kuwa kwa Watutsi na Wahutu, kwa Jamhuri ya Afrika ya mapambano ya waasi na kumekuwa na malalamiko R w a n d a , n d i y o h a l i Kati, labda kama ilivyo kufanikiwa kuyashinda kama hayo miongoni mwa inayotaka kutokea RAC Tanzania, hakuna namna m a j e s h i y a n c h i n a Waislamu katika nchi hivi sasa. ya kuchochea chuki za kikosi cha Afrika Kusini hii. Hili sina mgogoro kilichokuwa kikimlinda Kama h u w e z i kikabila zikalipua nchi. nalo kama mzungumzaji k u h a l a l i s h a m a u wa j i I k a o n e k a n a k w a Rais Francois Bozize, alivyojaribu kuliweka. ya Wahutu na Watutsi, vile Waislamu ni kama wapiganaji wa Seleka T a t i z o l i n a k u j a huwezi pia kuhalalisha wa n a i s h i e n e o l a o l a walimtangaza Michel p a l e a l i p o d a i k u w a mauwaji ya Waislamu na Kaskazini na limeachwa Djotodia kama kiongozi kinachotokea Afrika ya Wakristo. nyuma kwa muda mrefu, mpya wa CAR. Kati ni mapambano ya Michel Djotodia Kama ilivyokuwa kwa h u o u m e k u w a n d i o Waislamu ya kupigania Rwanda, kwamba sababu mwanya mzuri. Chuki aliapishwa Machi 24 kuwa h a k i n a k w a m a a n a za kisiasa zimetumika z ime pa nd i k i z wa s a s a Rais ambapo Marais Idriss hiyo akayapongeza na kupandikiza chuki kwa Inaendelea Uk. 7 Inaendelea Uk. 7

Hakuna Jihad RCA

Makala

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

Inatoka Uk. 6

Hakukaliki! Wakristo, Waislam washikiana mapanga, bunduki


wengi kukimbilia hapo wakitafuta hifadhi. Wa t u w a n a o g o p a kuondoka hapa Kanisani kurudi makwao, japo wanaishi jirani tu, wanaogopa kuuliwa. Wanasema waandishi hao wakiwanukuu watu waliojificha hapo. Inaelezwa kuwa zaidi ya watu 35,000 wamejificha katika kanisa hilo wakihofia kushambuliwa na Seleka ambao nao wanadai kuwa watu wa eneo hilo ndio wanaounda kikosi cha wanamgambo wa Kikristo wanaopita katika vijiji vya Waislamu wakiuwa watu ovyo. Baada ya kupata uhuru mwaka 1960, Afrika ya Kati iliongozwa na Rais David Dacko ambaye alikuja kupinduliwa mwaka 1965 akashika mwanajeshi JeanBdel Bokassa. Huyu Bokassa alijitangaza Mfalme mwaka 1976 na kuitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma (udikiteta). Hata hivyo, mfalme huyo alipinduliwa na kuuliwa mwaka 1988 kwa makosa ya ubadhirifu wa mali za nchi na mauwaji. U t a wa l a wa k i j e s hi ulifikia hatma mwaka 1993 ambapo Ange-Flix Patass, alichaguliwa kuwa Rais. Patass akapinduliwa mwaka 2003 akaingia Franois Boziz ambaye awali alikuwa kiongozi wa waasi. Makundi ya upinzani na uasi yaliendelea kuwepo na mwaka 2007 makundi matatu Union of Democratic Forces for Unity (UFDR), Union of Republican Forces (UFR) na Convention of Patriots for Justice and Peace (CPJP) yaliungana na kuunda Seleka. Mwaka 2012 Seleka waliteka eneo la Kaskazini na baadhi ya maeneo ya Katikati ya nchi. 2013 Seleka wakaingia mji mkuu, Bangui. Boziz akakimbia na kiongozi wa waasi Michel Djotodia kutangazwa Rais. Japo ikiwa na utajiri mkubwa wa madini muhimu, Afrika ya Kati ni moja ya nchi masikini sana Afrika. Hapana shaka ghasia na vita kama hii ya weyewe kwa wenyewe, itazidi kuisambaratisha nchi hiyo.

Deby wa Chad na Denis Sassou Nguesso, wa Congo (Brazaville), walihudhuria. Kama vile kushangaa, vyombo vingi vya habari vimekuwa vikimtaja Djotodia kuwa ni kiongozi wa kwanza Muislamu katika nchi ambayo wengi ni Wakristo. He is a Muslim, while the population of the Central African Republic is mostly Christian. Mengi ya magazeti yamekuwa yakiandika. Toka ilipopata uhuru wake mwaka 1960 kutoka kwa wakoloni, Ufaransa, Afrika ya Kati, imekuwa katika hali ambayo si ya kutulia, yakiwepo mapinduzi ya kijeshi na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo, hii ni mara ya kwanza migogoro na machafuko katika nchi hiyo kuchukua sura ya mgogoro wa kidini. Ukiacha malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa Waislamu kwamba wanabaguliwa, kunyanyaswa na kuhujumiwa; bado Wakristo na Waislamu wamekuwa wakiishi pamoja kwa amani hadi ulipofumuka mgogoro huu Machi mwaka huu 2013 mara tu baada ya kiongozi wa Seleka Michel Djotodia kuchukua madaraka. Akiongea kutoka mji mkuu Bangui, Mr Djotodia anasema lengo lake ni kuitisha uchaguzi baada ya muda mfupi na kwamba anashikilia madaraka kwa muda tu. Hata hivyo, ambalo limekuwa gumu kwake hadi sasa ni kuleta utengamano wa kijamii. Hakuna kuaminiana tena baina ya Waislamu na Wakristo hali ambayo imefikia kuwa Waislamu wakiwa Misikitini huswali na silaha zao kibindoni au kwa zamu huku wengine wakichunga usalama. Hali hiyo ilionekana Ijumaa iliyopita ambapo, waumini waliingia misikitini na bunduki zao aina ya Kalashnikov. Harakati za Seleka, z i l i a n z a t o k a m wa k a 2003 Bozize alipoingia madarakani baada ya kumpindua Rais AngeFlix Patass ambapo a n a d a i wa k u wa t o k a

Inatoka Uk. 6 wananchi wanachinjana. Tu n a p o a n g a l i a h a l i hii ya Afrika ya Kati, tuizingatie na hali ya hapa nchini ambapo, baadhi ya watu wamekuwa wakipiga propaganda na kuleta uchochezi wa kuonyesha kuwa Waislamu ni magaidi wa l i o p a n i a k u c h o m a makanisa na kuuwa viongozi wa Kikristo. Ya l i a n z a k u s e m w a na aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Stith na yakawa yanakaririwa mara kwa mara na baadhi ya wachungaji. La kusikitisha ni kuwa hata baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali, walimeza propaganda na kampeni hii chafu ya kuliangamiza Taifa. Hapana shaka tutakumbuka pale Kamanda wa Polisi alipotangaza kuwa Polisi watalinda makanisa na kuwalinda Wakristo, eti kwa hofu ya kushambuliwa na Waislamu. Tutakumbuka pia ile kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu Bwana Sumaye iliyopelekea kukamatwa

Hakuna Jihad RCA


kwa Profesa Jahazi. Lililo la uhakika ni kuwa propaganda chafu kama hizi zikiachwa mpaka zikakolea, tusijeshangaa yakitukuta ya Seleka na Ant-balaka. Muhimu kwa Waislamu: Zipo juhudi kubwa sana hivi sasa za kuitumbukiza nchi hii katika machafuko. Uchochoro unaotumika ni wa namna mbili: Moja kuwatangazia u g a i d i Wa i s l a m u . Likikubalika hilo, watu wabaya walioandaliwa wanaweza kushambulia shabaha fulani fulani halafu inadaiwa kuwa ni Waislamu. Shabaha hizo zikiwa za Wakristo, hapana shaka itaita hasira za Wakristo. Bila shaka bado tutakuwa na kumbukizi nzuri yaliyojiri baada ya kupigwa risasi padiri kule Unguja na baada ya lile bomu la Kanisani Arusha ambapo watu walikimbilia kusema kuwa mhusika alivaa kanzu na kibandiko! Kumbe mtuhumiwa namba moja ni Victor! Huyu Victor yupo wapi? Ulizeni. Hivi angekuwa ni Abu Bakr, hali ingekuwa vipi? Kwa upande mwingine uchochoro unaotumika ni kuwaaminisha Waislamu kuwa wapo katika Jihad-hakuna Uislamu unaoweza kufanyika hivi sasa ila kwenda kupigana Somalia au kuanzisha vikundi na kujifunza silaha kwa ajili ya kupambana na ukafiri. Wapo watu maalum, wanasaikolojia waliosomea kazi zao kwa kazi hizo za kupumbaza na ku-program watu. Katika hali kama hii, kuna haja kwa Masheikh wetu katika Da wah na m a wa i d h a ya o k u wa makini na kuzungumzia kwa undani nini harakati za Kiislamu na mbinu za Dawah. Kuna haja pia kurejea katika historia na Sira ya Mtume (s.a.w) kuangalia, kama ni suala la kusimamisha Uislamu katika jamii, unapita wapi na wapi. Unapita njia gani na namna ya kufikisha dawah kwa wasio Waislamu (na Waislamu jina) hadi kuifanya jamii iwe ya Kiislamu.

Wnanchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (Central African Republic-CAR). w a k a t i h u o ( 2 0 0 3 ) kulinda amani. Ni kama makubwa zaidi yametokea amekuwa akiwabagua imepatikana sababu ya katika mji wa Bossangoa, watu wa Kaskazini. ukoloni kwa mlango wa a l i p o z a l i wa F r a n c o i s Bozize. CAR ni tajiri wa dhahabu, nyuma. Wanasema, mji huo almasi na uranium, lakini Wajanja, mabeberu inaonekana kuwa madini w a n a v u n a a l m a s i , umekuwa kama hame hayo yamekuwa kama d h a h a b u , u r a n i u m , ukiwa umejinamia. Watu laana na nuksi kwa nchi Waafrika (Waislamu na w a m e k i m b i a w e n g i hiyo kama ilivyo Congo Wakristo) wa Afrika ya wakitafuta hifadhi katika (DRC). Kati wanachinjana. miji na vijiji vya jirani. Kwa vurugu na Kwa mujibu wa taarifa ya Ni katika Kanisa mauwaji haya, tayari jeshi waandishi wa BBC, Laeila Katoliki pekee ambapo la Ufaransa limeingia Adjovi na Abdourahmane p a n a o n e k a n a u h a i kwa kile kinachoitwa Dia, ghasia na mauwaji k u t o k a n a n a w a t u

8
Inatoka Uk. 1 Afrika na dunia kwa ujumla. Wakati Waafrika na sehemu kubwa ya dunia ikimtambua Mandela kwa sifa hizo, na kwa hakika ndivyo alivyokuwa, wengine walimwona ni gaidi! Wengi watashindwa kuamini kwamba Hayati Nelson Mandela, alikuwa katika orodha rasmi ya magaidi ya Marekani hadi mwaka 2008, na miongoni mwa watu waliokuwa wakitizamwa kwa jicho la karibu huku akitakiwa kupata ruhusa maalum (special permission) kuingia Marekani. Ugaidi wake kwa Marekani ulikoma hivi karibuni tu, hadi ilipotimu April, 2008, baada ya Baraza la Congress kupiga kura kuondoa jina lake katika orodha hiyo. Ni miaka mitano tu imepita tangu jina la Nelson Mandela kuondolewa katika orodha hiyo maarufu kama America's terrorist watch list. Mimi Hall, mwandishi wa USA TODAY anafichua kuwa Condoleezza Rice, ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa utawala wa Rais wa z a m a n i wa M a r e k a n i George Bush, aliita hali hiyo kwa Mandela kuwa ni "embarrassing," na baadhi ya wajumbe wa Bunge

Makala/Tangazo

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013


ruhusa maalum (special waiver ) kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuingia nchini humo. Mandela alikuwa mpigania uhuru wa kweli na dunia nzima imemtambua hivyo leo hata kesho. Alishirikiana na wenzake kama akina Marehemu Oliver Tambo, m a r e h e m u Wa l t e r Sisulu na wengineo katika chama cha ANC kuuondoa utawala wa kibaguzi Afrika Kusini. Lakini ni ajabau kwamba wamekuwapo wachache waliona kitendo chake hicho kama sawa na vile vya Alqaeda. Sababu kubwa ya kuonekana ugaidi ni kupambana na Makaburu katika kudai haki na uswa na kuondoa dhuluma dhidi ya watu weusi ambao ndio wenye nchi yao. Kwa tafsiri hii unapata ukweli kwamba, hata al Qaeda nao wanapambana na mabeberu wa Magharibi, lengo ni kuondoa hiyo hiyo dhulma na kusaka haki. Habari zimeeleza kwamba Rais wa z a m a n i wa M a r e k a n i Ronald Reagan, ndiye aliyembandika Mandela lebo ya ugaidi na chama chake cha ANC akakiita kuwa ni shirika la kigaidi pia. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher, naye pia alimpa Mandela sifa hiyo hiyo na kumuunga mkono Reagan. Shirika la habari la AP lina habari kwamba wote Ronald Reagan na Margaret Thatcher, wa l i m t a m b u a N e l s o n Mandela kuwa ni gaidi. Kuna madai kwamba hata Waziri Mkuu wa zamani wa Australia, John Howard, naye alitumia neno "terrorism" alipofanya rejea juu ya Mandela. Lakini Thatcher n a R e a g a n wa l i k u wa mashujaa wakubwa wa kisiasa wa Howard, na wakati fulani aliungana nao katika kupinga m a k ub a l i a no a m b a y o baadae yalimtoa nje ya kifungo Mandela na hatimaye kuhitimishwa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Pa m o j a n a H o wa r d k u wa k a t i k a m r e n g o huo wa kumdhalilisha Mandela, bado mwaka 1999 alisafiri hadi Pretoria kuonana na mtu ambaye Inaendelea Uk. 11

AN-NUUR

Mandela alikuwa katika orodha ya magaidi ya Marekani hadi 2008


la Congress waliahidi kurekebisha hali hiyo. Ukiacha Mzee Mandela, kibali hicho maalum cha kuingia Marekani kiliwahusu pia wajumbe wengine wa chama tawala African National Congress (ANC) kilichoikomboa Afrika Kusini katika makucha ya ubaguzi wa rangi cha African National Congress. Katika miaka ya 1970 na '80s, ANC kilitambuliwa rasmi na utawala wa M a k a b u r u wa c h a c h e u l i o k u wa u k i i t a wa l a Afrika Kusini, kama kikundi cha kigaidi. Marekani mara moja iliunga mkono msimamo wa Makaburu na kuwa nchi ya kwanza kuitambua ANC kuwa ni kundi la kigaidi. Baadae Bi. Rice aliieleza Kamati ya Bunge la Senate, kuwa Idara yake inakusudia kuondoa kuzuizi hicho kwa wajumbe wa ANC kuingia Marekani. "Hii ni nchi ambayo tunafamu kuwa sasa tuna uhusiano mzuri nayo, Afrika Kusini, niseme tu wazi kwamba suala la kuweka kizuizi ni jambo linalokera ambalo bado nakusudia kukiondoa ndani ya kipindi changu, Itakuaje Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini asimtaje kiongozi mkubwa Nelson Mandela," alinukuliwa akisema Rice. Wajumbe wa Rep u blica n , H owa rd Berman, D-Calif., aliyekuwa Mwenyekiti wa House International Relations Committee, walijaribu kusukuma muswada huo ambao ungeondoa jina la Mandela katika orodha ya magaidi (watch lists). Ilitarajiwa kuwa mswada huo utapitishwa kabla ya Mzee Mandela hajasherehekea kufikisha miaka 90 ya kuzaliwa Julai 18, 2008. "Ni namna gani utu unakosekana, ANC wameonyesha mfano muhimu: Mafanikio yake yameleta mabadiliko kutoka mapambano ya silaha hadi kufikiwa amani. Lazima tufurahie mabadiliko haya ," alisema Berman. Mwaka 1990, Mandela alitolewa gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 jela kwa kudaiwa kufanya makosa

NAFASI ZA MASOMO KIDATO CHA KWANZA 2014 KATIKA SHULE ZAKE ZA KIPEKEE
KUNDUCHI GIRLS ISLAMIC HIGH SCHOOL REG. S.358 UNUNIO ISLAMIC HIGH SCHOOL REG. G 397

SHULE ZINAPOKEA WALE WOTE WANAOTAKA NAFASI I. KIDATO CHA KWANZA 2014 II. WANAORUDIA MITIHANI KAIDATO CHA NNE NA KITUO NI HAPOHAPO III. WANAO HAMIA WENYE MAADILI SAFI SIFA ZA KIPEKEE KWA SHULE HIZI TEULE WALIMU WENYE UZOEFU NA WALIO BOBEA SHULE ZINA ZINGATIA MAADILI YA KIISLAMU MATOKEO KITAALUMA MAZURI SANA NI DHAMU BORA NA MALEZI SAHIHI KUNA FENSI (UZIO) IMARA NA USALAMA KUNA ZAHANATI SAFI NA VIFAA VYA KISASA. MASOMO YOTE YANAFUNDISHWA PAMOJA NA MAARIFA YA UISLAMU NA LUGHA YA KIARABU ADA NI NAFUU NA INALIPWA KWA AWAMU KUNDUCHI GIRLS NI BWENI TU NA KUNA FORM 5 NA FORM 6 UNUNIO NI SHULE YA BWENI NA DAY PIA WASICHANA WANAPOKELEWA PANACHUO CHA KIPEKEE CHA UALIMU UNUNIO USAHILI NI KILA JUMAMOSI SHULENI FOMU ZINAPATIKANA SHULENI AU TUPIGIE KUPATA NAFASI KUNDUCHI GIRLS UNUNIO HIGH SCHOOL MKUU WA SHULE 0713 346537 MAKAMU 0713 515054 MKUU WA SHULE O717 008860 MAKAMU 0718 551784 AU 0718551784 WABILLAH TAWFIQ

ya jinai wakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi dhidi ya makaburu, ambao ulikuwa ukiwatesa watu weusi Afrika Kusini. Mwaka 1994, alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini. Senetor. Judd Gregg, R-N.H., alikuwa mmoja wa watu waliotaka wajumbe wa chama cha ANC kuingizwa katika orodha ya wahalifu hatari iliyoitwa "bureaucratic snafu" na kuahidi kumaliza tatizo. Pia kuna vyama vingine vilitizamwa na Marekani kama magaidi tishio, mfano ni Hamas, ambao nao waliingizwa katika orodha hiyo ya magaidi. Homeland Security Secretary, Michael Chertoff anasema "kwa akili ya kawaida" inakuambia Mandela lazima aondolewe katika orodha ya magaidi. Anasema suala hili "linaibua hoja ya hatari na ngumu kuhusu makundi gani yachukuliwe kuwa ni ya magaidi na yapi siyo." Hata pale wajumbe wa chama cha ANC walipoomba visa kwenda Marekani, walilazimika k wa n z a k u h o j i wa n a kutakiwa kupata ruhusa maalum kuingia katika Taifa hilo. Mwaka 2002, Mwenyekiti wa zamani wa ANC, Tokyo Sexwale, alikataliwa kupata visa. Mwaka 2007, Barbara Masekela, Balozi wa Afrika Kusini nchini Marekani kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, alikataliwa visa na hata hiyo ruhusa maalum ili kumtembelea mjomba wake aliyekuwa mgonjwa hadi mjomba wake huyo alipofariki dunia. Laurie Oakes, katika mtandao wa www. adelaidenow.com, yeye anasema kuwa anapata wakati mgumu kuelewa, ni kwa jinsi gani Marekani na Uingereza kwa kipindi chote hicho walimworodhesha Mandela kama gaidi hadi Aprili mwaka 2008 walipomuondoa wakati wanaonekana kumpenda. Oakes, anaeleza kwamba hata alipoalikwa na Rais George W. Bush katika Ikulu ya White House Washington mwaka 2005, alilazimika kupata

9
Na Said Rajab
RAIS Barack Obama wa M a r e k a n i , a m e ya i t a makubaliano ya mpango wa nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ya Magharibi kuwa ni ya kihistoria. Kwa mara ya kwanza, tangu mwaka 2003 mazungumzo hayo yalipoanza, mataifa hayo yameweza kusimamisha kile kilichoitwa mpango wa silaha za nyuklia wa Iran. Barack Obama amesema: "Simply put, they cut off Iran's most likely paths to a bomb." Kwa maneno rahisi, makubaliano hayo yanafunga kabisa njia ya Iran kutengeneza bomu. Dola ya Kiyahudi ya Israeli inapinga vikali makubaliano h a y o . Wa z i r i M k u u wa Israeli, Benjamin Netanyahu, ameyaita kuwa ni "makosa ya kihistoria". Kwa upande wake, Iran imeshangilia sana makubaliano hayo. Kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei, amenukuliwa akisema: "Rehema za Mwenyezi Mungu na uungaji mkono wa taifa hilo ndiyo sababu za mafanikio yaliyofikiwa", wakati Hassan R o u h a n i , R a i s wa I r a n amesema: "Makubaliano haya yanazinufaisha nchi zote za ukanda huo na amani ya dunia". S a s a t u a n z e k u f a n ya uchambuzi wa makubaliano hayo, ili tuweze kufahamu vizuri, nani hasa aliyeshinda na nani aliyepoteza. Ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au mataifa ya Magharibi? Jawabu, bila shaka lipo katika kile kilichokubaliwa. Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Iran na Mataifa sita yenye nguvu, yanayojulikana kama P5 + 1, yaani Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, China na Ujerumani ni ya mpito, na ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye makubaliano mapana zaidi siku za mbele. Makubaliano hayo yaliyofikiwa mjini Geneva hivi karibuni, yameainisha masharti yafuatayo: Iran itasimamisha kuweka 'centrifuges' mpya za madini ya uranium, na pia kuacha kutumia maelfu ya 'centrifuges' ambazo zimeshawekwa lakini bado hazijaanza kurutubisha madini ya uranium. Ghala la mafuta ya nyuklia ya Iran katika kipindi cha miezi sita, haitaruhusiwa kuongezeka na kuvuka kiwango kilichopo sasa. Katika utekelezaji wa hilo, Iran itakabiliwa na chaguo la ama kusitisha urutubishaji wa madini ya uranium, au kubadili madini yake ya uranium na kuwa sahani za mafuta ya metali (metal fuel plates). Iran imekubali kusimamisha uzalishaji wote wa kile kinachoitwa asilimia 20 ya madini ya uranium yaliyorutubishwa, aina ya mafuta ambayo yanaweza kubadilishwa kwa urahisi na kuwa uranium iliyorutubishwa kwa kiwango cha juu zaidi kinachoweza kutumika kutengeneza mabomu ya nyuklia. Maghala yote ya Iran ya mafuta ya asilimia 20, ambayo ni chini kidogo ya paundi 450, yatalazimika kuzimuliwa kwa kubadilishwa na kuwa metali au kuchanganywa na uranium asilia ili kupunguza usafi wake. Iran itatakiwa kusitisha kazi ya kujenga 'fuel rods' na vifaa vingine vya kinyuklia katika kinu chake cha Arak, kinachoshughulikia madini ya plutonium. Vituo vya nyuklia vya Iran vitatakiwa kuangaliwa k a t i k a n a m n a i s i y o ya k a wa i d a , v i k i t e m b e l e wa k i l a s i k u n a wa k a g u z i wa kimataifa ambao pia watakuwa na uwezo wa kurekodi kwa kutumia vifaa vya video. Iran itapata motisha ya kiuchumi inayofikia dola za kimarekani bilioni 7 katika kipindi cha miezi sita ya utekelezaji wa mkataba huo wa mpito. Ni jambo la wazi kwamba kutoka kwenye makubaliano hayo, kuna idadi kadhaa ya vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran, kwa malengo ya kuvuruga uwezo wa nchi hiyo kuzalisha mabomu ya nyuklia. Isitoshe, Iran pia imefungua rasmi mlango wa ukaguzi wa kina zaidi wa kimataifa dhidi ya vinu vyake vya nyuklia. Ukaguzi huo unaweza kuvuruga kabisa uwezo wa kinyuklia wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu, ambao imeujenga kwa gharama kubwa na maumivu makali, katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Mafanikio ya mataifa ya Magharibi katika kuvuruga uwezo wa kijeshi wa Iraq, na uwezo wa silaha za kemikali wa Syria, kupitia ukaguzi wa Umoja wa Mataifa, ni dalili ya wazi ya kile kinachoweza kutokea

Makala

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

Muafaka wa nyuklia, Iran yapigwa bao!


Iran katika siku za baadaye. Pamoja na yote hayo, bado Iran inayaona makubaliano ya Geneva kama ushindi! Kwa mfano,Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammed Javad Zarif, amesisitiza kwamba makubaliano hayo ya Geneva, yanatambua wazi haki ya Iran kurutubisha madini ya uranium. Pia amesema makubaliano hayo yameondoa tishio la mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Iran. Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, ana mtazamo tofauti na huo. Kuhusu tishio la Marekani kutumia nguvu dhidi ya Iran, John Kerry wala hamung'unyi maneno: "Ukweli ni kwamba Rais ndiye mwenye chaguo la kutumia nguvu, kama Amiri Jeshi Mkuu, na ameshasema wazi kwamba bado hajaondoa tishio hilo mezani". Kwa muonekano wa nje, inaonyesha wazi kwamba Iran ndiyo iliyopoteza katika makubaliano hayo. Dola ya Kiyahudi na mlezi wake mkuu Marekani ndiyo washindi halisi. Israeli haitakiwi kuharibu sehemu y o y o t e ya m a k o m b o r a yake 100 ya kinyuklia. Na inavyoelekea, Marekani sasa itaitumia Iran kuleta utulivu nchini Syria, Iraq na Afghanistan. Huo ni uchambuzi mdogo tu, wa siasa za kimataifa katika eneo la Ghuba na Mashariki ya Kati. Sasa turudi kwetu. Mwenyezi Mungu anaelekeza nini? Wasomaji wangu naomba mnifahamu, lengo siyo kuishambulia Iran, bali ningependa kwa pamoja, tuyaangalie mambo hayo kupitia miwani ya Kiislamu. Uislamu unazikataza nchi za Waislamu kusalimisha rasilimali zake za kimkakati kwa mataifa ya kibeberu. Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur'an Tukufu: "Na Mwenyezi Mungu hatawajaalia makafiri njia ya kuwashinda Waislamu" Qur(4:141) Badala ya kusalimu amri kwa mataifa yenye nguvu ya Magharibi, na kusalimisha sehemu ya miundombinu yake ya kinyuklia, Iran ilipaswa kuendelea kujenga uwezo wa kuunda silaha mbalimbali za kinyuklia, ambazo zingeweza kutumika si tu kuilinda nchi hiyo, bali Umma mzima wa Kiislamu. Msimamo huo unaungwa mkono na Aya ifuatayo ya Mwenyezi Mungu: "Basi waandalieni nguvu mziwezazo na mafarasi yaliyofungwa tayari tayari ili kwazo muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, mnaowajua na msiowajua, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na chochote mtakachokitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, mtarudishiwa kamili sawa sawa wala h a m t a d h u l u m i wa " Q u r (8:60). Ukweli wa mambo ni kwamba kuulinda Umma wa Waislamu duniani, ni jambo lisilo na nafasi katika fikra za uongozi wa Iran. Iran imekuwa ikiusaidia kwa udi na uvumba utawala wa Bashar al - Assad nchini Syria, Hamid Karzai wa Afghanistan na Maliki wa Iraq. Vi o n g o z i h a o wa t a t u wanapambana vikali na m a k u n d i ya Wa i s l a m u kwenye nchi zao, ambayo ya n a t a k a k u s i m a m i s h a tawala za Kiislamu. Vi o n g o z i h a o wa t a t u pia wanaungwa mkono na mataifa yenye nguvu ya magharibi katika mradi huo. Iran kusalimisha mpango wake wa nyuklia kwa mataifa ya Magharibi, inathibitisha wa z i k wa m b a i l e I r a n tuliyokuwa tukiifahamu awali, sasa imebadilika sana. Utii wa Iran umehamia kwa maadui wa Waislamu, kama maneno ya Mwenyezi Mungu yanavyothibitisha: "Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako? Nao wanataka wakahukumiwe kwa njia isiyoafiki Sharia; na hali wameamrishwa kukataa njia hiyo. Na shetani anataka kuwapoteza upotevu ulio mbali (na haki)" Qur (4:60)

Inawatangazia nafasi za masomo katika shule zake za 1. Luqman Islamic Seminary ( Kidato cha I-IV) 2. Luqman Pre & Primary school (darasa la I- VII) MASOMO YANAYOFUNDISHWA NI: Sayansi, Biashara, Sanaa Lugha ya Kiarabu, Qur-aan na Dini ya Kiislamu. Fomu Zinapatikana: 1. Shuleni Luqman 2. Mapambano Tution Centre, Muone Mr. Mussa au Mr. Charles. Shule ipo Sinza jirani na Hospitali ya Palestina. Usaili utafanyika kila siku za kazi saa 2:00 asubuhi - 8:00 mchana. Jumamosi utafanyika saa 3:00- 6:00 mchana. Wahi kuchukua form. Ada zetu ni nafuu na zinalipwa kwa awamu Mlete mwanao kwa elimu na malezi bora Kwa mawasiliano zaidi piga simu. 0713 819 391 (Sekondari) 07657 757 075 (Primary) 0712 044 830

JUMUIYA YA WAISLAMU WA SINZA

10
Karibuni Mashababu kongamano la Afrika Mashariki
Hodi hodi gazetini, Mhariri samahani Niweke japo pembeni, nialike ikhiwani Kutoka kote nchini, pamwe nchi za jirani Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni. Mwaliko tunakupeni, wa kongamano la dini, Katu msijeukhini, vijana upokeeni, Pamoja jumuikeni, kujadili yenu dini Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni. Kenya twakualikeni, Uganda, Rwanda njooni Na Burundi karibuni, Tanzania kwa amani Jisikieni nyumbani, ndani ya Mwanza jijini Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni. Mwaliko uitikeni, wa shule na mitaani Kadhalika wa vyuoni, msijitenge pembeni Wa aidha karibuni, wa kada zote jamani Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni. Msijeuliza lini, mfike kongamanoni Sikizeni kwa makini, na mtie nukuuni Kumi na mbili fikeni, Desemba Mwanza jijini Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni. Kadhalika muda gani, ngoja nikujulisheni Aula nyote fikeni, mubakira kituoni Jamia Msikitini, u katikati jijini Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni.
Mwapaswa kuja na nini, mapema nakujuzeni 'Notibukuyo' na peni, vyote tia mkobani Na shuka zikumbukeni, kwa sitara naumuni Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni. Maakuli mtimani, 'sijewaza asilani Kadhalika walakini, kwa sharabu ondoeni Vyote hivyo kwa yakini, 'free' kongamanoni Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni. Nauli nakujuzeni, ya safari andaeni Ya kuja kongamanoni, na kurudi maskani Haya shime waumini, tiketi zenu 'bukuni' Mwaalikwa karibuni, vijana kongamanoni. Nimefika ukingoni, mwa mwaliko kukupeni Vijana uitikeni, kwa kuja kongamanoni Kalamu naweka chini, kwa hamu wakungojeni Pamoja tukongamane, kuhuisha yetu dini. Abuu Nyamkomogi Mwanza-Tanzania.

Shairi/Barua

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

Waislam chukueni tahadhari mnapouziwa nyama


Assalam alakum warahmatullah wabaratuh. Ndugu Mhariri pamoja na wasomaji wa gazeti letu tukufu la Kiislam, siku nyingi nilikuwa nikitamani kuwapa tahadhari Waislamu juu ya hatari mbaya ya kiimani na kiusalama inayotokana na nyama inayouzwa katika mabucha nchini. Nilikuwa natafakari pa kuanzia lakini hivi karibuni, Allah (sw) kanipa njia iliyoniweza kuwafikishia ujumbe Wa i s l a m u , h i v y o kuondosha dhima juu yangu kwa Allah juu ya yale ninayoyafahamu kuhusu nyama. Ndugu Mhariri, nina ushahidi ambao nimeupata kwa kufuatilia kwa muda wa miaka minne na kubaini kuwa, sehemu kubwa ya nyama inayosambazwa na kuuzwa katika mabucha mbalimbali si halali kiimani na pia si salama kiafya. Zipo sababu mbalimbali ambazo inshaa Allah nitaelezea chache miongoni mwa nyingi, hasa nikirejea mada ambayo iliandikwa katika gazeti la Mwananchi la Jumamosi Novemba 9, 2013 kama ilivyoandikwa N YA M A H ATA R I YAUZWA NCHINI. Ndugu Mhariri, nyama ili iwe halali n i l a z i m a m n ya m a achinjwe kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na uwepo usimamizi wa kanuni zinaelekeza uchinjaji Kiislam. Serikali ambayo ndiyo yenye machinjio ya wanyama, haijazingatia maslahi ya Waislamu k u l a n ya m a h a l a l i , hili nalithibisha kwa kuwa nilitembea katika machinjio ya Manispaa ya mji Fulani, yule mchinjaji wa Manispaa hata akili yake kidogo imeshaanza kupotoka kidogo, ila wanamuweka kwa kuwa hodari wa kukata shingo, hivyo basi tunaweza kusema kuwa si mchinjaji bali ni MUUAJI. Ndugu Mhariri, katika gazeti ambalo nimelitaja hapo juu mwindishi alihoji mfanya biashara wa ng`ombe, ambaye amekiri kuwa wanachinja kinyemela wanyama waliokufa i l i wa s i p a t e h a s a r a endapo wanyama hao watazikwa. Kama mtu anakiri kwa mwandishi wa habari juu ya kuchinja wanyama walokufa je, ni wangapi hawajakiri na yeye ni m a n g a p i k a ya f i c h a kifuani mwake hali ya kuwa Allah amesema, wa n a y o ya f i c h a n i makubwa kuliko wanayoyadhihirisha Ndugu Mhariri, kuna mtu mmoja ambaye ni mkaguzi wa nyama, nilijaribu kufuatana naye katika maneno yake ya kazi katika eneo fulani mkoa wa M o r o g o r o , a l i k u wa akilangua nyama za ng`ombe na mbuzi na kondoo machinjioni, kisha alienda kukagua n ya m a ya n g u r u we mitaani kisha aliazima mizani kutoka katika duka la kuuza vyakula ambayo hutumika kupimia sukari, mchele, unga nk. akapimia nyama ya nguruwe. Je mtu kama h u y u a m b a ye h a y o anayoyafanya haoni kama yana madhara je, atashindwa kuchanganya nguruwe na kondoo, au kutumia muhuri mmoja k u t h i b i t i s h a n ya m a ya nguruwe na huo huo akatumia kwenye nyama ya ng`ombe? Ndugu Mhariri, baadhi ya watu waliohojiwa kuhusu machinjio, walisema kuna machinjio nne zenye hadhi ya kimataifa. Moja ya machinjio hizo

niliitembelea miaka mitatu iliyopita na kuangalia shughuli za uchinjaji, nilishuhudia mbuzi zaidi ya 300 wakichinjwa kinyume kabisa na misingi ya U i s l a m u , h a l a f u mwisho wakavishwa vitambaa maalumu a m b a v y o h u v i s h wa nyama zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi, na zikagongwa muhuri wenye maandishi ya kiarabu yakimaanisha Kuchinjwa halali, kisha tukaarifiwa kuwa walikuwa wanasafirishwa kwenda Omani na Saudia Arabia. Ndugu Mhariri, dalili za hoja yangu ni nyingi, siwezi kuziandika zote kwa wakati huu, nilichotaka ni kuondosha dhima juu yangu kwa Allah (sw), kuwa niliona uovu na sikuwazindua ndugu zangu Waislamu. Kabla sijamaliza nichukue nafasi hii k u wa a s a Wa i s l a m u kuwa, kuna haja zile taasisi za Kiislamu za kuchunguza bidhaa halali za kama ile ya Jumuia na Taasisi za Kiislamu, kuchunguza mara kwa mara machinjio mbalimbali nchini ili kuhakikisha zinatekeleza majukumu yake Kiislamu na kiusalama, kwani kinyume na hivyo tutaendelea kulishwa vibudu na haramu na hatutakuwa na hoja mbele za Allah siku ya kulipwa. Ndugu Mhariri, suala la nyama lilizua mjadala siku zilizopita na hata baadhi ya Waislamu ambao walikuwa mstari wa mbele kufuatilia wakaitwa wachochezi. Sikuandika maoni haya kumchochea yeyote, bali kuwazindua Waislamu, naomba yafikishwe kwa Waislamu ili mwenye kuchukua tahadhari achukue, wewe na mimi tumejivua dhima kwa Allah. Abuu Abdullah. Dar es salaam.

11
Inatoka Uk. 8
yumo kwenye orodha ya magaidi ya Marekani. Tumeona pia hata baada ya kufariki wiki iliyopita Desemba 5, 2013, bila aibu wala soni, Waziri Mkuu wa U i n g e r e z a D a v i d Cameron na Rais wa Marekani Barack Obama, walikuwa vinara wakiwa ndio viongozi wa mwanzo kabisa kuwasili Afrika Kusini kuhani msiba wa mtu ambaye dola zao zilimtambua kuwa ni gaidi. Umaarufu wa Mandela na heshima aliyoipata duniani kote, imetokana na kazi ngumu na ya kujitolea katika kutetea haki za wanyonge wengi dhidi ya wazungu wachache, mwingi wa kusamehe hata baada ya kushika dola, kuleta maridhiano ya kitaifa kati ya wazungu wachache waliokuwa wakandamizaji n a we u s i wa l i o k u wa wakikandamizwa. Lakini kwa kuwa mataifa hayo hayakuridhishwa na kazi yake na walikumbatia maslahi ya Makaburu, walimwona Mandela na ANC yake kama magaidi waliostahiki kulaaniwa na kudhibitiwa. Kazi yake wakaibeza na wakamchafua. Kistaarabu na kuonyesha ulimwengu utu na uungwana, ilitarajiwa kuwa hotuba ya Rais Obama aliyoitoa

Habari

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

Mandela alikuwa katika orodha ya magaidi ya Marekani hadi 2008


katika uwanja wa FNB, Johannesburg wakati wa kuomboleza msiba wa mzee Madiba, pamoja na mambo mengine lakini kwanza angeiomba radhi serikali ya Afrika Kusini na ANC, k wa serikali yake kumdhalilisha mzee Mandela kwa muda mrefu. Pamoja na kwamba si utawala wa Obama uliohusioka na udhalilishaji huo, lakini ni Taifa lake lililoasisi udhalilishaji wenyewe. Kwa msingi huo alipaswa kuomba radhi watu wa Afrika Kusini na Taifa kwa ujumla kwa kumwingiza Mandela na ANC katika orodha ya magaidi kabla ya kumuondoa katika orodha hiyo mwaka 2008. Aidha Waziri Mkuu Cameron, kama ilivyostahili Obama, naye alistahili kuchukua hatua kama hiyo, hata kwa kupitia vyombo vya habari kama hakupata nafasi ya kuhutubia. Mzee Mandela kama ilivyo ada yake ya uungana ni vitendo, bila shaka alisha samehe na hata hivyo hunaye tena. Lakini Taifa la Afrika Kusini lipo, ANC ipo na sifa za Mzee Mandela bado zingalipo na bado

Uke wenza usihusishwe na Ukimwi


Inatoka Uk. 12
UKIMWI. Ajabu ni kwamba, matusi haya yamekuwa yakitokewa bila hata ya utafiti kufanyika na kudhihirisha madai yao, bila hata ya kutolea takwimu zozote kulinda hoja hizo wala kutolewa mfano wa dhahiri. Pamoja na kukosekana vigezo sahihi vya kuthibitisha madai haya ya wanaharakati, bado tafisiri iliyokuewpo kwa walio wengi ni kwamba, kwa Waislamu kuwa na ruhusa ya kuwa na mke zaidi ya mmoja, ni sawa na wale wazinifu, ambao wana mahawara wengi tu wasio na idadi huko mitaani. N a k wa k u wa z i n a a ndio chanzo kikuu cha maambukizi ya UKIMWI, basi wale wenye mke zaidi ya mmoja wanaonekana kuwa ndio wanaoeneza zaidi virusi vya ukimwi sawa na wazinifu wanaochukua wanawake baa, kwenye madanguro na wenye nyumba ndogo!. Licha ya jamii ya Waislamu kutetea utaratibu wao wa kiimani, bado hawakufua dafu dhidi ya propaganda za wanaharakati. Hata hivyo kila mwaka zinapotolewa takwimu za TACAIDS, zinashushua na kuvunja madai ya wanaharakati hao, ambao wengi wao kimsingi wanafanya kazi ajili kujikidhi kiuchumu kuliko kutoa huduma. Mikoa ya Pemba, Unguja, Ta n g a , L i n d i , M t wa r a , Kigoma yote inakaliwa na wakazi wengi Waislamu. Ni wazi kwamba katika mikoa hiyo, ndoa za Kiislamu za mke zaidi ya mmoja ni nyingi. Bado maambukiz ya UKIMWI ni kidogo kwa

Masheikh watoa darsa la ndoa


Na Mwandishi wetu. Wanandoa wametakiwa kukaa na kujadili mambo ya familia kwa pamoja kulingana na matatizo ya n a y o i s i b u f a m i l i a husika, ili kuweza kufikia lengo la malezi bora yenye maadili mema kwa familia zao na pia kupunguza matatizo ya kuvunjika ndoa nyingi. N a s a h a h i z o zimetolewa na Sheikh Mohamed Issa, katika Semina iliyoandaliwa n a a s a s i ya O F F T O JOB, wakishirikiana na Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) iliyofanyika k a t i k a H o t e l ya C i t y Garden jijini Dar es Salaam hivi karibuni. C h a n g a m o t o zinazozikabili familia nyingi baadhi yake ni uonevu, dhulma katika haki za wanawake, unyanyasaji na unyonyaji wa wanawake ndani ya familia, haya yamekuwa kansa inayokula familia nyingi zikiwemo za K i i s l a m u . Wa n a n d o a mume na mke kuwa na majadiliano ya mara kwa mara juu ya masuala ya familia yaoalisema Sheikh Issa. Akitoa mada katika semina hiyo, Sheikh Issa a l i wa t a k a wa n a n d o a kuishi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu pamoja na Sunah za Mtume (s.a.w) katika maisha yao yote, ili kupata radhi za Allah (s.w) na kupata kizazi kilicho bora hapa ulimwenguni. Aliwakumbusha wanandoa mara kwa mara kutambua majukumu yao kiroho na kifamilia, k wa m u m e n a m k e kuamrishana mema na kukatazana mabaya japokuwa mume amepewa nafasi ya kuwa kiongozi wa familia. Kwa upande wa uchumi, amewakumbusha wanandoa hao kuwa mume ndiye anayewajibika zaidi kuipatia familia mahitaji muhimu yakiwemo ya o c h a k u l a , m a l a z i , mavazi, elimu na mengi mengineyo. Aidha Sheikh Mohamed Issa amewataka Waislam kujenga utamaduni wa kutafuta ufumbuzi wa busara wa matatizo ya familia zao, ili kulinda ndoa zao. Moja ya njia bora na salama ilitajwa kuwa ni kutafuta elimu juu ya Uislamu na masuala ya ndoa ili kunusuru ndoa zao na kuishi maisha ya furaha na amani. Sheikh huyo amewasihi wanandoa kuwa ili wafurahie na kufaidi maisha ya ndoa, kamwe wasikumbushane makosa yaliyopita yaliyofanywa kati yao wawili, hasa wakati wanapohitilafiana au kugombana. Alisema kuwa ni jambo muhimu sana kwa wanandoa kujenga urafiki mkubwa kati yao na kuonyeshana mapenzi ya dhati, kuhurumiana,

anastahili kuheshimiwa kwa kazi yake. Hotuba hatuba aliyoitoa Rais Obama, licha ya kusifiwa na wengi na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kwa kupewa kipaumbele, lakini si lolote si chochote mbele ya kashfa hii ya kuwekwa Mzee Madiba katika orodha ya Magaidi kinyume na uhalisia wake, kwasababu tu ya uonevu, chuki na kumdhalilisha. Katika hili naona ilikuwa hotuba ya kinafiki na kujikosha zaidi.

mujibu wa takwmu. Itoshe tu kuwa funzo kwamba, Ndoa za Kiislamu hazina uhusiano wowote na hoja za wanaharakati za kuongezeka maambukizi. Yawezekana pia kuwa pamoja na kwamba katika mikoa mingine isiyokuwa na wakazi wengi Waislamu kama Njombe, Iringa, Mbeya na mingineyo, nayo ikawa na ndoa za mke zaidi ya mmoja, lakini nyingi zikawa za jadi. Ni wazi kwamba mikoa hiyo ina jamii ya Waislamu wachache ikilinganishwa na Pemba, Unguja, Tanga na Lindi. Sasa tujiulize mikoa hiyo imeongoza je kwa maambukizi ya Ukimwi? Mbona Unguja, Pemba, Tanga nako watu wa mke zaidi ya mmoja na maambikizi ni kiduchu? Niweke tu wazi kwamba hisia za chuki au za kuzusha katika mapambano ya UKIMWI, kamwe haziwezi kuleta tija katika vita hii ngumu dhidi ya maisha ya watu. Wenyewe haujali dini ya mtu, tajiri au maskini rangi wala kabila. Tukiwa wakweli kwa kubadili tabia, kwa kuacha tabia mbovu na kurejea katika maadili ya kiutu, tutaelimika na kusalimika. Asitudanganye mtu au mwanaharakati anayesaka sababu mufilisi ili tu kupitia NGO yake achume misaada k wa m a s l a h i ya k e k wa mgongo wa UKIMWI. Uislamu ni dini iliyotimilifu. Ina sheria, taratibu, miiko na maadili yake. Kila jambo lina sababu yake na utaratibu wake wa kuliendea. Kamwe utaratibu wa n d o a wa K i i s l a m u hauwezi kuwa chanzo cha maradhi leo mpaka kesho.

kusaidiana, kupongezana na kuheshimiana. Alisema mara nyingi Waislamu wanashauriwa kwamba panapotokea hitilafu kati ya mume au mke katika familia, basi yampasa mmoja kati uyao kuondoka alipo mwenzake, ili kutoa nafasi ya wote wawili kupoza hasira zao na baadae wanaweza kuwa pamoja na kuzungumza bila munkari juu ya hitilafu yao. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mara nyingi suluhu ya wawili wanaohitilafiana, haiwezi kupatikana wakati wahusika wakiwa katika hali ya hasira na kwamba matokeo yake ni kupatikana maamuzi ya hasara. Katika semina hiyo, Sheikh Issa pia alishauri kwamba mume na mke ili waweze kutambuana na kufahamiana vizuri bila kutiliana shaka, yafaa kila mmoja kuelezea hisia zake kwa mwenza wake mara kwa mara. Kwa upande wake mgeni rasmi katika semina hiyo, Sheikh Amran Kilemile, alisema ili wanandoa waweze kuishi katika ndoa iliyo imara na yenye kheri, ni wajibu kutekeleza taratibu za ndoa kwa mujibu wa maelekezo ya Aya na Hadithi za Mtume Muhammad (s a w).

12

AN-NUUR
MAKALA

12

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

Soma Gazeti la AN-NUUR kila Ijumaa

SAFAR 1435, IJUMAA DESEMBA 13-19, 2013

AN-NUUR

Mashahidi wa Serikali waingia mitini


Ni katika Kesi ya Imam Hamza, Jijini Mwanza
katika kesi yangu alikuwepo nje, lakini Wakili wa Serikali akasema mashahidi hawapo, kwa hiyo kesi ikapigwa mpaka Januari 17, 2014. Alisema Imam Hamza, akithibitisha hali hiyo. Kwa mujibu wa chanzo hicho, kilieleza kuwa Wakili wa Imam Hamza, ameomba kuwa hali hiyo iwe ni kwa mara ya mwisho, na kwamba endapo itafika siku hiyo ya kurudi Mahakamani, na mashadi hawatofika basi ameomba Mahakama itende haki. Wa k i l i w a S h e i k h , alichokiuliza ama kukisema mbele ya Mahakama ni kwamba hawa mashahidi wapo hapo Jijini Mwanza, na pia wanaanuani zenyekueleweka, zaidi ofisi zao zipo jirani ya Mahakama hiyo inakuwaje washidwe kupatikana.? Kilisema chanzo hicho kikimnukuu Wakili huyo. Akitoa maoni yake kufuatia mwenendo huo Imam hamza, alisema, Na Bakari Mwakangwale KESI inayomkabili Imam Hamza Shaban, Jijini Mwanza, imeairishwa hadi Januari 17, 2014, kutokana na m a sha hi di u p a n d e wa Serikali kushindwa kutokea Mahakamani. Kesi hiyo iliyounguruma Jumanne wiki hii, Mahakanai hapo, imeshindwa kufahamika mara moja sababu zilizopelekea mashahidi hao muhimu, kushindwa kufika kuanza kutoa ushadi wao dhidi ya kiongozi huyo wa Kiislamu. Hata hivyo kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka Mahakamani hapo, kilieleza kwamba shahidi namba moja ambaye ni afisa wa Jeshi la Polisi Jijini humo alionekana maeneo hayo ya Mahakama, akirandaranda. Sababu haijajulikana kwa nini hawajatokea, lakini kitu ambacho ninaweza kusema shahidi namba moja yeye pamoja na Waislamu wamekuwa na wasiwasi juu ya mwenendo wa kesi hiyo kwani alisema haelewi ni kwa nini shahidi yupo kisha Mahakama inaelezwa hayupo. Sasa tunapoambiwa mashahidi hawapo tunakuwa na mashaka na mashtaka yangu, si mimi tu, niliye muona wapo wengi waliomuona maeneo haya, nilimuona kabla sijaingia Mahakamani na baada ya kutoka pia nimemuona akiwa katika gari yake, waliokuwa nje walisema alikuwa anatoka kunywa chai. Alisema Imam Hamza. Akielezea mwendo wa kesi hiyo, alisema inampa m a s h a k a k wa n i t a ya r i alishakaa mahabusi kwa miezi minne bila dhamana, na kesi imekuwepo toka Februari 26, 2013, mpaka sasa ni Desemba 10, 2013, lakini imekuwa ikiahirishwa tu. Imam Hamza, alisema mpaka sasa ushahidi

Na Shaban Rajab
Ndoa ya mke zaidi ya m m o j a , h a i we z i k u wa sababu ya kusambaa virusi vya UKIMWI, bali tabia za watu iwe wamo katika ndoa au la. Wanaoleta hoja hizi, wanaonekana tu kuongozwa na chuki zao au kuwa na mawazo potofu. Hii inadhihirishwa na tafiti mbalimbali ambapo, kila ambapo panaonekana watu kuwa na tabia zisizo faa, ndio kwenye matatizo. Kwa upande mwingine, mahali kama Pemba ambapo, bado maadili ya kidini yana nafasi kubwa katika jamii, kiwango cha maambukizi ni cha chini sana. Desemba 1 Mosi mwaka huu, iliadhimishwa Siku ya UKIMWI Duniani. Siku hii iliasisiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 1998 na imeendelea kuadhimishwa kila ifikapo Desemba mosi kila mwaka. Kwa hapa kwetu Ta n z a n i a , s i k u h i y o iliadhimishwa kitaifa katika

Uke wenza usihusishwe na Ukimwi


Pemba, Tanga, Lindi imedhihirisha
huu, ikikusudiwa kutoa msukumo wa utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti UKIMWI ili kufikia azma ya maambukizi mapya sifuri, vifo sifuri na unyanyapaa sifuri ifikapo mwaka 2015. K w a k a w a i d a maadhimisho haya hutoa fursa kutathmini hali halisi na mwelekeo wa udhibiti wa UKIMWI, na kubaini changamoto na mafanikio katika kupambana na janga hili. Mwaka huu, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imetoa ripoti inayoonyesha takwimu za viwango vya maambukizi ya ukimwi katika mikoa ya Tanzania nzima. Katika takwimu hizo za TACAIDS, mkoa mpya wa Njombe unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya UKIMWI kwa asilimia 14.8, ikifuatiwa na mkoa wa Iringa kwa asilimia 9.1. Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya nne kwa asilimia tisa ukifuatiwa na Ruvuma wenye maambukizi kwa a s i l i m i a 7 . 2 , S h i n ya n g a asilimia7.4), Dar es Salaam asilimia 6.9, Rukwa asilimia 6.2, Katavi asilimia 5.9, Pwani asilimia 5.9,Tabora asilimia 5.1, Kagera asilimia 4.8 na Geita asilimia 4.7. Mikoa mingine ni Mara asilimia 4.5, Mwanza asilimia 4.2, Mtwara asilimia 4.10, Kilimanjaro asilimia 3.8, Kigoma asilimia 3.4, Simiyu asilimia 3.6, Morogoro asilimia 3.8, Singida asilimia 3.3, Dodoma asilimia 2.9, Manyara asilimia 1.5, Lindi asilimia 2.9, Tanga asilimia 2.4, Unguja asilimia 1.9 na Pemba asilimia 0.3. viwanja vya Mnazi |Mmoja jijini Dar es Salaam, ambapo shamra shamra zilianza tangu Novemba 25, 2013 na kufikia kilele hiyo Desemba Mosi 2013. Kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho, yalifanyika maonyesho ya shughuli mbalimbali za wadau wa harakati za kudhibiti UKIMWI nchini. Pamoja na shughuli zote hizo, lakini pia kulifanyika kongamano la kitaifa la kutathmini hali na mwelekeo wa udhibiti UKIMWI nchini, ambapo mkakati wa tatu wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI ulizinduliwa. Ta n z a n i a b i l a m a a m b u k i z i m a p ya ya VVU; vifo vinavyotokana na UKIMWI na unyanyapaa inawezekana, ndiyo iliyokuwa kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka

Takwimu hizi zinatokana na utafiti uliofanywa mwaka juzi hadi mwaka jana. Kwa ujumla takwimu hizi zinaonyesha kwamba kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kimepungua kiasi. Lakini mikoa ya Pemba na Unguja, Tanga na Lindi imetia fora kwa kuwa na kiwango kidogo zaidi cha maambukizi. Ikumbukwe tu kwamba kwa muda mrefu zimekuwepo hoja kutoka taasisi za wanaharakati na NGOs mbalimbali kwamba, moja ya njia zinazoongeza maambukizi ya UKIMWI ni ndoa za mke zaidi ya mmoja. Pamoja na kwamba zipo ndoa za kimila zinazokubali mume kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini jamii ya Waislamu ndio iliyokuwa ikilengwa zaidi na hoja hii, kwamba utaratibu wao wa ndoa unaoruhusu ndoa zaidi ya mkke mmoja unachochea maambukizi zaidi ya

Inaendelea Uk. 11

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

También podría gustarte

  • Annuur 1190
    Annuur 1190
    Documento20 páginas
    Annuur 1190
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1182
    Annuur 1182
    Documento20 páginas
    Annuur 1182
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1185
    Annuur 1185
    Documento20 páginas
    Annuur 1185
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1193
    Annuur 1193
    Documento20 páginas
    Annuur 1193
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1183 PDF
    Annuur 1183 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1183 PDF
    annurtanzania
    100% (2)
  • Annuur 1179 PDF
    Annuur 1179 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1179 PDF
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1180 PDF
    Annuur 1180 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1180 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1107
    Annuur 1107
    Documento16 páginas
    Annuur 1107
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1181 PDF
    Annuur 1181 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1181 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1178
    Annuur 1178
    Documento20 páginas
    Annuur 1178
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • ANNUUR 1176b PDF
    ANNUUR 1176b PDF
    Documento20 páginas
    ANNUUR 1176b PDF
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • ANNUUR 1175b PDF
    ANNUUR 1175b PDF
    Documento20 páginas
    ANNUUR 1175b PDF
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1173 PDF
    Annuur 1173 PDF
    Documento20 páginas
    Annuur 1173 PDF
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1112
    Annuur 1112
    Documento16 páginas
    Annuur 1112
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • ANNUUR 1110cc
    ANNUUR 1110cc
    Documento16 páginas
    ANNUUR 1110cc
    Anonymous x8QGwFF
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1105
    Annuur 1105
    Documento12 páginas
    Annuur 1105
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Documento0 páginas
    Rasimu Ya Katiba (Toleo La Pili)
    Muhidin Issa Michuzi
    0% (1)
  • Annuur 1096
    Annuur 1096
    Documento12 páginas
    Annuur 1096
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1091
    Annuur 1091
    Documento16 páginas
    Annuur 1091
    MZALENDO.NET
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1102
    Annuur 1102
    Documento12 páginas
    Annuur 1102
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Documento12 páginas
    Annuur 1090
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1088 PDF
    Annuur 1088 PDF
    Documento12 páginas
    Annuur 1088 PDF
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1093
    Annuur 1093
    Documento16 páginas
    Annuur 1093
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1094
    Annuur 1094
    Documento16 páginas
    Annuur 1094
    annurtanzania
    100% (1)
  • Annuur 1090
    Annuur 1090
    Documento12 páginas
    Annuur 1090
    annurtanzania
    Aún no hay calificaciones
  • Annuur 1089
    Annuur 1089
    Documento12 páginas
    Annuur 1089
    Hassan Mussa Khamis
    Aún no hay calificaciones