Está en la página 1de 12

ISSN 0856 - 3861 Na.

1040 DHUL-HIJJA 1433, JUMANNE OKTOBA 23 - 25, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Kariakoo mnatuma JWTZ Malawi mtapeleka nini?


Waziri wetu Nchimbi chutama, usitambe Msilitumbukize Jeshi letu kwenye aibu hii Yote haya mnafanya kwa masilahi ya nani?

Hofu ya maandamano ya Waislamu Dar:

Mwingine akojolea Quran Ukonga Dar

DKT. Emmanuel Nchimbi

FFU walivyozidiwa hadi kuitwa JWTZ

Ni kijana mwenye miaka 20 Atoweka hajulikani alipo Uk. 10

Simba Farid Ahmed

MALORI ya JWTZ yakiwa yamewabeba Askari wa jeshi hilo kuingizwa mitaani katika kamatakamata ya raia Kariakoo, jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita.

Polisi wasema hakutekwa, alijiteka Mwenyewe asema ameongeza ujasiri Asisitiza, ni kufa au Jamhuri ya Zanzibar

MMOJA wa raia akiwa chini ya ulinzi wa Askari katika mitaa ya Kariakoo, pia alikamatwa akiwa katika shughuli zake na kujumuishwa katika kadhia ya kamatakamata ya FFU, JWT na Mgambo Ijumaa wiki liyopita.

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

TAHARIRI/HABARI
kuchochea uhasama baina ya Waislamu na Wakristo, kingine kinachoonekana katika hatua hizi zinazochukuliwa na vyombo vya dola dhidi ya Waislamu ni kama namna iliyobuniwa ya kuzima hoja na agenda z a Wa i s l a m u . M a a n a ukishafanikiwa kuwakamata viongozi wa Waislamu au ukawapaka matope Waislamu kuwa ni Boko Haram, hapana shaka itakuwa ni njia ya uhakika ya kuzima madai ya Waislamu dhidi ya NECTA, suala la MoU, Mahakama ya Kadhi, OIC na mengine mengi. Tunachosema ni kuwa Waislamu wana madai ya msingi dhidi ya NECTA na

AN-NUUR
dhidi ya serikali. Hakuna namna ya kuzima madai haya ila kuyashughulikia. Ila kama tunadhani kuwa propaganda za kuleta ugoro wa Boko Haram na Boti za kukodi kuleta Uamsho kuchoma makanisa Dar es Salaam zitasaidia kuzima hoja za Waisalmu na wakati huo huo kudumisha amani; kwa hakika tutakuwa tunajidanganya.

S.L.P. 55105, Simu: Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

AN-NUUR

Propaganda hazitasaidia kudumisha amani nchini


Agenda ni NECTA, MoU, OIC, Dhulma
kwamba azma ya Waislamu hao ilikuwa sahihi au la. Lakini hoja kwetu ni jinsi vyombo vya dola vilivyoshughulikia jambo hilo. Kilichotokea ni kuwa badala ya vyombo vya dola kuzuiya watu wasike Ikulu, walichofanya ni kusababisha vurugu mitaani na kuleta kizingizio cha kuwapakazia watu makosa wasiyo kuwa nayo. Waziri Nchimbi anasema kuwa kuna watu wanataka kuchafua amani ya nchi na analeta hoja kuwa huenda wanatumiwa na watu wa nje. Mheshimiwa Nchimbi, labda tuulize, hivi ni m p a k a Wa i s l a m u w a nchi hii watumiwe au kuchochewa na watu wa nje ndio waone dhulma inayofanywa na NECTA wanayoilalamikia? Inahitaji mataifa ya nje kuona kuwa toka NECTA imeundwa imekuwa kama parokia au kigango cha kanisa? Lile suala linalolalamikiwa kwamba utunuku wa madaraja umekuwa siri na wenye walakini mkubwa ikituhumiwa kuwa ni kichochoro cha kuficha uovu wa shule zinazotakiwa kutesa kila mwaka ili zisije kuteseka, inahitaji kuchochewa na Al Qaidah au Al Shabab, kuliona? Hivi inahitaji mataifa ya nje kuwaonyesha Waislamu wa Tanzania kuwa serikali inaitumia Bakwata kuhujumu haki za Waislamu? Hata hili la juzi la Mufti Shaaban kuuwa hoja ya Mahkama ya Kadhi, hawalioni? Nimegusia suala la NECTA na Bakwata kwa sababu ndiyo masuala mawili ambayo Sheikh Ponda pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu walikuwa wakiyazungumzia hivi karibuni. Ukiacha lile la kutaka USIKU wa Alhamisi kuamkia Ijumaa Sheikh Mohammed Issa aliongea kupitia Redio Imani akiwatuliza na kuwataka watulie wakati viongozi wao wakishughulikia madai yao. Kwa waliomsikia Sheikh Mohammed Issa watakuambia kuwa aliongea kwa masikitiko na uchungu mkubwa huku akitoa machozi akionyesha jinsi dhulma ilivyozidi kwa Waislamu. Alisema, inasikitisha kuwa madai ya Waislamu yanapuuzwa yakiwepo lile la kulalamikia dhulma inayofanywa na Baraza la Mitihani Tanzania na sasa kibao kinageuzwa kinachoonekana na kupigiwa zumari ni madai ya kuchomwa makanisa. Viongozi wa Waislamu wanakamatwa ili kuzima agenda kama hiyo. Madai hayo ndiyo pia yaliyotolewa na Waislamu waliobahatika kuka katika lango la Ikulu ambapo walinukuliwa wakisema kuwa dhulma imezidi. Mtu mmoja katika wale waliofika lango la Ikulu muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kuwasili akitokea safari alinukuliwa live na kamera za televisheni akisema kuwa dhulma kwa Waislamu imezidi nchini na kwamba yeye atasema kweli hata kama askari waliokuwa wamemkamata watampiga au kumuuwa. Alisema, Quran imenajisiwa lakini hilo halionekani likizungumzwa. Kinachosemwa sasa ni kuharibiwa makanisa. Pamoja na nasaha alizotoa Sheikh Mohammed Issa na Masheikh wengine, inawezekana kuwa kuna b a a d h i y a Wa i s l a m u waliokuwa wamepania kwamba lazima wafike Ikulu kukisha kilio chao. Hoja yetu hapa, sio

MAONI YETU

Njama za kuilipua Zanzibar zakwama


Na Mwandishi Wetu
Hadi sasa kinachoonekana kama njama za kuilipua Z a n z i b a r, i s i k a l i k e n a kuirejesha kwenye siasa za chuki, tna, farka na uhasama, zimefeli. Hata hivyo, hali hiyo inaonekana kuwakasirisha baadhi ya watu ambao hawakusita kujitokeza hadharani kushutumu serikali na Jeshi la Polisi kwamba kwa waonavo wao, halijachukua hatua za kutosha. Pengine kilichokuwa kikitarajiwa ni kuwa baada ya kutekwa Sheikh Farid, liibuke zogo kubwa Polisi wapige watu Kijanjaweed na hata kuuwa hali itakayozidi kukasirisha wananchi na kufanya nchi isikalike. Likitokea hilo, iwe sababu kwanza ya kuvunja Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Maridhiano na kisha kuwaandama baadhi ya watu pamoja na taasisi za Kiislamu. Hata hivyo, Nusra ya Allah ilikuwa juu ya watu wa Zanzibar ambapo, wananchi walikuwa watulivu ukiacha zogo lililokuwa likifanywa na vijana wasiojali chochote ambao inadaiwa kuwa ni wale Janjaweed ambao baada ya kuifanyia kazi CCM katika chaguzi zilizopita, wametelekezwa. Kwa upande mwingine, Jeshi la Polisi lilionekana kufanya kazi yake vizuri ambapo waliwaandama tu wale waliokuwa wakileta ghasia mitaani na kwa nguvu iliyokuwa ikilingana na hali halisi. Hata hivyo, hali hiyo ambayo kwa hakika imekuwa ni nusra kwa nchi, inaonekana kuwa haikuwa matarajio ya baadhi ya watu ambao sasa wanailaumu serikali na hata kukia hatua ya kutoa kauli kwamba serikali ya Umoja wa Kitaifa na Maridhiano ivunjikilie kwa mbali. Katika kudhihirisha kuwa kuna watu wanatokota kwa hasira kuona Zanzibar ikiwa katika hali hii ya amani na utulivu, wamekuwa wakisambaza tna kupitia vipeperushi wakidai kuwa wanaochochea fujo hadi kuuwawa Polisi (FFU) kule Bububu, ni CUF. Na kwa sababu hiyo wanataka CUF watolewe serikalini wakisema sisi CCM basi tena Umoja na CUF. CCM kosa letu kuwatia mbwa msikitini, sasa tunasema kuwa basi tena litakalo kuwa na liwe. Kwa sisi CCM basi tena umoja na CUF. Kinasema kipeperushi kimoja kinachodaiwa kusambazwa na CCM wahadhina. Hata hivyo, wahadhina hao huku wakidai kuwa CUF ndio wanaochafua hali ya amani, wao wamejifanya kuwa ndio wapenda amani na watetezi wa amani hiyo. Wanasema katika kipeperushi hicho: Nyie CUF/Muamsho, Abubakar Khamis Bakari, Mussa Njino na Azizi mushazoea fujo na sisi CCM sera yetu amani, sasa mujiuzulutumechoka na nyinyi juu ya mauwaji ya askari wetu. Kipeperushi kikamalizia kwa kusema, ondokeniii murudi kwenuuuuu, bila kufafanua waende wapi (Pemba?). Maoni ya wengi na hata kauli za vijana katika vijiwe na maskani za CCM ambazo mwandishi amebahatika kupita na kusikiliza kauli za vijana hao ni kuwa, waliokuwa wakifanya zogo ikiwa ni pamoja na kuvamia maduka ya ulevi na kupora masanduku ya pombe ni vijana wa Janjaweed ambao wametelekezwa baada ya kutiwa ununda. Vi j a n a h a o w a l i p e w a mafunzo ya kijeshi, wakatiwa ukatili wakawa wanapiga watu mikwaju na hata kuuwa bila kuona vibaya wala hofu na bila kuchukuliwa hatua, (ufupi wa maneno waliondolewa hofu na ubinadamu) wakati wa chaguzi zilizopita. Baada ya kutiwa ukatili huo na baada ya kuwaingiza CCM madarakani, wenyewe wanadaiwa kusema kuwa hawakupewa yale waliyoahidiwa, wametelekezwa. Inadaiwa kuwa japo ni kweli kwamba kuna vijana wengi waliohusika katika vurugu, lakini inaaminika kuwa Ubaya ubaya hao waliotokana na Janjaweed, ndio walioonekana mitaani bila ya hofu ya FFU wakifanya uporaji na kupiga watu. Inadhaniwa kuwa waliohusika kumteka Sheikh Farid huenda walikuwa na lengo la kuchochea ghasia nchini. Kwamba wakitaraji kuwa wafuasi wake wangelipuka katika namna ambayo ingelazimisha vyombo vya dola kuchukua hatua ambazo matokeo yake ni kuleta ghasia zaidi. Hoja hiyo inakuja hasa baada ya Sheikh Farid mwenyewe kueleza hali ilivyokuwa ambapo inaonyesha kuwa waliomteka walikuwa wakimhoji maswali ya kawaida ya kipolisi. Kama aliyoeleza Sheikh Farid ni kweli, kwa nini wahusika wasingemwita tu Polisi au wakamkamata ikajulikana kwamba yupo Polisi anahojiwa?

Kwa nini wacheze drama hii wakati waliyomhoji angeweza kuitwa Polisi na kuhojiwa? Haya ndiyo maswali yanayoulizwa na watu wakijenga hoja kwamba hata kama waliohusika ni vyombo vya dola, lakini inaonyesha kuwa kuna watu walio ndani ya vyombo vya dola ambao hawafurahii hali hii ya amani na utulivu iliyopo. Inaelezwa kuwa kama mipango kama hiyo ingefanikiwa au kama itaendelezwa na kufanikiwa, huenda ikawarahisishia kazi mabeberu kupitia AFRICOM yao ambao kila penye harufu ya mafuta na gesi, hutaka kupadhibiti kijeshi na kikachero. Na njia nyepesi kama walivyokwishaingia Uganda wakidai kusaidia kumsaka Konny, ni kujenga mazingira ya kuonyesha kuwa nchi ina kitisho cha magaidi, Al Qaida na Al Shabab, na kwa hiyo kwa vile wao washajipa ukiranja wa kupambana na ugaidi duniani, basi huingia na kukaa. Wakishaingia ndio wamekaa, huna ubavu wa kuwatoa tena. Ni kwa sababu hiyo, wanaokula njama hizi wakiangalia masilahi yao binafsi katika siasa za Zanzibar, wanatakiwa kutizama na hatari wanayoikaribisha ambayo itawadhuru wao na vizazi vyao vijavyo. Wakati huo huo, imeelezwa kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Ameir Kificho anastahiki pongezi za dhati kwa uzalendo wa hali ya juu alioonyesha katika kuzima hoja za waliotaka kuleta hoja binafsi ambayo ilikuwa na lengo la kusambaratisha serikali ya umoja wa kitaifa. Kwa nafasi yake ya Uspika na pengeine kwa busara za uzee, Spika Kificho ilikuwa kama anawabembeleza wajumbe na kuwakumbusha wakumbuke kiapo walichochukua cha kuitumikia nchi na wananchi. Namna yake ilikuwa kama anawaambia kuwa wao wangetakiwa kuwa watu wa mwisho kuwasaliti wananchi na nchi, na sio wao kuwa wa mwanzo kuja na agenda za kuisambaratisha Zanzibar. Kwa upande mwingine, kwa muda wote ambao Sheikh Farid alikuwa haonekani, Masheikh wa Jumuiya ya Maimamu na wale wa Uamsho wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuwatuliza wananchi na wakati huo huo wakifanya vikao vya pamoja na Polisi kushauriana juu ya hali ilivyo.

Inaendelea Uk. 5

AN-NUUR
Na Alghaythiyah, Zanzibar.
MIMI msimamo wangu katika suala la kuitetea Zanzibar upo pale pale hadi Jamhuri ya Watu wa Zanzibar isimame. Hiyo ni kauli ya Sheikh Farid Ahmed Hadi mara baada ya kuachiwa na watu aliodai walimteka na kumzuiya kwa siku nne. Sheikh Farid alionekana Ijumaa Usiku baada ya kupotea kwa siku nne katika visiwa vya Zanzibar huku akionekana akiwa na afya njema pamoja na furaha baada ya kuonana na familia yake iliyopo Mbuyuni Mkoa wa Mjini Magharibi. Hata hivyo, Jeshi la Polisi limesema kuwa Sheikh Farid hakutekwa ila kinachoonekana ni njama za kujiteka mwenyewe. Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema kuwa si kweli kwamba Sheikh Farid alitekwa bali kinachoonekana ni kujiteka mwenyewe. Na kwa sababu hali hiyo ya kujiteka imeleta vurugu zilizosababisha uvunjifu wa amani, mali kuharibiwa na hata kuuliwa mtu, Polisi walikuwa wamemshikilia Sheikh Farid pamoja na viongozi wengine wa Uamsho na walifikishwa mahakamani jana na kusomewa shitaka la uchochezi wanalodaiwa kulifanya mwezi Agosti. Akifafanua juu ya kile alichokiita kujiteka Farid, Kamanda Mussa amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na dereva wake aliyempakia na kumwacha huko Mazizini, alimwambia aende zake wakati yeye (Sheikh Farid) akizungumza na watu waliokuwa katika gari aina ya NOAH. Hivi tujiulize, mtu watu huwajui unazungumza nao katika Noah kwa simu na kumwambia dereva wako aende zake, huko si kutekwa labda kujiteka. Alisema Kamishna Mussa. Hata hivyo, wakati Kamishna wa Polisi akisema hayo, Sheikh Farid ameelezea alivyokamatwa ambapo alisema kuwa hakutekwa bali alichukuliwa na jeshi la polisi na vikosi vya usalama wakitaka kumhoji kuhusiana na harakati zake za kuitetea Zanzibar ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kweli inazungumzwa neno kutoweka, lakini mimi sikutekwa, bali nilichukuliwa na watu ambao ni polisi na wakaniingiza katika gari na kunipeleka sehemu moja ambayo mimi nilikuwa siijui wakanifunga kitambaa machoni na kunipeleka sehemu nisiyoifahamu na kuniingiza katika nyumba moja nikiwa na kitambaa cheusi usoni, alisema. Sheikh Farid alipatikana majira ya saa 2:15 usiku baada ya umeme kukatika ambapo kwa mujibu wa maelezo yake anasema alishushwa ndani ya gari kama mzigo kwa kusukumwa sehemu ile ile ambayo awali alichukuliwa na ametambua hilo baada ya kuona ameshushwa katika msikiti ambao aliingia siku ya kwanza alipochukuliwa. Nilifungwa kitambaa cheusi na tokea nimefungwa

Simba Farid Ahmed

HABARI

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

SHEIKH FAarid Hadd (wa tatu kushoto). sikufunguliwa mpaka leo (Ijumaa) walipokuja kunitupa sehemu ile ile walionichukua ndio wakanifungua, na mimi mwenyewe sikuwa nimeweza kukifungua kwa muda wote huo kutokana na jinsi walivyokifunga. Alieleza. Akizungumzia hali aliyoikuta huko ndani ya nyumba alipokuwa ameingizwa, Sheikh Ahmed alisema kwa kuwa alikuwa amefungwa uso hakuweza kutembea sehemu yoyote ndani ya nyumba. Aidha alisema, hakuwahi kula kwa siku zote hizo ila kunywa maji tu aliyokuwa akinywa akienda msalani kujisaidia. Sijala kitu chochote kwa sababu hiyo nyumba haikaliwi na mtu, lakini hata kama ningeletewa chakula nisingekula kwa sababu siwezi kuwaamini kula chakula chao kwa hivyo nilichokuwa nafanya nikenda chooni kujisaidia ndio nakunywa maji ya mferejini kwa wingi sana na Alhamdulillah (Nashukuru Mungu) amenisaidia, aliongeza Sheikh huyo ambaye alikuwa amezongwa na umati mkubwa wa watu nyumbani kwake. Umati huo ulikusanyika nyumbani kwake kuanzia saa 3 usiku mara baada ya kusambaa habari kwamba kapatikana na wengine kukesha hapo. Ilikuwa takbiira, adhkar na kasda kuonyesha furaha ya waumini hao wa dini ya Kiislamu kwa kiongozi wao. Katika maelezo yake Sheikh Farid amesema kuwa kwa muda wote aliokuwa akishikiliwa hakuwahi kupigwa hata mara moja wala hajadhuriwa kwa hali yoyote zaidi ya kutiwa khofu wakati akifanyiwa mahojiano na baadhi ya wakati alikuwa akihojiwa kwa hasira na ukali ili atoe maelezo yote. Alisema kuwa walichokuwa wakitaka kujua ni kuhusiana na harakati zake na masuala mengi yalikuwa yakimlenga yeye binafsi, uhusiano wake na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein na uhusino wake na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na safari zake za kwenda na kurudi nchini Oman. Walitaka kujua kila kitu changu na kwa kweli walikuwa wanataka kujua kila kitu na ilikuwa ni vitisho na baadhi ya wakati walikuwa wakipiga risasi miguuni ili watimize lengo lao wanalolitaka, alisema Kiongozi huyo. Alipoulizwa juu ya watu waliokuwa wakimhoji alisema kuwa walikuwa wakitofautina kwa kuwa kila mmoja alikuwa akitumia namna yake ya kuhoji ambapo wengine wakitumia ukali na wengine wakihoji kwa utaratibu na upole. Akielezea mazingira ya nyumba hiyo aliyowekwa alisema ni khofu ilikuwa imetanda, lakini aliweza kuvumilia katika kipindi chote hicho kwa kuwa hakuwa akiona kitu chochote kwa kuwa alikuwa amefunikwa uso wote. Akitoa wito wake kwa umma aliwataka watulie na wasifanye fujo huku ombi lake kwa viongozi wa serikali likiwa kuwataka kutenda uadilifu na wawe wanatekeleza kauli zao kivitendo na sio kusema bila ya kutenda haki kwani amani haiwezi kudumishwa iwapo watu wanayimwa haki. Naomba watu watulie wasifanye fujo na wasifanye vurugu za aina yoyote, hizi ni awamu za kudai haki lakini wawe na subra kwani hii ni nchi yetu na tunaipenda na tutaitetea kwa nguvu zote na wito wangu kwa viongozi wa serikali wawe waadilifu na watende haki kwa sababu hii ni nchi yetu na hizi ni awamu za mabadiliko na asiyetaka mabadiliko, basi wakati utambadilisha akitaka asiteke, alisema. Sheikh Farid alisema licha ya vitendo vyote hivyo alivyofanyiwa, hatarejea nyuma kamwe na ataitetea Zanzibar hadi pumzi yake ya mwisho kwani anachokifanya yeye na wenzake ni kitendo kinachokubalika kisheria na hakuna wa kuwazuwia. Tutaitetea nchi yetu ya Zanzibar hadi tone la mwisho (la damu) kwa sababu tunachokifanya hatujavunja sheria wala hatujenda kinyume na sheria za nchi kwa hivyo tutaitetea Zanzibar mpaka iwe na dola kamili na mamlaka kamili haiulizwi na mtu na irudi katika hadhi yake kama ilivyokuwa mwaka 1963. Alisema Sheikh Farid. Akitoa maelezo ya kukamatwa kwake alisema kwamba awali alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mwanafunzi wake wa Madrassa ya Mahdi Mahfoudh kwamba anataka kuonana naye na kumtaka waonane katika eneo la Mbweni karibu na duka ambapo mbele yake kuna msikiti mdogo usiosaliwa na watu wengi. Mimi napigiwa simu na watu mbali mbali kwa hivyo nilipopokea simu kuwa mwanafunzi wangu wa Mahdi Mahfodh sasa wakati huo natoka nyumbani nilikuwa nahitaji umeme kwa hivyo mimi nilipoka pale nikamwambia yule kijana wangu kwamba nataka kununua umeme na nikamwambia kijana nenda kanunue umeme na mimi naingia humu msalani kujisaidia sasa yule kijana akaondoka kwenda kununua umeme, kile kitendo cha yule kijana kuondoka tu na mie ndio nimetoka chooni naona gari ndio hiyo imekuja imepaki na kuna mtu mmoja akashuka akaniita Maalim na akajitambulisha pale kwamba mimi ni askari wa usalama na naomba uingia humu ndani ya gari tunataka kukuhoji na ndipo wakati huo huo watu wengine wawili wakashuka ndani ya gari wakiwa wamejifunika nyuso zao vitambaa vyeusi isipokuwa macho wakiwa na mashinigani (bunduki) ...sasa mimi sikutaka tena nikimbie au vipi kwa sababu ningekataa pengine ingekuwa ni khatari zaidi sikuwa na sababu ya kukataa nikaingia ndani ya gari na nilipoingia tu nikafungwa kitambaa gari ikaondoka. Alisimulia mkasa huo Sheikh Ahmed. Alisema baada ya kuingia ndani ya gari gari hiyo haikurudi nyuma ilionekana inakwenda njia ya Uwanja wa Ndege kwa kuwa ilikuwa imeelekeza huko na kisha

kupita round about kama mara sita inazunguka tu hapo round about, ili kumpotezea lengo asifahamu wapi anapelekwa na kuanzia hapo hakuweza kujua wapi anapelekwa hadi hapo alipofika katika nyumba na kuwekwa huko kwa muda wote akiwa amefunikwa uso wake na hajafunguliwa hata mara moja zaidi ya siku ambayo amerudishwa sehemu ile ile na kutupwa kwa kusukumwa tu ndani ya gari. Muda mfupi baada ya taarifa hizo kuenea kwamba Sheikh Farid ameonekana, watu mbali mbali walikuwa wakitumiana ujumbe kwa njia ya simu na facebook wakiulizia alipo ili wamuone kwa macho yao. Sheikh Farid Ahmed alipotoka hapo alipotupwa, alikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa mama yake eneo la Malindi ambapo alikutana na watu mbali mbali na kusalimiana nao na kisha kwenda nyumbani kwake Mbuyuni karibu na Msikiti wa Mabuyuni katika uwanja wa mpira wa Malindi. Muda mfupi waumini wa dini ya Kiislamu walimiminika kwa wingi na kukaa nje ya geti la nyumba ya Sheikh Farid hapo Mbuyuni wakitaka kumuona kwani wengi wao walikuwa hawaamini kama angeachiwa akiwa hai kutokana na taarifa za awali zilizokuwa zikisambazwa kwamba Sheikh huyo amefariki dunia kwa kupigwa sindano ya sumu na wanajeshi. Wa u m i n i w a k i k e n a wakiume, wakubwa na watoto kwa wingi walikusanyika huku wakisikika wakimsifu na kumshukuru Mwenye enzi Mungu kwa kumrejesha kiongozi wao salama wakipiga Takrbir ...yaani Mwenyeenzi Mungu Mkubwa na kisha kuimba wimbo wa kumpongeza na kusema Simba ...ameachiwa ...Simba ameachiwa...Simba ameachiwa ambapo kulikuwa na dufu zikipigwa na wengine kuitikia. Wakati waumini hao wakiwa nje ya geti na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki) wakiwa ndani, waumini hao walikuwa wakipiga malelele kila mara wakimuomba Sheikh Farid atoke achungulie ili waweze kusalimiana nao ambapo baadhi ya wakati walikuwa wakipenya na kuingia ndani kwa lengo la kutaka kukumbatiana naye na kupiga picha. Katika mitandao ya facebook watu wengi hasa vijana wameweka picha zao wakiwa wamepiga pamoja na Sheikh Farid huku wengine wakibadilisha profile zao na kumuweka picha yake huku wengine wakisema huyo ndio shujaa wanayemtaka kuwa kiongozi wa nchi yao. Waumini walibakia hapo kwa muda na hata pale alipoambiwa kwamba amechoka na hangeweza kutoka nje, walisema shida yao wamuone japo achungulie nje. Kwa hiyo ikawa ni zoezi la Sheikh Farid kuchungulia mara kwa mara kuwasalimia waumini na kuwatolea mkono na kila baada ya muda alikuwa akisimama na kuchungulia huku akishangiliwa. Ilipofika saa nane usiku waumini walianza kuondoka kidogo kidogo na kufanya maandamano huku wakiimba wimbo wa Simba ametolewa na kuelekea katika barabara zote za Mjini huku wakipiga dufu.

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

MAKALA

AN-NUUR
ikabidi nikubali na nikaingia kwenye gari na wakanifunga kitambaa cha uso na pingu, sasa ilivotoka gari haiwezi kuja mjini kwa sababu ile ni njia ya kuelekea airport ilienda moja kwa moja na ikakata kushoto mimi nilizani tunaenda Mombasa, lakini kufika round about ya Mombasa ikazungusha mara tatu hadi nne hali mimi kunipoteza malengo nisijue gari inaenda wapi baada ya hapo sikujuwa tena gari inaelekea wapi hadi nakuja jishtukia nipo kwenye nyumba nikawekwa ndani ya chumba na wakanisahau hasa kwa siku ile hadi siku ya pili karibu kama saa nne. B i S a l m a : We w e mwenyewe ulipoikuta nyumba uliona katika mazingira gani? Amir Farid: Sijaona mazingira yoyote kwa sababu mimi nilikuwa nimefunikwa kitambaa. Bi Salma: Hujaweza kujifunua? Amir Farid: Ah sijaweza kujifungua mimi. Bi Salma: Kwa maana hiyo umelala mpaka asubuhi hali ya kuwa umefunikwa hujala hujafanya chochote? Amir Farid: Sijala, sijafanya chochote kwanza siwaamini siwezi nikala hata kama wataniletea chakula sili, mimi nilikuwa wakati nakwenda msalani nilikuwa nakunywa maji ya chooni kwenye bomba, hicho ndio nilichokuwa nikiponea mimi, lakini sikula chakula chao kabisaaaaa. Bi Salma: Kwa hiyo unatuambia kwa muda wa siku tatu hujala chochote? Amir Farid: Sijala kabisa kabisaa naam. Bi Salma: Na vipi mazingira ya ndani, hofu, vitisho labda kama umepigwa. Amir Farid: Wallah wakati wa kuhojiana hicho ndio kikubwa anaweza akaja katika lugha ya busara akakutizama na wewe utamjibu vipi anaweza akatumia vitisho waweza wakatofautiana wale watu wanaouhudhuria pale. Bi Salma: Hata walipokuwa wakikuuliza walikuwa bado wamekufunika? Amir Farid: Walikuwa wamenifunika hawanifunui kabisa kabisa. Bi Salma: Wamekufunua wakati gani? Amir Farid: Wakati wa mwisho kabisa walivokuja kunirejesha baada ya wakati nimo ndani ya Inaendelea Uk. 5

Bi Salma: A ssalaam aleykum? Amir Farid: Waileykm salaam. Bi Salma: Wazanzibari wana hofu kubwa sana mpaka wamesababisha machafuko kutokana na wewe kutokweka, labda unaweza kuzungumza kitu kidogo kutokana na kutoweka kwako? Amir Farid: Ah kwakweli inazungumzwa neno kutoweka, lakini kwa kweli nimechukuliwa na watu ambao wamejitambulisha kwangu ni askari polisi na wameonyesha vitambulisho na wengine walikuwa na silaha mashingani ndio walionichukua kwenye gari na kunifunga kipambaa na baada ya hapo naweza kuelezea safari ilikuwa ni ndefu nikipata utulivu. Lakini nikaingia kwenye nyumba bila ya kuijuwa ni nyumba gani na nimebakia humo mpa muda huu walipozima umeme ndio wakaamua kuniachia kipindi hichi cha saa mbili usiku. B i S a l m a : We w e mwenyewe unajuwa ni siku ngapi ulizokuwa mikononi mwao? A m i r F a r i d : Wa ll a h nakisia itakuwa toka Jumanne itakuwa siku tatu hadi nne. Bi Salma: Nakumbuka kipindi kile ambacho ulikuwa umekamatwa ulikuwa umejeruhiwa, umepigwa na lakini pia ulikuwa umefungwa kitambaa cheusi, je safari hii? Amir Farid: Safari hii wamefanya hayo hayo isipokuwa inatofautiana kidogo. Mara hii nashukuru kwa kunipiga hawaja nipiga alhamdullillah, lakini lililokuwa kubwa kwao wao walitaka kujua mambo mengi kuhusiana na harakati hizi tunazo fanya, safari zangu za Oman nilizokwenda, Arabuni na masuala mengi personal (Binafsi) kwa sababu wamechukua simu yangu na hawakunirudishia tena na wamenihoji mengi sana kuhusiana na namba zilizokuwa katika simu na meseji na kila kilichokuwamo na ndio maana wakaona bora wale gharama hiyo na hasara waliotia kwenye nchi lakini wakie malengo yao, wanavotarajia wao wenyewe kwa kujuwa kila kitu kutoka kwangu. Bi Salma: Walikuwa watu wangapi? A m i r F a r i d : Wa t u walionichukua hasa walikuwa wanne, alikuwa ni dereva, mtu aliyekuja kujitambulisha kama ni askari na askari wengine wawili walikuwa nyuma ya gari. Bi Salma: Hao watu waliokuchukuwa

Mahojiani ya ana kwa ana Sheikh Farid Ahmed Hadi na Salma Said usiku wa Ijumaa Oktoba 19 mara baada ya Sheikh kuonekana baada ya kutoweka kwa siku nne.

SHEIKH FAarid Hadd.

ukiwatizama unaweza kuzitambua sura zao? Amir Farid: Siwezi kuwatambua kwa sababu hao waliokuwa wananilinda walikuwa wamevaa socks wamefunika wamebakisha macho peke yake. Bi Salma: Lafudhi zao zikoje? Amir Farid: Lafudhi zao zilikuwa wengi wao inaonyesha wabara ndio wengi kuliko wa hapa. Bi Salma: Mambo gani ambayo walitaka kuyajuwa zaidi? A m i r F a r i d : Yo t e kuhusiana na harakati toka zilivoanza, mahusiana yangu mimi na Shein (Mheshimiwa Rais), serikali na je mahusiano yangu mimi na Maalim Seif (Makamo wa Kwanza wa Rais) yaani kiupi walikuwa wanataka wajuwe kila kitu na mwisho walifanya vitisho mpaka kukia kupiga risasi chini ilimradi wakie lengo lao wanalolitaka. Bi Salma: Mwanzo Polisi walikuwa wanasema kwamba wao hawajakuteka wala hawajakuchukua, lakini wewe ulivokuja kuchukuliwa tuliambiwa na dereva wako kwamba ulikuwa umepigiwa simu, je ulikuwa unafahamu ni nani aliyekupigia na kwa nini walikuambia tu njoo na wewe ukenda? Amir Farid: Mimi simu yangu inapigwa na watu wengi sana na watu wengi wanatuita na sisi kama ni viongozi huwa tunakwenda na kuonana na watu wengi tena wengine ni waandishi wa habari, wengine ni watu raia wa kawaida, wengine

wana ihlasi na wengine ni wafanyakazi katika serikali, kwa hiyo mimi naitwa na watu wengi na mara hii mtu aliyeniita (askari) amejinasibisha kuwa yeye ni mmoja katika wanafunzi wangu Mahad el Mahfudh hivo ndivo alivo jinasibisha lakini mie sikuweza kumuona yoyote na wala sikuweza kuona sura zao na sikuweza kujua chochote baada ya hapo zaidi ya kuhojiwa hakuna jingine zaidi ya vitisho. Bi Salma: Hebu tuelezee kidogo wakati unatoka katika gari yako ukaingia katika gari nyingine hali ilikuwaje? Amir Farid: Mimi wakati nimefika pale yule kijana wangu atawambieni mkionana naye, tumefika pale mimi na yeye tukaingia kwenye eneo la ule msikiti mdogo pale na ule msikiti time zote upo kimya kwa hiyo tulipofika pale watu walikuwa washamaliza kusali kabisaa hapana watu, ila mimi nilimuona mtu mmoja tu anatoka kijana kijana hivi, sasa nimeka pale nashangaa nikamwambia yule kijana wangu hapa nimeagana na mtu kanambia atakuja katika wanafunzi wangu, sasa wakati ule ule wakati tunatoka huku nyumbani mimi tayari nilikuwa ninashida ya kununua umeme na yule kijana pia alikuwa anahitaji umeme kwa ajili ya nyumbani kwake, kwa hiyo alipofika pale yule kijana mimi nilikuwa nimetia wasi wasi kidogo kwa hiyo baada

ya kupanda juu huku, na nikazungusha ile gari nikawa sioni kitu nikashusha ile gari baada ya kuishusha ile gari na kuitoa barabarani nikasema bora niache huu wasi wasi hauna lazima, acha huyu kijana kwa vile hii sehemu ya umeme naiyona kwa jicho kabisaa nikamwambia yule kijana basi nenda kanunue umeme pale mimi niache niingie hapa msikitini na naingia msalami na nimsubiri huyu jamaa, yule kijana wangu kitendo cha kuondoka na mimi kuingia msalani gari ishaingia pale kwa hiyo gari ikawa imesimama chini ya miti ambapo palikuwa giza. Bi Salma: Ndio mulipokubaliana mukutane hapo? Amir Farid: Tulikubaliana pale msikitini lakini ile gari haingii msikitini pale ndio sehemu ya parking, kwa hiyo baada ya kuka maeneo yale nimekaa yule mmoja akasema Maalim ile kuniita sasa mimi nikasongea kidogo lakini mimi nikawa nishaingiwa na wasi wasi nilipoingiwa na wasi wasi yeye akashuka na akajitambulisha na akasema yeye ni askari na akanionyesha kitambulisho kwa hiyo tulikuwa tunakuomba tukuchukue kwa sababu tulikuwa tuna shida ya kukuhoji na wakati huo huo na wale wawili (askari) walikuwa washashuka kwenye gari na walikuwa na bunduki kwa hiyo mimi sikuwa na (la) kufanya

AN-NUUR
Na Bakari Mwakangwale
WA L E w a p o n d a n i , mabomu ya nini? We hujui. Ukisikia uchokozi ndio huo. Wanawachokoza ili watoke wapambane nao. Hiyo ilikuwa kauli ya baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa wamekusanyika nje ya kituo cha Polisi Msimbazi Ijumaa iliyopita wakifuatilia vurugu zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo. Walitoa kauli hiyo kufuatia hatua ya FFU kupiga mabomu ya machozi ndani ya msikiti wa Idrisa huku Waumini wakiwa wamejazana ndani. Wengi wa waumini hao, walishindwa kutoka kwenda nyumbani mara baada ya swala kutokana na hali ya kutisha iliyokuwa mitaani Polisi wakiwa wametanda kila mahali huku wakiwapiga waumini na kuwapakia katika magari yao. Kwa ujumla, siku hiyo Waislamu Jijini Dar es Salaam, walijikuta wakifanya ibada za Sala za Ijumaa na swala ya Al-aswar katika hofu kubwa, kufuatia baadhi ya vikosi vya majeshi nchini kuzingira Misikiti. Majeshi yaliyoonekana kuranda mitaani hususani jirani na Misikiti, huku wakiwa na silaha mbalimbali, ni Jeshi la Polisi, Vikosi vya Kutuliza Ghasi (F.F. U), Askari wa Jiji, Mgambo pamoja na Jeshi la Wananchi (JWTZ), wakiwa tayari kwa kile kilichoelezwa kuwadhibiti Waislamu waliotaka kuandamana. Hali hiyo ilianza kuonekana mapema majira ya saa tano asubuhi, wakati Waislamu wakianza kuelekea Misikitini kwa ajili ya Ibada ya Swala ya Ijumaa, huku idadi ya askari wakiwa na silaha katika magari na pikipiki wakiongezeka kadri muda ulivyozidi kusonga mbele. Kutanda kwa askari na majeshi hayo, yakisaidiwa na helkopta, iliyokuwa ikiranda angani kwa muda mrefu, kuliibua vurugu kubwa hususani katika mitaa ya Kariakoo, baada ya kuanza kuwarushia mabomu pale walipoanza kutawanyika baada ya kumalizika kwa Ibada ya swala ya Ijumaa. Vurugu hizo zilipamba moto kutokana na kuwa Ijumaa ni siku maaluma kwa Waislamu kiibada, ambapo hukusanyika kwa wingi katika Misikiti maalum kwa ajili ya swala. Ambapo kama kwamba maafande hao walikuwa wamedhamiria kuanzisha vurugu, walirusha bomu la machozi na kutua ndani ya Msikiti wa Idrisa Kariakoo na kuzua tafrani kubwa kwa Waumini waliokuwa ndani ya Msikiti huo wakiendelea na ibada. Bomu hilo liliunguza zulia (Kapeti) la kuswalia na kuzimwa na Waislamu kabla ya kuleta madhara zaidi. Hali hiyo iliibua hasira kwa Waislamu na kuwa chanzo cha mapambano baina ya Waislamu, kuanzia Msikitini hapo, ambapo mawe yalianza kurushwa kutoka mitaa mbalimbali na kupelekea

Makala

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

maafande hao kuingia mitaani na kurusha ovyo mabomu ya machozi na risasi za moto. Mr. Nchimbi, hawa Waislamu waliokuwa ndani ya Msikiti wakiswali, uhalifu gani walifanya mpaka wakapigwa bomu la machozi? Mr. Suleiman Kova, uliona uhalifu gani ukifanyika ndani ya Msikiti huo mpaka ukaamua kuwatawanya watu waliokuwa wakiswali kwa mabomu? Kuingia mitaani kwa maafande, hususani Mgambo

FFU walivyozidiwa hadi kuitwa JWTZ


na F.F.U, kuliambatana na kamata kamata bila kujali anaye kamatwa ni Muislamu au Mkristo, aliyerusha jiwe au asiyerusha. Mashuhuda wa kamatakamata hiyo wanaeleza jinsi askari wa jiji, mgambo na FFU walivyokuwa wakiingia nyumba hadi nyumba wakipiga watu na kuwakamata na hata kuingia mahotelini na kuwachomoa wenye hoteli na wateja wao na kuanza kuwasulubu. Mama mmoja alichomolewa

MGAMBO wakimkokota mtoto toka ndani katika vurugu zilizotokea jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita.

ndani akikanda maandazi na kuanza kushushiwa kipigo ambapo askari walipoona waandishi wa habari wanakaribia na kamera zao, walikusanyika na kumzingira mkanda maandazi huyo ili kuzuiya kupatikana picha. Hali ya kusikitisha ilijiri ilipofika wakati wa swala ya alasiri ambapo polisi walizingira msikiti mbele na nyuma na wakaanza kupiga mabomu ovyo. Kabla ya hapo walika askari

wenye mbwa na kisha askari walipaza sauti wakiwataka Waislamu kutoka ambapo majibu kutoka msikitini yalikuwa kwamba watatokaje wakati wamezingira msikiti na kila aliyekuwa akitoka alikuwa akipambana na kipigo. Kilichofuatia ni kupigwa mabomu mfululizo huku msikiti ukiwa umezingirwa ambapo Waislamu walikuwa wakikimbia na kuingia nyumba zilizokuwa jirani. Hapo ndipo Askari wa Jiji na mgambo wakawa wanavamia nyumba na kupiga watu ovyo. Katika Misikiti ya Mtambani Kinondoni na Kichangani, Magomeni imeariwa kwamba mabomu ya machozi yalipigwa jirani na Misikiti hiyo kwa nyakati tofauti mara baada ya swala ya Ijumaa kwa lengo la kuwalazimisha Waislamu kuondoka katika Misikiti hiyo, jambo ambalo lilisababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule za Misikiti hiyo. Katika maeneo kadhaa ya Jijini, yalionekana kana kwamba kuna vita kali kwani yalionekana magari ya vikosi vya Jeshi la Wananchi ( J.W.T. Z) yakiwa na wanajeshi waliokuwa wamevaa helmeti kichwani na silaha, wakiranda mitaani. Tujaaliye Waislamu wale walikuwa walikuwa wamepanga kuandamana kwenda Ikulu, cha kuwafanya Polisi kuja kupiga watu msikitini nini? Kwa nini wasingoje kupambana na wale watakaothubutu kuingia mtaani Msimbazi na Uhuru kuelekea Ikulu? Alihoji mwandishi mmoja aliyekuwa akishuhudia tafrani ile nje ya msikiti wa Idrisa.

Inatoka Uk. 4
gari hawajanishusha wakanifungua pingu na wakanitoa kitambaa wakanisukuma nje shuka, nikashuka. Bi Salma: Wamekushusha wapi? A m i r F a r i d : Wamenishusha pale pale waliponichukua. Bi Salma: Wakati gani? Amir Farid: Wakati ule ule takriban. B i S a l m a : We w e mwenyewe ulikuwa unafahamu kuna kitu kimetokezea huku katika nchi au waliwahi kukugusia labda? Amir Farid: Mimi hawajanigusia kabisa, lakini baada ya kutoka tu kila niliyeonana naye alikuwa ananipa habari kama kumetoka maafa kuna watu wamepoteza maisha. Bi Salma: Sasa nini maoni yako kwa serikali yako? Amir Farid: Kwa kweli tunaiomba serikali itumie sheria na uadilifu, kinyume

Mahojiani ya ana kwa ana Sheikh Farid Ahmed Hadi na Salma Said usiku wa Ijumaa Oktoba 19 mara baada ya Sheikh kuonekana baada ya kutoweka kwa siku nne.
cha hivo watakuwa wanaimba tu amani katika nchi, lakini haiwezi kupatikana na iwe ni sheria kivitendo na hayo ndio ugomvi wenyewe kwa sababu hata mie mwanzo nilidhani wamenikamata kwa sababu nilizungumza kwa hasira sana katika msikiti wa Mwanakwerekwe, tena kwa hasira kwa kuzingatia hayo hayo kwa kumtuhumu (Rais, Mheshimiwa) Shein na kumtuhumu (Mheshimiwa Makomo wa Kwanza wa Rais) Maalim Seif na wengine wote viongozi wa juu kwa kweli nyie viongozi mupo, lakini hamtendi sheria na wala hamtetei sharia, haya ndio niliokuwa nikiyazungumza mimi, na niliyazungumza makali na kama mtarejea kutizama DVD mtaona kwa sababu inaudhi katika nchi watu wanazungumza kuwa wao wanataka sharia, lakini kivitendo sivyo, hawataki sharia. Mfano suala zima vinaletwa vitambulisho vya Mtanzania, wakati huo huo wananchi wanahitaji vitambulisho vya Mzanzibari hawapewi, mtu wala hakinadishwi na wala hakitetewi na hata kikitetewa mara moja tu, lakini baada ya hapo kimyaa inamaanisha serikali au Rais amekuwa ni mfalme katika nchi na anafanya atakavyo yeye hendi kulingana na katiba ya nchi maana katiba inasema wananchi ndio wafalme na sio yeye Rais na wananchi ndio wenye mamlaka. Kwa hiyo, nilazima afuate nini wananchi wanataka na kama ingelikuwa yafuatwa sheria katika nchi hii, yasinge tokea haya yote na hata hizi vurugu ni askari polisi (wanaozianzisha)

hakuna anaye anzisha. Bi Salma: Sasa nini maoni yako kwa wananchi? Amir Farid:Naomba wananchi watuliye na wasifanye vurugu za aina yoyote. Nchi yetu tunaipenda lakini wanatakiwa siku zote wawe imara katika kuitetea nchi na haki zao kwa sababu hizi ni awamu za sheria na uwazi na watu kupewa haki yao dunia nzima ndio inavyokwenda sasa hivi. Na wanatakiwa viongozi pia wajuwe mtu yoyote asiyekubali kubadilika, basi wakati utambadilisha kwa nguvu atake asitake. Bi Salma: Sheikh Farid swali langu la mwisho, Polisi wanaweza kusema au watu wa usalama wamekuchukua kwa sababu ya kukuuliza au kukutia hofu, licha ya maswali yote, vitisho vyote, nini msimamo wako katika kuitetea Zanzibar? Amir Farid: Mimi msimamo wangu katika suala la kuitetea Zanzibar upo pale pale hadi Jamhuri ya Watu wa Zanzibar isimame.

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

MAKALA

AN-NUUR
bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola, waliotarajiwa kuwa ndio walinzi wa usalama na amani ya nchi, wanaonekana kuwa washenga na mawakala wa agenda hii. Siku ya Ijumaa iliyopita Oktoba 19, gazeti moja liliibuka na kichwa cha habari katika ukurasa wake wa mbele kikisema: Uamsho watua Dar kumuunga mkono Ponda. Kisha katika vichwa vidogo vya habari likasema: Wawasili kinyemela kwa boti za kukodi. Wapania kuongeza nguvu kuchoma makanisa. Polisi wasema wanatikisa kibiriti, watawakabili. Katika ufunguzi wa habari hiyo gazeti hilo likasema kuwa wafuasi 150 wa taasisi ya Uamsho wamekodi boti tatu kutoka Zanzibar kuelekea Dar es Salaam na zimepangiwa Bagamoyo na Mbweni kwa siku tofauti. Kisha gazeti hilo likasema kuwa watu hao wamepewa maelekezo na viongozi wao (majina tunayahifadhi) ya kuhakikisha wanaendeleza falsafa za kuteketeza makanisa na majumba ya Wakristo huku Tanzania Bara bila kuacha vielelezo wala ushahidi. Likiendelea gazeti hilo la kila wiki likasema, ufuatiliaji wa nyendo za kundi hili umebaini kwamba, baadhi yao wametua Dar siku ya Alhamisi kwa jahazi maalum (jina tunalihifadhi) huko Mbweni na kukodi daladala ili waanze shughuli waliyotumwa. Likinukuu chanzo chake cha habari liliyemuita msiri wao ambaye ni katika walioandaliwa kuchoma makanisa likasema: Tu m e f i k a w a t u 4 5 wakiwemo wanawake 12 waliopewa mafunzo maalum ya judo, karate, miereka na kujichanganya mitaani bila kutiliwa shaka, na kituo cha kwanza tutatia kambi eneo la Tandika Yombo. Baada ya kuyasema hayo likaongeza likisema kuwa ingawa hakuna tarehe wala siku maalum ya kumaliza maelekezo ya kuvuruga mitaa ya Dar es Salaam na Tanga, lakini kivumbi kitakuwa siku ya Ijumaa watakapotia nguvu za ziada kuhakikisha kuwa wanalipa kisasi dhidi ya Wakristo kwa gharama yoyote. Katika kumalizia habari yake gazeti likasema: Habari tulizozipata jana (Alhamisi iliyopita) wakati gazeti hili linaenda mitamboni zimedai kuwa baadhi ya watu wenye

Na Omar Msangi
NCHIMBI atema cheche vurugu za Waislamu, yamesema baadhi ya magazeti yakimnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Dr. Emanuel Nchimbi. Waziri Dr. Nchimbi alikuwa akitoa kauli ya serikali juu ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wale aliodai kuwa wanataka kuitumbukiza nchi hii katika machafuko ya kidini. Waswahili wana msemo wao, muungwana nguo ikimvuka huchutama. Hasimami na kurukaruka au kukimbia akishangilia. Rais, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alizungumza vizuri sana alipotoa kauli juu ya lile tukio la kunajisiwa Quran zilizofuatiwa na ghasia zilizopelekea kuharibiwa baadhi ya makanisa. Ufupi wa maneno alikuwa akiwabembeleza Watanzania na kuwasihi watulizane, wasilipizane kisasi. Lakini mambo yaliyojiri baada ya kusari Mheshimiwa Rais, utadhani kulikuwa kuna watu wanasema, wakati ndio huu. Ukitizama namna hatua zilivyochukuliwa kuvamia Chuo cha Kiislamu Changombe kuwaondoa waliokuwa wamepiga kambi pale, alivyokamatwa Ponda sambamba na kutoweka Sheikh Farid kwa siku nne bila kujulikana alipo, ni hali inayoibua maswali yanayohitaji kupatiwa majibu. Wakati nikishika kalamu kuweka sawa mawazo na nukta muhimu katika kuandika makala na maoni haya, bado nilikuwa najiuliza: Yote haya yanafanyika kwa sababu gani? Uchochezi na uchokozi huu lengo lake nini? Je, haya yanafanywa kwa masilahi ya nchi hii au ni kama yale ya Iraq, Libya na sasa Syria? Je, ni kama yale ya Saddam Hussein ya kupewa silaha za kemikali k u w a t e k e t e z a Wa k u r d i kisha baadae wakamruka na kumhukumu kwa mauwaji ya halaiki? Hivi hawatambui hawa kuwa kama kuna watu wanawafanyia kazi ili wawabamize na hata kuwauwa Waislamu, lao likishafanikiwa ndio hao hao watakao waruka na kuwapeleka ICC, The Hague? Nimekuwa nikijiuliza maswali haya kwa sababu ukitizama utaona kuna juhudi za makusudi zinafanyika kuhakikisha kuwa kwanza kuna kuwa na hofu na kitisho cha uhakika. Baadhi ya vyombo

Kariakoo mnatuma JWTZ Malawi mtapeleka nini?

ASKARI Kavu wakiwa wamemkwida mmoja wa raia katika kamatakamata iliyofanyika Ijumaa iliyopita Jijini Dar es Salaam.
1. Neocon Neoconservative. Criminally insane spenders that believe in killing brown people for the new world order. Huge Orwellian government, unfathomable amounts of spending, bomb tens of thousands of people to death to rearrange the globe. Take the worst aspects of the liberal and conservative positions and combine them into one and you would have a NeoCon. Neocons are the greatest threat to life, liberty and property this country has ever known. 2. neocon Neoconservative. Originally used to describe left-wingers who crossed the floor, neocons are on the authoritarian right, rather than the traditionally conservative libertarian right. They tend to be very pro-war and adopt the mentality of Were better than you and we know it. Some more vulgar people call them Neocunts. I dont really like Kerry, but Id rather see him in power than those horrendous neocons who currently run things! 3. neocon 1. Small group of politicians coming from as early as the Ford administration up to the Bush II administration. 2. Have a fake pretense about believing in smaller government. In reality believe in big spending and tax cuts for their wealthy political and business friends, hence decit spending. 3. They fake being social conservatives, although true social conservatives believe they really care about social issues. Neocons distract the public by acting like they really care about social issues like gay marriage, abortion, and ag burning. Meanwhile they are busy conducting wars and stiing your freedom. 4. Believe in costly wars and creating boogeymen to try and make you think only they can keep you safe while they restrict your freedoms to protect you. This is their signature issue, to help keep them in power. 5. Actually despise any types of small government advocates, Barry Goldwater, traditional live and let live conservative, and libertarians. George Bush I and II, Dick Cheney, Donald Rumsfeld, Paul Wolfowitz, Richard Perle, are all a bunch of neocons. vya habari, vishaanza kuzungumzia kuwepo kwa matawi ya Boko Haram nchini kama lilivyonadi gazeti la Rai likisema: Boko Haram yaweka amani rehani Tanzania. Kila inavyoonekana kuwa hali ni tulivu, kuna watu wanaona bado. Kwa nini patulie? Imefeli propaganda ya Fazul na wale Al Qaida waliodaiwa kuingia nchini kuwinda nyama katika mbuga zetu ili kuwapelekea kitoweo Al Qaida kule Kandahar. Tukaambiwa kuwa Al Qaida hao walipokewa na wafanyabiashara wa Kiburushi kule Mbeya. Imefeli pia ile propaganda, usanii na kiroja cha mtoto wa shule ya msingi kuingia katika ubalozi wa Marekani na kigeleni cha mafuta ya taa akitaka kulipua Ubalozi huo. Juhudi zikafanyika kuwaunganisha Masheikh wa Mtambani kuwa ndio waliomfundisha ugaidi mtoto huyo. Baada ya yote hayo kufeli kuilipua nchi, Waislamu kupambana na Wakristo au kujenga mazingira kama yale ya Kenya na Al Shabab, sasa linakuja hili la Uamsho na kuchoma makanisa. Alimuradi kila kukicha kuna juhudi zinafanywa kukoroga, kuleta tna, uchonganishi na kukoleza kitisho. Nitaeleza. Lakini niseme kuwa kwa

Inaendelea Uk. 7

AN-NUUR
Inaendelea Uk. 7
sampuli ya wafuasi wa Uamsho wanaonekana huko Tandika wakivinjari karibu na makanisa na vilabu vya kuuzia pombe. Likaongeza likisema kuwa, wakati hali ya hofu ikizidi kuwakumba wananchi, Jeshi la Polisi limewatoa wasiwasi kwa kuthibitisha kuwa nyendo na njama za mashabiki wa makundi hayo zinajulikana na wanafuatiliwa tangu unyayo hadi kivuli kabla hawajaleta madhara. Nimenukuu kwa kirefu habari hii kwa sababu moja tu muhimu: Kuonyesha kuwa kuna mchezo mbaya unafanyika nchini hapa ambapo kama hatutakuwa makini, itakuwa ndio mauti yetu sote. Itakuwa msiba na tutamsaka mchawi tusimpate kwa sababu mchawi ni sisi wenyewe. Mvurugaji amani Kwa utaratibu wa kiserikali, habari ya gazeti hili inajulikana kwa serikali. Waziri Nchimbi anaijua, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaijua pia. Kwa hiyo nimeinukuu kwa urefu, sio kuwaambia wao, lakini wananchi ambao pengine hawakubahatika kuisoma ili waweze kufuata hoja nitakazotoa. Lakini jingine ni kuwa ukiisoma habari hii utaona kuwa Polisi walishataarifiwa kuwa kuna watu wanakuja kutoka Zanzibar kuchoma makanisa Dar es Salaam ndio maana mwandishi akawanukuu Polisi wakisema kuwa wanawafuatilia tangu unyayo hadi kivuli. Kwa upande mwingine, Zanzibar ni kisiwa kidogo na sehemu za kupaki na kuondokea boti zinafahamika. Kwa maana hiyo, haiwezekani kuondoka watu 150 na boti 3 za kukodi bila ya vyombo vya dola kujua. Tumeambiwa pia kuwa watu hao walishukia Bagamoyo na Mbweni, kisha wakakodi daladala. Mbweni na Bagamoyo nako, hakuna namna boti kama hizo zinaweza kuingia kwa siri serikali isijue, vinginevyo kutakuwa hakuna serikali wala vyombo vya usalama jambo ambalo ni muhali. Mr. Emanuel Nchimbi, Waziri wetu wa Mambo ya Ndani, labda sasa niulize, serikali imechukua hatua gani juu ya wale watu waliodaiwa kuingia Dar es Salaam kwa boti tatu za kukodi ili kufanya kazi ya kuchoma makanisa? Ilikuwaje serikali ikawaacha mpaka wakaingia Bagamoyo na Mbweni bila

MAKALA/HABARI

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

KARANDINGA la jeshi la Wananchi (JWTZ) likiwa katika moja ya mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita.

kuwakamata? Kama ilitaka kupata kidhibiti, ilichuka hatua gani baada ya kuwaona wakikodi daladala mpaka Tandika na kuanza kuvinjari katika makanisa ambayo tunaambiwa kuwa ndiyo shabaha (target)? Kule Marekani tunaambiwa kuwa FBI hutafuta mtu muhalifu au mtu anayetaka viza au uraiya au mtu tu mtaani lakini Muislamu, wakaingia naye dili kwa lengo la kumsaidia naye awasaidie. Basi watamshawishi kufanya vitendo vya kigaidi na mwisho

Kariakoo mnatuma JWTZ Malawi mtapeleka nini?


wa siku wanampa bomu bandia kisha wanamkamata na kudai kuwa ni gaidi. Sasa kama ni kweli kuna watu waliopewa mafunzo ya kareti, judo na silaha wakiwemo wanawake walioingia Dar es Salaam kutoka Unguja kwa lengo la kuchoma moto makanisa, na serikali haikuwakamata baada ya kupata habari, je, tuseme kuwa serikali inawajua na ndiyo iliyowatuma, kwa maana kuwa inafanya mchezo ule wa FBI? Na kama ni hivyo, wakishambulia makanisa, serikali itapata faida gani?

Masheikh wa Uamsho wasisitiza utulivu


Na Mwandishi Wetu

Kama nilivyosema, wasomi, makachero na wataalamu mbalimba nchini Marekani, wamekuwa wakilaumu mtindo huu wa serikali kupanga njama za kuwakamatisha Waislamu ugaidi ili iweze kuimarisha kitisho cha ugaidi ipate sababu ya kuwabamiza Waislamu na kuidhibiti Marekani yenyewe kwa kanuni za kijeshi. M r. N c h i m b i , k a m a serikali ilikuwa na taarifa za ujio wa watu waliotumwa kushambulia makanisa na hamkuchukua hatua, je, mlitaka nanyi washambulie ili

mpate sababu ya kuwahujumu Waislamu? Inavyoonekana ni kuwa kilichotokea jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita hadi Jeshi la Wananchi kuitwa katika kilichodaiwa kuongeza nguvu, kwa hakika ni aibu kwa nchi hii. Habari tuliyoinukuu inasema kuwa kundi lililoingia Dar es Salaam lilipanga kuwa kilele cha vurugu kingekuwa Ijumaa. Gazeti lilisema kuwa: Ingawa hakuna tarehe wala siku maalum ya kumaliza maelekezo ya kuvuruga mitaa ya Dar es Salaam na Tanga, lakinikivumbi kitakuwa siku ya Ijumaa watakapotia nguvu za ziada kuhakikisha kuwa wanalipa kisasi dhidi ya Wakristo kwa gharama yoyote. Katika hali ya kawaida kama wanavyofanya wenzao wa FBI, ulitaraji kuwa baada ya watu hawa kuingia Dar es Salaam na kupiga kambi Tandika, serikali ingewakamata na kwa vielelezo walivyokuwa navyo wakawafikisha mahakamani. Lakini inavyoonekana hapa ni kuwa ilitakiwa hasa vurugu la sawasawa litokee na kama ni makanisa yachomwe moto na watu wauliwe. Nasema haya kwa sababu ukitizama utaona kuwa yaliyotokea Kariakoo Ijumaa ilikuwa jambo la kulazimisha kana kwamba kulikuwa na watu kila wakiona Waislamu Inaendelea Uk. 8

MASHEIKH wa taasisi ya Uamsho wamewanasihi na kuwasisitiza Waislamu kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu ambapo viongozi wao wanashikiliwa na Polisi. Kupitia waraka uliotolewa na kusambazwa misikitini juzi, Waislamu wametakiwa kuwa na subra na wafike mahakamani jana kwa utulivu kusikiliza mashitaka watakayosomewa viongozi wao ambao ilikuwa wafikishwe mahakamani hiyo jana. K ama ( m n a v y o o n a ) hali ilivyo na mnavyosikia, mnaombwa muwe watulivu na mfanye subra na leo (juzi) hapo Msikiti wa Mbuyuni hapatakuwa na muhadhara si Adhuhuri wala Alasiri. Mnachoombwa na viongozi wenu muwe wavumilivu na watulivu hadi kesho (jana), mfike mahakamani bila ya fujo na mchukue kopi

Njama za kuilipua Zanzibar zakwama


Hata baada ya Sheikh Farid kupatikana, kauli yake aliyoipa uzito ni kuwaambia wananchi kutulia, wasifanye zogo la aina yoyote kwani wanachopigania ni haki yao na kwamba hawajakiuka sheria. Naomba wananchi watuliye na wasifanye vurugu za aina yoyote. Nchi yetu tunaipenda lakini wanatakiwa siku zote wawe imara katika kuitetea nchi na haki zao kwa sababu hizi ni awamu za sheria na uwazi na watu kupewa haki yao dunia nzima ndio inavyokwenda sasa hivi.
Inatoka Uk. 2

(nakala) za vitambulisho vyenu vya Mzanzibari. Ilisema sehemu ya waraka huo na kuongeza kutoa wito ukisema: Jingine ni kuwa msikae vikundi na mkawapa askari sababu,

tunasisitiza amani na utulivu na Waislamu ni wenye kutii amri za viongozi wao. Tunasisitiza amani na utulivu, pia subra na dua kwa wingi. Ukipata taarifa hii mjulishe na mwenzio toa nakala na

uwape wengine. Ulimalizia ujumbe wake waraka huo ambao maudhui yake yanaonekana kuwa tofauti kabisa na sifa wanayopachikwa Masheikh wa Uamsho.

Hiyo ilikuwa kauli ya Sheikh Farid mara baada ya kuonekana usiku wa Ijumaa iliyopita. Hata hivyo, pamoja na msimamo huo wa Sheikh Farid na Masheikh wa Uamsho, bado picha inayopakwa ni ile ya kuwatia ugaidi Masheikh hao na kuonekana kama maharamia wauwaji. Baadhi ya vyombo vya habari vimekia mahali pa kuwafananisha na Boko Haram wa Nigeria, Al Shabab na Al Qaidah. Kutumia misamiati hii ikiunganishwa na zile kauli za baadhi ya maaskofu na wana-CCM wahafidhina,

ndio kunakojenga dhana kwamba huenda jambo hili likawa na agenda za mbali zinazodhibitiwa, kuongozwa na kusimamiwa na mabeberu wanaotafuta sababu. Waswahili wana msemo wao kwamba mchuma janga hula na wakwao. Sasa wale waandishi waliodai kuwa Uamsho wameingia Dar es Salaam kwa lengo la kuchoma makanisa, wasije kudhani, wala wasijidanganye kuwa maadhali wametumika kufanikisha mipango ya mabeberu, wao watakuwa salama.

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

MAKALA

AN-NUUR
yaliyokwishajiri katika nchi nyingine. Aliwahi kusema Mwalimu wangu Ayub Rioba kuwa yeye hailaumu Marekani kwa inayofanya japo yanaonekana kuwa ni uharamia kwa wengine. Hoja yake ilikuwa kwamba kila nchi inatizama masilahi yake. Sasa kama Marekani itapata masilahi yake kwa kuwabamiza Watanzania au kuchochea mgogoro kati ya nchi na nchi, au kati ya jamii moja na nyingine katika nchi moja, itafanya. Lakini pamoja na ukweli huo, hivi sasa Wamarekani wanakuja juu. Wametanabahi kuwa mchezo wa serikali kuwabambikizia ugaidi Wa i s l a m u , u n a t u m i w a kuifanya nchi yao kuwa taifa la kipolisi. Kwa upande mwingine wanakuja juu pia wakidai kuwa nchi yao pamoja na ubabe wake, imekuwa kama mtumwa wa Israel na matajiri wachache wanaoishi kutokana na ubeberu wa kijeshi. Wanaoitwa Neocons na Israel wanasema piga Iraq, piga Afghanistan, piga Libya na sasa Syria. Wanaoumia kiuchumi, kudorora huduma za kijamii na vijana wao kufa vitani, ni wananchi. Wananchi sasa wanakuja juu. Swali ni je, Mtanzania, awe ni kiongozi wa serikali, mwandishi wa habari, kiongozi wa dini au mwananchi wa kawaida, atanufaika vipi Waislamu na Wakristo wakivurugana?

Quran ina msemo wake, inasema: Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ulimwenguni, husema, Sisi ni watengezaji. Hakika wao ndio waharibuji, lakini hawatambui. (Al Baqara 11-12). Katika taarifa yake Mheshimiwa Waziri wa M a m b o y a N d a n i , D r. Emanuel Nchimbi amesema kuwa Serikali inafanya uchunguzi kubaini kama vurugu hizo zina mkono wa makundi ya nje ya nchi. N i m k u m b u s h e Mheshimiwa Waziri kuwa katika mauwaji ya Mbwenchai, chanzo kilikuwa kauli ya Paroko wa Kanisa Katoliki aliyedai kuwa Waislamu walikuwa wakimtukana Yesu. Bila kuchunguza serikali ikawaangukia Waislamu kwa hasira hadi kuuwa. Baada ya kufanya mauwaji na kuwapongeza Polisi waliouwa Waislamu kwa kuwalenga shabaha, serikali ikaja na madai kuwa kulikuwa na Balozi za Nje zilizowafadhili Waislamu Siasa Kali. Labda tumuulize Mheshimiwa Nchimbi, baada ya uchunguzi wao waligundua ni Ubalozi upi ulichochea Yesu kutukanwa na kuchochea Mauwaji ya Mwembechai? Au waligundua kuwa Paroko Lwambano alitumwa na Vatican kuzua urongo ule ndio maana ikapiga kimya mpaka leo haijazitaja Balozi hizo? Mi ningemshauri Mheshimiwa Waziri wetu Emanuel Nchimbi kwamba kabla ya kuwatafuta anaodai walichochea mpaka wakalazimika kulitia fedheha Jeshi letu (JWTZ) ya kuranda Kariakoo utadhani ni wakati ule wakiwa Kyaka na Mtukula, aanze na kuwakamata na kuwahoji wale ambao boti zao zilikodishwa kuleta watu Dar es Salaam kushambulia makanisa. Akiwapata hao, atawapata pia waliowakodi, kambi wanazofundishia watu wao judo na kareti na kama wapo watu wa nje watawajua kupitia kwao. Na kulifanya hili ni jepesi kwa sababu gazeti lililotupa habari hizi limesema kuwa linawajua wote ila katika habari hii, lilihifadhi tu majina yao. Lakini zaidi gazeti limesema kuwa miongoni mwa wapasha habari wake ni katika hao waliochukuliwa Zanzibar kuletwa Dar es Salaam. Labda nikumbushe lilivyosema gazeti: Vyanzo vya kuaminikavimedokeza kwamba, wafuasi 150 wa Uamsho wamekodi boti tatu kutoka Zanzibar kuelekea Dar

Nchimbi, kama wapo maadui wa nje wanawatumia nyinyi sio Waislamu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dkt. Emmanuel Nchimbi.


es Salaam na zimepangiwa Bagamoyo na Mbweni kwa siku tofauti. Wafuasi hao ambao baadhi yao ni wapashaji habari wa gazeti hili inaelezwa walipewa maelekezo na viongozi wao (majina tunayahifadhi) ya kuhakikisha wanaendeleza falsafa za kuteketeza makanisa na majumba ya Wakristo huku Tanzania Bara. Kwa hiyo, Mr. Nchimbi, maadhali miongoni wa watu hao walioandaliwa kuchoma makanisa ni wapasha habari wa gazeti hilo linalolinukuu na ambalo unalo, kazi yako na ya serikali ni nyepesi kabisa. Anza na kukamata Boti iliyotua Bagamoyo na Mbweni. Lakini utueleze pia kwa nini hawakukamatwa toka Zanzibar au walipotua Mbweni mahali nyeti kwa nchi hii mkaacha mpaka mkalazimika kuita JWTZ kuwasaidia kupambana nao kama mnavyotaka Watanzania waamini kuwa Kariakoo mlikuwa mkipambana na watu wasioogopa virungu, mabomu ya machozi, mbwa wa polisi wala risasi za moto za FFU. Kwamba salama ilipatikana kwa kuwahusisha vijana wetu wanaopendwa na wananchi JWTZ! Charles Stith, aliyewahi kuwa Balozi wa Marekani nchini, aliwahi kusimama nchini ndani ya Kanisa na k u w a c h o c h e a Wa k r i s t o wachukue hadhari zao juu ya Waislamu. Haikupita muda, yakafuatia mauwaji Zanzibar 2001 ambayo yaliungwa mkono na Maaskofu. Ni kipindi hicho hicho serikali ikadai kuwa kulikuwa na Wa i s l a m u w a l i o h i t i m u mafunzo ya ugaidi nje ya nchi na wamerejea. Mara akakamatwa Profesa Dakitari Muislamu wa Muhimbili. Kutokea hapo ndio yanakuja kwa kasi haya ya usanii wa kina Fazul, mtoto wa shule na kigeleni cha mafuta ya taa, madai ya MsemaKweli kwamba Wa i s l a m u w a m e i n g i z a makontena ya mapanga kutoka nchi za nje kwa ajili ya kushambuilia Wakristo na sasa haya ya Boti za kukodi kutoka Zanzibar kuleta wafuasi wa Uamsho kushambulia makanisa. Ukitizama mlolongo huu wa matukio utaona kuwa yawezekana kweli kuna watu wa nje wanaochochea nchi hii izame katika machafuko. Na si kazi ngumu kujua lengo lao. Hasa ukitizama

Inatoka Uk. 7

Kariakoo mnatuma JWTZ Malawi mtapeleka nini?


au jiwe, FFU wale wangerusha mabomu, tayari hali ya mambo ingebadilika. Kulikuwa na sababu gani ya kuleta Landrova ya FFU pale? Kama ni kuandamana watu wangepita Jangwani, kwa nini wasingekaa mahali kuw a s u b i r i w a n a k u j a msikitini? Hali Karia koo ilikuwa
hivyo hivyo. Watu wanatoka msikitini, na Kariakoo inajulikana kwa wingi wa watu. Polisi wakiona kundi la watu wanapiga mabomu. Hata hivyo, inaonekana kuwa hali haikuwa imekia pale

wametulia wanakasirika kwa nini hawaleti fujo kwa hiyo wakawa wanafanya juhudi kuwachokoza. Mimi niliswali Ijumaa Msikiti wa Magomeni Kichangani na pale Imam alifanya kazi kubwa sana ya kuwatuliza Waislamu. Kwa kweli nampongeza kwa kazi nzuri aliyofanya na hoja zenye uzito alizojenga. H a t a h i v y o kilichonishangaza ni kuona gari la FFU likipita mbele ya msikiti wakati waumini wanatoka kwa makundi wakielekea nyumbani baada ya swala. Katika mazingira kama yale kuleta FFU msikitini huku wengine wanapiga picha, ni uchokozi. Angetokea mtu akawarushia maneno

palipokuwa pakitakiwa kama gazeti lilivyosema. Ndio wakati wa Alasiri Polisi wakazingira msikiti wa Idrisa na hata kupiga mabomu ndani. Kisha kila anayetoka anaandamwa na kupigwa. Watu wakawa

mabomu Msikiti wa Idrisa, kukamata watu wasio na hatia na kulitia Jeshi letu katika aibu hii kukoleza kitisho kwamba kuna magaidi wa ndani na nje? Tujaaliye hilo litatimia, nyie mtanufaika vipi?

Mheshimiwa Nchimbi, Afande Sheikh Suleiman Kova, Mr. Sadik (Mkuu wa Mkoa), drama hii ndiyo ya kuita Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)!!! Mliacha kuwakamata wale watu 150 walioingia na boti za kukodi kutoka Zanzibar ili mpate sababu ya kupiga

wanakimbia na kuingia katika nyumba jirani na msikiti. Polisi na mgambo wakawa wanavunja nyumba kuwatoa watu na kuwapiga. Unajua hali ya Kariakoo, munkari umepanda kwa waliomo na wasio kuwemo. Ghasia ikawa kubwa.

Jinsi uwongo wa serikali ulivyogeuka ukweli


Na Paul Craig Roberts
Septemba 30, 2012 Mtandao wa Kupashana Habari Katika safu iliyopita, Utamaduni wa Kujidanganya, niliandika kuwa Wamerikani wanaishi katika mkabala wa uwongo. Uwongo unatawala kila mjadala wa sera, kila uamuzi wa kisiasa. Safu hii itatumia habari mbili muhimu: makombora ya nuklia ya Iran na Julian Asaange, kudhihirisha jinsi uwongo ulivyogeuka kuwa ukweli, Mitandao ya kidola ya nchi za Magharibi inatumia kila uwongo kuinua hofu kuhusu serikali ya Iran. Hapo Septemba 28, katika ukurupukaji wenye kudhihirisha kutojali linachoongea, gazeti hafidhina la Uingereza, toleo la mtandao la Mail Online lilimwita Rais wa Iran kuwa ni dikteta. Nafasi ya urais nchini Iran hujazwa kwa kupigiwa kura katika uchaguzi shindanishi, na uwezo wa rais uko chini ya uangalizi wa wakuu wa kidini. Asaange anaandamwa kwa upande mmoja kwa madai ya ukabaji, halafu ujasusi. Vyombo vya habari vya Magharibi na Bunge la Marekani vinaunda makusanyiko ya waongo zaidi katika historia ya dunia. Moja ya maeneo ya uwongo wanayoyapenda sana ni kuwa Rais wa Iran, Ahmadinejad, anataka kuwaua Wayahudi wote. Angalia mkanda wa dakika sita na sekunde 42 wa video ya mkutano wa Ahmadinejad na viongozi wa kidini wa Kiyahudi. Usikinaishwe na jina la video hiyo. Washington Blog inafanya dhihaka. Wi k i i l i y o p i t a h a b a r i zilitawaliwa na mpango usiokuwepo lakini upo katika mitanda wa silaha za nuklia za Iran. Waziri Mkuu wa Israel, Netanyahu, akaingilia kwa kishindo kampeni ya uchaguzi Marekani, akitaka Obama afafanue mstari mwekundu wa kuishambulia Iran. Netanyahu anaamini kuwa ana nguvu zaidi kwa Obama, Rais wa taifa lenye nguvu zaidi pekee diniani, wakati uchaguzi unapokaribia. Israel haiwezi kuishambulia Iran peke yake bila kuhoa kuteketezwa kwa Israel. Lakini Netanyahu anakia tamati kuwa akiishambulia Iran wiki kabla ya uchaguzi mkuu nchini Marekani, Obama itabidi ajiunge au apoteze kura za Wayahudi kwa kutokuiunga mkono Israel katika majimbo kama Florida, ambalo lina Wayahudi wengi na viti vingi vya kumpigia kura mgombea wa chama kimojawapo. Kama uchaguzi unatoa hali ya nguvu sawa kwa wagombea, Netanyahu, mtu anayetawaliwa na kujigamba na maonyesho, anaweza kufanya kweli katika vitisho vyake na kuishambulia Iran, licha ya kupingwa na wakuu wa zamani wa ujasusi na jeshi, chama cha Silaha ya nuklia, tofauti na hapo, inahitaji ushindiliaji asilimia 95 (yaani, ya uzito au uwezo wake wa awali wa kukamata au kutoa nguvu smakujoto), hivyo kupata asilimia tano kutoka mwanzo na halafu kukia asilimia 95 ni kazi ngumu na ndefu. Nadhani nilianza kusikia madai ya serikali ya Israel kuwa Iran inatafuta silaha za nuklia kuanzia miaka ya 1990, karne iliyopita. Wakati Iran ilipotangaza kuwa, kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani, vikwazo ambavyo vinaathiri upatikanaji wa dawa hospitalini, Iran ilikuwa inataka kushindia urani kwa kiwango cha asilimia 20 ili kuweza kujipatia isotopes (atom zinazohitaji elektroni za ziada, zinazoyumba) za kitiba, madai ya serikali ya Israel kuwa hii itakia kutengeneza bomu yalifikia Iran kusema kuwa serikali ya Iran inaridhika kwa Ufaransa au nchi nyingine kuipatia isitope za tiba inazohitaji na isingefuatilia ushindiaji zaidi ya mahitaji ya uzalishaji wa umeme. Marekani na Russia pia zilitajwa kama watoaji tarajiwa wa mahitaji hayo. Kwa mujibu wa gazeti la New York Times la Septemba 29, 2011, Rais wa Iran aliliambia (gazeti la) Washington Post, na baadaye, kwa maneno hayo hayo kimsingi, New York Times: kama ninyi (Marekani na Ulaya) mtatupatia urani gredi 20 (iliyosindiliwa kwa kiwango hicho) tutaacha uzalishaji. Kwa amri ya Israel Washington ilikataa pendekezo la Iran. Kutatua tatizo siyo ilichokuwa inataka serikali ya Israel. Tatizo liko katika kuendeleza mzozo huo ili uweze kutumika kutayarisha shambulio dhidi ya Iran. Silaha za nuklia za Iran ni moja ya habari kubwa danganyifu za kusukwa, uwongo wenye nia ya kucha agenda halisi. Agenda halisi ni nini? Agenda halisi inayojificha nyuma ya wasiwasi kichaa kuhusu silaha za nuklia za Iran, ni mpango wa kihadhina wa serikali ya Israel kuhusu raslimali maji ya kusini ya Lenanon. Mara mbili serikali ya Israel imepeleka jeshi la Israel kuingia Lebanon Kusini na kutwaa eneo hilo na baadaye kulichukua liwe sehemu yake. Na mara mbili Hizhbollah wameshinda na kulifukuza eneo hilo jeshi linaloaminika sana la Israel. Wapiganaji elfu kadhaa wa Hizbollah waliweza kulishinda jeshi la Israel, ambalo linapewa silaha na mahitaji mengine kwa dola za walipa kodi wa Marekani wakati watu wa Marekani wanafungiwa nje ya nyumba zao za mikopo na kuachwa hawana ajira huku Washington ikifurahia kuhamishiwa kwa kazi zao ngambo, kwa sababu Syria na Iran zinawapa Hizbollah

AN-NUUR

MAKALA

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

RAIS Barack Obama wa Marekani


upinzani, na wengi zaidi kati ya wananchi wa Israel. Kwa maana nyingine, matokeo ya uchaguzi mkuu katika nchi yenye nguvu zaidi duniani itategemea kama rais aliyeko madarakani katika nchi hiyo yenye nguvu zaidi ni mnyenyekevu kiasi cha kutosha kwa waziri mkuu kichaa wa Israel. Kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Marekani unaweza kutegemea agenda ya Waziri Mkuu wa nchi ndogo ambayo ipo kwa sababu tu ya msaada wa kifedha, kijeshi na kidiplomasia wa Marekani, hasa kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa, ni sababu ya kuwasumbua Wamarekani ambao wanadhani kuwa wao ni raia wa nchi isiyokwepeka. Ni vipi hamkwepeki kama inabidi mfanye kama atakavyo Waziri Mkuu wa Israel? Vyombo vya habari vya Marekani vinahakikisha kuwa swali hili haliingii katika vichwa vya Wamarekani. Wamarekani wameambiwa kuwa kama Iran haina silaha za nuklia ina mpango wa kutengeneza silaha hizo. Ndicho ambacho wanasiasa wa vyama vote viwili, vyombo vya habari, na wahamasishaji kuunga mkono Israel wanavyowaambia. Wamarekani wanaambiwa hivi licha ya kuwa Shirika la Ujasusi la CIA na Makisio Rasmi ya Kijasusi yamebakia katika tamati kuwa Iran iliacha kutafuta kutengeneza silaha za nuklia mwaka 2003 na wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki waliofika nchini Iran hawajatoa ushahidi mpya wa kuwepo mpango wa silaha za nuklia na pia hakuna ushahidi wa kuelekezwa kwa urani iliyoshindiliwa (nguvu za uvutano, uwezo wa kuchanganyika) kwenda kwenye mpango wa kutengeza silaha za nuklia. Isitoshe, Iran ingeweza kufanya nini na silaha ya nuklia, kuacha tu kwa kuitumia dhidi ya nchi inayoishambulia Iran? Kuitumia kwa kushambulia nchi nyingine kungekia kuteketezwa kabisa kwa Iran. K w a n i n i Wa m a r e k a n i wanaamini kuwa Iran ina silaha za nuklia au inatengeneza silaha hizo wakati CIA inasema kuwa haifanyi hivyo? Jibu ni kuwa Netanyahu anasema hivyo, na waliochanguliwa katika serikali, Bunge na Ikulu ya Marekani wanaogopa kupingana na Waziri Mkuu wa Israel, kama ilivyo kwa vyombo vya utangazaji na uchapishaji habari nchini humo. Ni taifa lenye nguvu kuliko yote, Marekani! Watu wasiokwepeka inabidi wajikunyate katika vumbi mbele ya Netanyahu. Wamarekani hata hawafahamu aibu yao. Iran, tofauti na Israel, ilitia saini mkataba wa kimataifa wa kutokueneza silaha za nuklia. Nguvu za nuklia zinahitaji ushindiliaji mdogo, kiasi cha asilimia 5 au pungufu. Dakika ambako Iran itatangaza mpango wa nguvu za nuklia, serikali ya Israeli na mahawara wake mjini Washington walisema uwongo kuwa Iran inatengeneza bomu. Kwa kutumia haki zake za kisheria chini ya mikataba (ya kimataifa), Iran imeonekana kuwa ni dola ya kihuni na kihalifu na kuchukuliwa kama tishio kwa dunia.

misaada ya kifedha na silaha ambazo zinateketeza vifaru vya Israel. Syria, kwa uhakika, inajihami na maangamizi yanayoendeshwa na Israel na serikali yake kibaraka ya Marekani. Kuangushwa kwa Syria hakujaenda vizuri, k w a s a b a b u Wa r u s i n a Wachina hawakuridhia, kama walivyofanya kipumbavu Libya. Lakini serikali ya uhafidhina mkali ya Israel imekia tamati kuwa kwa vile sifa ya Marekani ipo katika kuangushwa kwa serikali ya Assad nchini Syria, hilo litafanyika. Hiyo inaiacha Iran. Serikali ya Israel inafahamu kuwa haiwezi kusema ukweli na kutaka Marekani iingie vitani na Iran ili Israel iweze kuiiba Lenanon ya Kusini. Ila kama hofu kuhusu silaha za nuklia za kubuni inaweza kutanda katika hisia za watu wa Magharibi kuunga mkono shambulio la Israel dhidi ya Iran, Iran inaweza kuondolewa kama mfadhili wa Hizbollah na Israel itaweza kuyaiba maji kutoka Lebanon. Hakuna mjadala wowote kuhusu agenda halisi kokote pale katika vyombo vya utangazaji na magazeti nchini Marekani. Nina mashaka kama kuna mjadala kama huo kokote Ulaya, ambayo ni mkusanyiko wa nchi vibaraka wa Marekani. Hivi tutakuwa na Vita Kuu ya Tatu ya dunia kwa Krismasi? Inawezekana, kama uchaguzi Marekani utakuwa ni patashika wakati unakaribia. Ikiwa matokeo ya uchaguzi yatakuwa hayatabiriki, Netanyahu anaweza akatupa karata na kumtegemea Obama kufuata watangulizi wake. Iran itashambuliwa, na matokeo yake hayawezi kufahamika. Tugeukie kwa Julian Asaange na Wikileaks. Kama Iran, Assange ameshutumiwa, siyo kwa msingi wa vitu dhahiri, bali kwa msingi wa uwongo. Washington, ambayo inajianika kama msambazaji wa haki za binadamu, imekuwa ikimtaabisha kama si kumtesa Bradley Manning tangu Mei 2010 bila kumkisha mahakamani katika jaribio la kumfanya Manning aseme kuwa yeye na Assange ni kundi la ujasusi linalofanya kazi dhidi ya Marekani. Assange amepata sifa duniani kote, kwa sababu Wikileaks ilichapisha habari zilizovujishwa kwenye mtandao huo ambazo vyombo-dola vya habari vinazizuia. Akiwa Sweden, Assange alikumbwa na wanawake wawili wanaotaka sifa ambao walimchukua nyumbani kwao kwenye vitanda vyao. Wanawake hao baadaye walijigamba ushindi wao katika mitandao ya kijamii, ila walipogundua kuwa wanashindana, wakamgeukia mla kuwili Assange na kumfungulia mashitaka. Mmoja akadai hakutumia kondomu kama alivyomtaka, na mwingine akadai kuwa alimruhusu ajisikie mara moja akafanya mbili.

10

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

TUWAENZI WASOMI HAWA


Katika kiza kinene, na mwitu wenye kutisha Sitaomba tuachane, wala kunikurupusha Mwazo yasongamane, ili nipate kumbusha Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Walikuwa mashujaa, haki kuipigania Hawakukata tamaa, mazuri walipania Walikuwa ulamaa, wenye Dini kutambua Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Wa kwanza wetu aziizi, Hassan bin Amiri Alikuwa kiongozi, aliyetaka mazuri Hakuleta uchochezi, kajenga umma kwa kheri Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Huyu ni mufti wetu, mwenye elimu ya kweli Aliunganisha watu, wote wakamkubali Na dini nchini mwetu, ikashamiri kikweli Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Alikamatwa kihuni, kwa fujo pia na chuki Akahamishwa nchini, kwa mtutu wa bunduki Zanzibaria nchini, huko kukawa handaki Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Bara Shekhe akatoka, Pwani akaelekea Na Umoja ukashuka,dhulma ikaenea Wanaki wakacheka, meno wakayakenua Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Wa pili kumhakiki, taswiraye kuileta Ni Profesa Maliki, Shekhe aso na matata Yeye alipenda haki, ili watu kuifata Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Huyu ni Mpakistani, aloletwa Tanzania Miaka ya sabiini, elimu kuja kutoa Alifundisha chuoni, UD wamtambua Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Alikusanya vijana, Darsa akazitoa Kawakumbusha kwa kina, dini yao kuijua Wakaamka vijana, dini wakapigania Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Lakini cha kushangaza, vita ikaanza mjia NYERERE chuki kaanza, na BAKWATA yake pia Lengo ni kumfukuza, nchini kutokomea Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Saa ishirini na nne, hizo wakampatia Nchi hii aihame, ni mkimbizi sawia Hawataki wamuone, arudi akotokea Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Shekhe akaelekea, Kenya akenda tulia Mizigo hakuchukua, vijana walimletea Profesa kapotea, vijana wamlilia Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Chanzo cha yote tokea, ni BAKWATA wachochezi Unaki walitia, NYERERE akawajizi Chuki wakashikilia, kufukuzwa viongozi Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Machozi yananitoka, kumbukumbu nasitisha Sitaweza kuandika, hapa hapa inatosha Simanzi imenishika, chozi ninalidondosha Daima tuuthamini, mchango wa watu hawa. Wito huu nauotoa, kwa Isilamu nchini BAKWATA si wa kulea, watudidimiza chini Wewe ukisha wajua, usiwaweke wandani Mwisho sote tuungane, baada ya dhiki faraja. Mwl.Mohammed Makimu UITC-DAR ES SALAAM mohdmak@hotmail.co.uk

Mwingine akojolea Quran Ukonga Dar


Na Shaban Rajab
WAKATI vyombo vya dola vikiwadhibiti Masheikh na kuendelea na kamatakamata katika maeneo mbalimbali kufuatia kile walichokiita kuwasaka wahuni waliochoma moto makanisa na kuiba mali huko Mbagala jijini Dar es Salaam, mtu mwingine tena amekojolea Quran. Daudi Kapaya (Mkristo) mwenye umri wa miaka 20 wa Ukonga Majumba Sita, kitongoji cha Mogo Mkengeni, juzi siku ya Jumamosi mwishoni mwa wiki, alikojolea kwa makusudi kitabu cha Quran (Juzuu Amma) huko Ukonga majira ya saa 4:38 usiku. Aw a l i k i j a n a K a p a y a aliwakuta vijana wakisoma gazeti la An-nuur nje ya duka iliyokuwa ikihusu kadhia ya Mbagala. Kijana huyo akasema kuwa hata yeye ana uwezo wa kukojolea Quran na asifanywe lolote. Hata mimi ninao uwezo wa kuikojolea hiyo Quran na isiwe lolote, alisema kijana Kapaya. Kijana mwenzake wa Kikristo waliyekuwa naye pamoja akamwambia, usicheze na dini za watu wengine, utapatwa na makubwa ambayo utakuja juta. Hata hivyo, kijana Kapaya akajibu yeye hayo hajali na kwamba anao uwezo huo. Akasogea dukani alipokuwepo muuza duka aliyefahamika kwa jina la Haruna Ahadi Makono, ambaye kwa wakati huo alikuwa akisoma Quran, Juzuu Amma. Kapaya akamkwapua Juzuu hiyo na kuibwaga chini na kuikojolea hapo hapo nje ya duka na kukimbia. Imeelezwa kuwa baada ya kukimbia, muuza duka, Haruna Ahadi na kijana mwingine walikwenda kwa Imam wa Msikiti wa al-Aqsa, Majumba Sita Ustadh Harid Masoud Mlanzi kumfahamisha juu ya tukio hilo.

SHAIRI/HABARI

AN-NUUR

Walipofika walimwamsha na kuwasikiliza waumini wake ambapo Ustadh Mlanzi aliamua kwenda kwa Mjumbe wa Shina No. 38, aliyefahamika kwa jina la Elimina Patrick, ambaye aliwapa barua ya kwenda Polisi. Imam na waumini wake walika Polisi kituo cha Staki Shari ambapo walimkuta askari mmoja ambaye alidai kuwa yeye hana uwezo wa kusikiliza shauri hilo hivyo warudi kituoni kesho yake ili waonane na Mkuu wa Kituo. Kesho yake siku ya Jumapili saa nne asubuhi walika kituoni na kukutana na mpelelezi wa kituo cha Staki Shari ASP Iddi Kiyogomo, ambaye alichukua maelezo na kufungua jalada STKRB/19378/2012 la kosa la kukashfu dini dhidi ya mtuhumiwa. Kufuatia tukio hilo, RCO wilaya ya Ilala Bw. Duwani Nyanda, aliwaomba Waislamu wawe watulivu ili kunusuru hali na kuahidi kwamba, suala hilo watalishughulikia wao kwa mujibu wa sheria.

SHURA YA MAIMAMU

BARAZA LA IDD

Inawatangazia Waislamu wote Jijini Dar es Salaam kuwa kutakuwa na Baraza la Idd siku ya Jumamosi. Wapi: Msikiti wa Mtambani Muda: Kuanzia saa 8 mchana Mada mbalimbali zitazungumzwa Ewe Muislamu usikose kuhudhuria Baraza hili muhimu kwa Mustakabali wa Uislamu na Waislamu nchini. WABILLAH TAWFIIQ

Sifa na masharti ya kujiunga

KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERSTanzania COLLEGE S.L.P. 62, Same Kilimanjaro, Mob: 0787 188964

NAFASI ZA KUJIUNGA NA KOZI YA UALIMU WA SHULE ZA AWALI, MSINGI NA MADRASA 2013

Muombaji atimize sifa na masharti yafuatayo: (i) Awe Muislamu aliye tayari kuishi Kiislamu (ii) Awe anajua kusoma Quran kwa ufasaha. (iii) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya Uislamu, Darasa la Watu Wazima kabla ya kujiunga. (iv) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne na awe anafundisha madrasa au kipindi cha dini katika shule za Msingi au Sekondari. Patakuwa na usaili siku ya tarehe 1/12/2012 saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyoainiashwa kwenye fomu ya maombi. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11/2012. Fomu italipiwa shilingi 5,000/- tu. Fomu zinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwa ukurasa wa 11 MKUU WA CHUO

AN-NUUR

TANGAZO

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012

11

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Kwanza kwa shule zifuatazo: Mkuzo Islamic High School - (Songea) - BWENI TU. Kirinjiko Islamic Sec. School (Same) BWENI TU Nyasaka Islamic Sec.School (Mwanza) BWENI TU. Ubungo Islamic High School (Dar es Salaam) KUTWA NA BWENI

NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA 2013

1. Shule hizi ni za Kiislamu, zenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi ya Kiislamu. 2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo: Elimu ya Dini ya Kiislamu, Usomaji Quran na mafunzo yake, Lugha ya Kiarabu, Kiswahili, English, Basic Mathematics, Physics, Chemistry, Biology, Geography, History, Civics, Book keeping na Commerce. 3. Patakuwa na mtihani tarehe 01/12/2012 saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyoorodheshwa kwenye fomu ya maombi. Muombaji anaweza kufanyia mtihani katika kituo chochote. 4. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11 /2012 5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini. 6. Pia, fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa atakayepata fomu kupitia tovuti (download) atatakiwa kulipia wakati wa kurejesha siku ya mtihani. Arusha Kilimanjaro Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni -0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Osi ya Islamic Education Panel - Mwanza -Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni-0714587193 Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA.-0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Osi ya Islamic Ed.Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin-0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Osis ya Islamic Ed. Panel karibu Nuru snack Hotel-0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.ss 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU0715 68 1 701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole-0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul Fallah: 0777125074Osi ya ust.Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627 USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA! MKURUGENZI WABILLAH TAWFIIQ

Dar es Salaam Morogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Maa -

AN-NUUR
DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 23-25, 2012
kwani kupitia malalamiko hayo kunasaidia kuamsha hamasa miongoni mwao, amb ao haw aelew i n ini kimewafikisha katika hali walionayo. Katika makala haya nitajaribu kuyapima kwa uzito madai haya ya pili kwa kujadili mahusiano yaliyopo kati ya Serikali na Kanisa, hususani Kanisa Katoliki. Pamoja na utumiaji wa nguvu na makali ya sheria zilizopata kuchukuliwa na Serikali dhidi ya viongozi wa Kanisa Katoliki kutokana na mapenzi ya Serikali juu ya Kanisa. Katika kitabu chake Bw. Bergen, kiitwacho Development and Religion in Tanzania, katika Ukurasa wake wa 98 mwanadishi huyo anasema:Catholic Missionaries came to East Africa to nd not new churches, but new provinces of the Roman Church Kwa mujibu wa tafsiri yangu Wamishionari wa Kikatoliki hawakuja hapa Afrika ya Mashariki kwa minaajili ya kuasisi Makanisa mapya, bali walikuja kuunda majimbo mapya ya Kanisa la Roma. Ni kwamba, Tanzania (Tanganyika) ipo Afrika Mashariki, na kwa mujibu wa mwandishi Bergen, Tanzania nayo ni moja ya majimbo ya Kanisa la Roma, au kwa lugha nyepesi tuseme Tanzania ni Koloni la Vatican! Je, ni kweli Tanzania (Tanganyika) ni Koloni la Vatican? Padri. Dk. Sivalon, naye katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara (19531985) anaeleza bayana kuwa Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa nchi yetu, alikuwa kiungo pekee kati ya Chama (CCM), Serikali na Kanisa Katoliki. Na kwa msingi huo viongozi wa Kanisa wamekuja kuwa na nafasi ya pekee kuelekeza hisia, mitazamo na siasa ya Tanzania, na wamefanya hivyo wakipania pia kuwa kuhujumu Uislamu. (Msomoe Sivalon Uk. 5-6, katika kitabu chake hicho). Naye mwandishi Bergen katika kitabu chake amemnukuu Mwalimu Nyerere akisema kamwe hawezi kwenda kinyume na kanisa lake. (Bergen Uk. 335). Agosti 3, 1970 Mwalimu Nyerere, alimwita Ikulu Padri Rweyemamu katika mazungumzo maalum ambapo Nyerere alimuahidi Rweyemamu kuwa, hivi sasa Kanisa ndilo lililoshika

Mhariri wa gazeti la AN-NUUR na wafanyakazi wake wanawatakia Waislamu wote Eid el Hajj Njema
kila mtu anakumbuka kilichotokea. Ama kwa wale ambao walikuwa ni wadogo kipindi hicho ni kwamba Jeshi la Polisi lilifika Msikiti wa Mwembechai na kuuwa Waislamu kwa risasi na kikumbukumbu ni maarufu kwa Mauaji ya Mwembechai. Kufuatia madai hayo ya Padri Lwambano, viongozi kadhaa wa nchi walifikia hatua ya kuliomba radhi Kanisa Katoliki na Wakristo kwa ujumla. Majina na vyeo vya viongozi hao wakuu wa Serikali yanafahamika. Baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi la Polisi, kazi ya kukatili maisha ya Waislamu na kubaka haki zao, kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini Polycarp Kadinali Pengo, aliipongeza Serikali kwa upande mmoja na Polisi kwa upande wa pili kufuatia mauaji hayo hayo ya Waislamu, Mwembechai. Pongezi hizo alizitoa April 12, 1998 wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Dar es Salaam (DTV). Kanisa likionekana kuuchukukia vilivyo Uislamu, liliongeza harakati za siri na za wazi na kwa kutumia nguvu za dola ili kupunguza kwa upande mwingine nguvu ya Uislamu, maana kuuzima kabisa ni jambo lisilowezekana. Askofu Mkuu Pengo alitoa taarifa ya kuenea Uislamu hapa Tanzania huku akihitaji msaada wa hali na mali katika kuhidhibiti hali hiyo. Na kweli, Serikali ilitekeleza kudhibiti Mihadhara na Wahadhiri, ambapo wahadhiri maarufu nchini wakiongozwa na Habib Mazinge, walitiwa mbaroni na kutupwa Magerezani. Aidha sehemu ya taarifa yake ilisema hivi; Uislamu umekuwa tishio kubwa sana kwa imani ya Kikristo nchini Tanzania, iwapo mihadhara y a Wa i s l a m u i t a a c h w a iendelee, Kanisa litegemee kukimbiwa na waumini wake na kusilimu, kwa hiyo juhudi lazima zifanywe kuzuia Mihadhara hiyo. Tunashindwa kujibu hoja zao Waislamu sababu zina ukweli ndani yake, maelezo haya yanapatikana katika kitabu cha Askofu Pengo kiitwacho Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwenye vijilia Sinodi ya Maaskofu wa Afrika kwa ajili ya Afrika.

Na Bakari Mwakangwale

Dola inavyolisaidia Kanisa kuuangamiza Uislamu


Kufuatia malalamiko hayo, wapo wale wa upande wa pili na hata miongoni mwa Waislamu wenyewe wamekuwa wakiwalaumu Waislamu kuwa wao kazi yao ni kulalamika tu! Pamoja na kulalamika, Waislamu wamekuwa wakijibidiisha katika kutafuta njia mbadala katika kujikwamua katika mambo mbalimbali yanayowasibu. Ndiyo, ni lazima walalamike si vyema wakafunga mdomo, ili hali wana uhakika wanafanyiwa hiyana, lakini pia kupitia kulalamika kwao wamekuwa wakianisha na kuweka wazi dhulma wanazofanyiwa

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Polycarp Kadinali Pengo.

NI miaka 51 sasa tangu Taifa hili lipate Uhuru. Waislamu hapa nchini wamekuwa wakiilalamikia sana Serikali kuhusu kuwepo kwa mgawanyo usio sawa katika utoaji wa elimu, madaraka na hata nafasi za ajira Serikalini. Hoja kuu ikiwa ni Wakristo kupewa upendeleo. Ufupi wa maneno wanasema kuwa nchi hii inaendeshwa na mfumokristo unaowahujumu Waislamu na kuwaimarisha Wakristo.

hatamu za kuongoza dola naye atahakikisha hali inaendelea kuwa hivyo. Tanzania is not Catholic country, but Catholics is strong, I want to give the church a better chance here. Akiwa na maana kwamba:japo Tanzania si nchi ya Kikatoliki, lakini Ukatoliki una nguvu, hivyo nataka kulipa Kanisa nafasi ya pekee hapa nchini (Msome, Bergen Uk. 335). Na hali hii ya Kanisa kuwa na nafasi kubwa Serikalini iko wazi. Waandishi wote hawa wanatuthibitishia kuwa, kuna ukweli fulani kwamba yapo mafungamano ya dhati kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Tanzania. Ni mafungamano hayo hayo ndiyo yameendelea kuwapa uweza viongozi wa Kanisa Katoliki kutoa maelekezo, maagizo na vilio vyao Serikalini na wakasikilizwa pamoja na kutekelezwa yale wanayoyahitaji hata kama yamelenga kuleta maafa kwa Waislamu. Mfano, mwaka 1998, Padri Lwambano, ambaye ni Paroko wa Kanisa Katoliki Mburahati Jijini Dar es Salaam, alisema kuiambia Serikali:- Lazima Serikali ichukue hatua kali sana kwa Waislamu wanaoendesha Mihadhara, sababu ni watu wabaya kabisa, nimepita Sinza na Mwembechai, n i m e k u t a Wa i s l a m u hao wanamtukana Yesu wanasema Yesu si Mungu, alisema Paroko huyo na kuongeza; Kama Serikali imeshindwa kuchukua hatua kali kukomesha Mihadhara ya Waislamu na kuendelea kutupaka matope kwa mgongo wa chupa, Serikali hii ijue sisi tutalishughulikia jambo hilo kwa nguvu zetu zote. Kauli hii ya Padri Lwambano, ilirushwa hewani na Kituo cha Radio Tumaini kinachomilikiwa na Kanisa hilo hapa nchini, Februari 13, 1998. Padri Lwambano bila kujali kuwa imani yake inaamini Yesu ni Mungu na Waislamu imani yao inaamini Yesu si Mungu, aliinyooshea kidole Serikali nayo ilifuata bila kujali yenyewe (Serikali) haina dini na raia wake wana dini, kwa imani tofauti. Katika utekelezaji wa agizo hilo bila shaka

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagaration Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

También podría gustarte